Monday, July 3

Mwili waokotwa kwenye bwawa la maji

Mwili wa mtu ambaye hajafahamika umeokotwa katika bwawa la maji lililopo Mtaa wa Nkende Shuleni katika Halmashauri ya Mji wa Tarime.
Hili ni tukio la tatu la watu kuuawa kisha miili yao kutupwa kwenye mabwawa ya maji katika kipindi cha miezi sita iliyopita. Hivi karibuni, mwili wa kijana ambaye alikuwa dereva wa bodaboda ulikutwa ukiwa umetupwa katika eneo hilo hilo.
Kamanda wa Mkoa wa Polisi Tarime/Rorya, Henry Mwaibambe, amethibitisha kuokotwa kwa mwili huo na kubainisha kuwa Jeshi la Polisi linafanya uchunguzi ili kuwabaini watu wanafanya mauaji hayo.
Chareles Kisege, ambaye ni mwenyekiti wa mtaa wa Nkende Shuleni na James Nyangai mwenyekiti wa mtaa wa Kimusi, wamesema matukio hayo yamezusha hofu miongoni mwa wananchi wanaoishi katika maeneo hayo.
Wamitaka serikali kuchukua hatua za haraka kuwadhibiti wauaji hao.
Licha juhudi za wananchi kutaka kuuopoa mwili huo, zoezi hilo limekuwa zito na gumu kutokana na kukosa zana.
Hata hivyo, mwenyekiti wa chama cha waendesha bodaboda wilayani hapa, Samwel Kegoye, amesema ingawa taarifa zinaonyesha kuwa mtu huyo aliyeuawa ni dereva wa bodaboda, wao badoi hawajapata taarifa hizo rasmi.

Miswada bungeni yapingwa kwa mavazi meupe na meusi

Dodoma. Wabunge wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni leo (Julai 3) wamevaa mavazi meupe na meusi wakipinga miswada inayozungumzia usimamizi na umiliki wa rasilimali kuwasilishwa kwa hati ya dharura.
Kiongozi wa kambi hiyo, Freeman Mbowe amesema hatua hiyo inalenga kuonyesha msiba kwa Taifa unaoendelea kutokea katika uchumi kutokana na kukosekana kwa muda wa kutosha kuchambua na kujadili miswada hiyo.
Miswada hiyo ni ya sheria ya mapitio na majadiliano kuhusu masharti katika mikataba ya maliasili za nchi na muswada wa sheria ya mamlaka ya nchi kuhusu umiliki wa maliasili.
Alipoulizwa kama kesho watavaa mavazi hayo kwa sababu hata muswada wa marekebisho ya sheria mbalimbali wa mwaka 2017 umewasilishwa kwa hati ya dharura, Mbowe amesema kesho ni kesho.

WANADAYASFORA WA MAREKANI WATOA HUDUMA ZA MATIBABU ZANZIBAR


Wananchi wa Tanzania wanaoishi Marekani wanadiaspora wakishirikiana na Madaktari bingwa wapo nchini kwa ajili ya kutoa huduma za matibabu ya maradhi mbalimbali yanayowasumbua wananchi.

Zoezi la kutoa huduma hizo za matibabu bure linafanyika kwa muda wa siku tatu katika Hospitali ya Mnazi mmoja.

Akizungumza na waandishi wa habari huko katika kitengo cha maradhi ya ngozi kwenye hospitali kuu ya Mnazi mmoja, Mwanadiaspora Idi Seif Sandaly amesema wameamua kuja nchini hapa kutoa huduma hizo ili kuwasaidia wananchi wenye matatizo mbalimbali.

“Tumekuja Zanzibar kwa lengo la kuwasaidia wananchi ambao wana maradhi mbali mbali na kuwapatia matibabu kwa kupitia jumuiya yetu ya marekani Health Education Development kwa kutibu maradhi ya ngozi , sukari na pressure pamoja na maradhi ya akinamama.” Amesema Mwanadiaspora huyo.

Sandaly amesema wapo kwa muda wa siku tatu na wamekuja na dawa za kutibia maradhi hayo ambapo dawa hizo wanazitoa bure bila ya gharama zozote kwa wananchi.

