Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini,Dkt Juliana Pallangyo akizundua mradi huo
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini,Dkt Juliana Pallangyo kushoto akipata maelezo ya mradi huo mara baada ya kutembelea kwenye eneo la mtambo huo kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Korogwe Mkoani Tanga,Mhandisi,Robert Gabriel.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini,Dkt Juliana Pallangyo akishiriki kucheza ngoma ya wananchi wa Kijiji hicho mara baada ya kuzinduaa mradi huo
NI ukweli usiopingika utekelezaji wa sekta ya viwanda inahitaji
nishati ya umeme katika shughuli zake mbalimbali ikiwemo za uzalishaji mali ili kuweza kupata mafaniko yanayoweza kusaidia kuinua uchumi wao.
Kwani bila kuwepo kwa nishati hiyo kwa baadhi ya maeneo hasa vijijini kuna pelekea kushindwa kufikia malengo yao kwa kuongeza uzalishaji wa bidhaa mbalimbali kwa kuhofia iwapo zitakaa muda mrefu zitaharibika.Licha ya hivyo lakini pia kukosekana kwa nishati hiyo kuna sababisha watanzania wenye nia ya kuanzisha viwanda vidogo vidogo kukwama kufikia malengo yao waliojiwekea kwa kuvianzisha.
Kufuatia kuwepo kwa changamoto hiyo, Shirika la Umoja wa Mataifa la Mfuko wa Mitaji na Maendeleo (The United Nations Capital Development Fund –UNCDF) kwa kushirikiana na kampuni ya Ensol Tanzania Limited waliamua kuanzisha mradi wa umeme wa jua (sola) kwenye kijiji cha Mpale Kata ya Mpale wilayani Korogwe Mkoani Tanga.
Mradi huo ambao umekuwa mkombozi mkubwa kwa wananchi wa Kijiji hicho umefadhiliwa na Shirika hilo ambao umelenga kuwasaidia kuondokana na changamoto ambazo zilikuwa zikiwakabili ikiwemo kutumia vibatari wakati wakienda kujifungua kwenye zahanati ya Kata hiyo.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi huo,Diwani wa Kata ya Mpale Tarafa ya Bungu wilayani Korogwe Mkoani Tanga,Shemakao Miraji anasema mradi huo ni faraja kubwa kwa wakazi wa Kijiji hicho na maeneo jirani ikiwemo kufungua fursa za kiuchumi lakini kuendana sanjari na kauli mbiu ya serikali ya viwanda.
Anasema awali walikuwa wakilabiliwa na changamoto kubwa ya wakina mama wajawazito kwenda kujifungulia kwenye zahanati hiyo kwa kutumia vibatari jambo ambalo lilikuwa ni hatari kwa maisha.
Diwani huyo anasema faida kubwa za mradi huo utasaidia kuboresha huduma za afya kwa wakina mama ambao walikuwa wakienda kwenye vituo vya afya kwa kutumia vibatari lakini baada ya kufika umeme huo utawasaidia kuondokana na kadhia hiyo ambayo ilikuwa ni hatari kwa maisha yao ambao ni nguvu kazi kuelekea uchumi wa viwanda.
"Kilio kikubwa cha wananchi wetu hapa ni maembe yanayoanguka na kuoza ha hatuwezi kupata namna nyengine ya kuweza kutuepusha na adha ya kuondokana nayo na hii itatusaidia kuondokana na dhamana hiyo lakini pia umeme huu utatusaidia kuingia kwen ye uchumi wa kati kwa kuanzisha viwanda vidogo vidogo vya chai na kukuza zao hilo"Anasema.
Naye kwa upande wake,Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini,Dkt Juliana Pallangyo anawapongeza kampuni hiyo na washirika wa kiufundi TTA kwa juhudi walizofanya kuchagua kijiji hicho kufanya utafiti,kubuni mradi huo kwa kutafuta fedha na kutafuta taratibu zote katika kutekeleza mradi huo huku akiwataka wananchi kuanzisha viwada vidogo vidogo.
“Katika kutafuta fedha nafahamu Ensol ilifanikiwa baada ya kushindwa nishwa na makampuni mengine kwani taasisi hizi zilizotajwa zinatoa fedha kwa mtindo wa ushindani na wanapokea maombi mengi ya ufadhili kutoka maeneo mbalimbali ya dunia na Afrika “Anasema
“Lakini pia nimefurahishwa na zaidi na huduma kadhaa zilizotolewa na mradi kwa jamii hii hapa kwanza kuwawezesha wananchi kuunganishwa na umeme ikiwemo kufanyiwa wayaringi kwa mkopo “Anasema.
Anasema ni kweli katika maeneo ya vijijini huduma ya umeme imefika lakini wananchi wengi wanashindwa kuunganishwa na umeme kwa sababu gharama ya kutandaza nyaya kwenye nyumba zao.
“Tunawashukuru sana Ensol kwa kufikiria kutatua changamoto hii na pia tunawashukuru Power Africa kwa kuunga mkono jambo hili kwa kutoa fedha na naamini wananchi wa hapa mpale watatumia fursa ya umeme ambayo sio rahisi kupatikana kuunganishwa nayo “Anasema.
