Wednesday, October 25

DAS IRINGA AWATAKA WALIMU KUTUMIA KINGA



Katibu tawala wa wilaya ya Iringa Joseph Chintinka akiwa kwenye mkutano mkuu wa chama cha walimu Tanzania (CWT) wilaya ya Iringa manispaa akizungumza na baadhi ya walimu walihudhuria mkutano huo. 
Baadhi ya walimu waliokuwa wanaimba wimbo wa walimu wakati wa mkutano mkuu wa chama cha walimu Tanzania (CWT) wilaya ya Iringa manispaa uliofanyika katika ukumbi wa chuo kikuu huria tawi la Iringa.

Na Fredy Mgunda, Iringa. 

Walimu wa halmashauri ya manispaa ya Iringa wametakiwa kutumia kinga (kondomu) ili kujikinga na magonjwa ya zinaa ambayo yamekuwa yakipunguza nguvu kazi ya taifa. Hayo yamesemwa na katibu tawala wa wilaya ya Iringa Joseph Chintinka wakati wa mkutano mkuu wa chama cha walimu Tanzania (CWT) wilaya ya Iringa manispaa.

Chintinka alisema kuwa kumekuwa na ongezeko la waathirika wa ugonjwa wa ukimwai kutokana na kufanya mapenzi bila kutumia kondomu.



“Jamani hapa Iringa kuna tatizo kubwa la ugonjwa wa ukimwi hivyo niwaombe walimu wangu tutumie kondomu ili kujiepusha na gonjwa hili vinginevyo vizazi vyetu vyote vitaambukizwa ukimwi” alisema Chintinka

Chintinka alisema njia ya kuwa salaama kuepukana na gonjwa hili ni kujikinga kwa kutumia kondomu maana hata watoto wetu wameathirika kutokana na wazazi kutokuwa makini na matumizi ya kinga

“Naombeni tuwakinge hawa watoto wetu ambao wameathirika ili wasiwaambukize watoto wengine maana bila hivyo tutakuwa na kizazi kilichoathirika” alisema Chintinka

Aidha Chintinka aliwaomba walimu walioathirika kujitokeza ili kupewa lishe ambayo inatolewa na serikali bure hivyo walimu wametakiwa kujitokeza na kuweka wazi kwa mwagili wake ili aweze kupata mgao wa pesa za lishe.

“Jamani walimu fungu la lishe kwa walimu walioathirikia ni nono kweli naombeni walimu mjitokeze ili mfaidi fungu hili nono maana mimi nafahamu sisi ndio tunaotenga naombeni fikisheni ujumbe huu kwa walimu wengine ambao hawajafika hapa” alisema Chintinka

Chintinka aliwataka watumishi wanaotoa siri za watumishi walioathirika kuacha tabia hiyo mara moja ili kuwaweka huru waathirika na wengine waweze kujitokeza na wapate lishe iliyotengwa na wilaya.

Kwa upande wake mwenyekiti wa chama hicho manispaa ya Iringa MWL. Zawadi Mgongolwa alikiri kuwepo kwa viongozi wa sekta hiyo ambao wemekuwa wakitoa siri za walimu na watumishi walioathirika na ugonjwa wa ukimwi.

"Kwa kweli mgeni rasmi umeongea ukweli kero kubwa kwa walimu ni kutolea siri nje kitu kinachowafanya walimu waathirika kujificha na maradhi yao” alisema Mgongolwa

Naye Katibu wa Chama cha Walimu wilaya ya Iringa mwl. Fortunata Njalale alimpongeza mgeni rasmi kwa ujumbe wake ambao umekuwa faraja kwa walimu na kuwaongezea hali ya kwenda kufanya kazi ya uwalimu kwa kujituma na kuongeza ufaulu kwa wanafunzi wao.

NAIBU WAZIRI MHANDISI ATASHASTA NDITIYE AFANYA ZIARA JNIA

JENGO la tatu la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA-TBIII) linalotarajiwa kukamilika Desemba 2018, litafungwa mfumo wa huduma ya viza kwa njia ya mtandao (e-visa), ambao utarahisha na kuharakisha upatikanaji wake.

Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Uhamiaji cha JNIA, Bw. Kaanankira Mbise amemwambia jana Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Uchukuzi na Mawasiliano), Mhe. Mhandisi Atashasta Nditiye alipotembelea eneo la uombeaji viza kwa abiria wa kimataifa wanaowasili, kuwa wanatarajia kutumia huduma hiyo ambayo ni rahisi na haraka.

