Saturday, August 5

Ubovu wa barabara wakwamisha usafiri kati ya Ngara na Biharamulo



Zaidi ya magari 500 yamekwama tangu jana usiku katika kijiji cha Nyabugombe kata ya Nyakahura wilayani Biharamulo kutokana na kuharibika kwa barabara kuu ya Biharamulo-Ngara.
Kijiji ambacho magari hayo yamekwama kipo kilometa mbili kabla ya kuingia wilayani Ngara.
Barabara hiyo iliyojengwa kwa kiwango cha lami miaka 32 iliyopita imeanza kuchimbika na lami kubanduka na kubaki vumbi licha ya kufanyiwa ukarabati mara kwa mara.
Ubovu huo unachangia uharibifu wa vyombo vya moto huku magari mengi yakishindwa kupanda milima kwenye barabara hiyo.
Wakizungumza na Mwananchi Digital na vyombo vingine vya habari katika eneo hilo, madereva wamesema wamezilaumu mamlaka kwa kushindwa kuwasimamia wakandarasi wanaopewa kazi ya kukarabati barabara hiyo.
Mathalani, wamesema ubovu wa eneo hilo ni wa kihistoria lakini anapowekwa mkandarasi hakuna usimamizi wa karibu unaofanyoika kiasi cha wakandarasi hao kulipua kazi.
“Ukumbuke kuwa magari mengoi yanayotumia barabara hii hubeba mizigo mizito hivyo inahitakija ijengwa kwa uimara wa hali ya juu,” alisema dereva mmoja ambaye hakupenda jina lake litajwe gazetini.
Kukwama huko kwa magari kumeathiri abiria wengi wanaodsafiri kati ya wilaya hizo mbili.
Alipotafutwa jwa simu, Mkuu wa Wilaya ya Biharamulo, Saada Malunde, alidai hajapokea taarifa ya kukwama kwa magari ispokuwa anafuatilia kwa ajili ya kutoa msaada kwa watu waliokwama.

No comments:

Post a Comment