Thursday, March 21

‘Tunahitaji dunia inayolinda maisha’

Vatican City. Mkuu wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis amesimikwa rasmi, huku akiitaka dunia kuungana kwa ajili ya kuwatetea wanyonge na kulinda mazingira.
Akizungumza wakati wa misa maalumu ya kumsimika katika wadhifa huo mpya iliyofanyika kwenye Kanisa Kuu la Mtakatifu Peter mjini Vatican, Papa Francis alisema hiyo ndiyo njia pekee ya kuijenga dunia iliyo njema na salama, isiyo na vifo visivyo vya lazima na maangamizi.
Francis akitoa hotuba yake alikuwa akishangiliwa na kufunikwa kila mara kwa sauti ya hadhira iliyokuwa ikimsikiliza, hasa alipozungumzia umuhimu wa kulinda mazingira, kusaidiana, kupendana na kutoruhusu namna yoyote ya maangamizi, chuki, wivu na majivuno yanayoweza ‘kuharibu maisha yetu’.
Alisema kwamba wajibu wake mkuu ni kunyoosha mikono yake na kulinda utu, hasa ‘wa maskini, wasiojiweza, wale wanaodharauliwa hasa ambao Mtakatifu Mathayo aliwataja alipokuwa akihitimisha falsafa ya upendo: wenye njaa, wenye kiu, wageni, wasio na mavazi, wagonjwa na wale waliofungwa magerezani’.
“Leo tunahitaji kuona mwanga wa matumaini katika giza lililopo mbele yetu na kuwa wanaume na wanawake wanaotoa tumaini jipya kwa wengine. Kulinda uumbaji, kulinda wanaume na wanawake, kuwaangalia kwa upendo na kujali, hii ikiwa njia pekee ya kutoa tumaini jipya, ili kutoa mwanga mpya na kuangaza kuliko na wingu nene,” alisema.
Kauli hiyo ilianza kutolewa na kiongozi huyo mkuu wa Kanisa lenye zaidi ya waumini 1.2 bilioni duniani tangu alipotangazwa rasmi kuchaguliwa na jopo la makadinali Jumatano wiki iliyopita, ambapo alianza kutangaza ujumbe wake wa amani wa kuwajali na kuwapenda maskini.
Katika misa hiyo maalumu iliyohudhuriwa na wageni maalumu 132 wakiwamo viongozi wa kidini na wa mataifa mbalimbali akiwamo Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe, ujumbe wake kwa wafuasi wa Kanisa hilo na watu wote duniani ulichukua muda mfupi usiofikia saa moja, hivyo kumfanya aonekane mtu mwenye staha na kujali muda.
“Ninawaomba wote wenye wajibu katika kusimamia uchumi, siasa, maisha ya watu kuwajibika.” pamoja na wanaume na wanawake wote wenye nia njema, tuwe walinzi wa uumbaji wa Mungu, tulinde mpango wa Mungu ulio wa asili, tulindane na kupendana na kuyalinda mazingira.”
Papa Francis alijumuika na waumini waliokusanyika katika uwanja huo ambapo alizunguka katika eneo hilo kwa kutumia gari maalumu, akisalimiana na waumini kuwabariki wasiojiweza na kuwabusu watoto wenye matatizo.

Lowassa afufua kashfa ya kigogo Ikulu

Dar es Salaam. Sakata la Mkuu wa Itifaki wa Ikulu, Anthony Itatiro, ambaye anahusishwa na njama za kutaka kuchota kiasi cha Sh3 bilioni kwa ajili ya safari hewa ya Rais, limechukua sura mpya baada ya Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje kutaka kujua hatima ya kigogo huyo jana.
Itatiro na maofisa wanne wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa walituhumiwa mwaka jana kuidhinisha kuchota kiasi hicho cha fedha bila ya kuwapo kwa ziara ya Rais kwenda nchi yoyote ya kigeni.
Mpango huo unadaiwa kusukwa Juni mwaka jana kwa maofisa haokuitaka Wizara ya Fedha kutoa kiasi hicho cha fedha kwa ajili ya safari hewa ya Rais.
Naibu Waziri wa wizara hiyo, Juma Mahadhi alitoa maelezo hayo baada ya kuulizwa swali na Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje ya Bunge, Edward Lowassa.
Lowassa, ambaye pia ni Mbunge wa Monduli aliuliza swali hilo ghafla kwa Mahadhi wakati akitoka nje, baada ya kumalizika kwa kikao cha kamati yake kilichofanyika kwenye ofisi za Bunge jijini Dar es Salaam.
Mahadhi, ambaye alilazimika kutoa ufafanuzi wa swali hilo baada ya kubanwa zaidi na waandishi wa habari, alisema Rais Kikwete ndiyo mwenye mamlaka ya kuchukua hatua dhidi ya Itatiro kutokana na ripoti ya uchunguzi ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) na Mkaguzi wa Ndani wa Wizara hiyo.
Alisema pia kuwa walishauriwa kuwa maofisa walioshirikiana na Itatiro nao wachukuliwe hatua za kinidhamu kufuatia njama hizo.
Alipotafutwa kuzungumzia suala hilo, Katibu Mkuu Ombeni Sefue hakupokea simu. Pia hakujibu pindi alipotumiwa ujumbe mfupi kwa njia ya simu. Naye Katibu Mkuu katika Ofisi ya Rais anayeshughulikia Utumishi, George Yambesi alisema hakuwa tayari kuzungumzia suala hilo kwani alikuwa likizo.
Mahadhi alisema wakati tukio hilo linatokea viongozi wakuu wa wizara hiyo walikuwa kwenye majukumu mengine ya Serikali, jambo ambalo lilisababisha nafasi zao kukaimiwa na watendaji hao.
“Wale maofisa walitumia mwanya wao wa kukaimu nafasi ile ndiyo wakasuka mpango huo,” aliongeza Mahadhi.
Alisema kutokana na hali hiyo baadhi ya maofisa hao wamechukuliwa hatua za kinidhamu ikiwamo ya kuwashusha vyeo na kuwabadilisha vitengo.
Mahadhi alisema kwamba huwa ni utaratibu wa kawaida kwa Rais anaposafiri maofisa wa Itifaki na wale wa Wizara ya Mambo ya Nje kupewa fedha na hazina kwa ajili ya kufanikisha ziara zake.
“Ila maofisa hawa walitumia mwanya huo kuihadaa Wizara ya Fedha kwa kuandaa hoja ya safari feki ili kupata fedha hizo,” aliongeza Mahadhi.
Maofisa wengine ni pamoja na ofisa katika Idara ya Itifaki, Shamim Khalfa, Kaimu Mhasibu Mkuu, Kasim Laizer, Mhasibu, Deltha Mafie na karani wa fedha) aitwaye, Shabani Kesi.

OBAMA AFANANISHWA NA SHETANI...


Rais wa Marekani Barack Obama amefananishwa na shetani baada ya muigizaji Mohamen Mehdi Quazann kucheza sinema inayofanana na muonekano wa shetani huku akionekana kufafana na Obama

Kwa mujibu wa repoti ya CNN filamu hiyo ambayo imeonekana kuteka mashabiki wengi teyari imeshaanza kurushwa vipande vichache vinavyoonyesha jinsi Obama alivyofanana na Mohamen huku akionekana kama shetani kupitia channel ya 'The History'

Mpaka sasa inaonekana filamu hiyo kupata mashabiki wengi na kuteka vichwa vya habari vingi huku mashabiki wengi wakiwa wamemiminika katika mtandao wa twitter na kupata tweets zaidi ya 200 kwa muda mfupi

PRO-24