“Tayari mkakati umeanza wa kuanzisha huduma hii ya e-visa hivyo tukifanikiwa utafungwa katika jengo hili jipya, ambapo itasaidia kwa abiria kuipata huduma hiyo kwa haraka kwani itatumia mtandao,” amesema Bw. Mbise.Hata hivyo, Bw. Mbise amesema kwa sasa wameboresha huduma hiyo kwa wasafiri wanaowasili katika jengo la pili la abiria (JNIA-TBII) , ambapo tayari wamepatiwa mashine nne za kisasa zinazosaidia kupunguza msongamano wa abiria wenye kuhitaji huduma hiyo, hususan kipindi cha mchana chenye ujio wa ndege nyingi za nje ya nchi.

“Hizi mashine zimeharakisha upatikanaji wa huduma kwani tumeweza kuhudumia abiria wengi kwa wakati mmoja, na msongamano umepungua kiasi tofauti na awali mashine zilikuwa chache.” amesema Mbise.Naye Mhe. Mhandisi Nditiye amesema baada ya ziara yake amegundua mashine za viza ni za muda mrefu na zinahudumia abiria mmoja kwa mrefu, na tayari ameuagiza uongozi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), kuwasilisha kwa maandishi mapendekezo yao ya namna ya kuharakisha huduma hiyo, ili serikali iyafanyie kazi kwa kusaidia kuondoa kero hiyo.

“Nimegundua kuna baadhi ya mashine za viza zimeongezwa lakini pia zilizopo zimechoka kwani ni za muda mrefu na zinahudumia abiria mmoja kwa muda mrefu na hii inaharibu sifa ya kiwanja chetu kwa wageni wanaokuja hapa nchini,” amesema Mhandisi Nditiye.Hata hivyo, amesema wanampango wa kuongeza madirisha ya benki yanayolipia viza hizo ili kuharakisha huduma hiyo, ambapo sasa ni machache kulinganisha na idadi kubwa ya abiria wanaowasili kwa ndege kubwa. Ndege hizo ni Emirates, Etihad, Oman Air, Qatar, South Africa Air na Ethiopia, ambazo zimekuwa zikipishana kwa muda mfupi.

Naye Kaimu Mkurugenzi wa TAA, Richard Mayongela amesema tayari wanampango wa kuongeza upana wa eneo hilo la wasafiri wanaowasili wa kimataifa, ambapo sasa kumekuwa na msongamano kutokana na ufinyu wake.“Hili jengo linazaidi ya miaka 30 na ukiangalia abiria waliokuwa wamekadiriwa wakati ule lilikuwa likikidhi mahitaji, lakini sasa abiria wameongezeka na eneo limekuwa dogo, hivyo tayari tumeanza kwa kuondoa baadhi ya ofisi ili kuongeza upana wake, ninaimani litapunguza msongamano uliopo sasa,” amesema Bw. Mayongela. 

Lakini pia Bw. Mayongela amesema sasa wapo katika mazungumzo na Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA), ili kuangalia namna bora ya kuzipangia muda ndege zinazopishana muda mdogo kwa wakati wa mchana ili ziachiane muda mrefu, ambapo kutasaidia kupunguza msongamano.Awali eneo hilo linakumbwa na changamoto kubwa ya msongamano wa abiria wanaohitaji huduma ya viza baada ya uchache mashine zinazosimamiwa na Idara ya Uhamiaji zilizokuwepo na kufanya abiria wanaohitaji huduma hiyo kutumia muda mrefu kuipata. 
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Uchukuzi na Mawasiliano), Mhe. Mhandisi Atashasta Nditiye (wa kwanza kushoto) akiwaeleza jambo Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Richard Mayongela (kulia) na Kaimu Mkurugenzi Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Bw. Johannes Munanka katika eneo la kuchukua mizigo baada ya kuwasili.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Richard Mayongela (aliyenyoosha mkono), akimfafanulia jambo Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Uchukuzi na Mawasiliano), Mhe. Mhandisi Atashasta Nditiye (wa nne kulia) wakiwa kwenye eneo la abiria wanaowasili kutoka nje ya nchi.
Bw. Kaanankira Mbise, Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Uhamiaji Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), akieleza namna abiria anavyopata huduma ya viza mbele ya Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Uchukuzi na Mawasiliano), Mhe. Mhandisi Atashasta Nditiye (kushoto), huku Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Richard Mayongela (kulia) akisikiliza kwa makini.

RAIS MHE.DKT. MAGUFULI APOKEA HATI ZA UTAMBULISHO KUTOKA KWA MABALOZI WA NCHI TATU


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 25 Oktoba, 2017 amepokea hati za utambulisho za Mabalozi watatu waliopangiwa kuziwakilisha nchi za Oman, Uholanzi na China hapa nchini.

