Marco Pellegri alipitisha mkono wake katika nywele zake na kuchukua simu yake iliokuwa katika mfuko wa ndani wa koti lake.
Jamaa huyo mwenye umri wa miaka 53 alikuwa akijizuia kutobubujikwa na machozi.
Lakini mwishowe alilazimika ,na alikaa katika kiti chake na kutokwa na machozi ya raha.
Pellegri amaye ndio msimamizi wa timu hiyo alikuwa amemuona mwanawe Pietro mwenye umri wa miaka 16 akifunga bao lake la kwanza na la pili kwa timu hiyo katika mechi ya ligi ya Serie A dhidi ya Lazio baada ya kuchukua mahala pake Ricardo Centurion katika kipindi cha kwanza.
Ilikuwa ndoto iliofanikiwa kwa babake mtoto huyo, Marco ambaye alikuwa akisema kwamba iwapo nitamuona Pietro akiichezea Genoa katika uwanja wa Luigi Ferraris atafurahi.
Atajihisi kana kwamba maisha yake yamekamilika.
Picha za Marcos akionekana akibubujikwa na machozi ziligonga vichwa vya habari duniani na zikamfanya Pietro kushindwa kujieleza alipoonyeshwa baada ya mechi ambapo Genoa ililazwa 3-2.
Na baadaye ilikuwa Pietro, saa alizokuwa ndani ya gari huku babake akimpeleka katika mechi moja hadi nyingine.
Mshambuliaji huyo mchanga pia naye alijawa na hisia.
Mwisho mazungumzo yalikuwa ya Petro kufunga mbele ya eneo la Gradinata Nord , eneo ambalo mashabiki wa Genoa hukongamana.
Wapellegri wanatoka Genoa.
Wanaishi Pegli, mji wa baharini uliopo magharibi ambapo Genoa ina uwanja wake wa soka.
Marco ameifanyia kazi klabu hiyo kwa miaka mingi, awali akiwa katika chuo cha mafunzo ya soka, na sasa akiwa mkufunzi wa Genoa.
Mkewe Marzia anatoka katika familia ya mashabiki wa Sampdoria.
Lakini Pietro amekuwa akiwaona wale wa Genoa pekee.
Wakati klabu hiyo iliposhushwa daraja hadi katika daraja la tatu kufuatia kashfa ya udanganyifu wa mechi miaka 12 iliopita ,Marco Rossi , nahodha wa klabu hiyo alikuwa akicheza playstation na mwana wa Pellegro.
Rossi aliichezea Genoa mara 286 na hadi leo amekuwa mfano mkubwa katika klabu hiyo. Pietro alipenda kuishabikia klabu moja pekee, Genoa.
Kitu kinachoweka historia ni kwamba licha ya kuwa kinda, klabu maarufu zimekuwa zikitaka kumsajili kwa miaka kadhaa.
Beppe Marotta, mkurugenzi wa Juventus , anadai kwamba alijaribu kumsajili Pietro miaka miwili iliopita wakati ambapo hakuna aliyemjua.
Msimu huu Inter Milan ilikubali kulipa Yuro milioni 60 kumsajili Pietro pamoja na kinda mwengine wa Genoa Eddie Salcedo, na ni sheria za Fifa za fair Play zilizozuia uhamisho huo.
Na kufikia siku ya mwisho ya dirisha la uhamisho, AC Milan ilitaka kumsajili Pietro baada ya kumuuza M'baye Niang.
''Lakini mpango huo haukufaulu'', alisema afisa mkuu mtendaji Marco Fassone.
Bado watajaribu tena.
Wengine wanasema ni mapema mno kubaini talanta ya kinda Pietro na kwamba dunia lazima iwe makini.
Nchini India, na katika maeneo mengi duniani, kuchanjwa au kuchorwa chale ambazo hufahamika zaidi kama 'tattoo' hutazamwa kama ishara ya uhuru au kuasi.
Vijana wengi wanachanjwa chale kuonyesha utambulisho wao, jambo ambalo linawatambulisha kwa njia ya kipekee - sifa zao halisi.
Lakini kwa Geeta Pandey, uamuzi wake wa kupata chale ulikuwa aina yake ya kuasi, njia yake ya kudhihirisha uhuru wake aliokuwa ameupigania sana.
Ilikuwa njia yake ya kusema: "Sitafuata kanuni zilizowekwa."
Anasema alikua akifikiria kwamba chale, pamoja na kutogwa kwenye sikio au pua, zilikuwa njia za kuwadunisha wanawake.
Hilo ni kwa sababu mamake alikuwa na chale kadha.
Na bibi yake alikuwa na hata zaidi.
"Na waliniambia kwamba hawakuwa na usemu kuhusu hayo," anasema.
Katika jamii nyingi maeneo ya mashambani katika jimbo la Uttar Pradesh kaskazini mwa India, anakotoka Pandey, ni lazima kwa wanawake ambao wameolewa kuwa na chale, ambazo kwa lugha yao hufahamika kama Godna.
"Familia yangu iliniambia kwamba iwapo singechanjwa chale, hakuna mtu hata mmoja kwenye familia hiyo ambayo angekunywa maji au kula chakula nilichokiandaa. Ningechukuliwa kuwa mtu mwenye uchafu, najisi, na asiyefaa kuguswa," mamake Pandey anasema mamake alimwambia.
"Babangu bila shaka hakuhitajika kutogwa au kuwa na chale kwa sababu, alikuwa mvulana."
Mamake aliozwa akiwa mtoto. Hakuna ametimiza miaka 11 wakati wa harusi yake miaka ya 1940.
Wiki chache baada ya sherehe hiyo, mwanamke mkongwe kutoka kijiji chake alifika nyumbani kwao kumchanja chale.
Historia ya chale
Binadamu wamekuwa wakichanjwa chale kwa maelfu ya miaka.
Zilitumiwa kuwatambua wafungwa, watumishi, vijakazi na watumwa.
Wagiriki na Warumi enzi za kale walikuwa na chale, India pia.
Wayahudi walichorwa chale zenye nambari za utambulisho walipokuwa wanazuiliwa na kufanyikwa kazi na Wanazi waliokuwa wanatawala Ujerumani wakati wa Vita Vikuu vya Pili vya Dunia.
Zilitumiwa pia kuwatambua binadamu na watu wa tabaka mbalimbali
Mara nyingi chale zilikuwa kama adhabu, na zilichukuliwa kama jambo la aibu au ishara ya kudunishwa.
Wakati mwingine, zilikuwa ishara ya kumilikiwa na mtu fulani - mfano chale yenye nembo au alama ya baba wa mtu au mume wa mtu.
Vifaa alivyotumia vilikuwa vya msingi sana: sindano na moto.
Mchakato wote ulihusisha kuchomwa kwa sehemu ya juu ya ngozi na kujaza rangi kwenye chale.
Nyakati hizo, hakukuwa na dawa za kupunguza maumivu au mafuta ya kuharakisha shughuli ya kupona.
Chale wakati huo zilichukua mwezi mzima kupona.
Zaidi ya miaka sabini baadaye, chale za mamake Pandey karibu zimefutika, lakini bado anaukumbuka uchungu alioupitia.
"Nililia sana. Nilikuwa nampiga mateke mwanamke huyo aliyekuwa ananichanja. Mwishowe, alienda na kulalamika kwa babu yangu. Alisema mimi ni msumbufu," mamake Pandey anasema.
Hajui chale alizochorwa zina maana gani na mwanawe Pandey haelewi pia.
"Labda pamechorwa phool-patti," anasema, maana yake maua na majani.
Keya Pandey, mwanaathropojia wa kijamii kwa sasa katika chuo kikuu cha Lucknow ambaye amefanya utafiti sana kuhusu chale katika maeneo ya mashambani India anasema michoro mingi huwa na maua na majani ya mimea mbalimbali.
Kadhalika, wengine huchanjwa chale za majina ya waume zao au baba zao.
Kuna wengine huchorwa majina ya vijiji vyao au nembo za ukoo au ishara nyingine za kitamaduni, bila kusahau pia miungu.
Bi Pandey anasema ameona chale katika karibu kila jamii India na anakadiria kwamba mamilioni ya wanawake wana chale.
Katika baadhi ya jamii, hasa makabila ambayo yameendelea kudumisha utamaduni, wanawaume na wanawake huwa na chale.
"Ni ishara ya utambulisho, katika uhai na katika mauti. Wazo kwamba unapofariki roho yako husafiri mbinguni au jehanamu na utaulizwa ulikotoka, na hivyo unaweza kufahamu asili yako kupitia chale," anasema Pandey.
Kuna jamii nyingine ambazo wanawake wake hupata chale kama mapambo.
Hata hivyo, kuna baadhi ya visa ambapo wanawake wa tabaka la chini walijichanja chale ili kuwafanya wasipodenze na hivyo kutowavutia wanaume wenye ushawishi ambao wakati mwingine wangewadhalilisha kimapenzi.
Lakini katika jamii nyingine, sana anakotoka Pandey, chale zilikuwa za wanawake pekee, ishara ya hali yake katika ndoa.
Kwa mamake na bibi yake, zilikuwa ishara ya kutakasika - kutokana na wazo kwamba iwapo mwanamke hangefanyiwa tambiko lenye uchungu hivyo, hangestahiki kukubalika katika jamii.
Utamaduni huo hata hivyo umeanza kufifia - na wanawake wengi na wasichana wanakataa kuchanjwa chale.
Maendeleo na maisha ya kisasa yameanza kubadili mtazamo wao na kadhalika mawasiliano na watu wengine kutoka nje ya vijiji vyao.
Utamaduni unaanza kubadilika na wasichana vijijini hawataki tena kupata chale.
Hilo linadhihirika zaidi miongoni mwa wasichana wa jamii ya Baiga.
Bi Pragya Gupta wa shirika la WaterAid India ambaye amezuru majuzi eneo la watu wa jamii ya Baiga kufahamu iwapo wana maji safi ya kunywa anasema wanawake wengi aliokutana nao wana chale.
Lakini wengi wa wasichana hawana.
Kuimarika kwa hali ya barabara, kuwepo kwa runinga na simu za rununu pia vimebadilisha mambo. Aidha, watoto wengi wanaenda shule na kubadili mtazamo wao kuhusu utamaduni huo.
"Nilikutana na Anita, 15. Ana chale usoni na aliniambia kwamba alihisi uchungu sana na kwamba hatachorwa chale nyingine. Mamake Badri, wa miaka 40, ana chale kote mwilini," Bi Gupta anasema.
Uasi wa Anita unaungwa mkono na mamake.
"Nilikwua sijasoma na nilipokea niliyoambiwa na wazazi wangu bila kuuliza maswali. Lakini yeye huenda shuleni na hataki chale, hilo ni sawa kwangu," anasema.
Miaka ya karibuni, raia wa India katika mitaa ya kifahari wameanza kupata chale pia, wakiiga waigizaji na wanamuziki nyota wa Hollywood.
Punder anasema marafiki zake wengi pia wana chale.
Lakini kwangu, kwa sababu ya utamaduni wangu, chale zinabaki mwiko - ishara ya kudunishwa kwa wanawake.
Inaaminika kuwa asilimia 1 hadi 3 ya idadi ya watu hawana hisia zozote za kingono.
Kwa miaka kadhaa Stacey alishindwa kufumbua fumbo la ni kwa nini hakutaka kushiriki ngono na mtu yeyete hata mumewe.
Kama anavyoelezea hapa ni daktari wake aliyemwambia ukweli.
Kwa muda mrefu sana nilidhani nina matatizo ya kiakili na kiumbile.
Nilihisi kwamba sio jambo la kawaida kutoshiriki ngono.
Marafiki zangu wangezungumza kuhsu marafiki zao wa kiume ama hata watu maarufu ambao wangependa kushiriki nao ngono lakini mimi sikuwa na mtu yeyote akilini ambaye nahisi tungeshiriki naye ngono.
Wakati nilipokuwa katika miaka yangu ya ishirini nilianza kuona tofauti niliyo nayo , lakini singeweza kuambia mtu yeyote kwa sababu yalikuwa mawazo, watanifikiria mimi sio mtu wa kawaida, kwa hivyo nikaamua kunyamaza.
Kutokuwa na hisia zozote za ngono ACE sio jambo la kawaida ijapokuwa mara nyengine uhisi kuvutiwa ki-mahaba.
Nilikutana na mpenzi wangu ambaye sasa ni mume wangu wakati nilipokuwa na miaka 19, na sikujua maana ya kutokuwa na hisia za kushiriki ngono, hivyobasi nilidhani niko nyuma na kwamba sielewi mambo.
Nilikuwa nikifikiria kwamba nampenda sana mwanamume huyu na iwapo atanichumbia nitakubali asiliia 100 kwa sababu najua ningependa kutumikia maisha yangu yote naye, lakini kwa nini sitaki kushiriki naye ngono? ni jambo la kushangaza.
Tulizuru maeneo mbali mbali na aliniambia kwamba yeye atasubiri hadi siku ninayohisi kushiriki ngono naye.
Alinisaidia sana na hakutaka kunilazimisha kufanya kitu ambacho sikupendelea.
