Saturday, August 19

WACHEZAJI WANAOWANIA TUZO YA FIFA 2017 WATAJWA

Shirikisho la mpira wa miguu Duniani (FIFA) limewataja wachezaji 24 wakiume watakaowania tuzo ya mchezaji bora wa FIFA na wachezi 10 kwa upande wa soka la wakike, huku zoezi hilo likiendeshwa na Makocha wa timu za mataifa mbalimbali Duniani, Manahodha, Waandishi wa habari pamoja na Washabiki wa soka. Zoezi la kupiga kura ili kumpata mwanandinga huyo bora wa FIFA linatarajiwa kuanza Jumatatu Agosti 21 na kufungwa Septemba 7, 2017.

wachezaji 24 waliotajwa kuwania tuzo ya Mwanasoka Bora wa FIFA 2017 kwa upande wa wanaume ni hawa hapa.




Hawa ndiyo wachezaji 10 waliotajwa kuwania tuzo ya Mwanasoka Bora wa FIFA 2017 kwa upande wa wanawake.


Bulaya akamatwa Bunda


Bunda. Mbunge wa jimbo la Bunda mjini Esther Bulaya amekamatwa na jeshi la Polisi akiwa katika Hotel ya Kifa Best Point Wilayani Tarime akidaiwa kujiandaa kutaka kufanya mkusanyiko kinyume cha sheria.
Kamanda wa polisi Tarime/Rorya Kamishina Msaidizi Mwandamizi Henry Mwaibambe amesema wabunge  Bulaya na John Heche hawatakiwi kujumuika kwenye mkutano mbunge wa jimbo ka Tarime.

Mashambulio Uhispania: Mambo tunayoyajua kufikia sasa

Paramedics are seen near to the scene of a terrorist attack in the Las Ramblas area on 17 August 2017 in Barcelona, Spain.Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionMaafisa wa matibabu wakiwa Las Ramblas
Mashambulio mawili ya kigaidi yaliyohusisha washambuliaji kuvurumisha magari kwenye umati wa watu yalitokea katika eneo la Catalonia, nchini Uhispania.
Hapa chini ni mambo tunayoyafahamu kufikia sasa.
Nini kilitokea?
Alhamisi alasiri, mwendo wa saa 16:50 saa za Uhispania (saa kumi na moja kasoro dakika kumi Afrika Mashariki) gari jeupe lilivurumishwa kwenye umati wa watu katika eneo la kitalii la Las Ramblas, eneo maarufu la kitalii katikati mwa Barcelona lenye kinjia cha umbali wa kilomita 1.2. Eneo hilo lilikuwa limejaa watalii.
Dereva wa gari hilo anadaiwa kuliendesha kwa kupindapinda na kujaribu kuwagonga watu wengi zaidi katika eneo la wapita njia. Wengi walianguka na wengine wakakimbilia usalama madukani na kwenye migahawa.
Watu 13 walifariki na wengine zaidi ya 100 kujeruhiwa.
Mshambuliaji alitoroka kwa miguu.
Polisi wa Uhispania wameeleza shambulio hilo kuwa la kigaidi.
Shambulio la pili lilitokea vipi?
Saa nane baadaye, gari aina ya Audi A3 lilivurumishwa hadi kwenye wapita njia katika mji wa Cambrils, 110km (maili 68) kusini magharibi mwa Uhispania.
Mwanamke mmoja alijeruhiwa vibaya na baadaye akafariki akipokea matibabu hospitalini.
Afisa wa polisi pia alijeruhiwa.
Gari la washambuliaji hao lilipinduka na watu watano wakatoka nje, baadhi wakiwa wamevalia mikanda bandia ya kujilipua.
Wote walipigwa risasi na kuuawa na maafisa wa polisi. Wanne walifariki papo hapo na wa tano akafariki baadaye.
Maafisa wanaamini kuna uhusiano kati ya mashambulio hayo ya Las Ramblas na Cambrils.
Kuna mshukiwa amekamatwa?
Alhamisi, mtu mmoja kutoka eneo la Melilla linalomilikiwa na Uhispania lakini linapatikana Afrika alikamatwa aktika eneo la Alcanar. Raia wa Morocco pia alikamatwa Ripoll. Miji yote miwili inapatikana jimbo la Catalonia, ambapo unapatikana mji wa Barcelona.
Stakabadhi za raia wa Morocco Driss Oubakir, 28, inadaiwa zilitumiwa kukodisha gari lililotumiwa kushambulia Las Ramblas lakini taarifa katika vyombo vya habari zinasema kuna uwezekano stakabadhi zake ziliibiwa na kutumiwa bila yeye kufahamu.
Driss OukabirHaki miliki ya pichaSPANISH NATIONAL POLICE
Image captionPicha ya Driss Oukabir iliyotolewa na polisi
Polisi pia wanamtafuta kaka mdogo wa Driss Oubakir, Moussa Oubakir, 18, anayetuhumiwa kuwa mshambuliaji aliyehusika shambulio la Las Ramblas, vyombo vya habari Uhispania vinasema.
Wahasiriwa walitoka maeneo mengi dunianiHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionWahasiriwa walitoka mataifa mbalimbali duniani
Ijumaa, polisi walitangaza kwamba wamemkamata mtu mwingine eneo la Ripoll. Haijabainika iwapo alihusika katika mashambulio hayo.
Kumetokea visa vingine?
Alhamisi jioni, saa 19:30 hivi, gari liliendeshwa na kuwagonga maafisa wa usalama waliokuwa kwenye kizuizi viungani mwa mji wa Barcelona.
Gari hilo baadaye lilipatikana likiwa na mwanamume aliyekuwa amefariki humo ndani.
Wizara ya mambo ya ndani ilikanusha taarifa za awali kwamba aliuawa kwa kupigwa risasi na polisi.
Maafisa hawajafutilia mbali uwezekano kwamba kisa hicho kilihusiana na shambulio la Las ramblas, lakini uchunguzi bado unaendelea.
Jumatano usiku, mlipuko uliharibu kabisa nyumba moja lAlcanar, 200km kusini mwa Barcelona, na kuua mtu mmoja na kuwajeruhi wengine saba.
AlcanarHaki miliki ya pichaEPA
Image captionMikebe ya gesi ya kutoa machozi ilipatikana katika jumba lililolipuliwa Alcanar
Waathiriwa walitoka wapi?
Wanatoka mataifa mengi duniani, na kufikia sasa watu kutoka mataifa 34 wametambuliwa.
Majeruhi wanatoka Ireland, England, Ufaransa, Australia, China, Pakistan, Venezuela, Algeria, Peru, Ujerumani, Uholanzi, Ugiriki, Hong Kong, Taiwan, Ecuador, Marekani, Argentina, Romania, Cuba, Austria na Ufilipino.
Las Ramblas, Barcelona, Spain August 17, 2017Haki miliki ya pichaREUTERS
Image captionBarcelona ni moja ya miji mashuhuri zaidi kwa watalii Ulaya.

