Friday, July 21

Mamba atishia amani Tanga



Tanga. Wakazi wa Mitaa ya Kange na Mkurumuzi jijini Tanga wamesema maisha yao yapo hatarini kutokana na bwawa lilioibuka baada ya kubomoka bwawa la samaki la kiwanda cha Rhino kuwa na mamba wakubwa.
Wakazi hao wamedai kuwa mwanamke mmoja alinusurika kuliwa na mamba mkubwa ambaye alikuwa amejificha katika kichaka.
Licha ya kufikisha malalamiko yao katika mamlaka husika na
kamati ya maafa ya Wilaya ya Tanga kutembelea, lakini ni miezi mitatu sasa hakuna hatua za kwuadhibiti wanyama hao zilizofanyika.
Mjumbe wa Halmashauri kuu ya Chama cha Maopinduzi (CCM) Kata ya Maweni, Said Bindo (72) amesema hali ilivyo inavyohatarisha usalama wa wakazi wa mtaa huo na kuitaka Serikali kutosubiri maafa yatokee.
“Tatizo hapa ni kwamba ni sababu huku wanaishi watu wa hali ya chini… kama wangekuwa wanaishi vigogo, hili bwawa lisingekuwepo. Kinachohitajika ni kutengeneza daraja litakalokuwa na uwezo wa kupitisha maji kwa wingi ili bwawa likauke,” amesema Kada huyo wa CCM.
Bindo, ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya siasa ya CCM tawi la Kange, amesema ameishi hapo  kwa kipindi cha zaidi ya miaka 50 na haijawahi kutokea hali kama hiyo.
“Sababu zinazotolewa tunaona kama ni visingizio… wanasema eti mara Halmsahuri itakapopata fungu, lakini kwa umri wangu na uzoefu nilionao, tatizo kama hili ni janga ambalo linahitaji kutatuliwa kwa fungu la dharura au kukiamuru kiwanda cha Rhino kujenga daraja kwa sababu ndiyo chanzo,” amesema Bindo.
Issa Shaaban, ambaye nyumba anayoishi inapakana na mto huo alilalamika kuwa jana jioni mke wa kaka yake alikurupshwa na mamba mkubwa lakini alifanikiwa kukimbia na kujiokoa.
Diwani wa kata ya Kange, Joseph Colyvirs, amesema tayari Baraza la Madiwani la Halmashauri ya jiji la Tanga limeshapitisha katika mpango wake wa kujenga makaravati katika mto huo ulioibuka hivi karibuni ili kuruhusu maji yapite.
“Yupo mwekezaji alifanya kazi ya kuzibua pale lakini kutokana na maji kuwa mengi iimeshindikana,” amesema diwani huyo.
Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Thobias Mwilapwa, amesema taarifa za kuibuka kwa bwawa katika eneo hilo anazo lakini tukio la kuonekana mamba halijamfikia na akaahidi kufanyia kazi haraka iwezekanavyo ili kunusuru maisha wananchi.

JPM aagiza Sh200 milioni za mradi wa maji jeshini zitumike kwa wananchi




Rais John Magufuli
Rais John Magufuli 
Kagera.  Rais John Magufuli ameagiza Sh200 milioni zilizopangwa kutumika katika mradi wa maji katika kambi ya jeshi zianze kuimarisha miradi ya maji kwa  wananchi kwanza.
Akizungumza jana, Alhamisi Julai 20  katika ziara  yake akiwa ameambatana na Rais wa Burundi, Pierre Nkurunzinza, Magufuli aliema  amebaini kuwa pampu za maji wilayani Ngara zimeharibika kwa zaidi ya wiki tatu na kuwa wilaya hiyo ina uhaba mkubwa wa maji.
Alimuita, Mhandisi wa Maji ajieleze ni kwa nini pampu hizo hazifanyi kazi na baada ya kumsikiliza ndipo alipofanya uamuzi huo.
Akifafanua kuhusu hali ya maji, mhandisi huyo alisema awali visima vya maji wilayani hapo vilikuwa vikihudumia watu 400 lakini kwa sasa wilaya hiyo ina watu zaidi ya 240,000 na hivyo visima hivyo havitoshelezi.
“Tulikuwa tuna idadi ndogo ya watu sasa hivi imeongezeka, lakini tangu pampu iharibike, tumetengeneza mbili na kisima kimoja hakina pampu,” alisema.
 Baada ya mhandisi huyo kufafanua hayo ndipo Rais alimuita Mkurugenzi wa Halmashauri kueleza mipango yake, ndipo Mkurugenzi huyo aliposema mradi wa maji wa Sh200 milioni utaanza kwanza katika kambi ya jeshi.
Kauli hiyo ndiyo iliyomfanya Rais Magufuli kushauri fedha hizo zitumike katika miradi ya maji katika makazi ya wananchi kwanza.
“Wanajeshi wapo 200 na wananchi wapo zaidi ya 20,000 sasa si bora waanze wananchi kwanza,” alisema.

