Saturday, November 4

Kiongozi wa genge auawa Mexico akibadili sura

Jesus Martin au El Kalimba amekuwa akisakwa na polisi kwa kuendesha biashara ya kuiba mafuta kwa kukata mabomba ya usafirishaji wa bidhaa hiyo muhimu.Haki miliki ya pichaEPA
Image captionJesus Martin au El Kalimba amekuwa akisakwa na polisi kwa kuendesha biashara ya kuiba mafuta kwa kukata mabomba ya usafirishaji wa bidhaa hiyo muhimu.
Kiongozi mmoja wa genge nchini Mexico ameuawa kwa kupigwa risasi wakati alipokuwa katika kliniki akifanyiwa upasuaji wa kubadili sura yake mbali na kuondosha alama zake za vidole.
Maafisa wanasema kwamba watu walio na silaha walivamia kliniki hiyo ya mjini Puebla na kumfyatulia risasi kiongozi huyo wa genge Jesus Martin, anayejulikana pia kwa jina la mtaani El Kalimba.
Maafisa hao wanaendelea kueleza tathmini yao kwamba tukio hilo ni baada ya ugomvi baina ya magenge hasimu ambapo pia watu wengine watatu wamefariki .
Jesus Martin au El Kalimba amekuwa akisakwa na polisi kwa kuendesha biashara ya kuiba mafuta kwa kukata mabomba ya usafirishaji wa bidhaa hiyo muhimu.
Ukubwa wa biashara hiyo umefananishwa na ile ya ulanguzi wa mihadarati nchini Mexico.

Patrice Evra afukuzwa uwanjani kwa kumshambulia shabiki wa Marseille

Patrick EvraHaki miliki ya pichaOFFSIDE
Image captionPatrice Evra
Patrice Evra ambaye kwa sasa huchezea Marseille ya Ufaransa alifukuzwa uwanjani baada ya kumshambulia mmoja wa mashabiki wa timu hiyo wakati wa kujiandaa kwa mechi.
Evra alimpiga kichwani shabiki wachezaji wakipasha misuli moto uwanjani kabla ya kuanza kwa mechi ya ugenini dhidi ya Vitoria Guimaraes katika ligi ndogo ya klabu Ulaya, Europa League.
Marseille walilazwa 1-0 mechi hiyo.
Picha za video zinamuonesha mchezaji huyo wa zamani wa Manchester United mwenye miaka 36 akiruka juu na kumpiga teke shabiki huyo.
Evra, ambaye alikuwa ametajwa kwenye benchi, alifukuzwa uwanjani hata kabla ya mechi kuanza.
Marseille walianza wakiwa na wachezaji 11.
Shirikisho la soka Ulaya Uefa limemfungulia mashtaka ya kufanya kitendo cha ghasia.
Amesimamishwa kucheza "angalau mechi moja" huku Uefa wakitarajiwa kuamua hatima yake 10 Novemba.
Patrice EvraHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionEvra amechezea Marseille mechi mbili pekee tangu jiunge nao kutoka Juventus Januari
Gazeti la Ufaransa la L'Equipe limesema mashabiki wa Marseille walikuwa wamemzomea Evra kwa karibu nusu saa wachezaji walipokuwa wakijiandaa kwa mechi.
Evra alikuwa ameenda kuzungumza nao kuwatuliza lakini badala ya kupunguza kelele, wakazidisha na hali ikabadilika ghafla.
Mwanahabari wa Ufaransa Julien Laurens amesema Evra - ambaye mara nyingi hupakia video za ucheshi kwenye mitandao ya kijamii - alitukanwa na kuambiwa: "Endelea kuandaa na kusambaza video zako, lakini uache kucheza kandanda."
L'EquipeHaki miliki ya pichaL'EQUIPE
Image captionGazeti la L'Equipe lilivyoripoti kisa hicho
Marseille wamesema wameanzisha uchunguzi kuhusu kisa hicho na kusisitiza kwamba mchezaji wakati wowote anafaa kujituliza hata anapozomewa au kurushiwa matusi.
Kisa hicho kimewakumbusha wengi kuhusu "kiki cha kung-fu" ya Eric Cantona wakati wa mechi kati ya Manchester United na Crystal Palace uwanjani Selhurst Park Januari 1995.
Mfaransa huyo alipigwa marufuku miezi tisa na Chama cha Soka cha England kutokana na kisa hicho ambacho kilitokea alipokuwa akiondoka uwanjani baada ya kulishwa kadi nyekundu.
Eric Cantona akimpiga Matthew SimmonsHaki miliki ya pichaACTION IMAGES
Image captionCantona hakujaribu kujitetea kwa kitendo hicho chake

