Monday, November 6

KESI INAYOMKABILI MKURUGENZI MKUU WA NIDA NA WENZAKE,UPELELEZI WAKE BADO HAUJAKAMILIKA


Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii.

Ni mwaka sasa, tangu kufikishwa mahakamani kwa aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho (NIDA), Dickson Maimu na wenzake lakini upelelezi dhidi ya kesi ya uhujumu uchumi na kusababisha hasara ya Sh 1.16 bilion inayowakabili bado haujakamilika.

Kesi hiyo ilifikishwa mahakama ni hapo kwa Mara ya kwanza Agosti 18,2017.

Upande wa mashtaka ukiongozwa na wakili wa Serikali Mkuu, Vitalis Peter mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Respicius Mwijage alidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika hiku wakili Leornad Swai kutoka Takukuru, akidai kuwa jalada la kesi hiyo lililokuwapo kwa Mkurugenzi wa Mashtaka DPP limekwisha rudishwa.

Hakimu Mwijage aliwaeleza upande wa Mashtaka wakamilishe upelelezi wa kesi hiyo ili washtakiwa kama walikula fedha za umma wafungwe kama hawajala waachiwe, siyo kula siku upelelezi haujakamilika maana yake nini.

Hakimu Mwijage aliiahirisha kesi hiyo hadi Desemba 6,2017 na kuutaka upande wa,Mashtaka siku hiyo uje na kitu na siyo upelelezi bado haujakamilika.

Mbali ya Maimu, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Meneja Biashara wa (NIDA), Avelin Momburi na Mkurugenzi wa TEHEMA, Joseph Makani.

Kaimu Mhasibu Mkuu wa NIDA, Benjamin Mwakatumbula, Mkurugenzi wa Kampuni ya Aste Insurance Brokers, Astery Ndege, Ofisa Usafirishaji, George Ntalima, Mkurugenzi wa Sheria, Sabina Raymond na Xavery Kayombo.

Katika kesi hiyo, washtakiwa wanakabiliwa na mashtaka ya kutumia madaraka vibaya, kula njama, kutumia nyaraka za uongo kumdanganya mwajiri na kuisababishia Serikali hasara ya zaidi ya Sh 1,169,352,931

MAKAMU WA RAIS AFUNGUA MKUTANO WA KIMATAIFA WA WADAU WA ELIMU YA UFUNDI NA MAFUNZO JIJINI DAR ES SALAAM


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa Ufunguzi wa mkutano wa Kimataifa wa Wadau wa Elimu ya Ufundi na Mafunzo ulioanza leo tarehe 6 na unatarajiwa kumalizika tarehe 8 november, katika ukumbi wa APC Bunju, Jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo ya namna ya mashine ya kuchora kadi za mifumo ya umeme inavyofanya kazi na Mhandisi Vedastus Sichilima kutoka D.I.T (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)​


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, leo amefungua Mkutano wa Kimataifa wa wadau wa elimu na mafunzo ya ufundi. Mkutano huo unaofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Hotel ya APC Bunju wilayani Kinondoni, umeandaliwa na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) kwa kushirikianana Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima ya nchini Finland. 

Akihutubia washiriki katika Mkutano huo wenye kaulimbiu isemayo “wekeza katika elimu ya ufundi na mafunzo kwa Tanzania kuwa ya uchumi wa viwanda” Makamu wa Rais alisema kaulimbiu hiyo inaenda sambamba na agenda ya serikali ya kutekeleza dira ya kuwa nchi ya viwanda na uchumi wa kati ifikapo 2025. “Ni dhahiri kuwa elimu ya ufundi ni nguzo muhimu ya kufikia agenda ya serikali ya kuwa Tanzania ya viwanda na kufikia uchumi wa kati ifikapo 2025” alisisitiza Makamu wa Rais

Makamu wa Rais alisema amefarijika kuona kuwa Mkutano huo umepambwa na magwiji wote kutoka taasisi na vyuo vya elimu ya ufundi pamoja na wadau wote wa utoaji wa elimu ya ufundi na mafunzo. Aidha, alisisitiza kuwa anatambua kuwa kutoa elimu ya ufundi ni mkakati muhimu sana utakaosaidia kubadili fikra na mitazamo ya raia walioelimika na kuwa mahiri katika stadi na maarifa ya kutosha kusaidia kukabiliana na changamoto za maendeleo ya nchi yetu.

