Tuesday, August 1

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AKAGUA MIRADI WILAYA YA MBEYA MJINI


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifungua Methadone Clinic ambao ni maalum kwa kuwahudumia na kuwapa ushauri nasaha waathirika wa madawa ya kulevya kwenye . hospitali ya Rufaa ya Mbeya Julai 31, 2017. Kushoto ni Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
PMO_7118
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa  Salim Jessa  (wanne kushoto) ambaye ni  Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda cha Malumalu kilichopo Iyunga jijini Mbeya  wakati alipoembelea kiwanda hichi Julai 31, 2017.  Watatu kushoto ni Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson Mwansasu. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
PMO_7147
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa  Salim Jessa  (kulia) ambaye ni  Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda cha Malumalu kilichopo Iyunga jijini Mbeya  wakati alipoembelea kiwanda hicho Julai 31, 2017. Kushoto kwake ni Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson Mwansasu. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
PMO_7255
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akipokea maua kutoka kwa mtoto , Felista (4) wa Shule ya Wenye Ulemavu ya Child Support Tanzania ya jijini Mbeya baada ya kuwasili kwenye kiwanda cha vinywaji baridi cha SBS – PEPSI kilichopo eneo la Iyunga jijini Mbeya Julai 31, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
PMO_7266
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na watoto wa Shule Wenye Ulemavu ya Child Support Tanzania ya jijini Mbeya baada ya kuwasili kwenye kiwanda cha vinywaji baridi cha SBS- Pepsi kilichopo Iyunga jijini Mbeya Julai 31, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
PMO_7364
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitembelea kiwanda cha vinywaji baridi  cha SBS- Pepsi kilichopo eneo la Iyunga jijini Mbeya, Julai 31, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
PMO_7413
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia wakazi wa Mbeya baada ya kuwasili kwenye Viwanja vya  Ruanda Nzove jijini humo kuhutubia mkutano wa hadhara, Julai 31, 2017. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
PMO_7422
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta jambo na Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
PMO_7441
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia mkutano wa hadhara kwenye Viwanja vya  Ruanda Nzove jijini Mbeya Julai 31, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

MWENYEKITI CHARLES MAKOGA : SHERIA MPYA KUTUMIKA KUKUZA MAPATO YA MJI WA MAFINGA


Mwenyekiti wa halmashauri ya Mafinga Mjini Charles Makoga akizungumza wakati wa baraza la madiwani wa halmashauri hiyo
Baadhi ya madiwani wa halmashauri ya Mji wa Mafinga wakiwa katika baraza pamoja na wataalamu mbalimbali wa halmashauri hiyo.


Na fredy Mgunda, Mafinga

Halmashauri ya Mji wa Mafinga mkoni Iringa inatarajia kukuza mapato katika mwaka Mpya wa 2017/2018 kutokana na kuanza kuzitumia sheria mpya za ukusanyaji mapato pamoja na kuvijua vyanzo vingine vya mapato ambavyo ndio vitasababisha kukuza uchumi wa halmashauri hiyo.

Akizungumza wakati wa baraza la madiwani Mwenyekiti wa halmashauri ya Mafinga Mjini Charles Makoga alisema kuwa sheria mpya walizoletewa toka mwezi wa tano zinawapa nafasi ya kuanza kuzitumia wakati wa kukusanya mapato katika maeneo ambayo walikuwa hawakusanyi.

"Tulikuwa hatukusanyi mapato katika maeneo ya stand,sehemu za maegesho ya magari,sokoni na maeneo mengine kwa kuwa sheria zilikuwa bado si rafiki kwetu kwenda kukusanya mapato ila kwa mwaka unaoanza tutakusanya mapato na kukuza mapato kutoka asilimia 56 hadi kuvuka lengo la serikali la asilimia 80" alisema Makoga

Makoga aliwataka wananchi na viongozi kushiriana kukusanya mapato kulingana vyanzo ambavyo madiwani wameviolozesha kwa manufaa ya halmashauri ya Mafinga Mjini ambavyo vipo kisheria kutoka serikali kuu.

Jamani naombeni mchango wetu kufanikisha swala hili la kukusanya mapato ili tufikie lengo la serikali kwa kuwa mwaka huu hatufikia lengo hilo ni aibu kubwa kwa serikali hii ya awamu ya tank ambayo inaenda kwa kasi kubwa kwa kukuza uchumi wa nchi.

Nao baadhi ya madiwani wa halmashauri ya mji wa mafinga Zacharia Vang'ota wa kata changarawe,Chesco lyuvale wa Kata ya kinyanambo walimtaka Mwenyekiti wa halmashauri hiyo kuzisimamia ipasavyo sheria ambazo zimetungwa na halmashauri pamoja na serikali ya jamhuli ya muungano wa Tanzania chini ya Rais Dr John pombe Magufuli ili kukuza mapato katika halmashauri hiyo.

"Ukiangalia hapa Mafinga tunavyanzo vingi vya mapato lakini watalaamu wetu hawavifanyii kazi ndio maana sisi madiwani tumeamua kuanzia sasa vyanzo vyote tulivyovibainisha leo kwenye baraza vifanyiwe kazi haraka sana ili kukuza mapato ya halmashauri yetu"walisema madiwani

Kwa upande wao baadhi ya wananchi wa Mafinga Mjini walisema kuwa Mji huo una changamoto nyingi hivyo serikali ya mji inatakiwa kuanza kuzitumia hizo sheria Mpya haraka ili hata wananchi wayatambue maeneo yanayopaswa kulipa kodi na kuewezesha halmashauri kukuza mapato na kutatua changamoto za Mji wa Mafinga.

"Angalieni nyie waandishi Mafinga maji ni tatizo kubwa,Barbara bado hazijatengenezwa hasa huku mitaani kwetu,Mji bado mchafu kila mtu anatupa takataka anavyotaka kwa kuwa hakuna mtu wa kumkamata ila ukiangalia sheria Mpya zipo lakini hazifanyiwi kazi na Mafinga maeneo ya maegesho ya magari hayalipiwi wakati miji mingine ni moja vya mapato hivyo viongozi wanapaswa kuanza kuzitumia sheria Mpya" walisema wananchi

NBC YASHEREHEA MIAKA 50 PAMOJA NA KUZINDUA KLABU YA BIASHARA JIJINI MWANZA.



 Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella (katikati), akisalimiana na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi baada ya kuzindua Klabu ya Biashara mjini Mwanza hivi karibuni. Kushoto ni Mjumbe wa Bodi ya NBC, Dk. Kassim Hussein. NBC imezindua Klabu ya Biashara iliyopewa jina la ‘NBC B-Club’ katika miji ya Kahama na Mwanza kwa kuandaa semina kwa wafanyabishara wajasiriamali.   NBC B-Club itasaida  huduma zisizo za kifedha kupitia mafunzo maalumu kwa kushirikiana  na wadau mbalimbali kuhusu mbinu za uendeshaji wa biashara na kuwajengea uwezo katika kuziendesha kwa ufanisi hivyo kukuza biashara hizo. 



  Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Theobald Sabi akihutubia wakati sherehe za uzinduzi rasmi wa Klabu ya Biashara jijini Mwanza hivi karibuni. Wengine kutoka kushoto ni Mjumbe wa Bodi ya NBC, Dk. Kassim Hussein, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella, aliyekuwa mgeni rasmi na Mkurugenzi wa Kitengo cha Wateja Binafsi, Filbert Mponzi.



 Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella akihutubia wakati wa semina ya wafanyabiashara katika uzinduzi rasmi wa Klabu ya Biashara ya NBC mjini Mwanza. Wengine kutoka kushoto ni Mjumbe wa Bodi ya NBC, Dk. Kassim Hussein, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Theobald Sabi na Mkurugenzi wa Kitengo cha Wateja Binafsi, Filbert Mponzi. 



 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Theobald Sabi akizungumza katika sherehe za maadhimisho ya mika 50 ya benki hiyo mjini Mwanza.



 Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella (katikati), akizungumza na ujumbe wa viongozi wa NBC waliofika ofisi kwake kumtembelea wakiongozwa na Dk. Kassim Hussein (kulia kwake) na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Theoblad Sabi (kushoto kwake). NBC ilizindua klabu za biashara katika miji ya Kahama na Mwanza pamoja na kusherehekea miaka 50 tokea ilipoanzishwa.  

NMB YAZINDUWA SIKU YA WALIMU MKOANI DODOMA



Afisa Tawala wa Mkoa wa Dodoma, Bi. Rehema Madenge akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dodoma (wa kwanza kulia) akifurahi pamoja na maofisa wa Benki ya NMB mara baada ya uzinduzi rasmi wa hafla ya siku ya walimu katika Mkoa wa Dodoma. Hafla ya uzinduzi wa siku ya Mwalimu ilifanyika mwishoni mwa wiki katika viwanja vya hazini jijini Dodoma.