Amesema katika matibabu yao wanatarajia kutoa huduma kwa zaidi ya Wananchi 3,000 watakaofika katika Hospital hiyo ya Mnazi mmoja.

Akifafanua kuhusu gharama za Dawa hizo ambazo wamekuja nazo kutoka Marekani amesema zaidi ya Dola Million moja za Marekeni zimetumika kwa ajili ya kununulia Dawa hizo.

Hata hivyo ameongeza kuwa Nusu za Dawa hizo zitatumika Zanzibar na Nusu yake zitapelekwa Mkoa wa Bukoba kwa lengo la kusaidia matibabu mkoani huko

Nae Daktari wa maradhi ya Ngozi kutoka Marekeni Dkt Mamotheo Lepheana amesema amefarijika kuona wananchi wamejitokeza kwa wingi hasa wa maradhi ya ngozi.

Sambamba na hayo mgonjwa aliyepata matibabu hayo ya ngozi Masika Juma Mussa mkaazi wa Mwera amesema ameshukuru kupatiwa huduma hiyo na kuiomba serikali iendeleze kuleta wataalam kama hao wanaotaka kusaidia jamii .

Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa Shirika hilo la kutoa huduma za Elimu ya afya Asha Mustafa Nyang’anyi amesema ameamua kuja Zanzibar kwa sababu wananchi wa hapa ni wakarimu na wanaojali kusaidiwa.
Mkurugenzi mtendaji wa Shirika la kutoa huduma za Elimu ya afya Nchini Marekani Bi. Asha Mustafa Nyang’anyi akizungumza na wandishi wa habari kuhusu ujio wao hapa Zanzibar.
Bwana. Amiri Muhammed Amiri akimuonesha fangas Daktari bingwa wa ngozi Mamotheo alipokuwa akitoa matibabu katika hospitali ya Mnazi mmoja Mjini Zanzibar. 
Baba wa mtoto Abdulmajid akiwaonesha madaktari bingwa wa maradhi ya ngozi namna mwanawe alivyodhurika kwa kufanya mabaka mwilini katika hospitali ya Mnazimmoja mjini Zanzibar. Picha na Makame Mshenga.


Na Mwashungi Tahir-Maelezo Zanzibar 03-07-2017

Wananchi wa Tanzania wanaoishi Marekani wanadiaspora wakishirikiana na Madaktari bingwa wapo nchini kwa ajili ya kutoa huduma za matibabu ya maradhi mbalimbali yanayowasumbua wananchi.

Zoezi la kutoa huduma hizo za matibabu bure linafanyika kwa muda wa siku tatu katika Hospitali ya Mnazi mmoja.

Akizungumza na waandishi wa habari huko katika kitengo cha maradhi ya ngozi kwenye hospitali kuu ya Mnazi mmoja, Mwanadiaspora Idi Seif Sandaly amesema wameamua kuja nchini hapa kutoa huduma hizo ili kuwasaidia wananchi wenye matatizo mbalimbali.

“Tumekuja Zanzibar kwa lengo la kuwasaidia wananchi ambao wana maradhi mbali mbali na kuwapatia matibabu kwa kupitia jumuiya yetu ya marekani Health Education Development kwa kutibu maradhi ya ngozi , sukari na pressure pamoja na maradhi ya akinamama.” Amesema Mwanadiaspora huyo.

Sandaly amesema wapo kwa muda wa siku tatu na wamekuja na dawa za kutibia maradhi hayo ambapo dawa hizo wanazitoa bure bila ya gharama zozote kwa wananchi.

Amesema katika matibabu yao wanatarajia kutoa huduma kwa zaidi ya Wananchi 3,000 watakaofika katika Hospital hiyo ya Mnazi mmoja.

Akifafanua kuhusu gharama za Dawa hizo ambazo wamekuja nazo kutoka Marekani amesema zaidi ya Dola Million moja za Marekeni zimetumika kwa ajili ya kununulia Dawa hizo.

Hata hivyo ameongeza kuwa Nusu za Dawa hizo zitatumika Zanzibar na Nusu yake zitapelekwa Mkoa wa Bukoba kwa lengo la kusaidia matibabu mkoani huko

Nae Daktari wa maradhi ya Ngozi kutoka Marekeni Dkt Mamotheo Lepheana amesema amefarijika kuona wananchi wamejitokeza kwa wingi hasa wa maradhi ya ngozi.

Sambamba na hayo mgonjwa aliyepata matibabu hayo ya ngozi Masika Juma Mussa mkaazi wa Mwera amesema ameshukuru kupatiwa huduma hiyo na kuiomba serikali iendeleze kuleta wataalam kama hao wanaotaka kusaidia jamii .

Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa Shirika hilo la kutoa huduma za Elimu ya afya Asha Mustafa Nyang’anyi amesema ameamua kuja Zanzibar kwa sababu wananchi wa hapa ni wakarimu na wanaojali kusaidiwa.

RAIS DKT. MAGUFULI AWASILI MKOANI MWANZA AWASALIMIA WAKAZI WA KONA YA BWIRU, GHANA NA AINGIA KUKAGUA UWANJA WA NYAMAGANA



 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongela mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Mwanza.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Viongozi wa Dini mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Mwanza.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia ngoma za asili kutoka kikundi cha Bujora mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Mwanza.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiombewa sala na Viongozi mbalimbali wa dini kutoka Kanda ya ziwa mara baada ya kuwasili mkoani Mwanza. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia wakazi wa Kona ya bwiru katika barabara ya Airport wakati akitokea uwanja wa ndege wa Mwanza.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia wakazi wa katikati ya jiji la Mwanza waliokusanyika kumpokea.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia wakazi wa katikati ya jiji la Mwanza waliokusanyika kumpokea.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia wakazi wa katikati ya jiji la Mwanza waliokusanyika kumpokea.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia wakazi wa katikati ya jiji la Mwanza waliokusanyika kumpokea.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia wakazi wa katikati ya jiji la Mwanza waliokusanyika kumpokea.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia wakazi wa katikati ya jiji la Mwanza waliokusanyika kumpokea.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akinunua Karanga kutoka kwa Mmachinga anayefanya biashara katikati ya jiji la Mwanza.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akinunua Karanga kutoka kwa Mmachinga anayefanya biashara katikati ya jiji la Mwanza.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono wakazi wa katikati ya jiji la Mwanza wakati akielekea Uwanja wa Nyamagana kuangalia mechi kati ya Buhongwa United na Timu ya Nyamwaga.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono wakazi wa katikati ya jiji la Mwanza wakati akielekea Uwanja wa Nyamagana kuangalia mechi kati ya Buhongwa United na Timu ya Nyamwaga.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Wachezaji wa Buhongwa Fc mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Nyamagana.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono washabiki wa mpira wa miguu wakati akitoka katika uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza. PICHA NA IKULU

Rugemalira, Sethi waongezewa mashtaka sita


Mfanyabiashara  Harbinder  Singh Sethi na James  Rugemalira wamepandishwa kizimbani kwa mara nyingine katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka 12, badala ya mashtaka sita waliyosomewa awali.

Miongoni mwa mashtaka hayo 12 ya  uhujumu uchumi yamo mashtaka matano ya kutakatisha fedha na kuisababisha hasara ya USD 22, 198, 544.60 na Sh 309,461,300,158. 27.
Akiwasomea hati mpya ya mashtaka, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Shedrack Kimaro kwa Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi alidai wanakabiliwa na mashtaka ya kula njama, kujihusisha mtandao wa uhalifu, kighushi,  kutoa nyaraka za kughushi, kujipatia fedha kwa njia za udanganyifu, kuisababishia Serikali hasara na kutakatisha fedha.

Washtakiwa hao katika shtaka la kwanza wanadaiwa, Rugemarila ambaye ni Mkurugenzi wa VIP na mmiliki mwenza wa zamani wa IPTL, Sethi ambaye ni Mwenyekiti Mtendaji wa PAP wanadaiwa kuwa   kati ya Oktoba 18, 2011 na Machi 19, 2014 jiji Dar es Salaam walikula njama katika nchi za Afrika Kusini, Kenya na India ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.

Kimaro alidai katika shtaka la pili la kujihusisha na mtandao, washtakiwa hao kati ya Oktoba 18, 2011na Machi 19, 2014 jijini Dar es Salaam wakiwa siyo watumishi wa umma na watumishi wa umma  walitekeleza mtandao huo wa uhalifu kwa lengo la kujipatia faida.

Kwa upande shtaka la tatu, Sethi  anadaiwa  kuwa   Oktoba 10, 2011 katika mtaa wa Ohio Ilala Dar es Salaam akiwa na nia ya ulaghai alighushi fomu namba 14 ya usajili wa makampuni  na kuonyesha yeye ni mtanzania anayeishi Kitalu namba 887 Mtaa wa Mrikau Masaki wakati akijua ni uongo.

Seth katika shtaka la nne anadaiwa kutoa nyaraka ya kughushi ambayo ni fomu namba 14a ya usajili wa kampuni kwa ofisa msajili wa kampuni, Seka Kasera kwa njia ya kuonyesha kwamba yeye ni mtanzania na Mkazi wa Mtaa wa Mrikau.

Katika shtaka la tano, washtakiwa wote, wanadaiwa kuwa kati ya  Novemba 28/29, 2011 na Januari 23, 2014 makao makuu Benki ya Stanbic Kinondoni  na Benki ya Mkombozi Tawi St Joseph kwa ulaghai washtakiwa hao walijipatia kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT), walijipatia USD 22,198,544.60 na Sh 309, 461,300,158.27.  
Katika shtaka sita la kusababisha hasara,  washtakiwa hao wanadaiwa kuwa   Novemba 29, 2013 katika Benki ya Stanbic tawi la  kati Kinondoni kwa vitendo vyao waliisababishia Serikali hasara ya USD 22, 198, 544.60 na Sh 309,461,300,158.27.

Kimaro alidai katika la saba, kuwa kati ya Novemba 29, 2013 na Januari 23, 2014 maeneo tofauti Dar es Salaam kwa pamoja walitenda kosa la kutakatisha fedha kwa kuchukua fedha kutoka BoT USD 22,198,544.60 na Tsh 309,461,300, 158.27 wakati wakijua fedha hizo zao la kujihusisha na genge la uhalifu.

Shtaka la nane, Kimaro alidai kuwa Novemba 29, 2013 katika tawi la kati la Benji ya Stanbic Tanzania Wilaya ya Kinondoni Sethi alitakatisha fedha kwa kuchukua BoT USD 22,198,544.60 wakati akijua fedha hizo zimetokana na zao la kujihusisha na genge la uhalifu.

Kwa upande wa shtaka la tisa, Sethi anadaiwa kuwa kati ya Novemba 29, 2013 na Machi 14,2014 katika tawi la kati la Benji ya Stanbic Kinondoni Dar es Salaam alitakatisha fedha, Sh 309,461,300,158.27 kutoka BoT wakati akijua fedha hizo zimetokana na zao la kujihusisha na genge la uhalifu.

Shtaka ya kumi,  inadaiwa Januari 23, 2014 katika Benki ya Mkombozi tawi la St Joseph Cathedral, Rugemalila  alitakatisha fedha, Sh 73, 573, 500,000 kutoka kwa Seth wakati akijua fedha hizo zimetokana na zao la kujihusisha na genge la uhalifu.

Kwa upande wa shtaka la 11, Kimaro alidai kuwa Januari 23,2014 katika Benki ya Mkombozi tawi la St Joseph Cathedral, Rugemarila alitakatisha fedha USD 22,000,000 kutoka kwa Seth wakati akijua fedha hizo ni zao la uhalifu.

Shtaka la 12, Seth anadaiwa kuwa Januari 28, 2014 katika tawi la kati la Benki ya Stanbic Wilaya ya Kinondoni alihamisha Rand (zar 1,305,800 kwenda kwenye akaunti namba 022655123 katika Standard bank Land Rover Sandton Johannesburg wakati akijua katika kipindi anahamisha fedha hizo zimetokana na zao la kujihusha na genge la uhalifu.