Waliowasilisha hati zao kwa Mhe. Rais Magufuli, Ikulu Jijini Dar es Salaam ni Mhe. Ali Abdullah Al Mahruqi – Balozi wa Oman hapa nchini, Mhe. Jeroen Verheul – Balozi wa Uholanzi hapa nchini na Mhe. Wang Ke – Balozi wa China hapa nchini.

Mhe. Rais Magufuli amewapongeza Mabalozi hao kwa kuteuliwa kuziwakilisha nchi zao hapa nchini na amewahakikishia kuwa Serikali yake itafanya kazi nao kwa ukaribu ili kuendeleza na kukuza zaidi ushirikiano kati ya nchi hizo na Tanzania hususani katika uchumi.

“Nimefurahishwa sana na ziara iliyofanywa na Mawaziri wa Oman hapa nchini, naomba ufikishe shukrani zangu kwa Mfalme wa Oman Mtukufu Sayyid Qaboos bin Said Al Said, naamini yote tuliyozungumza ikiwemo kubadilishana uzoefu katika mafuta na gesi, uwekezaji katika viwanda na ujenzi wa miundombinu tutayatekeleza kwa manufaa ya wananchi wa nchi zetu” amesema Mhe. Rais Magufuli alipozungumza na Balozi Ali Abdullah Al Mahruqi wa Oman.

Mhe. Rais Magufuli amemuambia Balozi Jeroen Verheul wa Uholanzi kuwa Tanzania inayo gesi nyingi na itafurahi kupokea wawekezaji kutoka Uholanzi ikizingatiwa kuwa nchi hiyo ina uzoefu na teknolojia kubwa katika sekta hiyo.

Kwa upande wa Balozi wa China hapa nchini Mhe. Wang Ke, Mhe. Rais Magufuli amesema uhusiano wa Tanzania na China ni wa kihistoria na kidugu, hivyo ametoa wito kwa Balozi huyo kuuendeleza na kuhakikisha fursa zenye manufaa kwa nchi zote zinatumiwa ipasavyo ikiwemo kukuza uwekezaji, biashara, utalii na ushirikiano katika usafiri wa anga. 

 Gerson Msigwa 
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, 
IKULU 
Dar es Salaam 
25 Oktoba, 2017.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Hati ya utambulisho kutoka kwa Balozi wa China hapa nchini Wang Ke, Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Balozi wa China hapa nchini Wang Ke akijitambulisha kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akitazama vitabu alivyokabidhiwa na Balozi wa China hapa nchini Wang Ke, Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Balozi wa China hapa nchini Wang Ke akiwa amesimama wakati wa nyimbo za Mataifa ya China na Tanzania zikipigwa katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam mara baada ya kuwasili. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Hati ya utambulisho kutoka kwa Balozi wa Uholanzi hapa nchini  Jeroen Verheul Ikulu jijini Dar es Salaam. 
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Balozi wa Uholanzi hapa nchini  Jeroen Verheul mara baada ya kupokea Hati zake za Utambulisho Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Hati ya Utambulisho kutoka kwa Balozi wa Oman hapa nchini Ali Al Mahruqi Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Oman hapa nchini Ali Al Mahruqi Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Balozi wa Oman hapa nchini Ali Al Mahruqi Ikulu jijini Dar es Salaam.
Balozi wa Oman hapa nchini Ali Al Mahruqi akiwa amesimama wakati wa nyimbo za mataifa mawili ya Oman na Tanzania zikipigwa mara tu baada ya kuwasili katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

MAMA SALMA AWAONYA WANAUME WANAOWAAMBIA WANAFUNZI WA KIKE WAMEPENDEZA


Mke wa Rais Mstaafu, Mama Salma amewaonya wanaume kuacha tabia ya kuwaambia wanafunzi wa shule za Msingi na Sekondari wamependeza kwa lengo la kuwarubuni na kuwashawishi kufanya nao mapenzi.
Rai hiyo amesema hayo mbele ya wahitimu na kidato cha nne katika mahafali ya pili ya Shule ya Sekonadari ya St Marcus iliyopo  Songwe.
Amesema tabia ya kuwasifia watoto wa kike kuwa wamependeza inashamiri  lakini lengo kuu ni kuwashawishi kimapenzi, ni vema tabia hiyo ikakoma na kila mwanajamii inapaswa kuikemea kwa nguzu zote.
“Niwambie wanaume wote wanaowaita wasichana wa shule wamependeza kwa lengo la kuwashawishi kufanya nao mapenzi wakome, waache tena wasiwarubuni watoto kwa maneno hayo machafu ambayo hayafai kwa watoto wa shule.
“Si kosa kwa mwanafunzi wa kike kuwa na rafiki wa kiume kwani ni rafiki wa kiume ambaye anaweza kukusaidia kimasomo lakini si kwa mapenzi. Unapaswa uwe na boyfriend wa kukusaidia kukokotoa Fizikia, bailojia na masomo mengine lakini siyo kufanya mapenzi narudi tena fungeni mapaja yenu’ alisema Salma

Picha 11 za harusi zitakazokushangaza

Mbwa harusini
Image captionMbwa harusini
Ni mojawapo ya siku kubwa ya maisha ya wanandoa na kama mtu aliyeandaa harusi atakelezea , kuchagua mpiga picha mzuri ni muhimu.
Hata iwapo ulikuwa na mawazo na huzuni, mpiga picha mzuri atakahikisha kuwa unaonekana unatabasamu.
Ukitazama hayo yote ni kitu cha kufurahisha kwamba upigaji picha wa harusi mara nyengine hukabiliwa na matatizo.
Watu wengine hudhania kwamba upigaji picha na mashemegi ni mojawapo ya siku ambayo ungetaka ifanyike na kukamilika kwa haraka
Picha ya Citlalli Rico
Image captionPicha ya Citlalli Rico
Citlalli Rico
Lakini mara nyengine ,wakati muhimu wa kupiga picha katika harusi hujiri wakati watu hawajajitayarisha wakati ambapo hawajui na wanaendelea na shughuli zao.
Na iwapo kuna mpiga picha mzuri basi huo ndio wakati wa kupiga picha na matokeo yake huwa ya kipekee.
Picha ya Joshua D'hondt
Image captionPicha ya Joshua D'hondt
Joshua D'hondt
Picha nzuri ya watu waliokunywa pombe wakicheza densi na watoto wakicheza wakati wa harusi zinaweza kuwa picha ambazo zitaongezea utamu wa picha za harusi zilizopigwa.
Na picha hizi za harusi zina vichekesho na visa tofauti vya kushangaza.
Gabriel Scharis
Image captionGabriel Scharis
Picha ya Lynda Wells
Image captionPicha ya Lynda Wells
Picha ya Ken Pac
Image captionPicha ya Ken Pac
Picha ya Tyler Wirken
Image captionPicha ya Tyler Wirken
Picha ya Pasquale Minniti
Image captionPicha ya Pasquale Minniti
Marius DraganHaki miliki ya pichaMARIUS DRAGAN
Image captionMarius Dragan
Picha ya Julian Wainwright
Image captionPicha ya Julian Wainwright
Marius Dragan
Picha hizi zinashirikisha visa vya kushangaza huku kukiwa na kesi zinazoanguka kakutoka juu , mbwa harusini mbali na ziara zenye hisia katika makaburi ya familia.
Julian Wainwright
Mwanamke kwa jina Nancy Smith alijiona katika picha moja na kuandika tamko hili akisema ni yeye aliyekuwa akivalishwa nywele bandia.
Mwanamke kwa jina Nancy Smith alijiona katika picha moja na kuandika tamko hili akisema ni yeye aliyekuwa akivalishwa nywele bandia.
Image captionMwanamke kwa jina Nancy Smith alijiona katika picha moja na kuandika tamko hili akisema ni yeye aliyekuwa akivalishwa nywele bandia.
David Clumpner
"Ahsanteni sana, aliandika. Mimi ndio huyo mwanamke katika picha.
Ni mwaka mgumu kwangu mimi kupatikana na ugonjwa wa saratani ya matiti na kufanyiwa matibabu kabla ya harusi ya mwanangu .
Wakati nilipokuwa nikijiandaa na wasichana katika harusi walikuwa wakinitazama na lilijawa na hissia. Naendelea vyema wakati huu na nawashukuru wote.

Je wajua kuna mipira ya kondomu ya mdomoni?

