Saturday, April 7

DC KIGAMBONI ATOA AMRI KWA WASIMAMIZI WA MRADI WA LAKE OIL KUFANYIWA MAHOJIANO MAALUM NA KAMATI YA ULINZI NA USALAMA


Mkuu wa wilaya ya kigamboni kwa kushirikiana na kamati ya ulinzi na usalama leo wametembelea kata ya Pemba mnazi eneo la Yaleyale panu kukagua utekelezaji wa maagizo aliyoyatoa Alhamisi ya wiki iliyopita walipokuwa wakikagua majengo yaliyopo pembezoni mwa fukwe za bahari.
Akiongea na vyombo vya habari katika matembezi hayo Mh.Hashim Mgandilwa amesema kuwa takribani wiki mbili zilizopita walikuwa wanatembelea maeneo ya fukwe za bahari ili kufanya ukaguzi kutokana na wilaya hiyo ya kigamboni kuwa lango la biashara haramu na wahamiaji halamu.


Pia amesema kuwa katika ukaguzi huo waliofanya eneo linalomilikiwa na mwekezaji wa Lake oil lilikutwa na tatizo kwa kuwa na gati linaloweza kutumiwa na chombo chochote cha maji katika kushusha na kupakia mzigo wowote na kuagiza gati hilo kubomolewa ndani ya siku tano lakini maagizo hayo yamekiukwa ambapo utejelezaji umeanza kutekelezwa leo kinyume na barua waliyoituma halimashauri ikionyesha utekelezaji huo kutendeka.
Hata hivyo mkuu wa wilaya akiwa kama mwenyekiti wa kamati ya usalama ameagiza kukamatwa kwa wahusika hao ili kufanyiwa mhojiano zaidi kwa sababu za kiusalama sambamba na kufika na vibali vinavyowaruhusu kufuga swala pamoja na hati miliki zinazoonyesha umiliki halali wa eneo hilo na kusisitiza kuwa kama hawatafanya hivyo watanyang’anywa eneo hilo na kukabidhiwa kwa mtu mwingine.
Viongozi hao waliokamatwa ni kiongozi mkuu wa miradi kutoka lake oil Fahim Mohammed na Mkurugenzi msaidizi wa lake oil Halid Mohammed, hata hivyo viongozi hao wamekana kukaidi agizo la mkuu wa wilaya na kuomba kupewa angalau muda wa mwezi mmoja kwani shughuli ya ubomoaji waliyoagizwa kufanya ni ngumu na inahitaji vifaa maalumu.
Kwa upande wake mwanasheria kutoka NEMC Manchale Heche amesema kuwa lake oil walipokea barua kutoka ofisi za NEMC ya kuwaruhusu kuendesha mradi pembezoni mwa bahari lakini hawakuruhusiwa kujenga nyumba za kudumu na walipewa masharti ambayo wameyakiuka.Hivyo Kufuatia ukiukwaji wa masharti hayo waliyopewa kutoka NEMC mwanasheria huyo amewafutia kibali cha kuendeleza mradi huo mpaka hapo watakapokutana na kufanya makubaliano ya kupata kibali kingine na kufuata masharti kama sheria inavyosema

JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI LAFUNGA MAFUNZO YA UZAMIAJI MAJINI KINA KIREFU

Kamishna wa Operesheni wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, (CF) Billy Mwakatage, akipokelewa na Maafisa wa Jeshi hilo pamoja na mwenyeji wake ambaye ni mmiliki wa Yatch Club Bw. Brian Fernandes, alipokwenda kufunga mafunzo ya uzamiaji majini kina kirefu daraja la pili kwa Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji. Mafunzo hayo yalikuwa yakifanyika katika kisiwa cha Bongoyo kilichopo ndani ya bahari ya hindi, Jijini Dar es Salaam.
Mzamiaji wa kikosi maalum cha Uokoaji majini wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Sajini Gift Longwe, akionesha mbinu mbalimbali za uzamiaji majini kwenye kina kirefu walizojifunza toka kwa wakufunzi kutoka nchini Ujerumani,  kwa mgeni rasmi Kamishna wa Operesheni wa Jeshi hilo, (CF) Billy Mwakatage (hayupo pichani). Wakati wa hafla ya kufunga mafunzo ya uzamiaji majini kina kirefu daraja la pili kwa Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, mapema leo Jijini Dar es Salaam. 
Kamishna wa Operesheni wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, (CF) Billy Mwakatage (katikati), akimkabidhi cheti mmoja ya wahitimu wa mafunzo ya uzamiaji majini kina kirefu, Sajini Gift Longwe (kushoto). Wakati wa hafla ya kufunga mafunzo ya uzamiaji majini kina kirefu daraja la pili kwa Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, mapema leo Jijini Dar es Salaam. 
Wazamiaji wa kikosi maalum cha Uokoaji majini wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Sajini Gift Longwe (kushoto) na Koplo Siwizan Kazimoto (kulia), wakionesha umahili wao wa uzamiaji majini kwenye kina kirefu mbele ya mgeni Kamishna wa Operesheni wa Jeshi hilo, (CF) Billy Mwakatage (hayupo pichani). Wakati wa hafla ya kufunga mafunzo ya uzamiaji majini kina kirefu daraja la pili kwa Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, mapema leo Jijini Dar es Salaam. (Picha na Jeshi la Zimamoto Na Uokoaji)

WAMBURA AJIBU MAPIGO TFF BAADA KUTUPILIA MBALI RUFAA YAKE

Na Bakari Madjeshi, Globu ya Jamii

ALIYEKUWA Makamu wa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania(TFF), Michael Wambura ameamua kufunguka na kujibu hoja ambazo zimetolewa dhidi yake.

Wambura ameweka wazi kujibu hoja moja baada ya nyingine kuhusu rufaa iliyosomwa jana na Kamati Rufani ya Maadili ya TFF.

Rufaa ya Wambura ilitupiliwa mbali baada ya Kamati ya Rufaa kuona haina mashiko.

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo, Wambura amesema yeye pamoja na jopo lake la Mawakili wanasubiri hukumu ya rufaa hiyo (Jumatatu) ili kuijadili kwa kina kuhakikisha rufaa inaendelea.

Amesema yaliyosomwa jana katika rufaa yake si yale yalioandikwa wakati wakupeleka rufaa hiyo.Amedai kuwa suala hilo lakisheria limetoka katika Mpira na badala yake linakwenda katika maisha yake binafsi.

Kuhusu Kesi ya Simba, Wambura amesema kuwa kesi hiyo ilifutwa tangu 13/4/2017, amesema haikuwa na mashiko mbele yake.Kwa upande wa Wakili wake, Emmanuel Muga amedai Kamati iliyotoa uamuzi ilibadirishwa kwa baadhi ya Wajumbe, amedai Kamati haikuwa halali.

