Saturday, October 28

Mvua yaua wengine wawili


Kibaha. Miili ya watu wawili akiwemo mgambo imeopolewa  baada ya kuzama maji kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha  maeneo mbalimbali.
Miili hiyo imeopolewa  saa  saba mchana  Oktoba 27 mjini Kibaha  kwenye mto Kiluvya na imetambulika ni ya Issa Ally (28) askari mgambo na Saimon Ramadhani (27).
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoani Pwani Blasilus Chatanda amesema leo kwamba mgambo huyo alikuwa  akijaribu kumuokoa mtoto  aliyetaka kusombwa na maji kutokana na mvua hiyo.
Amesema mgambo huyo amejitahidi kadri ya uwezo wake kuokoa maisha ya mtoto huyo ambaye hata hivyo hajaonekana mpaka leo.
Kamanda Chatanda amesema kwamba mwili wa mgambo huyo umeonekana baada ya maji kupungua.
Kamanda Chatanda amesema kwamba Ramadhani ambaye ni mkazi wa Muheza kata ya Pangani mjini Kibaha na alisombwa na maji wakati akijaribu kuvuka mto Mpiji. 
"Kama mnavyojua mvua imeendelea kunyesha sehemu mbalimbali mito imejaa maji, sasa inaonekana huyu naye aliyapuuza maji hayana kasi kubwa akawa anavuka yakamshinda nguvu yakamsomba na kusababisha kifo"amesema Chatanda.
Kaimu Kamanda huyo ameongeza kuwa miili hiyo imepelekwa kuhifadhiwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Pwani Tumbi kusubiri uchunguzi wa daktari.

Udart yahamisha baadhi ya shughuli zake Jangwani


Dar es Salaam. Mvua kubwa iliyonyesha jijini Dar es Salaam kwa siku mbili imesababisha kampuni ya Usafiri wa Mabasi Yaendayo Haraka (Udart) kuhamisha baadhi ya shughuli eneo la Jangwani.
Mbali ya kuathiri shughuli katika eneo hilo, Udart imesema mvua iliyonyesha Jumatano Oktoba 25 na Alhamisi Oktoba 26,2017 imesababisha mabasi 29 ya kampuni hiyo kuharibika.
Udart imehamisha huduma za kulaza magari, ujazaji wa mafuta na gereji.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano cha Udart, Deus  Bugaywa amesema leo Jumamosi Oktoba 28,2017 kuwa vituo vya Gerezani na Kimara ndivyo vitatoa huduma ya gereji.
Amesema vituo vya Kivukoni, Gerezani na Kimara vitatoa huduma ya kulaza magari na kuyajaza mafuta.
Bugaywa amesema mvua imeathiri mabasi 29 kati ya 134 yanayotoa huduma jijini Dar es Salaam.
Amesema vifaa vya mabasi vimesombwa na maji na pia baadhi ya vyumba vya ofisi vimeharibiwa.
"Kwanza, tunawaomba msamaha wateja kwa usumbufu uliojitokeza Alhamisi wakati wa mvua. Kwa sasa watuvumilie hadi Jumapili Oktoba 28,2017 huduma zitakaporejea vizuri. Mabasi 29 yalishindwa kuendelea na huduma baada ya kuathiriwa na mvua," amesema Bugaywa akizungumza na waandishi wa habari.
Amesema, "Mabasi hayo yalikuwa kwenye marekebisho katika injini, giaboksi na difu. Mvua zilipoanza maji yalijaa na matengenezo yalisimama. Kwa sasa mafundi wanaangalia athari na namna gani zishughulikiwe mapema ili magari yarudi barabarani."
Bugaywa amesema kwa sasa si rahisi kuwa na makadirio ya hasara iliyotokana na mvua.

Alipoulizwa kuhusu hatima ya kutumia majengo ya ofisi yaliyopo Jangwani, Bugaywa amesema suala hilo linahitaji majadiliano kati ya Serikali na wadau wote wanaohusika katika mradi huo.
"Tutakaa na wadau wote, Udart ni sehemu tu ya wadau, kwa hiyo tutakaa tuone ni kwa namna gani tunazuia au tunapunguza hasara kutokana na mvua," amesema Bugaywa.