Madaktari wa kujitolea wa China kuendelea kufanya kazi nchini


Dar es Salaam. Balozi wa China nchini, Wang Ke amesema Watanzania 15.2 milioni wametibiwa na madaktari wa kujitolea wa Taifa hilo ambao wamekuwa wakifika Tanzania tangu mwaka 1968.
Akizungumza jana Ijumaa Novemba 3,2017 wakati wa kuwaaga madaktari waliokuwepo nchini kwa miaka miwili, Balozi Wang amesema hilo ni kundi la 24 la madaktari kuingia nchini tangu mpango huo ulipoanza na wataendelea kuwaleta wengine.
Amesema madaktari hao wamekuwa wakitoa huduma wakisaidiana na wenzao wa Tanzania katika hospitali za Muhimbili, Dodoma, Tabora na Musoma.
Balozi Wang amesema madaktari hao 25 wamebobea katika magonjwa mbalimbali ukiwemo wa moyo.
"Mbali na kuhudumu katika hospitali hizo, walikwenda vijijini kuwafuata wagonjwa na kuwahudumia,” amesema.
Amesema katika awamu ya 24, madaktari hao wametoa dawa na vifaa tiba vyenye thamani ya Sh125 milioni.
Balozi Wang amesema baada ya madaktari hao kuondoka, watakuja wengine kwa kuwa mpango huo ni endelevu.
"Tutaendelea kuleta madaktari ili washirikiane na wenzao wa Tanzania kwa lengo la kuwapatia uzoefu," amesema.
Akizungumza katika hafla hiyo, Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema mpango wa Serikali ni kuhakikisha wagonjwa wote wanatibiwa nchini badala ya kuwapeleka nje ya nchi.
Amesema ili kufanikisha lengo hilo, Hospitali ya Taifa Muhimbili na hospitali za kanda zinahitaji kuboresha huduma zake.
Mwalimu amesema ndiyo maana Serikali imeiomba China madaktari 11 ambao watafanya kazi Muhimbili, Taasisi ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu Muhimbili (MOI), Hospitali ya Rufaa Mbeya na Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI).
"Tunashukuru kwa kutupatia madaktari hawa na tunatarajia Serikali ya China itaendelea kutusaidia wataalamu zaidi wa afya," amesema.
Waziri Mwalimu amesema mpango wa madaktari wa kujitolea kuja nchini umepunguza idadi ya wagonjwa wanaokwenda nje kutibiwa.
Kiongozi wa madaktari hao, Dk Sun Long amesema kwa miaka miwili waliyokaa Tanzania wamewapa uzoefu wenzao waliopo nchini.
Dk Sun ambaye ni daktari wa upasuaji wa moyo amesema madaktari wa moyo ni wachache Tanzania, hivyo ameshauri wasomeshwe wataalamu wa aina hiyo.