KATIBU WA BUNGE AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA KAMATI NDOGO TUME YA UTUMISHI WA BUNGE JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI.

Mwenyekiti wa kamati ndogo ya Tume ya Utumishi wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki, Mhe. Susan Nsambu (kushoto) akizungumza na Katibu wa Bunge, Ndg. Stephen Kagaigai (kulia) pale ugeni kutoka Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki ulipomtembelea leo tarehe 7 MachI, 2018 ofisini kwake Mjini Dodoma. Kwa lengo la kubadilishana uzoefu kwenye mambo ya ajira ya wafanyakazi, nidhamu, maendeleleo na maslahi ya wafanyakazi


Katibu wa Bunge, Ndg. Stephen Kagaigai (kulia) akizungumza na Mwenyekiti wa kamati ndogo ya Tume ya Utumishi wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki, Mhe. Susan Nsambu (kushoto) pale ugeni huo ulipomtembelea leo tarehe 7 Machi, 2018 ofisini kwake Mjini Dodoma, kwa ajili kubadilishana uzoefu kwenye mambo ya ajira ya wafanyakazi, nidhamu, maendeleleo na maslahi ya wafanyakazi.


Wajumbe wa kamati ndogo ya Tume ya Utumishi wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki wakifuatilia kikao kati yao na Katibu wa Bunge, pamoja na Baadhi ya Wakurugenzi wa Ofisi ya Bunge kikilenga kubadilishana uzoefu kwenye mambo ya ajira ya wafanyakazi, nidhamu, maendeleleo na maslahi ya wafanyakazi. Kutoka kushoto ni Mhe. Leontine Nzeyimana, Mhe. Aden Abdikadir (wa pili kushoto), Mhe. Dkt. Anne Leonardo (watatu kushoto) na Mkurugenzi wa Shughuli za Bunge, Ndg. Nenelwa Wankanga (kulia)
 

Wajumbe wa kamati ndogo ya Tume ya Utumishi wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki walioongozwa na Mwenyekiti wa kamati hiyo, Mhe. Susan Nsambu (watatu kulia) wakiwa katika kikao cha pamoja na baadhi ya Wakurugenzi wa Ofisi ya Bunge walioongozwa na Katibu wa Bunge, Mhe. Stephen kagaigai (wa pili kulia) kwa lengo la kubadilishana uzoefu kwenye mambo ya ajira ya wafanyakazi, nidhamu, maendeleleo na maslahi ya wafanyakazi. 


Katibu wa Bunge, Ndg. Stephen Kagaigai (wa pili kulia) akiwa katika picha ya pamoja na ugeni kutoka Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki ulioongozwa na Mwenyekiti wa kamati ndogo ya Tume ya Utumishi wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki, Mhe. Susan Nsambu (watatu kulia) pale ugeni huo ulipomtembelea leo tarehe 7 Machi, 2018 ofisini kwake Mjini Dodoma, kwa ajili ya kubadilishana uzoefu kwenye mambo ya ajira ya wafanyakazi, nidhamu, maendeleleo na maslahi ya wafanyakazi 

WADAU WA USAFIRI TABORA WATAKA MALORI NAYO YATUMIE “LOG BOOK” KUDHIBITI AJALI


Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri (katikati) akifafanua jambo jana wakati wa kikao cha kujitathimini kwa ajili ya kuja na majibu ya kuondoa ajali za barabarani mkoani humo kichofanyika jana Wilayani Igunga na kuhudhuriwa na Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Tabora na ile ya Wilaya ya Igunga na wadau mbalimbali wa usafiri. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Igunga John Mwaipopo na kushoto ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora Wilbroad Mtafungwa. 

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri (aliye na kofia ya kijani) akiwa kwenye ilipotokea ajali ya Basi la City Boy kugonagana uso kwa uso na lori siku ya Jumatano usiku. 

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri akiliangalia Basi la City Boy lilopata ajali ya kugonagana uso kwa uso na lori siku ya Jumatano usiku mara baada kuongozana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa na ile ya Wilaya ya Igunga kutembelea eneo la tukio. 
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri (mwenye kofia ya kijani) na Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa na ile ya Wilaya ya Igunga wakiliangalia Basi la City Boy lilopata ajali ya kugonagana uso kwa uso na lori siku ya Jumatano usiku. 
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri akiwafariji majeruhi wa ajali ya Basi la City Boy iliyogongana uso kwa uso na lori siku ya Jumatano usiku mara baada kutoka katika ilipotokea ajali wilayani Igunga 

………………. 

NA TIGANYA VINCENT 

RS TABORA 

KAMATI ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Tabora na Wadau wa Usafiri wamependekeza uanzishwaji wa matumizi ya vitabu(log book) kwa magari ya mizigo ili kudhibiti madereva kusafiri mwendo mrefu bila kupumzika na hivyo kusababisha ajali kwa magari yao au kugongana uso kwa uso na magari mengine kutokana na uchovu. 

Tamko hilo limetolewa jana wilayani Igunga na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri mara baada ya kikao cha kujitathimini kwa ajili ya kuja na majibu ya kuondoa ajali za barabarani mkoani humo. 

Mkuu huyo wa Mkoa alisema vitabu hivyo vitasaidia kuonyesha muda alitoka , mahali alitoka na kama amesafiri muda mrefu atalazimisha apumzike ili kuepusha ajali. 

Alisema malori yamekuwa yakisafiri mwendo mrefu bila hata dereva wake kupumzika jambo ambalo limesababisha magari hayo yapate ajali au wakati mwingine yawe chanzo kinachosabisha ajali katika magari ya abiria. 

Mwanri alisema kwa kulitambua hilo wanaona wakati umefika kwa magari ya mizigo nayo kuwa na vitabu(log book ) inayoonyesha muda alianza safari katika kituo chake cha kwanza na muda alipo baada ya kusimamishwa ili kuona kama kweli amezingatia matawaka ya kitaalamu na sharia ya kutokwenda kasi. 

Alisema kitaalamu dereva anatakiwa aendeshe chombo cha moto kwa muda usiozidi saa nane lakini mara nyingi madreva wa malori wamekuwa wakiendesha magari yao hata zaidi ya muda huo jambo ambalo limekuwa kiwasababisha baadhi yao kuendesha huko wakisinzia na kupelelea gari kukosa mwelekeo. 

Mwanri alisema ili kuepukana na hilo wadau wamependekeza wammiliki wa gari wa ya mizigo ya masafa marefu ni vema wawe na madereva wawili ili wasaidiane. 

Mkuu huyo wa Mkoa alisema hatua nyingine ambayo wameamua kuichukua ni pamoja na kuongeza askari na magari ya doria katika barabara kuu ya Igunga, Nzega kwenda Mwanza na Shinyanga. 

Alisema hatua hii inalenga kupambana na madreva ambao nyakati za usiku wakwenda mwendo mkali kwa sababu ya kujua kuwa nyakati hizo tochi hazifanyi kazi. 

Mwanri aliongeza kuwa Wadau wa usafiri wameiagiza Wakala wa Barabara Tanzania(TANROADS) mkoani Tabora kuhakikisha wanaziba mashimo yaliypo katika barabara kuu zote ili kuondoa uwezekano wa yenyewe kuwa chanzo cha ajali za barabarani. 

Aidha alisema kuwa Wadau wamekuwabaliana kuwa ukaguzi wa madereva na magari katika barabara kuu zinazopita Mkoani Tabora utakuwa unafanyika kila siku ili kujihakikishia kama gari linazo breki, taa zifanya kazi vizuri , matari yako vizuri na dreva ajatumia kilevi. 

Alisema hatua hiyo inalenga kujihakikishia kama chombo cha usafiri na dreva wake yuko katika hali nzuri. 

Hivi karibuni (4 /4/2018) kulitokea ajali ambapo basi la abiria Kampuni ya City Boy yenye namba T 983 DCE iligongana uso kwa uso lori lenye namba T .486 ARB Mitsubishi Fuso wilayani Igunga na kusababisha watu 12 kufa palepale na mmoja kufia katika Hospitali ya Rufaa Bugango. 

Taarifa za awali zinaoonyesha kuwa chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi wa dereva wa Fuso uliosababisha tairi kupasuka na gari kuhamia upande wa basi. 

Lori hiyo lilikuwa na viazi ambavyo lilivitoa Njombe Mwisho

LAZIMA WAWEPO MADEREVA WAWILI KWA MABASI YAENDAYO MIKOANI-KAMANDA MWANGAMILO

JESHI la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Kinondoni kimesema mabasi yanayofanya safari za mikoani na nchi jirani lazima wawepo  madereva wawili na hilo haliepukiki.

Akizungumza na Michuzi Blog, leo Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Kinondoni jijini Dar es Salaam Solomon Mwangamilo amesema ukaguzi wa mabasi na madeva wawili ni endelevu katika kuhakikisha abiria wanasafiri salama.

Mwangamilo amesema wamiliki mabasi wahakikishe wanazingatia usalama wa mabasi na abiria.Pia wahakikishe kunakuwa na madereva wawili ambao watapokeza kuendesha wakiwa safarini.Amesema basi likitoka katika kituo cha Ubungo lazima madereva wawili wasaini na mpaka wanafika katika kituo chao mwisho wanahakikiwa, hivyo hakuna mtu anayeweza kufanya udanganyifu kutokana na mtando uliopo katika jeshi la Polisi.

Mwangamilo amesema wanaoingiza mabasi ambayo mabovu na kutegemea wataondoka na abiria kituo cha mabasi Ubungo wanajidanganya  na wataofanya hivyo watakwenda jela.“Kazi yetu ni kuhakikisha wananchi wanasafiri na mabasi yakiwa salama kutokana ukaguzi unaofanyika kila kukicha na hakuna basi litakaloachwa huku likiwa lina ubovu wa kuhatarisha watumiaji wa usafiri huo” amesema Mwangamilo.


Aidha amesema askari katika mkoa wa Kinondoni hasa kituo cha mabasi Ubungo kuwa kufanya kazi ya ukaguzi bila kikomo katika kuwalinda usalama wa abiria wanatumia mabasi ya mikoani na nchi jirani.
Mkaguzi Polisi wa Kikosi cha Usalama Barabani wa Kituo cha Mabasi Ubungo, Ibrahim Samwix akifanya ukaguzi basi la Kampuni ya Tokyo Takara katika kituo hcho leo jijini Dar es Salaam.
Mkaguzi Polisi wa Kikosi cha Usalama Barabani wa Kituo cha Mabasi Ubungo, Ibrahim Samwix akifanya ukaguzi basi la Kampuni ya Tokyo Takara katika kituo hcho leo jijini Dar es Salaam.
Askari wa Usalama Barabarani Kituo Kikuu cha Mabasi Ubungo , Nuru Hussein akimpa maelekezo dereva wakati wakifanya ukaguzi mabasi kutuo hicho, leo jijini Dar es Salaam.
Abiria wakishuka katika Basi la Princess Line linalofanya safari zake Dar es Salaam ,Babati baada ya Basi hilo kuonekana na hitilafu takiribani ya masaa manne katika kituo cha Ubungo na kufanya kampuni kuwabadilishia basi lingine.
Askari wa Usalama Barabani katika kituo kikuu cha Ubungo, Koplo Rashid Abdallah akizungumza na abiria walio kaa zaidi ya masaa manne katika Basi la Princess Line, leo .jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Mabasi yalikutwa na kamera yetu katika kituo kikuu cha mabasi Ubungo

RAIS DKT MAGUFULI ATANGAZA AJIRA MPYA 1500 POLISI,ATAKA JKT WAPEWE KIPAUMBELE ,SI WATOTO WA VIGOGO


Na Ripota Wetu,Globu ya jamii

RAIS Dk.John Magufuli ametangaza nafasi 1500 za ajira mpya kwa Jeshi la Polisi nchini huku akitoa maelekezo, anataka vijana wa JKT ndio wapewe nafasi hizo na si kutafuta ndugu,jamaa na marafiki wa makamanda wa wilaya na mikoa.

Amesema kuna tabia imejengeka  pale inapotokea nafasi za ajira kwa ajili ya jeshi la polisi,baadhi ya makamanda wanatafuta watu wao na hivyo hata wakienda kwenye mafunzo wanapewa mafunzo kwa kuangalia waliowapeleka.

Rais Magufuli ametoa tangazo hilo wakati anazungumza na wananchi wa Mkoa wa Arusha baada ya tukio la kuzindua nyumba npya za Polisi zilozojengwa kwa ushirikiano wa Serikali na wadau wa maendeleo wa mkoa huo.Ambapo ameagiza nyumba hizo wapewe askari wa vyeo vya chini.

Amesema kutokana na kutambua na kuthamini kazi kubwa inayofanywa na Jeshi la Polisi nchini kwa kuhakikisha nchi inakuwa salama hivyo ameamua kutoa ajira mpya 1500 na kufafanua anataka kuona wanaopata ajira hiyo ni watoto wa masikini na si vinginevyo.

"Nataka hizi nafasi ambazo nimezitangaza hapa leo hii zielekezwe kwa JKT ambazo waliamua kujitolea kupata mafunzo na kwa sehemu ni vijana ambazo hawana ndugu, kamanda wa Polisi,mkoa au kiongozi wa serikali." Bali ni vijana ambao wanatoka familia masikini.Hivyo niombe kipaumbele cha ajira hiyo kielekezwe kwa vijana waliopita JKT.Tabia  ya kusikia wanaopewa nafasi ni ndugu wa wakubwa hapana,"amesema Rais Magufuli.

Pia amezungumzia namna ambavyo Jeshi la Polisi linafanya kazi vizuri ya kulinda usalama wa raia na mali zao huku akielezea wakati ameingia madarakani kuliibuka mauaji katika wilaya ya Kibiti na Mkuranga mkoani Pwani.Amefafanua katika mauaji hayo watu 59 wamepoteza maisha na kati yao wamo askari 17 ambao wamepoteza maisha wakati wakilinda usalama wa wananchi wa maeneo hayo.

 Dk.Magufuli amesema askari waliopoteza maisha Kibiti walikuwa na nia ya kuhakikisha nchi inakuwa salama na kimsingi ni Polisi ambao ni watoto wa watanzania masikini.Hivyo amesema hata hivyo polisi wamefanya kazi kubwa ya kuhakikisha mauaji hayo yanakoma na leo kuko salama na hata kama waliokuwa wanatekeleza mauaji  hayo bado wapo Polisi wamejipanga na wanaendelea kuimairisha ulinzi.

"Nakumbuka wakati wa mauaji ya Kibiti yakiendelea hali ilikuwa mbaya,wananchi waliokuwa wanaogopa kufanya shughuli za maendeleo,hata shamba kukawa hakuendeki.Nilitoa maagizo ambayo Jeshi la Polisi wameyafanyia kazi.Hivyo kutoka moyoni kwangu nawapongeza.

" Endeleeni na majukumu yenu na kila ambacho mnakifanya ili nchi ibaki salama mimi nawasapoti.Hivyo huu uamuzi wa kutoa ajira mpya ni kuonesha namna navyotambua majukumu yenu,"amesema Rais Magufuli.

Kuhusu changamoto zinazowabili Polisi amesema anatambua wanakabiliwa na changamoto nyingi za kimaisha na kwamba hata mkewe Mama Janet Magufuli amekuwa akimueleza kwani baba yake ni Polisi."Baba mkwe wangu ni Polisi,mke wangu anajua shida ambazo Polisi hasa wa chini wanazipata,amekaa kota za Polisi Moshi na zile za Ukonga.Baba yake alikua askari Polisi wa vyeo vya chini.Hivyo Polisi mimi ni shemeji yenu na najua shida zenu," amesema Rais Magufuli.

Kuhusu wanaostahili kupandishwa vyeo,Rais ameahidi kulishughulikia hill ingawa ametoa angalizo kwenye sifa za kupanda vyeo wapandishwe badala ya watu kupewa vyeo kwa upendeleo.Amesema kutoa vyeo kwa upendeleo kutakatisha tamaa wengine,hivyo utakapofika wakati haki itendeke na atafuatilia.

Akizungumzia ujenzi wa nyumba hizo amesema umegharimu kati ya Sh.milioni 700 hadi Sh.milioni 800 na swali analojiuliza je akitoa fedha ili zijengwe nyumba kama hizo kwa kila mkoa itawezekana maana hayo ndio mashaka yake kila siku.Ametoa mwito kwa wafanyabiashara nao kuiga mfano wa wenzao wa Arusha ambao wamechangia ujenzi wa nyumba za Polisi huku akiwataka wabunge kupitia fedha za mfuko wa maendeleo ya jimbo kuchangia ujenzi wa nyumba za Polisi.

Amesema akiwa mbunge Jimbo la Chato alichanga Sh.milioni 25 kwa ajili ya nyumba za Polisi na baada ya yeye kuchanga wakatokea wengine nao wakamsaidia katika kufanikisha ujenzi katika jimbo lake la Chato.

SERIKALI YAPATA MKOPO WA SHILINGI BILIONI 34 KUTOKA MFUKO WA MAENDELEO YA KIUCHUMI WA KUWAIT



Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango (SERA), Dkt. Khatibu Kazungu (kushoto) na Kiongozi wa ujumbe wa wataalamu na Mshauri wa Masuala ya Kilimo wa Mfuko wa Maendeleo ya Kiuchumi wa Kuwait (Kuwait for Arab Economic Development Fund), Dkt. Abdulrida Bahman, wakibadilishana rasimu ya mkataba wa mkopo wa dola milioni 15.3 za Marekani, kwa ajili wa kujenga mradi wa kilimo cha umwagiliaji maji katika Bonde la Luiche, mkoani Kigoma,

Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kulia), akiagana na Kiongozi wa ujumbe wa wataalamu na Mshauri wa Masuala ya Kilimo wa Mfuko wa Maendeleo ya Kiuchumi wa Kuwait (Kuwait for Arab Economic Development Fund), Dkt. Abdulrida Bahman, baada ya tukio la kusainiwa kwa rasimu ya mkataba wa mkopo wa dola milioni 15.3 za Marekani, kwa ajili wa kujenga mradi wa kilimo cha umwagiliaji maji katika Bonde la Luiche, mkoani Kigoma, tukio lililofanyika mjini Dodoma.
Ujumbe wa wataalamu kutoka Mfuko wa Maendeleo ya Kiuchumi wa Kuwait (Kuwait for Arab Economic Development Fund), ukiongozwa na Dkt. Abdulrida Bahman (wa tano kutoka kulia), na ujumbe kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, ukiongozwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (wa nne kutoka kulia), wakiwa katika picha ya pamoja nje ya Makao Makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango Mjini Dodoma, baada ya tukio la kusainiwa kwa rasimu ya mkataba wa mkopo wa dola milioni 15.3 za Marekani, kwa ajili wa kujenga mradi wa kilimo cha umwagiliaji maji  katika Bonde la Luiche, mkoani Kigoma.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango (SERA), Dkt. Khatibu Kazungu (kushoto) akisaini rasimu ya mkataba wa mkopo wa dola milioni 15.3 za Marekani kutoka Mfuko wa Maendeleo ya Kiuchumi wa Kuwait (Kuwait for Arab Economic Development Fund), kwa ajili wa kujenga mradi wa kilimo cha umwagiliaji maji katika Bonde la Luiche, mkoani Kigoma.
Ujumbe wa wataalamu kutoka Mfuko wa Maendeleo ya Kiuchumi wa Kuwait (Kuwait for Arab Economic Development Fund), ukiongozwa na Dkt. Abdulrida Bahman (kushoto), wakisikiliza maelezo kutoka kwa Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango (Mb) (hayupo pichani), kabla ya tukio la kusainiwa kwa rasimu ya mkataba wa mkopo wa dola milioni 15.3 za  Marekani, kwa ajili wa kujenga mradi wa kilimo cha umwagiliaji maji katika Bonde la Luiche, mkoani Kigoma.
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango (Mb) (kulia), akiongoza mazungumzo kabla ya tukio la kusainiwa kwa rasimu ya mkataba wa mkopo  wa dola milioni 15.3 za Marekani, sawa na zaidi ya shilingi bilioni 34 kutoka Mfuko wa Maendeleo ya Kiuchumi wa Kuwait (Kuwait for Arab Economic Development Fund), kwa ajili wa kujenga mradi wa kilimo cha umwagiliaji maji katika Bonde la Luiche, mkoani Kigoma.

Kiongozi wa ujumbe wa wataalamu na Mshauri wa Masuala ya Kilimo wa Mfuko wa Maendeleo ya Kiuchumi wa Kuwait (Kuwait for Arab Economic Development Fund), Dkt. Abdulrida Bahman, akitia saini rasimu ya mkataba wa mkopo wa dola milioni 15.3 za Marekani, kwa ajili wa kujenga mradi wa kilimo cha umwagiliaji maji katika Bonde la Luiche, mkoani Kigoma.

Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kulia), akiagana na mmoja wa wajumbe kutoka Mfuko wa Maendeleo ya Kiuchumi wa Kuwait (Kuwait for Arab Economic Development Fund), Dkt. Abdulrida Bahman, baada ya tukio la kusainiwa kwa rasimu ya mkataba wa mkopo wa dola milioni 15.3 za Marekani, sawa na zaidi ya shilingi bilioni 34.4, kwa ajili wa kujenga mradi wa kilimo cha umwagiliaji maji katika Bonde la Luiche, mkoani Kigoma, tukio lililofanyika mjini Dodoma.(Picha na Kitengo cha Mawasiliano-Wizara ya Fedha na Mipango)


Na Benny Mwaipaja, WFM, Dodoma

Serikali ya Kuwait kupitia Mfuko wa Maendeleo wa Kiuchumi wa Kuwait (Kuwait for Arab Economic Development Fund), na Serikali ya Tanzania zimetiliana saini rasimu ya mkataba wa kuipatia Tanzania mkopo wenye masharti nafuu wa dola milioni 15.3, sawa na zaidi ya shilingi bilioni 34, kwa ajili ya mradi wa kilimo cha umwagiliaji katika Bonde la Luiche, mkoani Kigoma, lenye ukubwa wa hekta 3,000.

Rasimu hiyo ya Mkataba imesainiwa na Kiongozi wa ujumbe wa wataalamu na Mshauri wa Masuala ya Kilimo wa Mfuko wa Maendeleo ya Kiuchumi wa Kuwait, Dkt. Abdulrida Bahman na kwa upande wa Tanzania ikisainiwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Khatibu Kazungu, mjini Dodoma.Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) amesema hatua hiyo imfikiwa baada ya timu ya wataalamu kutoka Kuwait kutembelea eneo la mradi mkoani Kigoma na kuridhishwa na umuhimu wake kiuchumi kwa wananchi wa mkoa huo na taifa kwa ujumla.
 
“Mradi huo una umuhimu mkubwa kwa watanzania kwa kuwa wataweza kuwa na kilimo cha umwagiliaji cha Mpunga na Mbogamboga kwa mwaka mzima badala ya kilimo cha msimu cha kutegemea mvua, na katika siku zijazo Kigoma itakua miongoni mwa mikoa inayozalisha mchele kwa wingi”, alisema Dkt. Mpango.
 
Dkt. Mpango amesema kuwa Serikali ya Tanzania na Kuwait zitatia saini mkataba rasmi wa mkopo huo wenye masharti nafuu ifikapo mwishoni mwa mwezi Juni mwaka huu ili mradi huo uanze kutekelezwa ili kuongeza kipato cha wananchi na kuwa na uhakika wa chakula.Amesema Nchi ya Kuwait imekuwa ikiisaidia Tanzania katika kutekeleza miradi mbalimbali ikiwemo ya ukarabati wa Hospitali ya Mnazi mmoja, Zanzibar kwa kiasi cha dola za Marekani milioni 13.6 sawa na shilingi bilioni 31.
 
”Kwa upande wa Tanzania Bara wametoa mkopo nafuu wa shiingi bilioni 115 kwa ajili ya kuboresha barabara ya Chaya hadi Nyahua (km 85) kwa kiwango cha lami ambayo ni muhimu kwa kuwa inaunganisha mikoa ya Magharibi mwa Tanzania” aliongeza Dkt. MpangoMiradi mingine ambayo nchi hiyo imeonesha nia ya kuisaidia nchi, ni pamoja na ujenzi wa jengo la abiria katika Uwanja wa Ndege wa Mwanza, uboreshaji wa barabara ya kutoka Morogoro hadi Dodoma na ujenzi wa barabara za mzunguko za kuingia na kutoka mjini Dodoma ambazo zitasaidia kuondoa msongamano wa magari yanayopita katikati ya mji huo kutokana na kuongezeka kwa idadi ya watu na vyombo vya moto baada ya Makao Makuu ya Serikali kuhamia Dodoma.
 
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Mpango ameishukuru nchi ya Kuwait kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Kiuchumi wa Kuwait, kwa nia yake njema na thabiti katika kusaidia nchi ya Tanzania kutekeleza kwa mafanikio miradi ya Maendeleo ya kiuchumi katika nia yake ya kupata maendeleo Stahiki.

Kwa upande wake Kiongozi wa ujumbe wa wataalamu na Mshauri wa Masuala ya Kilimo wa Mfuko wa Maendeleo ya Kiuchumi wa Kuwait, Dkt. Abdulrida Bahman, ameishukuru Serikali ya Tanzania kupitia Waziri wa Fedha na Mipango kwa ukarimu pamoja na Idara ya Taifa ya Umwagiliaji kwa ushirikiano mzuri katika hatua za kufanikisha utekelezaji wa mradi wa umwagiliaji wa Bonde la Luiche, Mkoani Kigoma.

“Tumetembelea eneo la mradi kwa takribani wiki mbili tumejionea uzuri wa nchi hii na fursa zilizopo, hii ni nchi tajiri na inaweza kuwa tajiri kuliko Kuwait kwa kuwa kila kitu kinachoweza kufanya nchi hii iwe tajiri kipo”.Alieleza Dkt. Bahman.
 

Amesema mradi huo wa umwagiliaji hautakuwa wa mwisho kupewa fedha na mfuko huo bali utaendelea kusaidia kutekeleza miradi mingine mingi kama ilivyokuwa ikifanya, kutokana na ushirikiano mzuri, wa kihistoria, na wa muda mrefu kati ya nchi hizo mbili.

RAIS DKT MAGUFULI AZINDUA NYUMBA ZA MAKAZI YA ASKARI POLISI NA KUSHUHUDIA MAZOEZI YA MEDANI KATIKA SIKU YA KARUME JIJINI ARUSHA


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo alipowasili kuzindua kituo maalumu ya Jeshi la Polisi cha Utalii na Diplomasia  jijini Arusha ambacho kimejengwa na wadau wa utalii  kwenye sherehe zilizofanyika leo Aprili 7, 2018
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mbuneg wa Viti Maalum Arusha Mhe. Catherine Magige alipowasili kuzindua kituo maalumu ya Jeshi la Polisi cha Utalii na Diplomasia  jijini Arusha ambacho kimejengwa na wadau wa utalii  kwenye sherehe zilizofanyika leo Aprili 7, 2018
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipata maelezo ya ujenzi wa kituo maalumu ya Jeshi la Polisi cha Utalii na Diplomasia  jijini Arusha ambacho kimejengwa na wadau wa utalii  kwenye sherehe zilizofanyika leo Aprili 7, 2018
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipata maelezo ya ujenzi wa kituo maalumu ya Jeshi la Polisi cha Utalii na Diplomasia  jijini Arusha ambacho kimejengwa na wadau wa utalii  kwenye sherehe zilizofanyika leo Aprili 7, 2018
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na viongozi wengine wakiwa katika picha ya pamoja na wadau waliosaidia  ujenzi wa kituo maalumu cha Jeshi la Polisi cha Utalii na Diplomasia  jijini Arusha  kwenye sherehe zilizofanyika leo Aprili 7, 2018
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru mmoja wa wadau waliosaidia  ujenzi wa kituo maalumu cha Jeshi la Polisi cha Utalii na Diplomasia  jijini Arusha  kwenye sherehe zilizofanyika leo Aprili 7, 2018
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe akiwa na viongozi wengine pamoja na wadau waliosaidia  ujenzi wa kituo maalumu cha Jeshi la Polisi cha Utalii na Diplomasia  jijini Arusha  kwenye sherehe zilizofanyika leo Aprili 7, 2018 
Msanii Maringo wa Maringo akiwa tayari kutumbuiza wakati  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wa hafla ya uzinduzi wa kituo maalumu cha Jeshi la Polisi cha Utalii na Diplomasia  jijini Arusha  kwenye sherehe zilizofanyika leo Aprili 7, 2018 
 Sehemu ya nyumba za makazi ya askari ya polisi za Naura zilizojengwa upya baada ya kuteketea kwa moto kwenye sherehe zilizofanyika jijini Arusha leo Aprili 7, 2018 

 Sehemu ya nyumba za makazi ya askari ya polisi za Naura zilizojengwa upya baada ya kuteketea kwa moto kwenye sherehe zilizofanyika jijini Arusha leo Aprili 7, 2018 

 Wana bendi ya Jeshi la Polisi kikiwa tayari kufanya kazi wakati wa sherehe za uzinduzi wa nyumba za makazi ya askari ya polisi za Naura zilizojengwa upya baada ya kuteketea kwa moto kwenye sherehe zilizofanyika jijini Arusha leo Aprili 7, 2018 

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo  na Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro  wakifunua pazia kuashiria kufunguliwa rasmi kwa nyumba za makazi ya askari ya polisi za Naura zilizojengwa upya baada ya kuteketea kwa moto kwenye sherehe zilizofanyika jijini Arusha leo Aprili 7, 2018 

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuliakipeana mikono na IGP Simon Sirro baada ya kuzindua rasmi kwa nyumba za makazi ya askari ya polisi za Naura zilizojengwa upya baada ya kuteketea kwa moto kwenye sherehe zilizofanyika jijini Arusha leo Aprili 7, 2018 
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipeana mikono na RPC wa Arsuah Charles Mkumbo  baada ya kuzindua rasmi kwa nyumba za makazi ya askari ya polisi za Naura zilizojengwa upya baada ya kuteketea kwa moto kwenye sherehe zilizofanyika jijini Arusha leo Aprili 7, 2018 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisaidiwa  na viongozi wengine akikata utepe  kuashiria kufunguliwa rasmi kwa nyumba za makazi ya askari ya polisi za Naura zilizojengwa upya baada ya kuteketea kwa moto kwenye sherehe zilizofanyika jijini Arusha leo Aprili 7, 2018 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea baada ya kuzindua rasmi kwa nyumba za makazi ya askari ya polisi za Naura zilizojengwa upya baada ya kuteketea kwa moto kwenye sherehe zilizofanyika jijini Arusha leo Aprili 7, 2018 
Jiwe la uzinduzi wa  nyumba za makazi ya askari ya polisi za Naura zilizojengwa upya baada ya kuteketea kwa moto kwenye sherehe zilizofanyika jijini Arusha leo Aprili 7, 2018 
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiaga wananchi wenye furaha  baada ya kuzindua rasmi kwa nyumba za makazi ya askari ya polisi za Naura zilizojengwa upya baada ya kuteketea kwa moto kwenye sherehe zilizofanyika jijini Arusha leo Aprili 7, 2018 
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na baasdhi ya wanafamilia wa Jeshi la Polisi  baada ya kuzindua rasmi kwa nyumba za makazi ya askari ya polisi za Naura zilizojengwa upya baada ya kuteketea kwa moto kwenye sherehe zilizofanyika jijini Arusha leo Aprili 7, 2018 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akipokea saluti ya heshima baada ya kuwasili katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha   kuadhimisha siku ya kumbukumbu ya miaka 46 ya kifo cha Rais wa kwanza wa Zanzibar  Hayati Sheikh Abeid Amani Karume leo Aprili 7, 2018
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akikagua gwaride la askari polisi  katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha  kuadhimisha siku ya kumbukumbu ya miaka 46 ya kifo cha Rais wa kwanza wa Zanzibar  Hayati Sheikh Abeid Amani Karume leo Aprili 7, 2018
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akikagua gwaride la askari polisi  katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha  kuadhimisha siku ya kumbukumbu ya miaka 46 ya kifo cha Rais wa kwanza wa Zanzibar  Hayati Sheikh Abeid Amani Karume leo Aprili 7, 2018

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akikagua gwaride la askari polisi  katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha  kuadhimisha siku ya kumbukumbu ya miaka 46 ya kifo cha Rais wa kwanza wa Zanzibar  Hayati Sheikh Abeid Amani Karume leo Aprili 7, 2018

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akikagua Kikosi cha bendi ya  Jeshi la Polisi katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha kuadhimisha siku ya kumbukumbu ya miaka 46 ya kifo cha Rais wa kwanza wa Zanzibar  Hayati Sheikh Abeid Amani Karume leo Aprili 7, 2018 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akikagua Kikosi cha bendi ya  Jeshi la Polisi katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha kuadhimisha siku ya kumbukumbu ya miaka 46 ya kifo cha Rais wa kwanza wa Zanzibar  Hayati Sheikh Abeid Amani Karume leo Aprili 7, 2018 

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akikagua Kikosi cha bendi ya  Jeshi la Polisi katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha kuadhimisha siku ya kumbukumbu ya miaka 46 ya kifo cha Rais wa kwanza wa Zanzibar  Hayati Sheikh Abeid Amani Karume leo Aprili 7, 2018 

