Saturday, August 12

Odinga ayakataa matokeo ya urais yanayotangazwa na tume Kenya

Raila Odinga akihutubia wanahabari Jumanne usikuHaki miliki ya pichaREUTERS
Mgombea urais wa muungano wa upinzani nchini Kenya National Super Alliance (Nasa) Raila Odinga amepinga matokeo ambayo yanaendelea kutangazwa na tume ya uchaguzi nchini humo, IEBC.
Bw Odinga amewaambia wanahabari kwamba tume hiyo imekuwa ikitangaza matokeo kwenye tovuti yake bila kufuata utaratibu ufaao.
Waziri mkuu huyo wa zamani amesema kabla ya matokeo yoyote kutangazwa, IEBC inafaa kuwapa maajenti wa vyama Fomu 34A kutoka vituoni.
Amesema kwa sasa, bila kuwepo kwa fomu hizo, ni vigumu kubaini matokeo yanayopeperushwa yanatoka wapi.
"Mfumo umeacha kufanya kazi. Sasa ni mitambo inayopiga kura. IEBC wamesema kwamba hakuna chama chochote kilichopinga matokeo. Lakini vyama vitapingaje matokeo bila kujua asili yake? Ni fomu 34A pekee zinazoonesha chanzo cha matokeo," amesema.
"Kwa hivyo, tunakataa matokeo yote yaliyotangazwa kwa sasa na kuitaka tume ya IEBC itoe fomu 34A za kila kituo kabla ya matokeo zaidi kutangazwa."
IEBC imekuwa ikitangaza matokeo ya urais mtandaoni, na kufikia saa tisa na robo alfajiri, matokeo hayo yalikuwa yanamuonyesha Rais Uhuru Kenyatta wa chama cha Jubilee akiwa mbele na kura 6331140 (55.27%) naye Bw Odinga akiwa na kura 5031737 (43.92%).
Matokeo hayo ni ya kutoka vituo 295319 kati ya vituo 40883 nchini humo.
"Hii ni kompyuta inayopiga kura," alisema Bw Odinga akikataa matokeo hayo.
Hali ya wasiwasi imekuwa ikitanda katika kituo cha taifa cha kujumlishia na kutangaza matokeo katika ukumbi wa Bomas jijini Nairobi.
Matokeo yalianza kutiririka baadaye Jumanne jioni baada ya shughuli ya kuhesabiwa kura kuanza. Matokeo hayo yamekuwa yakionesha Bw Kenyatta akiongoza.
Wakala mkuu wa muungano huo wa upinzani, naibu waziri mkuu wa zamani Musalia Mudavadi alikuwa awali amehutubia wanahabari na kutaja matokeo yanayotangazwa na tume hiyo kama utapeli.
Alitoa wito kwa wafuasi wa muungano huo kupuuzilia mbali matokeo yanayotangazwa.

Mwanamke Muislamu aliyevuliwa hijab na polisi alipwa $85,000

Kirsty PowellHaki miliki ya pichaCAIR
Image captionKirsty Powell
Mwanamke mmoja Muislamu ambaye alilazimishwa kuvua hijab yake na maafisa wa polisi mjini California amezawadiwa $85,000 (£65,000).
Kirsty Powell aliwasilisha kesi mahakamani dhidi ya baraza mji wa Long Beach baada ya kulazimishwa kuvua vazi lake la hijab kufuatia kukamatwa kwake 2015.
Ombi la Bi Powell la kutaka kuhudumiwa na afisa wa polisi mwanamke lilipuuzwa na akalazimika kulala jela bila hijab yake.
Idara hiyo sasa imebadili sera yake kuhusu mavazi ya kidini ya kichwani.
Maafisa wa kike sasa wanaruhusiwa kuondoa hijab zao mbali na maafisa wa kiume na wafungwa iwapo usalama wa maafisa hao unatishiwa, alisema jaji wa Long Beach Monte Machit akizungumza na gazeti la Los Angeles Times.
Hatahivyo baraza la mji wa Long Beach lilikubali kumaliza kesi hiyo kulingana na baraza la mahusiano ya waislamu .
Baraza hilo ambalo lilianzisha kesi hiyo lilisema kuwa maafisa wa polisi kwa lazima walivua hijab yake mwanamke huyo mbele ya maafisa wa polisi wanaume na makumi ya wafungwa.