Mgogoro wa madiwani, DC kupima uwezo wa waziri



Naibu waziri wa Tamisemi, Joseph Kakunda
Naibu waziri wa Tamisemi, Joseph Kakunda 
Tunduma. Mgogoro wa madiwani wa Halmashauri ya Tunduma na mkuu wa Wilaya ya Momba, Jumaa Irando umezidi kuwa mwiba kwa Serikali baada ya naibu waziri wa Tamisemi, Joseph Kakunda kufika mjini hapa na kusikiliza hoja za pande zote lakini akashindwa kutoa uamuzi.
Hata hivyo, Kakunda katika kikao kilichofanyika faragha bila kuhusisha vyombo vya habari, aliahidi kutoa uamuzi wa mgogoro huo kabla ya Novemba 6.
Mgogoro huo ulianza baada ya mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Ally Mwafongo na mbunge wa Tunduma, Frank Mwakajoka kutangaza hadharani kuondoa ushirikiano na Irando kuanzia kwa wenyeviti wa Serikali za mitaa kwa madai amekuwa akiingilia na kuchukua uamuzi kwa kutumia ubabe.
Hata hivyo, baada ya tamko hilo ambalo lilitolewa na Mwafongo katika mkutano wa hadhara mjini Tunduma Agosti 18, Irando naye akajibu mapigo kwa kuandika waraka maalumu kwa watendaji wote wa Serikali kutopokea maelekezo wala amri yoyote kutoka kwa madiwani hao. Pia, alifuta vikao vyote vya baraza la madiwani la halmashauri hiyo.
RC anyanyua mikono
Mgogoro baina ya vigogo hao umefikia hatua ya kukosa ufumbuzi wa kudumu baada ya mkuu wa Mkoa wa Songwe, Chiku Galawa naye kuonekana kushindwa kuutatua na kuamua kuitupia ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi).
Jumatatu ya wiki hii, naibu waziri huyo alilieleza gazeti hili kuhusiana na safari yake Tunduma kuwa, mgogoro wa viongozi hao ni mkubwa na unahitaji umakini na busara zaidi katika kuupatia ufumbuzi.
Jumanne, Kakunda alifika Tunduma na kufanya kikao cha faragha kusikiliza hoja za pande zote.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti kilichoamriwa na Kakunda baada ya kikao hicho, mkuu wa wilaya hiyo Irando na Mwafongo walisema kila upande ulipata nafasi ya kutoa hoja zake lakini hawakupewa uamuzi papo hapo.
Irando aliliambia gazeti hili kuwa Kakunda alisikiliza hoja za madiwani kwa kuwa taarifa zake (Irando) alishaziwasilisha wizarani muda mrefu. “Kwa upande wangu taarifa anazo kwa kuwa tulishapeleka muda mrefu hivyo hapa alikuwa anawasikiliza madiwani, tunasubiri jibu la uamuzi utakaoamriwa, ila sisi tunaendelea kuchapa kazi na mambo yapo vilevile,” alisema.
Naye Mwafongo alisema walitoa hoja zao katika kikao hicho huku akimshukuru Kakunda kwa kuwasikiliza kwa utulivu na kutoa ahadi ya kutoa suluhisho la mgogoro huo kabla ya Novemba 6.
“Kinachoonekana hapa kulikuwa na taarifa tofauti kuhusu mgogoro huu, tulitangaza kuondoa ushirikiano na Irando (mkuu wa wilaya) kutokana na kutoridhishwa na utendaji wake wa kibabe, hivyo tunaona hatoshi katika wadhifa wake lakini hatukusema hatuitambui Serikali kama wanavyodai,” alisema Mwafongo.
Alisema madiwani kupitia baraza lao wataendelea kufanya kazi za kuishauri Serikali kwa mustakabali wa maendeleo ya wananchi, lakini wanapoona mtu mmoja ama kikundi kinataka kufanya jambo kinyume na matarajio ya wengi watapaza sauti kwa kufuata taratibu zinatotakiwa.

Mahakama yaamuru DC akamatwe, mwenyewe asema hana taarifa


Mwanza/Bukoba. Mahakama ya Hakimu Mkazi Bukoba imetoa hati ya kumkamata na kumfikisha mahakamani Mkuu wa Wilaya ya Misenyi, Dennis Mwira kwa kosa la kupuuza amri ya Mahakama.
Amri hiyo ilitolewa juzi na Hakimu Mkazi, Samuel Maweda baada ya mkuu huyo wa wilaya kukaidi amri ya kuachia ng’ombe 541 wa wafugaji wa kitongoji cha Rwenkuba wilayani humo waliokamatwa isivyo halali.
Septemba 22, Mahakama hiyo ilitoa amri ya ng’ombe hao kuachiwa baada ya wananchi kufungua shauri la madai namba 21/2017 kupinga ng’ombe wao kukamatwa katika eneo lenye mgogoro unaoendelea katika mahakama kuu kitengo cha ardhi kwa shauri namba 14/2017.
Akizungumza na Mwananchi kwa njia ya simu juzi usiku Wakili wa wananchi143 waliofungua kesi mahakamani, Danstan Mutagahywa alisema baada ya Mkuu wa Wilaya na mdaiwa mwenzake, Ladislaus Martin ambaye ni Meneja wa Ranchi ya Misenyi kukaidi kutekeleza amri hiyo, waliwasilisha ombi la watu hao kukamatwa kwa kudharau amri ya Mahakama.
“Siyo tu wamekaidi kutekeleza amri halali ya Mahakama, DC na mwenzake pia wamegoma kupokea hati za wito na kufikia hatua ya kumkamata na kumweka mahabusu dalali wa Mahakama aliyepewa amri ya kutekeleza zoezi la kurejesha ng’ombe wanaoshikiliwa isivyo halali,” alisema Mutagahywa.
Alisema amri hiyo wataifikisha ofisini kwa Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Mkoa (RCO) wa Kagera.
Alimtaja dalali wa Mahakama aliyekamatwa na kuswekwa mahabusu kwa amri ya DC Oktoba 31, kuwa ni Ignatus Bashemela aliyeachiwa huru baada ya yeye kuwasilisha suala hilo ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera akionyesha nyaraka halali za Mahakama kuhusu jambo hilo.
Kauli ya DC
Akizungumza kwa njia ya simu mkuu huyo wa wilaya amesema aliagiza kukamatwa kwa dalali wa wafugaji wa ng’ombe kutoka Uganda ambaye alifika bila kutoa taarifa yoyote kwa mamlaka za Serikali.
Alisema mtu huyo alikwenda moja kwa moja katika eneo wanapotunzwa ng’ombe zaidi ya 80 walioingizwa nchini kutoka Uganda bila kufuata utaratibu.
“Hilo suala la dalali wa Mahakama nalisikia kwako niliyeagiza akamatwe ni dalali wa wafugaji wa ng’ombe kutoka Uganda ambao tumewakamata alifika bila kufuata taratibu nikaagiza akamatwe,”amesisitiza Kanali Mwila.
Aliongeza kuwa alikamata ng’ombe zaidi ya 400 na wamiliki wake kutoka Uganda walilipa faini na kuwarudisha kwao na kubaki ng’ombe 88 aliosema alipata taarifa kuwa wanataka kuchukuliwa kwa nguvu na watu ambao hata hawakupita kwenye ofisi yake.
Pia alisema hana taarifa yoyote ya kuwepo kwa hati ya Mahakama dhidi yake na kuwa anaendelea kuwasaka raia wawili wanaodaiwa kushirikiana na wafugaji wa Uganda kuingiza mifugo hiyo bila utaratibu.

