Monday, September 11

Kikosi maalum chatua Mwadui kuchunguza almasi


Kikosi Maalumu cha upelelezi kinachoundwa na maofisa wa vyombo vya ulinzi na usalama kutoka makao makuu jijini Dar es Salaam tayari kimeanza kazi ya kuchunguza shughuli za uzalishaji na biashara ya madini ya almasi katika mgodi wa Mwadui unaomilikiwa na kampuni ya Williamson Diamonds Limited.
Kutokana na mahojiano yanayoendelea, shughuli za mgodi huo ulioko Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga zimesimama kuanzia juzi kutoa fursa kwa viongozi na watumishi wa vitengo nyeti vinavyosimamia uchimbaji, uthamini na usafirishaji kuhojiwa.
Akizungumza kwa njia ya simu leo Jumatatu asubuhi Agosti 11, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainabu Tellack amethibitisha uwepo wa kikosi kazi hicho mkoani humo na kufafanua kuwa shughuli za mgodi huo zitarejea kama kawaida baada ya mahojiano kukamilika.
“Hawajafunga mgodi; kinachofanyika ni mahojiano na uchunguzi unaofanywa na maofisa wa ngazi za juu kutoka kwenye vyombo vya ulinzi na usalama. Yakikamilika shughuli zitarejea kama kawaida,” amesema Tellack
Licha ya kuthibitisha uwepo wa kikosi kazi hicho mkoani mwake, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Simon Haule amesema hawezi kuzungumzia utendaji wake kwa sababu linahusisha na kusimamiwa na maofisa kutoka makao makuu ya jeshi hilo jijini Dar es Salaam.
Bila kutaka kuingia kwa undani kuhusu suala hilo, ofisa uhusiano wa mgodi huo, Joseph Kaasa ameliambia Mwananchi kwa njia ya simu kuwa yuko kituo cha polisi na kuahidi kutoa taarifa atakapokamilisha kulichompeleka kituoni hapo.
Kampuni ya WDL juzi imesitisha kwa muda baadhi ya shughuli za uzalishaji mgodini.
Uongozi wa kampuni hiyo katika taarifa kwa wafanyakazi iliyotolewa juzi Jumamosi kwa tangazo namba 3311 imesema kwa mtazamo wa uchunguzi ulioanzishwa na Serikali na kwa sababu za kiusalama, umeamua kusitisha kwa muda baadhi ya shughuli za uzalishaji katika mgodi.
Taarifa hiyo imesema shughuli ambazo zitaendelea ni za huduma maalumu za ulinzi, tiba, umeme, maji, zimamoto na usafiri unaohitajika katika huduma hizo.
“Huduma za kiutawala zitaendelea kufanya kazi. Tutawajulisha wakati uzalishaji utakaporejea,” imesema .
WDL imesema inasubiri kuachiwa kifurushi namba WI-FY18 cha almasi iliyokuwa ikisafirishwa nje kutoka mgodini.
Hata hivyo, serikali imezuia kusafirishwa kifurushi hicho kwa misingi ambayo haijawasilishwa rasmi kwa uongozi wa kampuni ya WDL isipokuwa kwa taarifa zilizotangazwa na vyombo vya habari vya redio na runinga.
Hatuwezi kutoa maoni yoyote kutokana na matokeo ya uchunguzi huo. Vifurushi vyote vinavyosafirishwa kwa biashara nje hukadiriwa thamani yake hapa mgodini na watumishi wa Tansort (Hiki ni kitengo cha kukadiria thamani ya almasi na vito) ambao wanawakilisha Wizara ya Nishati na Madini. Kifurushi kinaposafirishwa kinapigwa mihuri miliwiili ya vyombo viwili vya serikali.
Sisi kama uongozi hatuna ujuzi wanaotumia tansort wa kukadiria na kuthamini au kukokotoa thamani ya alimasi. Huwa tunapokea hati ya ukadiriaji kutoka tansort ambayo hutumika kukadiria kwa muda malipo ya mrabaha wa serikali. Malipo ya mrabaha yanakamilishwa baada ya kupatiwa matokeo halisi ya zabuni ya wazi ya almasi za WDL (uaminifuunaothibitishwa na tansort) kutoka Wizara ya Nishati ana Madini.
kama mnavyotambua, serikali ni mbia asilimia 25 katika WDL. Tupo kwenye mazungumzo na serikali ili kuafikiana njia ya kufuata.
Tunawashukuru kwa kuendelea kutoa ushirikiano na kuelewa.

Wabunge wa CUF wavurugana bungeni


Wabunge wa CUF wameonekana kuvurugana bungeni kutokana na mgogoro unaoendelea katika chama hicho.
Mvurugano huo umeonekana leo Jumatatu mjini Dodoma baada ya wabunge wanaomuunga mkono Profesa Ibrahim Lipumba ambaye ni Mwenyekiti wa CUF anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kufanya uchaguzi na kumchagua Mbunge wa Mtwara Mjini, Maftaha Nachuma kuwa mwenyekiti wao bungeni.
Naibu Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson ametangaza kuwa Spika wa Bunge, Job Ndugai amepokea barua kutoka kwa Katibu wa CUF, Magdalena Sakaya kuhusu safu hiyo ya uongozi.
Baada ya tangazo hilo, Mbunge wa Malindi, Ally Salehe aliomba mwongozo wa Spika akitaka  kujua ni nani anaamua kuhusu uongozi wa wabunge bungeni kwa sababu wao wameshafanya uchaguzi na kumchagua Mbunge wa Temeke, Abdallah Mtolea kuwa mwenyekiti wao baada ya kufukuzwa kwa wabunge wanane.                       
Pia, amehoji inawezekanaje kuwa na viongozi wawili bila wa kwanza kufutwa.
Akijibu mwongozo huo, Dk Tulia amesema Spika amepokea taarifa ya viongozi hao lakini hajapokea taarifa ya uchaguzi wa upande wa akina Ally Salehe ambao unamuunga mkono Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad.
Amesema watakapopeleka taarifa yao ndipo Spika ataamua.

Waziri Kairuki aagiza watumishi 10 kusimamishwa kazi


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angellah Kairuki ameagiza kusimamishwa kazi watumishi zaidi ya kumi wa halmashauri za wilaya za Gairo na Kilosa.
Uamuzi huo unatokana na kulipwa mshahara hewa kwa aliyekuwa mwalimu wa Shule ya Sekondari Dumila ambaye hayupo kazini tangu mwaka 2009.
Kairuki ametoa agizo hilo alipozungumza na wakuu wa idara katika halmashauri hizo. Amesema ni kosa lisilovumilika mtumishi hayupo kazini tangu 2009 lakini ameendelea kulipwa hadi Agosti.
"Kuanzia leo naagiza waliokua maofisa utumishi, waweka hazina na maofisa elimu sekondari wa halmashauri hizi tangu 2009 watafutwe popote walipo na wasimamishwe kazi kupisha uchunguzi dhidi yao," amesema.
Waziri Kairuki ameagiza vyombo vya usalama kumtafuta mwalimu huyo popote alipo ili kurejesha fedha na afikishwe kwenye vyombo vya sheria.
Awali, ilidaiwa mwalimu huyo aliaga kwenda masomoni katika Chuo cha St. John lakini hakuripoti chuoni.

Mbunge ataka Spika ateue ujumbe kwenda kumjulia hali Lissu


Mbunge wa Baraza la Wawakilishi (CCM), Jaku Hashim Ayoub ameomba mwongozo wa Spika akitaka Bunge liteue wabunge wa kwenda kumuona mwenzao wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu anayepata matibabu mjini Nairobi, Kenya baada ya kujeruhiwa kwa risasi.
Lissu alijeruhiwa Septemba 7 akiwa ndani ya gari nyumbani kwake Area D mjini hapa na alisafirishwa siku hiyohiyo kwa matibabu katika Hospitali ya Aga Khan jijini Nairobi. Awali, alipatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma.
Akizungumza baada ya kipindi cha matangazo ya wageni bungeni leo Jumatatu, Jaku amesema Naibu Spika, Dk Tulia Ackson alifanya kitendo cha kibinadamu kuruhusu gari la ndugu zake limpeleke Lissu hospitali.
Amesema kwa ubinadamu, anaomba mwongozo wa Spika wateuliwe wabunge kwenda kumuona Lissu.
Dk Tulia akijibu mwongozo huyo amesema wapo wabunge Nairobi ambao humletea taarifa Spika kila wakati juu ya hali ya mbunge Lissu.
Amewataja wabunge hao kuwa ni Freeman Mbowe ambaye ni Mbunge wa Hai na  Mwenyekiti wa Chadema, pia Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni.
Mwingine ni Mbunge wa Iringa Mjini (Chadema), Mchungaji Peter Msigwa.

Ofisa kilimo achapwa bakora na wakulima


Zaidi ya wakulima 19 waliovamia vyanzo vya maji katika bwawa la Mwanzugi wilayani Igunga wamemchapa bakora Ofisa Kilimo wa Kata ya Igunga, Jamila Issa kwa kuwapiga picha.
Tukio hilo lilitokea jana Jumapili ofisa huyo alipokwenda kuangalia utekelezaji wa agizo alilotoa Agosti 27 la kuwapa siku 14 wakulima hao wawe wameondoka katika bwawa hilo.
Ofisa huyo amesema alienda eneo hilo akiwa amefuatana na baadhi ya viongozi wa mtaa kukagua iwapo wakulima wameondoka lakini waliwakuta wakiendelea na kilimo kwenye vyanzo vya maji.
“Nilipofika eneo hilo nilikuta wakulima zaidi ya 19 wakiendelea na kilimo, baadhi wakipanda nyanya na mahindi. Nilianza kuwapiga picha kupata ushahidi, walipobaini walinishambulia kwa fimbo huku viongozi niliofuatana nao wakitimua mbio,” amesema ofisa kilimo Issa.
Amesema baada ya kuanguka, wakulima walitimua mbio na majembe yao na fahamu zilipomrudia alienda kituo cha polisi kuchukua fomu kwa ajili ya  matibabu ambayo aliyapata katika Hospitali ya Wilaya ya Igunga na aliruhusiwa kurejea nyumbani.
Hata hivyo, amesema  hataogopa kufanya kazi na kuwachukulia hatua wote watakaoendelea kulima kwenye vyanzo vya maji.
Mtendaji wa Kata ya Igunga, Robert Mwagala amesema Polisi kwa kushirikiana na raia wema watawasaka wakulima waliomshambulia ofisa kilimo huyo.
Diwani wa Igunga, Charles Bomani amesema kitendo kilichofanywa na wakulima hao hakikubaliki, hivyo ni lazima hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yao.
Baadhi ya wakulima waliotii agizo la kuondoka kwenye bwawa hilo wamelitaka Jeshi la Polisi kuchukua hatua za haraka juu ya watu waliofanya ukatili huo.
Mkazi wa Kata ya Igunga, Idd Jackson amesema ni aibu na fedheha kumshambulia kiongozi akitekeleza majukumu yake, hivyo ni lazima hatua za kisheria zichukuliwe kwa waliohusika.

Rais Magufuli aeleza ni kwa nini aliteua kaimu Jaji Mkuu


Rais John Magufuli amefichua siri ya kumteua Profesa Ibrahim Juma kuwa Kaimu Jaji Mkuu akisema hakuwa na historia ya kutosha ya majaji wengi alipoingia madarakani.
Amesema alipoingia madaraka ilikuwa kipindi kifupi ambacho aliyekuwa Jaji Mkuu, Mohamed Chande Othman alistaafu hivyo ilimlazimu achukue muda mrefu wa kujiridhisha na alitumia Ibara ya 118 (4) kumteua Kaimu Jaji Mkuu.
Rais Magufuli amesema hayo leo Jumatatu, Ikulu jijini Dar es Salaam wakati wa kumwapisha Jaji Mkuu, Profesa Juma baada ya kumteua jana Jumapili.
Hafla hiyo imehudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.
“Nilifanya hivi si kwa sababu hakuna majaji au walikuwa hawafai, majaji wote ni wazuri na mnafanya kazi nzuri sana lakini sikutaka kuteua jaji baada ya mwaka mmoja nateua tena au baada ya miaka miwili anastaafu, nilitaka nikiteua akae miaka hata 10, awe ‘anatujaji’ wote tutakaokuwepo,” amesema Rais Magufuli.
Amesema kumteua Jaji Mkuu ni kazi ngumu, lazima ujue historia na tabia zake, pia kuangalia iwapo ataweza kuendana na dhamira yake ya kupambana na rushwa.
Rais Magufuli amesema rushwa ipo kila sehemu, hivyo baada ya kuchaguliwa na wananchi mwaka 2015 alikaa chini na kumwomba Mungu apate kiongozi atakayeenda kulisimamia jambo hilo kwa kipindi kirefu zaidi.
Amesema wapo majaji wengi na wenye sifa lakini baadhi yao wamebakisha muda mchache kustaafu.
“Katika kufanya uchambuzi wangu nikamwona Profesa Juma ambaye alikidhi vigezo vyangu. Nakupongeza sana Profesa Juma ni Mungu ambaye amekuchagua kwa hiyo, kawatumikie vizuri watu wa Mungu na utangulize mbele masilahi ya Watanzania,” amesema.
Rais Magufuli amesema ingawa bado kuna changamoto mbalimbali katika Mhimili huo, alimuhakikishia Profesa Juma kwamba Serikali inazitambua na aliwataka majaji kutembea kifua mbele kwa kuwa Serikali inatambua kazi nzuri wanayoifanya.
Amesema kazi nzuri yoyote haikosi watu wa kuiponda, akitumia msemo wa mti wenye matunda ndiyo unaopopolewa kwa mawe.
Kiongozi huyo mkuu wa nchi amesema alipomteua kuwa Kaimu Jaji alipondwa lakini alikuwa mvumilivu na hakupata shinikizo la mtu yeyote la kumteua Jaji Mkuu.

