Saturday, August 5

RAIS DKT. MAGUFULI PAMOJA NA RAIS MUSEVENI WA UGANDA WAWEKA JIWE LA MSINGI MRADI WA UJENZI WA BOMBA LA MAFUTA KUTOKA HOIMA UGANDA MPAKA BANDARI YA TANGA




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake, Rais wa Uganda Yoweri Museveni wakivuta utepe kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi la mradi mkubwa wa bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima Uganda hadi Tanga huku viongozi mbalimbali wa Tanzania na Uganda wakishuhudia. Shughuli hiyo ilifanyika katika kijiji cha Chongoleani nje kidogo ya jiji la Tanga.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake, Rais wa Uganda Yoweri Museveni wakivuta utepe kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi la mradi mkubwa wa bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima Uganda hadi Tanga huku viongozi mbalimbali wa Tanzania na Uganda wakishuhudia. Shughuli hiyo ilifanyika katika kijiji cha Chongoleani nje kidogo ya jiji la Tanga.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipeana mkono wa pongezi na mgeni wake Rais wa Uganda Yoweri Museveni mara baada ya uwekaji wa jiwe la msingi la mradi mkubwa wa bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima Uganda hadi Tanga huku Viongozi mbalimbali wa Tanzania na Uganda wakishuhudia. Shughuli hiyo ilifanyika katika kijiji cha Chongoleani nje kidogo ya jiji la Tanga
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Rais wa Uganda Yoweri Museveni wakiwa katika picha ya pamoja na waandishi wa habari mbalimbali waliohudhuria shughuli ya uwekaji wa jiwe la msingi la mradi mkubwa wa bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima Uganda hadi Tanga katika kijiji cha Chongoleani nje kidogo ya jiji la Tanga.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Uganda Yoweri Museveni mara baada ya kuwasili katika kijiji cha Chongoleani kwa ajili ya uwekaji wa jiwe la Msingi mradi wa bomba la mafuta ghafi kutoka nchini Uganda hadi Tanga.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipunga mkono pamoja na mke wake Mama Janeth Magufuli, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati wakiagana na Rais wa Uganda Yoweri Museveni katika uwanja wa ndege wa Tanga.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akicheza ngoma ya msanja na Mama Janeth Magufuli pamoja na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan mara baada ya kumsindikiza Rais wa Uganda Yoweri Museveni katika uwanja wa ndege wa Tanga.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia katika viwanja vya Chongoleani kabla ya tukio la uwekaji wa jiwe la msingi mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta.
Makamu wa Rais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akimpa mkono Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni baada ya kumaliza kuhutubia katika sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi la mradi wa bomba la kusafirisha mafuta ghafi kutoka Hoima Nchini Uganda hadi Tanga Nchini Tanzania.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Martin Shigela akiongea wakati wa sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi la mradi wa bomba la kusafirisha mafuta ghafi kutoka Hoima Nchini Uganda hadi Tanga Nchini Tanzania ambapo aliwaahidi Rais Magufuli na Rais Museveni kuwa wataulinda mradi huo kwa faida ya nchi hivi mbili na Afika Mashariki kwa Ujumla.
Baadhi ya wananchi wakifurahia jambo wakati wa hotuba ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwenye sherehe za uwekaji wa jiwe la Msingi la Mradi wa bomba la kusafirisha mafuta ghafi kutoka Hoima Nchini Uganda hadi Tanga Nchini Tanzania.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimueleza jambo Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni wakati wa sherehe za uwekaji wa jiwe la Msingi la Mradi wa Bomba la kusafirisha mafuta ghafi kutoka Hoima Nchini Uganda hadi Tanga Nchini Tanzania.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia katika viwanja vya Chongoleani kabla ya tukio la uwekaji wa jiwe la msingi mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Uganda Yoweri Museveni wakati wakielekea kuweka jiwe hilo la msingi.
Wananchi mbalimbali waliohudhuria katika sherehe hizo za uwekaji wa jiwe la msingi ujenzi wa bomba la mafuta.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Uganda Yoweri Museveni wakiwa katika picha ya pamoja na wasanii mbalimbali mara baada ya kutumbuiza.
Rais wa Uganda Yoweri Museveni akihutubia katika viwanja vya Chongoleani nje kidogo ya jiji la Tanga. PICHA NA IKULU

Ubovu wa barabara wakwamisha usafiri kati ya Ngara na Biharamulo



Zaidi ya magari 500 yamekwama tangu jana usiku katika kijiji cha Nyabugombe kata ya Nyakahura wilayani Biharamulo kutokana na kuharibika kwa barabara kuu ya Biharamulo-Ngara.
Kijiji ambacho magari hayo yamekwama kipo kilometa mbili kabla ya kuingia wilayani Ngara.
Barabara hiyo iliyojengwa kwa kiwango cha lami miaka 32 iliyopita imeanza kuchimbika na lami kubanduka na kubaki vumbi licha ya kufanyiwa ukarabati mara kwa mara.
Ubovu huo unachangia uharibifu wa vyombo vya moto huku magari mengi yakishindwa kupanda milima kwenye barabara hiyo.
Wakizungumza na Mwananchi Digital na vyombo vingine vya habari katika eneo hilo, madereva wamesema wamezilaumu mamlaka kwa kushindwa kuwasimamia wakandarasi wanaopewa kazi ya kukarabati barabara hiyo.
Mathalani, wamesema ubovu wa eneo hilo ni wa kihistoria lakini anapowekwa mkandarasi hakuna usimamizi wa karibu unaofanyoika kiasi cha wakandarasi hao kulipua kazi.
“Ukumbuke kuwa magari mengoi yanayotumia barabara hii hubeba mizigo mizito hivyo inahitakija ijengwa kwa uimara wa hali ya juu,” alisema dereva mmoja ambaye hakupenda jina lake litajwe gazetini.
Kukwama huko kwa magari kumeathiri abiria wengi wanaodsafiri kati ya wilaya hizo mbili.
Alipotafutwa jwa simu, Mkuu wa Wilaya ya Biharamulo, Saada Malunde, alidai hajapokea taarifa ya kukwama kwa magari ispokuwa anafuatilia kwa ajili ya kutoa msaada kwa watu waliokwama.

AfDB YASISITIZA WELEDI KWA WANAFUNZI WANAOFADHILIWA NA BENKI HIYO CHUO KIKUU CHA NELSON MANDELA


--
Benny Mwaipaja-WFM, Arusha

MKURUGENZI Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Kanda ya Afrika Mashariki, Dkt. Nyamajeje Weggoro, amewataka wanafunzi 45 kutoka Tanzania, Kenya, Uganda na Ethiopia, wanaosoma katika Chuo Kikuu cha Nelson Mandela cha Sayansi na Teknolojia kilichoko mkoani Arusha, kusoma kwa bidii na maarifa ili waweze kuzisaidia nchi zao kuinua sekta ya viwanda kwa njia ya utafiti na ubunifu wa teknolojia mbalimbali

Dkt. Weggoro ametoa rai hiyo alipotembelea Chuoni hapo ili kuangalia utekelezaji wa programu ya miaka mitano ya kuboresha masuala ya rasilimali watu inayofadhiliwa na Benki yake kwa gharama ya zaidi ya shilingi bilioni 8.2

Alisema kuwa Benki yake imeamua kuwekeza fedha nyingi katika eneo la Sekta ya elimu ya juu katika nyanja ya ufundi ili kuwapata vijana wa kutosha watakaoziba pengo lililopo na kuweka misingi mizuri ya maendeleo ya baadae hasa katika matumizi ya teknolojia na sayansi.

 “Nimefurahi sana kuona wanafunzi wanasoma na wana ari kubwa na kwamba fedha tulizozitoa zinatumika vizuri, tunadhani hata baada ya mradi huu wa  miaka 5 kukamilika, Benki itaweza kusaidia zaidi ufadhili wa fedha na vifaa” Alisema Dkt. Weggoro.

Kaimu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela, Prof. Joram Buza, ameishukuru Benki ya Maendeleo ya Afrika-AfDB kwa ufadhili huo, hatua iliyoongeza udahili wa wanafunzi katika chuo hicho.

“Mwaka wa masomo wa 2014/2015, Chuo kilidahili wanafunzi 7 pekee kutokana na changamoto wafadhili lakini baada ya ufadhili wa AfDB na Benki ya Dunia, wanafunzi wameongezeka hadi kufikia 135 jambo linalotia matumaini” alisema Pro. Buza.

Bi. Mwanaisha Mkangara na Bw. Alexander Mzura, wanaosomea shahada ya uzamivu katika masuala ya uhandisi na mifugo, kupitia ufadhili wa AfDB, wamesema kuwa masomo yao yatawaongezea ujuzi wa namna ya kufanya utafiti wa kihandisi na kuvumbua chanjo mbalimbali za mifugo.

AfDB inafadhili wanafunzi 45 ambapo 42 kati yao wanatoka Tanzania, huku Uganda, Kenya na Ethipia zikitoa mwanafunzi mmoja mmoja. 

 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB) Kanda ya Afrika Mashariki Dkt. Nyamajeje Weggoro akizungumza kuhusu umuhimu wa vijana wenye weledi wa kitaaluma katika kukuza uchumi, alipokutana na wanafunzi wa Chuo cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela Arusha (hawapo pichani) wanaofadhiliwa na Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB)




Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB), Kanda ya Afrika Mashariki, Dkt. Nyamajeje Weggoro (kulia) akiwa na Mkutano na Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela Arusha Prof. Joram Buza, alipotembelea chuo hicho kuangalia mradi wa kuwafadhili wanafunzi unaotekelezwa na Benki yake.


 Baadhi ya wanafunzi wa Chuo cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela Arusha wanaofadhiliwa na Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB) wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB) Kanda ya Afrika Mashariki Dkt. Nyamajeje Weggoro (hayupo pichani) alipotembelea Chuo hicho, ambapo aliwasisitiza kusoma kwa bidii ili kuhimili ushindani katika soko la ajira.


 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB) Kanda ya Afrika Mashariki, Dkt. Nyamajeje Weggoro (kulia), na Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela Arusha Prof. Joram Buza wakizungumza jambo baada ya kumalizika kwa mkutano na wanafunzi wa chuo hicho wanaofadhiliwa na AfDB.
 Afisa wa Idara ya Fedha za Nje anayeshughulikia Dawati la AfDB kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Said Nyenge (kulia) na Meneja wa Mradi wa Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB) wa ufadhili wa wanafunzi katika Chuo cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela, Arusha, Bw. Julius Lenguyana (kushoto), wakibadilishana mawazo baada ya kumalizika kwa mkutano kati yao kuhusu ufadhili wa AfDB katika mradi wa miaka 5 kwa baadhi ya wanafunzi wa chuo hicho.
 Meneja wa Mradi wa Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB) katika Chuo cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela Arusha, Julius Lenguyana (kulia) akimuongoza Mkurugenzi Mtendaji wa AfDB Kanda ya Afrika Mashariki Dkt. Nyamajeje Weggoro (kushoto) alipowasili chuoni hapo kuangalia utekelezaji wa mradi wa ufadhili wa wanafunzi unaotekelezwa na Benki yake kwa miaka mitano katika Chuo hicho.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB) Kanda ya Afrika Mashariki Dkt. Nyamajeje Weggoro (mbele wa pili kushoto),  Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela Arusha Prof. Joram Buza (kulia kwake), Mshauri wa Mkurugenzi huyo Bw. Amos Kipronoh Cheptoo (kushoto kwake) na Afisa Mwandamizi wa Idara ya Fedha za Nje anayeshughulikia Dawati la AfDB kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Said Nyenge (kulia), wakiwa katika picha ya pamoja na  wanafunzi wa Chuo cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela Arusha wanaofadhiliwa na Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB) kwa ngazi ya shahada ya uzamili na uzamivu.

TAARIFA KUHUSU UAMUZI WA SPIKA KWA WABUNGE WAWILI WA CUF WALIOFUKUZWA UANACHAMA


RC PAUL MAKONDA APOKEA VITANDA 150 NA MAGODORO 150 VYENYE THAMANI ZAIDI YA SHILINGI MILION 300


Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mheshimiwa Paul Makonda leo amepokea Vitanda 150 na Magodoro 150 vyenye thamani zaidi ya shilingi Milion 300 kutoka kampuni ya mafuta ya Camel chini ya Kampuni tanzu za Amsons Group, iliyoamua kuunga mkono juhudi za Mkuu wa Mkoa katika kuboresha sekta ya Afya.

Akizungumza baada ya kupokea Vitanda hivyo, Makonda amesema amedhamiria kuhakikisha changamoto zote zinazoikabili sekta ya Afya katika Mkoa wa Dar es Salaam zinamalizika ili kuhakikisha Wananchi wanapata huduma bora za afya.

“Sitaacha kutafuta kwa ajili ya Wananchi wa Dar es salaam, nitabisha hodi kila panapostahili ili mradi Wananchi wangu wawe wanapata huduma za Afya katika mazingira mazuri, ili siku moja waone kazi kubwa inayofanywa na Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt. John Magufuli, sisi tunataka Maendeleo na sio Siasa ndio maana hivi vitu vyote tunavyofanya vinatumiwa pia na wapinzani” Alisema Makonda.

Makonda amesema anatamani siku moja kila mama anaekwenda kujifungua alale kitanda kimoja mwenywe na sio kama ilivyo sasa ambapo wanatumia kitanda kimoja kinamama watatu hadi wanne.
   Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mheshimiwa,Paul Makonda akizungumza na waandishi wa habari leo baada ya kupokea  Vitanda 150 na Magodoro 150 vyenye thamani zaidi ya shilingi Milion 300 kutoka kwenye  kampuni ya mafuta ya Camel chini ya Kampuni tanzu za Amsons Group iliyomua kuunga mkono juhudi za Mkuu wa Mkoa katika kuboresha sekta ya Afya. 
.Meneja Uendelezaji wa Biashara Kampuni ya Camel Oil,Suleiman Amour (kulia) akimkabidhi   Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mheshimiwa,Paul Makonda Vitanda 150 na Magodoro 150 vyenye thamani ya zaidi ya shilingi Million 300 kutoka kwenye  kampuni ya mafuta ya Camel chini ya Kampuni tanzu za Amsons Group. Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.

TASAF YASHIRIKI MAONYESHO YA NANE NANE KANDA YA KATI DODOMA.


Na Estom Sanga-TASAF 

Vikundi vya baadhi ya Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini unaotekelezwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii- TASAF kutoka mikoa ya Dodoma, Pwani Manyara na Singida vinashiriki kwenye maonyesho ya nane nane yaliyoanza mwanzoni mwa wiki hii mjini Dodoma. 

Vikundi hivyo vilivyoko kwenye banda la Ofisi ya Rais kwenye eneo la maonyesho la Nzuguni nje kidogo ya mji wa Dodoma, vinaonyesha bidhaa zilizotengenezwa na vikundi hivyo baada ya kuwezeshwa na TASAF ikiwa ni njia mojawapo ya kuinua shughuli za uzalishaji mali na kuongeza mapato ya walengwa wa Mpango huo wenye lengo la kusaidia jitihada za serikali za kuwapunguzia wananchi kero ya umasikini. 

Bidhaa zinazotengenezwa na vikundi hivyo na ambazo zimeletwa kwenye maonyesho hayo ni pamoja na sabuni na mafuta ya manukato ambavyo vimetengenezwa kwa kutumia mmea wa mwani ambao humea kwenye maeneo ya baharini. 

Bidhaa nyingine ambazo zimezalishwa na vikundi hivyo vya walengwa wa TASAF ni pamoja na asali,ubuyu,mafuta ya alizeti na mifuko bora ya kuhifadhia nafaka ambavyo vimetokana na kazi za mikono ya walengwa hao ikiwa ni maojawapo ya sharti la kuzifanya kuinua uchumi na kujiongezea kipato kwa njia ya vikundi. 

Walengwa hao wamepongeza hatua ya serikali kupitia TASAF kuwashirikisha kwenye maonyesho hayo kwani hatua hiyo inasaidia kutangaza shughuli za uzalishaji mali zinzofanywa na walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya masikini ambao wanahitaji masoko ya bidhaa wanazozizalisha ili kukuza uchumi wao. 

“hii ni hatua muhimu katika kutangaza vikundi vya uzalishaji mali ambavyo kimsingi havina uwezo wa kutangaza bidhaa kupitia vyombo vya habari kutokana na gharama zake”amesema mwenyekiti wa kikundi cha uzalishaji asali cha Juhudi kutoka Kongwa mkoani Dodoma bwana Augen Lekas Makanda. 

Katika maonyesho hayo yaliyofunguliwa na Mkuu wa mkoa wa Singida, Dokta Rehema Nchimbi,TASAF pamoja na mambo mengine imekuwa ikitoa ufafanuzi wa utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya masikini pamoja na matumizi ya malipo kwa walengwa na kutumia utaratibu wa kielektroniki kama njia mojawapo ya kuboresha huduma zake kwa walengwa. 

Zifuatazo ni baadhi ya picha za wananachi wanaotembelea banda ya maonyesho la TASAF lililoko kwenye jengo la ya Ofisi ya Rais kwenye viwanja vya Nzuguni nje kidogo ya mji wa Dodoma.
 Baadhi ya maafisa wa TASAF wakitoa maelezo kwa wanafunzi waliotembelea banda la maonyesho la TASAF kwenye viwanja vya nane nane ,Nzuguni nje kidogo ya mji wa Doodoma.
 Mmoja wa walengwa wa TASAF kutoka kikundi cha Wakulima wa Mwani Msichoke cha Bagamoyo akitoa maelezo kwa wananchi waliotembelea banda la TASAF. Kikundi hicho kimewezeshwa na TASAF na sasa kinatengeza sabuni na mafuta kutokana na zao la mwani kama njia ya kujiongezea kipato.
Mtaalam wa Mawasiliano wa TASAF Bi. Zuhura Mdungi akitoa maelezo kwa baadhi ya watu waliotembelea banda la maonyesho la TASAF lililoko kwenye jingo la Ofisi ya Rais kwenye eneo la Nzuguni nje kidogo ya mji wa Dodoma.

 Mmoja wa maafisa wa TASAF, Bi. Grace Kibonde akitoa maelezo kwa baadhi ya watu waliotembelea banda la TASAF kwenye maonyesho ya nane nane  kwenye eneo la Nzuguni  nje kidogo ya mjini Dodoma
 Mmoja wa wajumbe wa kamati ya maandalizi ya Nane Nane kanda ya kati  Bi.Tabu Ally Likoko akipata maelezo kutoka kwa walengwa wa Mpango wa kunusuru kaya masikini ambao wameunda kikundi cha kuzalisha sabuni na mafuta kwa kuwezeshwa na TASAF .
 Baadhi ya wanafunzi wakipata maelezo ya namna shughuli za TASAF zinazvyotekelezwa kutoka kwa watumishi  wa taasisi hiyo inayotekeleza Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini nchini.

MAHAKAMA YAIMARISHA HAKI ZA WATOTO KWA VITENDO


Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Juma akikata utepe kuzindua Mahakama ya Watoto (Juvenile Court) leo jijini Mbeya. Hii ni Mahakama ya Pili ya Watoto nchini Tanzania baada ya ile iliyoko Kisutu Jijini Dar es salaam. Mahakama hii imejengwa kwa ushirikiano kati ya Mahakama ya Tanzania na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Watoto (UNICEF).
Mwakilishiwa UNICEF nchini, Stephanie Shanler akizungumza wakati wa Hafla ya uzinduzi wa Mahakama hiyo.
KaimuJajiMkuuwa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim JumaakifunguaPaziakuashiriauzinduziwa Mahakamaya Watoto (Juvenile Court) leojijiniMbeya. KatikatiniMwakilishiwa UNICEF nchini, Stephanie ShanlernakushotoniJajiKiongoziwaMahakamaKuuya Tanzania Mhe. Ferdinand Wambali.


……………………………………






Na Lydia Churi-Mahakama

Mahakama ni moja kati ya Mihimili mitatu ya dola wenye jukumu la msingi la kutoa haki sawa kwa wote na kwa wakati. Mhimili huu hufanya kazi ya kutafsiri Sheria mbalimbali zilizotungwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili kuwapatia wananchi haki. Kupitia Mpango Mkakati wake wa miaka mitano, Mahakama ya Tanzania imeendelea kusimamia haki za Watoto kama zilivyo haki nyingine wanazostahili kuzipata wananchi wa Tanzania.

UtekelezwajiwahakizaWatoto zilizoainishwakatika mikatabambalimbali yakikandana Kimataifa na kupewa nguvu ya kisheria kupitia Sheria ya Mtoto namba 21yamwaka2009,kunahitajiushirikianobainayaTaasisina wadau wa haki za watoto. Katika kulinda haki za watoto wa Tanzania, hivi karibuni, Mahakama ya Tanzania ilizindua Mahakama ya Watoto (Juvenile Court) katika jiji la Mbeya na kufanya idadi ya Mahakama hizo kufikia mbili hapa nchini. Mahakama nyingine ya Watoto iko Kisutu jijini Dar es salaam.

Maendeleo Endelevu hupatikana kwakuzingatia misingi ya hakiza Watoto

Kwa kutambua umuhimu wa watoto kuwa ni uhai wa taifa lolote,Mahakama ya Tanzania kwa kushirikiana na Mfuko wa Watoto wa Umoja wa Mataifa (UNICEF) ilichukua hatua za makusudi kuhakikisha haki za kisheria za watoto zinalindwa kwa kujenga jengo la Mahakama ya Watoto jijini Mbeya. Jengo hili linakuwa ni la pili maalum kujengwa kwa shughuli za Mahakama ya watoto pekee kwa Tanzania bara. Akizindua jengo hilo hivi karibuni, Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma alisema endapo haki za Watoto zitadharauliwa kwa mapanayakesasa,basi azmayamaendeleo endelevu ya nchi hapo baadaye, itakuwa hatarini.

AkinukuuandikolaShirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF), kuwa“Maendeleo Endelevu yanaanza na kukamilika kwamisingi ya watoto kuwa salama,wawe ni wenye afyabora na waliopata elimu bora” (Sustainable Development starts and ends with safe, healthy and well-educated children- UNICEF, May 2013). Katika nenolakelautangulizikatikaandikohilo, AnthonyLake,Mkurugenzi Mtendaji wa UNICEF aliandika kuwa:Hakizawatotona afya yaonjema, lazimaipewe kipaumbele katika maandalizi ya ajendayamaendeleoendelevuya baadayamwaka2015. Uwekezaji kwa manufaa ya watoto ni njiaborayakufutaumaskini,kuongezakasiyakuchanua kwa manufaa kwa wote.” Alisema andiko hilolinatukumbusha kuwa ustawi wa Watanzania unaanza na Ustawi wawatoto.

Ustawi wa watanzania unaanza na ustawi wa watoto

Kaimu Jaji Mkuu aliendelea kusema kuwa maana ya ustawi wa watanzania unaanza na ustawi wa watoto ni kwamba tayari Katiba imetamka kuwa lengo kuu na jukumu la Serikali ni ustawi wa wananchi na ustawi huo wa wananchini lazimaujengewe misingi imara ya ustawi wa watoto wa leo.

Alisema jamii ya watanzania bado inayo mengi ya kufanya ili kuendeleza asilimia 50 ya wananchi wake ambao wana umri wa miaka 18 na chini ya miaka hiyo. Alisema,kwa mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi iliyofanyika mwezi Agosti mwaka 2012, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilikuwa na idadi ya watu milioni 44,928,923 na kati ya hao, watoto wenye umri wa kuanzia miaka 0 hadi 17ni asilimia 50.1

Mikataba ya Haki za Watoto iliyoridhiwa na Tanzania 

Kutungwa kwa Sheria ya Mtoto namba 21 ya mwaka 2009 nchini Tanzania kunatokana na mikataba mbalimbali ya kimataifa inayotambua na kulinda haki za Watoto ambayo Tanzania iliridhia. Baadhi ya Mikataba hiyo ni Mkataba wa KimataifawaHakizaMtoto (UNConvention on the Rights of the Child -UNCRC), Mkataba wa Afrika wa Haki na Ustawi wa Mtoto (African Charter on the Rights andWelfareoftheChild-ACRWWC). Mikataba mingine ni ule wa United Nations Standard Minimum Rules for theAdministration of Juvenile Justice (Beijing Rules) na United Nations Guidelines for the Prevention of JuvenileDelinquency (The Riyadh Guidelines).

Matokeo Ya Kutungwa Kwa Sheria Ya Mtoto ya mwaka 2009

Tanzania ilitunga Sheria ya Mtoto Namba 21 ya 2009 kwa ajiliya haki, ulinzi na ustawi wa mtoto. Aidha, Sheria hii imekusanya mapendekezo yoteya ndani yanchi, ya kikanda naya kimataifa kuhusumaboreshoyahaki na maslahi mapana ya mtoto na kutoa nguvu yakisheria. Baada yakutungwakwaSheria hii, mihimili yadolaimepewa majukumu ya kutekeleza na kuwajibika. Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania anasema kwa upande wa mhimiliwaMahakama,inategemewaMahakamayaWatotoisaidiekuwajibikanakutekelezaSheriayaMtoto.
Alisema kunamaeneokadhaakatikaSheriayaMtotoambayo yanasimamiwanamamlakanyingine.Pamojana ukweli huo,badoMahakamaya Watotoinawezakutoa ushirikianokwamamlakahizoauamrizamahakamazikasaidiautendajiwa mamlaka hizo, kwa mfano; mazingira mbalimbali ambayo yameainishwa na SheriaNamba 21 ya 2009 kuwa ni hatarishi kwa mtoto kama vile uyatima, kutelekezwa, kuteswa, kuzurura, kukinzanana sheria ambapo alisema Mahakama ya Watoto inaweza kutoa tafsiri nakupanua wigo wa “mazingira hatarishi”. Mahakama ya Watoto inaweza kutoa tafsiri nakupanuawigowaUlinzina wajibuwawazazikwamatunzo ya mtoto,matibabu na elimu, sifa za mtu kuwa mlezi na uasili wa mtoto; namna gani Mahakama itawasilisha taarifa mbali mbali aukutumia rejista ya watoto walioasiliwa kwa Msajili waVizazi na Vifo pamoja na uzuiaji wa kazi za udhalilishaji kwa watoto wenye umri wa chini ya miaka18.

rof. Juma alisemaMahakamaya Watoto inaweza kutakiwa kutoa miongozokuhusu mafunzo ya kazi (apprenticeship) kwa watoto chiniya miaka 18 na kuchunguza mikataba ya mafunzo ya kaziambayo ni kandamizi au yasiyozingatia maslahi ya mtoto. MahakamayaWatoto pia inawezakutoamaamuziambayo yatazikumbushaSerikali zaMitaa wajibuwaowakuboresha ustawi wa watotowaliondani ya mamlakazaSerikali ya Mtaa husika. Mahakama inaweza kuitahadharisha Serikali Kuu naSerikali za Mitaa na Halmashauri wajenge shule maalumza watoto za kutosha. Hii itasaidia Mahakama ya Watotokuwa,badala yaadhabuyavifungogerezani,watotowaliopatikana na hatia watapelekwa. Kwakuanzisha nakuendesha Shule, Mihimili mingine nayo itakuwa inaisaidiaMahakama na Magereza kutekeleza wajibu wao kwamujibu wa Sheria Namba 21 ya 2009.

Aidha Serikali za Mitaa na Serikali Kuu zitakapoanzisha vituo vya kutunzia na kulelea watoto wenye shida ya malezi na Bunge kutoa fedha za kutosha kuendesha vituo hivyo zitaisadia Mahakama kwa kiasi kikubwa, alisema Kaimu Jaji Mkuu na kuongeza kuwa MahakamazaWatotopia zinawezakugunduamapungufukatikaSheriana kupendekezakuwa Waziri mwenyedhamana ya watoto atunge kanuni stahiki.


Sheria ya Mtoto Shirikishi nainataka Ushirikiano

Akizungumzia ushiriki na ushirikishwaji wa Sheria ya Mtoto, Kaimu Jaji Mkuu alisema Sheria kuwa sheria hii imesimamakatika misingi ya ushirikiano baina ya mihimili yote, ushirikianona wadau mbali mbali kama UNICEF na NGOs, taasisi ambazo zinashughulika na masuala ya haki za watoto. Alisema, Sheria hii pia inaitaka Mahakama ichukue uongozi, na kunamasuala ambayo mihimili mingine imepewa nafasi ya uongozi hivyo Mahakama inayo nafasi nzuri ya kuipa uhai sheria hii kwa kuwa kwanza, haki zote stahili zilizoainishwa ndani ya Sheriahii zinamfaidisha mtoto, pili, Sheria hii inapotafsiriwa,paleambapo wanaona kuna “kutofahamika, “utata” wawena ujasiri wa kuielekeza sheria kufikia malengo mazuriyaliyowekwa na Mikataba ya Kikanda na Kimataifa kuhusuhaki ya watoto.

Mahakama pia inayo nafasi nzuri ya kuipa uhai Sheria hii kwa sababu Mahakimu katika Mahakama ya Watotowatakuwa na nafasi ya karibu kabisa kuona namnavifungu mbali mbali vya Sheria hii vinavyofanyakazi, hivyo Kaimu Jaji Mkuu aliwaagiza Mahakama wanaosikiliza kesi za Watoto kuorodheshamapungufu ya Sheriahiina kuhyawasilisha kwenye kamati ya Kanuni ya Jaji Mkuu kwa ajili ya kupendekezakwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuhusu mabadiliko yaSheria.

Akisisitiza juu ya kulinda haki za Watoto, kaimu Jaji Mkuu aliwataka mahakamu wanaosikiliza kesi za Watoto wasome taarifa za Utekelezaji zinazowasilishwa na Tanzania na pia zile zinazowasilishwa na mataifa mengine kuhusu Tanzania ili waweze kugundua mapungufu yetu ya kiutekekezaji ili tuweze kupanga namna ya kuboresha utekekezaji. Mahakimu hao pia wametakiwa kufuatilia haki za Watoto pindi wanapofanya ukaguzi kwenye Magereza.


Ujenzi wa Jengo la Mahakama ya Watoto Mbeya 

Jengo la Mahakama ya Watoto jijini Mbeya lililojengwa kwa ushirikiano kati ya

Mahakama ya Tanzania na UNICEF limegharimu kiasi cha shilingi za kitanzania

Milioni 415 ambapo Mahakama imechangia kiasi cha shilingi milioni 214 na UNICEF shilingi milioni 201. Jengo hili lilianza kutumika April 18, 2017 na linaofisi mbili za Hakimu, Ofisi ya Wakili wa Serikali, ofisi ya Afisa Ustawi wa Jamii na chumba cha Mawakili wa Kujitegemea.

Sababu za Mahakama kujengwa Mbeya 

Jengo hili ambalo ni la pili la Mahakama ya Watoto nchini limejengwa jijini Mbeya kwa kuzingatia upatikanaji wa wadau na huduma zote muhimu za haki kwa mtoto. Huduma hizo ni pamoja na uwepo wa shule ya maadilisho (approved school) ikiwa ni pekee nchini, kuwepo kwa Mahabusu ya watoto mkoani humo, na kuwepo kwa dawati la jinsia la watoto lenye viwango vinavyotambulika lililoanzishwa na Jeshi la polisi. Mahakama hii pia ilianzishwa kutukana na uwepo wa timu ya ulinzi na usalama wa mtoto (child protection team) na kuwepo kwa mfumo wa marekebisho ya tabia kwa watoto (community rehabilitation programme).

Ushirikiano wa Mahakama na UNICEF katika masuala ya haki ya Mtoto

Katika kipindi cha takribani miaka mitano yaani tangu mwaka 2012, UNICEF na Mahakama walishirikiana katika kutengeneza kanuni za Mahakama yaWatoto ikiwa ni matakwa ya kifungu cha 99(1) cha Sheria ya Mtoto ya mwaka 2009 ambacho kinamtaka Jaji Mkuu kutengeneza kanuni za kutumika katika uendeshaji wa kesi katika Mahakama za Watoto.

UNICEF ilitoa msaada wa kitaaluma (technical support) na fedha katika kuandaa kanuni ambazo zilitangazwa katika Gazeti la Serikali No 182/2016. Uandaaji wa kanuni hizo ulihusisha wadau mbalimbali wa haki za watoto kama Majaji, Mahakimu, Mawakili wa Serikali, Maafisa Ustawi wa Jamii, na Mashirika yasiyo ya kiserikali vinayotoa msaada wa kisheria na vyombo vingine vinavyohusika na masuala ya mtoto.

Aidha, UNICEF imeshirikiana na Mahakama katika kuandaa mafunzo kwa wakufunzi (TOT) juu ya uendeshaji wa kesi za watoto kwa mujibu wa Sheria na kanuni za watoto.Wakufunzi walitoka Mahakamani, Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Idara ya Ustawi wa Jamii.

UNICEF pia imeshirikiana na Mahakama kutoa mafunzo kwa Mahakimu, Mawakili, wa Serikali na Waendesha Mashtaka, Maafisa Ustawi wa Jamii, taasisi zinazotoa msaada wa kisheria na Taasisi zisizo za Kiserikali katika Mkoa wa Dar es Salaam, Pwani, Mbeya, na Iringa. Aidha mafunzo kwa wadau wote yanaendelea kufanyika katika wilaya mbalimbali kwa kutumia wakufunzi waliopata mafunzo yaliyotolewa na UNICEF na Mahakama.

Kwasasa Mahakama na UNICEF watashirikana katika kutengeneza rejista za maalum mashauri ya watoto, kupitia mwongozo wa mafunzo (Training Manual) kwa kushirikiana na Chuo cha Mahakama Lushoto na Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa vitendo (Law School of Tanzania).

Sambamba na hilo kwa mwaka huu wa fedha UNICEF wataendelea kushirkiana na Mahakama katika mpango endelevu wa kutoa mafunzo kwa wadau wote wa haki za Watoto. Pia UNICEF imeonyesha nia ya kushirikiana na Mahakama katika ukarabati mdogo wa Mahakama ili kuziweka katika mazingira rafiki kwa watoto.

Hata hivyo, bado iko haja ya kuongeza idadi ya Mahakama za watoto nchini kutokana na kuwepo kwa kesi za watoto na nyingine ambazo kwa namna moja au nyingine zinawahusisha watoto katika mikoa mbalimbali nchini ili kutekeleza azma ya kulinda na kutetea haki za Mtoto.


Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mahakama ya watoto jijini Mbeya, Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Ferdinand Wambali aliiomba UNICEF kuangalia uwezekano wa kujenga majengo mengine manne ya Mahakama za watoto katika mikoa ya Arusha, Mwanza, Dodoma na Tabora ili kuwapatia Mahakimu fursa ya kujifunza kwa vitendo namna Mahakama za watoto zinavyofanya kazi.

ULAJI NYAMA ISIYO NA KIWANGO NI CHANZO CHA MAGONJWA.


Na: Agness Moshi – MAELEZO.

Ulaji wa nyama una faida lukuki kwa afya ya binadamu ikiwa ni pamoja na upatikanaji wa virutubisho vya aina ya protini ambayo ni rahisi kutumika mwilini, madini mbalimbali (Calcium, Magnesium, Phosphorus, Zinc na Chuma); vitamini aina ya folic asidi, E, B na B12 ambayo inapatikana katika nyama pekee.

Nyama pia inasaidia katika ukuaji na kuongeza afya ya mlaji kutokana na uwezo mkubwa wa kujenga mwili, kukarabati seli za mwili zilizokufa, kuzalisha chembe hai mpya, kurekebisha kinga ya mwili, kuongeza damu na kuimarisha mifupa.

Hata hivyo faida zote hizo zinapatikana tu, kwa walaji wa nyama iliyo bora na yenye kiwango. Hivyo ni vizuri wananchi wakazingatia kanuni za ulaji wa nyama yenye kiwango ili kujiepusha na athari zinazoletwa na nyama isiyo na kiwango.

Msajili wa Bodi ya Nyama Tanzania (TMB) Bi.Suzana Kiango amesema kuwa nyama yenye kiwango na bora huanzia kwenye utunzwaji wa mifugo wenye kuzingatia kanuni za uzalishaji bora, unenepeshaji wa mifugo yenye umri mdogo kwa kuwalisha chakula mchanganyiko kwa muda usiopungua siku 90 kabla ya kuchinja.

Bi.Kiango amesema kuwa hatua nyingine ni katika uchinjaji ambapo inashauriwa ufanyike kwenye machinjio bora ambayo yanakidhi viwango vya usafi. Hii ni pamoja na kuwa na sakafu na kuta zinazosafishika, maji ya kutosha na sehemu za kuning’iniza wakati wa kuchuna na kupasua.

“Kanuni za uchinjaji ni pamoja na kupumzisha mifugo ili kuipoteza fahamu na kumfanya mnyama asiogope na kuzalisha asidi nyingi inayosababisha nyama kuwa ngumu, pia iwe rahisi kutoa damu yote katika misuli. Uning’inizwaji wa chune mara baada ya kuchinjwa unasaidia kuondoa damu iliyo mwilini. Endapo damu haitatoka yote kwenye chune itasababisha nyama kuwa na rangi nyeusi na kuharibika mapema”, alisema Bi.Kiango.

Madhara ya ulaji wa nyama isiyo na viwango na bora ni pamoja na kupata magonjwa ya tumbo, kuharisha na kutapika endapo nyama itapata vimelea vya magonjwa hayo, kuugua magonjwa ya kuvimba miguu, kifua kikuu, shinikizo la damu, kisukari na kansa.

Hata hivyo, Bi. Kiango amesisitiza kuwa magonjwa haya yanaweza kuwatokea pia watu ambao hawatumii kabisa nyama kwa hivyo si nyama pekee ndio chanzo cha magonjwa haya japo inaweza kuwa sababu ya mtu kuugua.

“Bodi imeendelea kutoa elimu kwa watumiaji na wachinjaji wa nyama kupitia vyombo mbalimbali vya habari kama vile, redio, televisheni na magazeti. Pia katika maonesho mbalimbali kama Saba saba na Nane nane ambapo wataalamu wa bodi hutoa elimu kwa wananchi wanaotembelea mabanda ikiwa ni pamoja na kusambaza vipeperushi” amesema Bi.Kiango.

Namna nyingine ya kutoa elimu ni pamoja na kutumia matamasha ya nyama choma, wiki ya mayai na maonesho ya kuku, wiki ya chakula salama na siku ya chakula duniani. Wakati wa shughuli hizi wanashiriki hupatiwa elimu kuhusu faida na athari za kula nyama isiyo na viwango ili kunusuru afya zao.

Aidha walaji huelekezwa maeneo mbalimbali wanayoweza kupata nyama hiyo, na kwa upande wa wafanyabiashara wa nyama hupewa maelekezo ya kuboresha miundombinu ya kuzalisha, kuchinja na kuuza kwa kuzingatia viwango vya ubora na usalama.

Kutokana na baadhi ya wafanyabiashara ya nyama kuendelea kuwauzia walaji nyama isiyo na viwango kwa kujua au kutojua madhara ya nyama hizo, Bi.Kiango alisema kuwa Bodi inachukua hatua za kuhakikisha wafanyabiashara hao wanapata uelewa wa kutosha.

“Bodi imeanza kutoa mafunzo kwa watumishi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa ambao watashiriki katika kutekeleza majukumu ya Bodi ikiwa ni pamoja na kusimamia uzalishaji wa nyama na kuelimisha wachinjaji ,walaji na wadau wengine wanaojishughulisha na uzalishaji wa nyama”alifafanua Bi.Kiango.

Aliendelea kusema mafunzo hayo yameshatolewa kwa vitendo kwa watumishi wanne kutoka katika kila Mamlaka za Serikali za Mitaa za mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Morogoro na Dodoma ambapo hadi sasa jumla ya wadau 490 katika maeneo tajwa wamekwisha patiwa elimu hiyo. Pia mafunzo yanatolewa na wadau wengine ambao ni Chuo cha nyama cha VETA, Dodoma na Kampuni ya nyama ya jijini Arusha.

NDUGAI AKUTANA NA SPIKA WA BUNGE LA IRAN NA KUFANYA NAE MAZUNGUMZO


 Mhe. Spika Job Ndugai  leo amekutana na Spika wa Bunge  la Iran, Mhe. Dkt. Ali  Larijani na kufanya nae mazungumzo yenye lengo la kuimarisha mahusiano ya kibunge baina ya Bunge la Tanzania na Iran.

469 wafungwa kwa ujangili


WATU 469 wamefungwa vifungo vya muda mrefu kutokana na kujihusisha na vitendo vya ujangili kwenye mapori tengefu, mbuga na hifadhi za wanyama nchini.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe alitoa takwimu hizo mjini Dodoma jana wakati akizungumza na vyombo vya habari kuhusu mafanikio yaliyopatikana katika wizara hiyo katika kipindi cha mwaka moja kuanzia Julai 2016 hadi Juni mwaka huu.
Profesa Maghembe alisema wizara hiyo, imepata mafanikio makubwa kutokana na kufanya doria zaidi ya 350,000 kuzunguka kwenye mapori ya akiba, tengefu, hifadhi na mbuga za wanyama.
Alisema doria hizo zimesaidia kuwakamata watuhumiwa wa ujangili 7,085 na kuwafungulia kesi zaidi ya 2,097, ambapo kesi 276 zenye watahumiwa 469 zimekamilika na waliobainika wakatozwa faini Sh milioni 452. Aliongeza kuwa katika kesi nyingine 262 zenye watuhumiwa 472, zilikamilika na wahalifu walihukumiwa kwenda jela kifungu cha muda mrefu cha kuanzia miaka 20, 25 hadi 30.
“Pia wakati wakifanya doria walikamata zaidi ya silaha za aina mbalimbali 395 zikiwamo SMG 25, G3 1, rifle 27, SG 38, bastola 2 na magobore 262,” alisema. Aliongeza: “Pia askari walikamata jumla ya risasi 1,478 na magazini mbili za SMG zenye rasasi 11, mikuki 11, magunia ya mkaa 635, magogo 5,500 na magari 26, pikipiki 68, baiskeli 228, mitungi 265 na ng’ombe 88,435 kwa kuchungwa ndani ya hifadhi,” Kuhusu kupungua mauaji ya tembo, Waziri Maghembe alisema katika Mpango wa Ufuatiliaji wa Vifo vya Tembo umebaini kwamba mauaji ya tembo yamepungua Selous, Mikumi, Ruaha, Katavi na Tarangire na vifo 84 vimepungua, ambavyo vimesababishwa na mambo mbalimbali. Kupungua huko ni sawa ni asilimia 45, ukilinganisha na mwaka 2016/15 ambapo vilikuwa vingi zaidi.