Seneta Chapelle - Nadal mashakani kwa kutaka Trump auawe

NadalHaki miliki ya pichaALAMY
Image captionNadal anasema alikuwa na hasira alipoandika maoni hayo.
Seneta kutoka Missouri anachunguzwa na walinzi wa rais wa Marekani baada ya yeye kusema anatumai Rais Donald Trump atauawa.
Seneta huyo wa chama cha Democratic Maria Chappelle-Nadal alichapisha maoni hayo kwenye mtandao wa Facebook lakini baadaye akayafuta.
Walinzi wa rais wanasema "wanachunguzaa maoni yaliyotolewa na wengine" na kuwa "vitisho vyote dhidi ya Rais" vitafuatiliwa.
Seneta anakiri alikosea kwa kuandika hivyo kwenye Facebook lakini hatajiuzulu.
Aliandika "Hapana." Natumaini Trump atauawa!" wakati alikuwa anamjibu mtu kwenye Facebook.
Aliiambia St Louis Post-Dispatch: " Kwa hakika sikumaanisha kile nilichokiandika. Nimeiondoa, na ninadhani imefutwa.
"Sitajiuzulu. Nilichosema ni makosa, lakini sitakoma kuzungumzia kile kilichosababisha niseme hivyo, ambayo ni hasira na suitofahamu ambayo watu wengi nchini Amerika wanahisi sasa."
Wajumbe wa chama chake walikashifu maoni yake na wengine wametoa wito wa kujiuzulu kwake.
Kiongozi wa Democratic Caucus katika Seneti ya Missouri, Gina Walsh, alisema mwenzake "lazima awe na aibu kwa kuongeza sauti yake kwa yale yanayoendelea kwenye mazingira haya yenye sumu."
Seneta wa Democratic Claire McCaskill, ambaye pia ni wa Missouri, alisema: "Ninaushutumu, ni vibaya na hivyo lazima ajiuzulu."
Gavana wa Republican wa Missouri Eric Greitens amemwomba pia ajiuzulu.
Alisema: "Tunaweza kuwa na tofauti katika nchi yetu, lakini hakuna mtu anayepaswa kuchochea vurugu za kisiasa. Seneta lazima ajijiuzulu."
Hata hivyo, Seneta Chappelle-Nadal anasisitiza kuwa ana haki ya kuzungumza.
"Nimekataa kujiuzulu kwa kutumia haki yangu, hata kama nilivyosema ni makosa," alisema.