Washtakiwa hawakuruhusiwa kuongea chochote kwa sababu mahakama ya Kisutu haina mamlaka ya kusikiliza kesi hao.

Upande wa mashtaka ulidai upelelezi bado haujakamilika na washtakiwa wamepelekwa rumande hadi Julai 14, 2017.
Hata hivyo mashtaka ya kutakatisha fedha yanayowakabili washtakiwa hao hayana dhamana.

NIDA YAIBUKA MSHINDI WA KWANZA KATIKA KUNDI LA BANDA BORA KWA WIZARA NA TAASISI ZA SERIKALI


 Mwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NIDA ndugu Alphonce Malibiche akipokea tuzo toka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dr. John Pombe Joseph Magufuli wakati wa sherehe za ufunguzi rasmi wa maonyesho ya 41 ya Kimataifa ya Sabasaba yaliyofanyika hivi karibuni. NIDA ilikuwa mshindi wa kwanza katika kundi la banda bora kwa Wizara na Taasisi za Serikali.
 Wananchi wakijaza fomu za maombi ya Vitambulisho vya Taifa na huduma kwenye Banda la NIDA wakati wa maonyesho ya 41 ya Kimataifa ya Sabasaba. 
 Wananchi wakipata huduma kwenye banda la NIDA, ambapo huduma ya Usajili na Utambuzi inatolewa, kuchukua alama za kibaiolijia pamoja na utoaji Vitambulisho kwa wale watakaokidhi vigezo. 
 Baadhi ya Watumishi wa NIDA walioshiriki kufanikisha Maonyesho hayo wakiwa na nyuso za furaha baada ya kupokea Tuzo ya ushindi. Kutoka kulia ni Edna Wanna, akifuatiwa na Agnes Gerrald, Raymondn Sengate na Sarah Mashalla.
 Katikati ni Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na mratibu wa Banda la Maonyesho la NIDA akiwa ameshikiliwa Tuzo ya Ushindi pamoja na Ndugu Alphonce Malibiche Kaimu Mkuu wa Idara ya Uzalishaji Vitambulisho (kushoto) na kulia ni Ndugu Jamal Kaoneka wa Idara ya Uhamiaji wadau wakuu wa NIDA katika kufanikisha Usajili wa Vitambulisho.
Wa kwanza kulia ni Mkurugenzi mtendaji wa TRL ndugu Masanja Kadogosa akiwa kwenye picha ya pamoja na maafisa wa NIDA baada ya kutembelea Banda la NIDA na kuwapongeza kwa ushindi wa kishindo. Wengine katika picha kushoto ni ndugu Gideon Ndalu Mkurugenzi wa Mifumo ya Tehama NIDA na katikati ni Ndugu Alphonce Malibiche Kaimu Mkuu wa Idara ya Uzalishaji Vitambulisho.

RAIS DKT. MAGUFULI ALIPOTEMBELEA BANDA LA CRDB BANK KATIKA MAONYESHO YA SABASABA



Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiongozana na Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Bank PLC, Dkt. Charles Kimei wakati alipotembelea Banda la CRDB  kwenye Maonyesho ya Maonyesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa (sabasaba), yaliyoanza Juni 28 - Julai 8, 2017 ambapo kwa mwaka huu yameongezewa siku tano zaidi na kutarajiwa kumalizika Julai 13, 2017, yaliyozinduliwa na Rais mwishoni mwa wiki katika Viwanja vya Mwalimu J.K. Nyerere, Kilwa Road jijini Dar es salaam.
 Rais Dkt. John Pombe Magufuli akimuuliza jambo Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Bank PLC, Dkt. Charles Kimei wakati alipotembelea Banda la CRDB  kwenye Maonyesho ya Maonyesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa (sabasaba), yaliyoanza Juni 28 - Julai 8, 2017 ambapo kwa mwaka huu yameongezewa siku tano zaidi na kutarajiwa kumalizika Julai 13, 2017, yaliyozinduliwa na Rais mwishoni mwa wiki katika Viwanja vya Mwalimu J.K. Nyerere, Kilwa Road jijini Dar es salaam.
 Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Bank PLC, Dkt. Charles Kimei akieleza jambo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli wakati alipotembelea Banda la CRDB  kwenye Maonyesho ya Maonyesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa (sabasaba), yaliyoanza Juni 28 - Julai 8, 2017 ambapo kwa mwaka huu yameongezewa siku tano zaidi na kutarajiwa kumalizika Julai 13, 2017, yaliyozinduliwa na Rais mwishoni mwa wiki katika Viwanja vya Mwalimu J.K. Nyerere, Kilwa Road jijini Dar es salaam.
 Baadhi ya Wafanyakazi wa CRDB Bank PLC wakiendelea kutoa huduma za kibenki kwa wateja waliotembelea Banda lao.
Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Bank PLC, Dkt. Charles Kimei akielekeza jambo kwa baadhi ya watendaji wa benki hiyo, katika Banda la CRDB  kwenye Maonyesho ya Maonyesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa (sabasaba), yaliyoanza Juni 28 - Julai 8, 2017 ambapo kwa mwaka huu yameongezewa siku tano zaidi na kutarajiwa kumalizika Julai 13, 2017, yaliyozinduliwa na Rais mwishoni mwa wiki katika Viwanja vya Mwalimu J.K. Nyerere, Kilwa Road jijini Dar es salaam.

LAPF YAONGEZA WATEJA WA PENSHENI KATIKA MAONESHO YA SABASABA


 AfisaMatekelezo wa LAPF Agnes William akizungumza na mmoja wa wateja waliotembelea banda la mfuko huo wa hifadhi ya jamii katika maonesho ya kimataifa ya Sabsaba
 Mhasibu wa LAPF, Betty Mlewa akiwasikiliza wateja waliotembelea banda la mfuko huo wa hifadhi ya Jamii katika Maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya Sabasaba jijini Dar esSalaam
 Afisa Mfumo Robert Daniel na Afisa Matekelezo ,John Mwita wakiwaelekeza wateja jinsi ya kujaza fomu ya kujiunga na mfuko wa Pensheni wa LAPF katika maonesho ya 41 ya Biashara  Sabasaba jijini Dar es Salaam
 Afisa Ugavi wa LAPF ,Charles Makyao akitoa maelezo kwa mteja alipotembelea banda la mfuko huo wa hifadhi ya Jamii katika Maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya Sabasaba jijini Dar esSalaam
 Wateja waliotembelea banda la mfuko huo wa  Pensheni wa LAPF   katika Maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya Sabasaba jijini Dar esSalaam wakipatiwa huduma
 Wateja waliotembelea banda la mfuko huo wa  Pensheni wa LAPF   katika Maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya Sabasaba jijini Dar esSalaam wakipatiwa huduma

MAONESHO YA SABASABA 2017: WENGI WAJIUNGA NA PSPF KUPITIA MPANGO WA UCHANGIAJI WA HIARI PSS


 Meneja wa mpango wa uchangiaji wa Hiari, (PSS), wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Bi. Mwanjaa Sembe, (kulia), akimkabidhi kadi ya uanachama wa Mfuko huo kupitia mpango wa uchangiaji wa hiari, Mwanafunzi wa chuo cha Uhasibu (TIA), Bi.Demetriz Bayona, baada ya kujiunga na Mfuko huo leo Julai 2, 2017. 

Wananchi wengi waliotembelea banda la Mfuko huo leo, wamejiunga na mpango huo baada ya kupatiwa elimu na faida ambazo mwanachama anapata endapo atajiunga na mpango wa uchangiaji wa hiari ambapo kujiunga hakuna masharti isipokuwa kwa mtu yeyote mwenye kazi ya kumuingizia kipato na atatakiwa kuchangia au kuweka akiba ya kima cha chini cha shilingi elfu 10 kila mwezi. 

Miongoni mwa faifa ambazo mwanachama aliyejiunga na mpango huo ni pamoja na kujipatia bima ya afya, itakayomuwezesha kupata matibabu yeye mwanachama na wategemezi wake watatu. Lakini pia kujipatia mafao mablimbali yakiwemo fao la elimu, lakini pia mkopo wa nyumba na viwanja kutegemea na akiba ambayo mwanachama amejiwekea.
 Wanachama wapya wa PSPF wakijaza fomu za kujiunga na mpango wa PSS
 Bi Amina Mtoo akijaza fomu za kujiunga na uanachama wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF kupitia mpango wa uchangiaji wa hiari, (PSS), leo Julai 2, 2017
 Mwanachuo wa chuo cha Uhasibu jijini Dar es Salaam, Bi.Demetria Bayona, akisikiliza kwa makini faida za kujiunga na PSPF kupitia  mpango wa PSS kutoka kwa afisa wa Mfuko huo. Baada ya kuelewa faida zake, Mwanachuo huyo hatimaye alijiunga na kupatiwa kadi yake ya uanachama ndani ya dakika 20.
 Menenja wa Mpango wa uchangiaji wa hiari, (PSS), wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Bi. Mwanjaa Semba, (kulia), akitoa somo kwa mwananchi aliyetembelea banda la Mfuko huo kwenye maonesho ya 41 ya biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam leo Julai 2, 2017
 Meneja Usimamizi wa na utawala wa mifumo ya TEHAMA, wa  Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Bw. Bernard Ntelya, (kushoto), akimpatia maelezo mwananchi huyu aliyetembelea banda la PSPF Julai 2, 2017
 Afisa kutoka Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Hifadhi ya Jamii, (SSRA), (kulia), akifuatilia jinsi maafisa wa PSPF wanavyotoa huduma kwa wanachama na wananchi wanaotembela banda la Mfuko huo. SSRA imeweka maafisa wake kila banda la linalotoa huduma ya hifadhi ya Jamii ili kusikiliza malalamiko ya wanachama husika wa Mfuko hiyo.
 Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Bw. William Erio, (kushoto), akikaribishwa na Afisa Uhusiano wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Bi. Coletha Mnyamani alipotembelea banda hilo leo Julai 2, 2017.
 Afisa Uendeshaji wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Bw. Isack Kimaro, (kulia), akimuhudumia mwananchi huyu aliyefika kupata huduma kwenye banda la Mfuko huo leo Julai 2, 2017.
 Afisa wa PSPF, (kushoto), akimuhudumia mwananchi huyu aliyefika kupata huduma za Mfuko huo
 Bw. Kimaro (kulia), akimsaidia kutambua michango yake mwanachama huyu aliyefika kwenye banda la PSPF
 Afisa uendeshaji wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF anayeshughulikia masuala ya uchangiaji wa hiari (PSS), Bi. Asmahan H. Haji, akiwajibika ipasavyo kwenye dawati lake
 Bi Asmahan (kulia), akimkabidhi kadi ya uanachama wa PSPF kupitia mpango wa PSS, Bi.Amina Mtoo, ambaye alisindikizwa na mchumba wake, Bw. Ayoub Issa, leo Julai 2, 2017
 Afisa Uhusiano wa PSPF, Bi. Coletha Mnyamani, (kulia), akimkabidhi kadi ya uanachama wa PSPF, Bi. Gloria P. Nyange, akiwa na mwanae wa miaka minne Winprecious Noel baada ya kujiunga na PSS.
 Bi Mnyamani akimkabidhi kadi na nyaraka mbalimbali zinazoelezea jinsi mwanachama huyu mpya Bw.Kamaga Salim Kilolo, aliyejiunga na mpango wa uchagiaji wa hiari PSS.
 Mwananchi akijaza fomu chini ya usaidizi wa Afisa uendeshaji msaidizi wa PSPF
 Bi Asmahan H. Haji, (kulia), akimkabidhi kadi ya uanachama wa PSPF, Bi.Sabah A. Dossa, baada ya kujiunga na mpango wa PSS.
 Kabla ya kujiunga na mpango wa PSS, Bi. Amina Mtoo, (wakwanza kushoto) na mchumba wake, Bw. Ayoub Issa, walipata fursa ya kupewa elimu ya kina juu ya kujiunga na mpango huo na faida ambazo mwanachama atapata ikiwemo bima ya afya ambayo itawahusu wawili hao na wategemezi wao wawili
Bi. Mnyamani akimuhudumia mstaafu