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akimaliza kukagua gwaride  katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha kuadhimisha siku ya kumbukumbu ya miaka 46 ya kifo cha Rais wa kwanza wa Zanzibar  Hayati Sheikh Abeid Amani Karume leo Aprili 7, 2018 


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mstahiki Meya wa Jiji la Arusha Mhe. Calist Lazaro alipowasili katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha kuadhimisha siku ya kumbukumbu ya miaka 46 ya kifo cha Rais wa kwanza wa Zanzibar  Hayati Sheikh Abeid Amani Karume leo Aprili 7, 2018 
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Kamishna wa Polisi Jamii nchini CP Mussa Ally Mussa  alipowasili katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha kuadhimisha siku ya kumbukumbu ya miaka 46 ya kifo cha Rais wa kwanza wa Zanzibar  Hayati Sheikh Abeid Amani Karume leo Aprili 7, 2018 
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akipewa jarida la Jeshi la Polisi na IGP Simon Sirro  katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha kuadhimisha siku ya kumbukumbu ya miaka 46 ya kifo cha Rais wa kwanza wa Zanzibar  Hayati Sheikh Abeid Amani Karume leo Aprili 7, 2018 
Wote wanasimama na kuimba wimbo wa Taifa  katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha kuadhimisha siku ya kumbukumbu ya miaka 46 ya kifo cha Rais wa kwanza wa Zanzibar  Hayati Sheikh Abeid Amani Karume leo Aprili 7, 2018 
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli na wahudhuriaji wote wakiimba wimbo wa Taifa  katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha kuadhimisha siku ya kumbukumbu ya miaka 46 ya kifo cha Rais wa kwanza wa Zanzibar  Hayati Sheikh Abeid Amani Karume leo Aprili 7, 2018 

Gwaride la heshima  kuadhimisha siku ya kumbukumbu ya miaka 46 ya kifo cha Rais wa kwanza wa Zanzibar  Hayati Sheikh Abeid Amani Karume likipita mbele ya jukwaa kuu leo Aprili 7, 2018 
 Gwaride la heshima  kuadhimisha siku ya kumbukumbu ya miaka 46 ya kifo cha Rais wa kwanza wa Zanzibar  Hayati Sheikh Abeid Amani Karume likipita mbele ya jukwaa kuu leo Aprili 7, 2018 
 Bendi ya Jeshi la Polisi katika  kuadhimisha siku ya kumbukumbu ya miaka 46 ya kifo cha Rais wa kwanza wa Zanzibar  Hayati Sheikh Abeid Amani Karume likitoa heshima mbele ya jukwaa kuu leo Aprili 7, 2018 
 Kikosi cha pikipiki cha Jeshi la Polisi kikionesha namna kinavyopambana na wahalifu wanaotumia usafiri huo katika  kuadhimisha siku ya kumbukumbu ya miaka 46 ya kifo cha Rais wa kwanza wa Zanzibar  Hayati Sheikh Abeid Amani Karume likitoa heshima mbele ya jukwaa kuu leo Aprili 7, 2018 
 Mmoja wa "wahalifu" akiwa anajaribu kujihami wakati akiandamwa na kikosi cha pikipiki
 Mkurugenzi wa Masoko Utafiti na Huduma kwa Wateja, Tully Mwambapa  (wa pili kushoto) akiongoza ujumbe mzito wa benki ya CRDB katika  kuadhimisha siku ya kumbukumbu ya miaka 46 ya kifo cha Rais wa kwanza wa Zanzibar  Hayati Sheikh Abeid Amani Karume leo Aprili 7, 2018. Benki hiyo ni mmoja wa wadhamini wakubwa wa ujenzi wa makazi ya askari polisi
Gari maalumu la kunyunyizia maji ya kuwashawasha likionesha namna kikosi cha kutuliza ghasia cha Jeshi la Polisi kinavyoweza kupambana na waandamanaji  katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya  siku ya kumbukumbu ya miaka 46 ya kifo cha Rais wa kwanza wa Zanzibar  Hayati Sheikh Abeid Amani Karume leo Aprili 7, 2018 

 Askari wa Jeshi la Polisi wa kikosi maalumu cha kulinda viongozi wakionesha namna  kinavyoweza kupambana na maadui katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya  siku ya kumbukumbu ya miaka 46 ya kifo cha Rais wa kwanza wa Zanzibar  Hayati Sheikh Abeid Amani Karume leo Aprili 7, 2018 
 Askari wa Jeshi la Polisi wa kikosi maalumu cha kulinda viongozi wakionesha namna  kinavyoweza kupambana na maadui katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya  siku ya kumbukumbu ya miaka 46 ya kifo cha Rais wa kwanza wa Zanzibar  Hayati Sheikh Abeid Amani Karume leo Aprili 7, 2018 
 Askari wa Jeshi la Polisi wa kikosi maalumu cha kulinda viongozi wakionesha namna  kinavyoweza kupambana na maadui katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya  siku ya kumbukumbu ya miaka 46 ya kifo cha Rais wa kwanza wa Zanzibar  Hayati Sheikh Abeid Amani Karume leo Aprili 7, 2018 
 Askari wa Jeshi la Polisi wa kikosi maalumu cha kulinda viongozi wakionesha namna  kinavyoweza kupambana na maadui katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya  siku ya kumbukumbu ya miaka 46 ya kifo cha Rais wa kwanza wa Zanzibar  Hayati Sheikh Abeid Amani Karume leo Aprili 7, 2018 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli na viongozi wengine meza kuu wakipiga makofi wakati wa  maonesho ya vitendo ya vikosi vya kupambana na ghasia na kulinda viongozi katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha   kuadhimisha siku ya kumbukumbu ya miaka 46 ya kifo cha Rais wa kwanza wa Zanzibar  Hayati Sheikh Abeid Amani Karume leo Aprili 7, 2018

