Saturday, September 30

MAGONJWA YA MOYO HUUA WATU MILIONI 17 DUNIANI – DK. SANGA


Na.Paschal Dotto-MAELEZO

SERIKALI ya Awamu ya Tano kupitia Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), imewashauri wananchi kujenga utamaduni wa kupima afya mara kwa mara ili kuweza kugundulika mapema iwapo wanasumbuliwa na magonjwa mbalimbali.

Hayo yamesemwa na Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo wa Taasisi hiyo, Tulizo Sanga alipozungumza na waandishi wa habari wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Moyo Duniani yaliyofanyika katika viwanja vya Taasisi hiyo jijini Dar es Salaam.

Dk Sanga alisema tafiti zinaonesha zaidi ya watu milioni 17 hupoteza maisha kutokana na kuugua magonjwa ya moyo kila mwaka duniani.“Ni magonjwa ambayo husababisha vifo vya watu wengi duniani huku hali ikionekana kuwa mbaya zaidi katika nchi zinazoendelea,” alisema Dk Sanga.

Alisema tafiti zinaonesha pia zaidi ya watu milioni 75 huugua magonjwa hayo kila mwaka duniani.“Tanzania bado hatujafanya utafiti wa kina lakini tangu Taasisi hii imeanza kufanya kazi tunaona zaidi ya wagonjwa 300 kwa siku na wengi huja wakiwa katika hatua mbaya ya ugonjwa,” alisema.

Alisema tangu Septemba 25 hadi 29, mwaka huu madaktari wa JKCI wamewafanyia upasuaji wagonjwa 28 kwa kushirikiana wenzao wa Taasisi ya Madaktari Afrika ikiwa ni sehemu ya maadhimisho hayo.Kwa upande wake, Mtaalamu wa lishe wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), Louiza Shem alisema mfumo mbovu wa maisha hasa ulaji usiofaa na kutokufanya mazoezi kunachangia wengi kupata magonjwa ya moyo.

“Kwa bahati nzuri hamna chakula ambacho mtu hatakiwi kutumia ili kujiepusha na magonjwa ya moyo, huwa tunashauri jinsi gani na kwa kiasi gani uvitumie ili kuepuka kupata magonjwa haya,” alisema.

Mtaalamu huyo alitoa mfano “Kuna vyakula vya wanga kama vile wali, ugali na vinginevyo, unakuta mtu anakula… amejaza sahani.“Unapaswa kula kulingana na aina ya kazi unayofanya, kwa mfano wengi ambao tunafanya kazi ofisini hatutumii nguvu nyingi kulinganisha na wale wanaobeba mizigo, wengi tunakula nyama kwa kiwango kikubwa, ni vema kupunguza kiasi.

“Mafuta yanayopatikana kwenye nyama zinaongeza uzito kupita kiasi na huenda kuziba mishipa ya damu, ikiwa ni ya kichwani utapooza mwili na ikiwa ni kwenye moyo utapata ‘heart attack’,” alibainisha.Alishauri pia jamii kupunguza kiwango cha chumvi kwani inapotumika kwa kiwango kikubwa huathiri afya ya moyo.

“Kundi kubwa tunaloona linaathirika na magonjwa haya ni wale waliopo kwenye umri wa uzalishaji na umri unavyozidi kuongezeka ndivyo uwezekano wa mtu kupata ugonjwa huu unavyoongezeka,” alisema.

MANISPAA YA DODOMA YAANZA KUANDAA HATI MILIKI ZA ARDHI ZA MIAKA 99 KWA KASI, BARAZA LA MADIWANI LAPONGEZA



HALMASHAURI ya Manispaa ya Dodoma imekamilisha uandaaji wa hati 912 za umiliki wa ardhi za miaka 99 kama ilivyoagizwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta John Magufuli Mei 15 mwaka huu wakati akitoa tamko la kuivunja iliyokuwa Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu Dodoma (CDA) na shughuli zote kuhamishiwa katika Manispaa ya Dodoma. 

Akizungumza katika kikao cha dharura cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri hiyo kilichopokea taarifa rasmi ya makabidhiano ya majukumu ya iliyokuwa CDA kuhamia Manispaa ya Dodoma jana, Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Godwin Kunambi aliwaambia Madiwani na wananchi kwa ujumla waliohudhuria Baraza hilo kuwa, hatua hiyo imefikiwa katika kipindi cha miezi miwili ya Julai na Agosti, huku akiahidi kuwa,Manispaa hiyo itaendelea kutoa huduma hiyo na nyingine kwa kasi inayoendana na matarajio ya wananchi. 

Alisema kati ya hati hizo, hati 674 zilizowasilishwa kwa Kamishna Msaidizi wa Ardhi wa Wizara ya Ardhi zimeshasajiliwa na zipo tayari kwa ajili ya kukabidhiwa kwa wananchi husika, huku hati 238 zikiwa katika hatua ya kukaguliwa ili zisainiwe. 