“Lakini pia ni kwamba nishati hii ya umeme itapatikana kwa saa 24 kwa siku 7 za wiki bila kukatika hii ni habari njema kwa watumiaji wa umeme kwani iwapo huduma hiyo itakosekana bado ni changamoto hata maeneo ya mijini “Anasema.Anasema ni jambo jema kusikia kuwa hapa kwenu masuala ya mgawo wa umeme kukatika itakuwa ni suala la kusikia kwa wengine na huo ndio uzuri wa kutumia teknolojia ya umeme wa Jua.
“Pamoja na hayo lakini niwahamasishe wananchi wa hapa mpale kutumia vizuri uwepo wa nishati hiyo kwa kuanzisha shughuli za uzalishaji mali ikiwemo kuanzisha viwanda vidogo vidogo na miradi itakayoweza kuwaingizia fedha ili kujikwamua kiuchumi”Anasema.
“Msiishie kupata mwanga tu bali tumieni pia fursa hii kuanzisha
biashara na miradi itakayowaingizia fedha kwani umeme huu unatosha kuanzisha viwanda vidogo vidogo kama vinu vya kusagia nafaka ,mashine za useremala na kutengeneza samani “Anasema.
Anasema kwa kufanya hivyo wananchi wa kijiji hicho watakuwa wameendana sambamba na mwamko mpya wa Tanzania ya Viwanda ambao utafungua fursa kubwa za kiuchumi kwao.
Naibu Katibu huyo anasema kupitia huduma hiyo ni matumaini yake huduma za afya zitaboreka zaidi kijijini hapo kwani wananchi wengi wa maeneo ya jirani watakwenda kupata matibabu kwao kutokana na uwepo wa uhakika wa kutibiwa muda wote kunakosababishwa na nishati ya umeme.
“Nawaombeni halmashauri pamoja na serikali ya kijiji kujipanga
kuhakikisha umeme unaotumika unalipiwa kadri inavyotakiwa kila mwezi kwani haipendezi kuona nishati hiyo ipo lakini zahanati inakosa huduma hiyo kwa kushindwa kilipia “Anasema.
“Lakini pia nikuombe Mkurugenzi wa Halmashauri ya Korogwe pamoja na uongozi wa kijiji mjipange hata kwa kutumia fedha mtakazookoa kutoka kwenye manunuzi ya mafuta ya taa na gesi kwa ajili ya jokofu la madawa muweze kulipia umeme “Anasema.
“Serikali sasa kupitia wakala wa Nishati imezindua rasmi mpango wa tatu wa kusambaza umeme maeneo ya vijijini na tumeweka lengo la kufikia vijiji vyote ifikapo mwaka 2022.
Naye, Msimamizi Mkuu wa Mradi huo,Prosper Magali anasema shughuli za mradi huo zilianza rasmi Machi mwaka 2014 baada ya kutembelea kijiji hicho pamoja na vyengine vilivyopo wilayani Korogwe.
Anasema licha ya kutembelea wilaya hiyo lakini pia walitembelea maeneo mengine Tanzania kutafuta vijiji na maeneo yanayofaa kwa miradi ya uzalishaji mdogo wa umeme kwa kutumia teknologia ya umeme wa Jua.
Aidha anaeleza waliamua kuanza mradi wa mfano katika kijiji hicho baada ya kuwa kijiji bora kwa vigezo walivyoweka vya kiuchumi, kijamii na kimakjazi ukilinganisha na vyengine walivyotembelea.
“Shughuli ya mradi zilifuatiwa na zoezi la kufanya upembuzi yakinifu, Mpango wa kibiashara (Bussines Plan) pamoja na makadirio ya kiufundi mambo ambayo yalitusaidia kuandaa nyaraka za kuwasilisha kwa wafadhili na wawekezaji mbalimbali “Anasema.
“Baada ya hapo mmwaka 2014 mwishoni, Taasisi ya Energy and Environment Partnership (EEP) Program yenye makao yake makuu huko Pretoria nchini Afrika kusini inayopata ufadhili wa Serikali za Finland, Uingereza na Austria kupitia mpango wake wa kutoa ufadhili wa miradi ya nishati endelevu kwa nchi za kusini na mashariki ya Africa kwa mtindo wa
ushindani “Anasema
“June 10 mwaka 2015 tuliweza kusaini makubaliano rasmi ya EEP ya ufadhili wa miaka miwili wa mradi huu uliokuwa na thamani ya Euro 263,000 ikiwa ni asilimia 63 ya gharama za mradi “Anasema.
Anaongeza kuwa bado wanaendelea na zoezi la kutafuta fedha zaidi za kutekeleza mradi huo lakini kwa bahati nzuri baada ya mazungumzo ya muda mfupi, Taasisi ya Umoja wa Mataifa ya Maendeleo ya Mitaji (United Nations Capital Development Fund ya UNCDF).
Anaeleza kufuatia mazungumzo hayo taasisi hiyo ilikubali kutoa asilimia 22 ya gharama za mradi USD 124,000 na walitiliana saini ya makubaliano ya ufadhili wa fedha hizo Novemba mwaka 2015.
Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha.