Friday, August 4

A CLIMATE CHANGE INSPIRED PROJECT LAUNCHES IN DAR ES SALAAM


The Kilimanjaro Project, a climate change inspired project, held a meeting with environment stakeholders and members of the press to introduce the project. A prominent business leader, Mr. Ali Mufuruki was the guest of honor during the meeting which also served as the official launch of the project.

The Kilimanjaro Project is an art for change campaign for sustainable futures and climate change awareness, using Mount Kilimanjaro as an indicator that we are experiencing rapidly changing climates and environmental degradation. Through active partnerships, The Kilimanjaro Project will raise awareness through a communications campaign that will inspire sustainable behavioral change.

The Kilimanjaro Project Launch at Seacliff Hotel Dar es Salaam. From left are; An Advisory Board Member, Kelvin Twissa, Project Lead, Sarah Scott and Guest of Honour, Ali Mufuruki.

  The project will use Khangas as a tool to send message and raise awareness. In an installation planned to take place in October 2018, the kilimanjaro project lay six khangas up the six hiking trails of the mountain, each carrying a different message around key aspects of the environment; reforestation, waste management, conservation, water stewardship, and renewable energy. The six khangas will meet at the top of Mount Kilimanjaro, calling for people to come together.   

The Kilimanjaro Project is driven by the vision of better futures for coming generations. The main goal of the project is to raise awareness, enter dialogue, and create solutions around sustainable futures and climate change.


The Guest of Honour, Ali Mufuruki, addresses invited guests during the launch.

Other goals are participating in the Sustainable Development Goals by supporting conservation, tree planting, education and social enterprise / small business development in Tanzania; engaging local communities to participate in solutions for creating a climate resistant future; fundraising for related projects - conservation, reforestation and water resource management and creating active partnerships.

The first edition of the khangas, Tuje Pamoja- Let Us Come Together is available for sale in Dar es Salaam. Dar es Salaam residents can pay for the khangas through Mpesa 5588080 - The Kili Project and pick up khangas at selected points; The Novel Idea bookshop at Slipway, Masaki and at Clouds Media’s offices in Mikocheni. The event which was sponsored by Cool Blue Pure Drinking Water took place at Sea Cliff Hotel in Dar es Salaam on the morning of 3rd August and later in the day followed by a cocktail reception at Kilimanjaro Wonders Hotel in Marangu, Kilimanjaro.



The Project Lead, Sarah Scott, addresses invited guests during the launch. please upload a press release bellow

SSRA YASHIRIKI MAONESHO YA NANENANE YANAYOENDELEA KWENYE VIWANJA VYA NZUNGUNI MKOANI DODOMA


Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Uhamasishaji wa Mamlama ya Usimamizi wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Sarah Kibonde Msika (wa pili kushoto) akifafanua jambo kwa wageni waliotembelea banda lao wakati wa Maonesho ya Nanenane yanayofanyika Kikanda katika viwanja vya Nzunguni Mkoani Dodoma.



Afisa wa Mamlama ya Usimamizi wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Aminah Kisisa akigawa vipeperushi kwa moja ya wadau waliotembelea Banda la SSRA kwenye Maonesho ya Nanenane Kanda ya Kati.



Afisa wa Uhusiano na Uhamasishaji wa Mamlama ya Usimamizi wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Ally Masaninga akifafanua kwa mmoja ya wadau waliotembelea banda la Mamlaka hiyo wakati wa Maonesho ya Nanenane Kanda ya Kati.



Sehemu ya wafanyakazi wa SSRA wakati wa Maonesho ya Nanenane



Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Uhamasishaji wa Mamlama ya Usimamizi wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Sarah Kibonde Msika, akimkabidhi mfuko wa SSRA pamoja na Vipeperushi Mratibu wa Maonesho ya Nanenane Kanda ya Kati Bw, Mwinuka, Maonesho hayo yanaendelea Mkoani Dodoma



Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Uhamasishaji wa Mamlama ya Usimamizi wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Sarah Kibonde Msika akiwa na wadau waliotembelea Banda la SSRA wakati wa Maonesho ya Nanenane Kanda ya Kati.



