Tuesday, August 22

NANI MBABE NGAO YA JAMII KESHO?

 YANGA KUENDELEZA UBABE AU SIMBA KULIPIZA KISASI?


Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.


KUELEKEA mtanange wa kumaliza ubishi baina ya mahasimu wawili Simb ana Yanga huku kila upande ukijinasibu kufanya vizuri kwenye mchezo huo wa Ngao ya Jamii utakaochezwa kesho kuanzia majira ya saa 11 jioni Uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam.

Ni mechi ya watani wa jadi inayozungumzwa sana midomoni mwa watu, kila mmoja akijinasibu kumfunga mwenzake kwa idadi kubwa ya magoli na na kuinyakua Ngao ya Jamii.

Simba ikiwa imefanya usajili mkubwa sana na wagharama, wakiwajumuisha nyota wanne kutoka Azam Fc John Bocco, Shomari Kapombe, Aishi Manula na Erasto Nyoni pamoja na Kiungo Mnyarwanda kutoka Yanga aliyekipiga kwa misimu kadhaa Haruna Niyonzima.

Mbali na hao, wamemsajili golikipa wa Timu ya Taifa akitokea Mtibwa Sugar Said Dunda na Emanuel Mseja kutoka Mbao Fc, beki wa kulia Shomary Ally, beki wa kati kutoka Toto Africa Yusuf Mlipili, Salim Mbonde kutoka Mtibwa na Mshambuliaji Emanuel Okwi kutoka Sc Villa ya Nchini Uganda. Nicolaus Gyan kutoka Nchini Ghana na beki wa kushoto kutoka Mbao Jamal Mwambeleko 

Kwa upande wa Yanga, wameweza kufanya usajili kwa kuwasajili Ibrahim Ajib kutoka Simba, Raphael Daud kutoka Mbeya City, Pius Buswita kutoka Mbao Fc, Gadiel Michael kutoka Azam, Papii Kabamba Tshishimbi wa Mbabane Swallows na wameweza kuwapanisha vijana wao kutoka timu B Said Musa, Maka Edward ili kuja kuziba nafasi zilizoachwa wazi na wachezaji walioachwa pamoja na wale waliosajiliwa na timu zingine.


Yanga walifanikiwa kuwabakisha wachezaji muhimu kama Donald Ngoma, Thaban Kamosoku na Amisi Tambwe waliokuwa wamemaliza mikataba ya kuitumikia klabu hiyo ya Yanga.


Michuano hii ya Ngao ya Jamii, kwa kawaida huwa ni ‘Super Cup’, kwa maana ya kukutani­sha mabingwa wa michuano miwili to­fauti  bingwa wa FA dhidi ya  mshindi wa pili wa ligi kama bingwa wa ligi na FA.

Safari hii kuna uhalisia zaidi, watu wataona nani mkali kati ya bingwa wa ligi kuu ambaye ni Yanga na bingwa wa  Kombe la FA Simba na kwa mwaka 2017 inakuwa ni mechi ya mara ya 10 toka kuanzishwa mwaka  2001, kusimama na kurudi tena mwaka 2009.

YANGA 

Yanga imewezza kucheza   jumla ya mechi nane ambazo ambapo katika hizo mechi 3 wamecheza  dhidi ya Simba , Mtibwa  ni mara 1 na Azam mara  4 aambapo ndiyo timu ambayo imecheza mechi nyingi zaidi za Ngao ya Jamii tangu ilivyoanzishwa mwa­ka 2001 kati ya timu nne ambazo zime­wahi kucheza mechi hiyo.

SIMBA.


Simba imecheza Ngao ya Jamii  mara nne ikiwa dhidi ya mahasimu wao Yanga mara (3) , Azam mara (1) na kuchukua mara 2  kisha  kupotea na kuwaacha Azam wakicheza mfululizo ndani ya miaka 5 na kulinyakua mara moja msimu wa 2016/17.



YANGA 5, SIM­BA 4


Yanga imefanikiwa kui­funga Simba jumla ya mabao matano katika Ngao ya Jamii pindi ili­pokutana katika miaka tofauti ambapo mwaka 2001, Wa­najangwani hao waliibuka na ush­indi wa mabao 2-1 na mwaka 2010 waliifunga penalti 3-1. Lakini Simba imewafunga wapinzani wao hao jumla ya ma­bao manne yakiwemo mawili kwenye ushindi wa 2-0 mwaka 2011.