Ahadi za JPM zitatimizwa-Majaliwa




Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa 
Songwe. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amewahakikishia wananchi kwamba ahadi zote zilizotolewa na Rais Dk John Magufuli katika maeneo mbalimbali nchini zitatekelezwa hivyo amewaomba wananchi waendelee kuiamini na kushirikiana na Serikali yao.
Akiwa mkoani Songwe Waziri Mkuu amesema kwamba Serikali ya Awamu ya Tano ipo makini na imejipanga vizuri katika kutekeleza ahadi mbalimbali zilizotolewa na Rais Magufuli ikiwamo Ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015-2020 inavyoelekeza.
Waziri Mkuu amesema hayo baada ya mbunge wa jimbo la Songwe, Philipo Mulugo kumuomba awasaidie kumkumbusha Rais Magufuli kuhusu ahadi yake ya ujenzi wa barabara ya lami yenye urefu wa kilomita nne wilayani Songwe.
“Ahadi zote zilizotolewa na Rais Magufuli tutazitekeleza, ikiwemo na hii aliyoikumbusha Mulugo ya ujenzi wa kilomita nne za barabara ya lami. Tunawaomba wananchi muendelee kuwa na imani na Serikali yenu.” Amesema.
Waziri Mkuu pia amepiga marufuku wananchi kufanya shughuli za kibinadamu ndani ya mita 60 kutoka katika vyanzo vya maji na kuwataka washirikiane katika utunzaji wa mazingira ili kuliepusha Taifa kugeuka jangwa.
Amesema ni vema wananchi wakazingatia Sheria ya Mazingira inayozuia kufanya shughuli za kibinadamu zikiwemo za kilimo kwenye maeneo yote ya vyanzo vya maji ndani ya mita 60. Aliwaagiza wakuu wa idara kusimamia jambo hilo.
Waziri Mkuu amesema kwa sasa maeneo mengi yanakabiliwa na changamoto ya upatikanaji wa maji jambo ambalo linachangiwa na vitendo vya uharibifu wa mazingira vinavyofanywa na baadhi ya wananchi, hivyo aliwataka wabadilike.
Hata hivyo, amesema Serikali inaendelea na utekelezaji wa kampeni ya Rais Magufuli ya kumtua mama ndoo kichwani, ambapo itahakikisha wananchi wote wanapata huduma ya maji katika umbali usiozidi mita 400 kutoka kwenye makazi yao.
Pia Waziri Mkuu aliwaeleza wananchi hao kwamba, Serikali bado inaendelea kutafuta vyanzo mbalimbali vya maji na kuhakikisha vinabainishwa na kufanyiwa tathmini ili viweze kuendelezwa na kuongeza upatikanaji wa maji nchini.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Chiku Gallawa amesema watu wanaopata huduma za maji safi na salama katika maeneo ya mijini ni asilimia 42 na vijijini ni asilimia 41.6.
Amesema katika bajeti ya 2017/2018 halmashauri za mkoa huo zimetengewa jumla ya Sh 7.5 bilioni kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maji ikiwa ni pamoja na ujenzi wa matanki ya kuvunia maji ya mvua katika majengo ya Taasisi za Umma.
Pia mkoa huo unatekeleza mpango kazi wa usambazaji maji katika maeneo ya mijini na vijijini kwa kupanua mifumo ya usambazaji na kuzijengea uwezo mamlaka za maji na ifikapo Desemba mwaka huu wataongeza idadi ya wananchi wanaopata huduma hiyo kutoka asilimia 45.04 hadi asilimia 55.63.