Watoto waliokuwa wakicheza ufukweni mwa bahari wafa maji


Zanzibar. Watoto watatu wamefariki dunia baada ya kuzama baharini eneo la Muungoni mkoani Kusini Unguja.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Unguja, Kheri Mussa Haji amethibitisha vifo hivyo na kuwataja watoto hao kuwa ni Issa Kombo Hassan (11), Abrahman Zahran Ali (7) na Omar Aboud (10) wote wakazi wa Muungoni.
Amesema uchunguzi uliofanywa umebaini vifo vya watoto hao vimetokana na kunywa maji mengi.
Akizungumza kwa niaba ya familia za watoto hao, Sheha wa Muungoni, Shafii Hassan amesema watoto hao walikuwa wakicheza ufukweni mwa Bahari ya Hindi.
Amesema watoto hao baadaye waliingia kwenye dau lililokuwa limetia nanga eneo hilo ambalo lilielea na wakaingia baharini pasipo watu waliokuwa karibu kujua.
Shafii amesema baada ya muda kupita ndipo watu hao walipoanza kuulizana ni wapi walipokwenda watoto hao na hawakupata jibu.
Amesema msako wa watoto hao ulianza jana Ijumaa Oktoba 27,2017 kuanzia saa 11:00 jioni hadi saa mbili usiku walipoliona dau na miili yao kupatikana chini ya bahari.
Sheha huyo amesema miili ya watoto hao imeshakabidhiwa kwa jamaa zao kwa ajili ya mazishi.

Zitto aomba jumuiya za kimataifa kuchunguza kasi ya ukuaji uchumi nchini


Dar es Salaam. Chama cha ACT Wazalendo kimeziomba Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) na Benki ya Dunia (WB) kufanya uchunguzi maalumu wa takwimu za kasi ya ukuaji wa uchumi ya robo ya pili ya mwaka na kuchukua hatua endapo itabainika kile anachodai kuwa Serikali ilipika takwimu.
Kiongozi wa chama hicho, Zitto Kabwe ametoa msimamo wake huo leo Jumamosi jijini Dar es Salaam katika mkutano na waandishi wa habari.
Zitto amedai chama hicho kimebaini  takwimu zilizotolewa na Serikali za Aprili hadi Juni haziko sahihi.
Amedai takwimu za Serikali zinaonyesha kasi ya ukuaji wa uchumi katika robo ya pili ya mwaka ni asilimia 5.7, tofauti na za ukokotozi kwa kanuni za kiuchumi anazodai zinaonyesha ni asilimia 0.1.
"Hatujatafuta takwimu nyingine, hizi ni taarifa zilezile zilizotolewa na BoT na NBS lakini ukikokotoa utaona uchumi tulionao unasinyaa badala ya kukua na hali ikiendelea hivi hadi Juni 2018 kutakuwa hakuna uchumi Tanzania," amedai Zitto.
Amedai sababu hiyo inachangia maisha ya Watanzania kuendelea kuwa magumu ilhali Serikali imekuwa ikitoa taarifa za uchumi kukua.
Zitto amegusia pia takwimu za mapato yanayokusanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) akidai nazo haziko sahihi.
Amesema ni vyema wakati TRA ikitoa takwimu zake ikaeleza mapato kwa kila idara bila kuchanganya marejesho na madeni ambayo hayajalipwa.
"Taarifa yao ieleze kinagaubaga mapato ya idara ya forodha, walipa kodi wakubwa na walipa kodi za ndani. Wasiishie hapo, kati ya fedha wanazotaja kukusanya iwekwe wazi madeni na marejesho ni yapi tofauti na  inavyofanywa sasa," amesema.
Zitto ametaka Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kufanya ukaguzi wa mapato ya Serikali ya Julai na Agosti na kuweka wazi taarifa hiyo.

Waziri Mwijage asema ugumu wa maisha ni wa mpito


Dar es Salaam. Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage amesema maisha magumu wanayopitia wananchi kwa sasa yanatokana na mabadiliko ambayo Serikali inayafanya na hali itakuwa nzuri baadaye.
Mwijage alisema hayo jana Ijumaa Oktoba 27,2017 wakati wa hafla ya utoaji wa tuzo kwa kampuni 100 za kati zilizofanya vizuri mwaka huu. Shindano hilo huandaliwa na kampuni ya KPMG kwa ushirikiano na kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL) kupitia gazeti la The Citizen.
Waziri Mwijage amesema hiki ni kipindi cha mpito ambacho kina mwisho na Serikali inafanya mabadiliko mbalimbali ikitaka kujua matumizi yake halisi.
“Tumekuwa hatuna uhakika wa matumizi yetu au tunachonunua. Msiwe na wasiwasi, ni kipindi cha mpito na kina mwisho wake, tutatoka. Tuwe wavumilivu tu,” alisema Mwijage mbele ya jumuiya ya wafanyabiashara waliohudhuria hafla hiyo kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Alisema lengo la kuanzisha mpango wa pili wa maendeleo wa miaka mitano ni kujenga uchumi wa viwanda na kuleta maendeleo ya watu. 
Waziri Mwijage amesema anaamini mtu mwenye shughuli ya kufanya atapata chochote.
Amesema anatambua kwamba sekta binafsi ni mhimili wa uchumi wa Taifa na kwamba, ukitaka kujenga uchumi shindani lazima uwe na sekta binafsi yenye nguvu na ushindani mkubwa.
“Jukumu langu ni kuhakikisha kwamba sekta binafsi inakuwa na ushindani mkubwa na ili kufanikisha hilo ni lazima niwasikilize ninyi,” amesema.
Waziri Mwijage pia alielezwa na wafanyabiashara hao jinsi Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) inavyowanyanyasa, kuwabambikia kodi kubwa na jinsi maofisa wake wanavyojipa mamlaka makubwa.
Waziri Mwijage alisema anafahamu suala hilo.
“Nalifahamu suala la manyanyaso ndiyo maana nasema tuko kwenye kipindi cha mpito. Kuna watu nawaita ‘wasiojulikana’ kwa sababu wao hawajulikani upande wa polisi wala upande wa TRA,” alisema waziri huyo.
Akiwashukuru wageni waalikwa, Mhariri Mtendaji wa MCL, Bakari Machumu alisema ndani wiki mbili zijazo, gazeti la The Citizen litaandaa toleo maalumu litakalobeba maudhui ya shindano hilo.
Machumu amewapongeza waliojitokeza kushindana na washindi, akiitaka Serikali kusaidia kuwaelimisha wafanyabiashara kuhusu kodi kwa sababu baadhi yao wakisikia kuhusu shindano la kampuni 100 za kati wanajua kuna kuongezewa kodi.
Katika shindano hilo, kampuni 10 zilizofanya vizuri mwaka huu kwa kuanza na nafasi ya kwanza ni Dar Ceramic Centre 2001 Ltd, Songoro Marine Transport, Modern Fitting Mart Ltd, Transit Ltd, Meru Spring Water Ltd, Economic and Business Foundation Ltd, Computer and Network Technology, Premier Agencies Tanzania Ltd, Tanpack Tissue Ltd na Tahafresh Handling Ltd.
Mkurugenzi mtendaji wa Dar Ceramic Centre 2001 Ltd, Hussein Nathoo alisema siri ya mafanikio yao ni kupanua biashara. Mwaka jana ilishika nafasi ya sita katika shindano hilo ikiwa na matawi saba nchi nzima lakini sasa yapo 11.

Washindi wa Vipaji vya Sauti lafikia tamati jijini Dar, Kumi kwenda China


Washindi 25 wa shindano la vipaji vya sauti wakiwa kwenye fainali hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa LAPF jijini Dar es Salaam.


Msanii maarufu nchini Tanzania Kutoka kundi la Orijino Komedi maarufu kama Mpoki a k a Muarabu wa Dubai(wa kwanza kulia) kizungumza jambo mara baada ya kutaja washindi 25 waliofuzu kuingia fainali ya shindano la Vipaji vya Sauti katika tamthiliya za kigeni kwa awamu ya pili ya mwaka 2017.
Majajji wa shindano la vipaji vya sauti la awamu ya pili  lililofanyika katika ukumbi wa LAPF jijini Dar es Salaam leo. Wa kwanza kishoto ni Msanii wa filamu nchini Jacob Stephen maarufu kama JB, kulia  Msanii wa muziki wa asili, Mrisho Mpoto pamoja na aliyekuwa mshindi wa shindano la vipaji vya sauti mwaka 2016/17.

Baadhi ya washiriki wa shindano la vipaji vya sauti msimu wa pili wa mshindano hayo yanayodhamuniwa na Startimes Tanzania wakionesha namna wanavyoweza kuigiza sauti kwenye fainali iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Msanii maarufu nchini Tanzania Kutoka kundi la Orijino Komedi maarufu kama Mpoki a k a Muarabu wa Dubai akizungumza jambo kwenye fainali ya shindano la kusaka vipaji lililofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wageni waalikwa wakifuatilia shindano la vipaji vya sauti msimu wa pili kwa mwaka 2017.
 Makamu wa Rais wa Startimes Tanzania, Zuhura Hanif akizungumza na waandishi wa habari wakati wa  shindano la vipaji vya sauti msimu wa pili mwaka 2017 lililofanyika katika ukumbi wa LAPF jijini Dar es Salaam.
Washindi 10 wa shindano la vipaji vya sauti walioshinda kwenda nchini China kufanya kazi makao makuu ya Kampuni ya Startimes  kwenye fainali hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa LAPF jijini Dar es Salaam.
 Mmoja wa washindi walioingia kumi bora akipokea zawadi ya simu ya Startimes kutoka kwa Makamu wa Rais wa Startimes Tanzania, Zuhura Hanif mara baada ya kumalizika kwa shindano la vipaji vya sauti msimu wa pili lililofanyika katika ukumbi wa LAPF jijini Dar es Salaam.
 Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA), Dkt. Seleman Sewangi(kulia) akimkabidhi zawadi ya Television ya Startimes mshindi wa kwanza wa shindano la vipaji vya sauti msimu wa pili, Coletha Raymond mara baada ya kuibuka mshindi wa shindano hilo.

Mshindi wa kwanza hadi wa tatu wa shindano la vipaji vya sauti msimu wa pili mwaka 2017 wakiwa kwenye picha ya Pamoja.

Rais wa Dkt Magufuli aapisha Makatibu Wakuu , Naibu Makatibu Wakuu na Wakuu wa Mikoa wapya

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimuapisha Mhe. Adam Kigoma Malima kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 28, 2017 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimpatia nyenzo za kazi baada ya kumuapisha Mhe. Adam Kigoma Malima kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 28, 2017 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimuapisha Mhe. Alexander Pastory Mnyeti kuwa Mkuu wa Mkoa wa Manyara Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 28, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimkabidhi nyenzo za kazi baada ya kumuapisha Mhe. Alexander Pastory Mnyeti kuwa Mkuu wa Mkoa wa Manyara Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 28, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimuapisha Mhe.Joackim Leonard Wangabo kuwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa. Kabla ya uteuzi huu Bw. Wangabo alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu na anachukua nafasi ya Kamishna wa Polisi Zelote Stephen ambaye amestaafu.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimkabidhi nyenzo za kazi baada ya kumuapisha Mhe. Joackim Leonard Wangabo kuwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimuapisha  Mhe. Robert Gabriel Luhumbi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Geita. Kabla ya uteuzi huu Bw. Luhumbi alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Korogwe na anachukua nafasi ya Meja Jen. Ezekiel Kyunga ambaye amestaafu.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimkabidhi nyenzo za kazi baada ya kumuapisha  Mhe. Robert Gabriel Luhumbi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Geita. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimuapisha Mhe Bw. Gelasius Gasper Byakanwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara. Bw. Byakanwa alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai na anachukua nafasi ya Bi. Halima Dendego.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimkabidhi nyenzo za kazi baada ya kumuapisha Mhe Bw. Gelasius Gasper Byakanwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimuapisha Mhe.Bi. Christine Solomon Mndeme kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma kabla ya kumbadilisha na kuwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, kubadilishana na Dkt. Bilinith Mahenge anayehamia Dodoma Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 28, 2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimuapisha Mhe.Bi. Christine Solomon Mndeme baada ya kumuapisha kuwa  Mkuu wa Mkoa wa Dodoma kabla ya kumbadilisha na kuwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, kubadilishana na Dkt. Bilinith Mahenge anayehamia Dodoma Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 28, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimuapisha Mhe.Bi.Suzana Mlawi kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo. Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 28, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimkabidhi nyenzo za kazi baada ya kumuapisha Mhe.Bi.Suzana Mlawi kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo. Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 28, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimuapisha Mhe. Dorothy Mwanyika kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi
Vingozi wakati wa hafla ya kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimuapisha Mhandisi Joseph Kizito Malongo kuwa Katibu Mkuu  Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira.   
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimmkabidhi nyenzo za kazi baada ya kumuapisha Mhandisi Joseph Kizito Malongo kuwa Katibu Mkuu  Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira.  
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimuapisha   Prof. Simon S. Msanjila kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Madini.            
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimkabidhi nyenzo za kazi baada ya kumuapisha   Prof. Simon S. Msanjila kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Madini.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimuapisha  Dkt. Thomas Didimu Kashililah kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya KilimoIkulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 28, 2017 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimkabidhi nyenzo za kazi baada ya kumuapisha  Dkt. Thomas Didimu Kashililah kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya KilimoIkulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 28, 2017 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimuapisha   Naibu Katibu Mkuu (Viwanda) – Ludovick J. Nduhiye (ATAAPISHWA)
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimkabidhi nyenzo za kazi baada ya kumuapisha   Naibu Katibu Mkuu (Viwanda) – Ludovick J. Nduhiye (ATAAPISHWA)
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimuapisha  Mhe Dorothy Mwaluko kuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akikabidhi nyenzo za kazi baada ya kumuapisha  Mhe Dorothy Mwaluko kuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
      Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimuapisha Mhe. Butamo Kasuka Phillipo kuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimkabidhi nyenzo za kazi baada ya kumuapisha Mhe. Butamo Kasuka Phillipo kuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimuapisha  kuwa Naibu Katibu Mkuu (Biashara na Uwekezaji) – Prof. Joseph Buchwaishaija
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiweka sahihi katika hati yake ya kiapo baadavya kumuapisha  kuwa Naibu Katibu Mkuu (Biashara na Uwekezaji) Prof. Joseph Buchwaishaija
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimuapisha   Mhe    Nicholaus B. William kuwa Naibu Katibu Mkuu   Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 28, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli baada ya kumuapisha   Mhe    Nicholaus B. William kuwa Naibu Katibu Mkuu   Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 28, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimuapisha  Bi. Susana Mkap a kuwa  Naibu Katibu Mkuu (Utawala) - Wizara ya Fedha na Mipango.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimkabidhi nyenzo baada ya kumuapisha  Bi. Susana Mkap a kuwa  Naibu Katibu Mkuu (Utawala) - Wizara ya Fedha na Mipango.
Waapishwa wakila kiapo cha miiko ya maadili ya vingozi wa umma
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai akiongea machache
Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Juma akiongea
Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan akitoa nasaha zake
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiongea 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli 
Sehemu ya viongozi waandamizi wa nyanja mbalimbali wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan, Spika wa Bunge la jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai, Jaji Mkuu Profesa Ibrahim Juma na Katibu Mkuu kiongozi wakiwa katika picha ya kumbukumbu na viongozi wa mbalimbali pamoja na wale aliowaapisha Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 28, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan, Spika wa Bunge la jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai, Jaji Mkuu Profesa Ibrahim Juma na Katibu Mkuu kiongozi wakiwa katika picha ya kumbukumbu na viongozi wa mbalimbali pamoja na wale aliowaapisha Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 28, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan, Spika wa Bunge la jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai, Jaji Mkuu Profesa Ibrahim Juma na Katibu Mkuu kiongozi wakiwa katika picha ya kumbukumbu na viongozi wa mbalimbali pamoja na wale aliowaapisha Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 28, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan, Spika wa Bunge la jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai, Jaji Mkuu Profesa Ibrahim Juma na Katibu Mkuu kiongozi wakiwa katika picha ya kumbukumbu na viongozi wa mbalimbali pamoja na wale aliowaapisha Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 28, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan wakiwapongeza viongozi aliowaapisha Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 28, 
201
j47 na j488: Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan wakiwapongeza viongozi aliowaapisha Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 28, 
2017. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli  akipeana mikoo na naibu waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu anayeshughulikia walemavu  Mhe Stella Alex Ikupa  akiwa na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe Juliana Shonza
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimpongeza Mhe Nicholaus B. William aliyemuapisha kuwa Naibu Katibu Mkuu   Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 28, 2017. Kulia ni mke wa Mhe. William Bi. Foster Mbuna.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiagana na  Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan baada  ya kuwaapisha viongozi mbalimbali  Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 28, 
201
Wazira wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Augustine Mahiga akiteta jambo na Katibu Mkuu  mpya wa wizara hiyo  Prof. Adolf F. Mkenda (kati) na aliyekuwa Katibu Mkuu wizarani humo Dkt. Aziz Mlima.  PICHA ZOTE NA IKULU