Nasa waibua mjadala wakitaka eneo la Pwani kujitenga



Mombasa, Kenya. Baadhi ya wanasiasa na viongozi wa Muungano wa National Super Alliance (Nasa) eneo la Pwani wameibua mjadala wakitaka eneo hilo kuondolewa katika ramani ya Kenya.
Wanasiasa takriban 18 wameituhumu Serikali katika awamu zilizopita na ya sasa ya Jubilee inayoongozwa na Rais Uhuru Kenyatta na Naibu wake, William Ruto wakidai zimekuwa zikipuuza matakwa yao.
Kenya iliongozwa na Jomo Kenyatta ambaye ni baba yake Rais Uhuru, baadaye Daniel  Arap Moi aliyetawala kwa kipindi cha miaka 24.
Utawala wa awamu ya tatu ulikuwa chini ya Rais Mwai Kibaki kuanzia mwaka 2003 hadi 2012 alipoingia Rais Uhuru.
Wanasiasa hao wa Pwani wakiongozwa na Gavana wa Mombasa, Ali Hassan Joho na mwenzake wa Kilifi, Amason Kingi wamesema wameanza mazungumzo kuhakikisha eneo hilo linaondolewa kutoka katika ramani ya Kenya.
Pia, wanapinga uchaguzi wa marudio wa urais uliofanyika Oktoba 26,2017 uliompa ushindi Rais Uhuru.
"Safari ya kuiondoa Pwani kutoka Kenya imeanza, tutatumia njia zote kisheria za hapa nchini na kimataifa kuhakikisha tumefikia lengo hilo," amesema Gavana Joho alipozungumza na waandishi wa habari mjini Mombasa.
Mbali na mawakili, amesema wanashauriana na wakazi wa Pwani wakiwamo; viongozi wa kidini, wa vijiji na vijana ili suala hilo lisionekane ni la wanasiasa na viongozi pekee.
"Tunaelewa safari hiyo haitakuwa rahisi, lakini sharti tufikie shabaha yetu," amesema.
Alichosema Kingi
Kauli ya Joho ilienda sambamba na ya Gavana Kingi wa Kilifi ambaye amesisitiza kuwa hawafi moyo kwa suala hilo.
"Umefika wakati wa kuinusuru Pwani. Tumepuuzwa kwa muda mrefu sana," amesema.
Awali, suala la wanasiasa wa Pwani kutaka kuondoa maeneo hayo kutoka kwenye  ramani ya Kenya lilipuuzwa na kiongozi wa Nasa, Raila Odinga.
Waziri mkuu huyo wa zamani alisema haungi mkono pendekezo hilo na kwamba halitawezekana.
Kwa sasa kinachosubiriwa ni iwapo Raila atazungumza lolote kuhusu suala hilo.

Kitabu chenye utata kuhusu rais Zuma chapigwa marufuku Afrika Kusini

Kitabu chenye utata kuhusu rais Zuma chapigwa marufuku Afrika Kusini
Image captionKitabu chenye utata kuhusu rais Zuma chapigwa marufuku Afrika Kusini
Majasusi wa Afrikia Kusini wanataka kufutiliwa mbali kwa kitabu kipya chenye utata kuhusu madaia yua rais Zuma kujilimbikizia fedha kimakosa ,wakisema kuwa kitabu hicho kimajaa makjosa na kinakiuka sheria ya ujasusi.
Shirika hilo la ujasusi limetishia kwenda mahakamani iwapo wachapishaji wa kitabu hicho NP watakataa kukifutilia mbali kitabu hicho kwa Jina ''The Presidency Keepers''-Wale wanaomueka Zuma mamlakani na kutokwenda jela, kilichotungwa na mwandishi aliyeshinda tuzo la uandishi wa uchunguzi Jacques Pauw.
Kitabu hicho kinadai kwamba bwana Zuma kwa muda wa miezi minne alipokea mshahara kutoka kwa mfanyibiashara mmoja mbali na mshahara anaolipwa na serikali na kwamba hakuutangaza mshahara huo kwa watoza ushuru wa taifa hilo.
Baada ya nakala za kitabu hicho kuchapishwa siku ya Jumapili katika gazeti moja, msemaji wa bwana Zuma alitoa taarifa ,akikana makosa yoyote dhidi ya rais Zuma akidai kwamba alikuwa mwathiriwa wa kampeni mbaya ya kumchafulia jina.
Rais Jacob ZumaHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionRais Jacob Zuma
"Maswala ya ulipaji wa kodi ya rais hayana makosa '',ilisema taarifa hiyo.
Nakala za kitabu hicho zinauzwa kwa kasi huku raia wakijaribu kukinunua kabla ya kuisha katika soko.

WIZARA YA UJENZI YARIDHISHWA NA KASI YA JNIA-TBIII

WIZARA ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, imeridhishwa na ujenzi wa mradi wa jengo la tatu la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA-TBIII), ambapo unatarajiwa kukamilika Septemba 2018. Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (sekta ya Ujenzi), Mhe. Elias Kwandikwa wakati alipotembea maendeleo ya mradi huo unaojengwa na Mampuni ya ujenzi ya Bam International ya Uholanzi.

Mhe. Kwandikwa alisema mradi huo umefikia asilimia 66, ambapo wizara imekuwa ikihakikisha mkandarasi analipwa kwa wakati ili uweze kukamilika kama ilivyotarajiwa, na kukamilika kwake kutatoa picha ya kuelekea kwenye Tanzania mpya.

“Hivi karibuni nilitembelea kiwanja cha KIA (Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Kilimanjaro), nikaridhishwa na maendeleo ya ukarabati unaoendelea pale, na nikaona ni vyema pia kutembelea hili jengo na nimeliona na nimeridhishwa na kasi ya ujenzi unaoendelea, ninaamini kama wakandarasi walivyosema basi hadi kufikia Septemba 2018 litakuwa limekamilika kabisa,” alisema Mhe. Kwandikwa.

Hata hivyo, Mhe Kwandikwa alisema serikali inajenga awamu ya pili ya mradi huo kwa kutumia fedha za ndani, lakini pia kwa kushirikiana na wadau wengine, ambapo ni ishara nzuri kuwa siku zijazo kutakuwa na miradi mingi zaidi.

“Tunajenga mradi huu kwa fedha zetu za ndani, lakini pia kwa kushirikiana na wadau wengine, hii ni ishara nzuri kwamba sasa tunakokwenda tunao uwezo wa kuwa na miradi mingi zaidi kama hii tuliojenga kwa kutumia fedha zetu wenyewe,” alisema Mhe. Kwandikwa.

