Friday, June 9

Mwanafunzi wa darasa la sita abakwa hadi kufa



Sumbawanga. Mwanafunzi wa darasa la sita  katika Shule ya Msingi Kapanga, Kata ya Katuma Wilaya ya Tanganyika, Mkoa wa Katavi, amekutwa amekufa kwenye shimo baada ya kubakwa na watu wasiojulikana.
Kaimu  Kamanda wa  Polisi wa  Mkoa wa  Katavi,   Benedict  Mapujila  amesema tukio  hilo  lilitokea juzi saa 11 jioni katika kata hiyo.
Amesema  siku hiyo mwanafunzi huyo aliondoka  nyumbani  kwenda  shule,  lakini ilipofika jioni hakurejea.
Kaimu kamanda amesema hali hiyo ilisababisha wazazi wake wapate shaka kwa kuwa marehemu hakuwa na tabia ya kutorudi nyumbani.
Amesema siku iliyofuata wazazi wake walikwenda kufuatilia  shuleni lakini hawakumkuta na kwenda kutoa taarifa kwenye uongozi wa kijiji hicho.
“Viongozi wa kijiji na wananchi walianza msako wa kumtafuta binti huyo kutwa nzima  na ilipofikia saa 11 jioni  walikuta mwili wake umetupwa  kwenye  shimo  la kolongo,” amesema.
Kaimu Kamanda Mapujila amesema  sehemu za siri za binti huyo zilikutwa zimeharibika vibaya.
Amesema uchunguzi wa kitabibu umebaini mwanafunzi huyo alitokwa damu  nyingi hali iliyosababisha kifo.
Kaimu kamanda hakuna aliyekamatwa kutokana na tukio hilo ila polisi inaendelea na msako kuwabaini waliohusika.

No comments:

Post a Comment