Lagos mji wa pili mbaya zaidi kuishi duniani

Sehemu ya mji wa LagosHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionSehemu ya mji wa Lagos
Mji wa Lagos nchini Nigeria umeorodhwa wa pili mbaya zaidi kuishi duniani na jarida la The Economist.
Jarida hilo, katika ripoti yake ya Global Liveability Report ya mwaka 2017, imeorodhesha mji mkuu wa Syria, Damascus ambao umeathiriwa sana na mapigano kuwa pekee ulio mbaya kuushinda mji huo mkuu wa kibiashara wa Nigeria.
Mji bora zaidi kuishi duniani ni Melbourne nchini Australia.
Lagos ni miongoni mwa miji mitano kutoka bara la Afrika ambayo imo miongoni mwa miji 10 hatari zaidi kuishi duniani.
Miji hiyo mingine ni mji mkuu wa Libya, Tripoli, mji mkuu wa Algeria, Algiers, mji mkuu wa Zimbabwe, Harare na mji mkubwa zaidi nchini Cameroon, Douala.
Orodha hiyo huangazia mambo matano: uthabiti, huduma ya afya, utamaduni na mazingira, elimu na miundo mbinu.
Kuna mji mmoja Afrika hata hivyo ambao umeimarika pakubwa.
Abidjan, mji mkubwa zaidi nchini Ivory Coast, uliorodheshwa kuwa miongoni mwa miji mitano iliyoimarika pakubwa tangu kuandaliwa kwa ripoti kama hiyo miaka mitano iliyopita.

Kagame: Afrika iache kutegemea mifumo ya utawala ya Magharibi

Kagame akitia saini hati ya kiapo baada ya kuapishwa mjini KigaliHaki miliki ya pichaAFP/GETTY
Image captionKagame akitia saini hati ya kiapo baada ya kuapishwa mjini Kigali
Rais Paul Kagame wa Rwanda ameapishwa kuongoza taifa hilo kwa miaka mingine saba na akakemea mataifa ya magharibi yanayokosoa Afrika na kuilazimisha kufuata mitindo na mifumo ya utawala wa kimagharibi.
Amewaasa viongozi wa afrika kupigania kujiwezesha kwa mataifa yao kama linavyofanya taifa lake.
Hayo ameyasema katika sherehe za kumuapisha kuiongoza nchi hiyo kwa muhula wa tatu madarakani, baada ya kushinda uchaguzi wiki mbili zilizopita.
Sherehe za kula kiapo zimefanyika mjini Kigali na kuhudhuriwa na marais kutoka nchi 19 za Afrika.
Uchaguzi huo ulikosolewa na baadhi ya mataifa kama Marekani ambayo ilisema hali ya siasa nchini Rwanda inatoa fursa tu kwa mtu mmoja pekee kwendelea kuiongoza nchi hiyo.
Rais Kagame amesema miaka 23 baada ya Rwanda kukumbwa na mauaji ya kimbari wananchi wake sasa waliamua kujenga taifa linalojiwezesha.
Amekemea bila kutaja majina, mataifa yanayozitaka nchi za afrika kuiga mifumo ya utawala ya kimagharibi:
"Tulilazimika kupambana ili kulinda haki zetu na kufanya kile ambacho ni kizuri kwetu na tutaendelea kufanya hivyo. Lakini Rwanda haiwezi kuwa mfano pekee lazima kila mwananchi wa Afrika, kila taifa lipiganie kuishi bila kuetegemea wengine au bila kujali wengine wanavyotaka. Wanataka mifumo inayofanya kazi vizuri kwetu tuibadilishe na mifumo yao ambayo wananchi wao wameanza kupoteza imani nayo."
Mara tu baada ya uchaguzi kufanyika Marekani ambaye ni mshirika wa karibu wa Rwanda licha ya kupongeza wananchi wa Rwanda kwa uchaguzi nchi hiyo ilisema kulikuwa na dosari zilizojitokeza kabla na wakati wa uchaguzi.
Isitoshe nchi hiyo ilipokea shingo upande mabadiliko ya katiba yaliyompa fursa rais Kagame kugombea muhula wa tatu madarakani.
Katika uchaguzi huo rais Kagame alishinda kwa asilimia 98 ya kura.
Wapinzani wake ambao ni Philippe Mpayimana na Frank Habineza wa chama cha Green walijumlisha asilimia 1 tu ya kura.
Rais Kagame hakutaja ajenda yake ya miaka 7 ijayo, lakini baadhi ya wananchi wameeleza kufurahishwa na mafanikio ya utawala wake.
Miongoni mwa marais na wakuu wa serikali za mataifa ya Afrika waliohudhuria sherehe hiyo, alikuwepo rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni na Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya.
Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo ilimtuma spika wa bunge Obe Minaku nayo Tanzania ikawakilishwa na rais mstaafu Benjamin Mkapa.
Burundi haikuwakilishwa lakini alikuwepo rais wa zamani Pierre Buyoya aliyealikwa miongoni mwa marais wastaafu.