Hata hivyo, msimamizi wa Mradi huo, Mhandisi Barton Komba alisema, mkandarasi wa ujenzi huo ameshalipwa fedha zake zote, hivyo kwa sasa hadai serikali na anafanya kazi yake vizuri, ili kukamilisha na kukabidhi jengo pindi litakapokamilika. “Mpaka mwezi wa tisa mwakani utakuwa umekamilika kabisa, lakini pia jengo hili limejengwa kwa kuzingatia viwango vya kimataifa na litatoa huduma kwa watu wote hata ndugu zetu wenye mahitaji maalumu, ,” alisema Mhandisi Komba.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mhe. Elias Kwandikwa (wa tatu kushoto) akielekea kwenye ukaguzi wa ujenzi wa jengo la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere. Wa pili kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Mtengela Hanga.
Msimamizi wa mradi wa ujenzi wa Jengo la Tatu la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA-TBIII), Mhandisi Barton Komba (kulia) akimwonesha kitu Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mhe. Elias Kwandikwa (wa pili kulia), wakati alipotembelea na kukagua ujenzi wa jengo hilo.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mhe. Elias Kwandikwa (wa pili kulia), akizungumza na Mhandisi Barton Komba (wa tatu kushoto) wakati wakitoka kwenye ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi wa mradi wa jengo la tatu la abiria la Kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere.

TPDC YAGUSWA NA MAENDELEO YA JAMII

Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) limeanza kutekeleza shughuli za uwajibikaji kwa jamii katika mwaka wa fedha 2017/2018 ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za Serikali katika uboreshwaji wa Sekta mbalimbali kama Elimu, Afya, Maji na Utawala Bora.

Hayo yamezungumzwa na Meneja wa Mawasiliano wa TPDC, Marie Msellemu katika tukio la kukabidhi hundi za fedha kwa ajili ya kusaidia uimarishwaji wa Chama cha Maafisa Uhusiano Tanzania pamoja na kukabidhi fedha za kuwezesha ununuzi wa mafuta na dawa kwa Chama cha Wanawake Albino cha Ndugumbi lilofanyika tarehe 03 Novemba, 2017 Makao Makuu ya TPDC.

“Leo tunayo furaha ya kuanza rasmi shughuli zetu za uwajibikaji kwa jamii kwa kuhakikisha afya bora kwa ndugu zetu kutoka kikundi cha Wanawake Albino cha Ndugumbi kwa kuwapatia fedha za kuweza kufanya manunuzi ya dawa na mafuta ya kupaka ili kuimarisha afya ya ngozi zao na kujikinga dhidi ya maradhi ya Kansa na hivyo kurudisha tabasmu kwao na kuona kuwa Shirika lao la Mafuta la taifa linawajali na liko pamoja nao katika mapambano dhidi ya maradhi ya Kansa.”  Msellemu alieza katika tukio hilo.
Meneja Mawasiliano wa TPDC akikabidhi hundi kwa Uongozi wa Chama cha Maafisa Uhusiano Tanzania.

Baada ya kupokea msaada wa fedha kutoka TPDC, Mwamvua Kambi ambaye ni Katibu wa Ndugumbi ametoa shukrani kwa TPDC kwa kuwajali na kuwasikiliza kilio chao maana kilio chao kikubwa ni Kansa ya Ngozi ambayo kwa dawa na mafuta watakazonunua zitasaidia kupunguza mionzi ya Jua ambayo ni hatarishi kwa afya za ngozi zao na kwa msaada walioupata ni mkubwa na unawatosha pamoja na wenzao katika kikundi.”

Aidha Meneja Mawasiliano alieongezea kuwa kwa kutambua umuhimu wa kuboresha masuala ya Utawala Bora nchini, Shirika linaamini kuwa kwa kukisaida Chama cha Maafisa Habari wa Tanzania kitakua kimeimarisha eneo la Utawala Bora ambapo kupitia Kongamano la Maafisa habari ambalo litalenga kwenye kuimarisha mchango wao katika kuijenga Tanzania ya Viwanda wataendelea kufanya kazi kwa bidii kwa kuelimisha Umma wa Watanzania juu ya uwajibikaji wa kizalendo katika kuiletea Nchi Yetu Maendeleo ya kweli katika Sekta ya Viwanda.

David Mwaipaja ambaye ni Mratibu wa chama ametoa shukrani kwa mchango wa TPDC, “Tunashukuru saana kwa utayari mliounyesha wa kuhakikisha Chama cha Maafisa Uhusiano kinafikia Malengo yake na kiukweli matokeo makubwa kwa mlichokifanya leo hayataonekana leo hii lakini nafasi kubwa ya kushukuru itapatikana siku ya Mkutano Utakaolenga kuangalia Nafasi ya Maafisa Uhusiano katika Kuelekea Tanzania ya Viwanda ambapo mtapata nafasi ya kueleza umuhimu wenu au mchango wenu katika kuijenga Tanzania ya Viwanda”.
Meneja Mawasiliano wa TPDC akikabidhi hundi kwa Chama Ndugumbi Albino kwa ajili ya kuwezesha manunuzi wa mafuta ya ngozi.

