Lissu ambaye pia ni mwanasheria wa Chadema alijeruhiwa kwa risasi tano Alhamisi Septemba 7 akiwa ndani ya gari nyumbani kwake Area D mjini Dodoma akitokea bungeni.
Katika akaunti yake ya Twitter, Lowassa ame-tweet akisema, “Earlier today i paid a visit at Nairobi Hospital to see our MP, President of TLS and dear friend @tundulissutz He is recovering well. It is Sad times for Tanzania. Let us all keep praying.”
Kwa tafsiri isiyo rasmi amesema “Mapema leo nilitembelea Hospitali ya Nairobi kumwona mbunge, Rais wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) na rafiki kipenzi Tundu Lissu. Anaendelea vizuri. Ni kipindi cha masikitiko kwa Tanzania. Kwa pamoja tuendelee kuomba.”
Katika tweet hiyo, Lowassa ambaye ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, ameweka picha akiwa pamoja na Alicia ambaye ni mke wa Lissu; Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na dereva wa Lissu Simon Mohamed Bakari.
No comments:
Post a Comment