LIKIZO isiyo ya lazima kwa wanafunzi wa shule za msingi kwenye Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, kwa sababu ya ugonjwa COVID 19 ilisababisha wasichana 50 wasiendelee na masomo yao kutokana na kufungwa shule kwa takribani miezi mitatu mwaka jana.
Thursday, September 9
COVID 19 ILIVYOSABABISHA MAJANGA KWA WANAFUNZI SIMANJIRO
SERIKALI YATENGA TRILIONI 2.03 KUZIKWAMUA KAYA ZOTE MASKINI NCHINI
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa akitoa neno la utangulizi wakati wa Semina ya kuwajengea uelewa Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Utawala na Serikali za Mitaa kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) iliyofanyika leo kwenye Ukumbi wa LAPF jijini Dodoma.
Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Utawala na Serikali za Mitaa wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa alipokuwa akitoa neno la utangulizi wakati wa Semina ya kuwajengea uelewa Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Utawala na Serikali za Mitaa kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) iliyofanyika leo kwenye Ukumbi wa LAPF jijini Dodoma.Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Utawala na Serikali za Mitaa, Mhe. Humphrey Polepole (Mb) akizungumza wakati wa Semina ya kuwajengea uelewa Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) iliyofanyika kwenye Ukumbi wa LAPF jijini Dodoma. Kushoto kwake ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa.
Baadhi ya Watendaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) wakimsilikiza Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Utawala na Serikali za Mitaa, Mhe. Humphrey Polepole (Mb) (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza wakati wa Semina ya kuwajengea uelewa Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa kuhusu utekelezaji wa majukumu ya TASAF iliyofanyika kwenye Ukumbi wa LAPF jijini Dodoma.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF), Bw. Ladislaus Mwamanga akiwasilisha mada kuhusu utekelezaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) kwa Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa iliyofanyika kwenye Ukumbi wa LAPF jijini Dodoma.
Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Utawala na Serikali za Mitaa wakisikiliza mada kuhusiana na utekelezaji wa majukumu ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) iliyowasilishwa kwao na Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF, Bw. Ladislaus Mwamanga (hayupo pichani).
SERIKALI imetenga kiasi cha shilingi trilioni 2.03 kwa ajili ya kuzikwamua kaya zote maskini nchini kutoka katika lindi la umaskini ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini katika Kipindi cha Pili cha Awamu ya Tatu ya TASAF kilichoanza 2020 mpaka 2023.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa wakati wa semina ya kuwajengea uwezo Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Utawala na Serikali za Mitaa kuhusu utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini nchini iliyofanyika leo katika ukumbi wa LAPF jijini Dodoma.
Mhe. Mchengerwa amesema, kwa kuwa Serikali imetenga fedha za kutosha kuzifikia kaya zote maskini, amewaomba wajumbe wa kamati hiyo kufanya ufuatiliaji ili kaya zote maskini zinazostahili kupata ruzuku zinanufaika.
“Kama kuna kaya yoyote maskini imesahaulika, nawaomba mtupatie taarifa ili watendaji wetu wazifikie na kukamilisha taratibu za kuwawezesha kupata ruzuku na kuongeza kuwa, katika utekelezaji wa awamu hii, Serikali itahakikisha kila Mtanzania anayestahili kunufaika na mpango huu, anapata ruzuku,” Mhe. Mchengerwa amesisitiza.
Aidha, Mhe. Mchengerwa amesema licha ya TASAF kuziwezesha kaya maskini kiuchumi, pia imewawezesha watoto wa kike wanaotoka kwenye kaya hizo maskini kupata elimu kwa manufaa yao na taifa kwa ujumla.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Utawala na Serikali za Mitaa, Mhe. Humphrey Polepole (Mb) ameipongeza Serikali inayoongozwa na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa azma yake ya kutenga fedha za kutosha kuziwezesha kaya zote maskini nchini. Mhe. Polepole amesema, azma ya Mhe. Samia ya kutenga fedha hizo inaonesha nia ya dhati ya Serikali yake na Watendaji wake ya kuzikwamua kaya zote maskini.
Akiwasilisha mada kwa kamati hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF, Bw. Ladislaus Mwamanga amesema, idadi ya kaya za walengwa katika utekelezaji wa Mpango wa TASAF, Kipindi cha Pili cha Awamu ya Tatu inatarajiwa kufikia milioni moja laki nne na nusu, hivyo wanufaika kwenye kaya hizo watakuwa zaidi ya watu milioni 10.
Bw. Mwamanga amesema, ofisi yake imetekeleza zoezi la utambuzi wa kaya maskini kwa kushirikisha jamii na viongozi katika maeneo husika ili kutatua changamoto zilizojitokeza katika utekelezaji wa awamu iliyopita. Katika kuhakikisha hakuna udanganyifu wakati wa zoezi la uandikishaji wa kaya maskini, Watendaji wanaohusika na zoezi hilo wamesainishwa kiapo cha kutekeleza jukumu hilo kwa uadilifu.
KESI YA MBOWE KUENDELEA KUUNGURUMA KESHO
KESI ya ugaidi inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu itaendelea kusilizwa kesho Septemba 10, 2021 mbele ya Jaji Mustapha Siyani baada ya kupangiwa Jaji huyo mpya kufuatia kujitoa kwa Jaji Elinazer Luvanda aliyekuwa akiisikiliza mwanzo.
Leo Septemba 9,2021 Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, Magdalena Ntanda kesi amesema, kesi itaanza kuanzia saa 3 asubuhi na kwamba muda kamili utategemea magereza watawapeleka washitakiwa hao saa ngapi.
Awali, kesi hiyo ilipaswa kuanza kwa kuwasomea washitakiwa maelezo ya awali baada ya kusomewa maelezo ya mashahidi lakini upande wa utetezi ukiongozwa na wakili Peter Kibatala ulipinga hatua hiyo kwa kuwasilisha mapingamizi yenye hoja nne kwamba mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo na kwamba hati ya mashitaka ni batili na kuomba mahakama iwaondolee washitakiwa mashtaka hayo.
Hata hivyo, upande wa mashtaka ulipinga hoja hizo ukidai mahakama hiyo inayo mamlaka na hati ya mashtaka iko sahihi.
Kutokana na hali hiyo Jaji Elinazer Luvanda alitupilia mbali mapingamizi yote lakini kesi hiyo haikuweza kuendelea baada ya Mbowe kudai hana imani na jaji huyo katika kutenda haki na kumuomba ajitoe.
Katika Maelezo ya Mbowe ya kwa niniJaji ajitoe Katika shauri Hilo ametoa madai Mbalimbali ikiwa Ni Pamoja na kutupilia Mbali kila Mapingamizi yanayowasilishwa na Upande wa Utetezi.
Pia amedai Kuwa Mapingamizi yanayowasilishwa na upande wa Utetezi hayazingatiwi na kwamba hata vifungu vya sheria wanavyotumia kama mfano kwenye kutetea mapingamizi yao havizingatiwi wakati wa kutoa uamuzi wake jambo ambalo anadaia ni ukiukwaji wa haki za Msingi.
Mbowe alidai "Mheshimiwa Jaji naomba kunukuu taarifa....Jaji Elinaza Luvanda ni Mserikali na Tiss, yupo Mahakama ya Mafisadi kimkakati, anaelekezwa kumfunga Mbowe huku msajili akishughulika na Chadema, Rais atamuachia baada ya muda kila pingamizi atalitupilia mbali, haijalishi uhalali wake.'' mwisho wa kunukuu..."
Mbali na Mbowe washitakiwa wengine katika kesi hiyo ni Halfan Hassan, Adamu Kasekwa, Mohamed Abdillahi Ling'wenya ambao wanakabiliwa na mashitaka sita katika kesi ya Uhujumu Uchumi namba 63/2020.
Mbowe anakabiliwa na mashitaka mawili ambayo ni kula njama na kufadhili fedha kwa ajili vitendo vya kigaidi.
Inadaiwa washitakiwa kwa pamoja walikula njama za kutenda kosa, tukio wanalodaiwa kulitenda kati ya Mei Mosi, 2020 na Agosti Mosi 2020 katika hoteli ya Aishi iliyopo Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro na maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam, Morogoro na Arusha, walitenda kosa hilo.
Washitakiwa kwa pamoja wanadaiwa walikula njama za kulipua vituo mbalimbali vya mafuta na katika mikutano isiyokuwa ya kisiasa na kusababisha hofu kwa wananchi kwa lengo la kuutishia umma wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Katika mashitaka ya pili yanayomkabili Mbowe inadaiwa katika tarehe hizo, katika hoteli ya Aishi iliyopo Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro na maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam, Morogoro na Arusha, Mbowe aliwafadhili Halfan Hassan, Adam Kasekwa na Mohamed Lingwenya, huku akiwa na lengo la kutekeleza vitendo vya kigaidi ambavyo ni kulipua vituo ya mafuta na mikusanyiko ya wananchi.
Wahamiaji Haramu 12 Waishiwa Nguvu,Njaa Yawakomoa,Wakamatwa Baada Ya Mtafutano Na Polisi
Na Amiri Kilagalila,Njombe
Wahamiaji haramu 12 kutoka Ethiopia waliovikimbia vikosi vya Ulinzi na usalama vya jeshi la polisi na uhamiaji August 8 katika msako uliofanyika katika eneo la machungio la kijiji cha Uhambule wamekamatwa baada ya kushinda muda mrefu na njaa na kisha kuishiwa nguvu za kuendelea kukimbia katika mapori ya wilaya ya Wanging'ombe
Hapo jana vikosi vya Ulinzi na usalama kutoka jeshi la polisi na uhamiaji baada ya kuskia Kuna hali isiyo ya kawaida katika eneo hilo vilifanya msako mkali katika Kijiji kinatajwa kutumika Sana Kama kituo Cha wahamiaji haramu Cha Uhambule kilichopo wilayani Wanging'ombe mkoani Njombe na Kisha kufanikiwa kuwashika wahamiaji 26 huku wengine wakifanikiwa kumbilia porini ambapo Leo wamekamatwa Tena.
Kamanda kikosi cha uhamiaji kamishna msaidizi mwandamizi John Yindi baada ya kuwakamata watu hao amewapongeza wananchi wa eneo Hilo ambao wamekubali kutoa taarifa ya uwepo wa watu hao aambao walikuwa wakituma watu kuwasaidia kupata chakula mafichoni waliko.
“Swala la ulinzi na usalama ni la kila mtanzania kwa hiyo tunaomba muendelee kutoa taarifa kwa viongozi weny wa vijiji mnavyoona watu kama hawa”alisema kamanda Yindi
Nae Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Njombe Hamisi Issa ambaye alilazimika kuingia porini kuwasaka watu hao amesema Jana wamekamata 26 huku 15 wakifanikiwa kuwakimbia ambao Leo 12 wameshikwa ,hivyo wananchi waendelee kupinga uwepo wa watu hao Kijijini kwao kwakuwa hawajui na magaidi au vipi.
“Hili eneo watu wameona ni sehemu ya kujificha sasa hivi watu wanaogopa hata kuingia kwenye majani kule,jana wamekamatwa 26 na wengine watano jumla wamekuwa 31 kwa hiyo wako wengi hawa hata ukiwapa basi hawatoshi bado watatu kwa kuwa tumewapata 12,kuna watu wameleta huku na kwa hali kama hii hatuwezi kujua kama ni wema”alisema Kamanda Issa
Awali afisa Mtendaji wa Kijiji Cha Uhambule Yasinta Lupumbwe amesema wamewatia nguvuni watu hao na Kisha kuwaweka katika ofisi ya kata kwakuwa walianza kusimamishwa watu njiani na kuomba wanunuliwe chakula.
“Saa nne asubuhi alinipa taarifa katibu wa uhambule kwamba porini kule kuna wahamiaji amekutana nao wakawa wanamuomba awanunulie chakula,tukaongea nao tukajua ni wale wale miongoni ambao walichukuliwa tarehe nane.Wananchi hawa wa kijiji cha uhambule wakaandaa uji na chakula wamekula”alisema Yasinta Lupumbwe
MARUFUKU MACHINGA KUFANYA BIASHARA KWENYE NJIA ZA WATEMBEA KWA MIGUU - RC MAKALLA
- Asema agizo hilo ni kwa Wafanyabiashara Mkoa mzima.
- Amtaka DC Ilala na Uongozi wa Machinga kuweka utaratibu mzuri kuwapanga Machinga Kariakoo.
- Awapo mbinu ya kufunga baadhi ya Mitaa Kariakoo kwaajili ya kufanya Biashara.
- Aeleza dhamira yake ya kuboresha mandhari ya Dar es salaam
MKUU wa Mkoa wa Dar es salaam Amos Makalla amepiga marufuku ufanyaji wa biashara kwenye maeneo hifadhi ya barabara zote za Mkoa huo baada ya utaratibu huo kuwa chanzo cha uvunjifu wa amani na ongezeko la ajali.
RC Makalla ametoa maelekezo hayo alipotembelea Soko la Kariakoo na kujionea kero ya ufanyaji biashara holela kwenye maeneo ya watembea kwa miguu.
Kutokana na hilo RC Makalla amewaelekeza Mkuu wa Wilaya ya Ilala kufanya kikao na Wafanyabiashara hao Jumatatu ya Septemba 13 na kuainisha maeneo ya kuwapeleka wote waliovamia hifadhi ya barabara.
Aidha RC Makalla amewaelekeza kuangalia utaratibu mzuri wa kufunga na kufungua baadhi ya mitaa Kariakoo kwaajili ya kufanya biashara Kutokana na ufinyu wa maeneo ili Waweze kupata riziki.
Hata hivyo RC Makalla amesema kwa tathimini aliyofanya amebaini hali ya ufanyaji biashara holela Dar es salaam ipo kwa kiwango kikubwa na kuwanyima watembea miguu haki zao za msingi.
Pamoja na hayo RC Makalla ameelekeza Manispaa zote za Mkoa huo kuweka vibao vya kuzuia biashara kwenye maeneo ya watembea kwa miguu.
TANZANIA MWENYEJI WA ONESHO LA UTALII LA NCHI WANACHAMA WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI
KATIKA jitihada za kuvutia na kukuza uwekezaji katika sekta ya Utalii Mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wanaoshughulikia Masuala ya wanyamapori na utalii wamepitisha mkakati wa kutangaza utalii wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Akiongea leo na wandishi wa habari Jijini Dodoma Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mary Masanja amesema onyesho hilo litakuwa linafanyika kwa mzunguko katika nchi wanachama kila mwaka.
Amesema kwa kutambua utalii ni sekta mtambuka onesha hilo ni fursa muhimu ya kuhamasisha uhifadhi wa maliasili na malikale pamoja na kuchochea ukuaji wa utalii hususani utalii wa mikutano na matukio (MICE TOURISM) ambao ni zao jipya la utalii la kimkakati la kufanikisha kuongeza idadi ya watalii katika ukanda wa Afrika Mashariki.
"Napenda kuwajulisha kuwa Tanzania ndio itakuwa mwenyeji wa kwanza wa onesho hili la utalii wa jumuiya ya Afrika Mashariki ambapo kauli mbiu ya onesha hilo inasema " Utangazaji utalii stahimilivu kwa maendeleo jumuishi ya kijamii na uchumi, ".
Onesho la EARTE litafanyika jijini Arusha Oktoba 2021 ambapo litajumuisha siku tatu za maonesho na siku tano za ziara maalum ya kutembelea vivutio vya utalii pamoja na fursa za utalii wa ndani kwa Tanzania bara na Zanzibar," Amesema Naibu Waziri Masanja.
Akizungumzia jinsi ugonjwa wa Corona ulivyoathiri sekta ya utalii ambapo kabla ya ugonjwa idadi ya watalii walifika Milioni 1.5 lakini baada ya kuzuka kwa ugonjwa huo idadi ya watalii ilipungua na kufikia 620,000 huku makusanyo na mapato yakishuka.
" Kwa sasa hali inaenda vizuri baada Rais wa awamu ya sita Samia Suluhu Hassan kuleta chanjo ya ugonjwa wa Corona ambapo namba ya watalii kuingia nchini inapanda," amesema Naibu Waziri Masanja.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mary Masanja akizungumza na wandishi wa habari ofisini kwake jijini Dodoma.Naibu Waziri Wizara ya Maliasili na Utalii, Mary Masanja akizungumza na wandishi wa habari ofisini kwake jijini Dodoma leo alipokua akitangaza juu ya kuanza kwa onesho la utalii kwa Nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.