Timu ya Mamlama ya Usimamizi wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) katika picha ya pamoja wakati wa Maonesho ya Nanenane Kanda ya Kati yanayofanyika katika Viwanja vya Nanenane Mkoani Dodoma.

KWA SIMU TOKA :LONDON- MAHOJIANO MAFUPI KUHUSU KENYA LONDON



DSTV YAZINDUA MSIMU MPYA WA SOKA, LIGI YA UINGEREZA KUTANGAZWA KWA KISWAHILI


Wakati vuguvugu la soka ulimwenguni likizidi kupanda, Kampuni ya Multichoice Tanzania kupitia king’amuzi cha DStv imezindua kampeni maalum ya Msimu mpya wa Soka ijulikanayo kama ‘Full vyenga Bila Chenga’  ambapo watanzania kupitia DStv wataweza kushuhudia mubashara michuano mikubwa ya soka ulimwenguli inayotarajia kuanza hivi karibuni ikiwemo Ligi kuu ya Uingereza (PL) na ligi ya Hispania (La Liga) pamoja na makombe mengine maarufu Duniani.

Pazia la ligi kuu ya uingereza litafunguliwa jumapili Agosti 6 kwa mtanange wa ngao ya jamii kati ya Arsenal na Chelsea mchezo ambao utaonyeshwa  mubashara kupitia DStv.
 Mkurugenzi mtendaji wa Multichoice Tanzania Maharage Chande akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni maalum ya Msimu mpya wa Soka ijulikanayo kama ‘Full vyenga Bila Chenga’, Jijini Dar es salaam.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa msimu mpya wa soka iliyofanyika katika ofisi za Multichoice Tanzania jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi mtendaji wa Multichoice Tanzania Maharage Chande  amesema kuwa msimu huu wa soka, DStv inawahakikishia wateja wake wote kuliona soka katika muonekano bora zaidi huku wakiweza kufuatilia michuano hiyo kwa matangazo yatakayorushwa kwa lugha ya Kiswahili.

“Msimu huu watanzania, kupitia DStv, siyo tu kwamba wataona michuano mbalimbali ya soka ulimwenguni mubashara, bali pia watayaona katika ubora wa hali ya juu yaani High Definition na zaidi ya yote, tutawapatia fursa watanzania kufuatilia ligi kuu ya Uingereza kwa lugha ya Kiswahili”.

Amesema DStv imeendelea kuboresha huduma zake ikiwemo kuongeza vipindi na kurekebisha bei za vifurushi ili kuhakikisha kuwa watanzania wengi zaidi wanapata fursa ya kujionea matukio mbalimbali muhimu katika Nyanja zote za maisha ikiwemo michezo na burudani. Ametoa mfano wa ligi ya Hispania La Liga ambayo inaonekana yote katika kifurushi cha Bomba. Pia baadhi ya mechi za ligi kuu ya Uingereza (PL) pia zitaonekana katika kifurushi cha Bomba.
Kwa upande wake, Meneja Masoko wa Multichoice Tanzania Alpha Mria amesema kampeni ya Full Vyenga bila Chenga inamaanisha kuwa wateja wa DStv, msimu huu wa soka wataweza kuliona soka kwa muonekano bora zaidi, yaani bila chenga. “Tunatambua kuwa washabiki wa soka sasa wanataka walione soka vyema, kana kwamba nao wapo uwanjani. Kwa DStv, sasa hata mtu akilambwa chenga utaiona vyema, hata kama mtu anatoka jasho utaliona. Hakuna wingu wala ukungu, ni ‘full vyenga bila chenga’  alisema Alpha.

TAASISI ZA KIFEDHA ZASHAURIWA KUWA NA MASHARTI NAFUU YA UTOAJI MIKOPO



Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe Godfrey Zambi akinunua moja ya mkoba uliotengenezwa na kikundi cha Jauki kwenye banda la Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa mara baada ya kutembelea banda hilo wakati wa Maonesho ya 24 ya kilimo na sherehe za Nanenane katika Viwanja vya Ngongo nje kidogo ya Manispaa ya Lindi



Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe Godfrey Zambi akimtazama mnyama aina ya kakakuona wakati wa Maonesho ya 24 ya kilimo na sherehe za Nanenane katika Viwanja vya Ngongo nje kidogo ya Manispaa ya Lindi.



Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe Godfrey Zambi akitembelea mabanda mbalimbali ya wajasiriamali wakati wa Maonesho ya 24 ya kilimo na sherehe za Nanenane katika Viwanja vya Ngongo nje kidogo ya Manispaa ya Lindi



Baadhi ya Wajasiliamali wakimsubiri Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe Godfrey Zambi kutembelea katika banda lao wakati wa Maonesho ya24 ya kilimo na sherehe za Nanenane katika Viwanja vya Ngongo nje kidogo ya Manispaa ya Lindi.



Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe Godfrey Zambi akionyesha Dawa aina ya Mlonge inayotibu magonjwa mbalimbali wakati wa Maonesho ya24 ya kilimo na sherehe za Nanenane katika Viwanja vya Ngongo nje kidogo ya Manispaa ya Lindi.



Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe Godfrey Zambi akikagua baadhi ya viatu vilivyotengenezwa na wajasiriamali wakati wa Maonesho ya24 ya kilimo na sherehe za Nanenane katika Viwanja vya Ngongo nje kidogo ya Manispaa ya Lindi.



Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe Godfrey Zambi akikagua banda la Wakala wa vipimo wakati wa Maonesho ya 24 ya kilimo na sherehe za Nanenane katika Viwanja vya Ngongo nje kidogo ya Manispaa ya Lindi



Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe Godfrey Zambi akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kutembelea banda la Viwanda, Biashara na Uwekezaji wakati wa  Maonesho ya 24 ya kilimo na sherehe za Nanenane katika Viwanja vya Ngongo nje kidogo ya Manispaa ya Lindi


Na Mathias Canal, Lindi

Taasisi mbalimbali za fedha nchini zimeshauriwa kuwa na masharti nafuu ya utoaji mikopo ili kuwarahisishia wajasiriamali kuwa na fursa rahisi ya kupata mitaji kwa minajili ya kuendeleza biashara zao.

Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe Godfrey Zambi amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutembelea mabanda mbalimbali ya Maonesho ya 24 ya kilimo na sherehe za Nanenane katika Viwanja vya Ngongo nje kidogo ya Manispaa ya Lindi.

Katika Maonesho hayo yenye kauli mbiu ya “Zalisha kwa Tija Mazao na Bidhaa za Kilimo Mifugo na Uvuvi ili kufikia Uchumi wa Kati” wananchi watapata fursa yatawasaidia wananchi kupata wananchi watapata elimu ya matumizi ya teknolojia mbalimbali kwa muda mfupi lakini pia wadau kujionea na kujifunza huduma zitolewazo na serikali, mashirika ya umma na binafsi

Mhe Zambi alisema kuwa miongoni mwa changamoto ambazo zimekuwa mwiba mcvhungu kwa wajasiriamali ni pamoja na namna ya kupata mitaji kutoka katika taasisi mbalimbali za fedha jambo ambalo linarudisha nyuma maendeleo ya biashara. 

Alisema mikopo kutoka benki inatolewa kwa masharti makubwa na riba kubwa jambo ambalo ni kikwazo kwa wajasiriamali ambao wana mitaji midogo lakini inarudisha nyuma ufanisi wa wao na taifa kwa ujumla wake.

Alisema kuwa Sera ya nchi inaruhusu sekta binafsi kuendesha uchumi kupitia kampuni ndogo, za kati, na wajasilimali, hivyo mitaji kwa wajasiriamali ni jambo ambalo haliepukiki.