BENKI ya NMB imezindua rasmi siku ya walimu katika Mkoa wa Dodoma. Uzinduzi huo wa siku ya walimu Mkoa wa Dodoma ulizinduliwa rasmi na Afisa Tawala wa Mkoa wa Dodoma, Bi. Rehema Madenge akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Bw. Jordan Rugimbana. Hafla hii adhimu ilifanyika katika ukumbi wa Hazina na kuhudhuliwa na zaidi ya walimu 200 wa mkoa huo mwishoni mwa wiki. Uzinduzi wa hafla hii ni miongoni mwa mikakati ya NMB ya kuwafikia walimu nchini kote. Kusudi kubwa la hafla hiyo ya NMB na Walimu ni kuwaongezea uelewa walimu juu ya huduma za benki. Hii ni kutokana na umuhimu wa kundi hili kubwa katika jamii inayotuzunguka. 

NMB wanaimani kwamba mwalimu akielimika jamii nzima itakua imepata elimu ya huduma za kifedha. Lakini pia kwa kuzingatia ukubwa wa kundi hili NMB imekua ikitumia fursa hii kupokea mrejesho ya jinsi huduma za kibenki zinavyopokelewa na wateja wake. Akizungumza wakati wa hafla hiyo mjini Dodoma, Meneja mwandamizi wa wateja binafsi wa NMB, Omari Mtiga alisema NMB inazo huduma mbalimbali ambazo kusudi lake kubwa ni kumsaidia mteja aweze kujikwamua kiuchumi. 

Aliongeza kuwa zipo huduma za mikopo ya aina mbalimbali ambapo walimu wanaweza kunufaika nayo. Mikopo ambayo inatolewa na Benki ya NMB sio kwa ajili ya wafanyabiashara tu bali ni kwa ajili ya kila mtu mwenye vigezo vya kukopeshwa ambapo walimu ni miongoni mwa walengwa wa mikopo hii. Msichukue mkopo benki kama hamna mipango thabiti ya matumizi ya mkopo huo, Ni vyema kuchukua mkopo benki ukiwa na mipango endelevu," alisema Bw. Omari Mtiga. 

"...Tukiwa kwenye mikakati ya serikali ya Viwanda ni vyema mkatumia vizuri maonyesho ya Nane nane yanayotarajiwa kuanza kutembelea mabanda ambayo mtajifunza namna ya uwekezaji kwenye sekta viwanda ili kujikwamua kiuchumi kwa kutumia uwepo wa benki ya NMB kwenye jamii yetu bila kuathiri mwenendo wa jaira zetu. Alisema kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Bi. Rehema Madenge katika hafla hiyo. 


Mkuu wa Kitengo cha wateja binafsi wa NMB, Bw. Omari Mtiga (kushoto) akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa siku ya Mwalimu katika mkoa wa Dodoma mwishoni mwa wiki

.

Sehemu ya walimu waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa siku ya walimu mkoa wa Dodoma.


Picha za kumbukumbu na Sehemu ya walimu pamoja na Afisa Tawala wa Mkoa wa Dodoma, Bi. Rehema Madenge.

TANZANIA EXCELS IN STATISTICAL CAPACITY AMONG SUB-SAHARAN AFRICAN NATIONS, WB REPORT SHOWS


By Veronica Kazimoto, Dar es Salaam

Tanzania has been ranked second, behind South Africa in statistical capacity among Sub-Saharan African nations. This is according to the World Bank (WB) 2016 Statistical Capacity Indicator (SCI).

WB has been assessing national statistical capacity in developing countries since 2004 and has produced overall SCI score as well as scores for three categories, Methodology, Source Data and Periodicity. Regional overall and specific category SCI are also produced to allow for comparison.

For every dimension, a country is scored against specific criteria, using information available from the WB, IMF, UN, UNESCO, and WHO.

A composite score for each dimension and an overall score combining all three dimensions are derived for each country on a scale of 0 - 100. A score of 100 indicates that the country meets all the criteria.

The statistical methodology aspect measures a country’s ability to adhere to internationally recommended standards and methods, by assessing guidelines and procedures used to compile macroeconomic statistics and social data reporting and estimation practices by looking at an updated national accounts base year, use of the latest Balance of payment, external debt reporting and IMF’s Special Data Dissemination Standard and enrolment data reporting to UNESCO.

On source data, this measures data collection activities in line with internationally recommended periodicity, and whether data from administrative systems are available and reliable for statistical estimation purposes and periodicity of population and agricultural censuses, the periodicity of poverty and health related surveys, and completeness of vital registration system coverage.

The third aspect concerned with the periodicity and timeliness looks at the availability and periodicity of key socio-economic indicators of which nine are MDG indicators.

Tanzania scored 90 percent for periodicity, 80 percent for source data and 50 percent for methodology which, contributed to an overall SCI of 73.3 percent. Although this overall score ranks Tanzania as second behind South Africa (82.2%) there is still room for improvements, especially in methodology.

The National Bureau of Statistics (NBS) is committed to continuing strengthening of the National Statistical System.
A graph showing Tanzania as a second country among Sub - Saharan countries in better statistical capacity. According to the World Bank report, Tanzania scored 90 percent for periodicity, 80 percent for source data and 50 percent for methodology which contributed to an overall of 73.3 percent.

SERIKALI YAONGEZA MUDA WA KUNYONYESHA KWA WATUMISHI WA UMMA NA MASHIRIKA NA SEKTA BINAFSI


Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii .

SERIKALI imeongeza masaa ya unyonyeshaji kwa watoto kwa watumishi wa serikali, mashirika pamoja sekta binafsi ili kuwezesha watoto kuwa na afya bora inayotokana na maziwa ya mama.

Hayo ameyasema Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu wakati akifungua Wiki ya Unyonyeshaji, amesema kuwa mama mzazi baada ya kumaliza miezi mitatu ataingia kazini 3:30 na kuondoka saa 7:30 katika kumuwezesha mama kunyonyesha mtoto bila kuingiliwa na majukumu ya kikazi.

Ummy amesema kuwa watendaji wa Umma na mashirika pamoja na taasisi lazima wafanye hivyo katika kutambua umuhimu wa mama mzazi kunyosha kwa muda uliowekwa kwa kipindi cha miezi sita.

Amesema kuwa ni gharama kubwa katika kuhudumia watoto walio na utapiamlo ambao unatokana moja ni kukosa maziwa ya mama kwa muda mrefu hivyo kuepuka ni nyia rahisi ikiwemo kutengwa kwa masaa hayo.

Waziri Ummy amesema kuwa suala la lishe lazima liangaliwe kwa ukaribu na wadau wote katika kuweza kuwaondoa watoto katika utapiamlo ambao unafanya kudumaa kwa akili.

Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Chakula na Lishe Nchini(TFNC), Joyceline Kaganda amesema jitihada mbalimbali zimekuwa zikifanyika juu ya masuala ya lishe na wadau kwa mifumo mbalimbali.

Amesema kuwa wiki ya unyonyeshaji wa kina mama ni muhimu katika katika ukuaji wa mtoto wa kumjenga katika afya bora.

Kwa upande wa Mkurugenzi wa Ushirikiano wa Lishe nchini (Panita), Tumaini Mkindo amesema serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dk. Pombe Magufuli imwemeka kipaumbele katika ubaoreshaji wa lishe nchini.

Amesema kuwa sera zimeweza kuongezeka katika masuala ya lishe ikiwa eneo la kipaumbele katika mpango wa taifa wa miaka mitano pamoja mikoa na halmashauri kuwa na bajeti ya lishe.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akipata maelezo juu masuala ya lishe kutoka kwa mtaalam wa lishe wa Taasisi ya Chakula lishe nchini (TFNC),Neema Joshua wakati maadhimisho ya wiki ya unyonyeshaji leo.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akizungumza wakati wa ufunguzi wa wiki ya unyonyeshaji na uzinduzi usambazaji taarifa kwa njia ya simu leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Chakula na Lishe Nchini(TFNC), Joyceline Kaganda akizungumza juu ya mikakati ya lishe na umuhimu wa unonyeshaji leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Ushirikiano wa Lishe nchini (Panita), Tumaini Mkindo akitoa salamu za mashirika yasio ya kiserikali yanavyofanya kazi katika sehemu ya lishe kwa kuwa miradi mbalimbali.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akibonyesha kitufe kuashiria uzinduzi wa taarifa kupitia simu za mikoni katika ufunguzi wa wiki ya unyonyeshaji leo.
Sehemu ya wadau katika ufunguzi wa wiki ya unonyeshaji leo jijini Dar es Salaam.

JESHI LA ZIMAMOTO LAZINDUA KAMPENI YA NAMBA YA DHARURA 114 KUKABILIANA NA MAOKOZI YA MAISHA NA MALI


 Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji na Uokoaji, Thobias Andengenye, akizungumza wakati wa Uzinduzi wa Kampeni ya Namba ya Dharura 114, itakayotumiwa na wananchi kutoa Taarifa za majanga ya moto, ajali, mafuriko, tetemeko la ardhi na majanga mengine. Wengine ni Katibu Mtendaji wa Taasisi isiyo ya Kiserikali inayojishughulisha na kuzuia Uhalifu, ajali (UAC), Elliot Andrew na Naibu Kamishna Rasilimali Watu wa Jeshi hilo, Billy Mwakatage (kulia). Uzinduzi huo umefanyika leo Makao Makuu ya Jeshi, jijini Dar es Salaam. Picha na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.
 Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji na Uokoaji, Thobias Andengenye, akikabidhiwa kipeperushi na Katibu Mtendaji wa Taasisi isiyo ya Kiserikali inayojishughulisha na kuzuia Uhalifu, ajali (UAC), Elliot Andrew(kushoto), wakati wa Uzinduzi wa Kampeni ya Namba ya Dharura 114, itakayotumiwa na wananchi kutoa Taarifa za majanga ya moto, ajali, mafuriko, tetemeko la ardhi na majanga mengine. Kulia ni Naibu Kamishna Rasilimali Watu wa Jeshi hilo, Billy Mwakatage. Uzinduzi huo umefanyika leo Makao Makuu ya Jeshi, jijini Dar es Salaam. Picha na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.
 Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji na Uokoaji, Thobias Andengenye, akionyesha kipeperushi   wakati wa Uzinduzi wa Kampeni ya Namba ya Dharura 114, itakayotumiwa na wananchi kutoa Taarifa za majanga ya moto, ajali, mafuriko, tetemeko la ardhi na majanga mengine. Wengine ni Katibu Mtendaji wa Taasisi isiyo ya Kiserikali inayojishughulisha na kuzuia Uhalifu, ajali S(UAC), Elliot Andrew na Naibu Kamishna Rasilimali Watu wa Jeshi  wa jeshi hilo, Billy Mwakatage(kulia).Uzinduzi huo umefanyika leo Makao Makuu ya Jeshi,jijini Dar es Salaam.Picha na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji
 Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji na Uokoaji, Thobias Andengenye, akionyesha mfano wa uwekaji stika yenye Namba ya Dharura 114, itakayobandikwa kwenye vyombo vya usafiri na maeneo mengine kwa ajili ya  kutumiwa  na wananchi kutoa Taarifa za majanga ya moto, ajali, mafuriko, tetemeko la ardhi na majanga mengine. Uzinduzi huo umefanyika leo, Makao Makuu ya Jeshi, jijini Dar es Salaam. Picha na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.
 Maafisa wa Jeshi waliohudhuria Uzinduzi wa Kampeni ya Namba ya Dharura 114, itakayotumiwa na wananchi kutoa Taarifa za majanga ya moto, ajali, mafuriko, tetemeko la ardhi na majanga mengine, wakimsikiliza Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji na Uokoaji, Thobias Andengenye (hayupo pichani) wakati wa Mkutano na Waandishi wa Vyombo vya Habari. Uzinduzi huo umefanyika leo, Makao Makuu ya Jeshi hilo, jijini Dar es Salaam. Picha na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji na Uokoaji, Thobias Andengenye (watano kulia), akiwa katika picha ya pamoja na Maafisa Waandamizi wa Jeshi hilo, Viongozi na Wadau walioshirikiana na Jeshi hilo kuwezesha  Uzinduzi wa Kampeni ya Namba ya Dharura 114, itakayotumiwa na wananchi kutoa Taarifa za majanga ya moto, ajali, mafuriko, tetemeko la ardhi na majanga mengine. Uzinduzi huo umefanyika leo, Makao Makuu ya Jeshi, jijini Dar es Salaam.Picha na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.