Alifafaua zaidi kuwa, uandaaji huo wa hati unaenda sambamba na utoaji wa vibali vya ujenzi kwa haraka, ambapo mchakato wa kutoa kibali cha ujenzi unakamilishwa ndani ya siku saba tu baada ya maombi kupokelewa mpaka muombaji anakabidhiwa kibali chake. 

Kufuatia taarifa hiyo, wajumbe wa Baraza la Madiwani wakiongozwa na Meya wa Manispaa ya Dodoma Mstahiki Profesa Davis Mwamfupe wameipongeza Menejimenti ya Halmashauri na watumishi wote na kuwataka waendelee na juhudi hizo ili pamoja na mambo mengine kuufanya mji wa Dodoma ukue kwa kasi kwa kuwawezesha wananchi na wadau wengine kujenga. 
Mkurugenzi wa wa Manispaa ya Dodoma Godwin Kunambi (kulia) ambaye pia ni Katibu wa Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma Godwin Kunambi akizungumza wakati wa Baraza la Madiwani la Mnispaa hiyo.

UTIAJI SAINI WA MKATABA WA UJENZI WA MRADI WA RELI YA KISASA


  Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hodhi ya Rasilimali za Reli (RAHCO) Masanja Kadogosa (kulia) na pamoja na Mjumbe wa Bodi  kutoka Kampuni ya Ukandarasi ya Yapi Merkezi Insaat ya nchini Uturuki wakisaini Mkataba wa ujenzi wa mradi wa Reli ya Kisasa kutoka Morogoro- Makutopora (Dodoma). Halfa hiyo ilifanyika leo Septemba 29, 2017.
  Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hodhi ya Rasilimali za Reli (RAHCO) Masanja Kadogosa (kulia) na pamoja na Mjumbe wa Bodi  kutoka Kampuni ya Ukandarasi ya Yapi Merkezi Insaat ya nchini Uturuki wakibadilishana Mkataba wa ujenzi wa mradi wa Reli ya Kisasa kutoka Morogoro- Makutopora (Dodoma). Halfa hiyo ilifanyika leo Septemba 29, 2017.
   Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hodhi ya Rasilimali za Reli (RAHCO) Masanja Kadogosa (kulia) na pamoja na Mjumbe wa Bodi  kutoka Kampuni ya Ukandarasi ya Yapi Merkezi Insaat ya nchini Uturuki wakionyesha kwa waandishi wa habari  Mkataba wa ujenzi wa mradi wa Reli ya Kisasa kutoka Morogoro- Makutopora (Dodoma). Halfa hiyo ilifanyika leo Septemba 29, 2017.
     Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hodhi ya Rasilimali za Reli (RAHCO) Masanja Kadogosa akizungumza katika hafla ya utiaji saini wa mkataba wa mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa kutoka Morogoro- Makutopora (Dodoma). Halfa hiyo ilifanyika leo Septemba 29, 2017.
   Mwenyekiti wa Kamati ya Bajeti ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hawa Ghasia akizungumza katika hafla ya utiaji saini wa mkataba wa mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa kutoka Morogoro- Makutopora (Dodoma). Halfa hiyo ilifanyika leo Septemba 29, 2017.
   Baadhi ya Wahandisi kutoka kampuni ya Ukandarasi ya Yapi Merkezi Insaat ya nchini Uturuki wakifuatilia hafla ya utiaji saini saini wa mkataba wa mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa kutoka Morogoro- Makutopora (Dodoma). Halfa hiyo ilifanyika leo Septemba 29, 2017.
   Baadhi ya Wafanyakazi kutoka shirika la Reli Nchini (TRL) na kampuni hodhi ya Rasilimali za Reli (RAHCO) wakifuatilia hafla ya utiaji saini saini wa mkataba wa mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa kutoka Morogoro- Makutopora (Dodoma). Halfa hiyo ilifanyika leo Septemba 29, 2017.

   Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Uchukuzi) Dkt. Leonard Chamuriho akizungumza akizungumza katika hafla ya utiaji saini wa mkataba wa mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa kutoka Morogoro- Makutopora (Dodoma). Halfa hiyo ilifanyika leo Septemba 29, 2017.
  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa akibadilishana mawazo na Mjumbe wa Bodi ya Kampuni ya Ukandarasi ya Yapi Merkezi Insaat ya nchini Uturuki, Erdem Ariogl  pamoja na Kaimu Balozi wa nchini hiyo Yunus Belet wakati wa utiaji saini wa mkataba wa mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa kutoka Morogoro- Makutopora (Dodoma). Halfa hiyo ilifanyika leo Septemba 29, 2017.
1.    Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa akizungumza katika hafla ya utiaji saini wa mkataba wa mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa kutoka Morogoro- Makutopora (Dodoma). Halfa hiyo ilifanyika leo Septemba 29, 2017.(PICHA NA MAELEZO)

