Na Agness Francis, Blogu ya jamii
SSERIKALI ya Tanzania wakishirikiana na serikali ya Korea Kusini wamezindua utekeleza mradi utakaosaidia kuboresha upatiikanaji wa huduma bora za ardhi katika mkoa wa Mwanza na mradi huo utanzia Manispaa ya Ilemela na Nyamagana.
Ambapo hafla hiyo ya mradi huo umezinduliwa leo na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt Angeline Mabula katika ukumbi wa Hyatt Regency hoteli Jijini Dar es Salaam.
Katika ushirikiano huo wa kuimarisha utawala wa ardhi nchini ambapo makubaliano rasmi ya ushirikiano huo yalianza mwaka 2015, ikiwa ni msada wa vifaa vya upimaji na mafunzo yanayohusu matumizi ya vifaa vya kisasa vya upimaji, nayo yalianza mwaka 2016.
Naibu waziri Angeline Mabula ametamabaisha kuwa kuleta teknolojia hiyo mpya na nafuu itarahisishia serikali upimaji ardhi kwa kupanga na kupima kila kipande, pamoja na kusaidia wananchi kupata kumbukumbu na taarifa za ardhi kwa urahisi.
Mbali na hayo Dkt Angeline Mabula ametoa shukrani za dhati kwa Serikali ya Korea Kusini kwa kuona umuhimu wa utekelezaji wa mradi huo ambao utaleta mapinduzi makubwa katika sekta ya ardhi hapa nchini.
Balozi wa Korea Kusini Tanzania, Song Geum-Young akizungumza na mkurugenzi halmashauri ya Manispaa Ilemela pamoja na wakuu wa idara na taasisi wizara ya ardhi kuhusu ushirikiano uliopo kati ya Serikali ya Tanzania na Korea Kusini kuimarisha mfumo bora wa upimaji ardhi kwa urahisi.leo katika uzinduzi uliofanyika kwenye ukumbi Hayyat Regency Hotel Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa biashara wa Kampuni ya LX, Cho Man-Seung akizungumza na waandishi wa habari leo kuhusu kuwa mradi huo unatarajia kuanza kutekeleza hivi karibuni na utakuwa ni wa kisasa zaidi hapa Nchini.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi,Dkt Angeline Mabula akizungumza na waandishi wa habari kuhusu uzinduzi wa maradi wa uboreshaji wa huduma za ardhi leo uliofanyika kwenye ukumbi wa Hayyat Regency Hotel Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wageni waalikwa pamoja na wakuu wa idara na taasisi wizara ya ardhi waliohudhuria uzinduzi huo leo katika ukumbi Hayyat Regency Hotel Jijini Dar es Salaam. (Picha na Agness Francis, Blogu ya Jamii)