IMEANDALIWA NA KITENGO CHA HABARI NA ELIMU KWA UMMA-JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI, MAKAO MAKUU

DC MNDEME AMPONGEZA MAVUNDE KWA KUTATUA KERO YA MAJI KWA WANANCHI WAKE




Mkuu wa wilaya ya Dodoma Christine Mndeme akiwa ameketi katika mmoja ya kaya za wakazi wa Mhande akipata chakula baada ya kuzindua mradi wa maji. 
Mkuu wa wilaya ya Dodoma Christine Mndeme akifurahi jambo na wafadhili wa mradi wa maji wa Mhande kutoka Canada. 
Wananchi wa Mhande wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Chritine Mndeme katika uzinduzi wa mradi wa maji wa kijiji hicho. 
Mkuu wa wilaya ya Dodoma Christine Mndeme pamoja na Father Fransis wakifungua bomba la maji kama ishara ya uzinduzi wa mradi wa maji katika kijiji cha Mhande. 
Mkuu wa wilaya ya Dodoma Christine Mndeme akifurahi jambo na akina mama wa kijiji cha Mhande 
Mkuu wa wilaya ya Dodoma Christine Mndeme akisalimiana na father Fransis 
Mkuu wa wilaya ya Dodoma Christine Mndeme akiteta jambo na Brother Anthony ambaye ni muasisi wa mradi wa CPPS. 
Mkuu wa wilaya ya Dodoma Christine Mndeme akikagua eneo la pampu ya maji ya mradi wa maji wa Mhande. 
Mkuu wa wilaya ya Dodoma Christine Mndeme akicheza ngoma baada ya kuzindua mradi wa maji 
Mkuu wa wilaya ya Dodoma Christine Mndeme akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mhande 

……………………………………………………………..

Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini Christine Mndeme leo amezindua mradi wa Maji katika kijiji cha Mhande,Kata ya Ngh’ong’hona ambao umefadhiliwa na Shirika shirika la wamishionari wa damu takatifu ya Yesu(CPPS) uliogharimu kiasi cha Sh.Milioni 35.

Mradi huu umetokana na maombi ya Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Anthony Mavunde kwa Shirika la hilo kusaidia kutatua changamoto ya Maji katika kata hii ya Ngh’ongh’ona ambayo wananchi wake wamekuwa wakisumbuliwa na tatizo kubwa la upatikanaji maji safi na salama.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Mndeme amelishukuru shirika hilo la CPPS kwa ufadhili wa mradi huo na kumpongeza Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Anthony Mavunde kwa kuwa mstari wa mbele kutatua kero za wanachi wake hususani kero kubwa ya Maji katika kata ya Ngh’ongh’ona.

Amesema kutatuliwa kwa kero hiyo kumewatua kina mama ndoo kichwani kwa kuwa walikuwa wakienda kuchota maji umbali mrefu.

“Mwili unahitaji maji unapotafuta maji mbali roho inasononeka hata muda wa kusali unaukosa, tunashukuru sana shirika hili lakini wananchi tuna wajibu wa kuutunza mradi huu ambao ni wa thamani kubwa sana,”amesema

Hata hivyo amesema hatasita kuwachukulia hatua watu watakaoharibu miundombinu ya mradi huo wa maji huku akiwataka kuunda kamati ya maji ili kuendesha mradi huo.

Aidha amesema kwa kushirikiana na Mavunde watashughulikia upatikanaji wa umeme katika mradi huo wa maji ili uweze kutoa huduma ipasavyo kwa wananchi.

Naye, Diwani wa Kata hiyo Philipo Nangu amesema wananchi hao wamekuwa wakipata adha kubwa ya maji na kulazimika kutembea umbali wa zaidi ya kilomita 10 kufuata huduma hiyo vijiji jirani jambo lilosababisha kushindwa kufanya shughuli za kimaendeleo.

Kadhalika, Mavunde amesema amefanikiwa kupata ufadhili wa Shirika la GIZ la Ujerumani ambao watasaidia kusambaza huduma hiyo ya maji katika kata yote ya Ngh’ong’hona ili kumaliza changamoto ya Maji kwenye eneo hilo.

WATUMISHI HOUSING WAPELEKA MRADI WA NYUMBA 500 MKOANI DODOMA


Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

KATIKA juhudi za kuunga mkono uamuzi wa serikali wa kuhamishia shughuli za serikali katika Mkoa wa Dodoma, Kampuni ya Watumishi Housing imepanga kuwajengea watumishi nyumba bora na za kisasa Mkoani humo.

Kampuni hiyo yenye dhamana ya uwekezaji katika nyumba ikiwa ni mpango wa taifa wa makazi kwa watumishi, imeamua kuwekeza katika Mkoa wa Dodoma na wameshapata eneo la Njedengwa lenye ukubwa wa  hekari 55 likiwa limeshapimwa tayari kwa ujenzi wa nyumba 500.

Akielezea mikakati hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Watumishi Housing Fredy Msemwa amesema kuwa katika awamu ya kwanza ya ujenzi wa nyumba hizo zitajengwa nyumba 159 na zitakuwa kwa ajili ya watumishi watakaokuwa wamehamia Mkoani Dodoma na wale wanaoishi haoo.

