Tuesday, September 12

JPM AMJULIA HALI MEJA JENERALI MSTAAFU MRITABA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 12 Septemba, 2017 ametembelea hospitali ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ) Lugalo, Jijini Dar es Salaam na kumjulia hali Meja Jen. Mstaafu Vincent Mribata aliyelazwa hospitalini hapo baada ya kushambuliwa na watu wenye silaha wakati akiingia nyumbani kwake Ununio, Kinondoni Jijini Dar es Salaam.

Meja Jen. Mstaafu Mritaba alishambuliwa kwa risasi jana tarehe 11 Septemba, 2017 majira ya mchana na kisha kukimbizwa katika hospitali ya Jeshi Lugalo kwa matibabu.

Mkuu wa kituo cha tiba cha hospitali hiyo na daktari bingwa wa magonjwa ya moyo Brigedia Jenerali Paul Massawe amemueleza Mhe. Rais Magufuli kuwa Meja Jen. Mstaafu Vincent Mritaba anaendelea vizuri baada ya madaktari kufanikiwa kutoa risasi alizopigwa mkononi, kiunoni na tumboni.
Meja Jen. Mstaafu Mritaba amemshukuru Mhe. Rais Magufuli kwa kumjulia hali    na kumuombea dua ili apone haraka.

Mhe. Rais Magufuli aliyeongozana na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jen. Venance Mabeyo pia ametembelea wodi ya majeruhi na kuwajulia hali wagonjwa wanaotibiwa katika wodi hiyo na baadaye akawasalimu wananchi waliofika hospitali hapo kwa ajili ya kupata matibabu.
Mhe. Dkt. Magufuli amewapongeza Madaktari wa hospitali ya Jeshi Lugalo kwa huduma za matibabu wanazotoa kwa askari na wananchi wengine                           na amewahakikishia kuwa Serikali itaendelea kufanyia kazi changamoto mbalimbali zinazowakabili katika utekelezaji wa majukumu yao.



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli pamoja na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo (kushoto) na Brigedia Jenerali Dkt. Paul Massawe Meja  Jenerali Mstaafu Vicent Mritaba akielezea alivyoshambuliwa kwa  risasi mkononi, tumboni na mguuni  wakati akiingia  nyumbani kwake Ununio wilaya ya Kinondoni
jijini Dar es salaam.


 ais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli pamoja na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo (kushoto) wakioneshwa na Brigedia Jenerali Dkt. Paul Massawe Brigedia baadhi ya risasi  zilizotolewa kwenye mwili wa  Meja Jenerali Mstaafu Vicent Mritaba  baada ya kushambuliwa wakati akiingia  nyumbani kwake Ununio wilaya ya Kinondoni jijini Dar es salaam.



 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli pamoja na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo (kushoto) na Brigedia Jenerali Dkt. Paul Massawe,  Brigedia Jenerali Mstaafu Vicent Mritaba na wauguzi wakiomba dua wakiongozwa na Mama Margareth Vicent Mritaba hospitali ya Jeshi Lugalo jijini Dar es salaam alikolazwa Meja Jenerali Mritaba akitibiwa majeraha baada ya kushambuliwa kwa risasi mkononi, tumboni na kiunoni  wakati anaingia nyumbani kwake Ununio wilaya ya Kinondoni jijini Dar es salaam.



 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na mtoto Nathan Martin  wakati akitoka kumjulia hali Meja jenerali Mstaafu Vicent Mritaba aliyelazwa Hospitali ya Jeshi Lugalo jijini Dar es salaam alikolazwa akitibiwa majeraha baada ya kushambuliwa kwa risasi mkononi, tumboni na kiunoni  wakati anaingia nyumbani kwake Ununio wilaya ya Kinondoni jijini Dar es salaam.



