Monday, July 24

TANZANIA NA KENYA ZAMALIZA TOFAUTI ZA KIBIASHARA


Na: Paschal Dotto - MAELEZO.

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Kenya zimefanya mazungumzo ya pamoja na kutatua  vikwazo vilivyokuwa vikiikabili  sekta ya biashara baina ya nchi hizo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Jijini Dar es Salaam Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Augustine Mahiga ametoa taarifa juu ya kumalizika kwa tofauti za kibiashara baina ya nchi hizo. 

 “Bidhaa za Tanzania zilizowekewa vikwazo na nchi ya Kenya ni unga wa ngano pamoja na  gesi ya kupikia (LPG). Aidha juhudi, za Serikali ya Tanzania kuona vikwazo hivyo vinaondolewa na Serikali ya Kenya kwa wakati hazikuzaa matunda, hivyo Serikali ya Tanzania nayo iliweka vikwazo kwa bidhaa za maziwa na sigara kutoka Kenya kuingia katika soko la Tanzania,” amefafanua Dkt. Mahiga.

Amesema kuwa kutokana na mahusiano mazuri ya udugu yaliyopo kati ya Tanzania na Kenya na  kwa kujali manufaa mapana ya Jumuiya ya Afrika Mashariki viongozi wakuu wa nchi hizo mbili, Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli walikubaliana kuzungumza na kutoa vikwazo vya biashara hizo. 

Aidha, Dkt. Mahiga amesema, nchi hizo zimekubaliana kuunda Tume ya pamoja ambayo itakuwa na jukumu la kuepusha tofauti za kibiashara kati ya Tanzania na Kenya pamoja na kutolea ufumbuzi changamoto za kibiashara kati ya nchi hizo mbili pindi zinapojitokeza.

Tume hiyo itaongozwa na Mawaziri wa mambo ya Nje wa Tanzania na Kenya na kujumuisha mawaziri wanaohusika na masuala ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, Biashara, Fedha, Mambo ya Ndani ya Nchi, Kilimo, Uchukuzi na Utalii wa nchi hizo. 
 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Tanzania Balozi Dkt. Augustine Mahiga (kulia) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu mazungumzo ya pamoja kuhusu mahusiano ya kibiashara kati ya Serikali ya Tanzania na Kenya mapema hii leo jijini Dar es Salaam, katikati ni Mkurugenzi, Idara ya Ushirikiano wa Kikanda toka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Balozi Innocent Shiyo na kushoto ni Kaimu Balozi wa Kenya nchini Tanzania Peter Sang.
 Mkurugenzi, Idara ya Ushirikiano wa Kikanda toka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Balozi Innocent Shiyo akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu mazungumzo ya pamoja kuhusu mahusiano ya kibiashara kati ya Serikali ya Tanzania na Kenya mapema hii leo jijini Dar es Salaam, kulia ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Tanzania Balozi Dkt. Augustine Mahiga.

Baadhi ya waandishi wa habari wakimfuatilia Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Tanzania Balozi Dkt. Augustine Mahiga (hayupo pichani) wakati akitoa ufafanuzi kuhusu mazungumzo ya pamoja kuhusu mahusiano ya kibiashara kati ya Serikali ya Tanzania na Kenya mapema hii leo jijini Dar es Salaam. Picha na Eliphace Marwa -Maelezo

WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII, PROF. JUMANNE MAGHEMBE AMEWAPOKEA MABILIONEA 28 KUTOKA MABARA YOTE DUNIANI KATIKA HIFADHI YA TAIFA YA SERENGETI


Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe 
amewapokea Mabilionea 26 wa taasisi ya Young Presidents Organisation  (YPO) wakiwa na wenza wao katika Hifadhi ya Taifa  Serengeti kwa ajili ya kutembelea vivutio vya utalii katika ziara yao ya siku 3 nchini Tanzania.

Mabilionea hao ambao wanatoka katika mabara yote duniani wapo nchini Tanzania kama sehemu ya ziara yao katika nchi 8 duniani ikiwemo Uingereza, Rwanda, Maldives, Nepal, Bhutan na Rajastan.

Katika hafla ya Chakula cha jioni alichowaandalia Wageni wake,  Prof. Maghembe aliwakaribisha Tanzania na kwenye Maajabu ya Dunia yanayobebwa na Hifadhi ya Taifa ya Serengeti. Alisisitiza "hakuna eneo lolote katika uso wa Dunia lenye mkusanyiko wa wanyama wanaokula majani (herbivores) na wale wanaokula nyama (canivores) kama Serengeti". 

Prof. Maghembe aliwaeleza Wageni wake kuwa kuhifadhi ni gharama kubwa inayobebwa na Tanzania kwa niaba ya Dunia. Hivyo akawaomba wageni hao wawe mabalozi wa kuitangaza Tanzania kama eneo lenye  amani na vivutio vyenye ubora wa pekee. Hatua hiyo italeta watalii wengi na kuiongezea Tanzania mapato.

Aidha, aliwaomba warudi tena kuwekeza nchini ili washiriki kwenye uchumi unaokua kwa wastani wa 7% kwa kipindi cha miaka 15 sasa.

(SOURCE: WWW.WIZARAYAMALIASILINAUTALII.BLOGSPOT.COM).
Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe akizungumza na Mabilionea 26 kutoka taasisi ya Young Presidents Organisation  (YPO) wakiwa na wenza wao katika moja ya hoteli ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti wakati wa mapokezi yao jana kwa ajili ya ziara yao ya siku tatu nchini Tanzania.
 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), Alan Kijazi (katikati waliosimama) akizungumza na Mabilionea hao. Kulia kwake ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe .
Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe akizungumza na Mabilionea hao jana katika moja ya hoteli ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti. Kushoto kwake ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), Alan Kijazi.
Kiongozi wa msafara wa Mabilionea hao, Perry Amber akizungumza wakati wa mapokezi hayo jana katika moja ya hoteli ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti. 
Mabilionea hao kutoka taasisi ya Young Presidents Organisation (YPO) wakimsikiliza Waziri Maghembe.

RAIS DKT MAGUFULI AFUNGUA MIRADI MINNE YA MAENDELEO NA KUHUTUBIA WANANCHI


Rais wa Jamhuri Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli na Kulia kwa Mh Rais ni Balozi wa India Nchini Mhe Sandeep Arya, Kulia kwa Mh Rais ni Waziri Maji Mhandisi Gerson Lwenge, akifuatiwa na Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli na viongozi balimbali wa Mkoa wa Tabora wakikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa mradi wa Maji toka Ziwa Victoria Kwenda Kwenye Mji wa Tabora, Igunga na Nzega Julai 24, 2017.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli na Balozi wa India Nchini Mhe Sandeep Arya,wakiteta jambo mara baada ya Rais kuweka Jiwe la Msingi na Ufunguzi rasmi wa mradi wa Maji toka Ziwa Victoria Kwenda Kwenye Miji ya Tabora, Igunga na Nzega leo Julai 24, 2017.
Rais wa Jamhuri Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Joseph Magufuli akipeana mkono na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa mara baada ya ufunguzi wa Ujenzi wa Uwanja wa Ndege Tabora leo Julai 24, 2017.
Rais wa Jamhuri Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Joseph Magufuli akipata maelezo ya Mradi Ukarabati, Ujenzi na Upanuzi wa Uwanja wa Ndege Tabora toka kwa Mhandisi wa Ujenzi wa Uwanja huo Mhandisi Neema Joseph.
Rais wa Jamuhuri Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania,  Dkt John Pombe Joseph Magufuli  akikata utepe kwenye Ufunguzi wa barabara ya Tabora -Puge -Ngeza yenye Urefu wa Kilometa 114.9 akiwa na  Waziri wa Ujenzi na Mawasiliano Prof Makame Mbarawa na viongozi wengine wa mkoa wa Tabora.
Rais wa Jamuhuri Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania,  Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiwasalimia wananchi wakati wa ziara mkoani Tabora.

UJENZI WA UWANJA WA MAO TSE TUNG KUGHARIMU BILIONI 12


Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akitembelea harakati za ujenzi wa Uwanja wa Michezo wa Mao Tse Tung uliopo Mpirani Kikwajuni Mjini Zanzibar. Kushoto ya Balozi Seif ni Waziri wa Hbari, Utamaduni, Utalii na Michezo Rashid Ali Juma.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Omar Hassan Omar akimuonyesha Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif hayupo pichani ramani ya Uwanja wa Mao Tse Tung utakavyokuwa baada ya kukamilika kwake.
Balozi Seif katika picha ya pamoja na Uongozi wa ngzi ya juu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo pamoja na wahandisi wa nujenzi wa uwanja wa michezo wa Mao Tse Tung.
Balozi Seif akiagana na Mshauri wa Rais wa Zanzibar katika masuala ya Utamaduni Chimbeni Kheir baada ya kuangalia harakati za ujenzi wa uwanja wa michezo wa Mao hapo Mpirani Kikwajuni Mjini Zanzibar.  Picha na – OMPR – ZNZ.


Harakati za ujenzi wa Uwanja wa Michezo wa Mao Tse Tung uliopo Mpirani Kikwajuni Mjini Zanzibar zinaendelea karibu Miezi Miwili sasa chini ya Wahandisi wa Kampuni ya Kimataifa ya Zhengtai Group ya Jamuhuri ya Watu wa China.


Ujenzi huo unafuatia msada mkubwa ulioidhinishwa na Serikali ya Jamuhuri ya Watu wa China kwa Serikali ya Zanzibar katika azma ya kuimarisha uhusiano wa muda mrefu wa pande hizo mbili ukizingatia heshima uliopewa Uwanja huo wa kuitwa jina la Muasisiwa Taifa la China Hayati Mao Tse Tung.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alipata fursa ya kutembelea Uwanja huo kujionea harakati za ujenzi huo kazi ambayo inaonyesha mafanikio mazuri.

Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Omar Hassan Omar alisema eneo hilo litakuwa na Viwanja Viwili Vikubwa vya chezo wa Soka, viwanja vyengine vidogo vya Michezo ya ndani pamoja na eneo maalum la Mazoezi.

Hassan alimueleza Balozi Seif kwamba Moja ya Viwanja hivyo utajumuisha Majukwaa Mawili ya watazamaji ambapo mipango ya baadae Wizara inayosimamia Michezo itafikiria kuweka Vibaraza ili kuwapa fursa nzuri watu kutazama michezo kwa utulivu zaidi. 

Alieleza kwamba Uwanja huo utakaokuwa wa Kijamii zaidi tofauti na viwanja vyengine vinavyotoza viingilio vikubwa unatarajiwa kugharimu Dola za Kimarekani Milino Tano sawa na Shilingi Bilioni 12 za Kitanzania.

Naye Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Rashid Ali Juma alisema Serikali imezingatia mambo muhimu yaliyohitajika kufanywa kabla ya kuanza kwa ujenzi huo ili kuwaondoshea usumbufu wajenzi wa Mradi huo.

Waziri Rashid alisema mahitaji hayo muhimu ilikuwa ni pamoja na huduma za maji, huduma za umema pamoja na ulinzi wa vifaa na mali za Kampuni inayojenga Uwanja huo ya Zhengtai Group.

Naye kwa upande wake Mkuu wa Wahandisi wa ujenzi wa Uwanja wa MaoTse Tung kutoka Kampuni ya Zhengtai Group ya Nchini Bwana Ligen Zhang alimuhakikishia Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwamba kazi hiyo itaendelea kutekelezwa ili imalizike kwa wakati ulipangwa.