 Msellemu anansisitiza kuwa “kwa Mwaka huu wa fedha TPDC inatarajia kutekeleza ujenzi wa kituo cha Afya Tunduru, ujenzi wa vyoo kwa wananfunzi wenye ulemavu Shule ya Msingi Shangani na vyoo kwa Shule ya Msingi Kilwa Kivinje, ujenzi wa Zahanati katika kijiji cha Mingoji pamoja na kufadhili zoezi la upimaji wa afya kupitia Taasisi ya Moyo katika kuendesha zoezi la upimaji afya litakalofanyika Wilayani Luangwa Mkoani Lindi.”

Msellemu amefafanua kuwa hii si mara ya kwanza kwa TPDC kutekeleza jukumu lake la msingi katika uwajibikaji kwa jamii inayoizunguka ila ni mwanzo tu wa shughuli hizo kwa mwaka huu wa fedha.

“TPDC tumekuwa na utaratibu wa kutekeleza majukumu yetu kwa jamii toka huko nyuma ambapo tuliweza kuchangia madawati na viti kwa shule za Msingi na Sekondari kwa Mikoa ya Lindi, Mtwara na Dar es Salaam, ujenzi wa madarasa, mabweni, vyoo, ofisi za serikali za mitaa na n.k”.

TPDC kama Shirika la Mafuta la Taifa linao wajibu wa kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa Sheria za Nchi na kama Sheria ya Mafuta ya Mwaka 2015 inavyoelekeza namna ya utekelezaji wa wajibu wa Sekta ya Mafuta na Gesi kwa jamii, Shirika litaendelea kutekeleza wajibu huo kwa lengo la kuhakikisha manufaa ya Gesi Asilia nchini yanapatikana kwa wananchi si kwa kutokana na mapato ya gesi asilia pekee kwa Serikali lakini pia kwa kuboresha Sekta za Elimu, Afya, Maji, Utawala Bora, Miundombinu na kadhalika.
Viongozi wa Chama cha Maafisa Uhusiano Tanzania na Chama cha Ndugumbi pamoja na Meneja na Maafisa wa TPDC mara baada ya makabidhiano ya Hundi katika Ofisi za TPDC Dar es Salaam.

ZIARA YA KAMISHNA WA EU NEVEN MIMICA YALETA NEEMA KWA TANZANIA

 Kamishna wa Jumuiya ya Umoja wa Ulaya (EU) anayeshughulikia mahusiano ya Kimataifa na Maendeleo, Mhe. Neven  Mimica, (kushoto), akiwa na balozi wa EU nchini, Mhe.Roeland van der Geer, wakati amkizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa ziara yake ya siku mbili nchini Novemba 3, 2017.(PICHA NA HABARI/K-VIS BLOG;Khalfan Said)
 NA K-VIS BLOG/Khalfan Said

ULE msemo wa kiswahili wa "mgeni njoo mwenyeji apone", unaweza kutumika kufatsiri neema ambayo taifa limepata kufuatia ziara ya siku mbili nchini ya Kamishna wa Jumuiya ya Umoja wa Ulaya (EU) anayeshughulikia mahusiano ya Kimataifa na Maendeleo, Mhe. Neven  Mimica, pichani juu.
Mhe. Mimica alianza ziara yake Novemba 2, kwa kutiliana saini makubaliano na Serikali kupitia Wizara ya Fedha na Mjpango, ambapo EU imeahidi kutoa kiasi cha Euro milioni 50 ambazo zitatumika kupeleka umeme vijijini.
Serikali inapambana kuhakikisha vijiji elfu 12 (12,000) ambavyo bado havina umeme nchini vinapata huduma ya umeme ifikapo 2020.Kwa mujibub wa Afisa Habari wa EU hapa nchini Bi.Susanne Mbise, msaada huo wa Euro milioni 50 utasaidia kupeleka umeme kwenye vijiji 3,000.
Ziara ya Kamishna Mimica, ililenga kutembelea shughuli mbalimbali ambazo EU imekuwa ikifadhili,
Miongoni mwa maeneo ambayo Kamishna Mimica alitembelea ni pamoja na bandari ya Dar es Salaam, ambapo akiongea na uongozi wa bandari hiyo, Kamishna Mimica a,lieleza utayari wa EU katika kusaidia kub oresha bandari hiyo kwani ina msada mkubwa sio tu kwa Tanzania bali pia kwa nchi majirani.
Kamishna Mimica pia ametembelea kituo kinachosaidia vijana cha Nafasi Art Space kilichoko  Mikocheni jijini Dar es Salaam ambapo aliweza kusikiliza maoni yao na kujadiliana nao masuala mbalimbali yahusuyo changamoto za ajira na pia ukatili dhidi ya mtoto wa kike. "Kamishna Mimica amesema EU itatoa Euro  milioni 500 ili kusaidia kupambana na ukatili dhidi ya wanawake na watoto". amesema Bi. Mbise.
Kamishna huyo wa EU, alikutana na kujadiliana na makampuni makubwa ya kibinafsi ili kuona jinsi sekta binafsi inavyofanya shughuli zake hapa nchini na ziara hiyo ilimuwezesha pia kukutana na viongozi wa asasi za kiraia hapa nchini.
 Mhe. Mimica, akipokewa na Kaimu Mkurugezni Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania, (TPA), Bw. Lazaro twange, alipotembelea bandari ya Dar es Salaam, Novemba 3, 2017. EU ni mdau mkubwa katika kjuisaidia TPA kuimarisha miundombinu yake.
 Mhe. Mimica akizun gumza na uongozi wa juu wa TPA.
 Mhe. Mimica akipeana mikono na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Mhe. Dotto James, baada ya kusaini makubaliano ambapo EU itatoa Euro milioni 50 kusaidia usambazaji umeme vijijini. Takriban vijiji 3,000 kote nchini vitafaidika na msaada huo. Serikali inapambana kuwafikishia umeme wana vijiji wa vijiji 12,000 a,mbavyo bado havijapata umeme na mpango huu umepangwa kukamilika 2020.
 Mhe. Mimica akiwa na mazungumzo na mabalozi wanaotoka nchi za EU.
 Mhe. Mimica akisalimiana na Afisa Habari wa EU hapa nchini, Bi. Susanne Mbise. wakati a,lipofika Wizara ya Fedha na Mipango kusaini msaada huo wa fedha Euro milioni 50.
 Kamishna wa Jumuiya ya Umoja wa Ulaya (EU) anayeshughulikia mahusiano ya Kimataifa na Maendeleo, Mhe. Neven  Mimica, (kushoto), akiwa na balozi wa EU nchini, Mhe.Roeland van der Geer, wakiwadsili Nafasi Art Space, Mikocheni jijini Dar es Salaam, ambapo alifanya maxungumzo na vijana mbalimbali kuhusu changamoto za ajira, ukatili dhidi ya wanawake na namna gani wanavyokabiliana nazo.
 Bi. Nasra akielezea kuhusu kazi ya sanaa ya mikono inayofanywa na vijana wa Nafasi Art Space.
 Msanii Nancy, wa Nafasi Art Space, (kulia), akishirikiana na Nasra pia wa Nafasi Art Space, wakimpatia maelezo Mhe. Mimica kuhusu sanaa za mikono wanazofanya.
 Mhe. Mimica na ujumbe wake wakiwa katika mazungumzo na vijana wanaojishughulisha na masuala ya sanaa na kuzuia ukatili dhidi ya wasichana na akina mama.
 Oscar Kimaro, (kulia), kutoka Restless Development, akizungumza kwenye mkutano na Mhe. Mimica uliofanyika Nafasi Art Space, Mikocheni jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Jasmina Milovanovic kutoka Save the Children na Rebeca Corey wa Nafasi Art Space.
 Mhe. Mimica, akizungumza jambo wakati akipatiwa maelezo na Rebeca Corey wa Nafasi Art Space.
 Mgunga Mwanyenyelwa ,kutoka kituo cha Baba Watoto, akizunhgumza kwenye mkutano huo na Kamishna Mimica.
 Kamishna alipata fursa ya kukutana na kuzunguzma na viongozi wa asasi za kiraia.
 Wasanii wa Nafasi Art Space wakifanya vitu vyao.
 Msafara wa Kamishna Mimica ukipita barabara ya Bagamoyo Novembe 3, 2017 kuelekea Mikocheni kituo cha Nafasi Art Space.
 Msafara ukiwasili  Mikocheni jijini Dar es Salaam.
 Msafara wa Mhe. Mimica ukiwa bandari ya Dar es Salaam.
 Msafara wa Mhe. Mimica ukiwa bandari ya Dar es Salaam.