VIWANDA MOROGORO VYA PONGEZWA KWA KUNUSURU UHARIBIFU WA MAZINGIRA


 Katikati Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na mazingira Mhe. Luhaga Mpina, Mbele yake ni Bw. George Mratibu wa Kiwanda cha Ngozi Morogoro , cha ACE LATHER TANZANIA LTD, wakiwa katika ukaguzi wa mtambo wa kisasa wa kutibu majitaka kiwandani hapo ambapo Mpina yupo Mkoani Morogoro katika ziara ya ukaguzi wa utekelezaji wa Sheria ya Mazingira na kanuni zake, kufuatia maagizo aliyoatoa awali katika ziara ya viwanda hivyo.

 Kushoto kaimu mkurugenzi wa mamlaka ya maji safi na maji Taka mjini Mororgoro, inginia Halima Mbiru, akimuonyesha Naibu Waziri Mpina Mpaka wa mabwawa ya maji taka mali ya mamlaka hiyo, hayapo katika picha. Mhe. Mpina alifanya ziara ya ukaguzi wa mabwawa hayo mapema leo.
 Katika picha ni washiriki katika ziara ya Naibu Waziri Mpina alipokagua Mabwawa ya majitaka kama yanavyoonekana katika picha.
Kushoto, Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina kulia ni Mwenyeji wake  Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt Kebwe Steven Kebwe katika kikao kabla ya kuanza ziara ya ukaguzi wa viwanda Mkoani hum oleo. (Picha na Evelyn Mkokoi)

Tanzania yakabidhiwa mashine ya kutoa dawa ya usingizi wakati wa upasuaji.


 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii , Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akisisitiza jambo wakati wa hafla ya kupokea msaada wa mashine ya kutoa dawa za usingizi zilizotolewa na Muungano wa Utepe Mweupe Tanzania (WRATZ). Mashine hiyo yenye thamani ya Sh. Mil.55 imetolewa na Kampuni ya Kas Medics Limited ikiwa ni matokeo ya uhamasishaji wa kupunguza vifo vya wakina mama na watoto leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo (Idara kuu ya Afya) Dkt. Mpoki Ulisubisya na  Mratibu wa Taifa wa Muungano wa Utepe Mweupe wa Uzazi Salama (WRATZ) Rose  Mlay. 
Mratibu wa Taifa wa Muungano wa Utepe Mweupe wa Uzazi Salama (WRATZ) Rose  Mlay akielezea jambo wakati wa hafla ya kukabidhi msaada wa mashine ya kutoa dawa za usingizi iliyotolewa na Muungano wa Utepe Mweupe Tanzania (WRATZ). Mashine hiyo yenye thamani ya Sh. Mil.55 imetolewa na Kampuni ya Kas Medics Limited ikiwa ni matokeo ya uhamasishaji wa kupunguza vifo vya wakina mama na watoto leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Waziri wa Afya, Jamii , Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii , Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akisalimiana na Mkurugenzi wa Kampuni ya Kas Medics Limited Nishitha Kulshreshtha  mara baada ya kukabidhiwa kukabidhiwa msaada wa mashine ya kutoa dawa za usingizi iliyotolewa na Muungano wa Utepe Mweupe Tanzania (WRATZ) kufuatia udhamini wa kampuni hiyo leo Jijini Dar es Salaam. Mashine hiyo yenye thamani ya Sh. Mil.55 ni matokeo ya uhamasishaji wa kupunguza vifo vya wakina mama na watoto leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo (Idara kuu ya Afya) Dkt. Mpoki Ulisubisya.

 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii , Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akipata maelezo kuhusu namna mashine ya kutolea dawa za usingizi inavyofanya kazi wakati wa hafla ya kukabidhiwa msaada wa mashine hiyo iliyotolewa na Muungano wa Utepe Mweupe Tanzania (WRATZ) leo Jijini Dar es Salaam. Mashine hiyo yenye thamani ya Sh. Mil.55 imetolewa na Kampuni ya Kas Medics Limited ikiwa ni matokeo ya uhamasishaji wa kupunguza vifo vya wakina mama na watoto leo Jijini Dar es Salaam.

Na.Paschal Dotto-MAELEZO.

Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imekabidhiwa mashine maalumu ya kutoa dawa za usingizi kwa mama wajawazito wenye uzazi pingamizi wakati wa upasuaji kwaajili ya kuokoa maisha yao.

Akizungumza katika makabidhiano hayo leo Jijini Dar es Salaam Waziri mwenye dhamana ya Afya Mh.Ummy Mwalimu alisema kuwa, hiyo ni hatua kubwa katika kupambana na vifo vya wakina mama wajawazito pamoja na watoto wachanga.

