Na: Genofeva Matemu –WHUSM
Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza amevitaka vyombo vya habari vya serikali kufuata maadali na miiko ya uandishi wa habari kwa kuzingatia weledi ili umma eweze kupata habari zilizokidhi vigezo vya uandishi wa habari.
Rai hiyo ameitoa jana jijini Dar es Salaam alipofanya ziara katika Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) pamoja na Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) na kuzungumza na watendaji wa taasisi hizo.
“Vyombo vya habari vya serikali viwe mfano bora kwa kuwa mstari wa mbele kuhakikisha kuwa watanzania wanapata taarifa sahihi na kwa wakati kwani vyombo hivi ni moja kati ya mhimili mkubwa wa nchi na kama vitatumika vibaya madhara yake ni makubwa sana” amesema Mhe. Shonza
Aidha Mhe. Shonza amesema kuwa Serikali inathamini na kutambua mchango unaotolewa na vyombo vya habari vikiwemo vyombo vya serikali TBC katika kufikisha taarifa za ukweli na uhakika katika jamii.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) Dkt. Ayob Rioba amemhakikishia Mhe. Shonza kuwa TBC itaendelea kuzingatia weledi na maadili katika kuhabarisha umma huku ikiendelea kubuni vipindi mbalimbali vitakavovutia jamii kuangalia televisheni hiyo.
Naye Mkurugenzi Mtendaji Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) Dkt. Jim Yonazi amesema kuwa TSN imeendelea kuhakikisha kuwa taifa linahabarishwa kwa hakika kwa kutumia nyenzo mbalimbali na uzoefu tangu ilipoanzishwa miaka 88 iliyopita hivyo kuchangia katika maendeleo ya nchi yetu
“kwa sasa TSN ni zaidi ya magazeti, imejikita zaidi kuwa kampuni inayotoa huduma za habari kwa kutumia nyenzo mbalimbali za kiteknolojia ili kuweza kuendana na kasi ya maendeleo ya sayansi na taknolojia” amesema Dkt. Yonazi.
Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) Bw. HAB Mkwizu (kulia) akizungumza na Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (katikati) alipofanya ziara katika Kampuni hiyo jana Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji TSN Dkt. Jim Yonazi
Mkurugenzi Mtendaji TSN Dkt. Jim Yonazi akizungumza wakati wa ziara ya Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (kushoto) katika Kampuni hiyo jana Jijini Dar es Salaam
Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (kushoto) akizungumza na Menejimenti ya Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) alipofanya ziara katika Kampuni hiyo jana Jijini Dar es Salaam
Mhariri wa gazeti la Daily News Bw. Leonard Mwakalebela (kushoto) akimwelezea Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (kulia) namna habari zinavopitiwa na kupangwa katika gazeti hilo alipofanya ziara katika kampuni ya TSN jana Jijini Dar es Salaam
Meneja wa uchapishaji wa magazeti ya Serikali Bw. Boniface Mwajombe (kulia) akimuonyesha Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (katikati) mpangilio wa habari unavokuwa kabla ya gazeti kuchapishwa wakati wa ziara ya Naibu Waziri huyo katika kampuni ya TSN jana Jijini Dar es Salaam
Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza akiangalia mashine ya kuchapishia magazeti ya Serikali inavyofanya kazi alipofanya ziara katika Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) jana Jijini Dar es Salaam
Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (watano kushoto) katika picha ya pamoja na menejimenti ya Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) alipofanya ziara katika kampuni hiyo na kuangali shughuli zinazofanywa na kampuni hiyo jana Jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi Mkuu Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) Dkt. Ayob Rioba (kushoto) akizungumza na Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (kulia) alipofanya ziara TBC jana Jijini Dar es Salaam
Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (katikati) akimsikiliza Mkuu wa TBC Fm Bw. Othuman Iddy (kushoto) alipotembelea studio za TBC Fm wakati wa ziara yake TBC jana Jijini Dar es Salaam
Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (katikati) akimsikiliza mkuu wa TBC International Bw. Deogratius Salufu (kulia) alipotembela studio za redio hiyo jana wakati wa ziara yake katika Shirika la Utangazani la Taifa (TBC) Jijini Dar es Salaam
Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (kulia) akiwa katika meza ya kusomea taarifa ya habari ya Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) jana wakati wa ziara yake katika TBC Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) Dkt. Ayob Rioba
Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (watatu kushoto) katika picha ya pamoja na menejimenti ya Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) jana wakati wa ziara yake TBC Jijini Dar es Salaam. Watatu kulia ni Mkurugenzi Mkuu TBC Dkt. Ayob Rioba. Picha na: Genofeva Matemu - WHUSM