Zambi alisema kuwa wajasiriamali wakipatiwa huduma za fedha na kukuza mitaji yao, wana nafasi kubwa ya kuleta maendeleo ya mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.

Zambi amesifu maandalizi mzuri ya Sherehe hiyo inatayarishwa na kuratibiwa na Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi na kuhusisha Taasisi, Wizara na mtu mmoja mmoja kwa wote wanaoshughulika na kilimo.


Maonesho ya sikukuu ya wakulima Nanenane yanahusisha shughuli za wakulima, wafugaji wa mifugo, wafugaji wa nyuki, wavuvi, wanamazingira, wasindikaji wa bidhaa za mazao ya kilimo na mifugo, wizara taasisi/makampuni ya umma, makampuni binafsi, mabenki, Taasisi za umma na binafsi na mashirika yasiyo ya kiserikali.

Pia uzalishaji bora wa mazao ya nafaka, ubunifu wa teknolojia rahisi za kutotoa mayai, Kuongeza thamani ya mazao ya mifugo, Makampuni ya mawasiliano, ambapo Taasisi za elimu zitaonyesha ubunifu wa kumsaidia mfugaji, Tiba za asili, Wasindikaji wakubwa na wadogo wa mazao ya Kilimo, Mifugo, Uvuvi, Asali, na Nta. 

WASHIRIKI KUTOKA TANZANIA WA “YOUNG AFRICAN LEADERS INITIATIVE (YALI) 2017” WATEMBELEA UBALOZI WA TANZANIA, WASHINGTON, D.C


Tarehe 2, Agosti 2017) Washiriki 42 wa Mandela Washington Fellowship 2017 kutoka Tanzania waliofika mwezi Juni, 2017, walitembelea Ubalozi wa Tanzania, Washington, D.C. na kukutana na Balozi Wilson M. Masilingi. 

YALI, ni programu iliyoanzishwa na Rais mstaafu wa Marekani, Barack Obama kuwasaidia vijana wa Afrika kutembelea Vyuo vikuu vya Marekani kujifunza, kwa ufadhili wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani (U.S. Department of State). Baada ya kumaliza mafunzo katika vyuo mbalimbali Watanzania hao walitembelea Washington, D.C. kupokea vyeti na kutembelea Ubalozi wa Tanzania.

Balozi Masilingi aliwaasa kuwa wazalendo, kupendana na kuwa waadilifu katika kuendeleza uchumi wa nchi yetu kwa kuanzisha na kukuza biashara. Aliwashauri pia kushirikiana na Ubalozi na Diaspora ya Watanzania waliopo Marekani, kukuza sekta ya utalii, biashara, elimu na ujenzi wa viwanda.


Balozi Tanzania nchini Marekani, Wilson M. Masilingi akizungumza na Washiriki wa YALI, Mandela Wahington Fellows. (kulia) Afisa wa Ubalozi, Dismas Assenga.



Yali Mandela Washington Fellows 2017 wakiongea na Mhe. Balozi.



Balozi Wilson M. Masilingi akiwa na washiriki wa YALI Mandela Washington Fellows, 2017.

MHANDISI RAMO MAKANI AKAGUA SHUGHULI ZA UTALII NA MFUMO WA UKUSANYAJI MAPATO KATIKA HIFADHI YA TAIFA YA MLIMA KILIMANJARO



Naibu Waziri wa Maliasili, Mhandisi Ramo Makani (wa nne kushoto) akizungumza na watalii kutoka Marekani wakati wa ziara yake ya kukagua shughuli za utalii na mfumo wa ukusanyaji mapato katika geti la Machame ndani ya Hifadhi ya Taifa Mlima Kilimanjaro jana. Alipowauliza watalii hao ni wapi walipata habari za mlima huo, walijibu kuwa kila mtu anajua kuhusu mlima Kilimanjaro!. Wengine kutoka kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Kippi Warioba, Mhifadhi Mkuu wa KINAPA, Betrita Loibooki na nyuma yake ni Mbunge wa Vunjo, James Mbatia.



Naibu Waziri wa Maliasili, Mhandisi Ramo Makani (wa tatu kulia) akisikiliza maelezo kutoka kwa Mhifadhi wa KINAPA, Steven Moshi (wa pili kulia) namna mfumo wa ukusanyaji mapato unavyofanya kazi katika Hifadhi ya Taifa Mlima Kilimanjaro wakati wa ziara yake ya kukagua shughuli za utalii na mfumo wa ukusanyaji mapato katika geti la Machame jana. Kulia anayeshuhudia ni Mbunge wa jimbo la Vunjo, James Mbatia.



 Naibu Waziri wa Maliasili, Mhandisi Ramo Makani (katikati) akipanda mlima Kilimanjaro wakati wa ziara yake ya kukagua shughuli za utalii na mfumo wa ukusanyaji mapato katika geti la Machame jana. Kushoto kwake ni Mbunge wa Jimbo la Vunjo, James Mbatia, Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Kippi Warioba (kulia kwake), Mkurugenzi wa Idara ya Utalii, Zahoro Kimwaga (kushoto) na Mbunge wa Moshi Vijijini, Anthony Komu (kulia).


Naibu Waziri wa Maliasili, Mhandisi Ramo Makani (wa pili kulia) akisikiliza na kujibu kero mbalimbali za wapagazi wanaopandisha mizigo ya watalii katika mlima Kilimanjaro wakati wa ziara yake ya kukagua shughuli za utalii na mfumo wa ukusanyaji mapato katika geti la Machame jana



Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa Kilimanjaro, Betrita Loibook akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wahifadhi, mtalii na waongoza watalii. (PICHA NA HAMZA TEMBA - WIZARA YA MALIASILI NA UTALII)

Hafla ya uzinduzi wa Tawi la NBM Haydom Mkoa wa Manyara


l
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Sara Msafiri Ally ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Hanang akizindua jengo la tawi la NMB lililopo katika mji mdogo wa Haydom. 

Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Sara Msafiri Ally ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Hanang (wa tatu kulia) kikata utepe kuashiria uzindua wa jengo la tawi la NMB lililopo katika mji mdogo wa Haydom. Wa pili kulia ni Meneja wa NMB Kanda ya Kati, Straton Chilongola.

 KILIO cha wakazi wa jimbo la Haydom wilaya ya Mbulu mkoani Manyara cha kukosa huduma za kibenki toka Tanzania ipate uhuru,kimepata ufumbuzi wa kudumu baada ya NMB benki, kufungua tawi katika mji mdogo wa Haydom. 

Kwa mujibu wa mbunge wa jimbo la Haydom, Flatei Massay, katika kipindi chote hicho, wananchi wa jimbo hilo wamekuwa wakilazimika kufuata huduma za kibenki Mbulu mjini, umbali wa zaidi ya kilometa 90.  

Mbunge Massy alisema kitendo cha kufuata huduma za kibenki umbali mrefu kiasi hicho, kumekuwa na madhara mengi na makubwa, ikiwemo gharama kubwa ya usafiri na pia usalama wa fedha. “Umbali huo umesababisha wakulima, wafanyabiashara na wananchi kwa ujumla, kutunza fedha zao majumbani. 

Miaka ya nyuma majambazi yalitumia bomu kubomoa kasiri (sefu) la kutunzia fedha mali ya hospitali ya rufaa ya misioni Haydom na yalifanikiwa kuiba fedha, Pia fedha nyingi ziliungua kwa moto wa bomu”, alisema na kuongeza; “Zipo hisia kwamba majambazi hayo yalihisi hospitali hiyo haipeleki fedha benki kwa wakati kutokana na umbali mrefu benki ilipo, kwa hali hiyo yalitarajia kupata fedha za kutosha”. 

Mbunge huyo alisema kufunguliwa kwa benki hiyo yenye mashine mbili za kutolea fedha, wananchi na wafanyabiashara, wanapaswa kuitumia kikamilifu, ili kupanua kilimo na biashara zao. Kwa upande wake mgeni rasmi katika ufunguzi huo, kaimu mkuu wa mkoa wa Manyara, Sara Msafiri Ally, ameihimiza benki ya NMB kuongeza juhudi zaidi katika kuendelea kutoa mikopo na huduma zingine kwa wakazi wa vitongoji vyote mkoani Manyara. Alisema serikali ya awamu ya tano imeweka mikakati mizuri ya kupunguza umaskini, hivyo mikopo inayotolewa na mabenki ikiwemo NMB, itasaidia kuendeleza kukuza uchumi na kuongeza ajira. 

Ameongeza kwa kuwahimiza wananchi wa Haydom, kuchangamkia uwepo wa benki ya NMB, ili kutumia huduma zao za kibenki kupata maendeleo yao binafsi, wilaya ya Mbulu na mkoa wa Manyara kwa ujumla. “Serikali inawapongeza NMB kwa kutambua umuhimu wa kusaidia jamii. Ni ulweli usiofichika kuwa faida mnayopata katika huduma zenu za kibenki, inatokana na wananchi. Hivyo kusaidia jamii ni njia nzuri ya kurudisha shukrani kwa waliosaidia mkapata faida”, alifafanua Sara. Awali meneja wa NMB kanda ya kati, Straton Chilongola, alisema NMB tawi la Haydom, litahudumia vijiji na viitongoji vya Maghani, Labai, Maritadu, Endamilayi, Getanyamba na Dongobeshi. 

Aidha, alisema benki hiyo imeendelea kubuni bidhaa mbalimbali na zenye kuzingatia mahitaji halisi ya soko kwa wakati husika. “Moja ya bidhaa hizo, ni kampeni ya ‘FANIKIWA’ akaunti ambayo ni mahususi kabisa kwa wajasiriamali wadogo wadogo. Wajasiriamali hao ni pamoja na baba/mama lishe, wauza chipis, wenye maduka ya biashara yakiwemo ya nguo”, alifafanua Chilongola. Akifafanua zaidi,alisema akaunti hiyo inampa fursa mteja kupata mkopo wa shilingi laki tano hadi shilingi 30 milioni. 

Pia meneja huyo, alisema wanayo akaunti nyingine ya ‘Wajibu’ ambayo ni mahususi kwa ajili ya watoto wenye umri wa miaka 0-18. “Kwa upande wa teknolojia, tuna akaunti ya ‘Chap Chap’. Akaunti hii mteja anaweza kufungua akaunti kwa muda mfupi na papo hapo kupata kadi yake ya ATM, na kuanza kufanya miamala wo wote”, alisema Chilongola. Benki ya NMB, ina matawi zaidi ya 200 na mashine za kutolea fedha zaidi ya 700 nchi nzima.Ina wateja zaidi ya milioni mbili jambo linaloifanya kuwa benki pekee nchini yenye hazina ya wateja wengi kuliko benki zinginezilizopo nchini. 


Burudani zikiendelea.

 

Meneja wa NMB kanda ya kati, Straton Chilongola, akitoa taarifa yake kwenye hafla ya uzinduzi wa tawi la NMB Haydom mkoani Manyara. Hafla hiyo imefanyika katika mji mdogo wa Haydom.

 

Baadhi ya wakazi wa mji mdogo wa Haydom,waliohudhuria uzinduzi wa tawi la NMB katika mji mdogo wa Haydom wilaya ya Mbulu mkoani Manyara juzi.

 

Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Sara Msafiri Ally ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Hanang akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa tawi la NMB tawi la Haydom wilaya ya Mbulu uliofanyika juzi katika mji mdogo wa Haydom.Wa kwanza kushoto (waliokaa) ni meneja NMB kanda ya kati, Straton Chilongola na mbunge wa jimbo la Haydom, Flatei Massy.