Waziri Ummy alitoa pongezi kwa watu waliojitolea kupanda mlima Kilimanjaro kwa ajili ya kuunga mkono kampeni ya kuokoa maisha ya mama na mtoto wakiongozwa na Dkt.Ahmed Mohamed Makuwani, ambapo alisema kuwa waliopanda mlima Kilimanjaro wamewezesha kupatikana kwa msaada wa mashine hiyo, hivyo akawashukuru na kuomba wadau wengine kuiga mfano huo.

“Tunawashukuru Utepe Mweupe wa Uzazi Salama kwa kazi kubwa na nzuri wanayoifanya katika kushirikiana na serikali ili kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi na vifo kwa watoto wachanga, hatua hii inatufariji sana na naomba watanzania na wasio watanzania wenye mapenzi mema na afya ya mama na mtoto kuendelea kusaidia juhudi hizi ”, alisema Waziri Ummy.

Akieleza mafanikio katika sekta ya Afya waziri Ummy alisema kuwa kuna zaidi ya vituo vya afya 480 nchi nzima na kati ya hivyo vituo 109 vinavyumba vya upasuaji ambayo ni sawa na asilimia 20 huku akibainisha kuwa kufikia Juni, 2018 serikali inatarajia kujenga vyumba vya upasuaji 170 vitakavyosaidia upasuaji wa mama wenye uzazi pingamizi na idadi hiyo itaongezeka na kufikia vituo 279.

Aidha Waziri Ummy alisema kuwa licha ya kujenga vyumba hivyo watahakikisha upatikanaji wa vifaa, ujenzi wa maabara kubwa, wodi za kinamama pamoja na nyumba moja ya mtumishi katika vituo vya afya vyenye vyumba vya upasuaji.

Kutokana na mpango mkakati wa kupambana na vifo vya wajawazito na watoto wachanga Serikali inatarajia kufikia asilimia 50 mpaka asilimia 80 ifikapo mwaka 2020 ambayo ni kampeni ya Serikali ya Awamu ya Tano inayotarajia kuzinduliwa hivi karibuni ijulikanayo kama ‘Jiongeze Tukuvushe salama’ kampeni ambayo inalenga kuwasaidia wakina mama wajawazito popote walipo ili kuokoa maisha yao.

Naye Mratibu wa Utepe Mweupe Dkt. Rose Mlay alisema kuwa mashine hiyo ni maalum katika kunusuru maisha ya mama na mtoto lakini pia inaweza kutumika kwa mtu yeyote mwenye matatizo ya kufanyiwa upasuaji.

Kwa upande wake katibu mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya alisema mashine hiyo iliyotolewa na shirika la the Guardian Health yenye themani ya Shilingi milioni 55 ina ubora na kiwango cha kutosha katika kutoa huduma kwa mgonjwa wakati wa upasuaji.

“Mashine hii ni ya kipekee kwa sababu ina uwezo wa kutengeneza oksijeni na haihitaji mitungi ya gesi kwa hiyo ni mashine nzuri kwa wagonjwa na akinamama wenye uzazi pingamizi”, alisema Dkt.Mpoki.

Dkt. Mpoki alisema kilichopo sasa ni kufundisha wataalam watakaohusika na matumizi ya mashine hiyo ili waweze kuitumia ipasavyo na kuahidi kuwa atahakikisha inatunzwa ili iweze kudumu kwa muda mrefu. 

BETTER HEALTH, WATER AND FOOD FOR TANZANIA WITH THE HELP OF NUCLEAR TECHNOLOGIES AND INTERNATIONAL PARTNERS


Science and technological innovations play a fundamental role in assisting African leaders to root causes of poverty, hunger and climate change. 

It is therefore no surprise that nuclear science and innovative nuclear technologies are playing a major role in providing viable solutions to help achieve these targets. It is well known globally that nuclear technologies have much to offer in the fight against poverty, hunger, dread diseases, and water shortages, not to mention its ability to provide sustainable and environmentally friendly electricity. 


Let’s take a closer look these various applications.

Nuclear medicine helps millions of people across the globe to successfully fight cancer and has reducedthe mortality rate of non-communicable diseases by one third. Moreover, nuclear science centers and research facilities are indispensable in the production of radioisotopes which are used in complex medical treatments. African countries have already made significant steps in nuclear science development under the guidance of the United Nation’s International Atomic Energy Authority (IAEA) and its key member states.

For example, in Zambia “people can access treatment locally for a fraction of the cost they would pay by travelling outside the country. More than 17,000 new cases of cancer have been diagnosed and treated over the last 10 years,” said MulapeKanduza, Chief medical physicist of the Cancer Diseases Hospital (CDH) in Lusaka.“Without the assistance of the IAEA, it would have been very difficult for us to set up a highly technical centre like this one and care for so many patients,” said Dr Lewis Banda, the CDH’s Senior Medical Superintendent.

IAEA provides training and seminars to improve cancer management across the globe.With the help of nuclear technologies Tanzanian doctors can now deliver more precise radiation treatment to patients with oncological diseases using modern scanning methods previously not available in the region. These new methods make it possible to treat more patients than before with more accuracy.

“We now have the skills to more fully understand the extent of a tumour and ultimately plan better and more precise treatment for our patients,” said Dr Mark Mseti, a radiation oncologist at the Ocean Road Cancer Institute in Dar es Salaam, which receives technical support and equipment through the IAEA. Previously, DrMseti participated in IAEA training on 3D planning for target volume definition and contouring for radiotherapy.

Another issue is water supply. As the population continues to grow rapidly in emerging countries, the availability of potable water remains one of the most pressing issues for the mankind. Innovativenuclear technologies can be used to desalinate ocean wateror to reducecontaminants in contaminated water, making it safe to use.

Water purification and desalination can be of huge benefit to Tanzania, where it is difficult for many people in arid regions to access clean water. Implementation of these technologies is of high importance for the East African country where nearly 23 million people don’t have full access to safe potable water. 

And there is a huge issue of food supply. For decades African nations have suffered the devastating consequences caused by the tsetse fly. According to the United Nations (UN) Food and Agriculture Organization the bloodsucking insect kills more than three million head of livestock in sub-Saharan Africa every year, resulting in more than US $4 billion in losses in region. With the help of nuclear technologies Tanzanian island of Zanzibar have already won the battle against the tsetse fly thanks to the nuclear based sterile insect technique (SIT).

Since the eradication of the tsetse fly in 2014 socio-economic studies have shown that the total number of all cattle breeds have increase by roughly 38%.Milk production has nearly doubled from 4.6 to 10 liters after the introduction of nuclear based techniques. Radiation has proved to be an effective solution for the eradication of many infectious insects on almost every continent on Earth. SIT has been applied to hundreds of species of fruit flies, moths, mosquitoes and screwworm flies.

And neighboring Zambia has drastically increased its maize and other crop varieties productivity using nuclear techniques to make them more resistant to external factors. Moreover, nuclear technologies not only made it possible to increase crop productivity but at the same time reduced negative environmental effects of other agricultural practices. Now Zambian farmers enjoy better harvests despite previous downfalls due to climate change and severe droughts.

It is worth noting that Zambia is well on the way of building its own multipurpose nuclear scientific center with the help of foreign partners like IAEA and Russian nuclear corporation Rosatom.Viktor Polikarpov, Rosatom Regional Vice President for Sub-Saharan Africa, notes: “Radiation treatment of food products is one of the various applications of the state-of-the-art radiation technologies offered by Rosatom to its foreign partners. Today about 515 radiation facilities created with the use of Russian technologies are in operation in 22 countries worldwide, including the UK, France, Germany, Finland, Japan, China, South Korea and India”.

DC WA KAKONKO KANALI NDAGALA APIGA MARUFUKU UNYANYASAJI KWA WAZEE,KUWATUHUMU WANAZUIA MVUA



MKUU wa Wilaya ya Kakonko Kanali Hosea Ndagala amewaagiza Wananchi wa Wilaya ya Kakonko kuacha tabia ya kuwatuhumu baadhi ya wazee kuwa Wanazuia Mvua na kutaka kuwaondoa ikiwa ni pamoja na kuwauwa kwa kwa imani za kishirikina , na vikundi vitakavyo gundulika vinawatuhumu watachukuliwa hatua ili kukomesha vitendo hivyo.

Akizungumza na Wananchi jana katika maadhimisho ya siku yaWazee Wilayani humo katika kijiji cha Kasanda ,Ndagala alisema kumekuwa na tabia ya Wananchi wengi kuwatuhumu baadhi ya wazee kuwa wanazuia mvua, jambo ambalo ni imani za kizamani na zilizopitwa na wakati.
 
 "Kwa hiyo mimi nawaomba tuendelee kushirikiana na wazee wetu hawa kwa kuwa pia wana mchango wao mkubwa katika jamii,ni vyema tukawafanya wazee wetu waishi kwa amani na kuachana na imani hizo zinazoweza kuleta chuki na uhasama mkubwa baina yetu",alisema Ndagala.

Alisema vitendo kama hivyo vilijitokeza mwaka jana, baadhi ya wazee walitaka kuuwawa kwa tuhuma hizo,aliema na kuongeza kuwa imani hizo zinapaswa kupuuzwa kwani zinaweza kuchochea uvunjifu wa amani Kwa Wazee hao ambao ni hadhina kubwa kwa jamii. 
 
"Niwaombe wananchi mshirikiane na Wazee waliopo katika maeneo yenu, tumeona mchango wao ni mkubwa sana katika jamii na Taifa kwa ujumla Kauli mbiu ya maadhimisho ya mwaka huu ni thamini mchango wa wazee kwa maendeleo ya Nchi yetu, na serikali inalitambua hilo ndio maana inatoa kipaumbele kwa Wazee kwa kuhakikisha wanakuwa na Afya njema kwa kupatiwa matibabu bure kutokana na mchango wao", alisema Ndagala.
 
Aidha Ndagala alimuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo kuandaa watumishi watakao kuwa wakishughulikia masuala ya Wazee na kuhakikisha jamii ina tambua na kuthamini mchango wa wazee na kuihamasisha jamii kutambua umuhimu wa wazee na kuihamasisha jamii kuwathamini wazee na kuwapenda kwa kuweka mipango shirikishi kwa wazee na jamii ilikuweka usawa kati yao.

Alieleza kuwa Serikali inaendelea kuwajali wazee kwa kutoa huduma ya afya bure,Wilaya imeamua kuwatambua wazee na kutoa huduma za Afya bure kwa wazee 1700 wamepatiwa vitambulisho vya msamaa vya matibabu vya muda na kumuagiza Mkurugenzi kuandaa utaratibu mzuri wa wazee kupatiwa vitambulisho vy a kudumu.

Nao Wazee hao katika risala yao iliyo wasilishwa na Mwenyekiti wa chama cha wazee Wilaya ya Kakonko Mbonipa Kisama, waliishukuru Serikali ya awamu ta tano kwa kutambua umuhimu wa wazee na kuwapa kipaumbele kwakuwapatia matibabu bure na kuiomba serikali kuanza kutoa petion jamii waliyo ahidiwa kwa muda mrefu kwa Wazee iliwaweze kufanya shughuli ndogo ndogo za kujikimu katika kipindi hicho na kuondolewa tozo za kijamii kwa wazee.

Alisema Wazee wanamahitaji yao ya ziada iliwaweze kuishi bila wasiwasi wilaya ina wazee 7103 ambapo wazee wanawake ni 3135 na wanaume ni 3975 ambao ni Wanachama wa chama cha Wazee ambapo kupitia chama hicho serikali imeweza kitumia Wadau kufanya sensa ya kuwatambua wazee na mahitaji yao na kuweza kutoa msaada kwa Wazee wasio jiweza.

Aidha Wazee hao waliyashukuru mashirika ya Help age international na shirika la TCRS kwa kutoa misaada kwa wazee wasio jiweza na kuomba kuendelezwa kwa misaada ya kisheria na haki za wazee kuishi na kutoa mchango wa huduma za kijamii kwa Wazee na wanaamini maombi waliyatoa serikali itatue changamoto hizo ilikuondokana na changamoto hizo.

Hata hivyo katika maadhimisho hayo yaliadhimishwa kwa Wazee kucheza michezo mbalimbali ikiwa ni pamoja na mpira wa miguu, uvutaji wa kamba na ukimbizwaji wa kuku ambapo mshindi alikabidhiwa mbuzi na kiasi cha shilingi 20,000/= na Mkuu huyo kuomba michezo hiyo kwa wazee kuendelezwa katika kila kata ili kuimarisha Afya za wazee hao .
 Baadhi ya Wazee wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye maadhimisho hayo
 Mkuu Wawilaya ya Kakonko Kanali Hosea Ndagala akikabidhi zawadi ya Mbuzi kwa timu ya wazee wa kijiji cha Kasanda iliyofanya vizuri katika michezo wakati wa maadhimisho hayo ya Wazee.
  MKUU wa Wilaya ya Kakonko Kanali Hosea Ndagala akikabizi vitambulisho vya matibabu kwa baadhi ya wazee wilayani Kakonko.
  MKUU wa Wilaya ya Kakonko Kanali Hosea Ndagala akikabizi vitambulisho vya matibabu kwa baadhi ya wazee wilayani Kakonko.
 Baadhi ya wazee wakicheza ngoma katika maadhimisho ya siku ya wazee.

IGP SIMON SIRRO AFANYA MAZOEZI NA MAOFISA NA ASKARI WA MAKAO MAKUU YA POLISI


 Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro akiongoza maofisa na askari wa Makao Makuu ya Jeshi la Polisi leo jijini Dar es Salaam katika mazoezi ya pamoja ambayo hufanyika kila mwisho wa mwezi. IGP amewahimiza Makamanda wa Polisi wa Mikoa yote kuhakikisha wanafanya mazoezi ya pamoja ili kuendelea kuboresha afya za maofisa na askari. 
Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro akiongoza maofisa na askari wa Makao Makuu ya Jeshi la Polisi leo jijini Dar es Salaam katika mazoezi ya pamoja ambayo hufanyika kila mwisho wa mwezi. IGP amewahimiza Makamanda wa Polisi wa Mikoa yote kuhakikisha wanafanya mazoezi ya pamoja ili kuendelea kuboresha afya za maofisa na askari. 