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na Mwalimu  Aloys Konolipa wa Shule ya Msingi Kidugalo wilayani Kisarawe Mkoa wa Pwani alipopita kuwapa pole wagonjwa wengine baada ya kumjulia hali Meja  Jenerali Mstaafu Vicent Mritaba aliyelazwa Hospitali ya Jeshi Lugalo jijini Dar es salaam alikolazwa akitibiwa majeraha baada ya kushambuliwa kwa risasi mkononi, tumboni na kiunoni wakati akiingia nyumbani kwake Ununio wilaya ya Kinondoni. 
Picha na IKULU

SERIKALI: MATUMIZI YA DOLA NCHINI HAYAATHIRI KUSHUKA KWA THAMANI YA SHILINGI


Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), alipokuwa akijibu swali la msingi la Mbunge wa Vwawa Mhe. Japhet Hasunga (CCM)

Serikali imesema kuwa kushuka au kupanda kwa thamani ya shilingi nchini hakusababishwi na bidhaa na huduma mbalimbali kutozwa kwa dola bali kunatokana na misingi ya shughuli mbalimbali za kiuchumi (Macroeconomic fundamentals) pamoja na hali halisi ya uchumi wa nchi zinazofanya biashara na Tanzania. 

Hayo yameelezwa Bungeni mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), alipokuwa akijibu swali la msingi la Mbunge wa Vwawa Mhe. Japhet Hasunga (CCM), aliyetaka kujua mikakati ya Serikali katika kuimarisha thamani ya shilingi ya Tanzania na kupiga marufuku matumizi ya fedha za kigeni nchini. 

Akijibu swali hilo Dkt. Kijaji aliainisha kuwa nakisi ya urari wa biashara, mfumuko wa bei na tofauti ya misimu (seasonal factors) ni sababu kuu zinazosababisha kushuka na kupanda kwa thamani ya shilingi nchini.
Dkt. Kijaji aliliambia Bunge kuwa ili kuimarisha thamani ya shilingi Benki Kuu inaendelea kuthibiti mfumuko wa bei ili usitofautiane sana na wabia wa biashara nchini. 

“Benki Kuu imethibiti biashara ya maoteo (speculation) katika soko la fedha za kigeni ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kuwa miamala ya fedha za kigeni inafanywa na benki kwa ajili ya shughuli za kiuchumi tu na sio biashara ya maoteo, hali hii itasaidia upatikanaji wa fedha za kigeni katika soko la rejareja ili kupunguza shinikizo la kuporomoka kwa thamani ya shilingi.”Alisema Dkt Kijaji. 

Dkt. Kijaji alifafanua kuwa pamoja na hatua zinazochukuliwa na Benki Kuu ufumbuzi wa kudumu wa kutengamaa kwa thamani ya shilingi nchini hutegemea zaidi kupungua kwa nakisi ya urari wa biashara ya bidhaa, huduma na uhamisho wa mali nchi za nje. 
Imetolewa na: 

Benny Mwaipaja
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Fedha na Mipango

ZOEZI LA UCHUKUAJI WA LESENI ZA MACHAPISHO LAZIDI KUSHIKA KASI



 Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akimkabidhi Leseni ya Usajili wa machapisho mwakilishi wa Jarida la PLUS 255 MAGAZINE Bw. Francis Maduhu mara baada ya kukamilisha taratibu za usajili leo Jijini Dar es Salaam. Zoezi la utoaji wa Leseni kwa machapisho linafuatia utekelezaji wa kifungu namba 5(e) cha Sheria ya Huduma za Habari ya mwaka 2016. Kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi anayeshughulikia Usajili Bw. Patrick Kipangula.



 Mwakilishi wa Jarida la PLUS 255 MAGAZINE Bw. Francis Maduhu akionyesha Leseni ya machapisho aliyokabidhiwa kwa ajili ya Jarida lake leo Jijini Dar es Salaam. Zoezi la utoaji wa Leseni za machapisho linafuatia utekelezaji wa kifungu namba 5(e) cha Sheria ya Huduma za Habari ya mwaka 2016.



 Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akimpongeza mwakilishi wa Jarida la PLUS 255 MAGAZINE Bw. Francis Maduhu baada ya kumkabidhi Leseni ya Usajili wa machapisho kufuatia kukamilisha taratibu za usajili leo Jijini Dar es Salaam. Zoezi la utoaji wa Leseni za machapisho linafuatia utekelezaji wa kifungu namba 5(e) cha Sheria ya Huduma za Habari ya mwaka 2016. Kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi anayeshughulikia Usajili Bw. Patrick Kipangula.

Picha na: Idara ya Habari - MAELEZO

RC MAKONDA ATEMBELEA ENEO LILILOTENGWA KWA AJILI YA KUUZIA MAGARI (SHOW ROOM) LEO.


 .Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul Mkonda (kulia)akikagua eneo  lililotengwa kwa ajili ya kuuza magari (Show Room) kwa jiji Dar es Salaam   lililopo Kigamboni-Kisarawe leo jiijini Dar es Salaam, ambapo show room  zilizo katika sehemu mbalimbali zinatakiwa kwenda katika eneo hilo na hawatalipa kodi ya maeneo hayo ndani ya miaka mitatu.



 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul Mkonda akizungumza mara ya baada ya kukagua eneo la lililotengwa kwa ajili kuuzia magari Kigamboni –Kisarawe jijini Dar es Salaam.







Muonekano wa eneo hilo lililotengwa kwa ajili kuuzia magari Kigamboni –Kisarawe jijini Dar es Salaam.picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.

UNCDF YAISAIDIA ENSOL KUPELEKA UMEME VIJIJINI

Shirika la Umoja wa Mataifa la Mfuko wa Mitaji na Maendeleo (The United Nations Capital Development Fund-UNCDF), ikishirikiana na kampuni ya Ensol Tanzania Ltd. (Ensol) wamezindua mfumo wa umeme wa nishati ya jua katika kijiji cha Mpale kilichopo wilaya ya Korogwe, na hivyo kuwezesha umeme katika eneo hilo kwa mara ya kwanza. 

Mradi huo ulizinduliwa rasmi na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Dk. Juliana Pallangyo ambaye aliipongeza kampuni ya Ensol na washirika wake ikiwemo UNCDF kwa juhudi zake kubwa za ushawishi wa umeme hasa umeme mbadala wa jua ili kuboresha ustawi wa jamii na kukuza uchumi wa mtu binafsi na taifa. 

Dk. Pallangyo alisema kwamba serikali ya Tanzania inawashukuru watu wa Ensol kwa juhudi zao kubwa za kupeleka umeme vijijini. Alisema kwa Ensol kuweza kufikisha umeme katika maeneo ya ndani kabisa ya kijiji cha Mpale, kuwaunganisha wananchi na umeme wa saa 24 na wamefanikiwa kubadili maisha ya wananchi hao. Mkuu wa Wilaya ya Korogwe, Mhandishi Robert Gabriel (kushoto) akizungumza machache kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Dkt Juliana Pallangyo kuzindua rasmi mradi wa uzalishaji mdogo wa umeme wa 48KW kwa teknolojia ya nishati ya jua katika kijiji cha Mpale wilayani Korogwe, mkoa wa Tanga.

 Alitoa wito kwa jumuiya hiyo kutumia umeme sio kwa kuwasha taa pekee bali pia katika kusukuma mbele kazi za uzalishaji. Dk. Pallangyo alifurahishwa na kituo cha afya Mpale kuunganishwa na mfumo wa nishati ya jua na kuwataka maofisa wa wilaya kulipa Ankara zao kwa wakati ili kuhakikisha kwamba huduma zinapatikana bila kukoma kwa wananchi. 

Kijiji cha Mpale kipo katika maeneo ya milimani katika kata ya Mpale wilaya ya Korogwe mkoani Tanga. Kijiji chenye wakazi 9000 na nyumba 730, tangu kuanzishwa kwake mwaka 1972 hakijawahi kuwa na umeme. Wengi wa wanavijiji walikuwa wakitegemea mno mafuta ya taa ambayo kwa kiasi kikubwa yalikuwa si masafi kwa ajili ya kuwashia taa zao. Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Dkt. Juliana Pallangyo akitoa nasaha wakati wa uzinduzi rasmi wa mradi wa uzalishaji mdogo wa umeme wa 48KW kwa teknolojia ya nishati ya jua katika kijiji cha Mpale wilayani Korogwe, mkoa wa Tanga. Kulshoto ni Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mfuko wa Mitaji na Maendeleo (UNCDF), Peter Malika.

Mpaka sasa Ensol imeshaunganisha umeme kwa kaya 50. Aidha mpango unafanyika wa kutanua mradi ili ifikapo Juni 2018 nyumbna 250 ziwe zimeunganishwa. Mreadi huo wa kuunganisha wanakijiji na nishati inayozalishwa kwa nguvu za jua ulianza mwaka 2014 wakati Ensol walipozuru vijiji kadhaa vya mkoa wa Tanga kuangalia uwezekano wa kupata kijiji cha mfano na kubaini kuwapo kwa kijiji cha Mpale. 

“Ushirikiano wa UNCDF ulikuwa muhimu katika mradi huu gridi ndogo ya nishati ya jua. Pamoja na kwamba tulipokea fedha kutoka UNCDF na wadau wengine, UNCDF imekuwa ndio chombo cha kuingiza masuala ya kitaalamu na ushauri mwingine. Kushirikiana na UNCDF kumeongeza kuaminika miongoni mwa wadau na taasisi za kifedha,” anasema Prosper Magali, Meneja wa mradi wa Mpale.Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mfuko wa Mitaji na Maendeleo (UNCDF) nchini, Peter Malika akizungumza jambo wakati wa uzinduzi wa rasmi wa mradi wa uzalishaji mdogo wa umeme wa 48KW kwa teknolojia ya nishati ya jua katika kijiji cha Mpale, wilayani Korogwe mkoa wa Tanga.

Bw. Magali aliongeza, "Ninaamini kama si msaada wa UNCDF huu mradi usingekuwepo hapa ulipo. Tumepokea fedha kutoka EEP na wafadhili wengine. Lakini ni kwa sababu ya UNCDF tumeweza kupata fedha kutoka katika taasisi nyingine za ufadhili". Mkuu wa UNCDF Tanzania, Peter Malika alisema kwamba umeme ni chanzo cha maendeleo na kwamba sekta binafsi ina nafasi ya kusaidia serikali katika juhudi zake za kuangaza maeneo ya vijijini. 

“Kwa kuwezesha Mpale kuwa na umeme tunawasaidia wananchi wa kijiji hiki kufanya maendeleo ya kiuchumi. Fursa nyingi za kiuchumi zitaibuka, kituo cha afya kitaweza kuboresha huduma zake na wanafunzi watakuwa na muda zaidi wa kusoma.” Mkurugenzi Mtendaji wa Ensol Tanzania, Hamisi Mikate akielezea mchakato wa kufanikisha mradi huo ulivyoenda mpaka kukamilika wakati wa ufunguzi wa rasmi wa mradi wa uzalishaji mdogo wa umeme wa 48KW kwa teknolojia ya nishati ya jua katika kijiji cha Mpale wilayani Korogwe, mkoa wa Pwani.

Mafanikio ya mradi huo ni matokeo ya ushirikiano wa karibu kati ya serikali ya mitaa na wananchi wakati wote wa mchakato wa kufanikisha mradi. “Wananchi wamefarijika tangu kampuni ya Ensol itembelee kijiji hicho kwa mara ya kwanza na kuzungumza kuhusu uletaji wa umeme wa nishati ya jua. Tumekuwa na ushirikiano mkubwa tangu siku ya kwanza ambapo wamekuwa wakitushirikisha,” anasema Mwenyekiti wa kijiji Augustine Rugambwa. 

Bw.Rugambwa aliongeza: “Nimefurahishwa sana kwamba mradi huu umekuja wakati wa uongozi wangu. Ni nafasi adimu ambayo nitaikumbuka maisha yangu yote. Tunawashukuru sana UNCDF kwa kutukumbuka hata sisi tuliopembezoni. Kupitia Ensol tutaingiza nishati ya umeme majumbani mwetu. UNCDF tunawashukuru kwa msaada wenu huu. Kamwe hatutawasahau.” Mkurugenzi wa Miradi wa Ensol na Meneja wa Mradi wa Umeme Mpale, Prosper Magari akizungumza jambo na kutoa shukrani kwa UNCDF kwa kuwezesha kufanikisha mradi huo wakati wa uzinduzi rasmi wa mradi wa uzalishaji mdogo wa umeme wa 48KW kwa teknolojia ya nishati ya jua katika kijiji cha Mpale, wilayani Korogwe, mkoa wa Tanga.

“Tunaamini kwa msaada tulioupata kutoka UNCDF na wengine, mradi huu utakuwa endelevu na utakaokuwa unatengeneza faida kwani wateja watakuwa wanalipa Ankara zao kila mwezi. Kwa hiyo fedha zitakazopatikana zitatumika kuufanya mradi kuwa endelevu,” alisema Prosper. “Tunatumia mradi kama huu kama mafunzo. 

Lengo letu ni kuwa na miradi mingine kama hii 15 katika kipindi cha miaka mitano ijayo. Tumetembelea maeneo ya nyanda za juu Kusini kuona vijiji vinavyoweza kupatiwa mradi wa umeme wa jua. Tumekubaliana na serikali za mikoa na tawala za mitaa kuwapeleka nishati ya umeme jua na tunatarajia kuwaunganisha na watu nyumba elfu kumi. 

Kuna vijiji vingi kama hiki cha Mpale vinavyohitaji umeme, kwa hiyo fursa za umemejua ni kubwa sana!” aliongeza Prosper. Bw Malika alisema kwamba UNCDF itaendelea kufanyakazi kwa karibu na Ensol na taasisi nyingine za umma na binafsi kuwezesha kufikisha umeme katika maeneo yanayofikika wka shida nchini Tanzania. Mwenyekiti wa kijiji cha Mpale, Augustine Rugambwa akisoma risala fupi kwa mgeni rasmi (hayupo pichani) wakati wa uzinduzi wa rasmi wa mradi wa uzalishaji mdogo wa umeme wa 48KW kwa teknolojia ya nishati ya jua katika kijiji cha Mpale uliofanyika mwishoni mwa juma wilayani Korogwe, mkoa wa Tanga.Kikundi cha utamaduni Mpale, Millongwe wakitoa burudani wakati wa uzinduzi rasmi wa mradi wa uzalishaji mdogo wa umeme wa 48KW kwa teknolojia ya nishati ya jua katika kijiji cha Mpale, wilayani Korogwe, mkoani Tanga.Mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Dkt. Juliana Pallangyo (katikati) akishiriki kucheza ngoma ya 'Mdumange' ya kabila la Wasambaa wakati wa hafla ya uzinduzi rasmi wa mradi wa uzalishaji mdogo wa umeme wa 48KW kwa teknolojia ya nishati ya jua katika kijiji cha Mpale, wilayani Korogwe mkoa wa Pwani.Mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Dkt. Juliana Pallangyo akifunua kitambaa kuzindia rasmi mradi wa uzalishaji mdogo wa umeme wa 48KW kwa teknolojia ya nishati ya jua katika kijiji cha Mpale wilayani Korogwe, mkoa wa Tanga ambao utasaidia wananchi kuondokana na changamoto ya upatikanaji wa huduma hiyo muhimu. Kushoto ni Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mfuko wa Mitaji na Maendeleo (UNCDF), Peter Malika.Mgeni rasmi na meza kuu wakitazama wakisoma maneno yaliyoaandikwa kwenye kibao hicho baada ya kuzinduliwa rasmi.Mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Dkt. Juliana Pallangyo katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali waliohudhiria uzinduzi rasmi mradi wa uzalishaji mdogo wa umeme wa 48KW kwa teknolojia ya nishati ya jua katika kijiji cha Mpale wilayani Korogwe, mkoa wa Tanga.Mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Dkt. Juliana Pallangyo akibadilishana mawazo na Mkuu wa wilaya ya Korogwe, Mhandisi Robert Gabriel (kushoto) na Mkurugenzi wa Miradi wa Ensol na Meneja wa Mradi wa Umeme Mpale, Prosper Magari katika chumba maalum cha kusambazia umeme katika kijiji cha Mpale mara kuzindua rasmi mradi huo.Muonekano wa ndani wa mitambo ya kusambazia umeme kwenye kijiji cha Mpale.Mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Dkt. Juliana Pallangyo akitembelea chumba cha betri za solar zinazosambaza umeme katika kijiji hicho.Jenereta la akiba linaloweza kuhudumia kijiji cha Mpale endapo kutatokea hitilafu yoyote.Mmoja wa wageni walioshiriki uzinduzi huo akipata huduma ya kunyoa ndevu baada mradi huo wa umeme wa nishati ya jua kuzinduliwa rasmi katika kijiji cha Mpale, wilayani Korogwe, mkoa wa Tanga.Pichani juu na chini ni sehemu ya viongozi mbalimbali wa serikali, wananchi wa kijiji cha Mpale, wafanyakazi wa ENSOL na UNCDF waliohudhuria uzinduzi rasmi mradi wa uzalishaji mdogo wa umeme wa 48KW kwa teknolojia ya nishati ya jua katika kijiji cha Mpale wilayani Korogwe, mkoa wa Tanga.Jengo la mradi wa uzalishaji mdogo wa umeme wa 48KW kwa teknolojia ya nishati ya jua katika kijiji cha Mpale wilayani Korogwe, mkoa wa Tanga.