Rais Paul Kagame kuapishwa Rwanda

Rais Paul Kagame wa Rwanda
Image captionRais Paul Kagame wa Rwanda
Rais wa Rwanda Paul Kagame anaapishwa leo kuiongoza nchi hiyo kwa muhula wa tatu wa miaka 7.
Hii ni baada ya kushinda uchaguzi wiki mbili zilizopita kwa kupata asilimia 98 ya kura.
Sherehe za kula kiapo zinafanyika kwenye uwanja wa taifa Amahoro mjini Kigali.
zaidi ya marais 20 kutoka mataifa ya Afrika wanahudhuria sherehe hizo.
Miongoni mwao ni rais wa Sudan Omar Al Bashir ambaye anasakwa na mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ICC.
Rwanda siyo mwanachama wa mahakama hiyo.
Katika uchaguzi wagombeaji wengine 2 Philippe Mpayimana na Frank Habineza wa chama cha Green waliambulia asilimia 1 jumla ya kura zao.
Uchaguzi huo ulikosolewa na baadhi ya mataifa kama Marekani ambayo ilisema hali ya siasa nchini Rwanda inatoa fursa tu kwa mtu mmoja pekee kwendelea kuiongoza nchi hiyo.

Mbunge amtaka Magufuli kumuiga Kenyatta na kuruhusu maandamano

Rais John Pombe MagufuliHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionRais John Pombe Magufuli
Mbunge wa Arusha mjini nchini Tanzania kupitia Chadema, Godbless Lema amemtaka rais John Pombe Magufuli kumuiga mwenzake wa Kenyatta Uhuru Kenyatta kupitia kuwaruhusu wapinzani wake wa kisiasa kufanya siasa zao bila vikwazo, kulingana na gazeti la The Citizen nchini Tanzania.
Akihutubia mkutano wa umma katika wadi ya Murieti, Lema alimsifu rais Kenyatta na kusema ameoonyesha ukomavu wa kisiasa kwa kuwaruhusu wapinzani wanaomtuhumu kwamba alihusika na udanganyifu katika uchaguzi mkuu uliokamilika hivi majuzi kufanya maandamano mbali na kuwapatia maafisa wa usalama kuwalinda
Kulingana na gazeti hilo ,Rais Uhuru Kenyatta ambaye alikuwa akitetea kiti chake aliibuka mshindi katika uchaguzi huo kwa kupata asilimia 54 ya kura huku mpinzani wake Raila Odinga akijipatia asilimia 44.
Kulingana na Lema maandamano ya upinzani pamoja na mikutano ya uma itaisaidia serikali kwa sababu chama tawala kitaelewa maswala yanayowakabili raia na kuyafanyia kazi huku upinzani ukitekeleza haki yao ya kidemokrasia kupitia kushirikiana na umma mbali na kutatua maswala muhimu yanayowakabili raia.
''Demokrasi ni swala tata, mara nyengine linaweza kuathiri uchumi. Wawekezaji wengi huchunguza kiwango cha demokrasia katika taifa kabla ya kuwekeza. Iwapo tutaendelea na mkondo huu basi utatukwaza katika siku za usoni'', alisema.