Tamko la Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wazee Duniani, Oktoba 1, 2017


Mhe. Iddi Ramadhani Mapuri
Makamu Mwenyekiti 
TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) inaungana na wadau wote duniani katika kuadhimisha siku ya wazee duniani. Wakati dunia inaadhimisha siku hii, Tume inatoa wito kwa jamii ya Watanzania kuondoa vitendo vyote vya unyanyasaji dhidi ya wazee ili kuhakikisha kuwa wanaishi katika kutekeleza kauli mbiu ya taifa inayosema “Kuelekea uchumi wa viwanda: Tuthamini mchango, uzoefu na ushiriki wa wazee kwa maendeleo ya taifa.

Uzee na kuzeeka havikwepeki; hivyo ustaarabu wa jamii au nchi yoyote duniani si wingi wa raslimali na mazingira mazuri bali katika uwekaji wa mifumo madhubuti ya kulinda na kutetea haki za makundi maalum yanayohitaji ulinzi wa jamii husika. Kwa kulitambua hilo Desemba 14, 1990, Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika Azimio lake Na. 45/106 ulipitisha tarehe 01 Oktoba, ya kila mwaka kuwa siku ya wazee Duniani. Vipaumbele katika Azimio hilo ni pamoja na suala la uhuru wa wazee, wazee kushiriki na kushirikishwa katika shughuli za maendeleo, kutunzwa na kuheshimiwa.

Hivyo siku hii ya tarehe 01 Oktoba, dunia inawapa nafasi wazee kukutana pamoja na kubadilishana mawazo juu ya nini cha kufanya kuhusiana na mustakabali wa haki zao kwa ujumla, katika kuleta maendeleo ya Taifa tunapoelekea Tanzania ya viwanda.

Katika kutambua, kulinda kukuza na kutetea haki za wazee serikali imeridhia Mkataba wa Afrika wa Haki za Binadamu na Watu, yaani “The African Charter on Human and People’ Rights (ACHPR)” pamoja na Itifaki ya kusimamia haki za wazee ’’Protocol to the African Charter on Human and People’ Rights on the Rights of elder persons in Africa”.  Kadhalika kuna Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Kiraia na Kisiasa, yaani TheInternational Convenant on Civil and Political Rights (ICCPR), na Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Kiuchumi, Kijamii na Kiutamaduni, yaani The International Convenant on Economic, Social and Cultural Rights (ICESCR).

Kitaifa, kuna Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 pamoja na marekebisho yake ibara ya 12 (2) na ibara ya 14 ambazo zimeeleza juu ya wazee kupewa heshima na kupata hifadhi kutoka kwa jamii wanamoishi.

Aidha, kuna Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora ambayo ni Idara huru ya Serikali iliyoanzishwa kwa mujibu wa Ibara ya 129 (1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, na Sheria Na. 7 ya Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora ya mwaka 2001 ambayo ni kitovu cha kulinda, kutetea na kukuza haki za binadamu nchini.

Takwimu za wazee kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2002, Tanzania ilikuwa na wazee 1,952,041 (sawa na wanaume 940,229 na wanawake 1,011,812) na katika sensa ya mwaka 2012 idadi ya wazee iliongezeka hadi kufikia 2,507,568 (wanaume 1,200,210 na wanawake 1,307,358) sawa na 5.6% ya wananchi wote. Hivyo, kwa kadiri idadi ya wazee inavyoongezeka ndivyo changamoto zinazowakabili zinavyoongezeka. Hivyo jitihada mahsusi lazima zifanyike kukabiliana nazo.

Tume kama taasisi ya kitaifa yenye jukumu la kulinda, kukuza na kutetea haki za binadamu imefanya jitihada mbalimbali kuhakikisha kuwa wazee wanapata haki zao. Jitihada hizo ni pamoja na:
i)      Kushughulikia malalamiko yanayohusu uvunjifu wa haki za binadamu na ukiukwaji wa misingi ya utawala bora kwa wastaafu hasa katika suala linalohusu mapunjo na wastaafu kutolipwa stahiki zao kwa wakati.

ii)     Tume imekuwa ikitoa elimu ya haki za binadamu ikiwemo haki za wazee kwa viongozi wa ngazi mbalimbali ikiwemo taasisi za serikali, asasi za kiraia na wadau mbalimbali wa haki za binadamu na umma kwa ujumla.

iii)   Tume imeshiriki kikamilifu katika mchakato wa kutunga sheria ya wazee kwa kutoa maoni yanayohakikisha kuwa haki za wazee zinalindwa na kuhifadhiwa. Pia inashiriki katika mchakato wa mpango wa pensheni jamii.

iv)   Tume imetoa matamko mbalimbali kulaani mauaji ya wananchi wakiwemo wazee yanayotokea katika maeneo mbalimbali nchini.

