Thursday, October 19

SAA 24 BAADA YA KUJIUZULU KWA JACKSON MAYANJA, SIMBA YAMTAMBULISHA KOCHA MPYA MRUNDI

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
UONGOZI wa klabu ya Simba leo mchana umemtambulisha kocha mpya atakayevaa viatu vya aliyekuwa kocha msaidizi Jackson Mayanja pamoja na meneja mpya anayechukua nafasi ya Dr Cosmas Kapinga.
Akitoa utambulisho huo mbele ya  waandishi wa habari,  Afisa habari wa Simba Haji Manara amesema kuwa Kocha Masoud Djuma kutoka Rayon Sports ya nchini Rwanda na kocha bora wa msimu uliopita kupitia klabu hiyo anakuja kuchukua nafasi ya Jackson Mayanja aliyeachia ngazi kutokana na kuwa na matatizo ya kifamilia nchini Uganda.

Manara amesema kuwa, kabla ya kufikia makubaliano ya kuachana na Mayanja tayari walikuwa wameshaanza mazungumzo na kocha Djuma kuja kusaidiana na kocha Jospeh Omog kuinoa klabu hiyo.
Akizungumza baada ya kutambulishwa Kocha Djuma, amesema kuwa amekuja Simba kusaidiana na kocha Omog kuwezesha kupata mataji mbalimbali na sio kufanya maajabu kama watu watakavyodhani.

“Sijaja kufanya maajabu, nimekuja kuisaidia Simba kwa kidogo nilichonacho ili kuisogeza mbele zaidi ”, alisema Djuma huku akiweka wazi zaidi kuwa amekuja kufanya kazi na falsafa yake ni kocha mwenye pande mbili  mkali na mpole lakini huwa mkali pale ambapo mchezaji anataka kuharibu kazi.
Kocha Masoud Djuma akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutambulisha na afisa wa habari wa Simba Haji Manara (Kulia) akichukua nafasi ya Jackson Mayanja aliyejiuzulu jana.
“Mimi ni mtu wa pande mbili kwa ufupi ni kama kiganja cha mkono, kina pande mbili. upande mmoja mpole lakini kwa upande mwingine ni mkali. Nimekuja hapa kufanya kazi ili kuipeleka Simba mbele na mimi nisogee mbele.”amesema Djuma.

Kuelekea mechi ya watani wa jadi Okotoba 28, Djuma ameweka wazi kuwa toka amezaliwa ameanza kusikia  Simba na Yanga kwahiyo anazijua vizuri , “Nimezaliwa nimekuwa nazisikia Simba na Yanga, kila sehemu kuna mechi zenye presha kubwa siwezi kuahidi lolote kuhusu mechi ya Simba na Yanga kwa sababu mpira una matokeo matatu.”
Ili kuliboresha benchi la ufundi, Klabu ya Simba imemtambulisha meneja anayerirhi mikoba ya Cosmas Kapinga, Richard Robert mwenye uzoefu wa masuala ya mpira na utawala ambapo awali aliwahi kuwa meneja wa wanja wa ndege na pia katika kituo cha JKM Park.
Afisa habari wa Simba Haji Manara akimtambukisha kocha mpya Masoud Djuma (Kulia) aliyechukua nafasi ya Jackson Mayanja pamoja na meneja mpya wa Simba Richard Robert leo katika mkutano na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam. 


Tulia mjomba upone, Nape amwambia Lissu


Dar es Salaam. Mbunge wa Mtama (CCM), Nape Nnauye amemtaka Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu atulie hadi apone kabla hajasema mengi.
Katika kurasa zake za mitandao ya kijamii ya leo Alhamisi akiwa ameambatanisha na picha ya Lissu ameandika, “Mjomba tunamshukuru Mungu kwa tabasamu hili la matumaini! Nakuombea afya iimarike kabla hujasema mengi! Tulia mjomba upone kabisa kwanza!”