Nilifanya makosa makubwa kwa kutafuta katika mtandao sababu za kimatibabu ambazo husababisha mtu kutokuwa na hisia za kushiriki tendo la ngono.
Maadili ya kijamii yanaelezea kwamba ngono na watoto ndio sababu ya ndoa na marafiki zangu wote walikuwa wakiolewa na kupata watoto.
Nilifikiri mungu wangu kuna hili tarajio kwamba ninafaa kushiriki tendo la ngono na mumewe wangu ili kupata watoto.
Nilianza kuota ndoto za ajabu kwamba mumewe wangu huenda ataniwacha kwa msichana mwengine anayefanana nami lakini ambaye atakubali kulala naye na ikafikia kiwango ambacho wasiwasi wangu nilishindwa kuuvumilia.
Nilifikiria, wajua nini? ni muhimu kusuluhisha swala hilo , nilitaka kujua ni nini kilichokuwa kikiendelea, wakati huo nikiwa kati ya miaka 27 ama 28.
Nilifanya makosa ya kufanya utafiti katika mtandao na hayo yalikuwa makosa makubwa sana, kulikuwa na mambo mengi ambayo yalikuwa ya kawaida kama vile homoni zilizokuwa zikitoweka mara kwa mara , lakini kile ambacho niliiona ni kuwa na uvimbe katika ubongo.
Nilisema, mungu wangu nitafariki kutokana na uvimbe katika ubongo.
Nilienda kwa daktari wangu na kusema, tazama ni hatari?, nitafariki?
Aliniambia, tulia una tatizo la kutokuwa na hisia za kushiriki ngono.
Nilisema, ni nini hiyo? nini?
Sijawahi kuhisi kile watu wengi hutaja kuwa na hisia za kingono.
Hivyobasi alinielekeza katika mitandao na hapo ndipo nilipokutana na watu kama mimi.nilifurahi.
Sikuwahi kusikia kwamba kuna watu wasiokuwa na hisia za ngono.
Nilifanya utafiti zaidi na kuanza kujihisi kawaida, hivyobasi nilizungumza na mume wangu kuhusu swala hilo.
Na alisema, nilidhani kwamba kila kitu kilikuwa sawa .
Amekuwa mtu mzuri sana, amekuwa akinielewa sana.Baadhi ya watu walio na tatizo kama langu walikuwa na haya ya kusema:
Nina umri wa miaka 60 na sijawahi kukutana na mtu mwengine ambaye yuko kama mimi. Sijawahi kusikia hadharani .
Nilipotambua kwamba sina hisia za kushiriki ngono nilizungumza na watu kadhaa na huku wengine wakijitokeza na kuliangazia swala hili kwa uwazi nimepata majibu mabaya sana.
Kundi moja la wachezaji wenzagu katika chuo kikuu waliamua kunipangia kwenda kujiburidisha usiku kwa lengo la kutaka nishiriki ngono walipogundua kwamba sijashiriki ngono bila kujali kwamba nilikuwa na tatizo.
Kuna watu wengi wasio na hisia za ngono ambao wanapoanza uhusiano na mtu mwengine wanashiriki ngono na wanaendelea kama kawaida , lakini kwangu mimi kila wakati ninapokaribi kufanya tendo hilo mwili wangu unakataa kabisa.
Ni utoto mwingi na watu ninapowaambia hushangaa na kuniuliza ni vipi unaweza kupata watoto.
Ijapokuwa kuna njia nyingi za kupata watoto iwapo ninataka, ni swala ambalo linawezekana.
Nimegundua tatizo lango kwa miaka mitatu sasa.
Nasherehekea kuwa mtu mwenye tatizo hili, nafurahia na napenda kuzungumza na wengine ili watu zaidi kuelewa na sio kuwahukumu watu wasio na hisia za kufanya ngono.
Nadhani iwapo ningejua kwamba nina tatizo hili nilipokuwa na miaka 18 ama 19 nadhani afya yangu ya kiakili ingekuwa bora wakati mwingi wa miaka yangu ya 20.
La kushangaza zaidi ni kwamba wakati kabla ya kugundua tatizo langu mume wangu alikuwa akiniita Stace Ace
Familia ya mwanariadha mlemavu wa miguu kutoka nchini Afrika Kusini, Oscar Pistorius aliyefungwa kwa kosa la kumuua mpenzi wake. Reeva Steenkamp imetoa tamko lenye nia ya kwenda mahakamani kufuatia kusudio la watengeneza filamu inayohusu maisha ya mwanariadha huyo .