Tume inapongeza sana jitihada zinazochukuliwa na Serikali ya awamu ya tano katika kushughulikia masuala ya wazee. Jitihada hizo ni pamoja na:
i)        Kuimarisha Wizara inayoshughulikia masuala ya wazee kwa kutaja neno “wazee” katika jina la Wizara.

ii)       Kuimarisha huduma za afya kwa kuongeza bajeti ya Afya inayoiwezesha Serikali kununua dawa na vifaa tiba kwa wakati.

iii)      Kuweka madirisha ya wazee katika hospitali na vituo vya afya.

iv)     Kuanzisha mchakato wa mfuko wa Afya ya jamii.

v)       Kuanzisha mchakato wa malipo ya pensheni kwa wazee wote.

vi)     Kuanzisha mchakato wa kupambana na mauaji ya wazee.

vii)    Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) imeanzisha mpango wa malipo ya pensheni jamii kwa wazee wenye umri  wa miaka 70+.

viii)   SMZ pia imo katika mchakato wa kutoa vitambulisho maalum kwa wazee vitakavyowawezesha kupata huduma mbalimbali.

ix)     SMZ imeimarisha huduma za wazee kwa kuanzisha idara ya wazee.

Pamoja na jitihada ambazo zimefanywa na Serikali, Tume, Asasi za Kiraia, Mikataba, Maazimio na Itifaki za kikanda na kimataifa, bado wazee wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ambazo kimsingi huvunja haki. Changamoto hizo ni pamoja na:
i)     Ukosefu wa Sheria maalum inayoweka ulinzi na kuzitambua haki za wazee.

ii)    Wazee walio wengi kutofaidika na mafao mbalimbali ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (Pensheni jamii) licha ya kwamba maendeleo yaliyofikiwa na nchi hii ni matokeo ya mchango wa wazee kwa kazi zao walizofanya.

iii)  Umaskini wa kipato miongoni mwa wazee.

iv)  Usalama mdogo kwa wazee kutokana na ukatili na manyanyaso wanayofanyiwa, hususani vitendo vya unyanyasaji kwa wanawake, walemavu na mauaji ya wazee kutokana na imani potofu. Kwa mfano, takwimu za Wizara ya Mambo ya Ndani (2016) zinaonyesha kuwa wazee wameendelea kuuawa katika sehemu mbalimbali nchini. Kwa mfano, mwaka 2014 waliuawa wazee 557, mwaka  2015 wazee 190 na katika kipindi cha mwezi  Januari hadi Oktoba 2016 wazee 119 waliuawa. Mikoa  inayoongoza kwa mauaji  ya wazee kwa kipindi cha Julai 2015 hadi Machi 2016 ni: Tabora (49), Shinyanga (17), Mbeya (15), Geita (11), Rukwa (9), Njombe (9) na Simiyu (7).

Kutokana na changamoto hizo, na ili kuhakikisha kuwa haki za wazee zinalindwa, zinadumishwa, zinakuzwa na kuendelezwa, Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora inatoa mapendekezo yafuatayo kwa Serikali, wadau na jamii kwa ujumla:
i)        Elimu ya haki za binadamu na misingi ya utawala bora itolewe kwa wananchi wote. Hii itasaidia katika kujenga jamii inayoheshimu haki za binadamu nchini.

ii)       Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ikamilishe kutunga Sheria ya Wazee ili kurahisisha utekelezaji wa Sera ya Wazee ya mwaka 2003.

iii)      Serikali iendelee kuboresha huduma za afya na zitolewe bure kwa wazee wote, ikiwa ni pamoja na kukamilisha mpango wa afya ya jamii.

iv)     Serikali ikamilishe mpango wa malipo ya pensheni jamii (Social Pension) kwa wazee wote.

v)       Serikali kupitia vyombo vya ulinzi na usalama ihakikishe panakuwepo ulinzi madhubuti kwa wazee ikiwa ni pamoja na kuwakamata wahusika wa mauaji ya wazee na kuwafikisha katika vyombo vya dola kwa wakati na jamii ijitokeze kutoa ushahidi.

vi)     Kamati za ulinzi za Kata na Vijiji ziimarishwe ili kulinda maisha ya wazee.

vii)    Kupitia mkakati wa kunusuru kaya maskini unaosimamiwa na TASAF, kipaumbele kitolewe kwa wazee kote nchini.

viii)   Mabaraza ya wazee yaanzishwe na kuimarishwa ili kutoa nafasi ya ushirikishwaji wa wazee katika maendeleo ya nchi.

Mwisho, Tume inatoa rai kwa Serikali na wananchi wote kwa ujumla kulinda na kutetea haki za wazee. Aidha, tuthamini mchango, uzoefu na ushiriki wa wazee kwa maendeleo ya taifa.

“Uzee na kuzeeka havikwepeki”

Imetolewa na: 
Iddi Ramadhani Mapuri
Makamu Mwenyekiti 
TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA 

Oktoba 1, 2017