Umuhimu wa kutumia kondomu za mdomoni
Image captionUmuhimu wa kutumia kondomu za mdomoni
Nilipokuwa na umri wa miaka 20 shirika moja la wahisani walileta boksi la mipira ya kondomu katika chuo chetu.
Zilisambazwa miongoni mwetu kama maelezo ya kujikinga kiafya, huku tukipigwa na butwaa.
''Wakati ilipofika kwangu nilichukua pakiti moja. Ilikuwa mara yangu ya kwanza kukumbana na mipira ya kondmu ya mdomoni''.
Njia pekee ya kufikiria kuhusu 'dental dams' ni kuzichukulia kama kondomu za mdomoni.
Zina umbo la mraba na nyengine la mstalili na huwekwa katika uke ama sehemu ya nyuma kwa lengo la kufanya ngono ya kutumia mdomo bila kupitisha maambukizi.
Mara tu mipira hiyo inapowekwa katika maeneo yanayofaa unaweza kuendelea na shughhuli yako huku mipira hiyo ikiwa na ladha tofauti.
Haionekani kuwa mizuri lakini inazuia maambukizi.
Nchini Uingereza , vijana waliopo kati ya umri wa miaka 15-24 wako katika hatari kupatikana na magonjwa yanayosababishwa na ngono STI ikilinganishwa na watu wazima.
Mwaka 2016, vijana kati ya umri wa miaka 15-24 ambayo ni asilimia 62 walipatikana na ugonjwa wa klamidia , asilimia 50 na kisonono, asilimia 49 walikuwa na maambukizi katika sehemu za siri, huku asilimia 42 wakiwa na ugonjwa wa vidonda katika sehemu za siri
Wapenzi wa jinsia moja wako katika hatari ya kuambukizwa na magonjwa ya zinaa.
Ikilinganishwa na ngono kati ya wanawake ambao huonekana kuwa na hatari ya viwango vya chini, huku baadhi ya watu wakidhania kwamba wapenzi wa jinsia moja katika jinsia ya kike na wanawake wanaoshiriki katika mapenzi hayo na wanaume pamoja na wanawake hawako hatarini kupimwa magonjwa hayo ya zinaa.
Picha za orodha ya kinga wakati wa kufanya ngonoHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionPicha za orodha ya kinga wakati wa kufanya ngono
''Wakati nilipoanza kuwa na mpenzi katika miaka yangu ya ujana sikujua kwamba ngono salama ilikuwa muhimu kwa wapenzi wa jinsia moja hususan wasagaji''.
''Wapenzi wangu wa kwanza walikuwa pia hawajui kwa hivyo hatukutumia kinga yoyote'' .
''Lakini mpira huo wa kondomu wa mdomoni ulinifanya kugundua kwamba wasagaji pia ni muhimu kufanya ngono salama sawa na mtu yeyote yule''.
Kama mipira ya kondomu, mipira hiyo ya Dental Dams inaweza kuharibiwa na huuzwa katika pakiti.
Lakini kama kondomu sio rahisi kununua.
Zinaweza kupatikana katika maduka ya kuuza dawa na hununuliwa mitandaoni.
Kila mtu anaelewa kuhusu mipira ya kondomu na dawa za kuzuia mimba , Zote tulifunzwa shuleni.Lakini kondomu za mdomoni haziangaliliki.Ni wazi kwamba uingiliaji katika sehemu ya uke sio lazima ishirikishe uume katika wasagaji ama wanandoa.
Kuna hatari ya kusababisha maambukizi kupitia uingiliaji wa kidijitali hususan kama mtu ana kidonda ama mkwaruzo katika mkono na iwapo una kidonda na ulikigusa kabla ya kufanya ngono.

Chama cha siasa kumlipa Eminem dola 412,000 kwa kutumia wimbo wake bila ruhusa

Rapper Eminem performs Not Afraid at the 2010 BET Awards in Los Angeles, 27 June 2010Haki miliki ya pichaREUTERS
Image captionWimbo Lose Yourself ni moja ya nyimbo maarufu zaidi za Eminem
Chama kimoja cha siasa nchini New Zealand kimeamrishwa na mahakama kulipa dola 412,000 kwenye kesi iliyowasilishwa na mwanamuziki raia wa Marekani Eminem.
Chama cha National Party, kilitumia mdundo wenye sauti sawa na wimbo wa Eminem wa Lose Yourself, katika matangazo yake ya uchaguzi.
Wimbo huo kwa jina Eminem-esque ulikuwa na tofauti kidogo na wimbo wake Eminem.
Kesi hiyo iliyoanza mwezi Mei ndiyo ya hivi punde kuhusu midundo inayofanana na muziki halali.
Wachapishaji wa nyimbo za Eminem Eight Mile Style, walipeka kesi mahakamani baada ya chama cha National Party, kutumia mdudo wa wimbo huo ulioshinda tuzo ya Oscar katika kampeni yake mwaka 2014.
Mawakili wa chama walisema kuwa mdundo uliotumiwa haukuwa wa wimbo wa Lose Yourself, lakini wimbo unaojulikana kama Eminem-esque, ambao waliununua kutoka maktaba ya muziki.
Hata hivyo mahakama iliamua siku ya Jumatano kuwa mdundo huo ulifanana na wimbo wa Eminem.