Tuesday, August 29

Vigogo kampuni binafsi wazindua kitabu cha Tanzania ya viwanda


Dar es Salaam. Ukosefu wa vipaumbele, umeme wa uhakika, mitaji na mfumo mzuri wa elimu vimetajwa kuwa changamoto ya viwanda vya Tanzania kukua kwa kasi na kufikia dhamira ya kuwa nchi ya viwanda.
Hayo yameanishwa kwenye kitabu kiitwacho Tanzania’s Industrialisation Journey, 2016-2056 kilichoandaliwa na Umoja wa Maofisa Watendaji Wakuu wa Kampuni Binafsi (CEOrt) na kuzinduliwa leo Agosti 29 na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango.
Mmoja wa waandishi wa kitabu hicho na Mwenyekiti wa CEOrt, Ali Mufuruki amesema wamekiandika kuunga mkono dhamira ya Serikali ya kuifanya Tanzania nchi ya viwanda.
Amesema ili kufikia dhamira hiyo, lazima kuwepo vipaumbele ili kuondoa uwezekano wa kutumia fedha nyingi kuwekeza katika maeneo mengi bila kuwa na tija.
“Ipo haja ya kuchagua maeneo machache ya kuanzia kwa kuweka nguvu kubwa ili kupata mafanikio,” amesema.
Amesema ili kuwa na viwanda vinavyofanya uzalishaji ni lazima kuwepo umeme wa uhakika na si wa kubahatisha.
Pia, amesema ndani ya kitabu hicho wameelezea umuhimu wa kuwa na mitaji ya uhakika katika miradi inayoratibiwa na nchi kuliko kutegemea kutoka nje.
“Tukiwa na uhakika wa mitaji tunaweza kuendesha miradi yetu vizuri, kwa sababu mtu wa nje anaweza asione umuhimu wa mradi hivyo akaamua asitoe fedha lakini wenyewe tukiwa na uhakika tutakuwa na mahali pa kuanzia,” amesema.
Akizungumzia kitabu hicho, Waziri wa Fedha, Dk Mpango amesema kimewasaidia watunga sera kubaini na kutatua changamoto zinazoikabili sekta ya viwanda.
“Kumekuwepo na ombwe kwa muda mrefu kati ya Serikali na sekta binafsi ambao ndiyo waendeshaji wakubwa wa viwanda. Mara nyingi tumekuwa tunaandika wenyewe watunga sera lakini inakosekana sauti ya sekta binafsi ambao wanaweza kusema tufanye nini ili tufanikiwe kwa nguvu na haraka zaidi,” amesema.

Mahiga aeleza Sadc ilivyojizatiti kukabili ugaidi

Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika

Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, 
Dk Augustine Mahiga 
Tanga. Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Dk Augustine Mahiga amesema kikundi chochote cha kigaidi au kiharamia kitakachoingia katika moja ya nchi zilizo katika ukanda wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (Sadc) kitajuta.
Akizungumza  kwa sababu kikundi hicho cha uigaidi kitashambuliwa na majeshi ya nchi zote katika ukanda huo iwapo kitaanza uchokozi.
Amesema nchi za Sadc zimeamua kujizatiti katika ulinzi kwa kuunganisha majeshi yake ili kujiweka sawa na tishio lolote la ugaidi na uharamia zikiamini uchumi wake hautaimarika kama moja ya nchi itakuwa inasumbuliwa na ugaidi.
“Wakazi wa Tanga wamebahatika kuona mazoezi ya pamoja ya majeshi ya Sadc na kujionea yalivyo imara. Naamini kundi lolote la ugaidi au uharamia litakalothubutu kuingia katika nchi yoyote litajuta,” amesema.
Balozi Mahiga amesema hayo wakati akifunga mazoezi ya pamoja ya kijeshi yaliyopewa jina la Ex-Matumbawe yaliyoendeshwa na majeshi kutoka nchi saba zilizo katika jumuiya ya Sadc yaliyofanyika mkoani Tanga na kuhitimishwa jana Agosti 28.
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania (JWTZ), Jenerali Venance Mabeyo, amesema mazoezi ya Ex-Matumbawe yenye madhumuni ya kimkakati, utendaji kivita na ki-mbinu yamefanyika nchini kwa mara ya kwanza baada ya kuendeshwa Zambia, Lesotho, Afrika Kusini, Namibia, Angola na Zimbabwe.

Jengo la 92 Hotel Sinza lavunjwa


Tingatinga likivunja jengo lilikuwa na Hotel ya

Tingatinga likivunja jengo lilikuwa na Hotel ya 92 kando ya Barabara ya Shekilango Sinza jijini Dar es Salaam. Picha na Salim Shao 
Dar es Salaam. Jengo maarufu la 92 Hotel lililopo eneo la Shekilango, Sinza limevunjwa kutokana na amri ya Mahakama kutokana na kesi ya madai.
Watu walioshuhudia jengo hilo likivunjwa wamesema kazi hiyo ilianza majira ya saa 11 alfajiri.
Akizungumza katika eneo la tukio, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya udalali ya Rimina, Abdallah Bakari, amesema wao wanatekeleza kazi hiyo kutokana na amri iliyotolewa na Mahakama Kuu Divisheni ya Ardhi.
Bakari amesema kabla ya kuvunja jengo hilo lenye maduka na ambalo pia linatumika kwa shughuli za ibada, walitoa notisi ya siku 14, ili kuwapa muda watu waliomo ndani wahamishe mali zao.
Hata hivyo, baadhi ya wapangaji wamesema hawakupatiwa taarifa jambo lililosababisha baadhi ya mali zao kuharibika wakati wa kazi hiyo.

Kituo cha Sheria chatoa tamko mlipuko ofisi za mawakili

Rais wa Chama cha wanasheria wa

Rais wa Chama cha wanasheria wa Tanganyika(TLS),Tundu Lissu  akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam katika kupinga shambulizi la ofisi za IMMMA Advocate lililotokea hivi karibuni. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi mtendaji wa Shirika la wanawake katika Sheria na aendelao Afrika,Dk Judith Odunga na Mkurugenzi wa kituo cha sheria na Haki za binadamu (LHRC),Dk Kijo Bisimba.Picha na Ericky Boniphace 
Dar es Salaam. Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), kimemtaka Kaimu Jaji Mkuu, Ibrahim Juma kukemea hadharani shambulizi lililofanyika katika ofisi za wanasheria za Immma Advocates.
Mkurugenzi wa LHRC, Dk Hellen Kijo-Bisimba amesema tangu kutokea mlipuko usiku wa kuamkia Agosti 26, hakuna kiongozi wa Serikali ambaye amekemea.
Amesema hata kaimu jaji mkuu anayesimamia mhimili wa Mahakama naye amekaa kimya kama vile hakuna tukio lililotokea.
Dk Kijo-Bisimba amesema leo Agosti 29 kuwa, kitendo cha mawakili kuvamiwa kimewatia hofu wanataaluma hao.