WAFUNGAJI SIM­BA, YANGA ZILI­VYOKUTANA

Yanga 2-1 Simba (2001)

Mabao ya Yanga yali­fungwa na Edibily Lunyam­ila na Ally Yusuph ‘Tigana’ la Simba lilifungwa na Steven Ma­punda.

Simba 1-3 Yanga (2010) penalti

Penalti ya Simba ilifungwa na Mohamed Banka huku Emmanuel Okwi na Uhuru Seleman wakikosa penalty, na kwa upande wa Yanga zilipigwa na Godfrey Bonny, Stephano Mwasyika na Isack Boakye.

Simba 2- 0 Yanga (2011)

Wafungaji Haruna Moshi ‘Boban na Felix Sunzu.

AZAM MECHI 5, IME­CHUKUA MA R A MOJA

Azam ndiyo timu yenye historia ya kucheza Ngao ya Jamii mara nyingi zaidi na kushindwa kuchukua kombe hilo . Azam wa­mecheza mara tano kwenye mechi hizo na ku­fanikiwa kushinda mara moja pekee.

BALOZI, ADADI NA BITEKO WAKUTANA NA WAJUMBE WA CHAMA CHA MABUNGE YA JUMUIYA YA MADOLA TAWI LA CANADA



 Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama na Mbunge wa Muheza, Mhe. Balozi Adadi Rajabu (kulia) akizungumza pale ujumbe wa Wabunge kutoka Bunge la Canada ambao ni Wajumbe wa Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Tawi la Canada ulipotembelea Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  leo Mjini Dodoma, ukiwa na lengo la kubadilishana uzoefu katika utendaji wa kazi baina ya Mabunge hayo. Ujumbe huo uliongozwa na Mwenyekiti wa Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Tawi la Canada ambae pia ni Mbunge, Ndg. Yasmin Ratansi (wa pili kushoto), kushoto ni Mjumbe wa Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Tawi la Canada ambae pia ni Mbunge, Ndg. Kerry Diotte na wa pili kulia, ni Katibu wa Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Tawi la Canada Ndg. Remi Bourgault.



 Mwenyekiti wa Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Tawi la Canada ambae pia ni Mbunge, Mhe. Yasmin Ratansi (wa pili kushoto) akizungumza pale ujumbe wa Wabunge kutoka Bunge la Canada ambao ni Wajumbe wa Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Tawi la Canada ulipotembelea Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  leo Mjini Dodoma, ukiwa na lengo la kubadilishana uzoefu katika utendaji wa kazi baina ya Mabunge hayo, kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini na Mbunge wa Jimbo la Bukombe, Mhe. Dotto Biteko, anaefuta ni Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama na Mbunge wa Muheza, Mhe. Balozi Adadi Rajabu , kushoto ni Mjumbe wa Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Tawi la Canada ambae pia ni Mbunge, Mhe. Kerry Diotte na katikati ni Katibu wa Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Tawi la Canada Ndg. Remi Bourgault.



Ujumbe wa Wabunge kutoka Bungela Canada ambao ni Wajumbe wa Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Tawi la Canada walipotembelea Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakiongozwa na Mhe.Yasmin Ratansi (watatu kushoto), Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama na Mbunge wa Muheza, Mhe. Balozi Adadi Rajabu (wa pili kushoto), Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini na Mbunge wa Jimbo la Bukombe, Mhe. Dotto Biteko (wanne kushoto) na Katibu wa Bunge, Dkt. Thomas Kashililah (wa tatu kulia). Ujumbe ukiwa na lengo la kubadilishana uzoefu katika utendaji wa kazi baina ya Mabunge hayo.
(PICHA NA OFISI YA BUNGE)

MASHIRIKA YA NDEGE, TTB WAKUBALIANA



Mkurugenzi Mtendaji Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Bibi Devota Mdachi na Meneja Mkazi Shirika la Ndege la Ethiopian Airlines, Bwana Dahlak Teferi wakibadilishana hati za makubaliano ya kufanikisha maonyesho ya utalii ‘Swahili International Tourism Expo,’ jijini Dar es Salaam jana, maonyesho hayo yatakayofanyika Oktoba 13-15 mwaka huu.


Mkurugenzi mtendaji wa Bodi ya utalii Bi Devota Mdachi akizungumza katika hafla ya kutia saini ushirikiano wa kufanikisha maonyesho ya utalii ‘Swahili International Tourism Expo,’ jijini Dar es Salaam jana, maonyesho hayo yatakayofanyika Oktoba 13-15 mwaka huu, (kushoto) Mhandisi Ladislaus Matindi Mkurugenzi mtendaji Air Tanzania wapili( kulia) Bwana Dahlak Teferi Meneja wa Ethiopian Airlines, (kulia) Lima Silva Mwakilishi wa mauzo mwandamizi Shirika la ndege la Ethiopia, Ethiopian Airlines.