China yamuonya Trump kuchunga matamshi yake

Rais Xi Jinping
Image captionRais Xi Jinping
Rais wa China Xijinping amemtaka rais Donald Trump kuchunga mtamshi na vitendo vinavyozidisha hali ya kuzua wasiwasi ,chombo cha habari cha kiserikali kimeripoti.
Rais Trump na Korea Kaskazini wamekuwa wakirushiana cheche za maneno huku rais rais huyo wa Marekani akionya kuikabili kivita vikali Korea Kaskazini.
Lakini China ambaye ni mshirika mkuu wa Korea Kaskazini ametaka pande zote mbili kuwa na uvumilivu.
Rais Kim Jong-un na mwenzake wa Marekani Donald Trump wamekuwa wakirushiana cheche za vitisho
Image captionRais Kim Jong-un na mwenzake wa Marekani Donald Trump wamekuwa wakirushiana cheche za vitisho
Taarifa ya ikulu ya Whitehouse imesema kuwa Marekani na China zilikubaliana kwamba Korea Kaskazini inafaa kusitisha uchokozi na tabia mbaya.
Hofu kubwa inayoendelea kutanda kuhusu mpango wa kinyuklia wa Korea Kaskazini ilizidi baada ya taifa hilo kufanyia majaribio makombora yake ya masafa marefu mnamo mwezi Julai.

Trump atishia kuisababishia Korea Kaskazini "shida kubwa" kwa sababu ya Guam

Donald Trump na Mike Pence in Bedminster, New Jersey, on 10 August 2017Haki miliki ya pichaREUTERS
Image captionTrump amesema Kim Jong-un atajuta sana, na upesi sana, iwapo atatishia kisiwa cha Guam tena
Rais wa Marekani Donald Trump ameitahadharisha Korea Kaskazini kwamba nchi hiyo inafaa kutarajia shida kubwa, kubwa" iwapo kitu chochote kitatendeka kwa kisiwa cha Marekani cha Guam.
Akiongea akiwa Bedminister, New Jersey, aliahidi kwamba kisiwa hicho katika Bahari ya Pasifiki kitakuwa "salama kabisa, na mniamini".
Bw Trump amesema Marekani itaiwekea Korea Kaskazini vikwazo zaidi, "vikali zaidi".
Baadaye alizungumza na Rais wa China Xi Jinping, ambaye alisisitiza umuhimu wa kutatua mzozo huo kwa njia ya amani, runinga ya serikali ya China ilisema.
Rais Xi alitoa wito kwa wahusika wote kuwa na subira na kujizuia dhidi ya kutoa maneno au kufanya vitendo ambavyo vinaweza vikazidisha uhasama.
Aidha, alisema ni kwa maslahi ya China na Marekani kwamba kusiwepo na silaha za nyuklia katika rasi ya Korea.
Ikulu ya White House ilisema Marekani na China zilikubaliana kwamba Korea Kaskazini ni lazima ikomeshe "tabia yake ya uchokozi na kuongeza uhasama."
"Twatumai kwamba mambo yatakuwa sawa," Bw trump alisema awali, akionekana kuwa na msimamo wa matumaini siku moja baada yake kuonekana kukata tamaa.
"Hakuna anayependa suluhu ya amani zaidi ya Rais Trump, hilo ninaweza kuwaambia."
Mapema Ijumaa, Trump alikuwa amesema jeshi la Marekani liko tayari kukabiliana na Korea Kaskazini wakati wowote ule.
"Suluhu ya kijeshi sasa ipo, imepangwa na iko tayari, Korea Kaskazini wakidhubutu kuchukua hatua isiyo ya busara. Twatumai Kim Jong-un atachagua njia nyingine!" Trump ameandika kwenye Twitter.
Alisema hayo huku Korea Kaskazini ikimtuhumu kwa kukaribia kutumbukiza rasi ya Korea katika vita vya nyuklia.
Trump aliandamana na waziri wa mambo ya nje Rex Tillerson (kushoto) na balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa Nikki Haley mjini Bedminster, New JerseyHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionTrump aliandamana na waziri wa mambo ya nje Rex Tillerson (kushoto) na balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa Nikki Haley mjini Bedminster, New Jersey
Pyongyang inakamilisha kuandaa mpango wake wa kurusha makombora karibu na kisiwa cha Marekani cha Guam.
Urusi imesema majibizano kati ya Washington na Pyongyang yanafaa "kututia wasiwasi sana."
Waziri wa mambo ya nje wa Urusi Sergei Lavrov alisema kiwango cha hatari ya kutokea mzozo wa kivita ipo "juu sana" huku akipendekeza mpango wa pamoja wa Urusi na China wa kutanzua mzozo huo.
Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amesema hakuna suluhu yoyote inayoweza kupatikana kupitia jeshi, na kwamba "kuongezeka kwa majibizano sio suluhu."
Alipoulizwa kuhusu tamko lake Ijumaa kwamba jeshi la Marekani liko tayari kukabiliana na Korea Kaskazini wakati wowote ule, Trump aliwaambia wanahabari: "Natumai kwamba wanafahamu (Korea Kaskazini) uzito wa nilichokisema na nilikisema ndicho ninachokusudia...maneno hayo ni rahisi sana, rahisi sana kuyaelewa."
Aliongeza: "Iwapo yeye (Kim Jong-un) atatoa vitisho vyovyote zaidi hata kwa lugha fiche ... kuhusu kisiwa cha Guam au eneo jingine lolote ambalo ni la Marekani au mshirika wa Marekani, atajutia sana kwa kweli na atajutia hilo haraka sana."
Bw Trump ameandika hivyo kwenye Twitter baada ya kutishia mapema wiki hii kupitia Twitter kwamba "Korea Kaskazini wasidhubutu kutoa vitisho zaidi kwa Marekani. Watajibiwa kwa moto na ghadhabu ambayo ulimwengu haujawahi kushuhudia."
Aidha, Ijumaa, shirika rasmi la habari la Korea Kaskazini KCNA liliituhumu Marekani kwa "jaribio la kihalifu la kusababisha mkasa wa kinyuklia katika taifa hilo la rasi ya Korea."
Shirika hilo lilisema Marekani inafanya kila juhudi kufanyia majaribio silaha zake za nyuklia katika rasi ya Korea.
Marekani ndiyo "mpanga njama ya tishio hili la nyuklia, mraibu wa vita vya nyuklia," taarifa ya KCNA imesema.
Awali, alikuwa ameitahadharisha Korea Kaskazini kwamba inafaa kuwa na "wasiwasi sana" iwapo itatenda lolote kwa Marekani.
Alisema utawala wa taifa hilo utakuwa shida kubwa "ambayo ni mataifa machache sana yaliyowahi kukumbana nayo" iwapo "hawatabadilika".
Kadhalika Bw Trump alikuwa awali ameshutumu serikali za awali za Marekani akisema zilionyesha udhaifu sana zikikabiliana na Korea Kaskazini na pia akashutumu mshirika wa karibu wa Korea Kaskazini, akisema kwamba inafaa "kufanya juhudi zaidi."
Alisema: "Nawaambia, iwapo Korea Kaskazini itafanya jambo lolote hata kwa kufikiria tu kuhusu kumshambulia mtu tunayempenda au tunayewakilisha au washirika wetu au sisi wenyewe inaweza kuwa na wasiwasi sana, sana."
"Nitawaambia ni kwa nini...ni kwa sababuu mambo yatawatendekea ambayo hawajawahi kufikirtia kwamba yanaweza kutokea."
Hata hivyo, aliongeza kwamba Marekani bado iko huru kushiriki katika mashauriano.
Aliongeza: "Nawaambia hivi, Korea Kaskazini inafaa kujiweka sawa au wataona shida kubwa kiasi ambacho ni nchi chache sana zilizowahi kushuhudia."
Andersen Air Force Base, Guam July 18, 2017Haki miliki ya pichaREUTERS
Image captionMarekani ina kambi ya jeshi la wanahewa la Andersen kisiwa cha Guam
Korea Kaskazini ilisema Jumatano kwamba inapanga kurusha makombora ya masafa wa wastani na ya masafa marefu kuelekea kisiwa cha Guam, ambapo kuna kambi ya ndege za kivita za kuangusha mabomu za Marekani.
Hata hivyo, kufikia sasa hakujakuwa na dalili zozote kwamba huenda kisiwa hicho cha Guam kikashambuliwa.
Map showing Guam

Kisiwa cha Guam na umuhimu wake

  • Kisiwa cha Guam kina ukubwa wa kilomita mraba 541 (maili mraba 209) na kinapatikana bahari ya Pasifiki kati ya Ufilipino na Hawaii.
  • Ni jimbo "lisilo na mpangilio wowote, na lisilojumuishwa kikamilifu" la Marekani, lenye wakazi karibu 163,000.
  • Kambi za jeshi la Marekani hutumia karibu robo ya ardhi ya kisiwa hicho. Marekani ina wanajeshi 6,000 kisiwa hicho na kuna mipango ya kuwasafirisha maelfu wengine huko.
  • Ni kituo muhimu katika shughuli za kijeshi za Marekani, ambapo huwezesha wanajeshi wa nchi hiyo kufika maeneo mengi muhimu Pasifiki, mfano eneo la bahari linalozozaniwa la South China Sea, rasi ya Korea na mlango wa bahari wa Taiwan.
Bw Trump alikuwa amewaambia wanahabari Jumanne kwamba: "Korea Kaskazini wasidhubutu kutoa vitisho zaidi kwa Marekani. Watajibiwa kwa moto na ghadhabu ambayo ulimwengu haujawahi kushuhudia."
Seneta mkongwe wa Marekani John McCain hata hivyo alikuwa na shaka kuhusu tamko la Trump.
"Viongozi wengi wakuu ambao nimewahi kuwaona, huwa hawatoi vitisho ikiwa hawako tayari kuvitekeleza na sina uhakika kwamba Rais Trump yuko tayari kuchukua hatua," alisema Bw McCain.
Korea Kaskazini ilikuwa imeghadhabishwa na vikwazo vipya ilivyowekewa na Umoja wa Mataifa siku ya Jumamosi.
Vikwazo hivyo vina lengo la kupunguza mapato kutoka kwa mauzo ya bidhaa nje ya Korea Kaskazini kwa theluthi moja.
KCNA imesema Korea Kaskazini, ambayo imefanyia majaribio silaha za nyuklia mara tano, itajibu vikali na kwamba "Marekani italipia" kwa kuchangia kutunga vikwazo hivyo.
Waziri mkuu wa Australia Malcolm Turnbull amesema taifa lake liko tayari kushiriki katika vita dhidi ya Korea Kaskazini iwapo nchi hiyo ya rasi ya Korea itatekeleza shambulio dhidi ya Marekani.
"Iwapo kutakuwa na shambulio dhidi ya Marekani, Mkataba wa Anzus wa mwaka 1951 utaanza kutekelezwa na Australia itajitokeza kuisaidia Marekani," alisema kwenye mahojiano na kituo kimoja cha redio, "vile vile ambavyo Marekani ingefika kutusaidia iwapo tutashambuliwa."

Vitu sita usivyo vijua kuhusu kisiwa cha Guam na ambavyo vitakushangaza

Ricardo Blas JrHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionRicardo Blas Jr
Sio kila mara unasikia kuhusu kisiwa cha Guam ambacho ndio kikubwa zaidi katika bahari ya Pacific na kinamilikiwa na Marekani.
Kimekuwa katika habari kwa sababu Korea Kaskazini imetishia kushambulia kambi yake ya kijeshi ikiwa ni miongoni mwa mgogoro na Marekani.
Inajiri baada ya rais Donald Trump kusema kuwa taifa hilo linafaa kutarajia vita vikali kutoka kwa Marekani.
Huku Guam ikiangaziwa haya hapa mambo sita unayofaa kujua kuhusu kisiwa hicho.

Ni eneo ambalo liko mbali zaidi kwa raia wa Marekani kutembelea bila kutoka Marekani.

Eneo la Tumon Bay ni maarufu miongoni mwa wataliiHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionEneo la Tumon Bay ni maarufu miongoni mwa watalii
Licha kumilikiwa na Marekani, kiko maili 8000 kutoka Marekani na inachukua takriban saa 19 kusafiri kwa ndege kutoka mji wa New York.
Wamarekani wanaweza kuelekea katika kisiwa hicho bila kutumia pasipoti.

Kila mtu aliyezaliwa kisiwani Guam ni Mmarekani lakini hawezi kumpigia kura rais.

Sherehe inafanyika katika baranara mjini TumonHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionSherehe inafanyika katika baranara mjini Tumon
Tangu mwisho wa vita vya dunia , watu wawili waliokuwa wakiishi katika kisiwa hicho walipewa uraia lakini hawawezi kumpigia kura rais wa Marekani. Wana mwakilishi mmoja wa serikali laki yeye hana uwezo wowote kuhusu utengenezaji wa sera.
Guam ni kambi muhimu ya kijeshi
Ndege ya kijeshi ya Marekani inapaa kutoka GuamHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionNdege ya kijeshi ya Marekani inapaa kutoka Guam
Robo ya kisiwa hicho kinamilikiwa na jeshi la Marekani na kinatumiwa kama kambi ya wanamaji na wanaanga
Pia inakadiriwa kwamba karibia asilimia 10 ya watu wa Guam wenye idadi ya 160,000 ni ya wanajeshi.

Raia wa Guam wanajulikana kama Chamorro.

Guam ni kisiwa cha kisasa chenye majumba marefu na maeneo manne ya kitaliiHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionGuam ni kisiwa cha kisasa chenye majumba marefu na maeneo manne ya kitalii
Chamorro ni jina la jumla linalopewa watu wanaoshi katika kisiwa cha Guam na watu wanaoshi katika visiwa vya Micronesia katika bahari ya Pacific.
Utamaduni wao unafanana na ule wa Uhispania zaidi ya Umarekani kwa sababu Uhispania ilidhibiti kisiwa hicho kwa takriban miaka 300 hadi 1898.

Watu katika eneo hilo hawatozwi kodi

Tumon ndio wilaya ya kutalii kisiwani GuamHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionTumon ndio wilaya ya kutalii kisiwani Guam
Watalii kutoka Taiwan , Korea Kusini na Japan huchukua saa nne kusafiri hadi katika kisiwa hicho kwa likizo ya kupata jua mbali na kununua vitu ambavyo havilipishwi kodi.
Maduka yote makubwa huuza bidhaa za mitindo na mengi hufunguliwa kwa saa 24 kwa siku.
Ricardo Blas Jr. ndio mtu maarufu zaidi katika kisiwa cha Guam
Blas Jr. akishindana katiika michezo ya olimpiki ya 2012.Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionBlas Jr. akishindana katiika michezo ya olimpiki ya 2012.
Mtu huyo mwenye umri wa miaka 30 ni mchezaji wa judo ambaye alishiriki judo katika michezo ya Olimpiki ya 2008 na 2012 na alibeba bendera ya Guam katika mashindano yote lakini akashindwa kupata medali licha ya kuwa mhcezaji judo mwenye uzani mzito zaidi wa kilo 214