Kesi ya uchaguzi Kenya

Israel: Iran inajenga kiwanda cha makombora Syria

Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema kuwa Iran inatengeza kiwanda nchini Syria na Lebanon ili kutengeza makombora.Haki miliki ya pichaALAMY
Image captionWaziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema kuwa Iran inatengeza kiwanda nchini Syria na Lebanon ili kutengeza makombora.
Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema kuwa Iran inajenga viwanda nchini Syria na Lebanon ili kutengeza makombora.
Benjamin Netanyahu ameishutumu Iran kwa kuifanya Syria kuwa kambi yake kutengeza vifaa vya kijeshi kama mpango wake wa kutaka kuiangamiza Israel.
Majeshi ya Iran yanamsaidia rais Bashar al Assad katika vita vya Syria huku ikiliunga mkono kundi la wapiganaji wa Lebanon Hezbollah.
Matamshi ya Netanyahu yanajiri baada ya kufanya mazungumzo na katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Gutierrez mjini Jerusalem.
Bwana Guterres amefanya ziara yake ya kwanza katika enewo hilo tangu kuchukua mamlaka mnamo mwezi januari.
Bwana Netanyahu hakutoa maelezo kuhusu viwanda hivyo vya Iran lakini akaonya kwamba hicho ''ni kitendo ambacho Israel haitakubali''.
Wiki mbili zilizopita, kampuni ya Israel Imgesat ilichapisha picha ilizosema zinathibitisha ripoti ya gazeti moja la upinzani nchini Syria kwamba kiwanda cha makombora kilikuwa kikijengwa kaskazini magharibi mwa Syria chini ya uangalizi wa Iran.
Picha zinazoonyesha kuwa Iran huenda inajenga viwanda vya kutengezea makombora nchini SyriaHaki miliki ya pichaIMAGESAT INTERNATIONAL NV/REUTERS
Image captionPicha zinazoonyesha kuwa Iran huenda inajenga viwanda vya kutengezea makombora nchini Syria
Imagesat International ilisema kuwa kiwanda hicho katika eneo la wadi Jahannam , karibu na mji wa Baniyas uliopo katika pwani ya Mediterania kinafanana na kile cha kutengeza makombora karibu na Tehran.
Hakujakuwa na tamko lolote kutoka kwa Iran inayotaka taifa hilo Wayahudi kuangamizwa.
Bwana Netanyahu pia alimshinikiza Guterrez kuhusu walinda amani wa UN nchini Lebanon ,Unifil , ambapo Israel inadai wameshindwa kuwazuia wapiganaji wa Hezbollah kujiongezea silaha tangu vita vya 2006.
Bwana Guterres aliahidi kufanya kila awezalo ili kuhakikisha kuwa Unifil inaafikia malengo yake .
Ninaelewa wasiwasi wa kiusalama wa Israel na narejelea kwamba wazo hilo ama lengo la kuangamiza Israel ni swala ambalo halitakubalika kwa maoni yango.
Mkataba wa Unifil unatarajiwa kuongezwa mwisho wa mwezi.

ZANZIBAR YAIPONGEZA BODI YA UTALII TANZANIA

Kamati ya Baraza la Wawakilishi ya Maendeleo ya Wanawake, Habari na Utalii ya Zanzibar wameitembelea Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) kwa lengo la kudumisha ushirikiano na kujifunza mbinu mbalimbali zinazotumiwa na Bodi katika kuvitangaza vivutio vya utalii vya Tanzania ndani na nje ya nchi. 

Meneja Masoko wa Bodi ya Utalii, Bw. Geofrey Meena alitoa ufafanuzi wa kina kuhusu shughuli zinazofanywa na Bodi ikiwa pamoja na namna inavyoshirikiana na Balozi za Tanzania zilizopo katika nchi mbalimbali, Mabalozi wa Hiari wa Utalii wanavyosaidia kutangaza utalii wa Tanzania katika nchi zao, Namna Bodi inavyoshirikiana na vyombo mbalimbali vya Habari vya ndani na nje katika kutayarisha vipindi vya utalii wa Tanzania. 
 
Aidha Bw, Meena alisisitiza kuwa mialiko ya Timu maarufu za mchezo wa mpira wa miguu kuwa moja ya njia yenye manufaa makubwa katika kuitangaza Tanzania 

Ujumbe huo uliyongozwa na Waziri wa Habari, Utalii, Utamaduni na Michezo wa Zanzibar, Mhe. Rashid Ali Juma ambaye alionyesha kuridhishwa na juhudi zinazofanywa na Bodi, alisema “ziara yetu imekuwa ni ya mafanikio kwani tumeweza kujifunza mikakati inayotumiwa na Bodi katika kutekeleza jukumu lake la kutangaza utalii wa Tanzania hasa Utalii wa Ndani”.
 
 Pia ujumbe huo uliipongeza Bodi kwa kuwa na mipango madhubiti ya utangazaji pamoja na kutengeneza video maalumu inayotumika kuvitangaza vivutio hivyo katika matukio mbalimbali ya kimataifa. Ziara hiyo Ilifanyika tarehe 28/08/2017.



Meneja Masoko wa Bodi ya Utalii, Bw. Geofrey Meena akitoa maelezo kwa wajumbe wa kamati ya Baraza la wawakilishi ya Maendeleo ya Wanawake, Habari na Utaliiya Zanzibar walipotembelea ofisi za Bodi ya Utalii, Dar es Salaam.



Mjumbe wa Kamati ya Baraza Wawakilishi ya Maendeleo ya Wanawake, Habari na Utalii ya Zanzibar akitumia lugha ya alama kutafsiri jambo kwa moja ya mjumbe wa Baraza Hilo.



Waziri wa Habari, Utalii, Utamaduni na Michezo wa Zanzibar, Mhe. Rashid Ali Juma (Katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Kamati ya  Baraza la Wawakilishi ya Maendeleo ya Wanawake, Habari na Utalii ya Zanzibar.

RAS-DODOMA- WAKUMBUKENI IDARA ZA ELIMU KATIKA PLANREP MPYA.


Beatrice Lyimo- Maelezo,Dodoma

Watendaji wa wa Serikali wametakiwa kufanya kazi kwa kujituma na weledi ili kuendana na dhana ya Serikali ya awamu ya Tano inayosisitiza uwazi na uwajibikaji katika kuwahudumia wananchi katika maeneo yakutolea huduma.

Akizungumza wakati akifungua mafunzo kwa watumiaji wa mfumo wa kielektroniki wa kuandaa Mipango,Bajeti na Ripoti (PlanRep)za Mamlaka za Serikali za Mitaa Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma Bibi Rehema Madenge amesema kuwa dhamira ya Serikali ni kuongeza tija katika kuwahudumia wananchi.

“Sasa ni lazima watumishi wa umma katika maeneo yakutolea huduma mbadilike na muendane na Dhana ya Serikali ya Awamu ya Tano ya Hapa Kazi Tu inayosisistiza kutoa huduma bora zinazolenga kuboresha maisha ya wananchi wa chini” Alisisitiza Bi Rehema

Akifafanua Bi Rehema amesema kuwa matokeo ya matumizi ya mfumo huo ulioboreshwa yanaonekana na yatagusa maisha ya wananchi wote katika maeneo yao kwa kuwa yatasaidia kuongeza tija na uwajibikaji hali itakayosaidia kuchochea kasi ya ukuaji wa uchumi.

Aliongeza kuwa mfumo wa PlanRep ulioboreshwa utatumika kuanzia ngazi ya msingi yaani vituo vya kutolea huduma za kijamii ikiwemo Zahanati,Hospitali na Shule.Mfumo huu wa kuandaa Mipango,Bajeti na Kutoa Ripoti utapunguza gharama kwa kiasi kikubwa zilizokuwa zikitumika awali kabla ya kuanza kwa mfumo huu mpya.

Kwa upande wake, Kiongozi wa Timu ya Mifumo ya TEHAMA kutoka mRadi wa PS3 Desderi Wengaa amesema kuwa lengo la mradi huu ni Uimarishaji Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) unatakekelezwa na Serikali ya Tanzania ukilenga kuimarisha Mifumo katika Sekta ya Umma ili kuboresha utoaji wa huduma za Serikali za Mitaa kwa Jamii hasa zile zenye uhitaji zaidi.

“Mradi huu unafanya kazi katika maeneo makuu matano ambayo ni Utawala Bora, Ushirikishwaji wananchi, Rasilimali watu, Rasilimali Fedha, Mifumo ya TEHAMA pamoja na Tathimini na ufutiliaji” alisema Desderi Wengaa.

Kiongozi huyo aliongeza kuwa, mfumo huu umesukwa na wataalamu wazalendowa hapa nchini na upo tayari kupokea mabadiliko kulingana na mahitaji ya wakati, na vilevile utasaidia kupunguza muda na gharama za uaandaaji wa Mipango na Bajeti.

Mradi wa uimarishaji Mifumo ya Sekta za Umma(PS3) ni mradi wa miaka mitano ulia mnamo Julai 2015 na kutarajiwa kukamilika Julai 2020 ambapo utarahisisha utendaji kazi na kusaidia kutatua changamoto zilizokuwepo awali.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma Bibi Rehema Madenge akifungua mafunzo kwa watumiaji wa Mfumo mpya wa Kielektroniki ulioboreshwa (PlanRep) yanayofanyika mjini Dodoma yakiwashirikisha Waganga Wakuu wa Mikoa,Halmashauri,Maafisa Mipango,Makatibu wa Afya,Wachumi na Wahasibu.
Mkurugenzi wa TEHAMA kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI bw. Erick Kitali akizungumza wakati wa hafla ya ufunguzi wa mafunzo hayo.
Kiongozi wa Timu ya Mifumo kutoka Kutoka mradi wa Uimarishaji Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) bw. Desderi Wengaa akitoa maelezo kuhusu utendaji wa Mfumo huo wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo mjini Dodoma.
Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma Bibi Rehema Madenge akiwa kwenye picha ya pamoja na sehemu ya washiriki wa mafunzo hayo mara baada ya hafla ya ufunguzi.Picha zote na Frank Mvungi-Maelezo Dodoma.

TAMSHA LA MICHEZO NA UTAMADUNI KUIMARISHA SEKTA YA UTALII KISIWANI PEMBA


Na Ali O. Ali
Afisa Mdhamini Wizara ya Habari Utalii Utamaduni na Michezo Mh. Khatibu Juma Mjaja ameelezea  matumaini yake ya mafanikio katika sekta ya utalii kisiwani Pemba kupitia tamasha la michezo na utamaduni lililoandaliwa na Taasisi ya Rafiki Network.
Akizungumza mara baada ya kupokea cheti cha shukrani Ofisisni kwake Chake Chake Bwana Mjaja amesema Rafiki Network imefungua njia katika kuimarisha utalii wa ndani na nje ya nchi kutokana na kuandaa na kusimamia Tamasha la kimichezo liloandaliwa kwa ubunifu na ustadi huku likijumuisha michezo mbali mbali ya asili ambayo niburudani kwa wenyeji na kivutio kwa wageni.
Mh. Mjaja ameuomba uongozi wa Taasisi ya Rafiki Network kuhakikisha kwamba Tamasha hili linakua endelevu ambapo amebainisha kwamba kuendelea kwa tamasha hilo kila mwaka kutasaidia kukuza hali za watu katika Nyanja mbali mbali kiuchu na kiutamaduni.
Akifafanua ubunifu uliofanyika katika maandalizi ya Tamasha la kimichezo Kisiswani Pemba, Mh. Mjaja amesifu uteuzi na mpangilio wa barabara zilizotumika katika mchezo wa mbio za Baiskeli nakuongeza kwamba mpangilio huo uliwapa fursa wananchi waliowengi kuweza kushiriki kikamilifu katika michezo mbali mbali. Afisa huyo pia amewapongeza Azam TV kwa kurusha matangazo ya moja kwa moja ya Bonanza hilo.
Nae Afisa Mdhamini Kamisheni ya Utalii Pemba Maalim Suleiman Amour Suleiman amepokea Cheti cha Shukrani kutoka kwa Taasisi ya Rafiki Network kutokana na mchango wake mkubwa katika kufanikisha Tamasha hilo.
Taasisi ya Rafiki Network iliandaa Tamasha la kimichezo Kisiwani Pemba mnamo Julai 28-30 ambalo lilijumuisha michezo mbali mbali ikiwa ni pamoja na mchezo wa Ng’ombe, Mashindano ya Baiskeli, Mashindano ya  kuogelea na Resi za Ngalawa.
 Afisa Mdhamini Wizara ya Habari Utalii Utamaduni na Michezo Mh. Khatibu Juma Mjaja akipokea Cheti cha Shukrani kutoka kwa Mkurugenzi wa Habari na Mahusiano wa Taasisi ya Rafiki Network Bw. Ali Othman Ali Ofisini kwake Chake Chake Pemba.
Afisa Mdhamini Kamisheni ya Utalii Maalim Suleiman Amour Suleiman akipokea Cheti cha Shukrani kutoka kwa Mkurugenzi wa Habari na Mahusiano wa Taasisi ya Rafiki Network Bw. Ali Othman Ali Ofisini kwake Chake Chake Pemba.

THE UNTOLD | THE WAIT IS OVER!!


 The much anticipated show 'UNTOLD' is now officially available on our YouTube channel UNTOLD. Our main goal is to Educate, Inspire and Entertain. You can now watch the first episode featuring Wasia Maya, who shares his life journey from Tanzania to the United States and talks about all the adversity he faced in his younger days. His story is truly exceptional and many of us can learn from it. 

TANESCO




Kampuni ya Acacia, kwa ushirikiano na TANESCO, imejenga kituo cha kupozea umeme kilichopo katika mgodi wake wa dhahabu wa Bulyanhulu ambacho kimeweza kuongeza uhakika wa upatikanaji wa umeme katika maeneo ya mgodi huo.

Acacia imewekeza shilingi bilioni 5.5 katika mradi huo ambao utanufaisha maeneo yanayozunguka migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu na maeneo mengine ikiwa ni pamoja na Kahama, Shinyanga, Msalala, na sehemu nyingine za Geita.

Ujenzi wa Kituo hicho ulianza Desemba 2016 na unatarajiwa kukamilika hivi karibuni.
Haya ni maendeleo makubwa kwa viwanda na biashara zinazozunguka eneo hilo ambazo zitafaidika na uwepo wa umeme wa uhakika jambo litakalosaidia kuboresha ufanisi na kuongeza uzalishaji.

Mkuu wa kitengo cha miradi ya maendeleo wa mgodi wa Bulyanhulu, Jiten Divecha ameeleza kuwa tatizo la mabadiliko ya nguvu ya umeme limekuwepo kwa muda mrefu na limekua likisababisha uharibifu mkubwa wa mashine.“Ujenzi wa kituo hiki utasaidia kupunguza athari zinazotokana na kuongezeka au kupungua kwa nguvu ya umeme katika migodi yetu hivyo kuboresha shughuli za uzalishaji. Wakazi na viwanda vinavyotumia umeme katika wilaya ya Msalala mkoani Shinyanga na wilaya zingine za mkoa wa Geita zitafaidika na uwekezaji huu pia,” alisema Jiten.

Aliongeza: "Acacia inajitahidi kuleta manufaa ya kiuchumi ya pamoja kwa jamii zinazotuzunguka na wadau wake kupitia miradi endelevu."
Wakati wa ujenzi wa kituo hicho, ajira mbalimbali zilitolewa kwa jamii zinazozunguka mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu.
Akizungumzia fursa hiyo, David Nyanda alisema: “tunathamini sana ujenzi wa mradi huu kwa sababu tumepata fursa za ajira. Japokuwa fursa hizi ni za muda, tunaweza kupata mapato ili kuendesha familia zetu hasa katika kipindi hiki cha ukame.”

Polisi yachunguza upya kifo cha Naji

Naji Al-AliHaki miliki ya pichaMET POLICE
Image captionNaji Al-Ali
Polisi wa Uingereza wamesema wanachunguza tena mauaji ya mchora Katuni wa Kipalestina Naji Al-Ali.
Alipigwa risasi wakati alipokuwa akitembea kuelekea ofisini kwake jijini London Julai 1997.
Naji al- Ali anajulikana zaidi kutokana na katuni zake ambazo zilikuwa zikichapishwa katika gazeti la Kuwaiti, na mara kadhaa alikuwa akiwashutumu viongozi wa Kiarabu na utawala.
Polisi wa mji wa London wamesema wanamatumaini kwamba watu ambao hawakutaka kuzungumza wakati mauaji yalipotokea pengine sasa wataweza kuzungumza.

Korea Kaskazini yaichokoza Japan

Kiongozi wa Korea kaskazini na makamanda wakeHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionKiongozi wa Korea kaskazini na makamanda wake
Korea kaskazini imerusha makombora yake ambayo yalipita Japan kabla ya kudondokea baharini.
Makombora hayo yalisafiri kuelekea mashariki karibu kilomita elfu moja juu ya kisiwa cha Japan cha Hokkaido.
Tukio hilo limechochea tahadhari ya hatari ambayo watu walielekezwa kujificha katika maeneo yaliyo chini ya ardhi ama kwenye majengo yaliyo imara.
Waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe amesema urushwaji huo wa makombora ambao haujawahi kutokea , umeleta kitisho kikubwa kwa taifa lake.
Hakuna juhudi zilizofanywa na Japan kulitengua kombora hilo lakini ilitoa onyo la kiusalama ikiwaambia raia wake katika eneo la Hokkaido kujificha chini ya majumba yaliojengwa ardhini.
Wanajeshi wa Marekani na Japan wanafanya zoezi la pamoja katika eneo hilo la Hokkado, rais wa Korea Kusini Moon Jae-in aliagiza uwezo wa utumiaji wa nguvu ili kujibu shambulio hilo.
Ndege nne za Korea Kusini zilifanya zoezi la kurusha makombora siku ya Tuesday.
Bwana Abe alisema kuwa amezungumza na rais wa Marekani Donald Trump na kwamba wote wamekubaliana kuiongezea shinikizo Korea Kaskazini.
Katika mfululizo wa majaribio yake ya makombora ya hivi karibuni Korea kaskazini haijawahi kurusha makombora yaliyopita juu ya ardhi ya nchi hiyo, hivyo tukio hili la sasa limeleta wasiwasi mkubwa.
Waziri mkuu wa japan Shinzo Abe amesema urushwaji huo wa makombora ambao haujawahi kutokea , umeleta kitisho kikubwa kwa taifa lake.Haki miliki ya pichaREUTERS
Image captionWaziri mkuu wa japan Shinzo Abe amesema urushwaji huo wa makombora ambao haujawahi kutokea , umeleta kitisho kikubwa kwa taifa lake.
Katika siku za hivi karibuni Pyongyang ilijaribu kombora lake lililopata mafanikio kutokana na uwezo wake wa kuweza kuifikia Marekani na kuonyoa kuwa inasimamia mipango yake ya kushambulia kwa makombora eneo la Marekani la Guam, kilomita elfu mbiili kusini mashariki mwa Japan.

Trump aagiza maafisa wa polisi kupewa vifaa vya kijeshi Marekani

Mwanasheria mkuu Jeff Sessions asema ni muhimu kwa polisi kupokea vifaa ili kufanya kazi yao vyemaHaki miliki ya pichaAFP
Image captionMwanasheria mkuu Jeff Sessions asema ni muhimu kwa polisi kupokea vifaa ili kufanya kazi yao vyema
Rais wa Marekani Donald Trump ameondoa marufuku iliowekwa na Obama kuhusu kuwapatia maafisa wa polisi vifaa vya kijeshi.
Agizo hilo la rais sasa litawaruhusu maafisa wa polisi kupokea vifaa vya kijeshi ikiwemo magari ya kijeshi na kofia zisozoweza kuingia risasi.
Mwanasheria mkuu Jeff Sessions amesema kuwa lengo lake kuu ilikuwa kuimarisha usalama miongoni mwa raia.
Bwana Obama alilizuia jeshi kutowapatia maafisa wa polisi vifaa vyake kufuatia mgogoro wa Missouri.
Marufuku hiyo ilifuatia shutuma kwamba maafisa wa polisi walikuwa wazito kupitia kiasi kukabiliana na waandamanaji kufuatia mauaji kijana mmoja mweusi yaliotekelezwa na polisi mzungu 2014.
Rais huyo wa zamani alikuwa na wasiwasi kuhusu maoni ya raia kuhusu maafisa wa polisi waliovalia magwanda mazito ya kijeshi akisema kuwa ilikuwa muhimu kwamba maafisa wa polisi walifaa kuonekana kuwa miongoni mwa jamii badala ya kuonekana kuwa maadui.
Lakini bwana Sessions alidai kwamba hatua hiyo ya Obama ilikuwa imepita mipaka.

Trump aizungumzia Texas

Mafuriko TexasHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionMafuriko Texas
Rais Donald Trump ameahidi kuliunga mkono jimbo la Texas katika kipindi hiki ambacho kimbunga Harvey kinaendelea kuharibu eneo hilo.
Wakati akijiandaa kwenda katika jimbo hilo leo, amesema kuyalinda maisha ya watu kutakuwa ni kipaumbelke cha kwanza kwake.
Amesema mchakato wa kulijenga tena eneo hilo utakuwa ni kazi ya muda mrefu na ngumu.
Mamilioni ya dola za Kimarekani zinahitajika, huku bunge la nchi hiyo la Congress likihitajika kuidhinisha fedha hizo.