Msemwa amesema, eneo la Njedengwa ni eneo ambalo limeendelezwa tayari likiwa lina huduma zote za kijamii ikiwemo barabara ya lami, maji, umeme na miundo mbinu mingine ambayo inalifanya kuwa eneo bora zaidi kwa makazi ya watumishi na yatai ujenzi umeshaanza na utakamilika baada ya miezi nane (8) na zitakuwa katika mfumo wa aina mbili zile zilizoisha kabisa na zitakazokuwa zimeisha kwa asilimia 80.

Nyumba hizo zitakuwa na mahitaji ya kutosha kabisa kwa watumishi wa umma wa kipato tofauti na utapatikana kwa njia ya mkopo endelevu kupitia benki washirika huku nyumba zilizokamilika kabisa zitauzwa kwa shilingi milioni 56 na zile zilizokamilika kwa asilimia 80 zitakuwa kwa milioni 46 zote zikiwa pamoja na VAT.

Mbali na hilo, Msemwa amesema wamepokea msaada wa vifaa vya upimaji wa viwanja na miji kutoka benki ya Dunia kwahiyo itarahisisha katika upimaji wa viwanja na pia kuanza kutoa huduma zote za makazi kuanzia uuzaji wa viwanja vilivyopimwa pamoja na nyumba zilizokamilika na huduma hii itaanzia mkoani Dodoma.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Watumishi Housing Fredy Msemwa  akielezea namba walivyojizatiti katika kuiunga mkono serikali uamuzi wa kuhamishia shughuli za serikali katika Mkoa wa Dodoma ikiwa imepanga kuwajengea watumishi nyumba bora na za kisasa Mkoani humo.
Mkuu wa Kitengo cha Masoko wa Watumishi Housing Raphael Mwabuponde akiwaelezea waandishi wa habari namna ya watumishi kupata nyumba hizo zitakazojengwa katika Mkoa wa Dodoma.

HOSPITALI ZOTE ZA MIKOA ZIJENGE VITUO VYA METHADONE-MAJALIWA


 WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amegiza hospitali zote za mikoa nchini kujenga vituo vya kutolea huduma ya Methadone kwa ajili ya kuwahudumia waathirika wa dawa za kulevya.

Alitoa agizo hilo jana (Jumatatu, Julai 31, 2017) alipozindua kituo cha kuhudumia waathirika wa dawa za kulevya katika Hospitali ya Rufaa ya Mbeya, ambapo alisema Serikali inaendelea na mpango wake wa kudhibiti uingizwaji wa dawa hizo.

Kituo hicho kinatarajiwa kuhudumia watumiaji wa dawa za kulevya katika mikoa yote ya Nyanda za Juu Kusini, ambayo ni Iringa, Njombe, Ruvuma, Katavi, Rukwa, Songwe na Mbeya.

Waziri Mkuu alisema vituo vya kuhudumia waathirika wa dawa za kulevya ni msaada mkubwa kwa vijana kwa kuwa mbali na kupewa dawa pia watafundishwa stadi za maisha ili wanapomaliza matibabu waweze kushiri katika shughuli za maendeleo ikiwemo kujiajiri.

Hata hivyo aliwaomba wananchi kuendelea kushirikiana na Serikali katika kuwafichua wazalishaji, watumiaji na wafanyabiashara wa dawa za kulevya kwa sababu ni watu wanaoishi nao katika jamii.

Kwa upande wake, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kupambana na Kudhibiti Dawa za Kulevya, Rodgers Sianga alisema licha ya matumizi ya dawa za kulevya kuathiri mfumo wa fahamu pia watumiaji wako katika hatari ya kuugua homa ya ini.

Alisema vituo hivyo licha ya kutoa dawa ya methadone pia waathirika wa dawa za kulevya ambao watagundulika kuwa na maradhi mengine kama ukimwi, kifua kikuu, matatizo ya kisaikolojia pamoja na homa ya ini pia watatibiwa katika vituo hivyo.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali hiyo, Dkt.Godlove Mbwanji alisema matumizi ya dawa za kulevya yamechangia ongezeko la wagonjwa wa akili mkoani Mbeya, ambapo mwaka jana  pekee walibainika wagonjwa 486.

SERIKALI, WADAU KUANDAA RIPOTI YA KWANZA YA KITAIFA YA UTEKELEZAJI WA HAKI ZA WATU WENYE ULEMAVU NCHINI


Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mara ya kwanza imeanza maandalizi ya ripoti ya utekelezaji wa haki za watu wenye ulemavu tangu Tanzania kuridhiria Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Watu wenye ulemavu mwaka 2009.

Katika kufanikisha suala hili, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali imeandaa kikao kazi kinachoshirikisha wadau wa haki za watu wenye ulemavu nchini ili kushirikiana katika maandalizi ya rasimu ya awali ya ripoti ambayo itajadiliwa,kuboreshwa na hatimaye kuwasilishwa katika Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa ikiwa ni hatua stahiki katika utekelezaji wa Mkataba wa Haki za watu wenye Ulemavu.

Kikao kazi hiki kinafanyika Mkoani Morogoro kuanzia leo tarehe 31 Julai 2017 mpaka tarehe 2 Agosti 2017 kwa lengo mahususi la kua na uelewa wa pamoja wa mfumo wa uandaaji ripoti za haki za watu wenye ulemavu wa Umoja wa Mataifa,kujadili na kutathmini utekelezaji wa Sheria ya Watu wenye Ulemavu,kutoa elimu kwa wadau kuhusu usimamizi na ulinzi wa haki za watu wenye ulemavu na kuandaa rasimu ya awali ya haki za watu wenye ulemavu.

Akifungua kikao kazi hicho,Ndugu Erick Shitindi , Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Vijana,Kazi,Ajira na Watu wenye Ulemavu ameeleza kuwa kwa mujibu wa kifungu cha 35 sehemu ya i na ii, ya Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Watu wenye Ulemavu, kila nchi inapaswa kuwasilisha ripoti ya kitaifa miaka miwili mara baada ya kuridhia mkataba husika jambo ambalo Tanzania haijwahi kulitekeleza kutokana na changamoto mbalimbali ikiwemo ukosefu wa fedha kwa ajili ya maandalizi ya ripoti hiyo.

“Kwa mantiki hiyo,maandalizi ya ripoti hii yamekuja wakati muafaka na itaifanya Tanzania kuingia katika historia ya kutekeleza mikataba mbalimbali ya haki za binadamu ikiwemo haki za watu wenye ulemavu na kwa ujumla nchi ilishaanza kuchukua hatua ikiwa ni pamoja na kutunga Sheria ya watu wenye ulemavu (The Persons with Disabilities Act,2010)”.anasistiza Katibu Mkuu Shitindi.

Naye Bi. Sarah Mwaipopo, Mkurugenzi anayeshughulikia masuala ya Katiba na Haki za Binadamu,kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ameeleza kua Serikali inao wajibu kisheria kuratibu maandalizi ya ripoti na kutolea taarifa masuala mbalimbali ya utekelezaji wa haki za binadamu nchini kama ilivyoainishwa katika kifungu cha 14 cha Sheria ya Utekelezaji wa Majukumu ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ( Section 14 of the Attorney General (Discharge of Duties) Act,2005).

Pamoja na Katiba, Sheria na Mikataba mbalimbali ya Kimataifa kutambua haki za watu wenye ulemavu, Bwana Coomaaravel Pyaneandee, ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Haki za watu wenye ulemavu ya Umoja wa Mataifa aneleza kuwa zipo changamoto ambazo zimeendelea kuwepokatika usimamizi na utekelezaji wa haki za watu wenye ulemavu ambazo ni pamoja na ukosefu wa takwimu sahihi za idadi ya watu wenye ulemavu,unyanyapaa katika jamii na ngazi ya familia,kukosekana mfumo mzuri wa elimu jumuishi,asasi za kiraia kushindwa kutumia nafasi yake kufanya kazi vizuri na serikali hivyo kushindwa kupaza sauti ipasavyo,kutokua na uelewa kuhusu watu wenye ulemavu na mahitaji yao na ukosefu wa miundombinu stahiki katika sehemu mbalimbali kwa watu wenye ulemavu.

Wadau wanaoshiriki katika maandalizi ya rasimu ya awali ya ripoti ya haki za watu wenye ulemavu ni Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali,Tanzania Bara na Zanzibar,Chama cha watu wenye Ualbino Tanzania,Shirikisho la Watu wenye Ulemavu Tanzania, Tume ya Uchaguzi Tanzania Bara na Zanzibar, Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora,Chama cha Walemavu wenye Utindio wa Ubongo,Chama cha Wazazi wenye watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi,Wizara ya Habari, Sanaa,Utamaduni na Michezo,Jeshi la Polisi Tanzania,Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii,Wizara ya Afya Zanzibar,Chama cha Watu walioumia Uti wa mgongo Tanzania,Under the Same Sun,Wizara inayoshughulikia masuala ya uwezeshaji wazee,watoto na watu wenye ulemavu Zanzibar na Chama cha Wasiiona Tanzania na Ofisi ya Taifa ya Takwimu.