Sambamba na hilo, Makamu wa Rais aliwapongeza waajiri waliojitokeza katika mkutano huo na kuwaasa kwamba wao ni kiungo muhimu sana katika kuleta maana halisi ya mkutano huo. Makamu wa Rais alisema ili kuzalisha na kuendeleza rasilimali watu bora katika kada ya kati ni lazima kuwepo mahusiano mazuri baina ya taasisi zinazotoa mafunzo ya ufundi na waajiri. Mahusiano hayo ndiyo yatakayozalisha wataalam bora kwa ajili ya maendeleo ya Taifa letu.

Akizitaja changamoto zinazoikabili sekta ya elimu hapa nchini, Makamu wa Rais alisema ni pamoja na kutokuwepo kwa muunganiko wa kutosha kati ya taasisi zinazotoa elimu na mafunzo ya ufundi na waajiri kama vile viwanda, mabenki, taasisi za afya na vyombo vya habari. Aidha, upo uelewa mdogo miongoni mwa wadau na jamii kwamba elimu ya ufundi inahusu masuala ya useremala, uashi, ufundi makenika, kushona nguo na mambo yanayofanana na hayo. Pamoja na hayo upungufu wa miundombinu stahiki katika vyuo vya ufundi ili kutoa mafunzo yenye viwango vya ubora wa hali ya juu nayo ni changamoto.

Makamu wa Rais alisema wakati nchi inaelekea kwenye uchumi wa Viwanda, hatuna budi kujipana kuandaa wataalamu wa kutosha hivyo Serikali imeelekeza Baraza kuanda, kupitia upya na kuboresha Mitaala kwenye maeneo muhimu ili kuendana na mahitaji ya soko la ajira.

Makamu wa Rais alisisitiza kuwa utoaji wa Elimu ya Ufundi inayojibu matatizo ya jamii, inayoandaa vijana wenye umahiri wa kuweza kupambana na changamoto za maendeleo katika ulimwengu wa sasa wa Sayansi na Teknolojia.

Mwisho Makamu wa Rais alisema kuwa ni matarajio yake Mkutano huu utatoa maazimio na ufumbuzi wa namna ya kukabiliana na changamoto za utoaji wa Elimu ya ufundi na kuishauri Serikali ipasavyo juu ya hatua za kuchukua ili elimu itolewayo iendane na mahitaji ya Soko la ajira.

Makamu wa Rais aliwashukuru na kuwapongeza Taasisi ya Elimu ya watu Wazima ya Finland kwa kushirikiana na NACTE katika kuandaa mkutano huo .

Aidha aliwapongeza Jamhuri ya Watu wa Finland kwa kuadhimisha miaka 100 ya uhuru.

JALADA LA KESI YA RAIS WA SIMBA EVANS EVEVA NA MWENZAKE BADO LIMENASA KWA DPP


Na Karama Kenyunko, Glogu ya Jamii

Kwa mara nyingine tena upande  wa mashtaka katika kesi ya uhujumu uchumi, inayomkabili Rais wa klabu ya Simba, Evans Aveva na mwenzake, umedai jalada la shauri hilo bado liko kwa Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP). Aveva anashtakiwa pamoja na makamu wa rais wa klabu hiyo, Godfrey Nyange maarufu Kaburu ambapo wote kwa pamoja wanashtakiwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Wakili wa Serikali Mkuu, Vitalis Peter akishirikiana na Wakili wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Leonard amedai hayo leo Novemba 6, 2017 mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Victoria Nongwa.

Vitalis alidai, upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika na kwamba jalada la uchunguzi bado lipo kwa DPP, hivyo wanasubiri lirudishwe. Kufuatia taarifa hiyo, wakili wa utetezi, Evodius Mtawala, aliomba mahakama iusisitize upande wa jamhuri kutilia mkazo upelelezi dhidi ya shauri hilo. Kesi hiyo imeahirishwa hadi Novemba 10, mwaka huu, kwa ajili ya kuja kutajwa, washtakiwa wamerudishwa mahabusu

Vigogo hao wa Simba wanakabiliwa mashitaka matano ya kughushi, kuwasilisha nyaraka ya uongo na kutakatisha Dola za Marekani (USD) 300,000. Washitakiwa hao wanadaiwa  Machi 15, 2016,  walikula njama ya kughushi fomu ya maombi ya kuhamisha fedha ya tarehe  wakionyesha Klabu ya Simba inalipa mkopo wa  USD 300,000 kwa Aveva wakati si kweli.

Aveva anadaiwa  Machi 15, 2016 katika benki ya CRDB, tawi la Azikiwe, lililoko  Ilala, Dar es Salaam, huku akijua alitoa nyaraka hiyo ya kughushi.

 Aveva na Nyange wanadaiwa kati ya Machi 15 na Juni 29,2016, Dar es Salaam  kwa pamoja walikula njama ya kutakatisha fedha kwa kupata USD 300,000 wakati wakijua ni zao la kosa la uhalifu la kughushi.

Aveva anadaiwa Machi 15,2016 katika benki ya Barclays, Mikocheni, Dar es Salaam,  alijipatia USD 300,000 wakati akijua zimetokana na kosa la kughushi.

 Nyange anadaiwa Machi 15,2016 katika benki ya Barclays tawi la Mikocheni alimsaidia Aveva  kujipatia USD 300,000 wakati akijua fedha hizo zimetokana na kughushi.

WAZIRI UMMY AWATAKA MAAFISA MAENDELEO YA JAMII KUAMSHA ARI YA JAMII KUSHIRIKI KATIKA SHUGHULI ZA MAENDELEO


 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy A. Mwalimu (Mb), (Kushoto) akisalimiana na Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi. Sihaba Nkinga (katikati) wakati alipowasili kufungua Mkutano wa Mwaka wa wataalam wa Sekta ya Maendeleo ya Jamii unaofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Mipango Mjini Dodoma.
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy A. Mwalimu(Mb), akisalimiana na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Jamii Bw. Patrick Golwike wakati alipowasili kufungua Mkutano wa Mwaka wa wataalam wa Sekta ya Maendeleo ya Jamii unaofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Mipango Mjini Dodoma.
 Mkurugenzi wa Maendeleo ya Jamii Bw. Patrick Golwike akitambulisha washiriki wa Mkutano Mkuu wa Kitaifa wa Sekta ya Maendeleo ya Jamii kwa mwaka 2017 unaofanyika Chuo cha Mipango mkoani Dodoma na kujumuisha Maafisa Maendeleo ya Jamii ngazi ya Taifa, Sekretarieti za Mikoa na Halmashauri za Mitaa na wawakilishi kutoka Sekta na Mashirika mbalimbali nchini.
 Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI Elimu Bw. Tikson Nzunda akifafanua neno wakati wa Mkutano MKuu wa Kitaifa wa Sekta ya Maendeleo ya Jamii kwa mwaka 2017 unaofanyika Chuo cha Mipango mkoani Dodoma kuhusu umuhimu wa kuwatumia wataalamu wa Maendeleo ya Jamii katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo yao.
 Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi. Sihaba Nkinga akitambulisha malengo ya Mkutano Mkuu wa Sekta ya Maendeleo ya Jamii 2017 na kumkaribisha Mgeni rasmi Mheshimiwa Waziri Ummy Mwalimu kufungua Mkutano wa Mwaka wa Wataalamu wa Maendeleo ya Jamii
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy A. Mwalimu(Mb) akisisitiza maafisa Maendeleo ya Jamii nchini kuamsha ari ya wananchi kushiriki katika shughuli za kimaendeleo kuelekea uchumi wa Viwanda wakati akifungua Mkutano wa wataalam wa Sekta ya Mandeleo ya Jamii unaofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Mipango Mjini Dodoma.
 Baadhi ya Maaafisa Maendeleo ya Jamii wakisikiliza maelekezo ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy A. Mwalimu(Mb)(hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Wataalam wa Sekta ya Maendeleo ya Jamii nchini unaofanyika katika Ukumbi wa Chuo cha Mipango Dodoma.  
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy A. Mwalimu(Mb) akiwa katika picha ya pamoja na watendaji wa Idara Kuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto pamoja na Ofisi ya Rais TAMISEMI mara baada ya kufungua Mkutano wa wataalam wa Sekta ya Maendeleo ya Jamii Mjini Dodoma.
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy A. Mwalimu(Mb) (katikati) akijadiliana jambo na Naibu katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI Elimu Bw. Tikson Nzunda (kulia) mara baada ya kufungua Mkutano wa wataalam wa Sekta ya Maendeleo ya Jamii Mjini Dodoma kushoto ni Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi. Sihaba Nkinga. Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW

Na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW
Serikali imewataka Wataalam wa Maendeleo ya Jamii kurejesha ari na hamasa ya jamii kushiriki katika kazi za maendeleo ili kutoa mchango katika kufikia Tanzania ya Viwanda na yenye uchumi wa kati.

Kauli hii imetolewa MJini Dodoma na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy A. Mwalimu wakati akifungua Mkutano Mkuu wa 12 wa Sekta ya Maendeleo ya Jamii unafoanyika katika ukumbi wa Chuo cha Mipango Dodoma.

Mhe. Ummy Mwalimu  amesema kuwa kupitia Mkutano huo Wataalam wa Maendeleo ya Jamii wanatakiwa  kutoa  mapendekezo kuhusu mbinu bora zitakazosaidia kurudisha ari na hamasa ya jamii kushiriki katika maendeleo na hivyo kusaidia kufikia uchumi  wa kati na wa viwanda.

Mhe. Ummy Mwalimu amefafanua kuwa wataalam wa maendeleo ya jamii ndiyo wenye jukumu la kuhamasisha utekelezaji wa miradi ya kisekta hususan kilimo, afya, elimu, na miundo mbinu na kadhalika.

“Wataalam wa  Maendeleo ya Jamii watumie fursa hii kujitathmini ili kupata majibu ya namna bora ya kutekeleza majukumu yao ya kuamsha ari ya wananchi kushiriki kwenye uzalishaji na kutokomeza ukatili wa jinsia ambao unapunguza kasi ya kufikia uchumi wa kati na maendeleo jumuishi” alisema Mhe. Ummy.

Waziri Ummy ameeleza kuwa Kaulimbiu ya Mkutano wa Sekta ya Maendeleo ya Jamii kwa Mwaka 2017  ambayo ni  “Amsha Ari ya Ushiriki wa Wananchi Kufikia Uchumi wa Viwanda” inatafsiri azma ya Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Dkt. John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya kuwa na Tanzania ya Viwanda ili kufikia uchumi wa kati. 
     
Naye Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi. Sihaba Nkinga amesema kuwa katika awamu ya sasa Wataalamu wa Maendeleo ya Jamii wana wajibu wa kuelimisha na kuamsha ari ya wananchi kufanya kazi za uzalishaji kwa bidii kwa kuzalisha mali ghafi zinazohitajika na viwanda na kuwekeza kwenye viwanda vidogo vidogo na vya kati.

Bibi Sihaba Nkinga amefafanua kuwa malengo ya Mkutano huo umezingatia  tathmini ya mchango wa Sekta ya Maendeleo ya Jamii katika kuamsha  ari na hamasa ya wananchi kushiriki na kuchangia maendeleo kwa kushirikiana na viongozi wa Sekta na Idara nyingine katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Naye Mkurugenzi wa Maendeleo ya Jamii Bw. Patrick Golwike amewaasa Wataalamu wa Maendeleo ya Jamii kwa kushirikiana na wadau  kutoa elimu na kuhamasisha wananchi kujitoa katika kufanya kazi za kujiletea maendeleo katika maeneo yao.

Lengo la Mkutano huu wenye kauli mbiu isemayo “Amsha Ari ya Ushiriki wa Wananchi Kufikia Uchumi wa Viwanda” ni kuhakikisha Wizara na wadau wanashirikiana katika kuamsha ari ya wananchi kufanya kazi za maendeleo na kusimamia Mpango ya kutokomeza ukatili wa jinsia ambao kwa kikasi kikubwa unapunguza kasi ya Taifa kufikia uchumi wa viwanda.

MKURUGENZI MKAZI WA SHIRIKA LA MISAADA LA MAREKANI –USAID-AIPONGEZA TASAF.

Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Misaada la Marekani –USAID- Bwana Andrew Karas amesema shirika hilo litaendelea kuunga mkono kazi inayofanywa na serikali ya Tanzania kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii –TASAF – katika kukabiliana na umaskini nchini.

Bwana Karas ametoa hakikisho hilo alipotembelea makao makuu ya TASAF jijini Dar es salaam na kufahamishwa juu ya utekelezaji wa Mfuko huo hususani katika Mpango wake wa Kunusuru Kaya masikini ambao pia Shirika hilo limekuwa likiufadhili.

Amesema mafanikio yaliyoanza kupatikana kwa walengwa wa Mpango huo kuanza kujihusisha na shughuli za uzalishaji mali ni suala muhimu katika kuwajengea uwezo na kusaidia jitihada za serikali za kutokomeza janga la umasikini nchini kote.“Tutaendelea kusaidiana na serikali ya Tanzania katika kuhakikisha kuwa Mpango huu unatekelezwa kwa mafanikio makubwa “ amesisitiza Bwana Karas.

Kwa upande wake ,Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF ,Bwana Ladislaus Mwamanga amemweleza Mkurugenzi Mkazi huyo wa USAID kuwa hatua kubwa imefikiwa katika kusaidia juhudi za serikali za kuwaondoa wananchi wanaokabiliwa na umasikini kwa kuwashirikisha katika shughuli za kujiongezea kipato.

“Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya masikini wametumia fedha na elimu wanayopata kupitia TASAF kujiongezea kipato na kuboresha maisha yao” amesisitiza bwana Mwamanga.

Amemweleza Mkurugenzi Mkazi huyo wa USAID kuwa uboreshaji wa makazi, uanzishaji wa miradi midogo midogo kama ufugaji wa kuku,bata,mbuzi ,nguruwe na shughuli za kilimo ni miradi ambayo walengwa wamekuwa wakijihusisha tangu kuandikishwa kwenye Mpango.

Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini unatekelezwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF tangu mwaka 2013 na unahudumia kaya MILIONI MOJA NA LAKI MOJA zenye takribani watu milioni SITA ,Tanzania Bara ,Unguja na Pemba.
Mkurugenzi Mkazi wa USAID ,Bw. Andrew Karas (aliyevaa shati jeupe) akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF,Bw. Ladislaus Mwamanga juu ya utekelezaji wa shughuli za TASAF.
 Baadhi ya watendaji wa  TASAF wakimsikiliza Mkurugenzi Mkazi wa USAID wakati wa ziara hiyo aliyoifanya kwenye makao makuu ya Mfuko huo jijini Dar es salaam.

AMINA MOLLEL: WAZAZI MSIWAFICHE WATOTO WENYE ULEMAVU NDANI

mbunge wa viti maalumu CCM Amina Mollel akiwa anacheza ngoma ya kimasai pamoja na baadhi ya wamasai waliojitokeza katika sherehe za kupandisha ngazi ya rika kutoka katika rika la kurianga kuingia katika rika la Nyangulo (habari picha na woindeshizza blog )
Mbunge akiwa na wananchi waliouthuria katika sherehe hizo
Mbunge wa viti maalumu CCM Amina Mollel akiwa anasalimia na moja na mzee aliekuwa rrika la kurianga ambae kwa sasa ameingia katika rika la Nyangulo.


Wazazi hususa ni jamii ya kimasai wametakiwa kuachana na zana ya kuwatenga na kutowapeleka shule watoto wa kike na wale ambao ni walemavu badala yake wawapeleke mashuleni kwani wao ndio viongozi wa baadae.

Hayo yamebainishwa na mbunge wa viti maalumu kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Amina Mollel wakati alipokuwa akizungumza kama mgeni rasmi katika sherehe za kupandisha ngazi rika kutoka katika rika la kurianga kuingia katika rika la Nyangulo ,sherehe ambazo zilifanyika katika Kijiji cha Oldenderet Kata ya Nduruma mkoani Arusha

Alisema kuwa kunabaadhi ya wazazi wamekuwa wakiwaficha watoto wao kisa ni walemavu jambo ambalo linawakosesha haki zao ikiwemo ya kupata elimu kutokana na kufichwa huko