MWANRI AMTEUA MKUU WA WILAYA YA TABORA KUONGOZA UKAGUZI WA VIWANDA


MKUU wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri ameteua Mkuu wa Wilaya ya Tabora, Queen Mlozi kuongoza Kamati aliyoichagua kwa ajili ya kufuatilia viwanda mbalimbali ili kuangalia hali halisi na kama vimeshindwa kufanyakazi viweze kupewa Wawekezaji wengine. Mwanri aliteua Kamati hiyo jana mjini Tabora wakati wa Mkutano na wadau mbalimbali na Mmiliki wa Kiwanda cha Nyuzi cha Tabora.

Wengine waliochaguliwa ni Katibu Tawala Msaidizi wa Mkoa wa Tabora Dkt. Philipo Ntiba, Afisa Biashara Mkoa Lucas Kusare ambaye ni Katibu wa Kamati, Mwanasheria wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Richard Lugomela na Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano Serikalini, Tiganya Vincent.

Alisema kuwa Kamati hiyo itaanza na Kiwanda cha Nyuzi Tabora ambapo itaangalia mpango kazi wake , itakagua mashine zote kama zinafanyakazi na uwezo wa kifedha wa mwekezaji huyo kama anao mtaji wa kutosha wa kuendesha kiwanda.

Mambo mengine yatakayofuatiliwa na Kamati hiyo ni pamoja na kuangalia matatizo ambayo Mwekezaji huyo aliyaeleza kuwa ukosefu wa soko la nyuzi zake kutokana na viwanda ambavyo ndio vilikuwa vikinunua kwake kuanza kuagiza toka nje bidhaa hizo.

Mkuu huyo Mkoa aliongeza kuwa mambo mengine ambayo Kamati itayafanya ni kuangalia fursa za masoko ya bidhaa za Kiwanda hicho kama vile Bohari Kuu za Dawa (MSD), Chama Kikuu cha Ushirika wa Wakulima wa Tumbaku Kanda ya Magharibi (WETCU) na wafanyabiashara wengine wanaweza kununua bidhaa zake.
Alisema kuwa Kamati hiyo itatakiwa kila baada ya siku tatu impelekee taarifa ya maendeleo ya kazi yao.

Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa Mkoa ametoa mwezi mmoja kwa Mmiliki wa Kiwanda cha Nyuzi Tabora kuhakikisha mashine zake zinafanyakazi.

Alisema kuwa baada ya kipindi kuisha atakwenda kukagua na akikuta hakuna kitu atalazimika kumuomba Waziri wa Viwanda aje kuchukua hatua ikiwemo kumpa mwekezaji mwingine.

Mkuu huyo Mkoa alisema kuwa hata kama mali ghafi kwa sasa hivi hakuna anataka ni kujiridhisha kuwa mashine zote ni zima wakati akiwa anasubiri msimu wa pamba ujao ili apate mali ghafi.

Mkuu wa Mkoa wa Tabora yuko katika zoezi la kuhakiki viwanda vyote ili kujiridhisha kama vinafanyakazi na vile ambavyo wamiliki wake wameshindwa waweze kuvirudisha Serikalini

SANAA MASHULENI

SHINDANO LA SANAA KWA WANAFUNZI WA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI ZA MIKOA YA UKANDA WA PWANI BARA NA VISIWANI: WITO WA KUWASILISHA KAZI ZA UBUNIFU WA SANAA

Chama cha Wanayansi wa Elimu Bahari ukanda wa Magharibi mwa Bahari ya Hindi (WIOMSA) kwa ushirikiano kati ya WIOMSA, Taasisi ya Sayansi Bahari (IMS) na Idara ya Sayansi Akua na Teknolojia ya Uvuvi (DASF) zote kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania (TAFIRI) na Mkataba wa Kimataifa wa Uhifadhi, Usimamizi na Uendelezaji wa Mazingira ya Bahari na ya Ukanda wa Pwani wa Magharibi mwa Bahari ya Hindi (Mkataba wa Nairobi), kinaandaa Kongamano la 10 la Kisayansi. 

Kongamano hilo litafanyika kuanzia tarehe 30 Oktoba hadi tarehe 4 Novemba katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere ulioko Dar es Salaam, Tanzania.

Katika Kongamano hili la 10 kutakuwa na mashindano ya kazi za sanaa kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari za mikoa ya ukanda wa pwani wa Bahari ya Hindi. Kwa upande wa Tanzania Bara itahusisha mikoa ya Tanga, Pwani, Dar es Salaam, Lindi na Mtwara na kwa Zanzibar itahusisha shule zilizopo Unguja na Pemba. Dhamira ya mashindano hayo ni: “Umuhimu wa Mazingira ya Pwani na Bahari kwa Tanzania”. 

Bahari ni muhimu sana kwa jamii zetu na kwa ustawi wa maisha yako. Kwa hiyo tumia mawazo yako, ubunifu wako na maarifa uliyo nayo katika kuwasaidia wengine waelewe mawazo yako kuhusiana na umuhimu wa mazingira ya ukanda wa pwani na ya bahari kupitia kazi yako ya sanaa. Chora, paka rangi, tumia program za kompyuta za uchoraji au eleza mawazo yako hayo kwa kutunga wimbo.
Wanafunzi watumie ubunifu wao wenyewe kueleza maoni yao juu ya dhamira husika. Uwasilishaji wa ubunifu huo unaweza kufanyika kwa njia zifuatazo: michoro (zikiwemo katuni/vibonzo) au utunzi wa nyimbo.

Kazi zote za sanaa ziwasilishwe kabla ya tarehe 30 Septemba 2017 kwa njia ya mtandao ambao ni http://symposium.wiomsa.org/art-competition/

Kwa maelezo zaidi juu ya vigezo na masharti ya kushiriki na mfumo wa uwasilishaji wa sanaa, pakua tangazo kamili la shindano hili kwa kubofya link hii chini: