Wakati vuguvugu la soka ulimwenguni likizidi kupanda, Kampuni ya Multichoice Tanzania kupitia king’amuzi cha DStv imezindua kampeni maalum ya Msimu mpya wa Soka ijulikanayo kama ‘Full vyenga Bila Chenga’ ambapo watanzania kupitia DStv wataweza kushuhudia mubashara michuano mikubwa ya soka ulimwenguli inayotarajia kuanza hivi karibuni ikiwemo Ligi kuu ya Uingereza (PL) na ligi ya Hispania (La Liga) pamoja na makombe mengine maarufu Duniani.
Pazia la ligi kuu ya uingereza litafunguliwa jumapili Agosti 6 kwa mtanange wa ngao ya jamii kati ya Arsenal na Chelsea mchezo ambao utaonyeshwa mubashara kupitia DStv.
Mkurugenzi mtendaji wa Multichoice Tanzania Maharage Chande akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni maalum ya Msimu mpya wa Soka ijulikanayo kama ‘Full vyenga Bila Chenga’, Jijini Dar es salaam.
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa msimu mpya wa soka iliyofanyika katika ofisi za Multichoice Tanzania jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi mtendaji wa Multichoice Tanzania Maharage Chande amesema kuwa msimu huu wa soka, DStv inawahakikishia wateja wake wote kuliona soka katika muonekano bora zaidi huku wakiweza kufuatilia michuano hiyo kwa matangazo yatakayorushwa kwa lugha ya Kiswahili.
“Msimu huu watanzania, kupitia DStv, siyo tu kwamba wataona michuano mbalimbali ya soka ulimwenguni mubashara, bali pia watayaona katika ubora wa hali ya juu yaani High Definition na zaidi ya yote, tutawapatia fursa watanzania kufuatilia ligi kuu ya Uingereza kwa lugha ya Kiswahili”.
Amesema DStv imeendelea kuboresha huduma zake ikiwemo kuongeza vipindi na kurekebisha bei za vifurushi ili kuhakikisha kuwa watanzania wengi zaidi wanapata fursa ya kujionea matukio mbalimbali muhimu katika Nyanja zote za maisha ikiwemo michezo na burudani. Ametoa mfano wa ligi ya Hispania La Liga ambayo inaonekana yote katika kifurushi cha Bomba. Pia baadhi ya mechi za ligi kuu ya Uingereza (PL) pia zitaonekana katika kifurushi cha Bomba.
Kwa upande wake, Meneja Masoko wa Multichoice Tanzania Alpha Mria amesema kampeni ya Full Vyenga bila Chenga inamaanisha kuwa wateja wa DStv, msimu huu wa soka wataweza kuliona soka kwa muonekano bora zaidi, yaani bila chenga. “Tunatambua kuwa washabiki wa soka sasa wanataka walione soka vyema, kana kwamba nao wapo uwanjani. Kwa DStv, sasa hata mtu akilambwa chenga utaiona vyema, hata kama mtu anatoka jasho utaliona. Hakuna wingu wala ukungu, ni ‘full vyenga bila chenga’ alisema Alpha.
No comments:
Post a Comment