KAULI YA WAKILI PETER KIBATALA KUHUSU KUKAMATWA KWA TUNDU LISSU


BALOZI KAIRUKI ATAKA WATANZANIA KUCHANGAMKIA SOKO LA MUHOGO CHINA


MITAA YA JIJI LA MBEYA YAPIGWA TOCHI



IGP SIRRO AANZA ZIARA YA KIKAZI MKOANI KAGERA


 Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro (kushoto) akizungumza na Kamanda wa Polisi mkoa wa Kagera Kamishna Msaidizi Muandamizi wa Polisi (SACP) Augusine Ollomi, muda mfupi alipowasili. IGP Sirro yupo mkoani humo kwa ziara ya kikazi yenye lengo la kujitambulisha na kuzungumza na askari pamoja na kujua chamgamoto wanazokutana nazo wakati wakitekeleza majukumu yao
 Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro, akizungumza na baadhi ya askari wa kikosi maalum kinachofanya doria za kupambana na wahalifu aliokutana nao katika eneo la Nyakanazi mkoani Kagera, IGP Sirro yupo mkoani humo kwa ziara ya kikazi yenye lengo la kujitambulisha na kuzungumza na askari pamoja na kujua chamgamoto wanazokutananazo wakitekeleza majukumu yao.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (Mb), akitafakari jambo na Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro walipokutana katika viwanja vya Lemela wilayani Ngara mkoa wa Kagera, wakisubiri kuwasili kwa Rais Dkt. John Magufuli na Rais Pierre Nkurunziza wa Jamhuri ya Burundi. Picha na Demetrius Njimbwi – Jeshi la Polisi.

NANO ENERGIZER NOW IN TANZANIA / KICHOCHEO CHA NANO SASA KINAPATIKANA TANZANIA





























Kwa ajili ya kuikarabati na kuipa ulinzi Injini na gearbox ya gari yako bila kuifungua. Huziba mikwaruzo yote ndani ya Injini na gearbox na kuirudisha nguvu ya Injini kama ilivyokuwa mpya. Hupunguza matumizi ya mafuta 5% hadi 21%. Huongeza nguvu ya Injini na hutoa ulinzi wa Injini hadi kufikia kilomita 40,000. Hupatikana kwa injini na geabox za aina zote.
Hupatikana kwa aina zote za magari, Compressor, Jenereta, Bajaji na Pikipiki
KIMETHIBITISHWA NA:
SHIRIKA LA UBORA LA KIMATAIFA – ISO
SHIRIKA LA VIWANGO TANZANIA – TBS
MKEMIA MKUU WA SERIKALI TANZANIA
KIMEPENDEKEZWA NA WATENGENEZAJI MAGARI:
TOYOTA
MERCEDES BENZ
GM DAEWOO
VOLVO
HONDA
HYUNDAI
AUDI
KIMEFANYIWA MAJARIO NA KUTHIBITISHWA NA TAASISI:
CHUO KIKUU CHA TAIFA KYUNGPOOK - KOREA
CHUO KIKUU CHA TAIFA CHA SEOUL - KOREA
TAASISI YA MASHINE NA VIFAA YA KOREA
CHUO KIKUU CHA YEUNGNAM - KOREA
TAASISI YA KOREA YA TEKNOLOJIA YA MAGARI
JESHI LA ULINZI LA TAIFA LA KOREA
KITUO CHA JESHI LA ANGA LA INDIA
KIMETENGENEZWA NA NANO TECH INTERNATIONAL KOREA KINASAMBAZWA NA POWER ENERGY ENGINEERING LTD:
KWA MAWAKALA WASILIANA NASI KWA NAMBA ZIFUATAZO
                               0715 480174 / 0719346060
INAPATIKANA:
UBUNGO MATAA JENGO LA OILCOM - O715 480174
MWENGE JAPAN AUTO SPARE (MARRYLAND BAR) -  0714 363637
BK JAPAN AUTO SPARE PARTS SEGEREA STAND - 0653 519653
KARIAKOO - DUBAI TRADERS, LUESHA GENERAL (KISANGANI), ZANLUB

