Thursday, April 26

Askari watanda mitaani Mbeya


Askari wenye silaha, wameonekana katika maeneo mbalimbali ya jiji la Mbeya hasa katika miji ya Mbozi, Tunduma na Mkoa wa Songwe.
Askari hao wameonekana wakiranda randa mitaani huku wakishikilia silaha za moto kutokana na kuwapo kwa tishio la maandamano nchi nzima.
Maeneo waliyoimarisha ulinzi ni pamoja na njia ya panda ya Ilomba ambako kuna  barabara kutoka Isyesye na Mwambene kuingia barabara kuu ya Mbeya-Zambia.
Maeneo mengine ni ‘Airport’ ya zamani na Barabara Kuu ya Mbeya- Zambia, ambako askari wa kutosha walipiga kambi wakiwa na magari zaidi ya sita.
Magari mengine yalionekana yakifanya doria mitaa ya Kabwe, Mwanjelwa, Soweto na barabara ya kwenda Ilemi kutoka Crossway-Kabwe.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Mussa Taibu amesema hali ya usalama kwa jiji la Mbeya na maeneo mengine ya mkoa huo ni shwari na wananchi wametii sheria bila shuruti huku wakiendelea shughuli zao kama kawaida.

Tisa wakamatwa kwa kuandamana Dar


Jeshi la Polisi Kanda Maalumu limewakamata watu tisa kwa tuhuma za kufanya maandamano.
Akizungumza na MCL Digital leo Aprili 26, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Lazaro Mambosasa amesema watuhumiwa hao wamekamatwa Mtaa wa Samora, Posta katikati ya mji.
"Tumewakamata watuhumiwa tisa akiwamo, mwanafunzi wa Chuo cha Kilimanjaro kilichopo Mwenge akiwa na bango linalohamasisha maandamano," amesema Mambosasa na kuongeza:
“Tunaendelea kumhoji na wenzake wanane, tutakapokamilisha mahojiano hatua zaidi zitafuata.”
Kuhusu hali ya usalama Kamanda Mambosasa amesema jeshi limejipanga kuimarisha ulinzi usiku na mchana hakuna mtu yeyote atakayevunja sheria.

MZEE MAJUTO KUPELEKWA NCHINI INDIA KWA MATIBABU

Msanii mkongwe wa filamu za vichekesho nchini, King Majuto anatarajia kupelekwa nchini India kwa matibabu kutokana na tatizo linalomkabili. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, mara baada ya kutoka kumsalimia Mzee Majuto ambaye amelazwa katika hospitali ya Tumaini, Mwenyekiti wa Uzalendo Kwanza Steve Mengele 'Steve Nyerere' amesema kuwa uamuzi huo umekuja baada ya kuona mzee Majuto amekuwa akihangaika mara kwa mara kutafuta matibabu.

 "Tumeona mzee wetu anahangaika na matibabu ya mara kwa mara ambayo hayakamiliki sasa tumekuja na wazo la kumpeleka nchini India ili akatibiwe tatizo lake liishe na huu ndiyo wakati mwafaka wa watu tujitoe si mpaka mtu ashindwe kuongea tuanze michango," alisema nyerere. "Jamani ifike wakati tujitoe kumsaidia mtu akiwa yupo hai na tusisubiri afariki ndiyo tuanze kuchanga, wakati ni sasa akiwa anaumwa tunamchangia anapatiwa matibabu na anaendelea na maisha," amesema Nyerere.

 Tunamshukuru Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutuunga mkono kusaidia mwenzetu, pia Mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM Taiga (NEC) Salim Asas ambaye yeye amesema atatusaidia kwa hali na mali na ameanza kutupa tiketi 2 za ndege. Tunataka mwenzetu akatibiwe maradhi yake yaishe aendelee na majukumu yake ya kujenga nchi na familia yake kwa ujumla. 