“kwakweli wazazi wanavyoficha watoto wao hususa ni walemavu wanawanyima haki yao mfano kama mimi ningefichwa leo kweli ndugu zangu ningeweza kuwa kiongozi hivyo napenda kuwasihi wazazi wasiwafiche watoto hawa kwani wakiwapeleka shule kupata elimu itakuwa vizuri kwani pale watakapo maliza shule wanakuja kuwasaidia “alisema Amina

Aidha pia aliwataka wazazi hawa wa jamii ya kimasai na hata wale wa makabila mengine kuacha kuwaozesha watoto wakike mapema kwani watoto hao wakike nao wanahaki ya kupata elimu kwani elimu ni bure ,kuanzia ngazi ya msingi hadi sekondari hivyo ni vyema kama wazazi wakawasimamia watoto hususa ni wakike wakaenda shule

Aliongeza kwa kuwasihihi watoto wa kike kuweka kipaumbele swala la elimu kwani elimu ndio kila kitu katika maisha yao na iwapo watasoma kwa bidii wanaweza kuwa viongozi wakubwa wa serikalini hapo baadae

Alisema kuwa kunabaadhi ya watoto wa kike wamekuwa wanaacha kusoma kisa wanakimbilia maisha kitu ambacho sio kizuri kwani wanaweza kukimbilia maisha yakawapiga hivyo ni muhimu sana kama watasoma kwanza alafu maisha watayapata baadae baada ya kumaliza kusoma na kupata kazi zao nzuri

Vikundi vya VICOBA Mikoa ya Kanda ya Ziwa vyapata mkopo wa Bilioni 2.8


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira, Vijana na Watu Wenye Ulemavu,Bi. Jenista Mhagama akimkabidhi Mkurugenzi  Mtendaji wa FERUSCO Sustainable Development,Bw. Felisi Ngonyani mbele mfano wa hundi yenye thamani ya Tsh. Bilioni 1.2 wakati wa uzinduzi wa utoaji mikopo katika mikoa ya kanda ya ziwa, Katibu Mtendaji wa Baraza la Taiifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, Bi. Beng’i Issa  wapili kulia, Waziri wa Nishati,Dkt.Medard Kalemani wa pili kushoto, Mkuu wa Mkoa wa Geita,Bw. Robert Lughumbi wa tatu kushoto, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Geita na Mbunge, Bw. Joseph Musukuma kulia na Meneja Tawi  TPB Mwanza, Bw. Shaban Telatela kushoto. 
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira, Vijana na Watu Wenye Ulemavu, Bi. Jenista Mhagama  wa tatu kulia akimkabidhi mfano wa hundi Mkurugenzi wa Mtandao wa ViVOBA Endelevu (Visudent) Kamara Mohamed kulia, Katibu Mtendaji wa Baraza la Taiifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Bi. Beng’i Issa wa pili kulia, Waziri wa Nishati, Dkt.Medard Kalemani wa pili kushoto, Mkuu wa Mkoa wa Geita,Bw. Robert Lughumbi wa watu kushoto, Meneja Tawi  TPB Mwanza, Bw. Shaban Telatela kushoto. 
Wanachama wa Vikundi vya VICOBA wakiwa katika uzinduz wa utoaji wa mikopo ya uwezeshaji ambapo vikundi 272 vilipata mikopo toka Benki Posta (TPB) na Taasisi ya Hudua za Kifedha na Mikopo- UTT Microfinance Chini ya Udhamini wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), 

Vikundi vya VICOBA 272 vya mikoa ya Kanda ya Ziwa vimenufaika na uwezeshaji wa mikopo ya Tsh. bilioni 2. 8 toka Benki ya Posta (TPB) na Taasisi ya Hudua za Kifedha na Mikopo- UTT Microfinance PLC ili wanachama wake waweze kuitumia katika shughuli za ujasiriamali na kushiriki katika uchumi wa taifa lao.

Vikundi vya VICOBA vilivyo nufaika na mikopo hii vinatoka katika Wilaya au halmashauri za Mikoa ya Kagera, Geita, Mwanza, Simiyu na Mara kwa lengo la kuviwezesha viweze kushiriki katika kuondoa umasikini miongoni mwa wananchi.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa utoaji mikopo hiyo mkoani Geita, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu,Sera,Bunge, Ajira, Vijana na Watu Wenye Ulemavu,Bi. Jenista Mhagama alisema mkopo huo ni sehemu ya Uwezeshaji wananchi kupitia vikundi vya ViCOBA ili waanzishe au waimarishe miradi yao ya ujasiriamali.

 ‘’Huu ni uwezeshaji Mkubwa na tunataka mkatumie fedha hizi kuendeleza miradi yenu ya ujasiriamali ili ikazalishe na muweze kuondokana na hali duni ya vipato,” na hiyo pia itawasaidia kushiriki katika uchumi wa nchi,aliongeza kusema,Bi Mhagama.

Mikopo hiyo imetolewa na TPB na UTT Microfinance PLC chini ya udhamini wa Baraza la Taifa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC).

Akifafanua zaidi alisema TPB ilitoa Tsh.bilioni 2.7 kwa vikundi 228 na UTT Microfinance imetoa Tsh.milioni  100, 300,00 kwa vikundi viwili vyenye wanachama 30.

Pia alizitaka taasisi zote za kifedha hapa nchi kuanza kwenda katika wilaya au halmashauri kutoa huduma za kifedha kama mikopo ilia wananchi waweze kuzitumia katika mirdi yaujasiriamali.

Katibu Mtendaji wa baraza hilo,Bi. Beng’i Issa alisema mikopo hiyo imedhaminiwa na baraza kupitia mfuko wa taifa wa uwezeshajii wananchi kiuchumi imetolewa kwa masharti nafuu na ni mwendelezo wa udhamini inaoufanywa ili mikopo itolewe kwa wajasiriamali kupitia SACCOS na VICOBA.

“Vikundi hivi ni matunda ya taasisi mwanvuli  zilizokubali kushirikiana na serikali kuvianzisha na kufundisha elimu ya VICOBA,” serikali itaendelea kushirikiana na taasisi hizi katika kazi ya kuzidi kuwawezesha wananchi aliongeza kusema



Alizitaja taasisi hizo mwamvuliza za VICOBA ni pamoja na Peoples Long Life Initiative (PLI), Ferusco Organisation VICOBA Sustainable Development Agency (FOVSDA), Upepo Wetu na VICOBA Sustainable Development Nertwork VISUDENT.

Kwa Mujibu wa Bi. Issa ni kwamba taasisi hizo mwanvuli pia zitahusika katika kusimamia maresjesho ya mikopo ya vikundi ili kuhakikisha zinarudi kwa wakati na vikundi vingine viweze kupata.

Alisema serikali kwa sasa imejielekeza katika kufikia uchumi wa viwanda na viwanda na  uwezeshaji huo unalenga wananchi wananzishe au kukuza viwanda vidogo vidogo ili mazao ya hapa nchini yaweze kuongezewa tham ani.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Geita,Bw. Robert Lughumbi alisema mikopo niyo ni ya kujivunia na yenye manufaa makubwa katika kukuza vipato vya wananchi kuondokana na umasikini katika kanda hiyo.

Serikali inafanya kazi kubwa ya kuweka mazingira wezeshi na kuibua fursa na serikali za mikoa ya kanda yetu tutahakikisha mikopo hii inaleta tija,” Wanachama wa vikundi hivyo wanafanya shughuli mbalimbali za kijasiriamali, aliongeza Kusema,Bw. Lughumbi.

Baraza hilo la Taifa linafanya kazi chini ya sheria uwezeshaji namba 16 ya mwaka 2004 na limedhamiria kuhakikisha uwezeshaji huo unawakomboa wananchi kiuchumi.

POLISI KIKOSI CHA RELI

POLISI KIKOSI CHA RELI ,WANAWAKE DAWATI LA JINSIA WASHEREHEKEA KUANZISHWA KWA MTANDAO NA KUTEMBELEA WATOTO WALIOLAZWA KATIKA TAASISI YA MOYO (JKCI)

 Askari wa Jeshi la Polisi kikosi cha Reli Koplo Grace Ndyamukama akimjulia hali mtoto aliyelazwa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) walipotembelea Taasisi hiyo leo  ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 10 tangu kuanzishwa kwa Mtandao wa Polisi  Wanawake Dawati la Jinsia. Kulia ni Mama wa mtoto Nasra Khalfan.
 Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP) ambaye pia ni Mkuu wa kituo cha Polisi Reli Martha Mdinka akimpa zawadi ya dawa ya meno, maji ya kunywa na juisi  Hadija Selemani ambaye amelazwa na mtoto katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) walipotembelea Taasisi hiyo leo  ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 10 tangu kuanzishwa kwa Mtandao wa Polisi  Wanawake Dawati la Jinsia.
  Askari wa Jeshi la Polisi kikosi cha Reli Rhoda Israel  akimpa zawadi ya juisi  Sada Issah ambaye amelazwa na mtoto katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) walipotembelea Taasisi hiyo leo  ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 10 tangu kuanzishwa kwa Mtandao wa Polisi  Wanawake Dawati la Jinsia.
 Maafisa wa  Jeshi la Polisi kikosi cha Reli wakigawa zawadi za maji ya kunywa, dawa za mENO,  juisi, mafuta ya kupakaa, sabuni za kuogea na kufulia kwa watoto waliolazwa  katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 10 tangu kuanzishwa kwa Mtandao wa Polisi  Wanawake Dawati la Jinsia.
 Askari wa Jeshi la Polisi kikosi cha Reli Jane John akimpa zawadi za maji ya kunywa, dawa ya meno,  juisi, mafuta ya kupakaa na  sabuni Maimuna Daud  ambaye amelazwa na mtoto katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) walipotembelea Taasisi hiyo leo  ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 10 tangu kuanzishwa kwa Mtandao wa Polisi  Wanawake Dawati la Jinsia.
Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP) ambaye pia ni Mkuu wa kituo cha Polisi Reli Martha Mdinka akiongea jambo na wagonjwa walipotembelea Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)  leo  ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 10 tangu kuanzishwa kwa Mtandao wa Polisi  Wanawake Dawati la Jinsia.
 Maafisa wa  Jeshi la Polisi kikosi cha Reli wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumaliza kutembelea Taasisii ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na kugawa zawadi za maji ya kunywa, dawa za meno,  juisi, mafuta ya kupakaa, sabuni za kuogea  na kufulia kwa watoto waliolazwa  katika taasisi hiyo  ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 10 tangu kuanzishwa kwa Mtandao wa Polisi  Wanawake Dawati la Jinsia.
Picha na JKCI

Rais Robert Mugabe amemfuta kazi Makamu wa Rais

Emmerson MnangagwaHaki miliki ya pichaAFP
Image captionEmmerson Mnangagwa
Makamu wa raia nchini Zimabawe Emmerson Mnangagwa amefutwa kazi, kwa mujbu wa wizara ya habari nchini humo.
Bw. Mnangagwa, 75, alionyesha tabia za kukosa uzalendo, waziri Simon Kahaya Moyo alisema.
Kufutwa kwake ni ishara kuwa mke wa rais Robert Muabe, Grace, atafuata nyayo za mumeme za kuwa rais wa Zimbabwe
Mapema Grace alitoa witi wa kutaka mumewe amfute kazi Mnangawa.
Bwana Mnangagwa, ambaye ni mkuu wa zamani wa idara ya ujasusi amekuwa kwenye mstari wa mbele kumrithi Rais Mugabe.

Mahakama ya juu yasitisha uchaguzi wa rais Liberia

George Weah (L) and Joseph Boakai (R)Haki miliki ya pichaREUTERS/ EPA
Image captionGeorge Weah (kushoto) na makamu wa Rais Joseph Boakai
Mahakama ya juu nchini Liberia imeamrisha kusitishwa kwa duru ya pili ya uchaguzi wa rais kufuatia madai ya kuwepo udanganyifu ikiwa imesalia siku moja kabla ya uchaguzi.
Ilisema kuwa uchaguzi huo hautafanyika hadi tume ya uchaguzi ichunguze madai hayo.
Madai hayo yalitolewa na mgombea wa chama cha Liberty Charles Brumskine, ambaye alichukua nafasi ya tatu wakati wa uchaguzi wa kwanza.
Hakuna tarehe mpya iliyotangazwa baada ya tarehe 7 mwezi huu.
Aliyekuwa nyota wa kandanda George Weah na makamu wa rais Joseph Boakai, wanatarajiwa kumenyana katika duru ya pili.