Msaidizi mkuu wa Donald Trump katika ikulu ya White House Steve Bannon afutwa

Steve BannonHaki miliki ya pichaAFP
Mkuu wa mikakati wa Rais Donald Trump katika ikulu ya White House Steve Bannon amefutwa kazi na kuwa msaidizi wa karibuni zaidi wa Trump kuondoka katika wadhifa wake.
Katibu wa mawasiliano na wanahabari katika ikulu hiyo Sarah Huckabee Sanders amethibitisha kwamba Ijumaa ilikuwa siku ya mwisho kwa Bannon kazini.
Kuondoka kwake kumejiri baada ya kutathminiwa kwa wadhifa wake na Mkuu wa Watumishi wa Rais John Kelly.
Bw Bannon ni mtetezi wa taifa mwenye kufuata siasa za mrengo wa kulia.
Alikuwa mkuu wa tovuti ya Breitbart.com na alisaidia pakubwa kueneza ujumbe wa "America First" (Marekani Kwanza) wa Trump wakati wa kampeni za urais mwaka jana.
Lakini wakosoaji wamemtuhumu Bannon, 63, kwa kuwa na chuki dhidi ya wayahudi na kuwa mtu anayeamini katika ubabe wa wazungu.
Bw Bannon anadaiwa kushindania udhibiti wa ikulu dhidi ya mirengo ya watumishi wenye misimamo ya wastani ikulu, wakiwemo baadhi ya jamaa wa Trump.
Bw Trump alianzisha uvumi kumhusu Bannon alipoulizwa kuhusu mustakabali wake wiki iliyopita lakini akajibu: "Tutasubiri tuone."
Mahojiano ya Bannon na jarida la msimamo huru la American Prospect wiki hii yanadaiwa kumkera Trump.
Bannon alinukuliwa akipuuzilia mbali wazo la kutumia jeshi kutatua mzozo kuhusu Korea Kaskazini, jambo lililotazamwa kama kwenda kinyume na msimamo wa Trump.
Aliambia jarida hilo kwamba Marekani ilikuwa katika "vita vya kiuchumi na China" na kwamba analenga kuwaondoa watu wenye msimamo wa wastani serikali ya Trump ambao anaamini wana msimamo usio mkali sana dhidi ya China.
Bannon baadaye aliambia washirika wake kwamba alidhani alikuwa anaongea akipiga gumzo tu na kwamba hakutarajia angenukuliwa.
Nani mwingine ameondoka White House?
Anthony Scaramucci, mkurugenzi wa mawasiliano - 31 Julai
Reince Priebus, mkuu wa watumishi wa rais ikulu - 28 Julai
Sean Spicer, mkuu wa mawasiliano na wanahabari - 21 Julai
Mike Dubke, mkurugenzi wa mawasiliano 30 Mei
Michael Flynn, mshauri mkuu wa usalama wa taifa - 14 Februari

Bannon alichukuahatamu kama kiongozi wa kampeni ya urais ya Trump Agosti 2016.
Aliwahi kuhudumu katika jeshi la wanamaji la Marekani, mwekezaji wa benki katika Goldman Sachs, produsa wa filami Hollywood na mkuu wa Breitbart News.
Anadaiwa kuwaambia marafiki zake kwamba huenda akarejea katika shirika hilo la Breibart lenye msimamo mkali ambalo limekuwa likimuunga mkono Trump.

Faru aliyesombwa na mafuriko kutoka nchini Nepal hadi India aokolewa

The young female rhinoHaki miliki ya pichaISHWOR JOSHI
Image captionFaru huyo wa kike alipatikana umbali wa kilomita 42 kutoka mbuga ya Chitwan iliyo kijiji cha Bagah.
Faru kutoka familia ya wale walio kwenye hatari ya kuangamia ambaye alisombwa na mafuriko kutoka nchini Nepal hadi India ameokolewa na kurudishwa nyumbani.
Faru huyo wa kike alipatikana umbali wa kilomita 42 kutoka mbuga ya Chitwan iliyo kijiji cha Bagah.
Faru wengine wanne kutoka mbuga hiyo wanahitaji kuokolewa na mmoja tayari amepatikana akiwa amekufa.
Bonde la Chitwan nchini Nepal, iliyo mbuga ya wanyamapori ambayo ni makao kwa faru 600, imeathirika vibaya na mafuriko.
Wiki iliyopita ndovu kadha na mashua vilitumiwa kuwaokoa karibu watu 500 waliokuwa wamekwama eneo hilo.
Teams help unloads the returning rhinoHaki miliki ya pichaISHWOR JOSHI
Image captionKundi la maafisa 40 wa Nepal walitumwa kumridisha nyumbani faru huyo wa umri wa miaka miwili unusu.
The young rhino emerges from her crateHaki miliki ya pichaISHWOR JOSHI
Image captionKundi la maafisa 40 wa Nepal walitumwa kumridisha nyumbani faru huyo wa umri wa miaka miwili unusu.
Kundi la maafisa 40 wa Nepal walitumwa kumridisha nyumbani faru huyo wa umri wa miaka miwili unusu.
Mamia ya watu raia wa India walifika kutazama shughuli hiyo ya uokoaji.
Msimu wa mvua unaonza mwezi Juni hadi Septemba husababisha mafuriko kote eneo hilo kila mwaka.
Katika jimbo la Assam nchini India, faru sita wameripotiwa kufa maji kufuatia mafuriko katika mbuga ya Kaziranga.