Nyerere amewaomba wadau mbali mbali akiwemo Azam, DSTV na wengine wote wenye mapenzi mema kumsaidia mzee Majuto ili apone na aendelee na shughuli. Kwa Upande wa Mzee Majuto amewashukuru watu wote ambao wamekuwa wakijitokeza kumsalimia na waendelee kumuombea ili apone. "Sina cha kuwapa zaidi ni kuwaombea muendelee na moyo mlionao, mimi sina pingamizi kwenda kutibiwa nchini India, nipo tayari kamilisheni mipango yote mje kunichukua," amesema. Ujumbe wa Steve Nyerere uliambatana na msanii mwenzake Aunty Ezekiel pia wakiwemo na waandishi wa habari wa mitandao ya jamii.
Mwenyekiti wa Uzalendo Kwanza Steve Mengele 'Steve Nyerere' akimsalimia Mzee Majuto ambaye amelazwa katika hospitali ya Tumaini jijini Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Uzalendo Kwanza Steve Mengele 'Steve Nyerere' akiongea machache mara baada ya kumtembelea Mzee Majuto ambaye amelazwa katika hospitali ya Tumaini jijini Dar es Salaam. Mzee Majuto akitoa shukrani zake mara baada ya kutembelewa na kuonyeshwa mwanga wa matibabu zaidi nchini India.
Msanii Aunty Ezekiel akimsalimia Mzee Majuto.

RAIS DKT. MAGUFULI AWAONGOZA MAELFU YA WATANZANIA KATIKA SHEREHE ZA MIAKA 54 YA MUUNGANO WA TANGANYIKA NA ZANZIBAR ZILIZOFANYIKA MKOANI DODOMA


Amiri Jeshi Mkuu, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa amesimama wakati akipigiwa wimbo wa Taifa kabla ya kwenda kukagua gwaride la heshima lililoandaliwa na vikosi mbalimbali vya Majeshi ya Tanzania katika maadhimisho ya Sherehe za miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zilizofanyika katika uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma.
Amiri Jeshi Mkuu, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akielekea kukagua gwaride la heshima lililoandaliwa na vikosi mbalimbali vya Majeshi ya Tanzania katika maadhimisho ya Sherehe za miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zilizofanyika katika uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma.
Amiri Jeshi Mkuu, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikagua gwaride la heshma katika maadhimisho ya Sherehe za miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zilizofanyika katika uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma.
Amiri Jeshi Mkuu, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein mara baada ya kuwasili katika jukwa kuu kwa ajili ya maadhimisho ya Sherehe za miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zilizofanyika katika uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma.


Vikosi mbalimbali vya Jeshi la Wananchi, Magereza na Polisi vikipita kutoa heshma mbele ya Amiri Jeshi Mkuu, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli (haonekani pichani )katika ya maadhimisho ya Sherehe za miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zilizofanyika katika uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma.
Kikosi cha Makomando wa (JWTZ) kikipita na kutoa heshma mbele ya Amiri Jeshi Mkuu, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli (haonekani pichani )katika ya maadhimisho ya Sherehe za miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zilizofanyika katika uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma.
Mmoja wa Makomando wa JWTZ akitoa Heshma kwa kupiga Saluti wakati akipita mbele ya Amiri Jeshi Mkuu, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli (haonekani pichani )katika ya maadhimisho ya Sherehe za miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zilizofanyika katika uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma.
Mmoja wa Makomando wa JWTZ akiwasili ndani ya uwanja wa jamhuri kwa kutumia kamba katika maadhimisho hayo ya Miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Mmoja wa Makomando wa JWTZ akionesha umahiri wake wa kuvuta gari kwa kutumia meno katika ya maadhimisho ya Sherehe za miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zilizofanyika katika uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma.
Amiri Jeshi Mkuu, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipiga makofi na Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Pili wa Rais wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Benjamin Mkapa Pamoja na Jaji Mkuu Profesa Ibrahim Juma, wakati kikundi cha Halaiki kilipokuwa kikipita mbele kutoa heshma katika ya maadhimisho ya Sherehe za miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zilizofanyika katika uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma.

Askari wa Jeshi la Magereza wakionesha umahiri wa kupambana na vikwazo mbalimbali katika ya maadhimisho ya Sherehe za miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zilizofanyika katika uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma.
Amiri Jeshi Mkuu, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa amesimama pamoja na Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli, Spika wa Bunge Job Ndugai wakati kikundi cha vijana wa Halaiki walipokuwa wakipita mbele kutoa heshma.
Amiri Jeshi Mkuu, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia katika maadhimisho ya Sherehe za miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zilizofanyika katika uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma. PICHA NA IKULU.

Madonna ashindwa kuzuia barua za uhusiano wake na Tupac Shakur kupigwa mnada

MadonnaHaki miliki ya pichaREUTERS
Msanii wa muziki wa pop Madonna amepoteza kesi ya kumzuia rafikiye wa zamani kutouza barua za kuvunjika kwa uhusiano wa kimapenzi kati yake na Tupac Shakur, ikiwemo kichana.
Jaji wa New York alitupilia mbali kesi ya Madonna dhidi ya Darlene Lutz akisema kuwa muda wa kuvipata vitu hivyo umekwisha.
Mojawapo ya vitu hivyo ni braua ya kuvunjika kwa uhusiano kati yake na msanii Tupac Shakur aliyefariki 1996 ambaye alikuwa na uhusiano wa kisiri na Madonna.
Mnada huo sasa utafanyika mwezi Julai, kulingana na mtandao wa Burudani TMZ.
Madonna alidai kwamba hakujua kwamba bi Lutz alikuwa akimiliki barua za Tupac alizoandika 1995 hadi aliposikia kuhusu mnada huo wa mtandaoni mwaka uliopita.
Tupac (R) na MadonnaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionMadonna na Tupac walikuwa na uhusiano wa kisiri kwa muda usiojulikana
Katika barua hiyo iliojaa hisia, msanii huyo wa Rap alimwambia Madonna kwamba kuwa na uhusiano na mtu mweusi kutamsaidia katika kazi yake na kwamba sura yake itaharibika iwapo ataanza uhusiano na mtu mweupe.
Wapenzi hao walikuwa katika uhusiano wa kisiri ambao ni hivi majuzi ambapo Madonna alikubali kutangaza wazi.
Msanii huyo na bi Lutz walikosana mwaka 2003 na baada ya kumaliza mgogoro kuhusu mchoro mwaka uliokuja, Madonna alitia saini barua ya kujiondoa katika madai yoyote ya rafikiye wa zamani , jaji Gerald Lebovits alisema katika uamuzi wake siku ya Jumatatu.
Hivyobasi alielezea kwamba nyota huyo wa muziki wa Pop hawezi tena kumshtaki kutokana na vitu alivyovipiga mnada.
Madonna aliiambia mahakama mwaka uliopita wakati alipojaribu kuzuia mnada wa vitu hivyo kwamba umaarufu wake haumpatia uwezo wa kutaka kuhifadhi hati yake ya faragha ikiwemo vitu kama hivyo.
Mawakili wa bi Lutz wamemshutumu Madonna kwa kuwa na vita vya kibinafsi dhidi yake.

Madaktari wafanikiwa kufanya upandikizaji wa kwanza wa uume duniani

Jopo la madaktari katika chuo kikuu cha Johns Hopkins walipomfanyiaHaki miliki ya pichaJOHNS HOPKINS MEDICINE
Image captionJopo la madaktari katika chuo kikuu cha Johns Hopkins walipomfanyia upandikizaji wa uume
Jopo la madaktari wamefanikiwa kufanya upandikizaji wa kwanza wa uume na korodani.
Upasuaji huo waliomfanyia askari alijeruhiwa na bomu huko Afghanistan katika chuo cha Johns Hopkins mjini Baltimore, Maryland,
Madaktari hao walitumia uume na korodani zilizoondolewa kwa watu waliokufa.
Madaktari hao wamesema askari huyo atarudishiwa uwezo wa kufanya mapenzi ,jambo ambalo sio rahisi kama mtu akifanyiwa upasuaji wa uume.
Upasuaji huo umefanyiwa upasuaji mara nne kumi na moja na upandikizi huu ulitumia masaa kumi na nne tarehe 26 machi mwaka huu.
Huu ni upasuaji wa kwanza kumalizika salama na kurejesha sehemu hizo kurudi kwenye hali yake ya kawaida.
Madaktari wanasema kwamba korodani kutoka kwa mfadhili hazijapandikizwa kutokana na sababu za maadili.
Askari aliyefanyiwa upandikizaji ametaka kutofahamika ,
„Nilipoamka nilijisikia kuwa nimerudi kwenye hali yangu ya kawaida,kiukweli niko sawa kwa sasa".
Askari huyo alieleza.
Wataalamu wa upasuaji huo wanatarajia kuwa askari huyo atapona ndani ya miezi 6 hadi 12.

Bakteria wanaweza kuathiri namna unavyojisikia au kuwaza

Bakteria wanaweza kuathiri namna ambavyo tunavyofikiri au kuwaza
Image captionBakteria wanaweza kuathiri namna ambavyo tunavyofikiri au kuwaza
Kama kuna kitu chochote kile kinatufanya sisi tuwe binadamu ni fikra ,mawazo na hisia.
Na bado kuna mjadala unaoangalia mtazamo mpya uliojitokeza kudai kwamba bakteria wanaoingia tumboni bila kuonekana wanasababisha athari katika akili zetu.
Sayansi inajumuisha pamoja trilioni ya vijiumbe maradhi ambavyo vinaishi ndani yetu sote na hivyo huathiri afya zetu za kimwili
Lakini hata hivyo hali hii hujumuisha msongo wa mawazo,ugonjwa wa utindio wa ubongo na ugonjwa wa akili ,vyote kwa pamoja vinahusishwa kusababishwa na viumbe hawa vidogo.
Tunajua kwa karne namna ambavyo matumbo yetu yamekuwa yakiathirika,fikiria tu namna ambavyo tumbo linaweza kukuuma kabla ya mtihani au usaili wa kazi lakini sasa ilionekana katika mitazamo miwili tofauti .
Baadhi ya watafiti wanaamini kwamba huu ni wakati wa kufanya mabadiliko ya kutokomeza vimelea vinavyowafanya watu wajisikie hali ya tofauti au kuchanganyikiwa akili na watu kutengemaa kwakuwa na afya nzuri. .
Bakteria wanaweza kuathiri ubongo
Image captionBakteria wanaweza kuathiri ubongo
Watafiti wanaonyesha kwamba bakteria hao huongeza homoni za watu kuwa na msongo wa mawazo.
Utafiti uliofanywa na wanasayansi ukihusisha vimelea vilivyofanyiwa jaribio kwa panya ambao waliokuwa nao na wasiokuwa nao,tabia zao zilikuwaje n ahata namna ambayo ubongo wao ulivyofanya kazi.
Lakini kukuwa kwao ni tofauti kabisa na ulimwengu halisi. Binadamu daima tunawasiliana na viumbe vidogo katika mazingira yetu, hakuna hata mmoja wetu asiye na vijidudu hivi.
Aidha aina ya maisha tunayoisha pia husababisha kuwaamsha hao bakteria,kama vile kutokula mlo kamili au mdogo unatuweka katika mazingira rahisi zaidi ya kuathirika na vimelea hivyo.
Asilimia kubwa ya miili yetu ina vimelea vya maradhi
Image captionAsilimia kubwa ya miili yetu ina bakteria maradhi
Inawezekana kuwa asilimia kubwa ya mwili wako una vimelea hivi vya maradhi ambavyo vinajumuisha bakteria,virusi na fangasi.
Hivyo namna ambavyo hakuna uwiano wa kinga ya mwili na vimelea basi hali ya msongo wa mawazo inaweza kujitokeza na kubadilika kwa tabia.
Vijidudu wanaoingia tumboni wanaweza kusababisha msongo wa mawaz
Image captionVijidudu wanaoingia tumboni husababisha athari katika ubongo
Kuna ushaidi wa awali unaothibitisha uhusishwaji wa vimelea hivyo katika ubongo .
Wataalamu wana nia ya kuwezesha kubadili tabia inayosababisha kuenea kwa ugonjwa huu na kuhamasisha afya njema kwa kila mtu.