MWANZA - LIBERTY (MKABALA NA COCONUT HOTEL) - 0626 450450

UONGOZI MPYA WA CHAMA CHA MAAFISA MAWASILIANO WA SERIKALI, (TAGCO) WAKABIDHIWA MIKOBA


NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM
UONGOZI mpya wa Chama cha Maafisa Mawasiliano wa Serikali, (TAGCO), umekabidhiwa rasmi usukani wa kuongoza taasisi hiyo muhimu katika mawasiloiano ya serikali nchini.
Hafla ya makabidhiano hayo ilifanyika jijini Dar es Salaam, Julai 20, 2017 ambapo Mwenyekiti wa TAGCO aliyemaliza muda wake, Bw. Innocent Mungy, alimkabidhi “nyenzo” za kufanyia kazi Katibu Mkuu mpya wa TAGCO, Bw. Abdul Njaidi, ambapo shughuli hiyo ilishuhudiwa na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari MAELEZO anayeshuhulikia Huduma za Habari na Picha, Bw. Rodney Thadeus, Mweka Hazina wa chama  hicho aliyemaliza muda wake, Bw. Peter Malinzi, Mweka Hazina Msaidizi Mteule, Bw.Gerald Chami.
Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Mwenyekliti aliyemaliza muda wake, Bw. Innocent Mungy alisema, “tunawakabidhi TAGCO, hiki ni chombo muhimu sana kwa mawasiliano ya serikali, hivyo hakikisheni mnakiongoza vyema ili maelengo kusudiwa yafikiwe,”.alisema Bw. Mungy.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa TAGCO, Bw. Abdul Njaidi alisema, “Tunashukuru kwa kukabidhiwa usukani wa TAGCO, tunajua hiki chombo ni muhimu sana katika kuhakikisha wananchi wanapatiwa taarifa sahihi za shughuli za Serikali yao inazofanya, tutatekeleza majukumu yetu kwa umakini na uaminifu mkubwa, tunaomba ushirikiano kutoka kwa uongozi uliopita na wanachama wote wa TAGCO na watendaji wote serikalini,”. Alisema Bw. Njaidi wakati akitoa neon la shukrani.
Viongozi wengine wapya wa TAGCO ni Bw. Pascal Shelutete (Mwenyekiti), Bi. Sarah Kibonde Msika (Makamu Mwenyekiti), Bi. Tabu Shaibu (Mweka Hazina), Bi. Gaudensia Simwanza (Katibu Msaidizi), Bw. Owen Mwandubya (Katibu Mwenezi) na Bw. Mpokigwa Mwakasipo (Katibu Mwenezi Msaidizi).
TAGCO nichama kinachowa kutanisha pamoja Maafisa Mawasiliano wa Taasisi mbambali za umma, serikali na Halmashauri zote hapa nchini, lengo likiwa ni kupena ujuzi na uwezo wa kuhakikisha taarifa za serikali zinawafikia wananchi kwa usahihi na kwa wakati.
 
Mwenyekiti wa Chama cha Maafisa Mawasiliano wa Serikali, (TAGCO), ambaye amemaliza muda wake, Bw. Innocent Mungy, (wapili kulia), akimkabidhi nyaraka za chama, Katibu Mkuu mpya wa chama hicho, Bw. Abdul Njaidi. (wapili kushoto), ikiwa ni ishara ya kukabidhi rasmi majukumu ya kiuongozi jijini Dar es Salaam Julai 20, 2017. Wengine pichani walioshuhudia hafla hiyo ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari MAELEZO anayeshughulikia Huduma za Habari na Picha, Bw. Rodney Thadeus, (watatu kushoto), Bw. Gerald Chami, (wakwanza kushoto), ambaye ni Mweka Hazina Msaidizi na Bw.Peter Malinzi, (kulia), Mweka Hazina aliyemaliza muda wake.

Mwenyekiti wa Chama cha Maafisa Mawasiliano wa Serikali, (TAGCO), ambaye amemaliza muda wake Bw. Innocent Mungy, (wapili kulia), akishuhudia wakati  Katibu Mkuu mpya wa chama hicho Bw. Abdul Njaidi. akisaini  nyaraka za makabidhiano.

Rais Nkurunziza afanya ziara rasmi ya kiserikali nchini Tanzania.


Rais wa Burundi Mhe. Pierre Nkurunziza akiwasalimia wananchi wa Mji wa Ngara kwenye Mkutano wa Hadhara uliofanyika katika Uwanja wa Posta Mjini Ngara 20 Julai 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Rais wa Burundi Mhe. Pierre Nkurunziza mara baada ya Rais wa Burundi kuwahutubia wananchi wa Mji wa Ngara kwenye Mkutano wa hadhara uliofanyika katika Uwanja wa Posta Mjini Ngara 20 Julai 2017.
Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia mamia ya wananchi wa Mji wa Ngara kwenye Mkutano wa Hadhara uliofanyika katika Uwanja wa Posta Mjini Ngara Mkoani Kagera 20 Julai 2017.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpokea Rais wa Burundi Mhe. Pierre Nkurunziza mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Lemela mjini Ngara Mkoani Kagera Julai 2017
Rais wa Jamuhuri ya Burundi Mhe. Pierre Nkurunziza akiwapungia wananchi alipowasili katika viwanja vya Lemela mjini Ngara Mkoani Kagera Julai 20,2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Rais wa Burundi Mhe. Pierre Nkurunziza wakiwa wamesimama wakipokea salamu za heshima kutoka kwa majeshi ya ulinzi na usalama.
Rais wa Burundi Mhe. Pierre Nkurunziza akikagua graride la lililoandaliwa na jeshi la ulinzi la Tanzania JWTZ katika viwanja vya Lemela mjini Ngara Mkoani Kagera Julai 20,2017
Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mgeni wake Rais wa Burundi Mhe. Pierre Nkurunziza mara baada ya Kumpokea katika Uwanja vya Lemela mjini Ngara Mkoani Kagera 20 Julai 2017.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Rais wa Burundi Mhe. Pierre Nkurunziza akiwasalimia wananchi wa Mji wa Ngara kwenye uwanja wa Lemela mjini Ngara Mkoani Kagera 20 Julai 2017.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiteta Jambo na Rais wa Burundi Mhe. Pierre Nkurunziza Mara baada ya kumpokea katika Mji wa Ngara kwenye uwanja vya Lemela mjini Ngara Mkoani Kagera 20 Julai 2017.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkaribisha Rais wa Jamuhuri ya Burundi Mhe. Pierre Nkurunziza kwa maongezi mjini Ngara Mkoani Kagera 20 Julai 2017.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na ujumbe wake katika mazungumzo maalum ya kiserikali na Rais wa Burundi Mhe. Pierre Nkurunziza na ujumbe wake Mjini Ngara Mkoani Kagera 20 Julai 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, Rais wa Burundi Mhe. Pierre Nkurunziza pamoja na mama Janeth Magufuli katika Maongezi.
Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na mgeni wake Rais wa Burundi Mhe. Pierre Nkurunziza wakiwapungia mikono wananchimwa mji wa ngara wakati wakiwasili katika uwanja wa posta mjini Ngara kwa ajili ya mkutano wa hadhara.
Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na mgeni wake Rais wa Burundi Mhe. Pierre Nkurunziza wakiwapungia mikono wananchi wa mji wa Ngara waliohudhulia katika uwanja wa posta mjini Ngara kwa ajili ya Mkutano wa hadhara.
Umati wa ananchi wa mji wa Ngara waliohudhulia katika uwanja wa posta mjini Ngara kusikiliza Hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika uwanja wa posta mjini Ngara 20 Julai 2017.
Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na mgeni wake Rais wa Burundi Mhe. Pierre Nkurunziza katika uwanja wa Lemela Mjini Ngara Mkoani Kagera 20 Julai 2017 baada ya kumaliza ziara yake Rasmi ya kiserikali Nchini. PICHA NA IKULU.

taarifa kwa vyombo vya habari


JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU

Simu : +255-22-2114512, 2116898
Tovuti : www.ikulu.go.tz
Faksi : 255-22-2113425
OFISI YA RAIS,
IKULU,
1 BARABARA YA BARACK OBAMA,
11400 DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Rais wa Jamhuri ya Burundi Mhe. Pierre Nkurunziza leo tarehe 20 Julai, 2017 amefanya ziara ya Rasmi ya Kiserikali ya siku moja hapa nchini kwa mwaliko wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.
Ziara hiyo imefanyika katika Wilaya ya Ngara Mkoani Kagera ambapo Mhe. Rais Nkurunziza amepokelewa rasmi kwa kupigiwa mizinga 21 na kukagua gwaride rasmi lililoandaliwa na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwa heshima yake katika eneo la Lemela na baadaye mazungumzo rasmi na dhifa ya kitaifa iliyofanyika Mjini Ngara.
Baadaye viongozi hao wamezungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa Posta ya zamani Mjini Ngara.
Akizungumza katika mkutano huo, Mhe. Rais Magufuli aliyeongozana na Mkewe Mama Janeth Magufuli amemshukuru Mhe. Rais Nkurunziza kwa kukubali mwaliko wake na amemhakikishia kuwa Serikali yake ya Awamu ya Tano itaendeleza na kuimarisha zaidi uhusiano na ushirikiano wa kihistoria na kidugu na nchi ya Burundi hususani katika kukuza biashara na uwekezaji.
“Tanzania ni ndugu zako na Watanzania ni ndugu wa watu wa Burundi, umekuja kwa mazungumzo ya kiuchumi, tumezungumza mambo mengi ya kuimarisha biashara kati Tanzania na Burundi, katika takwimu za mwaka 2016 biashara kati ya Tanzania na Burundi ilikuwa na thamani ya Shilingi Bilioni 116.5, kiwango hiki ni kidogo kwa nchi ya Burudni ambayo ina watu zaidi ya Milioni 10 na Tanzania ambayo ina watu zaidi ya Milioni 52” amesema Mhe. Rais Magufuli.
Halikadhalika Mhe. Rais Magufuli amesema Serikali ya Tanzania inaendelea na juhudi zake za kujenga reli ya kati kwa kiwango cha kisasa (Standard Gauge) ambayo itaunganisha bandari ya Dar es Salaam na nchi za Burundi na Rwanda na hivyo amemhakikishia Mhe. Rais Nkurunziza kuwa reli hiyo itakuwa kichocheo kikubwa cha uchumi wa Tanzania na nchi hizo.  
Aidha, Mhe. Rais Magufuli amempongeza Mhe. Rais Nkurunziza kwa juhudi zake za kusimamia amani nchini mwake na ametoa wito kwa wakimbizi wa Burundi ambao bado wapo nchini Tanzania kuitikia wito wa Rais wao aliyewataka warudi nchini Burundi ili wakaendelea kujenga Taifa lao kwa kuwa hali ni shwari.
Pia Mhe. Rais Magufuli amemuagiza Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba kusitisha utoaji wa uraia kwa wakimbizi hao ili utaratibu huo usitimiwe kama kigezo cha watu kuzikimbia nchi zao.
Kwa upande wake Mhe. Rais Nkurunziza amemshukuru Mhe. Rais Magufuli kwa mwaliko wake na amesema Tanzania na Burundi ni ndugu na majirani ambao uhusiano na ushirikiano wake ulianza hata kabla ya uhuru.
Mhe. Rais Nkurunziza ametoa wito kwa wafanyabiashara wa Tanzania kwenda kufanya biashara Burundi na wafanyabisahara wa Burundi kuja Tanzania bila wasiwasi na amebainisha kuwa hali ya Burundi ni shwari kwani hata wakimbizi waliokimbilia Tanzania miaka miwili iliyopita wameanza kurejea nchi Burundi kwa hiari yao na wanaendelea na shughuli zao kama kawaida.
“Tunataka kuwajulisha wenzetu Watanzania na Warundi wenzetu ambao walikimbilia Tanzania, Burundi ya leo ni nchi yenye amani, tunawaalika Warundi wenzetu, kaka zetu na dada zetu ambao walikimbilia hapa Tanzania, warudi nchi kwao tujenge nchi yetu iwe na amani ya kudumu.
Tunapata faraja kwamba Warundi wenzetu ambao walikimbilia Tanzania miaka miwili iliyopita ambao wanafikia idadi ya 150,000 wameanza kurudi Burundi bila ya kupitia Shirika la Wakimbizi Duniani (UNHCR), kwa hiyo tunasema wote rudini nyumbani” amesema Mhe. Rais Nkurunziza.
Katika ziara hii Mhe. Rais Magufuli ameongozana na Mawaziri watano na Mhe. Rais Nkurunziza ameongozana na Mawaziri watano ambao pamoja na viongozi wengine wa taasisi na vyombo vya ulinzi na usalama wameshiriki mazungumzo rasmi.
Mhe. Rais Nkurunziza amemaliza ziara yake rasmi ya kiserikali ya siku moja hapa nchini na amerejea nchini Burundi.
Kesho tarehe 21 Julai, 2017 Mhe. Rais Magufuli ataendelea na ziara yake Mkoani Kigoma ambapo ataweka jiwa la msingi la ujenzi wa barabara ya Nyakanazi – Kibondo na barabara ya Kidahwe – Kasulu pamoja na kuzungumza na wananchi.


Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Ngara, Kagera
20 Julai, 2017