Friday, June 9

BARAZA LA TAIFA LA USALAMA BARABARANI LATOA TATHIMINI


 Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani ambaye ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Massauni, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani), kuhusu utekelezaji wa mpango mkakati wa kupunguza ajali za barabarani nchini katika kipindi cha miezi sita, mjini Dodoma leo, kulia ni Makamu Mwenyekiti wa baraza hilo ambaye ni Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Edwin Ngonyani.
 Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani ambaye ni Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Edwin Ngonyani (kulia), akifafanua jambo katika mkutano na Waandishi wa Habari kuhusu hatua za utekelezaji wa mpango mkakati wa kupunguza ajali za barabarani nchini katika kipindi cha miezi sita, mjini Dodoma leo, kushoto ni Mwenyekiti wa Baraza hilo Mhandisi  Hamad Massauni.
 Mjumbe wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Julius Chambo (Kushoto), akisikiliza kwa makini taarifa ya utekelezaji wa mpango mkakati wa kupunguza ajali za barabarani nchini katika kipindi cha miezi sita, iliyotolewa na Mwenyekiti wa Baraza hilo Mhandisi Hamad Massauni (hayupo pichani), mjini Dodoma leo.
Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani ambaye ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Massauni, akitoa taarifa ya utekelezaji wa mpango mkakati wa kupunguza ajali za barabarani nchini katika kipindi cha miezi sita kwa wajumbe na waandishi wa habari, mjini Dodoma leo. 

Imetolea na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

JK aeleza changamoto anazokumbana nazo kwenye kilimo cha mananasi



Pwani. Rais mstaafu, Jakaya Kiwete amezungumzia  shughuli za kilimo anazozifanya huku akianika changamoto mbalimbali zinazomkabili.

Akizungumza leo Ijumaa muda mfupi mara baada ya Mwenge wa Uhuru kufika kwenye shamba lake la mananasi lenye ukubwa wa eka zaidi ya 200 mkoani hapa, amesema ingawa kilimo alianza tangu mwaka 1989, lakini suala la palizi na ukosefu wa maji ni moja ya changamoto anazokabiliana nazo.
"Nilianza kilimo miaka mingi sana na mpaka nastaafu nilikuwa naendelea na kilimo, lakini changamoto kubwa katika kilimo ni suala la palizi hususan haya mananasi unaweza palilia zaidi ya mara tatu," amesema.
Amesema kuwa ingawa mananasi yanazaa vizuri kama yatapata huduma zote kikamilifu, lakini mkulima anaweza kupambana na ukosefu wa masoko pindi unapofikia msimu wa mavuno.
"Hata kama viwanda vitajengwa kwa wingi lakini ili mkulima apate faida ya juu ya kilimo hasa cha mananasi ni lazima kuwe na bei nzuri, lakini kama wanunuzi watakuwa wananunua bei isiyo na masilahi hakutakuwa na maendeleo kwa wakulima,"amesema.
Amesema kuwa mikakati aliyonayo kwa kushirikiana na taasisi na wakulima mbalimbali ni kutafuta mbegu za  mananasi kutoka nje ya nchi na mkakati wa kuanzisha kilimo cha mananasi kwa njia ya umwagiliaji hali aliyosema itawainua wakulima wengi na kujikwamua katika janga la umaskini.
Mkimbiza Mwenge wa Uhuru kitaifa, Amour Hamad Amour amempongeza Kikwete kwa kuonyesha mfano bora hususan kuendeleza kilimo cha mananasi huku amiwahimiza Watanzania kuiga mfano huo.

Mwanafunzi wa darasa la sita abakwa hadi kufa



Sumbawanga. Mwanafunzi wa darasa la sita  katika Shule ya Msingi Kapanga, Kata ya Katuma Wilaya ya Tanganyika, Mkoa wa Katavi, amekutwa amekufa kwenye shimo baada ya kubakwa na watu wasiojulikana.
Kaimu  Kamanda wa  Polisi wa  Mkoa wa  Katavi,   Benedict  Mapujila  amesema tukio  hilo  lilitokea juzi saa 11 jioni katika kata hiyo.
Amesema  siku hiyo mwanafunzi huyo aliondoka  nyumbani  kwenda  shule,  lakini ilipofika jioni hakurejea.
Kaimu kamanda amesema hali hiyo ilisababisha wazazi wake wapate shaka kwa kuwa marehemu hakuwa na tabia ya kutorudi nyumbani.
Amesema siku iliyofuata wazazi wake walikwenda kufuatilia  shuleni lakini hawakumkuta na kwenda kutoa taarifa kwenye uongozi wa kijiji hicho.
“Viongozi wa kijiji na wananchi walianza msako wa kumtafuta binti huyo kutwa nzima  na ilipofikia saa 11 jioni  walikuta mwili wake umetupwa  kwenye  shimo  la kolongo,” amesema.
Kaimu Kamanda Mapujila amesema  sehemu za siri za binti huyo zilikutwa zimeharibika vibaya.
Amesema uchunguzi wa kitabibu umebaini mwanafunzi huyo alitokwa damu  nyingi hali iliyosababisha kifo.
Kaimu kamanda hakuna aliyekamatwa kutokana na tukio hilo ila polisi inaendelea na msako kuwabaini waliohusika.