Uchaguzi Kenya 2017: Uhuru Kenyatta atangazwa mshindi wa urais

Uhuru KenyattaHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionUhuru Kenyatta, baada ya kutangazwa mshindi, ametoa wito kwa wananchi kudumisha umoja
Tume ya taifa ya uchaguzi Kenya imemtangaza Rais Uhuru Kenyatta wa chama cha Jubilee kuwa mshindi wa uchaguzi wa urais uliofanyika Jumanne.
Rais Kenyatta alipata kura 8, 203, 290.. ambayo ni asilimia 54 naye mpinzani wake mkuu, mgombea wa muungano wa upinzani wa National Super Alliance Raila Odinga akapata kura milioni 6,762,224 ambayo ni asilimia 44.
Akitangaza matokeo hayo mwenyekiti wa tume ya uchaguzi nchini Kenya IEBC Wafula Chebukati alisema kuwa ni asilimia 78 ya wapiga kura milioni 19 waliosajiliwa pekee walioshiriki katika shuguhuli hiyo ya kidemokrasia.
Alisema kuwa licha ya matatizo machache kukumba mfumo mpya wa kutangazia matokeo, tume yake ilifanikiwa kutangaza matokeo hayo bila tashwishi yoyote.
Wafuasi wa Jubilee wakisherekea
Image captionWafuasi wa Jubilee wakisherekea
Aliongezea kuwa hatua zilizochukuliwa kuandaa uchaguzi huo ni hakikisho tosha la ukomavu wa kidemokrasia nchini.
Alisema kuwa Wakenya wengi walijitokeza na kivumilia hali ya anga ili kushiriki katika zoezi hilo la kidemokrasia kutokana na uaminifu walio nao kwa tume hiyo ya uchaguzi.
Aliongezea kwamba licha ya kukumbwa na changamoto chungu nzima katika mahakama waliweza kuandaa uchaguzi huo kwa njia ya haki uwazi na uhuru,
Akitoa hotuba yake rais Uhuru Kenyatta amewashukuru wafuasi wake na Wakenya wote kwa jumla kwa kumpatia muhula mwengine.
wafuasi wa Jubilee wakifurahia kutangazwa kwa rais Uhuru Kenyatta kama msahindi wa uchaguzi mkuu
Image captionwafuasi wa Jubilee wakifurahia kutangazwa kwa rais Uhuru Kenyatta kama msahindi wa uchaguzi mkuu
Aidha amemtaka mpinzani wake mkuu Raila Odinga na wafuasi wake kushirikiana naye katika kujenga Kenya akisema kuwa Uchaguzi huja na kumalizika lakini wakenya ni sharti wasalie kama mandugu na majirani wema.
''Katika kila mashindano kuna mshindi na aliyeshindwa ,hivyobasi namuomba ndugu yangu mkubwa Raila Odinga na wafuasi wake kushirikiana nami katika kulijenga taifa hili kwa sababu uchaguzi huja na kumalizika lakini wakenya ni sharti wanedlea kuwa majirani wema'', alisema Uhuru Kenyatta .
Na muda mfupi tu baada ya Uhuru Kenyatta kutanzwa rais mteule wafuasi wake kote nchini walisherehekea ushindi huo kwa vifijo na nderemo.
Muungano wa upinzani ulikuwa umepinga utaratibu uliokuwa unatumiwa na tume hiyo kupeperusha matokeo ya uchaguzi huo.
Aidha, viongozi wa muungano huo walikuwa wamedai mitambo ya tume hiyo ilidukuliwa na matokeo kubadilishwa.
Viongozi hao walikuwa Alhamisi wametangaza kwamba mgombea wao, Bw Odinga ambaye aliwahi kuwa waziri mkuu katika serikali ya Mwai Kibaki, kuwa mshindi wa uchaguzi huo.

Matoeko kamili ya wagombea wote kama yalivyotangazwa na Bw Chebukati

MgombeaChamaKuraAsilimia
Uhuru KenyattaJubilee8,203,29054.27
Raila OdingaODM6,762,22444.74
Mohamed Abduba DidaARK38,0930.25
Japheth Kavinga KaluyuMgombea wa kujitegemea16,4820.08
Michael Wainaina MwauraMgombea wa kujitegemea13,2570.09
Joseph Nthiga NyagahMgombea wa kujitegemea42,2590.28
John Ekuru AukotThirdway Alliance27,3110.18
Cyrus JirongoUDP11,7050.08
Muda mfupi kabla ya matokeo hayo kutangazwa, Muungano wa upinzani ulikuwa umesema hauungi mkono tangazo la matokeo la IEBC.
Ajenti mkuu wa muungano huo Musalia Mudavadi alisema malalamiko yaliyowasilishwa na muungano huo kwa tume hayajashughulikiwa ipasavyo.
Bw Mudavadi amesema baada ya kukutana na tume hiyo, walifahamishwa kwamba baadhi ya mambo yao yatashughulikiwa baada ya matokeo kutangazwa.
"Mikutano ilikuwa kama shughuli ya uhusiano mwema tu," amesema.
Tume ilikuwa imewaalika maajenti wakuu kwa mkutano kabla ya kutoa tangazo la matokeo.
Lakini upinzani umesema hautashiriki katika kukubaliana na tangazo la tume hiyo.
Naibu ajenti wa muungano huo James Orengo ametilia shaka waangilizi ambao walikuwa wamesema uchaguzi ulikuwa huru na wa haki.
Amesema waangalizi hao walifaa kuchunguzwa kwanza.
Bw Orengo amesema pia kwamba muungano huo haupangi kwenda kortini kupinga matokeo.
Viongozi wa kanda ya Afrika Mashariki, wakiwemo Rais wa Rwanda Paul Kagame na Yoweri Museveni wa Uganda wamempongeza Rais Kenyatta kwa ushindi wake.