Filamu hiyo, iliyopewa jina la Blade Runner Killer,, inayotarajiwa kutolewa nchini Marekani mwezi ujao.
Familia ya mwanariadha huyo inasema kwamba huo ni uwazi mbaya kabisa wa ukweli.
Nayo familia ya marehemu Steenkamp imekinza madai hayo kwamba hadithi ama maudhui ni kutokana na mtazamo wa Reeva na mama yake.
Maafisa kutoka kote duniani wanakutana nchini Ufaransa kujaribu kutafuta njia za kuzuia kwa asislimia 90 ya vifo vinavyosababishwa na ugonjwa wa kipindupindu ifikapo 2030.
Ugonjwa huo unasambaa kupitia maji machafu huwaua karibu watu 100,000 kila mwaka.
Ni mara ya kwanza serikali, shirika la afya duniani, mashirika ya misaada na wafadhili wametoa ahadi kama hiyo.
Hii inakuja wakati Yemen inandelea kupambana na moja ya milipuko mibaya zaidi ya ugonjwa wa kipindupindu katika historia yake.
Ugonjwa wa Kipindu pindu katika karne ya 21 umeelezewa kama ''aibu kubwa kwa dunia,"
Ugonjwa huo ulitokomezwa nchini Uingereza na Marekani zaidi ya miaka 100 iliyopita , lakini unaendelea kusababisha vifo katika mataifa mengi yanayoendelea.
Si ghali kutibu ugonjwa huo na unaweza kuepukika kabisa ikiwa watu watapata maji safi na vyoo visafi.
Miji miwili mikubwa zaidi nchini Australia itakumbwa na joto la nyusi joto 50 miaka michache inayokuja , kwa mujbu wa utafiti.
Miji ya Sydney na Melbourne inatarajiwa kukumbwa na hali hiyo licha ya kasi ya kuongezeka kwa joto duniani kudhibitiwa na mkataba wa Paris wa kuzuia kuongezeka joto kwa viwango visivyozidi nyusi joto mbili
Kuzuia kuongezeka joto chini ya viwango hivyo kunaweza kuzui viwango hivyo kufika nyusi joto 50, kwa mujibu wa wanasayansi.
Mji wa Sydney ulifikia nyusi joto 45.8 mwaka 2013 huku Melbourne nao ukafika nyusi joto 46.4 mwaka 2009.
Utafiti huo ulitangazwa maeneo ya Victoria na New South Wales, lakiniawatafiuri wanasmeakwa semu zingien za Australia pia zitaathiriwa.
Kati ya miaka iliyokumbwa na joto la juu zaidi duniani ni mwaka 2015.
Mmoja wa watafiti Dr Lewis, alisema kuwa miji hiyo itashuhudia nyusi joto 50 kati ya mwaka 2040 na 2050.
Msimu wa joto wa hivi majuzi nchini Australia ulivunja rekodi 205 huku msimu wa baridi ukiwa wenye joto zaidi kwa mujibu wa baraza huru la hali ya hewa nchini humo.
Mwezi uliopita watu nchini Austalia walionywa kujiandaa kwa mto mkali wa nyika mwak 2017-2018.
Nao wanadiplomasia wa Cuba wamepewa muda wa siku saba kuondoka Marekani.
Takriban watu 21 wanaofanya kazi kwenye ubalozi wa Marekani nchini Cuba wamelalamikia matatizo ya kiafya yakiwemo kupoteza uwezo wa kusikia na kisungusungu.
Ripoti za awali zinasema kuwa mashambulizi ya kutumia sauti ndiyo yalichangia.
Cuba imekana kuwalenga wafanyakazi wa ubalozi wa Marekani na Marekani yenyewe haijailaumu serikali ya Cuba kwa mashambulizi hayo.
Mkosoaji mkubwa wa rais wa Rwanda Paul Kagame, Diane Rwigara ameshtakiwa kwa kuchochea uasi dhidi ya serikali.
Ameshtakiwa pamoja na mama yake Adeline Rwigara na dada yake Anne Rwigara.
Diane Rwigara aluzuiwa kuwania urais wa mwezi Agosti nchini Rwanda.
Rais wa sasa Paul Kahame alishinda uchaguzi huo kwa asilimia 99, na kupelekea madai kuwa kuikuwa na udanganyifu madai yalipingwa na mamlaka ya nchi hiyo.