Katibu Mkuu Chadema aripoti Polisi


Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Vincent Mashinji ameamua kwenda kuripoti Makao Makuu ya Jeshi la Polisi jijini hapa.
Taarifa iliyotolewa leo Jumatatu na Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Chadema, Tumaini Makene imesema Dk Mashinji ameambatana na wasaidizi wake kutoka makao makuu ya chama hicho.
“Katibu mkuu amewasili Makao Makuu ya Jeshi la Polisi, jijini Dar es Salaam, kuitikia wito wa Polisi uliotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto, kuwa anatakiwa kufika Ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI)” amesema.
Awali, leo Jumatatu Dk Mashinji alisema  hawezi kwenda kuripoti kwa kuwa hakuambiwa siku maalumu ya kwenda.
Kamanda Muroto amemtaka Dk Mashinji afike ofisi ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai mkoani Dodoma au ofisi kama hiyo iliyopo Kituo Kikuu cha Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam ili kutoa ushirikiano kwa jeshi hilo kuhusu tukio la kushambuliwa kwa risasi Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu.
“Nina taarifa za kuitwa Polisi, lakini haziko ‘specific’.  Ni wakati wowote naweza kwenda? na hawajasema nikaripoti wapi. Kwa hiyo, wakinihitaji watakuja kuniambia,” amesema Dk Mashinji akizungumza na Mwananchi leo.
Lissu alipigwa risasi na watu wasiojulikana Septemba 7 mchana alipokuwa akielekea nyumbani kwake Area D mjini Dodoma.
Kwa sasa Lissu anaendelea na matibabu katika Hospitali ya Aga Khan jijini Nairobi, Kenya.

Lowassa amtembelea Lissu kumjulia hali


Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa yupo Nairobi nchini Kenya kumjulia hali Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu aliyelazwa katika Hospitali ya Aga Khan, baada ya kushambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana.
Lissu ambaye pia ni mwanasheria wa Chadema alijeruhiwa kwa risasi tano Alhamisi Septemba 7 akiwa ndani ya gari nyumbani kwake Area D mjini Dodoma akitokea bungeni.
Katika akaunti yake ya Twitter, Lowassa ame-tweet akisema, “Earlier today i paid a visit at Nairobi Hospital to see our MP, President of TLS and dear friend @tundulissutz He is recovering well. It is Sad times for Tanzania. Let us all keep praying.”
Kwa tafsiri isiyo rasmi amesema “Mapema leo nilitembelea Hospitali ya Nairobi  kumwona mbunge, Rais wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) na rafiki kipenzi Tundu Lissu. Anaendelea vizuri. Ni kipindi cha masikitiko kwa Tanzania. Kwa pamoja tuendelee kuomba.”
Katika tweet hiyo, Lowassa ambaye ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, ameweka picha akiwa pamoja na Alicia ambaye ni mke wa Lissu; Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na dereva wa Lissu Simon Mohamed Bakari.

Rais wa zamani wa Georgia Mikheil Saakashvili aingia Ukrain kwa nguvu

Former Georgian President Mikheil Saakashvili is surrounded by his supporters as he arrives at a checkpoint on the Ukrainian-Polish border in Krakovets, Ukraine September 10, 2017Haki miliki ya pichaREUTERS
Image captionRais wa zamani wa Georgia Mikheil Saakashvili (katikati)aingia Ukrain kwa nguvu
Mikheil Saakashvili ambaye ni rais wa zamani wa Georgia na pia gavana wa zamani wa jimbo nchini Ukrain amevuka na kuingia nchini Ukrain aisaidiwa na mamia ya wafuasi wake.
Bwana Saakashvili alisema kuwa alisukumwa bila kutarajia kwenye mpaka na umati wa watu waliokuwa wamekasirika kuwa mpaka ulikuwa umefungwa.
"Walitusukuma na kutebeba hadi nchini Ukarain," alesema Saakashvili.
Maafisa nchini Ukrain wanasema kuwa aliiangia nchini humo kinyume na sheria na walinzi 15 na mpaka walijeruhiwa.
Kulikuwa na mivurutano kwenye mpaka kati ya wafuasi wa bwana Saakashvili na maafisa wa mpaka.
Former Georgian President Mikheil Saakashvili (L) and former Ukrainian Prime Minister Yulia Tymoshenko are seen at the railway station in Przemysl, Poland, close to the Ukrainian border on September 10, 2017Haki miliki ya pichaAFP
Image captionMikheil Saakashvili na waziri mkuu wa zamani Yulia Tymoshenko
Bwana Saakashvili ambaye awali alikuwa ni raia wa Georgia na kisha raia wa Ukrain kwa sasa hana uraia wa nchi yoyote baada ya uraia wake wa Ukrain kufutwa na mshirika wake wa zamani raid Petro Poroshenko.
Pia anatakiwa nchini Georgia kwa kesi zinazohusu uhalifu ambazo anadai kuwa zimechochewa kisiasa.
Mapema Jumapili treni yake ilizuiwa katika kituo huko Przemysl nchini Poland baada ya walinzi wa Ukrain kumzuia kuingia.
Bwana Saakashivili alijiunga na wafuasi wake kadha akiwemo waziri mkuu wa zamani wa Ukrain na kiongozi wa sasa wa upinzani Yulia Tymoshenko.
A line of Ukrainian border guards stand at the crossing with Poland not far from Lviv (10 Sept 2017)Haki miliki ya pichaEPA
Image captionRais wa zamani wa Georgia aingia Ukrain kwa nguvu
Mwaka 2015 aliteuliwa gavana wa Odessa na Bw. Poroshenko lakini wawili hao walitofautiana mwezi Novemba mwaka uliopita baada ya Bw Saakashvili kumlaumu rais wa kuzuia jitihada za kumaliza ufisadi.
Lakini alipokuwa akikubali uaria wa Ukrain alisalimisha uraia wa Georgia.
Akiwa nchini Ukrain anaweza kukamatwa na kurudishwa nchini Geogia ambapo atafunguliwa mashtaka.

Kimbunga Irma chalipiga kwa nguvu jimbo la Florida

Kimbunga Irma chaingia jimbo la FloridaHaki miliki ya pichaAFP
Image captionKimbunga Irma chaingia jimbo la Florida
Kimbunga Irma kimepiga visiwa vilivyo kusini mwa jimbo la Florida nchini Marekani kikiwa katika kiwango cha nne, kwa mujibu wa watabiri wa hali ya hewa.
Kimbuga hicho kumepiga visiwa vilivyo nyanda za chini na upepo wa kasi ya hadi kilomita 209 kwa saa kabla ya kuelekea kaskazini magharibi kwa ghuba ya Florida.
Zaidi ya watu milioni 6.3 waliambiwa waondoke Florida, huko onyo likitolewa kuwa kubunga hicho kinaweza kuwa tisho kwa maisha.
Irma tayari kimeharibu eneo ya Caribbean ambapo takribana watu 25 wameuawa.
Viwango vya maji tayari vimeanza kuogezeka katika maeneo ya pwani ya Florida, eneo ambalo linatarajia kimbunga kikubwa kuwasili.
Taharuki na hatma ya baadaye ya mji wa Tampa, ambao unakabiliana ana kwa ana na njia inakopitia kimbunga hicho, haijulikani.
Ramani ya mwendo wa Kimbunga Irma
Image captionRamani ya mwendo wa Kimbunga Irma
Tampa inasemekana kuwa ni mji ulioko katika mazingira magumu zaidi nchini Marekani, hasa kuhusiana na hatari ya kugongwa mara kwa mara na vimbunga.
Pia wakuu jimbo la Florida wametangaza hali ya tahadhari ya kutotoka nje, katika baadhi ya maeneo ya jimbo hilo, ukiwemo mji wa Miami.

Picha ya waziri mkuu wa Australia akishika mtoto na bia mkononi yazua maoni mitandaoni

Malcolm Turnbull kisses his young granddaughter while holding her in one hand and a beer in another, at a sporting match in Sydney on SaturdayHaki miliki ya pichaMALCOLM TURNBULL
Image captionPicha ya waziri mkuu wa Australia akishika mtoto na bia mkononi yazua maoni mitandaoni
Watu nchini Australia wamejitokeza kumtetea waziri mkuu Malcolm Turbull baada ya picha yake akimshika mjukuu wake na bia mkononi kuzungumziwa kwa wingi,.
Bwana Turbull alisambaza picha hiyo mwenyewe akimshika mjukuu wake kwenye uwanja mmoja wa kandanda mjini Sydney siku ya Jumamosi.
Picha hiyo ilichapishwa kwenye ukurasa wake wa Facebook.
Lakini ilizua maoni ya kumkosoa Bw Turnbul kutokana na kuwepo kwa bia.
"inakera kushika mtoto na bia mkononi," aliandika Marg Walker.
Suala hilo lilipata maoni mengi wakati lilianza kuangaziwa na vyombo vya habari.
Baada ya lawama kuibuka pia wale waliomtetea nao walinza kutoa maoni yao wakisema kuwa Bw. Turnbull hajafanya lolote baya.

UN: Mauaji ya kikabila yanafanyika Myanmar

A Rohingya refugee man pulls a child as they walk to the shore after crossing the Bangladesh-Myanmar border by boat through the Bay of Bengal in Shah Porir Dwip, Bangladesh, 10 September 2017Haki miliki ya pichaREUTERS
Image captionZaidi ya watu 300,000 waisilamu wa Rohingya, wamekimbia kwenda Bangaladesh tangu ghasia zianze mwezi uliopita
Oparesheni ya kiusalama inayowalenga waislamu wa Rohingya nchini Myanmar ni mfano wa mauaji ya kikabila, mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa amesema.
Zeid Raad Al Hussein ameitaka Mynamar kusitisha oparesheni mbaya ya kijeshi katika jimbo la Rakhine.
Zaidi ya watu 300,000 waisilamu wa Rohingya, wamekimbia kwenda Bangaladesh tangu ghasia zianze mwezi uliopita.
Jeshi linasema kuwa linajibu mashambulizi yaliyofanywa na wanamgambo wa Rohingya na kukana kuwalenga raia.
Ghasia hizo zilianza tarehe 25 mwezi Agosti wakati wapiganaji wa Rohingya walishambulia vituo vituo vya polisi kaskazini mwa Rakhine na kuwaua maafisa 12 wa ulinzi.
Rohingya ambao wameikimbia Myanmar tangu wakati huo, wanasema kuwa wanajeshi walijibu vikali kwa kuchoma vijiji na kuwashambulia raia kwa minajili ya kuwafukuza.
Rohinga ambayo ni jamii ndogo ya waislamu wasio na utaifa wamekumbwa na mauaji kwa muda mrefu nchini Myanmar ambayo inasema kuwa wao ni wahamiaji haramu.

Watu 7 wauawa kwa kupigwa risasi Dallas Marekani

A video screengrab shows police vehicles arriving at the scene of the shooting in Plano, Dallas, TexasHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionWatu 7 wauawa kwa kupigwa risasi Dalllas Marekani
Mtu mwenye bunduki amewaua watu saba kwenye nyumba moja mjini Dallas, Texas nchini Marekani, kabla ya kuuliwa kwa kipigwa risasi na polisi.
Watu wawili ambao nao walipigwa risasi wako hospitalini.
Msemaji wa polisi David Tilley alisema kuwa mshambuliaji aliuawa na polisi kwa kwanza ambaye alifika wakatin wa ufyatulianaji wa risasi. Polisi huyo hakujeruhiwa.
Kile kilichochangia shambulizi hilo bado hakijulikani au ikiwa mshambuliaji aliwafahamu waathiriwa.
"Tunajaribu kuangalia suala hili kwa kina," Bwa Tilley alisema.
Gazeti moja huko Dallas liliripoti kuwa wale waliouawa walikuwa wakitazama timu ya Dallas Cowboys, ambayo ni timu ya kandanda ya Marekani wakati walishambuliwa.
Polisi hawajatoa jina la mshambuliaji au muathirwa yeyote lakini wote wametajwa kuwa watu wazima.