Mhubiri aliyetabiri kuwa Mugabe angefariki tarehe 17 mwezi huu ajitetea

Muhubiri aliyetabiri kuwa Mugabe angefariki tarehe 17 ajiteteaHaki miliki ya pichaAFP
Image captionMhubiri aliyetabiri kuwa Mugabe angefariki tarehe 17 ajitetea
Mhubiri ambaye alitabiri kuwa Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe angefariki siku ya Jumanne, kwa sasa anajaribu kujitetea kwa sababu utabiri wake haukutimia, akisema kuwa Mungu amebadilisha fikra zake.
"Sababu iliyosababisha Mungu kuhairisha hili, hakuniambia - kwa hivyo sijui ni kwa nini Mungu aliamua kuchukua mkondo huo. Ninajua watu wengi walikuwa wakitarajia kutimia kwa unabii kwa sababu ya kile kinachoendelea nchini mwetu."
Mhubiri huyo raia wa Zimbabwe Philip Mugadza alijaribu kuishawishi mahakama ya juu nchini humo kutupa kesi dhidi yake kwa kutabiri kuwa Rais Robert Mugabe, 93, angefariki tarehe 17 mwezi Oktoba mwaka 2017.
Kesi hiyo itarudi mahakamani ambapo mhubiii Mugadza - kiongozi wa kanisa la The Remnant ameshtakiwa.
Wakati wa kukamatwa kwake wakili wake Gift Mtisi aliiambia BBC kuwa "anakubali kusema hivyo. Anasema hakudanganya - huo ni ujumbe kutoka kwa Mungu. Polisi watahitaji kuthibitisha kuwa Mungu hakusema hilo."
Mawakiia wake pia waliitaka mahaka ya katiba kutupilia mbali mashtaka hayo kwa misingi kuwa yanakiuka haki yake ya uhuru wa kusema.
Mwendesha mashtaka anasema kuwa muhubiri huyo alitukana dini ya kikiristo na tamaduni za Afrika kwa kutabiri kifo cha Mugabe.
Kutabiri kifo cha kiongozi ni mwiko, kulingana na imani za kitamaduni.

Hoteli kubwa ya kifahari yateketea moto Myanmar

A firefighter extinguishes a fire at Kandawgyi Palace hotel in Yangon early on 19 October 2017Haki miliki ya pichaAFP/GETTY IMAGES
Image captionMoto huo ulianza mapema Alhamisi
Moto mkubwa imeteketeza hoteli kubwa ya kifahari katika mji wa Yangon nchini Myanmar na kumuua mtu mmoja.
Watu wengine walijeruhiwa kwenye moto huo ambao ulianza mwendo wa saa 20:30 GMT siku ya Jumatano katika hoteli ya Kandawgyi Palace.
Hoteli hiyo ilikuwa maarufu wa watalii.
Firefighters work at the scene of a fire at Kandawgyi Palace hotel in Yangon early on 19 October 2017Haki miliki ya pichaAFP/GETTY IMAGES
Image captionMoto mkubwa uliwaka
Iliwachukua mamia ya wazima moto saa kadha kuuzima moto huo. Zaidi ya wageni 140 waliondolewa.
Haijuliana moto huo ulinza kwa njia gani huku ripoti za kukanganya zikisema kuwa kulikuwa na mlipuko wa mtungi wa gesi au hutilafu ya umeme.
Firefighters work at the scene of a fire at Kandawgyi Palace hotel in Yangon early on 19 October 2017.Haki miliki ya pichaAFP/GETTY IMAGES
Image captionMamia ya wazima walitumwa kuuzima moto huo
"Hakukuwa na king'ora na vurugu zilikuwa ni kama kulikuwa na walevi hotelini," mtalii mmoja alisema, akiongeza kuwa ni mfanyakazi mmoja ambaye alimuelekzea eneo salama.
Wageni wamehamishwa kweda kwa hoteli zingine mjiji Yangon.
Picture of Kandawgyi Palace Hotel in Yangon before the October 2017 fire - ONE TIME USE ONLYHaki miliki ya pichaALAMY
Image captionHoteli ya kifahari kabla ya kuteketea
People do exercises near a fire at Kandawgyi Palace hotel in Yangon, Myanmar October 19, 2017 .Haki miliki ya pichaREUTERS
Image captionMoshi bado ulikuwa ukitoka kwenye mabaki ya hoteli hiyo
Hoteli hiyo ili kando ya ziwa Kandawgyi, ilijengwa miaka ya 1990 lakini huenda uwepo wake uliazia miaka ya 1930 wakati eneo hilo lilikuwa likitumia kama klabu ya wanajeshi wa Uingereza.