Hata hivyo Bwana Ligen alisema licha ya changamoto chache zilizojichomoza ikiwemo rasilmali ya mchanga lakini juhudi zitachukuliwa katika kuona mradi huo unakwenda vyema bila ya kuathiri ratiba nzima iliyowekwa.

Akitoa shukrani zake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliipongeza Serikali ya Jamuhuri ya Watu wa China kwa misaada inayotowa kwa Zanzibar katika kuimarisha miradi ya maendeleo.

Balozi Seif alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa upande wake itajitahidi kushirikiana na wahandisi wa Ujenzi huo wa uwanja ili kuona Mradi huo unakamilika katika kipindi kilichokusudiwa.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amewaonya Wananchi kuacha tabia ya wizi wa vifaa vilivyotengwa kwa ajili ya kazi hiyo kwani kufanya hivyo ni aibu kwa vile jamii ya Kimataifa itashangaa kuona miradi iliyotengwa kuwanufaisha Wananchi inafanyiwa hujuma.

Aliagiza vyombo vinavyohusika na ulinzi kuwachukulia hatua kali za kisheria na kinidhamu wale wote wanaofanya vitendo viovu vya kutaka kuiba vifaa vya ujenzi.

Othman Khamis Ame

Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar

YANGA YAENDELEA KUJIFUA UWANJA WA UHURU


  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

Kikosi cha Yanga kimeendelea tena na mazoezi mapema leo baada ya kupewa mapumziko ya siku mbili kutoka kwa Kocha Mkuu wa timu hiyo  Mzambia George Lwandamina.

Yanga waliokuwa wanafanya mazoezi ya Gym kwa takribani wiki  moja na nusu ikiwa ni katika programu ya Mwalimu Lwandamina ya kuwaweka fit wachezaji hao baada ya kuwa mapumzikoni kwa kipindi kirefu.

Leo mapema asubuhi kikosi hicho kiliingia katika Uwanja wa Uhuru kwa ajili ya kuendelea na mazoezi ya kujiandaa na msimu mpya wa ligi kuu 2017/18 huku wakitarajiwa kuwa mechi kadhaa za kirafiki.

Mechi ya kwanza ya kirafiki itakuwa ni Agosti 5 dhidi ya timu ya Singida inayonolewa na aliyewahi kuwa kocha wa timu hiyo Mholanzi Hans Van De Pluijm mchezo utakapigwa kwenye dimba la Uwanja wa Taifa.
 

Mshambuliaji wa Kimataifa wa Burundi Amis Tambwe akiwa katikati akipambana na wachezaji wa Yanga katika mazoezi ya timu hiyo yanayoendelea kwenye Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es salaam.
 Beki wa kulia wa Yanga Juma Abdul akiwa amemiliki mpira akijaribu kumtoka mchezaji mwenzake  katika mazoezi ya timu hiyo yanayoendelea kwenye Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es salaam.
 Wachezaji wa Yanga wakiwa katika mazoezi ya timu hiyo yanayoendelea kwenye Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es salaam.
Kocha George Lwandamina akijadiliana jambo na Beki kisiki Kelvin Yondani katika mazoezi ya timu hiyo yanayoendelea kwenye Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es salaam.

BALOZI SEIF AKUTANA NA UJUMBE WA KAMPUNI YA MONEO CONSULTING KUTOKA MAURITIUS


Visiwa vya Zanzibar na Mauritius vina fursa ya kubadilishana uzoefu katika miradi ya Maendeleo ili kujiongezea ujuzi na maarifa yanatayowawezesha Wananchi wake kuimarika zaidi kiuchumi hali itakayosababisha Mataifa yao kuongeza mapato.

Mwenyekiti wa Kampuni ya Kimataifa ya Ushauri kutoka Kisiwa cha Mauritius { Moneo Consulting } Bwana Devanand Virahsawmy akiuongoza ujumbe wa viongozi wa Kampuni hiyo alisema hayo wakati wa mazungumzo yake na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Vuga Mjini Zanzibar.

Bwana Devanand Virahsawmy alisema Sekta ya elimu ambayo ndiyo mama katika Taifa lolote Duniani inaweza kuwa mwanzo wa ushirikiano huo unaoweza kutoa nafasi kwa vijana wa pande hizo mbili kujipatia Elimu ya Msingi, Sekondari hadi vyuo Vikuu .

Alisema mpango huo wa pamoja kupitia Kaisheni ya pamoja kwa Nchi zilizozunguukwa na Bahari ya Hindi utaongeza chachu ya uchumi kwa Vijana waliobobea Kitaaluma sambamba na ongezeko la ajira.

Bwana Devanand alisema Visiwa vya Mauritius tayari vimeshapiga hatua kubwa ya maendeleo hasa katika Sekta ya Utalii kiwango ambacho wanaweza kusaidia Taaluma kwa Nchi zilizo jirani na Visiwa hivyo.


Mwenyekiti huyo wa Kampuni ya Moneo Consulting alimueleza Balozi Seif pamoja na Mawaziri, Makatibu Wakuu na Watendaji Wakuu wa SMZ Kwamba Uongozi wa Kampuni yake upo Zanzibar kuitika wito Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wa kuangalia fursa za Uwekezaji.

Alieleza kwamba Kampuni hiyo tayari imeshijengea uwezo wa kuendesha miradi mbali mbali ya Kiuchumi na Maendeleo akiitaja baadhi yake kuwa ni pamoja na Miradi ya Umeme, Bara bara, Utalii, Benki ya Ufukweni { Off show Bank } Viwanda vya vidogo vidogo pamoja na Uvuvi wa Bahari Kuu.

Akitoa ufafanuzi wa mipango ya Uwekezaji Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Uwekezaji Vitega Uchumi Zanzibar {ZIPA} Nd. Salum Nassor Khamis alisema Zanzibar imeanza kufanya mabadiliko ya uchumi wake katika Miaka ya 90 ili kutoka nafasi kwa Taasisi yenye uwezo wa uwekezaji kushiriki kwenye mabadiliko hayo. 

Ndugu Salum alisema ushirikishwaji wa Sekta binafsi katika kuchangia uchumi wa Taifa umezingatiwa ili kujenga jamii itakayokwenda sambamba na mabadiliko ya Kiuchumi Duniani.

Naye kwa upande wake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliueleza Ujumbe huo wa Kampuni ya Ushauri ya Moneo kwamba Zanzibar ina mtazamo wa kuwekeza katika sekta ya Uvuvi wa Bahari Kuu.

Alisema Rasilmali ya Bahari ni eneo linaloweza kujenga uchumi imara utakaoweza kuongeza mapato ya Taifa sambamba na kupunguza ufinyu wa ajira uliowakumba Vijana wengi wanaomaliza masomo yao Nchini.

Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar

24/7/2017.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akisalimiana na Mwenyekiti wa Kampuni ya Kimataifa ya Ushauri kutoka Mauritius (Moneo Consulting) Bw. Devanand Virahsawmy Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.
Balozi Seif na Baadhi ya Mawaziri wa SMZ, Makatibu Wakuu na Watendahi Wakuu wa SMZ akizungumza na Ujumbe wa Kampuni ya Moneo Consulting kutoka Mauritius.
Mwenyekiti wa Kampuni ya Kimataifa ya Ushauri kutoka Mauritius (Moneo Consulting) Bw. Devanand Virahsawmy akisisitiza jambo wakati ujumbe wake ulipofanya mazungumzo na Balozi Seif.
Balozi Seif akiwa katika picha ya pamoja na Ujumbe wa Kampuni ya Moneo Consulting na badhi ya Mawaziri, Makatibu Wakuu na Watendaji Wakuu wa SMZ. Picha na – OMPR – ZNZ.

Neno La Leo: Tumbili Hata Akizeeka Haachi Hulka Yake!


Image may contain: 1 person, standing, tree and outdoor
Ndugu zangu,

Katika ulimwengu huu kuna tabia na hulka. Hivi viwili vina tofauti. Kuna sifa na uwezo, navyo ni viwili tofauti.

Tabia ya mwanadamu yaweza kubadilika, lakini si hulka yake. Na mwanadamu anaweza kuwa na sifa za kufanya jambo lakini akakosa uwezo, na kinyume chake. 

Na kibaya zaidi ni pale majungu na fitna yanapogubika sifa na uwezo wa mtu. Kwamba badala ya mwanadamu kupimwa kwa sifa na uwezo wake, majungu na fitna dhidi ya mwanadamu huyo yanawekwa mbele, na hivyo kufanywa kuwa kipimo.

Ndio, kuna wanadamu wenye kuishi kwa kupika majungu na fitna dhidi ya wanadamu wenzao. Tofauti na tabia, hizo ni hulka za wanadamu hao, haziwezi kubadilika.

Mwone tumbili alivyo, tumbili hata akizeeka, haachi hulka yake. Kupalamia miti ni hulka ya tumbili. Hivyo, tumbili hata akizeeka, hafikiri hata siku moja kukaa chini ya mti na kupumzika. Atahakikisha anapalamia hata mti mfupi wa mpapai, alimradi tu akae juu ya mpapai. Hapo atajiona ametimiza utumbili wake. 

Nini adili ya jambo hili?

Tumbili limekuwa neno maarufu sasa. David Kafulila alipata kuitwa tumbili Bungeni. Kumbe, Kafulila hakuwa tumbili, waliomwita Kafulila tumbili ndio tumbili wenyewe.

Bahati mbaya, nchi yetu ina tumbili wengi na wamepewa nafasi za uongozi na maamuzi. Ni jambo jema kwa Rais wa Jamhuri kalitambua hilo. Kazi yetu ni kumsaidia Rais na watendaji wake wasio tumbili, kuwaonyesha waliko tumbili kwenye nafasi za kuwatumikia Wananchi na kwa maendeleo ya nchi.

Ni Neno La Leo.
Maggid.
Iringa.

Trump aunga mkono Urusi kuwekewa Vikwazo


Ikulu ya White House imesema kuwa Rais Donald Trump, anaunga mkono makubaliano yasiopendelea upande wowote yaliyoafikiwa katika bunge la Congress ya kuiwekea vikwazo Urusi.

Imesema kuwa Rais Donald Trump, anaunga makubaliano yasiopendelea upande wowote yaliyoafikiwa katika bunge la Congress ya kuiwekea vikwazo Urusi.

Afisa habari wa Ikulu ya White House Sarah Huckabee-Sanders anasisitiza kuwa, licha ya hatua hiyo awali white house ilipinga mswada wa uamuzi huo, japo kuwa kwa sasa inafurahia mswaada wa mwisho uliopitishwa.

Bunge la Congress linataka Urusi iadhibiwe kwa madai ya kuingilia uchaguzi wa urais uliofanyika mwaka jana nchini Marekani.

Bunge hilo linatarajiwa kupiga kura hapo kesho siku ya jumanne kupitisha muswada huo kuwa sheria inayoitaka ofisi ya Rais kutoingilia mwenendo wa hatua za kidplomasia dhidi ya Moscow.

Ikulu ya white house hata hivyo imekuwa na kauli zinazotofautiana mara baada ya msimamo wa bunge la Congress katika vikwazo vipya dhidi ya tuhuma za Urusi.

Kupitishwa kwa sheria hiyo na bunge la congress kutamnyima uwezo Rais Trump, kuondoa kikwazo chochote kitakachopitishwa dhidi ya Urusi.

IGP SIRRO AKUTANA NA KAMATI YA ULINZI NA USALAMA MKOANI MWANZA


Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Simon Sirro (katikati), akimsikiliza Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongella, wakati alipofika ofisini kwake jana. IGP Sirro, yupo mkoani humo ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya kikazi, yenye lengo la kujitambulisha kwenye Kamati ya Ulinzi na Usalama pamoja na kuzungumza na askari wa Jeshi hilo. kulia ni Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza, Naibu Kamishna wa Polisi, DCP Ahmed Msangi.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Simon Sirro (aliyesimama), akizungumza na baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa wa Mwanza, kwa lengo la kujitambulisha, ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya kikazi yenye lengo la kuzungumza na askari wa Jeshi hilo.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Simon Sirro, akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa wa Mwanza, alipofika kwa lengo la kujitambulisha, ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya kikazi yenye lengo la kuzungumza na askari wa Jeshi hilo.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Simon Sirro, akizungumza na baadhi ya askari wa Jeshi hilo baada ya kumaliza kikao kazi na maofisa na askari ambapo aliwasisitiza kuzingatia weledi wakati wa kutekeleza majukumu yao. Picha na Demetrius Njimbwi – Jeshi la Polisi.


RAIS DKT. MAGUFULI AANZA ZIARA MKOANI TABORA NA KUZINDUA MIRADI YA BARABARA


 Rais wa Jamuhuri Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli na Mke wake Mama Janeth Magufuli na Mkuu wa Mkoa wa Tabora  Agrey Mwanri wakiondoa kitambaa kuashiria Ufunguzi wa Barabara ya Tabora Ndono - Urambo yenye urefu wa kilometa  94 iliyojengwa kwa kiwango cha lami Mkoani Tabora 
Rais wa Jamuhuri Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akikata utepe kuashiria Ufunguzi wa Barabara ya Tabora Ndono - Urambo yenye urefu wa kilometa  94 iliyojengwa kwa kiwango cha lami Mkoani Tabora 
 Rais wa Jamuhuri Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akihutubia Wananchi wa Kariua Mkoani Tabora wakati wa Ufunguzi wa Barabara ya Kariua -Kazirambwa yenye urefu wa kilometa 56 iliyojengwa kwa kiwango cha lami Mkoani Tabora 
 Wananchi wa Kariua na Viunga vyake Wakimsikiliza Mh Rais wa Jamuhuri Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiwahutubia wakati wa Ufunguzi wa Barabara ya Kariua -Kazirambwa yenye urefu wa kilometa 56 iliyojengwa kwa kiwango cha lami Mkoani Tabora Mhe Rais yupo mkoani humo 
 Wananchi wa Mji wa Urambo na Viunga vyake Wakimsikiliza Mh Rais wa Jamuhuri Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiwahutubia wakati wa Ufunguzi wa Barabara ya Tabora Ndono - Urambo yenye urefu wa kilometa  94 iliyojengwa kwa kiwango cha lami Mkoani Tabora 
 Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli,akiwapungia Mikono kwa Kuwasalimia Wananchi wa Kariua na Viunga vyake Walio jitokeza kumsikimsikiliza Mh Rais wa Jamuhuri Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli wakati wa Ufunguzi wa Barabara ya Kariua -Kazirambwa yenye urefu wa kilometa 56 iliyojengwa kwa kiwango cha lami Mkoani Tabora 
 Rais wa Jamuhuri Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akihutubia Wananchi wa Urambo Mkoani Tabora wakati wa Ufunguzi wa Barabara ya ya Tabora Ndono - Urambo yenye urefu wa kilometa  94 iliyojengwa kwa kiwango cha lami Mkoani Tabora 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli na Mke wake Mama Janeth Magufuli wakimpa pole Mama Mzazi wa aliyekuwa Spika wa Bunge la Tanzania Marehemu Samweli John Sitta.
Picha zote na IKULU