Israel yafutilia mbali mpango wa kuwatimua wahamiaji Waafrika

Waandamanji Israel dhidi ya mpango wa kuwahamisha kwa lazimaHaki miliki ya pichaAFP/GETTY
Image captionHtama ya wahamiaji wa Afrika imezusha mzozo mkubwa
Israel imefutilia mbali mpango wa kuwatimua kwa lazima maelfu ya wahamiaji haramu wa kutoka Afrika.
Katika barua iliyoiandikia mahakama ya juu zaidi ya Israel, serikali imesema kwamba kuwatimua kwa lazima wahamiaji kutoka mataifa ya Afrika, "sio suala kuu katika ajenda".
Hatahivyo, maafisa wa uhamiaji wa Israel bado wanatafuta njia za kuwahamisha wahamiaji hao kwa hiari, ilisema barua hiyo.
Htamaya wahamiaji haramu takriban 30,000 kutoka mataifa ya Afrika imekuwa ni suala linalozuhs amzozo mkubwa.
Mahakam ya juu zaidi nchini humo awali ilisitisha mipango ya kuwahamisha wahamiaji hao - wengi wao kutoka Eritrea na Sudan - ila iwapo watakubali kwa hiari kupokea kitita cha fedha na tiketi ya ndege kutoka Israel.
Waziri mkuu Benjamin Netanyahu baada ya hpo aliafutilia mbali makubaliano na Umoja wa mataifa kuwatafutia makaazi wahamiaji hao katika mataifa ya magharibi.
Wazir mkuu wa Israel Benjamin NetanyahuHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionWaziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ameshutumiwa nyumbani na kimataifa kuhusu suala hilo
Chini ya makubaliano hayo, Israel ilistahili kutoa makaazi ya muda kwa mhamiaji Israel kwa kila mhamiaji anayetafutiwa makaazi ng'ambo.
Siku ya Jumatatu, Wanachama 18 wa Democratic katika bunge la wawakilishi inaarifiwa wamemuandikia Netanyahu barua wakimuambia kwamba 'wameshangazwa' na 'kuvunjwa moyo' na hatua yake kufutilia pendekezo hilo la Umoja wa mataifa wakieleza kuwa iliwaacha wahamiaji katika njia panda na bila ya muelekeo wa 'hatua inayofuata'.
Wahamiaji wanatoka wapi?
Baadhi ya wahamiaji wa Afrika nchini Israel wanatoka Eritrea - taifa la chama kimoja ambalo viongozi wake wameshutumiwa kwa uhalifu dhidi ya binaadamu na jopo la uchunguzi la Umoja wa mataifa na taifa la Sudan lililoathirika na vita.
Wanasema wametoroka hatari nyumbani na kwamba sio salama kwao kurudi katika nchi nyingine ya Afrika, lakini Israel inatizama baadhi ya watafuta hifadhi hao wa Afrika kuwa wahamiaji wa kiuchumi.
Wengi wao waliwasili kutoka Misri miaka kadhaa nyuma, kabla ya ukuta mpya kujengwa katika mpaka jangwani.
Hili limesitisha kwa kiwango kikubwa uhamiaji huo haramu.
Wahamiaji wa kutoka Afrika katika kituo cha kizuizi kusini mwa IsraelHaki miliki ya pichaEPA
Image captionWahamiaji wa kutoka Afrika katika kituo cha kizuizi kusini mwa Israel
Suala hili linazusha mzozo kiasi gani?
Uamuzi uliopitishwa Januari kuwapa wahamiaji kitita cha pesa na tiketi ya ndege kutoka Israel kwa hiari au kwa namna nyingine kwa kushurutishwa umeshutumiwa Israel.
Baadhi ya wakosoaji nchini na kwa baadhi ya jamii ya wayahudi walioko ng'amb o - wakiwemo mabalozi wa zamani na manusura ya mauaji ya kimbari - Holocaust - wanasema mpango huo hauna maadili na ni doa katika sura ya kimataifa ya taifa hilo.
Shirika la Umoja wa mataifa la kuwashughulikia wakimbizi limesema hatua hiyo inakiuka sheria za nchini na kimataifa na kulishuhudiwa maandamano makubwa Israel.
Netanyahu amesema kupingwa kwa hatua hiyo ni upuuzi mtupu usiokuwa na msingi na kwamba Israel itawapa hifadhi "wakimbizi wa kweli".
Hatahivyo, wanaharakati wamegusia kwamba ni wahamiaji wachache tu kutoka Eritrea na Sudan waliotambuliwa kama wakimbizi nchini Israel tangu nchi hiyo ipokee jukumu la kushughulikia maombi ya wahamiaji kutoka kwa Umoja wa mataifa mnamo 2009.

Mabwawa mawili yakaribia kufurika nchini Kenya kufuatia mvua kubwa

mafuriko
Image captionmafuriko
Mabwawa mawili nchini Kenya yanakaribia kufurika kutokana na mvua kubwa , inayotishia maisha ya maelfu wa raia , kulingana na shirika la msalaba mwekundu lililozungumza na BBC.
Abbas Gullet , mkuu wa shirika la msalaba mwekundu nchini Kenya amewashauri raia wanaoishi katika eneo la Afrika mashariki na kati kuelekea katika maeneo ya juu.
Alisema kuwa takriban watu 200,000 wamewachwa bila makao kutokana na mafuriko huku wengi wakilazimikika kuishi katika shule ama maeneo yalio wazi.
Mafuriko yatatiza jtihada za kuwasaidia waathirika Kenya
Barabara zimejaa maji huku maporomoko yakiripotiwa katika maeneo mengine.
Mabwawa hayo ya Masinga na Kamburu hupata maji yake kutoka Mlima Kenya.
Watu wamekuwa wakisambaza picha katika mitandao ya kijamii kuhusu hatma ya mafuriko hayo, ikiwemo picha moja ya afisa wa msalaba mwekundu aliyekuwa akimsaidia mzee mmoja kusini mashariki mwa kaunti Tanariver , ambapo watu 50,000 wamelazimika kuyawacha makaazi yao.