Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akihutubia wakati wa ufunguzi wa warsha ya wadau wa sekta ya ujenzi kuhusu uboreshaji wa utendaji kazi wa Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC), jijini Dar es Salaam.
Wadau wa sekta ya ujenzi wakimsikiliza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (hayupo pichani), katika warsha ya sekta hiyo kuhusu uboreshaji wa utendaji kazi wa Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC), jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (kushoto), akizungumza jambo na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo (Sekta ya Ujenzi), Mhandisi Joseph Nyamhanga (kulia), katika warsha ya wadau wa sekta ya ujenzi kuhusu uboreshaji wa utendaji kazi wa Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC), jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC), Prof. Mayunga Nkunya (kulia), akifafanua jambo na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (kushoto), jijini Dar es Salaam.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC), Dkt. Samson Mturi akitoa taarifa kwa mgeni rasmi Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (hayupo pichani), katika warsha ya wadau wa sekta ya ujenzi kuhusu uboreshaji wa utendaji kazi wa Baraza hilo, jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (kushoto), akitoa maelekezo kwa Mkurugenzi wa Huduma za Biashara Bw. Milton Lupa (aliyesimama), kutoka Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), wakati alipokagua mradi wa ujenzi wa nyumba za magomeni, jijini Dar es Salaam.
Mkadiriaji Majenzi na Msanifu Majengo Neema Kifua (wa pili kulia), akitoa taarifa kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa kuhusu maendeleo ya mradi wa ujenzi wa nyumba za magomeni, alipotembelea mradi huo leo, jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amewataka wadau wa sekta ya ujenzi kuanza kuweka twakwimu takwimu zinazohusu masuala ya ujenzi hapa nchini.
Akifungua warsha ya wadau wa sekta ya ujenzi kuhusu uboreshaji wa utendaji kazi wa Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC), Prof. Mbarawa, amesisitiza umuhimu wa sekta hiyo kuimarisha taarifa za aina, vifaa, viwango vinavyohitajika kimataifa na gharama katika shughuli za ujenzi wa barabara, viwanja vya ndege, nyumba na miundombinu mingine.
“Sekta ya Ujenzi ina mchango mkubwa katika ujenzi wa miundombinu ya kiuchumi na kijamii hivyo uwepo wa taarifa mbalimbali unahitajika ili kurahisisha uelewa wa wananchi wa kawaida katika masuala ya ujenzi na gharama zake”, amesema Prof. Mbarawa.
Aidha, Waziri Prof. Mbarawa amewahakikishia wadau wa sekta ya ujenzi kuwa Serikali itaendelea kuweka mazingira wezeshi ili kuhakikisha sekta hiyo inakidhi matarajio ya watanzania wengi kwa lengo la kuwajengea miundombinu iliyo bora na imara.
Ameongeza kuwa mapendekezo yatakayotolewa na wadau hao yatarahisisha utekelezaji wa miundombiu mbalimbali ambayo italeta chachu kwa sekta nyingine zikiwemo za kilimo, nishati, utalii, viwanda, madini na uendelezaji wa biashara na nchi nyingine za kikanda.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara hiyo (Sekta ya Ujenzi) Mhandisi Joseph Nyamhanga amesema ongezeko la miradi ya ujenzi imechangia Serikali kutafuta wataaalm waliofanya tafiti kwa ajili ya uboreshaji wa baraza hilo wataongeza tija na ufanisi wa sekta hii muhimu ya ujenzi kwa wadau, wananchi na Serikali.
Naye, Mwenyekiti wa Baraza la NCC Prof. Mayunga Nkunya amemuhakikishia Waziri Prof. Mbarawa kuwa baraza lake litasimamia michango yote itakayotolewa na wadau hao na kuahidi kushughulikia changamoto zinazoikabili NCC ikiwemo za takwimu ili kuhakikisha sekta hiyo inaendelea kukua kwa kuwa ni sekta mtambuko.
Sekta ya Ujenzi ni mojawapo ya sekta zinazokua kwa kasi hapa nchini na ina mchango mkubwa kwa Pato la Taifa ambapo mwaka 2016 sekta hiyo ilichangia asilimia 14 ya Pato la Taifa.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano