Tuesday, October 10

UHURU KENYATTA AONGEA BAADA YA RAILA ODINGA KUJITOA KATIKA UCHAGUZI WA MARUDIO

TAARIFA KUTOKA JWTZ: ASKARI WAWILI WA TANZANIA WAUWAWA DRC

NAIBU WAZIRI AWESO AKAGUA MIUNDOMBINU YA MAJI UBUNGO



Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji leo amefanya ukaguzi wa miundombinu ya maji eneo la Ubungo na kujionea miundombinu hiyo ambayo mingi imepasuka na kuvujisha maji mengi kutokana na uchakavu au kuhujumiwa miundombinu hiyo.

Katika maeneo aliyopita ameweza kuona upotevu mkubwa wa maji unaotokana na mabomba yaliyopasuka kuvuja, na kusababisha maji mengi kupotea baada ya kuwafikia wananchi kwa ajili ya matumizi.

Naibu Waziri Aweso alisema ipo haja ya kuchukua hatua na kuhakikisha miundombinu hiyo inafanyiwa ukarabati, ili kudhibiti tatizo la upotevu wa maji ambalo limekuwa changamoto kubwa jijini Dar es Salaam.

“Nitakaa na taasisi za DAWASA na DAWASCO tuweke mikakati ya kutatua changamoto hii, ili kuhakikisha kiwango cha upotevu wa maji kinapungua, kwa kuwa ni moja sababu ya wananchi kukosa maji ya uhakika, kwa kuwa mengi yanapotea baadala ya kuwafikia walengwa”, alisema Naibu Waziri.
 Fundi wa DAWASCO akiendelea na kazi ya kurekebisha bomba lililopasuka eneo la Riverside, Ubungo.
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso akizungumza na msimamizi wa matengenezo wa DAWASCO Kanda ya Tabata, aliyekuwa akisimamia matengenezo katika eneo la Riverside, Ubungo kwenye moja ya miundombinu ya maji iliyoharibika.
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso akiwa katika eneo la Kibangu, Ubungo akikagua moja ya maeneo yaliyo na miundombinu mibovu ya maji.

TANGA CEMENT YATOA MIFUKO ELFU MOJA YA SARUJI KWA AJILI YA UJENZI NYUMBA ZA POLISI ARUSHA


Jeshi la Polisi mkoani hapa, limepokea jumla ya tani hamsini sawa na mifuko elfu moja ya Saruji yenye thamani ya shilingi Milioni kumi na Mbili na Laki Tano toka kampuni ya Saruji yaTanga (Tanga Cement) ili ziweze kusaidia ujenzi wa nyumba za Askari wa Jeshi hilo ambalo hivi karibuni walipatwa na majanga ya moto yaliyosababisha nyumba za familia 13 kuungua na kuteketeza karibu kila kitu. 
Akipokea shehena hiyo kwa niaba ya Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Naibu Kamishna (DCP) Charles Mkumbo aliishukuru Kampuni ya Tanga Cement kwa kujitoa na kutambua mchango wa askari katika kuimarisha usalama, na kuahidi kusimamia ili ujenzi huo kasi yake iongezeke.
Alisema mbali na Kampuni hiyo pia aliwaomba watu wengine binafsi pamoja na Makapuni mengine waige mfano toka kwa kampuni hiyo kuisaidia jamii hasa katika sekta mbalimbali kama vile elimu, afya  na majanga kama haya.
Kamanda Mkumbo pia alitumia fursa hiyo kushukuru watu binafsi , makampuni,  taasisi pamoja na majeshi ya Ulinzi na Usalama kama vile Jeshi la Wananchi (JWTZ), Jeshi la Polisi Kilimanjaro, Chuo cha Polisi Moshi na Jeshi la Magereza.
Wengine ni kiwanda cha Magodoro cha Tanfoam, kiwanda cha A to Z, Ofisi ya Mwanasheria mkoani hapa, Green Valley School na Kampuni ya Otterlo Business Corporation Ltd (OBC) pamoja na watu binafsi ambao walitoa msaada wa fedha, Chakula, Saruji nguo pamoja na Magodoro.
Kwa upande wake Meneja Biashara wa kampuni hiyo Bw. Peet Brits alisema kwamba, wao kama kampuni wameweka mkazo kusaidia katika elimu, afya, maendeleo ya Jamii pamoja na mazingira lakini kwenye majanga mbalimbali kama vile ajali za moto.
Alisema kwamba anafahamu kazi zinazofanywa na Jeshi la Polisi katika kudumisha usalama ambapo unasaidia kuvutia mazingira mazuri ya kibiashara hapa nchini. Alisema wametoa msaada huo ili usaidie kujenga makazi ya familia za askari.
Bw. Brits alisema anajua walichochangia hakiwezi kutosheleza lakini wanaamini kitasaidia kwenye ujenzi wa nyumba hizo na kuzitaka kampuni pamoja na taasisi  kusaidia Jeshi la Polisi ambalo linaimarisha usalama hali ambayo inasaidia kuweka mazingira mazuri ya kibiashara.
 Meneja Biashara wa Tanga Cement Peet Brits akimkabidhi Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha Naibu Kamishna (DCP) Charles Mkumbo mifuko ya Saruji iliyotolewa na Kampuni hiyo ili iweze kusaidia ujenzi wa nyumba za Polisi zilizoungua moto hivi karibuni (Picha na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha)
 Baadhi ya mafundi na wasaidizi wao wakiendelea kujenga nyumba za Polisi jijini hapa (Picha na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha)
Moja ya lori lililobeba mifuko ya Saruji iliyotolewa na kampuni ya Tanga Cement kwa Jeshi la Polisi mkoani Arusha.
Picha na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha)

Raila Odinga ajiondoa kwa kinyang'anyiro cha urais Kenya

Kiongozi wa National Super Alliance (NASA) Raila Odinga (Katikati) akizungumza na waandishi wa habari mjini Nairobi, Kenya, Sept. 26, 2017.
Aliyekuwa mgombea wa urais kwa tikiti ya muungano wa National Super Alliance (Nasa), Raila Odinga, Jumanne alitangaza rasmi kujiondoa kwenye kinyang'anyiro cha marudio ya uchaguzi uliotarajiwa kufanyika tarehe 26 mwezi Oktoba
Odinga aliyatangaza hayo alipowahutubia waandishi wa habari mjini Nairobi.
Haya yamejiri wakati wabunge wa mrengo wa upinzani wakisusia vikao vya kamati ya bunge kuhusu azma ya ubadilishaji wa sheria ya uchaguzi.
.Miswada hiyo iliyowasilishwa na wabunge wa chama tawala cha Rais Uhuru Kenyatta, iwapo itapitishwa katika viwango vyote na kuwa sheria, katika kura ya Urais ijayo, tume ya uchaguzi itatakiwa kutangaza matokeo ya kura hiyo sambamba kupitia mfumo wa kielektroniki na mfumo usio wa kielektroniki kutoka vituo vyote vya upigaji kura
Na iwapo mifumo hiyo miwili itatofautiana, mfumo usiokuwa wa kielektroniki ndio utakaoidhinishwa. Vile vile, matokeo ya kura hiyo hayatabatilishwa iwapo mfumo wa kielektroniki haukutumika kutangaza mshindi.
Hata hivyo upinzani, wakilishi wa makanisa pamoja na mabalozi wa nchi za kigeni wameonekana kujitenga na mswada huo.

WASIOLIPIA HATIMILIKI KUPOTEZA MAENEO YAO

NA CLARA MATIMO – MWANZA
SERIKALI  kupitia Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza, imetahadharisha wananchi kuwa watapoteza haki ya kumiliki viwanja vyao endapo watashindwa kulipia malipo ya kuandaliwa hatimiliki.
Angalizo hilo lilitolewa na Ofisa Mipango Miji wa Manispaa ya Ilemela Mkoani Mwanza, Kenedy Chiguru, juzi baada ya kuona wananchi  hawajalipia gharama za kuandaliwa hati wakidhani kwamba gharama walizotoa kupimiwa maeneo yao ndizo zitakazotumika kuandaliwa hatimiliki.
Akizungumza na  MTANZANIA ofisini kwake, alisema urasimishaji makazi katika baadhi ya mitaa iliyopo ndani ya  kata 15 wilayani humo ni utekelezaji wa agizo la Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi, la Oktoba 12, mwaka jana akiwa katika ziara ya kikazi mkoani humo.
Chiguru alisema Waziri Lukuvi aliagiza ukamilishaji wa upimaji wa viwanja 35,019, kati ya hivyo Halmashauri ya Ilemela viwanja 16,141 na Nyamagana 1,8878.
“Urasimishaji makazi ulikuwa na mwitikio mkubwa wakati wa upimaji, wananchi wengi walijitokeza na kulipia gharama za kupimiwa maeneo yao, lakini baada ya kuona vigingi vimepandwa kwenye viwanja vyao wanadhani ndiyo mwisho wa zoezi.
“Dhana hiyo ni potofu kwa sababu ili utambulike kisheria na uwe na uhakika pia usalama wa kiwanja chako ni hadi pale utakapokuwa na hatimiliki ya kiwanja hicho.
“Wananchi wengi bado hawajajitokeza kulipia gharama za maandalizi ya hatimiliki wakati zoezi linaenda kufikia ukomo Oktoba 15, mwaka huu,” alisema Chiguru.
Aidha, Ofisa huyo wa Mipango Miji alisema  Jiji la Mwanza limeandaliwa Mpango Kabambe (Master Plan) ulioanza mwaka 2015 hadi 2035, uzinduzi wake utakapofanyika umilikishaji wa viwanja utafanyika kwa kuzingatia matumizi yaliyowekwa na mpango huo tu na si vinginevyo, huku akiwataka wananchi watumie fursa hiyo mapema kabla zoezi halijafikia mwisho.

Hatari ya kuvalia viatu bila soksi

A man wearing shoes but no socksHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Ukivalia viatu vyako bila soksi unajiweka katika hatari ya makubwa zaidi kuliko kunuka kwa miguu pekee.
Chuo cha tiba ya miguu nchini Uingereza kinasema karibuni kumekuwa na ongezeko la maambukizi ya maradhi yanayosababishwa na kuvu kutokana na kuvuma kwa mtindo wa kuvalia viatu bila soksi, hasa miongoni mwa vijana.
Mtaalamu Emma Stephenson anasema amekuwa akipokea wanaume wa kati ya miaka 18-25 walio na matatizo kwenye miguu yao ambayo yametokana na kutovalia soksi au kuvalia viatu visivyowatosha vyema.
Kutovalia soksi siku hivi kumekuwa mtindo maarufu wa mavazi, na mwanamuziki Sam Smith ni miongoni mwa watu wanaojitokeza hadharani wakiwa na viatu bila soksi.
Singers and Songwriters Sam Smith and Jimmy NapesHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Wanaume wengi katika maonesho ya mitindo pia mara nyingi huonesha mavazi wakiwa na viatu bila soksi.
Mwanamuziki Tinie Tempah amejishindia tuzo nyingi kwa sababu ya mitindo na mara nyingi katika maonesho ya mitindo ya Londo huketi viti vya mbele.
Yeye pia huwa mara nyingi havai soksi - lakini anafahamu madhara yake?
Tinie TempahHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionTinie (kati) ambaye jina lake halisi ni Chukwuemeka Okogwu anaonekana akiwa bila soksi
"Miguu ya binadamu kwa kawaida hutoa nusu painti (ambayo ni sawa na lita 0.28) ya jasho kila siku," Emma Stephenson anasema.
"Unyevu mwingi na joto unaweza kusababisha maambukizi ya maradhi yanayotokana na kuvu mfano ugonjwa unaosababisha mwasho na kuchubuka kwa ngozi (kwa Kiingereza athlete's foot)."
Kwa mujibu wa Emma, madhara yake yanaweza kuwa mabaya.
"Moja ya visa vibaya nilivyowahi kukumbana navyo ni cha mwanamume mmoja wa miaka 19 aliyefanya kazi ya kuosha magari. Miguu yake ilikuwa inatokwa na jasho sana na ilikuwa imechubuka sana."
Lakini bila shaka itachukua ujasiri kumwambia bingwa wa UFC Conor McGregor kwamba anaweza kupata matatizo kutokana na mtindo wake wa kuvalia viatu.
UFC champion Conor McGregorHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Emma anashauri kwamba siri ni kutozidisha, iwapo bado utataka kutovalia soksi.
Jaribu usivae viatu bila soksi kwa muda mrefu.
Jaribu pia kuweka kitu cha kukausha jasho kwenye soli ya kiatu chako kabla ya kukivalia bila soksi.
Kadhalika, kuwa makini kuchunguza miguu yako. Ukigundua unaumwa pahali tafuta usaidizi upesi.

Zaidi ya walimu 20,000 waliofeli mtihani wa wanafunzi wao kufutwa Nigeria

Zaidi ya walimu 20,000 waliofeli mtihani wa wanafunzi wao kufutwa Nigeria
Image captionZaidi ya walimu 20,000 waliofeli mtihani wa wanafunzi wao kufutwa Nigeria
Mamlaka katika jimbo lililo kaskazini mwa Nigeria la Kaduna zinasema kuwa zaidi ya walimu 20,000 wa shule za msingi watafutwa baada ya wao kufeli mtihani unaotahili kufanywa na wanafunzi wao.
Hii inafuatia madai kuwa nyingi ya shule za msingi na sekondari nchini Nigeria huzalisha wanafunzi wasiohitimu vyema.
Gavana wa jimbo la Kaduna el-Rufai alisema kuwa walimu waliohitimu wataajiriwa kuchukua mahala pa wale watakaofutwa.
Haijulikani hatua hii itachukuliwa lini.
Afisa mmoja wa cheo cha juu katika jimbo la Kaduna aliambia BBC kuwa mitihani zaidi itatolewa siku zinazokuja kwa walimu wa sekondani.
Wadadisi wanasema kuwa idadi hiyo ni ishara ya viwango duni vya elimu nchini Nigeria ambapo inadaiwa kuwa walimu huajiriwa kwa misingi ya kisiasa.

WATU WANNE WAHUKUMIWA KWENDA JELA MIAKA 30 NA VIBOKO 12.


Na Karama Kenyunko, Blogu ya jamii.
MAHAKAMA ya Hakimu  Mkazi Kisutu imewahukumu watu wa nne kutumikia kifungo cha mika 30 jela na kuchapwa viboko 12, sita wakati wa kuingia na sita wakati wa kutoka baada ya kupatikana na hatia dhidi ya kosa la wizi wa kutumia silaha.

Hukumu hiyo iliyosomwa na hakimu Mkazi, Respicious Mwijage imewataja waliofungwa kuwa ni Donald Nzweka, Michael Pascal,Ally Akili na Kurwa Mwakagenda.

Akisoma hukumu hiyo Hakimu Mwijage amesema, upande wa mashtaka umeweza kuthiitisha kosa hilo pasipo kuacha shaka na kuwa washtakiwa walishiriki kutenda kosa na kwamba mahakama ilijiuliza kwamba kosa la kutumia silaha ili lithibitike Jamhuri wana wajibu wa kuthibitisha bila kuacha shaka kwamba mshtakiwa kabla ya kutenda awe na kifaha hatari au wawe zaidi ya mmoja na kwamba baada ya tukio hilo walitumia nguvu kwa mtu waliyeporwa.

Katika kesi hii, mlalamikaji na mashahidi wengine walieleza kuwa usiku wa julai 7 majambazi walivunja mlango mkuu wa nyumba yao kwa kutumia bomu ambalo lilitambuliwa na polisi kuwa baruti na kasha kuendelea kuvunja milango mingine ambapo baada ya hapo waliingia katika chumba walichokuwa wamekaa, ambacho kilikuwa na mwanga, mshtakiwa mmoja alishika panga na kuanza  kuwapiga kwa kutumia ubapa.

Amesema, kwa kuzingatia ushahidi huo hakuna shaka kwamba mashahidi waliweza kuwatambua  majambazi na kuwa utetezi wa washtakiwa kwamba walikamatwa maeneo tofauti na kupelekwa oysterbay polisi na kupigwa na kunyanyaswa siyo ya kweli.

Kabla ya kusomwa kwa adhabu hiyo, Hakimu Mwijage aliuliza upande wa mashtaka kama walikuwa na lolote na kusema juu ya washtakiwa ambapo wakili wa serikali Gloria Mwenda, alidai washtakiwa ni  wakosaji wa mara ya kwanza na akaomba wapewe adhabu kali ili iwe fundisho kwa jamii.

“Nimeridhika ushahidi wa mashahidi 11 walioletwa na upande wa mashtaka ambao wameweza kuthibitisha bila ya kuacha shaka kuwa mlitenda kosa, nawahukumu kwenda jela miaka 30 na kuchapwa viboko 12, sita siku mnaingia na sita siku ya kutoka" amesema Mwijage.

Awali ilidaiwa, Julai 7 ,2013 huko maeneo ya Boko Magengeni, jijini Dar es Salaam, washtakiwa hao waliiba simu nne pesa taslimu  150,000 na cheni za dhababu mbili ambapo vitu vyote vina thamani ya  2050,000 mali ya Hobokela Mwakijambile.

Mtuhumiwa auawa na wenzake chini ya ulinzi wa polisi


Moshi. Mkazi wa jijini Dar es Salaam, Robert Massawe (51), ambaye polisi wanadai ni mtuhumiwa wa uporaji na mauaji, ameuawa kwa kupigwa risasi na watu wanaodaiwa kuwa ni wahalifu wenzake.
Kabla ya kuuawa katika majibizano ya risasi, mtuhumiwa huyo anadaiwa alikamatwa akiwa na SMG yenye risasi 24, simu 19 zilizoporwa maeneo mbalimbali na laini za simu 58.
Taarifa iliyotolewa leo Jumanne na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Hamisi Issah imesema mtuhumiwa aliuawa na wenzake saa tisa usiku wa kuamkia jana wilayani Rombo.
Amesema mtuhumiwa pamoja na mkewe walikamatwa jijini Dar es Salaam na baada ya kuhojiwa na polisi inadaiwa alieleza matukio ya ujambazi aliyoshiriki na alikubali kuwaonyesha mahali alipoficha bunduki.
Polisi imesema simu tatu kati ya 19 wamegundua ziliporwa Moshi na moja alikuwa akiitumia mkewe ambaye anashikiliwa Dar es Salaam.
Kamanda Issah amesema aliwaeleza polisi kuhusu mpango wa kufanya tukio la ujambazi katika Kijiji cha Chilio, Kata ya Holili wilayani Rombo jana alfajiri.
Amesema askari walifuatana naye chini ya ulinzi hadi Moshi kwenye dampo lililopo jirani na kiwanda cha ngozi ambako bunduki ilifukiwa ardhini ikiwa na risasi 24.
“Chini ya ulinzi wa askari kanzu, alipowaona wenzake alipiga kelele kuwajulisha polisi walikuwepo eneo hilo,” amesema.
Kamanda Issah amesema kelele ziliwafanya watuhumiwa hao kukimbia huku wakifyatua risasi hovyo na baadhi zilimpiga Massawe mkono wa kushoto, mgongoni na mguuni hivyo kusababisha kifo chake.
Polisi imesema mtuhumiwa alishiriki matukio manane ya uporaji wa fedha na mauaji kwa kutumia silaha na amewahi kufungwa kwa ujambazi lakini aliachiwa baada ya kukata rufaa.

AGA KHAN KUWASILI NCHINI KESHO

Imam wa Waislamu wa Madhehebu ya Shia Ismaili na Mwenyekiti wa Mtandao wa Maendeleo wa Aga Khan (AKDN), Aga Khan, anatarajia kuwasili nchini kesho kwa ziara ya siku mbili kwa mwaliko wa Rais John Magufuli.
Mratibu wa Mawasiliano wa Jumuiya ya Aga khan, Aly Ramji, amesema ziara hiyo imelenga kupanga mikakati zaidi ya kukuza ushirikiano kati ya Mtandao wa AKDN na Serikali ya Tanzania katika kukuza uchumi wake.
“Ujio huu wa Aga khan nchini Tanzania ni muhimu sana kwani mbali na kualikwa na rais, lakini pia wataweza kujadili mambo mbalimbali katika hatua ya kukuza ushirikiano na kuleta maendeleo katika nyanja mbalimbali.
“Taasisi za AKDN ni kati ya mashirika makubwa ya kijamii na kiuchumi nchini Tanzania na huchangia maisha ya Watanzania wote, hivyo naamini kupitia ujio huu, utazaa matunda zaidi,” amesema Ramji.
Aidha, amesema Aga Khan atapokelewa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) na Waziri wa Mambo ya Nje, Dk. Augustine Mahiga.

Watu wapiga kura kumchagua rais mpya Liberia

lection workers walk past ballot boxes and voting materials at the National Electoral Commission headquarters in Monrovia, Liberia October 9, 2017Haki miliki ya pichaREUTERS
Image captionWatu nchini Liberia wapiga kura kumchagua rais mpya
Watu nchini Liberia wanapiga kura kumchagua mrithi wa mwanamke wa kwanza kuchaguliwa Rais barani Afrika na mshidi wa tuzo la amani la Nobel, Ellen Johnson Sirleaf.
Aliyekuwa mcheza kandanda nyota George Weah, na makamu wa rais Joseph Boakai ndio wagombea wakuu kwenye kinyanganyiro hicho.
Liberia, nchi iliyobuniwa na watumwa walioachiliwa huru kutoka Marekani karne ya 19, haijakuwa na mabadiliko ya amani ya madaraka kwa kipindi cha miaka 73.
Bi Sirleaf aliwashauri watu kupiga kura kwa amani kwenye taifa hilo ambalo bado linajijenga kutoka kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe vya miaka 14.
George Weah, addresses supporters during a campaign rally in Monrovia on October 8, 2017Haki miliki ya pichaAFP
Image captionBw Weah anawania kwa mara ya tatu
"Kura yako inakuhusu wewe na familia yako, sio chama wala kabila," alisema Sirleaf wakati akihutubia taifa.
Jumla ya wagombea 20 wa urais wanawania urais kumritjhi Bi Sirleaf.
Wao ni pamoja na Alex Cummings, mkurugenzi wa zamani wa kampuni ya Coca-Cola na MacDella, mwanamitindo na mpenzi wa zamani wa Bw Weah.
Bi Sirleaf, 78, anaondoka madarakani baada kuongoza kwa mihula miwili.
Aliingia madarakani mwaka 2006 baada ya mtangulizi wake Charles Taylor, kulazimishwa kuondoka madarakani na waasi mwaka 2003.
Joseph N Boakai, Presidential Candidate of the governing Unity Party(UP), and incumbent Vice president of Liberia speaks to supporters during a campaign rally in the port city of Buchanan City, Grand Bassa County, Liberia, 25 September 2017Haki miliki ya pichaEPA
Image captionBoakai amekuwa makamu wa rais tangu 2006
Taylor kwa sasa anatumikia kifungo cha miaka 50 jela nchini Uingereza kwa makosa yanayohusu uhalifu wa kivita na mzozo katika nchi jirani ya Sierra Leone.
Bwana Weah, 51, amemteua mke wa zamani wa Taylor Jewel Howard, kama mgombea mwenza.
Hili ndilo la jaribio la tatu la George Weah kuwania urais.
Bi Sirleaf amishindwa kumfanyia kampeni Bw Boakai na kuzua uvumi kuwa wawili hao huenda wametofautiana.
Karibu watu milini 2.2 wamejiandikisha kupiga kura kwenye uchaguzi huo. Uchaguzi wa bunge nao unafanyika leo.

Polisi watumwa kabla ya hotuba kuu Catalonia

Catalan leader Carles Puigdemont at a cabinet meeting in Barcelona, 10 OctoberHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionCarles Puigdemont, rais wa eneo la Catalonia
Kiongozi wa Catalonia Carles Puigdemont anakabiliwa na shinikizo kali za kumtaka achane na mipango ya kulitenganisha eneo hilo kutoka Hispania, kabla ya hotuba muhimu kwa bunge la eneo hilo.
Kuna uvumi kuwa huenda akatangaza uhuru kufuatia kura ya maoni iliyokumbwa na utata.
Polisi waliojihami wametumwa nje ya majengo ya bunge la Catalonia mjini Barcelona kabla ya hotuba hiyo.
Meya ya Barcelona amemshuri Bw. Puigdemont na waziri mkuu wa Hispnia Mariano Rahoy kutuliza hali.
Catalonia's regional police force, the Mossos d'Esquadra, guard the regional assembly parliament building in Barcelona, 10 October 2017Haki miliki ya pichaREUTERS
Image captionPolisi waliojihami wametumwa nje ya majengo ya bunge la Catalonia mjini Barcelona kabla ya hotuba hiyo
Hotuba ya Bw. Puigdemont inakuja baada ya kura ya maoni iliyoandaliwa Oktoba mosi ambapo maafisa wa Catalonia wanasema kuwa karibu asilimia 90 ya wapiga kuwa waliunga mkono uhuru.
Asilimia 43 ya wapiga kura walijitokeza kupiga kura.
Kura hiyo ilitajwa kuw iliyo kinyume na sheria na mahaka ya katiba ya Hispania.
Wapiga kura wa "HAPANA" waliisusia pakubwa kura hiyo na kulikuwa na ripoti kadha za udanganyifu.
Carles Puigdemont and Mariano RajoyHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionCarles Puigdemont, kushoto, na Mariano Rajoy