Kikosi maalumu cha kupambana na ugaidi kikionesha kazi zake  katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha   kuadhimisha siku ya kumbukumbu ya miaka 46 ya kifo cha Rais wa kwanza wa Zanzibar  Hayati Sheikh Abeid Amani Karume leo Aprili 7, 2018
 Kikosi maalumu cha kupambana na ugaidi kikionesha kazi zake  katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha   kuadhimisha siku ya kumbukumbu ya miaka 46 ya kifo cha Rais wa kwanza wa Zanzibar  Hayati Sheikh Abeid Amani Karume leo Aprili 7, 2018
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli na viongozi wengine meza kuu wakioneshwa na  Kamishina wa Operesheni na mafunzo wa Jeshi la Polisi (CP) Nsato Marijani nakala za matokeo ya uchunguzi wa shambulizi la bomu wakati wa maonesho ya mapambano na magaidi yaliyofanywa na vikosi maalumu vya jeshi la polisi katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha   kuadhimisha siku ya kumbukumbu ya miaka 46 ya kifo cha Rais wa kwanza wa Zanzibar  Hayati Sheikh Abeid Amani Karume leo Aprili 7, 2018
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli na viongozi wengine meza kuu wakioneshwa na  Kamishina wa Operesheni na mafunzo wa Jeshi la Polisi (CP) Nsato Marijani nakala za matokeo ya uchunguzi wa shambulizi la bomu wakati wa maonesho ya mapambano na magaidi yaliyofanywa na vikosi maalumu vya jeshi la polisi katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha   kuadhimisha siku ya kumbukumbu ya miaka 46 ya kifo cha Rais wa kwanza wa Zanzibar  Hayati Sheikh Abeid Amani Karume leo Aprili 7, 2018
 Kikosi maalumu cha kupambana na ugaidi kikionesha kazi zake  katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha   kuadhimisha siku ya kumbukumbu ya miaka 46 ya kifo cha Rais wa kwanza wa Zanzibar  Hayati Sheikh Abeid Amani Karume leo Aprili 7, 2018
 Kikosi maalumu cha kupambana na ugaidi kikipita na kutoa heshiama jukwaa kuu baada ya kuonesha kazi zake  katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha   kuadhimisha siku ya kumbukumbu ya miaka 46 ya kifo cha Rais wa kwanza wa Zanzibar  Hayati Sheikh Abeid Amani Karume leo Aprili 7, 2018
Kwaya ya Chuo cha Mafunzo cha Jeshi la Polisi kikitumbuiza  katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha   kuadhimisha siku ya kumbukumbu ya miaka 46 ya kifo cha Rais wa kwanza wa Zanzibar  Hayati Sheikh Abeid Amani Karume leo Aprili 7, 2018
 Kwaya ya Chuo cha Mafunzo cha Jeshi la Polisi kikitumbuiza  katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha   kuadhimisha siku ya kumbukumbu ya miaka 46 ya kifo cha Rais wa kwanza wa Zanzibar  Hayati Sheikh Abeid Amani Karume leo Aprili 7, 2018
 Kwaya ya Chuo cha Mafunzo cha Jeshi la Polisi kikitumbuiza  katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha   kuadhimisha siku ya kumbukumbu ya miaka 46 ya kifo cha Rais wa kwanza wa Zanzibar  Hayati Sheikh Abeid Amani Karume leo Aprili 7, 2018 
 Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo akikaribisha wageni na kusoma risala ya mkoa  katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha   kuadhimisha siku ya kumbukumbu ya miaka 46 ya kifo cha Rais wa kwanza wa Zanzibar  Hayati Sheikh Abeid Amani Karume leo Aprili 7, 2018 
  Mkurugenzi wa Masoko Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB Bi. Tully Mwambapa katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha   kuadhimisha siku ya kumbukumbu ya miaka 46 ya kifo cha Rais wa kwanza wa Zanzibar  Hayati Sheikh Abeid Amani Karume leo Aprili 7, 2018 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akijadiliana jambo na Waziri wa Mambo ya Ndani Dkt. Mwigulu Nchemba na IGP Simon Sirro katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha kuadhimisha siku ya kumbukumbu ya miaka 46 ya kifo cha Rais wa kwanza wa Zanzibar  Hayati Sheikh Abeid Amani Karume leo Aprili 7, 2018 
 Wakuu wa Wilaya za mkoa wa Arusha wakiwa katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha kuadhimisha siku ya kumbukumbu ya miaka 46 ya kifo cha Rais wa kwanza wa Zanzibar  Hayati Sheikh Abeid Amani Karume leo Aprili 7, 2018 
 IGP Simon Sirro akihutubia katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha kuadhimisha siku ya kumbukumbu ya miaka 46 ya kifo cha Rais wa kwanza wa Zanzibar  Hayati Sheikh Abeid Amani Karume leo Aprili 7, 2018 
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Mhandisi Masauni akihutubia katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha kuadhimisha siku ya kumbukumbu ya miaka 46 ya kifo cha Rais wa kwanza wa Zanzibar  Hayati Sheikh Abeid Amani Karume leo Aprili 7, 2018 
 Waziri wa Mambo ya Ndani Dkt. Mwiguli Nchemba akihutubia katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha kuadhimisha siku ya kumbukumbu ya miaka 46 ya kifo cha Rais wa kwanza wa Zanzibar  Hayati Sheikh Abeid Amani Karume leo Aprili 7, 2018 

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akiomba uwanja usimame kwa dakika kadhaa kumboleza kifo cha Rais wa kwanza wa Zanzibar  Hayati Sheikh Abeid Amani Karume leo Aprili 7, 2018 
  Maafisa waandamizi wa Polisi na wa JWTZ wakifurahia jambo wakati wa hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli  katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha kuadhimisha siku ya kumbukumbu ya miaka 46 ya kifo cha Rais wa kwanza wa Zanzibar  Hayati Sheikh Abeid Amani Karume leo Aprili 7, 2018
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akihutubua Taifa  katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha kuadhimisha siku ya kumbukumbu ya miaka 46 ya kifo cha Rais wa kwanza wa Zanzibar  Hayati Sheikh Abeid Amani Karume leo Aprili 7, 2018
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza IGP Simon Sirro kwa kujenga jeshi la polisi imara wakati akihutubua Taifa  katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha kuadhimisha siku ya kumbukumbu ya miaka 46 ya kifo cha Rais wa kwanza wa Zanzibar  Hayati Sheikh Abeid Amani Karume leo Aprili 7, 2018 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akihutubua Taifa  katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha kuadhimisha siku ya kumbukumbu ya miaka 46 ya kifo cha Rais wa kwanza wa Zanzibar  Hayati Sheikh Abeid Amani Karume leo Aprili 7, 2018
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akihutubua Taifa  katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha kuadhimisha siku ya kumbukumbu ya miaka 46 ya kifo cha Rais wa kwanza wa Zanzibar  Hayati Sheikh Abeid Amani Karume leo Aprili 7, 2018
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akihutubua Taifa  katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha kuadhimisha siku ya kumbukumbu ya miaka 46 ya kifo cha Rais wa kwanza wa Zanzibar  Hayati Sheikh Abeid Amani Karume leo Aprili 7, 2018
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akihutubua Taifa  katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha kuadhimisha siku ya kumbukumbu ya miaka 46 ya kifo cha Rais wa kwanza wa Zanzibar  Hayati Sheikh Abeid Amani Karume leo Aprili 7, 2018 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akipiga tumba katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha baada ya kuhitimisha maadhimisho ya siku  ya kumbukumbu ya miaka 46 ya kifo cha Rais wa kwanza wa Zanzibar  Hayati Sheikh Abeid Amani Karume leo Aprili 7, 2018. Picha na IKULU