New Zealand kumpata waziri mkuu mwanamke mwenye umri mdogo zaidi

Jacinda ArdernHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionKatika umri wa miaka 37 Jacinda Ardern anataraji kuwa waziri mkuu mwenye umri mdogo zaidi nchini New Zealand
New Zealand inajiandaa kwa serikali ya Muungano ambayo itaongozwa na kiongozi wa chama cha Labour, Jacinda Ardern
Bi Ardern amekuwa kiongozi wa upinzani kwa miezi mitatu sasa. Katika umri wa miaka 37 anataraji kuwa waziri mkuu mwenye umri mdogo zaidi nchini New Zealand tangu mwaka 1856.
Chama chake cha Lebour kilichukua nafasi ya pili mwezi Septemba ambapo hakuna chama kiliweza kupata wingi wa kura.
Sasa kinatarajiwa kuingia madarakani baada ya chama kidogo cha New Zealand First party kukubali kujiunga na serikali.
Muungano huo mpya pia utaungwa mkono na chama cha Green Party.
Jacinda Ardern with political supportersHaki miliki ya pichaAFP
Image captionKatika umri wa miaka 37 Jacinda Ardern anataraji kuwa waziri mkuu mwenye umri mdogo zaidi nchini New Zealand
Jacinda Arden tayari ameonyesha kuwa anaweza kufanya kampeno nzuri na kufanya mikataba ya kisiasa lakini bado anakabiliwa na chamgamoto mpya.
Kwanza ni kuwashawishi watu nchini New Zealand ambao hawakumpigia kura kuwa chama hicho ambacho kilichukua nafasi ya pili kitaongoza.
Pia kuna uhusiano wa kujengwa na serikali ya Australia ambayo ilikilaumu chama cha New Zealand Labour party kwa upinzani dhidi yao wakati wa suala ya uraia mara mbili.

Mazungumzo ya Serikali, Barrick nchi nyingine kujifunza


By George Njogopa, Mwananchi gnjogopa@mwananchi.co.tz
Dar es Salaam. Rais John Magufuli amesema mafanikio yaliyofikiwa baada ya kuwepo majadiliano kati ya wataalamu wa Tanzania na wale wa kampuni ya Barrick Gold Mine kuhusu biashara ya madini ya dhahabu yameweka rekodi ya aina yake hatua ambayo inaweza kuzisukuma nchi nyingine za Afrika kuja Tanzania kujifunza namna inavyoweza kujadiliana na wawekezaji wa kigeni na hatimaye kukubaliana.
“Tanzania tumeonyesha mfano na kweli tukiamua tunaweza. Haya majadiliano hayakuwa kitu rahisi lakini mwisho wa siku tumefanikiwa na naamini nchi nyingine za Afrika zitataka kuja hapa kujifunza namna tulivyofanikiwa,” amesema Magufuli wakati akizungumza leo Alhamisi baada ya kufikiwa makubaliano hayo.
Amesema amejifunza kuwa mazungumzo daima huwa yana faida na licha kuona ugumu wake lakini aliendelea kuiamini timu yake huku akiitia moyo kutorudi nyuma.
Amesema kuanzia sasa Tanzania imeweka kiwango kipya kuhusu mikataba ya madini na kwamba kiwango hicho kilichofikiwa na kampuni ya Barrick ndicho kitatumika katika majadiliano na kampuni nyingine.
“Nasema sasa hili jambo linaendelea pia katika madini mengine ikiwamo Tanzanite na yule asiyetaka basi aondoke atuachie madini yetu... tumepewa na mwenyezi Mungu na tutaendelea kuchukua msimamo huu huu,” amesema.
Rais Magufuli amewataka Watanzania kuendelea kuwa na moyo wa kizalendo akisisitiza jukumu la kuijenga nchi haitafanywa na raia mwingine wa kigeni bali ni wao.
“Huu ni mwanzo wa kuitengeneza Tanzania yetu na kila Mtanzania lazima ajue wajibu wake maana hakuna mgeni atakayekuja hapa kututengenezea nchi hii,” amesema.

BREAKING: MAJADILIANO KATI YA TANZANIA NA TIMU YA WAWAKILISHI WA KAMPUNI YA BARRICK GOLD YAFIKIA TAMATI

Majadiliano kati ya Tanzania na timu ya wawakilishi wa kampuni ya Barrick Gold inayomiliki migodi ya madini hapa nchini yamekamilika na makubaliano kati ya pande hizo yametiwa saini leo tarehe 19 Oktoba, 2017 mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu, Jijini Dar es Salaam.
Timu ya Barrick Gold Corporation ilikuwa imeongozwa na Mwenyekiti Mtendaji wa kampuni hiyo Prof. John Thornton wakati timu iliyowakilisha Serikali ya Tanzania imeongozwa na Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba John Aidan Mwaluko Kabudi.
Miongozi mwa mambo waliyokubaliana ni kutekeleza mwelekeo mpya wa biashara ya madini ambapo kutakuwa na mgawanyo sawa wa faida (yaani Tanzania kupata asilimia 50 na Barrick Gold Corporation kupata asilimia 50 ya faida) na kuundwa kwa kampuni ya ubia wa usimamizi wa migodi ya madini iliyopo Tanzania ambayo itakuwa na makao makuu yake Mwanza na ofisi ndogo Dar es Salaam nchini Tanzania badala ya nchini Uingereza.
Mengine ni kufunga ofisi za uhasibu na fedha zilizopo Johannesburg Afrika Kusini na kuhamishia Tanzania na kutekeleza masharti yote ya mabadiliko ya sheria mpya ya madini na rasilimali za nchi ya mwaka 2017.
Aidha, Barrick Gold Corporation imekubali kuwepo kwa wawakilishi wa Serikali katika bodi za migodi yake yote hapa nchini, kazi mbalimbali za kwenye migodi kufanywa na kampuni za Kitanzania, Migodi kutoa ajira za kudumu kwa wachimbaji, wachimbaji hao kuishi majumbani kwao badala ya kuishi kwenye makambi ya migodi na mashauri yote ya kesi mbalimbali kufanywa hapa nchini.
Kampuni ya Barrick Gold pia imekubali kutoa Dola za Kimarekani Milioni 300 sawa na takribani Shilingi Bilioni 700 kama malipo ya kuonesha nia njema ya kufidia fedha zilizotokana na upotevu wa mapato kupitia biashara ya kampuni hiyo.
Akizungumza baada ya kutia saini makubaliano hayo Prof. Thornton amempongeza Mhe. Rais Magufuli kwa msimamo wake unaojenga misingi ya biashara ya kuaminiana na uwazi, ambayo ni muhimu na ya namna yake kwa biashara katika karne hii ya 21.
Prof. Thornton amesema Barrick Gold Corporation watazingatia makubaliano haya na wanaamini kuwa yamefungua ukurasa muhimu utakaowezesha kufanya biashara kisasa.
Kwa upande wake Mhe. Rais Magufuli amezipongeza timu zote mbili yaani Tanzania na Barrick Gold Corporation kwa kazi kubwa ziliyofanya kufikia makubaliano hayo na kwa kipekee amempongeza Prof. Thornton kwa nia yake thabiti ya kukubali kufanyika kwa mazungumzo na kukubali mambo yaliyofikiwa.
Mhe. Rais Magufuli amesema makubaliano hayo yataisaidia nchi kuzalishaji ajira zaidi, kupata manufaa mbalimbali yanayostahili ikiwemo fedha za kugharamia huduma za kijamii kwa wananchi na yanajenga msingi imara ambao utaiwezesha Tanzania kunufaika na rasilimali zake za madini.
Mhe. Dkt. Magufuli amemuagiza Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Kabudi kuunda timu zitakazoshughulikia biashara ya madini ya Tanzanite na Almasi pamoja na migodi mingine ya dhahabu haraka iwezekanavyo ili nchi iweze kunufaika ipasavyo.
“Nataka machimbo yote ya dhahabu mchakato kama huu ufanyike, pia nakuagiza Prof. Kabudi biashara ya madini ya Tanzanite na Almasi nako ni lazima kufuate utaratibu huu, asiyetaka aondoke” amesema Mhe. Rais Magufuli.
Pia Mhe. Rais Magufuli amewataka Watanzania kuunga mkono juhudi hizi badala ya baadhi yao kuzibeza kwa kuwa zina manufaa kwa taifa na wananchi wake. 
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
19 Oktoba, 2017 
 Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya Barrick Gold Corporation Profesa John L. Thornton akiwasili katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam Jumanne jioni tayari kushiriki katika mazungumzo ya mwisho na hatimaye makubaliano baina ya Kamati ya serikali na timu ya wataalamu wa kampuni hiyo kuhusiana na makinikia pamoja na biashara ya madini kwa ujumla. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimlaki  Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya Barrick Gold Corp.Profesa John L. Thornton alipokutana nae wakati wa kupokea ripoti ya makubaliano baina ya Kamati ya Serikali na  timu ya wataalamu wa Barrick Gold kuhusu bishara ya madini Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 19, 2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea  na Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya Barrick Gold Corp.Profesa John L. Thornton alipokutana nae wakati wa kupokea ripoti ya makubaliano baina ya Kamati ya Serikali na  timu ya wataalamu wa Barrick Gold kuhusu bishara ya madini Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 19, 2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akishuhudia Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya Barrick Gold Corp. Profesa John L. Thornton akiwa na Afisa Uendeshaji wa Barrick Gold  Richardc William huku Waziri wa Sheria na Katiba Profesa Palamagamba Kabudi na Florens Luoga nao pia wakiweka saini ripoti ya makubaliano baina ya Kamati ya Serikali na  timu ya wataalamu wa Barrick Gold kuhusu bishara ya madini Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 19, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akishuhudia Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya Barrick Gold Corp. Profesa John L. Thornton akiwa na Afisa Uendeshaji wa Barrick Gold  Richardc William huku Waziri wa Sheria na Katiba Profesa Palamagamba Kabudi na Florens Luoga nao pia wakiweka saini ripoti ya makubaliano baina ya Kamati ya Serikali na  timu ya wataalamu wa Barrick Gold kuhusu bishara ya madini Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 19, 2017

Wasanii wa filamu wamfariji Lulu Michael


Dar es Salaam. Msanii wa fani ya uigizaji filamu nchini, Wema Sepetu ni miongoni mwa watu waliomfariji Elizabeth Michael ‘Lulu’ anayekabiliwa na kesi ya kuua bila kukusudia iliyoanza kusikilizwa leo katika Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam.
Wasanii wametumia mtandao wa Instagram kumfariji mwigizaji Lulu ambaye ni mshindi wa tuzo za filamu za AMVCA.  
Jackline Wopler, Katarina Karatu, Nisha, Aunt Ezekiel na wengine wametuma picha za mwigizaji huyo zikiambatana na maneno ya kumfariji wakimweleza kuwa atavuka salama katika mtihani huo.
Kupitia ukura wake wa Instagram, Wema ameweka picha ya Lulu na kuandika, “This Too Shall Pass Baby… God is Great u know… so have faith… ur in my prayers,” akiwa na maana hata hili litapita, Mungu ni mkubwa hivyo anatakiwa kuwa na imani na atamwombea.
Lulu anadaiwa Aprili 7,2012 alimuua bila ya kukusudia mwigizaji mwenzake Steven Kanumba, eneo la Sinza Vatican jijini Dar es Salaam. Kesi inasikilizwa na Jaji Sam Rumanyika.


Mahakama kutoa uamuzi wa pingamizi kesi ya Mdee, Bulaya


Dodoma. Mahakama Kuu Oktoba 30,2017  itatoa uamuzi wa pingamizi zilizowasilishwa na upande wa Serikali katika maombi ya wabunge wa Chadema waliosimamishwa kuhudhuria mikutano mitatu ya Bunge kwa
kosa ya kudharau kiti cha Spika.
Wabunge hao waliosimamishwa katika Bunge la bajeti Juni, 2017 ni Halima Mdee wa Kawe na Ester Bulaya wa Bunda Mjini.
Mdee na Bulaya wamefungua mashtaka
katika Mahakama Kuu wakidai uamuzi huo umekiuka Kanuni za Bunge na Katiba.
Katika kesi hiyo leo Alhamisi Oktoba 19,2017 mawakili wa wabunge hao, Jeremia Mtobesya na Fred Kalonga wameiomba Mahakama iwaelekeze Spika wa Bunge au Katibu Bunge wawapatie taarifa walizoomba na kutoa ruhusa ya kuzitumia.
Wakili Mkuu wa Serikali, Angaza Mwipopo aliyewasilisha pingamizi kwa hati ya kiapo amedai wabunge hao hawakutumia fursa zingine walizonazo kabla ya kufungua shtaka hilo mahakamani.
Jaji Awadhi Mohamed aliyesikiliza pingamizi hizo ameahirisha maombi hayo akisema uamuzi atautoa Oktoba 30,2017.

Watu 21 washikiliwa polisi kwa kuingia nchini isivyo halali


Tabora. Polisi mkoani Tabora inawashikilia wahamiaji haramu 21 kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) wanaodai kukimbia mapigano kwao.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Wilbroad Mutafungwa amesema watu hao walikamatwa juzi Oktoba 17,2017 katika stendi kuu ya mabasi mjini Urambo.
Amesema waliokamatwa wanaume ni wawili, wanawake watano na watoto 14 ambao walitokea Kigoma na walikuwa wakitafuta usafiri wa kwenda mjini Tabora.
Kamanda Mutafungwa amesema leo Alhamisi Oktoba 19,2017 kuwa watu hao walikamatwa baada ya polisi kupata taarifa kutoka kwa wasiri.
“Hawajasema walikuwa wakitaka kuelekea nchi gani lakini wanadai wamekimbia machafuko nchini kwao na wanatafuta kambi ya wakimbizi kwa ajili ya hifadhi,” amesema.
Kamanda Mutafungwa amesema watu hao ni kutoka familia tano zenye watu wanne, saba, watatu, sita na nyingine mmoja.
Ametoa wito kwa wananchi kuhakikisha wanatoa taarifa polisi wanapowashuku wahamiaji haramu ili hatua ziweze kuchukuliwa dhidi yao.
Mutafungwa ameema polisi inashirikiana na Idara ya Uhamiaji katika kushughulikia suala wahamiaji hao.
Mmoja wa watu hao, Dieudonne Buloze akizungumza kwa lugha ya Kiswahili amesema walisafiri kwa njia ya maji hadi nchini sehemu wasiyoijua na kuingia Tabora.
“Tumekimbia mapigano kati ya Serikali na waasi na tunataka kuwa kwenye makambi ya wakimbizi,” amesema.
Watu hao walipewa chakula baada ya kulalamika kuwa wana njaa.







Dk Mahiga aongoza ujumbe wa Tanzania mkutano wa Maziwa Makuu



Waziri wa Mambo ya Nje, Dk Augustine Mahiga

Waziri wa Mambo ya Nje, Dk Augustine Mahiga 
Dar es Salaam. Waziri wa Mambo ya Nje, Dk Augustine Mahiga ameongoza ujumbe wa Tanzania kwenye Mkutano wa Saba wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Ukanda wa Maziwa Makuu (ICGLR) akimwakilisha Rais John Magufuli.
Mkutano huo umefanyika leo Oktoba 19,2017 mjini Brazzaville, Jamhuri ya Congo ukitanguliwa na mingine ya awali katika ngazi ya wataalamu wa masuala ya fedha, wakuu wa vyombo vya usalama, wakuu wa majeshi, waratibu wa nchi na mawaziri wa mambo ya nje.
Taarifa kwa vyombo vya habari imesema mkutano huu umehudhuriwa na wakuu wa nchi, Serikali na wawakilishi wao kutoka mataifa ya Angola, Burundi, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Jamhuri ya Kongo, Kenya, Rwanda, Sudan, Sudan Kusini, Tanzania, Uganda na Zambia.
Ajenda kuu ya mkutano huo ilikuwa ni kupitia na kujadili hali ya siasa, ulinzi na usalama katika eneo la Nchi za Maziwa Makuu na hasa katika nchi za Burundi, DRC, Jamhuri ya Kongo, Jamhuri ya Afrika ya Kati na Sudan Kusini. Nyingine ilikuwa kupokea taarifa ya michango ya nchi wanachama.
Kuhusu hali ya usalama katika Nchi za Maziwa Makuu kwa jumla iliripotiwa kuwa inaendelea kuimarika kwa kiwango kikubwa isipokuwa kwa DRC ambako  operesheni zinaendelea kufanywa na Kikosi cha Umoja wa Mataifa nchini DRC- Monusco (FIB) dhidi ya vikundi vya waasi vya ndani ya DRC na vile vinavyotoka nje ya nchi hiyo.
Mkutano huu ulifuatiwa na mwingine wa nane wa wakuu wa nchi na Serikali wa Mpango wa Amani na Usalama katika Maziwa Makuu.
Taasisi zingine za kimataifa zilizoalikwa kwenye mikutano hiyo ni Umoja wa Mataifa (UN), Umoja wa Afrika (AU) na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (Sadc).
Ujumbe wa Sadc uliongozwa na Katibu Mtendaji wake, Dk Stergomena Tax.