Mkurugenzi mtendaji wa Bodi ya Utalii Tanzania Bi Devotha Mdachi akiwa kwenye picha ya pamoja na Wadau wa Utalii mda mfupi baada ya hafla ya kutia saini ushirikiano wa kufanikisha maonyesho ya utalii ‘Swahili International Tourism Expo’ iliyofanyika Jijini Dar es Salaam jana’ wa tatu (kulia) Mhandisi Ladislaus Matindi Mkurugenzi Mtendaji Air Tanzania wa pili (kushoto) Dahlak Teferi Meneja wa Shirika la Ndege la Ethiopia, Ethiopian Airlines. Ends

Viwanda 42 Zaidi Kuunganishwa Mfumo wa Gesi


Na Said Ameir-MAELEZO

Serikali imesema kuwa viwanda vingine 42 vitaunganishwa na mfumo wa matumizi wa matunizi ya gesi asilia katika kipindi cha miaka miwili ili kuongeza tija tofauti viwanda 37 vya sasa ambavyo tayari vinatumia gesi hiyo.

Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dk. Medard Kalemani aliiambia Kamati ya Fedha ya Bunge jana kuwa Serikali imejipanga kuhakikisha kuwa changamoto zinazokwaza zoezi la kuvipatia viwanda nishati hiyo zinatatuliwa haraka.

“Tuna gesi ya kutosha futi za ujazo trilioni 57.25 ambapo hadi sasa tunatumia wastani wa futi za ujazo milioni 70 ikiwa ni kama asilimia kumi tu hivi” alieleza Waziri Kalemani.Kwa hivyo alisema azma ya Serikali ni kuona viwanda vinatumia gesi katika uzalishaji na kubanisha kuwa Tanzania inaongoza kwa kuwa na nishati hiyo katika Afrika Mashariki. 

Waziri Kalemani aliieleza kamati hiyo kuwa hivi sasa wateja wakubwa wa gesi hiyo ni viwanda lakini Serikali ipo mbioni kutekeleza mkakati wa kusambaza gesi hiyo kwa ajili ya matumizi ya nyumbani.

Katika maelezo yake kwa kamati hiyo ambayo ilitembelea kituo cha kupokelea gesi asilia huko Kinyerezi na miradi ya uzalishaji umeme kwa kutumia gesi hiyo ya Kinyerezi I na Kinyerezi II, Naibu Waziri huyo alidokeza kuwa Serikali ina mpango wa kuanzisha kiwanda cha kusindika gesi asilia ili iweze kusafirishwa nchi za nje.

Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha ya Bunge Hawa Ghasia ameitaka TPDC kutayarisha mpango maalum kwa kuainisha na kutenga maeneo maalum ambayo yatawekewa miundombinu ya gesi ili uwekezaji wa viwanda uzingatie ramani hiyo.

“Tungetengeneza kanda maalum tukaziandaa kwa ajili ya viwanda kwa kuziwekea miundombinu ya gesi tofauti na sasa ambapo serikali inalazimika kuvifuata viwanda viliko kuvipelekea nishati hiyo” alishauri Mwenyekiti huyo.Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Mwenyekiti huyo alieleza kuwa shirika hilo lina nafasi ya pekee katika kuifanya Tanzania kufikia lengo lake la kuwa nchi ya viwanda kama itatekeleza vyema miradi ya matumizi ya gesi viwandani.

Aliueleza uongozi wa TPDC na waandishi wa habari walioambatana katika ziara hiyo kuwa madhumuni ya ziara ya kamati yake katika miradi hiyo ni kuangalia utayari wa shirika hilo katika kuchangia maendeleo ya uchumi wa viwanda bila ya vikwazo.

Mwenyekiti huyo alieleza kuwa kamati yake imeridhika na kazi inayofanyika hadi sasa na kueleza matumiani ya kamati yake kuwa miradi ya Kinyerezi I na Kinyerezi II itamalizika kwa wakati na kufikia malengo yaliyowekwa. Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TPDC Mhandisi Kapulya Musomba mpango wa shirika lake sasa ni kutekeleza programu yake ya kusambza gesi nchi nzima kwa kuanzia na mikoa ya Arusha, Mbeya, Mwanza na Tanga.

Alisema shirika lake lipo tayari kukipatia kiwanda au mwekezaji nishati hiyo katika sehemu yeyote ambayo bomba la gesi hiyo limepita na kwamba ingependeza kuona Tanzania ina viwanda vingi ili gesi yote iweze kutumika humu nchini pasi na kusafirishwa nchi za nje. Mapema akijibu maswali kutoka kwa wajumbe wa Kamati hiyo, Mhandisi Musomba alisema shirika lake linatumia mifumo miwili ya usalama wa bomba lenye urefu wa kilomita 551 linalosafirisha gesi kutoka Mtwara hadi eneo hilo.

Aliitaja kuwa ni mfumo unaojitegemea wa bomba hilo ambapo zinapotokea hitilafu hujizima na wataalamu hufuatilia kuelewa hitilafu iliopo na mfumo wa pili ni ulinzi shirikishi ambao wanawatumia wananchi kulinda bomba hilo.

Mbali na viwanda 37 kuunganishwa katika mfumo wa matumizi ya gesi, shirika hilo pia limeziunganisha familia 70 katika mfumo wa matumizi ya gesi hiyo katika maeneo ya Mikocheni jijini Dar es salaam.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dk. Medard Kalemani

TAASISI YA THPS YAZINDUA MPANGO MKAKATI WA KUSAIDIA MIFUMO YA AFYA 2016-2020.



Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Afya), Dkt. Mpoki Ulisubisya akizungumza wakati wa Uzinduzi wa Mpango Mkakati wa kusaidia mifumo ya afya wa miaka mitano ambao utatekelezwa kati ya mwaka 2016-2020 na Taasisi ya Tanzania Health Promotion Support (THPS).  Tukio hilo lilifanyika jijini Dar es Salaam.



Wageni na wafanyakazi wa taasisi ya THPS waliohudhuria katika Uzinduzi wa Mpango Mkakati wa kusaidia mifumo ya afya wa miaka mitano ambao utatekelezwa kati ya mwaka 2016-2020 na Taasisi ya Tanzania Health Promotion Support (THPS). Tukio hilo lilifanyika jijini Dar es Salaam.




 
Mwanzilishi na Mwenyekiti wa Bodi wa Taasisi ya Tanzania Health Promotion Support (THPS) Dkt. Augustine Massawe akizungumza katika uzinduzi wa Mpango Mkakati wa kusaidia mifumo ya afya wa miaka mitano ambao utatekelezwa kati ya mwaka 2016- 2020. Tukio hilo lilifanyika jijini Dar es Salaam.





Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tanzania Health Promotion Support (THPS), Dkt. Redempta Mbatia akizungumza juu ya uzinduzi wa Mpango Mkakati ya kusaidia mifumo ya afya na kuelezea malengo ya taasisi hiyo kwa miaka ijayo kati ya mwaka 2016-2020. Tukio hilo lilifanyika jijini Dar es Salaam. 


 
 
Mmoja ya vijana waelimisha Rika kutoka Zanzibara akitoa somo jinsi ya kujitambua.





Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Afya), Dkt. Mpoki Ulisubisya akizindua Mpango Mkakati wa kwanza wa kusaidia mifumo ya afya wa Taasisi ya Tanzania Health Promotion Support (THPS) ambao utatekelezwa kati ya mwaka 2016-2020. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Dkt. Redempta Mbatia na wadau wengine. Tukio hilo lilifanyika jijini Dar es Salaam.



Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Afya), Dkt. Mpoki Ulisubisya (wa nne toka Kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Dkt. Redempta Mbatia (wa tako kutoka kushoto) pamoja na wadau wa afya wakionyesha chapisho la Mpango Mkakati wa kwanza wa kusaidia mifumo ya afya  wa Taasisi ya Tanzania Health Promotion Support (THPS) ambao utatekelezwa kati ya mwaka 2016-2020.
Taasisi isiyo ya kiserikali ya Tanzania Health Promotion Support (THPS) inayosaidia Wizara za afya Tanzania Bara na Zanzibar kutoa kinga ya Virusi vya Ukimwi (VVU), huduma, matibabu na msaada kwa kuimarisha mifumo ya afya imezindua mpango mkakati wa kwanza wa miaka mitano.

Akizungumza katika uzinduzi huo wa mpango mkakati uliofanyika Jijini Dar es salaam leo. Mwanzilishi na Mwenyekiti wa Bodi wa THPS, Dkt. Augustine Massawe alisema mpango mkakati wa kwanza wa taasisi hiyo ambao utatekelezwa kati ya mwaka 2016 mpaka 2020 umelenga kusaidia juhudi za Wizara ya afya, Serikali za mitaa, Washiriki wengine na Wadau kuhakikisha huduma bora za afya zinazoshugulikia afya ya umma ikiwemo magonjwa yanayoambukizwa na yasiyoambukizwa ili kuboresha matokeo ya afya kiujumla katika jamii. 

Dkt. Massawe alisema anatarajia mpango mkakati utazingatia mawazo kati ya wadau muhimu wa THPS na kujenga uamuzi wa pamoja wenye matokeo mazuri. “tunataka kugusa maisha ya Watanzania wengi kwa kuathiri ubora wa huduma za afya na kujenga taifa huru la VVU/UKIMWI. Nina matumaini kuwa mpango mkakati uliofikiriwa utakuwa kama chombo cha usimamizi wa taasisi katika kuweka vipaumbele, kuzingatia nishati na rasilimali, kuimarisha shughuli mbalimbali na kuhakikisha wafanyakazi na wadau wengine wanafanya kazi kwa malengo.

Akizungumzia juu ya uzinduzi wa mpango mkakati, Mkurugenzi Mtendaji wa THPS, Dkt. Redempta Mbatia alielezea malengo ya taasisi kwa miaka ijayo ni kutazamia mbali VVU/ UKIMWI na kushughulika na magonjwa mengine yenye vitisho katika jamii, kulenga katika uhamasishaji wa rasilimali na kuchunguza ushirikiano wa pamoja na sekta binafsi ili kuendelea kutoa huduma zake.

“Mpango mkakati huu umekuja wakati muafaka ili kuhakikisha tunafikia idadi kubwa ya watu wenye mahitaji, wakati huo huo tukikuza na kuendeleza taasisi. Tunataka kuendelea kuzingatia maeneo muhimu ikiwa ni pamoja na huduma bora za afya, uwezo endelevu wa kifedha, utawala bora na uwajibikaji wa pamoja na wafanyakazi wenye uwezo na kujitolea. Kama taasisi mpya nchini Tanzania tunathamini sana Imani, msaada na fursa ya kutumikia watanzania inayotolewa na serikali kuu, serikali za mtaa, wafadhili, washirika watekejezaji na wadau wengine muhimu kutoka pande zote mbili za jamhuri. Mwisho kabla ya kumaliza tunashukuru kwa msaada endelevu wa kifedha na kiufundi kutoka kwa wafadhili wetu: Watu wa Marekani kupitia PEPFAR/ CDC na taasisi ya taifa ya afya Marekani (NHI) , UNAIDS , Chuo kikuu cha Harvard, Chuo kikuu cha Colombia na taasisi ya mfuko wa uwekezaji kwa watoto uliopo Uingereza”. 

Aidha Dkt. Mbatia alisisitiza kuwa mwelekeo wa mpango mkakati kwa miaka mitano ni kufaidika kwa njia ya moja kwa moja na isiyo ya moja kwa moja kwa mamilioni ya Watanzania. Mpango huo umesimama kama nguzo ya kuongeza na kubuni ufumbuzi wa afya bora ya kupambana na VVU na UKIMWI, mifumo ya utoaji afya na changamoto nyingine za afya zinazoathiri Watanzania.

NAIBU WAZIRI MPINA AKUTANA NA KAMATI YA ARDHI NA MAWASILIANO YA BARAZA LA WAWAKILISHI KUTOKA ZANZIBAR



Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais, Mh. Luhaga Mpina akiongea wakati wa ziara ya Kamati ya Ardhi na Mawasiliano ya Baraza la Wawakilishi kutoka Zanzibar, iliyomtembelea Ofisini kwake jijini Dar Es Salaam wa kwanza kulia nia Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mh. Hamza Hassan Juma na wa kwanza kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati.



Sehemu ya Wajumbe wa Kamati ya Ardhi na Mawasiliano ya Baraza la Wawakilishi kutoka Zanzibar wakimsilikiza Naibu  Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais, Mh. Luhaga Mpina(hayupo pichani) wakati wa ziara yao Ofisini kwa Waziri huyo.



Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais, Mh. Luhaga Mpina akisiliza kwa makini hoja zilizokua zikitolewa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mh. Hamza Hassan Juma(kulia) wakati wa ziara hiyo.



Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais, Mh. Luhaga Mpina akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Kamati ya Ardhi na Mawasiliano ya Baraza la Wawakilishi kutoka Zanzibar, iliyomtembelea Ofisini kwake jijini Dar Es Salaam

ATCL KUENDELEA KUBORESHA HUDUMA ZA NDEGE ZANZIBAR


Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani, akiongea na Baraza la Wawakilishi la Kamati ya Ardhi na Mawasiliano kutoka Zanzibar na uongozi wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), (hawapo pichani), wakati wa ziara ya kikazi ya Kamati hiyo, jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Kamati ya Ardhi na Mawasiliano kutoka Zanzibar, Mhe. Hamza Hassan Juma, akizungumza na wajumbe na watendaji, katika ziara ya kikazi kwenye Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) Eng. Ladislaus Matindi (katikati) akifafanua jambo kwa wajumbe wa Baraza la Wawakilishi la Kamati ya Ardhi na Mawasiliano kutoka Zanzibar, wakati wa ziara ya kikazi kwenye Shirika hilo, jijini Dar es Salaam.
Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi la Kamati ya Ardhi na Mawasiliano kutoka Zanzibar wakimsikiliza kwa makini Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Eng. Edwin Ngonyani (hayupo pichani), wakati wa ziara ya kikazi katika Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), jijini Dar es Salaam.


Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi kavu na Majini (SUMATRA), Gilliard Ngewe, akifafanua jambo kwa wajumbe wa Baraza la Wawakilishi la Kamati ya Ardhi na Mawasiliano kutoka Zanzibar wakati wa ziara ya kikazi katika Mamlaka hiyo, jijini Dar es Salaam.


…………………………………………………………….


Serikali imesema kuwa Shirika la Ndege nchini (ATCL), litaendelea kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kuhakikisha inaboresha huduma za usafiri wa anga katika visiwa vya Unguja na Pemba.


Akizungumza katika kikao kilichokutanisha Baraza la Waakilishi la Kamati ya Mawasiliano na Ardhi kutoka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na uongozi wa Shirika hilo, Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Edwin Ngonyani, amesisitiza kuwa changamoto ambazo wameziwasilisha katika kikao hicho zitafanyiwa kazi ili kuleta tija kwa pande zote mbili.


“Nawahakikishia wajumbe wa kamati hii kuwa changamoto mlizonazo tutazifanyia kazi haraka kwani ATCL sasa imezaliwa upya na hivyo itahakikisha inaboresha maslahi ya kuliinua na kuliendeleza shirika ili kuweza kukidhi mahitaji ya hapa na visiwani”, amesema Naibu Waziri Ngonyani.


Aidha, Mhandisi Ngonyani ameongeza kuwa katika kuhakikisha huduma za usafiri wa anga visiwani humo zinaimarika, tayari Serikali imeshaanza kulipa deni lililokuwa linadaiwa na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege la shilingi milioni 241 ambalo shirika hilo linadaiwa kutokana na tozo ya maegesho ya ndege na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.


Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Hamza Juma, amemwomba Naibu Waziri Mhandisi Ngonyani kuangalia upya suala la ajira katika Shirika la ATCL ili liweze kubeba sura ya Muungano na kuwawezesha wataalam wenye sifa kutoka Zanzibar nao kupata nafasi hizo.


“Tunaomba Shirika na baadhi ya Taasisi zinazofanya kazi kwa kushabihiana na masuala ya Muungano kuzingatia utoaji wa ajira katika nafasi wanazozitangaza kwani Zanzibar ina wataalam wenye sifa lakini hawapati fursa” amesisitiza Mwenyekiti wa Kamati.


Naye, Mwenyekiti wa Bodi ya ATCL, Mhandisi Emmanuel Korosso, amesema kuwa Shirika hilo linaendelea kuimarika na kusambaza huduma katika viwanja mbalimbali vya ndege nchini licha ya kuwa na changamoto za uhaba wa marubani.


Katika hatua nyingine, Kamati hiyo imetembelea Makao Makuu ya Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi kavu na Majini (SUMATRA) na kupendekeza kwa Mamlaka hiyo kutoa kipaumbele katika suala la ajira na vibali kwa mabaharia kutoka Zanzibar ambao wamesajiliwa chini ya Mamlaka ya Usafiri wa Baharini Zanzibar (ZMA), kufanyika kwa wakati.


Ziara ya kamati hiyo imelenga kutatua, kupunguza na hatimaye kumaliza kero za Muungano ambazo zinagusa Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.