Saturday, November 25

MAJALIWA: TANESCO KAWAHUDUMIENI WANANCHI VIJIJINI


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameliagiza Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) liwafuate wananchi walioko katika vijiji vinavyotarajiwa kuunganishiwa umeme kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na kuwahudumia.

Amesema Serikali imetenga shilingi trilioni moja kwa ajili ya kusambaza umeme katika vijiji vyote ambavyo bado havijaunganishiwa nicety hiyo nchini, hivyo ni vema wakawatembelea wananchi katika maeneo yao na kuwahudumiahuko huko.

Waziri Mkuu alitoa kauli hiyo jana jioni (Ijumaa, Novemba 24, 2017) kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa michezo Tunduru, ambapo aliwasisitiza watumishi wa TANESCO kutokaa maofisini na badala yake wakawahudumie wananchi katika vijiji vyao.

Alisema katika kipindi hiki ambacho Serikali inatekeleza miradi ya kusambaza umeme vijini kupia REA, TANESCO wanatakiwa kwenda vijijini na kuwaandikisha wananchi wanaohitaji huduma hiyo pamoja na kufungua vituo vya muda vya malipo.

Waziri Mkuu alisema hatua hiyo itawapunguzia wananchi gharama za kusafiri hadi kwenye makao makuu ya wilaya kufuata huduma mbalimbali ikiwemo ya kulipia gharama za kuunganishiwa umeme katika nyumba zao.

Alisema Serikali imedhamiria kusambaza huduma ya nishati ya umeme katika vijiji vyote nchini vikiwemo vya wilaya ya Tunduru ambapo wananchi hao wataunganishiwa umeme huo kwa gharama ya sh. 27,000 tu.

Pia Waziri Mkuu aliesema wananchi hawatowajibika tena katika kulipia gharama za nguzo wala fomu za maombi ya kuunganishiwa umeme, kwa sababu tayari gharama hizo zimeshabebwa na Serikali.

Waziri Mkuu aliongeza kwamba lengo la Serikali ya awamu ta tano chini ya Rais Dkt. John Magufuli ni kufikisha umeme kwenye vijiji vyote Tanzania na kwa vile ambavyo viko kwenye maeneo yaliyo mbali na gridi vitafungiwa sola, jambo ambalo litafungua fursa za ajira na kukuza uchumi kwa wananchi na Taifa.

Waziri Mkuu alisema huduma hiyo ni muhimu kwani mbali ya kutumika katika matumizi ya majumbani, pia kwa kusogezwa karibu na maeneo ya pembezoni itawezesha zahanati, shule ,viwanda na vituo vya afya kuwa na umeme.

Awali Waziri Mkuu alitembea na kukagua shughuli za ujenzi wa mradi wa kituo cha afya kinachojengwa katika eneo la Nakayaya wilayani Tunduru pamoja na kukagua ghala la kuhijfadhia korosho na kisha kupokea taarifa ya kiwanda cha kubangulia korosho cha Korosho Afrocan Limited.


IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU, 
JUMAMOSIni, NOVEMBA 25, 2017.

Kanzi Data Ya Kuhifadhi Taarifa Za Wadau Wa Tasnia Ya Filamu Kuleta Maslahi Katika Tasnia


Rais wa Shirikisho la Filamu Bw. Simon Mwakifwamba akizungumza wakati wa kusaini mkataba wa kutengeneza Kanzi Data itakayohifadhi taarifa za wanatasnia ya filamu kati ya kampuni ya Cogsnet na Shirikisho la Filamu leo Jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi wa Cogsnet Bw. Nkundwe Moses Mwasaga akielezea namna kampuni hiyo itakavyohifadhi data za wanatasnia ya filamu wakati wa kusaini mkataba wa kutengeneza Kanzi Data itakayohifadhi taarifa za wanatasnia ya filamu kati ya kampuni ya Cogsnet na Shirikisho la Filamu leo Jijini Dar es Salaam
Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fissoo akifafanua jambo wakati wa kusaini mkataba wa kutengeneza Kanzi Data itakayohifadhi taarifa za wanatasnia ya filamu kati ya kampuni ya Cogsnet na Shirikisho la Filamu leo Jijini Dar es Salaam
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Harrison Mwakyembe akizungumza wakati wa kusaini mkataba wa kutengeneza Kanzi Data itakayohifadhi taarifa za wanatasnia ya filamu kati ya kampuni ya Cogsnet na Shirikisho la Filamu leo Jijini Dar es Salaam
Rais wa Shirikisho la Filamu Bw. Simon Mwakifwamba (wapili kushoto waliokaa) pamoja na mwanasheria wa kampuni ya Cogsnet Bw. Thomas Herman (katikati waliokaa) wakisaini mkataba wa kutengeneza Kanzi Data itakayohifadhi taarifa za wanatasnia ya filamu kati ya kampuni ya Cogsnet na Shirikisho la Filamu leo Jijini Dar es Salaam. Waliosimama katikati ni Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Harrison Mwakyembe
Rais wa Shirikisho la Filamu Bw. Simon Mwakifwamba (kulia) akikabidhiana mkataba na mwanasheria wa kampuni ya Cogsnet Bw. Thomas Herman (kushoto) baada ya kusaini mkataba wa kutengeneza Kanzi Data itakayohifadhi taarifa za wanatasnia ya filamu kati ya kampuni ya Cogsnet na Shirikisho la Filamu leo Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Harrison Mwakyembe (waliokaa katikati) katika picha ya pamoja na wadau wa tasnia ya filamu baada ya kusaini mkataba wa kutengeneza Kanzi Data itakayohifadhi taarifa za wanatasnia ya filamu kati ya kampuni ya Cogsnet na Shirikisho la Filamu leo Jijini Dar es Salaam. Wapili kulia ni Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fissoo.Picha na: Genofeva Matemu – WHUSM


Na: Genofeva Matemu – WHUSM

Wadau wa tasnia ya filamu nchini wametakiwa kujitokeza kwa wingi kujiunga katika vyama vilivyopo chini ya Shirikisho la filamu ili waweze kuingia katika mpango wa Kanzi Data inayolenga kuhifadhi taarifa za wasanii na kuinua maslahi ya tasnia kupitia tuzo na mashindano mbalimbali yatakayoandaliwa.

Rai hiyo imetolewa na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Harrison Mwakyembe wakati wa kusaini mkataba wa kanzi data itakayohifadhi taarifa za wasanii wa filamu kati ya Kampuni ya Cogsnet na Shirikisho la Filamu leo Jijini Dar es Salaam.

“Ni wajibu wetu kuhamasisha wadau wa tasnia ya filamu kuingia katika mfumo wa kanzi data kwani mpango huu umedhamiria kuboresha na kuendeleza maslahi ya tasnia ya filamu na kuleta maendeleo ya msanii mmoja mmoja” amesema Mhe. Mwakyembe

Awali Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fissoo amesema kuwa tasnia ya filamu imekua ikikosa fursa nyingi kutokana na wadau kutokua katika kanzi data inayowatambua vizuri hivyo ujio wa kanzi data hii utakua mkombozi kwa tasnia.

Bibi. Fissoo amesema kuwa suala la kanzi data limilikiwe na wadau wote kwa kupata uelewa na kila litakalofanyika katika kanzi data hiyo lifanywe kwa maslahi ya sekta ya filamu kwani filamu ni uchumi, filamu ni ajira na filamu ni kwa maendeleo endelevu.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kampuni ya Cogsnet Bw. Nkundwe Moses Mwasaga amesema kuwa kampuni yake inaingia mkataba wa kuunda kanzi data ya wanatasnia ya filamu na shirikisho la filamu kwa ajili ya kuongeza msukumo wa kuifanya tasnia ya filamu kukua na kuendelea kwa kasi zaidi.Aidha Bw. Mwasaga amesema kuwa kanzi data hiyo itasaidia kujua mapato yanayopatikana kupitia kazi za filamu lakini pia namna tasnia ya filamu inavyochangia katika pato la taifa.

Naye Rais wa Shirikisho la Filamu Bw. Simon Mwakifwamba amesema kuwa mchakato wa kufanikisha kanzi data itakayohifadhi taarifa za wanatasnia ya filamu unahitaji wanachama wasiopungua laki tano kwa kuanzia, na wanachama hao ni lazima wawe ndani ya vyama vilivyopo chini ya shirikisho la filamu huku kila mwanachama atakayekuwepo katika kanzi data hiyo atatakiwa kuchangia shilingi elfu moja kwa kila mwezi.

Serikali kutoa leseni kwa hospitali na vituo vya afya vya Umma vitakavyokidhi vigezo vya ubora


Naibu Waziri Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt.Faustine Ndugulile(katikati)akiongea na Viongozi na Watendaji wa Afya Afya Mkoa na Wilaya ya Mtwara wakati wa zoezi la kutoa ngao na vyeti kwa vituo vya afya vilivyo na ubora wa huduma za afya.Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe.Evod Mmanda na kulia ni Mganga Mkuu wa Mkoa Dkt.Wedson Sichalwe
Mkuu wa Wilaya MHE.Evod Mmanda akiongea wakati wa mkutano huo
Mkurugenzi wa Idara ya Ubora na Uhakiki wa Huduma za Afya toka Wizara ya Afya Dkt.Mohamed Mohamed akielezea tathimini ilivyofanyika katika Mkoa huo mwaka 2016 na Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu Kuibuka mshindi kwa kupata ngao na cheti
Dkt.Ndugulile akimkabidhi Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu Dkt.Furaha Mwakafyila Ngao baada ya kuibuka mshindi wa Huduma za afya katika vituo vya afya
Afisa Tawala wa Wilaya ya Nanyumbu Salumu Palango akimpongeza Kaimu Mganga Mkuu wake baada ya kupokea ngao


Naibu Waziri akimpongeza Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu baada ya kuibuka mshindi.Dkt.Ndugulile aliipongeza Wilaya hiyo kwa mpangilio mzuri wa utoaji huduma pamoja na utunzaji wa kumbukumbu kwenye stoo ya dawa katika kituo cha afya cha Mtambaswala ambacho kimeanza miezi miwili iliyopita lakini kimeonyesha ufanisi wa hali ya juu.
Picha ya pamoja mara baada ya Naibu Waziri kutoa ngao na vyeti kwa washindi kwa Mkoa wa Mtwara
Dkt.Ndugulile akisoma taarifa ya dawa katika Zahanati ya Ziwani iliyopo Manispaa ya Mtwara,ambapo Naibu Waziri huyo alichukizwa hali ya miundombinu na uwajibikaji wa Zahanati hiyo na kuwapa miezi miwili wawe wamefanya marekebisho kama walivyoelekezwa.
Mkuu wa Zahanati ya Shangani akipokea cheti kutoka kwa Naibu Waziri wa Afya



Serikali inatarajia kutoa leseni kwa hospitali na vituo vya afya vya Umma vitakavyokidhi vigezo vya ubora wa kutoa huduma za afya ili mwananchi wajue kituo atakachoenda kina ubora gani wa huduma hivyo nchini

Hayo yamesemwa jana na Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt.Faustine Ndugulile wakati akiongea na Viongozi na Watendaji wa afya wa Mkoa na Wilaya zake kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara wakati wa zoezi la kutoa ngao kwa wilaya iliyofanya vizuri na vituo vya afya vilivyofanya vizuri wakati wa zoezi la tathimini ya kutoa nyota kwa vituo vya kutolea huduma za afya.

Dkt.Ndugulile alisema hivi sasa serikali inasisitiza kuweka ubora wa huduma za afya katika vituo vyote vya afya vya umma ili kukidhi ubora unaotakiwa wa kutoa huduma kwa wananchi”tunakwenda mbali zaidi usipokuwa na vigezo hospitali yako na kituo chako hutopewa leseni”

Hata hivyo amewataka wale wote waliopewa maelekezo ya nini wafanye basi viongozi wawajibike kwa kurekebisha changamoto zilizopo na wasingoje idara ya uhakiki ubora kutoka wizarani waje kukagua kwani Lengo liliowekwa na wizara ni kila kituo cha afya kupata nyota tatu hadi kufikia mwezi juni mwakani.

“Nyinyi wengine wote hamkustahili kupata cheti hata kimoja hapa,Mkoa wa Mtwara asilimia 3 za vituo vyenu vina nyota mbili na asilimia 51 vina nyota moja na zaidi ya nusu mna nyota 1 na asilimia 46 mna nyota sifuri hali ya utoa huduma bado”Nimetoka hapo zahanati ya Ziwani,kwakweli hapana,ubora wa kutoa huduma pale hapana wakati mpo mjini.

Kwa upande mwingine amewataka kamati za afya ngazi ya Mkoa na Wilaya kufanya kazi na kusimamia katika kuyafanyia kazi maelekezo yote waliyopatiwa kwani maboresho mengine hayahitaji fedha hivyo kamati hizo zitimize wajibu wao”Niwaombe mbadilike kwani mambo madogo madogo yatakuja kuwagharimu hivyo msimamie hali ya utoaji wa ubora na huduma za afya kwa mkoa wa mtwara ni mbaya,nikirudi wakati mwingine sitoongea kirafiki hivi”alisisitiza

Aidha,aliwataka watendaji hao kubadilika katika utendaji wao na hivyo kusimamia upatikanaji wa dawa katika vituo vyao vya afya ili kusiwepo na malalamiko kutoka kwa wananchi kwamba wamekosa dawa

“Dhama imebadilika,hivyo kila mmoja awajibike,awamu hii ni nyingine,hatutaki kusikia dawa hakuna na mwananchi analalamika amekosa dawa kwenye kituo cha afya,Mhe.Rais anaipenda sekta ya afya na ameongeza bajeti ya dawa na anatoa pesa zote,sitaki kusikia dawa hakuna na Wilaya itakayoshindwa basi viongozi wake nao hawatoshi”aliongeza Naibu Waziri

Naye Mkurugenzi wa Idara ya Uhakiki Ubora toka Wizara ya afya Dkt. Mohamed Mohamed alisema wizara ilingia kwenye mpango wa kuboresha huduma kwenye vituo vinavyotoa huduma za afya ya Msingi mwaka 2014 kwa kuhusisha kufanya tathimini vituo vyote vya afya nchini na kuvipa kategoria ya nyota moja hadi tano ikiwemo wa kuandaa mipango ya kuimarisha ubora katika vituo hivyo.

“Tathimini ya awali ilifanyika katika vituo vyote vya kutolea huduma za afya ya msingi nchini mwaka Aprili,2015 na Desemba 2016”

Alitaja maeneo yaliyoangaliwa na kufanyiwa tathimini ni uendeshaji wa vituo ,utendaji wa wafanyakazi,uwajibikaji,miundombinu ya kituo,mkataba kwa mteja pamoja na mazingira salama ya kutolea huduma na ubora wa huduma wenyewe.

Jumla ya vituo 6997 vilifanyiwa tathimini nchini na katika Mkoa wa Mtwara tathimini ya awali ilifanyika mwezi mei 2016 na vituo 221 vilifanyiwa tathimini na matokeo ya awali yalikua vituo 6 vilipata nyota 2(3%),vituo 112 vilipata nyota 1(51%) na vituo 103 vilipata nyota 0(47%).

Katika zoezi hilo Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu iliibuka mshindi kwa kupata ngao,na kituo cha afya Nanyumbu kilipata cheti.Kituo kingine cha afya kilichopaya cheti ni kituo cha Nagaga cha Masasi pamoja na za zahanati ya Nanjota na Nambaya zote za Halmashauri ya Masasi zilifanya vizuri.Pia zahanati ya Shangani ya halmashauri ya Manispaa ya Mtwara ilipata cheti

Wanachama wa Shirikisho la waganga wa Tiba Asili Tanzania (SHIVYATIATA)wawajia juu viongozi wao


BAADHI ya wanachama wa Shirikisho la waganga wa Tiba Asili Tanzania (SHIVYATIATA) wamewajia juu viongozi wa Shirikisho huku wakihoji uhalali wao wa kuendelea kufanya kazi.

Wamesema kuwa viongozi hao muda wao wa kuongoza ulishapita na wanachama walishatoa msimamo wa kuwataka kujiudhuru ili kupisha kufanyika kwa uchaguzi mwaka kesho.

Akizungumza kwa niaba ya wezake mmoja wa wanachama hao Rajabu Hassan amesema wamepata taarifa kwamba kuna baadhi ya viongozi wa shirikisho hilo wamekwenda mjini Dodoma kusimamia uchaguzi wa shirikisho vyama kwa ngazi ya mkoa kinyume cha taratibu.

Amesema maamuzi ya Halmashauri kuu ya shirikisho hilo ilikuwa kuwa chaguzi zote ambazo zitafanyika ngazi za wilaya na mikoa zisimamiwe na wajumbe wa halmashauri kuu na si viongozi wakuu na hiyo nikutokana wao walipewa kuendesha shirikisho kwa muda ambapo muda wao umekwisha kimsingi.

“unajuwa ndugu mwandishi kimsingi viongoza hawa hawana Sifa na kinachosubiliwa na mkutano mkuu na Hata hivyo mwenyekiti anakwenda yeye pekee yake kinyume na katiba kwani kila kitu anakwenda kufanya yeye. “Amesema Hassan

Nakuongeza kuwa pia mwenyekiti huyo amekuwa mbabe kwani ikitokea mwanachama anahoji jambo basi anatishia kumfutia uwanachama pamoja na kumuondoa kwenye makundi yao ya mawasiliano.

Naye mwanachama mwingine kwa sharti la kutotaja jina lake amesema wanajuwa mchezo unaofanyika na viongozi hao nikutaka kujitengenezea mazingira ya kuchaguliwa katika mkutano mkuu ujao uliopangwa kufanyika ndani ya shirikisho hilo mwakani.

Mmoja wa wataalamu wa Tiba hiyo ya dawa asili nchini akizungumzia hatua ya viongozi hao kuendelea kufanya kazi amesema kimsingi hadi sasa hakuna shirikisho na linasemewa mtaani tu.

” Kisheria hakuna chombo kinachoitwa shirikisho kwani uhalali wake ulishapita na hata kinachofanyika ndani ya shirikisho kwa sasa ni batili. “amesema.

Kwaupande wake Mwenyekiti wa Baraza la Tiba asili nchini Richrd Kayombo amesema mambo yanayoendelea ndani ya shirikisho hilo ni ya kwao wao kama Baraza wanafanya kazi na mganga mmoja mmoja.

Awali waliwataka watengeneze chombo kitakachowazungumzia mambo yao lakini mambo yanayofanyika wanajuwa wenyewe.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa shirikisho hilo Abdallahman Lutenga amewataka wanachama wake kutambua kuwa shirikisho ni mahala patakatifu hakuna mchwa wala nani atakayeingia hapo.

Amesem yeye anamamlaka ya kusimamia chaguzi kwani ndio rais wa shirikisho lakini ndio anaye teua na kuitisha mikutano ya shirikisho hilo.

” Nataka nikuambie kwanza wakati mwingine muwe mnauliza kwanza huko chini kabla ya kuja kwangu kwani mimi ni kiongozi mkubwa na nina kazi nyingi na anatambulika na Serikali. “amesema





Hassan Rajabu mmoja mwanachama wa shirikisho la vyama vya waganga wa tiba asili Tanzani.

CHUO KIKUU MZUMBE CHAZINDUA RIPOTI YA UTAFITI JUU YA KILIMO CHA MKATABA KUELEKEA UCHUMI WA VIWANDA





Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Prof. Joseph Buchweishaija, akisaini kitabu cha wageni alipowasili Chuo Kikuu Mzumbe mkoani Morogoro Novemba 24, 2017.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Prof. Lughano Kusiluka (katikati), akiongozana na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Prof. Joseph Buchweishaija (kushoto) pamoja na Mratibu wa Mradi wa POLICOFA, Prof. Joseph Kuzilwa (kulia).

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Prof. Joseph Buchweishaija, akizungumza wakati wa uzinduzi wa Ripoti ya Utafiti Juu ya Fursa na Changamoto za Kilimo cha Mkataba uliofanyika chuoni hapo mkoani Morogoro Novemba 24, 2017. 
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Prof. Lughano Kusiluka, akizungumza wakati wa uzinduzi wa Ripoti ya Utafiti Juu ya Fursa na Changamoto za Kilimo cha Mkataba uliofanyika chuoni hapo mkoani Morogoro Novemba 24, 2017. Kulia niKaimu Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma, Dk. Hawa Tundu. 

Baadhi ya washiriki.


Baadhi ya wanachuo.
Mratibu wa Mradi wa Utafiti wa POLICOFA, Prof. Joseph Kuzilwa akitoa mada wakati wa uzinduzi wa Ripoti ya Utafiti Juu ya Fursa na Changamoto za Kilimo cha Mkataba uliofanyika chuoni hapo mkoani Morogoro Novemba 24, 2017.
Washiriki. 

Mratibu wa Mradi wa Utafiti wa POLICOFA, Prof. Joseph Kuzilwa akitoa mada wakati wa uzinduzi wa Ripoti ya Utafiti Juu ya Fursa na Changamoto za Kilimo cha Mkataba uliofanyika chuoni hapo mkoani Morogoro Novemba 24, 2017.

Mnufaika wa Mradi wa POLICOFA,  Edward Makoye, akitoa mada juu ya utafiti anaofanya kuhusu zao la Tumbaku.

Mmoja wa wanufaika na Mradi wa POLICOFA anayesomea PHD Chuo Kikuu Mzumbe, Anne Mwakibete, akitoa mada juu ya utafiti anaofanya katika kilimo cha Miwa Kilombero. 
Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa Chuo Kikuu Mzumbe, Sylvia Lupembe, akizungumza wakati wa uzinduzi wa Ripoti ya Utafiti Juu ya Fursa na Changamoto za Kilimo cha Mkataba.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Prof. Joseph Buchweishaija, akikata utepe wakati wa uzinduzi wa Ripoti ya Utafiti Juu ya Fursa na Changamoto za Kilimo cha Mkataba uliofanyika chuoni hapo mkoani Morogoro Novemba 24, 2017. Katikati ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Prof. Lughano Kusiluka.
aibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Prof. Joseph Buchweishaija, akionyesha nakala ya kitabu cha ripoti ya utafiti juu ya fursa na changamoto za kilimo cha mkataba. Kulia ni Mratibu wa Mradi Prof. Joseph Kuzilwa na Katikati ni Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma, Kaimu Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma, Dk. Hawa Tundui.

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Prof. Lughano Kusiluka (kushoto), akimkabidhi Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Prof. Joseph Buchweishaija, nakala ya kitabu cha ripoti ya utafiti juu ya fursa na changamoto za kilimo cha mkataba wakati wa hafla ya uzinduzi wa ripo hiyo. 

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Prof. Joseph Buchweishaija (wa pili kulia), Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Prof. Lughano Kusiluka (wa pili kushoto), Kaimu Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma, Dk. Hawa Tundui (kulia) na kushoto ni Kaimu Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Utawala na Fedha, Dk. Nsubiri Isaga. 

Mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Prof. Joseph Buchweishaija (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa chuo pamoja na watafiti.

Mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Prof. Joseph Buchweishaija (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa chuo pamoja na wahadhiri wa chuo hicho.

Nini siri ya vigogo kuhama vyama vyao?

Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis
Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi (kulia) akizungumza katika mkutano na wahariri wa vyombo vya habari nchini, Dar es Salaam hivi karibuni. Picha ya Maktaba 
Habari kubwa wiki hii ni kuhama vyama kwa baadhi ya waliokuwa vigogo wa vyama vya upinzani na kuhamia chama tawala, CCM. Vyama vilivyoathirika zaidi ni Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na ACT – Wazalendo.
Vigogo waliohamia CCM na kutangaza uamuzi wao katika kikao cha Halmashauri Kuu (NEC) ya chama hicho ni pamoja na aliyekuwa Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Chadema (Bavicha), Patrobas Katambi na Waziri wa zamani wa Mambo ya Ndani, Lawrence Masha.
Wengine walitoka ACT – Wazalendo, ni aliyekuwa mshauri wa chama hicho (sasa ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji), Profesa Kitila Mkumbo; aliyekuwa Katibu Mkuu, Samson Mwigamba, Mshauri wa Sheria, Albert Msando na aliyekuwa Mjumbe wa Kamati Kuu, Edna Sanga.
Siku hiyo pia, Rais Magufuli alitangaza kumsamehe kwa aliyekuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake (UWT) na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Sophia Simba. Sophia alifukuzwa uanachama kwa madai ya kukisaliti katika Uchaguzi Mkuu wa 2015.
Hatua hii ya vigogo hao kuhama vyama vyao imekuja wakati tukielekea katika uchaguzi mdogo wa madiwani kujaza nafasi 43 kwenye halmashauri tofauti 36 zilizobaki wazi kwa sababu mbalimbali. Wengi wanaona kuwa usajili huu mkubwa ni njia ya kuongezea nguvu kampeni ya CCM katika uchaguzi huu.
Wengine wanasema labda hiki ni kisasi cha CCM dhidi ya upinzani uliofanikiwa kumpata Waziri wa zamani wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu ambaye pia alikuwa mbunge wa Singida Kaskazini aliyejiondoa kwenye chama hicho.
Vyama vijiulize
Ni rahisi sana kupuuza waliohama na kudai wana njaa, wana tamaa na kadhalika. Inawezekana kuwa ni kweli, lakini inawezekana hoja walizozitoa dhidi ya vyama vyao vya upinzani pia zina uzito wake na hazingefaa kupuuzwa.
Ufuatiliaji wangu katika uendeshaji wa vyama, nimegundua jambo moja, wanaohama CCM mara nyingi ni kwa sababu ya udhaifu wa sera na utekelezaji wa sera hizo; lakini kwa upande wa upinzani wengi wanaovihama vyama hivyo ni kwa sababu ya muundo na uendeshaji wenyewe wa vyama, usiotoa fursa kwa watu wapya kupenya nafasi za juu.
Kwa vyama vya upinzani, inaonekana kuna genge la wachache ambao ndio huamua kati yao nani ashike madaraka, badala ya kuachia demokrasia ifanye kazi. Mwaka 2015 na miaka yote ya kupokezana vijiti vya urais, ndani ya CCM kumekuwa na kinyang’anyiro cha kupigania tiketi ya urais kupitia mchakato mzuri na shirikishi katika vikao mbalimbali vya chama, hadi kufikia mkutano mkuu.
Watu huchujwa kwa vigezo vya kimaadili vinavyojulikana. Ni michakato kama hii ndiyo inayotoa fursa kwa akina Magufuli waliokuwa nje ya waliotarajiwa kupata madaraka.
Nimeandika sana hili na sitaacha kuliandika, kwamba, umefika wakati sasa vyama vya upinzani viboreshe demokrasia ya ndani ya vyama vyao, na waache kufikiria kuwa wachache miongoni mwao ndio wanaojua nani anafaa kuwa kiongozi mkuu.
Suala la ajenda pia ni la kuzingatiwa, kama ambavyo liliibuliwa na David Kafulila ambaye pia amehama Chadema. Yeye anaamini vyama vya upinzani vimehama katika ajenda ya kupambana na ufisadi. Mimi naamini ufisadi ungalipo, ila umebadilika sura yake tu.
Hivyo basi, vyama vya upinzani vinapaswa kuendelea na kupambana na ufisadi uliochukua sura mpya katika awamu hii.
Ufisadi mpya katika awamu ya tano unaweza kuuona katika ukiukwaji wa sheria na maadili ya kiuongozi kwa baadhi ya maofisa wa umma, kwa kisingizio cha maslahi ya umma, taifa na kadhalika pamoja na undumilakuwili (double standard) katika kuchukua hatua mbalimbali.
Kuhama haki ya kiraia lakini...
Kuhama chama, kimsingi, ni haki ya kiraia. Kama ambavyo, mtu ana haki ya kujiunga na chama, pia anayo haki ya kujitoa. Hakuna kulazimishana. Hata hivyo, chama kimoja kinapotumia faida ya kuwa madarakani na uwezo wa kifedha ‘kuhamasisha’ walio katika vyama vingine kuhama, hapo pana tatizo.
‘Uhamasishaji’ wa kumfanya mtu ahame unaweza kufanyika kwa namna mbili, uhamasishaji chanya na uhamasishaji hasi.
Uhamasishaji chanya ni kumhonga mtu ama kwa pesa au cheo. Mfano wake ni kama zile tuhuma zilizowahi kutolewa na chama kimoja cha upinzani, na kufikishwa Takukuru, kuwa madiwani wao walihongwa pesa au kuahidiwa ajira ili wajiuzulu nafasi zao. Uhamasishaji hasi ni pale chama kimoja kinapotumia vitisho dhidi ya ‘uwekezaji’ au ‘biashara’ ya mtu.
Kama hamahama hii inayoendelea inatokana na mapenzi yao, kwa hiari yao, bila ushawisho wa kihalifu au mbinyo wowote, hakuna tatizo. Lakini tukumbuke kuwa, kumekuwa na tuhuma za rushwa katika kuchochea wanasiasa kuhama vyama, huku wengine wakidhaniwa kuwa wametishwa na hali inavyoendelea. Kama ni kweli, basi uhamaji huu wa vigogo, unaweza kudhoofisha demokrasia na siasa za ushindani.
Hakuna ushahidi wa moja kwa moja uliothibitika katika mahakama unaoonyesha kuwa kulikuwa na uhongaji wa vigogo waliohama karibuni au wale madiwani waliojiuzulu, lakini ushahidi wa mazingira ya jumla ya siasa za Tanzania katika awamu hii unaweza kushawishi watu kuamini kuwa kuhama huku siyo kwa kutaka bali ni kukidhi maslahi binafsi.
Si siri kuwa wapinzani katika awamu ya tano wapo katika mazingira magumu. Licha ya vikwazo vingi katika ufanyaji siasa, wengi wamejikuta wakikamatwa na kufunguliwa mashtaka mbalimbali ya uchochezi na mengineyo. Kwa ujumla, mazingira si rafiki kwa siasa za upinzani.
Ni hoja yangu kuwa, kama Serikali inaona haja na umuhimu wa kuwa na siasa za ushindani, ni bora iangalie upya mazingira inayoyajenga ya ufanyaji siasa. Ama la, kama imeonekana, siasa za ushindani hazina umuhimu tena, tunaweza kuendelea katika hali hii na hakika upinzani utadhoofika na karibuni tunaweza wote tukawa CCM.
Kwa dhana ile ya kuwa waliohama walibinywa wakashindwa kuvumilia na hivyo kuamua kujisalimisha, kuna baadhi ya watu wanawalaumu hao waliohama na kujisalimisha kuwa ni wajinga na waoga.
Ninachoamini mimi ni kuwa, ikiwa Serikali inataka kweli kuua upinzani, inaweza kwa sababu ukweli ni kwamba kila chuma kina kiwango chake cha kuyeyuka, kadhalika sisi binadamu. Kuna mahali tukifikishwa, tunakubali yaishe.
Katika maisha, kuna mambo muhimu kuliko chama, kama familia kwa mfano. Kama kuna jambo unafanyiwa ambalo linaenda kuathiri familia yako, unawezaje kuitoa kafara eti ili tu kuthibitisha uzalendo wako kwa chama.
Hoja yangu ni kwamba, kama kuna mbinyo usio wa haki, tusiwalaumu waliohama vyama, bali chama tawala na Serikali yake. Uhai wa upinzani unategemea sana dhamira nzuri ya Serikali.
Wanasiasa vigeugeu
Kuhama chama ni haki ya mtu, lakini kuna gharama kubwa kwa hao wahamaji. Na hapa zaidi nazungumzia zaidi aina ya wahamaji sugu – kama Kafulila, Masha, Kitila n.k- ambao hutoka chama A, akaenda chama B kisha akarudi chama A.
Ukihama vyama kwa aina hii, kuna namna ambayo watu wanaweza kukutazama – kama vile mtu asiyeaminika, muongo, mnafiki, anayeangalia tumbo lake zaidi asiye na msimamo, anayeyumba, asiye tayari kupambana na changamoto bali huzikimbia.
Hata wale wahamaji wa mara moja akina Katambi na Msando nao wanatia shaka ukizingatia matamshi yao ya ukosoaji dhidi ya CCM, tena siyo ya zamani bali ukosoaji dhidi ya Serikali ya awamu hii ya sasa. Katika muktadha mpana uhamaji huu wa wanasiasa kutoka chama kimoja hadi kingine, unatupa picha juu ya ‘tasnia’ ya siasa na hali ya wanasiasa.
Wanasiasa wetu, wanaweza kukwambia jambo moja asubuhi lakini mchana akatoa lugha tofauti kabisa. Hali hii inakufanya ujiulize, wanaposimama majukwaani wanamaanisha wanachokisema au tuwazingatie kama wana tasnia wenzao- wa Bongo Movie,

Vigogo CCM waibuka dakika za lala salama

Mgombea Udiwani wa Kata ya Nangwa Wilaya ya
Mgombea Udiwani wa Kata ya Nangwa Wilaya ya Hanang’, Mkoani Manyara kwa tiketi ya CCM, Portajia Baynit akiomba kura kwa wananchi wa kata hiyo katika kampeni ziliyofanyika Kijiji cha Nangwa hivi karibuni. Picha ya Maktaba 
Dar es Salaam. Wakati kampeni za uchaguzi mdogo wa madiwani katika kata 43 nchini zinamalizika leo wananchi katika kata hizo kesho watawachagua madiwani wao baada ya kushuhudia mpambano mkali katika dakika za lala salama.
Tofauti na kampeni za miaka mingine ambapo vyama vya siasa vilikuwa vikichuana tangu Tume ya Uchaguzi (NEC) inapopuliza kipenga kuashiria kuanza kwa kampeni, safari hii hali imekuwa tofauti; Awali chama tawala kilionyesha kusuasua huku vyama vya upinzani vikiwekeza nguvu zaidi tangu mwanzo.
Tangu NEC ilipotangaza kuanza kwa kampeni za uchaguzi huo mdogo viongozi wa juu wa vyama vya upinzani, hasa Chadema na ACT wamekuwa wakionekana katika majukwaa hayo huku CCM wakificha silaha zao.
Lakini mara baada ya mikutano juu ya CCM – Kamati Kuu (CC) na Halmashauri Kuu Taifa (NEC) iliyomalizika mwanzoni mwa wiki, vigogo wa chama hicho, bila shaka baada ya kupokea tathmini ya kampeni hizo, walianza kuonekana katika majukwaa wakiwanadi wagombea.
Hali hii imeongeza chachu kwenye kampeni hizo na kuamsha ushindani katika siku za mwisho.
Chadema ilivyotumia fursa
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na viongozi wengine wa chama hicho kwa zaidi ya wiki tatu mfulululizo walipita katika mikoa mbalimbali ambako uchaguzi wa marudio unafanyika.
Mbali na Mbowe, wengine waliokuwa katika misafara ya kampeni za chama hicho ni pamoja na Mawaziri wakuu wa zamani, Edward Lowassa na Frederick Sumaye, Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Vincent Mashinji, Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na mambo ya Nje, John Mrema, wajumbe wa Kamati, Baraza Kuu pamoja na wabunge wa chama hicho.
Pengine chama hicho kiliona kiu ya wananchi ambayo walikosa mikutano ya kisiasa muda mrefu na kuonekana kutamani kusikia kinachoendelea kwenye ulingo wa siasa za mageuzi nchini, hivyo kuamua kuitumia fursa hiyo kikamilifu kwa kutuma viongozi wazito.
Hili lilijidhihirisha katika msafara wa kampeni za chama hicho kutokana na wananchi wengi kujitokeza kwenye mikutano hiyo na kusababisha misafara mirefu ya pikipiki, baiskeli na wengine kujipanga kandokando ya barabara wakiwalaki viongozi wa chama hicho.
Hata hivyo, hatua hiyo ilionyesha wazi kuwapa wakati mgumu polisi na kutumia mabomu ya machozi katika baadhi ya maeneo kama jijini Mwanza na Moshi kuwatawanya mashabiki waliojitokeza kuwalaki viongozi wa kuu wa chama hicho.
Mbowe aliwahi kunukuliwa na gazeti hili akisema mikutano hiyo ya uchaguzi ina umuhimu mkubwa tofauti na ya hadhara huku mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu alituma salamu kutokea Hospitali ya Nairobi, ambako anatibiwa baada ya kushambuliwa kwa risasi mjini Dodoma Septemba 7, akitaka wananchi kutumia nafasi hiyo kutoipigia kura CCM.
Akizungumzia hilo, Mkurugenzi wa Itifaki, mawasiliano na mambo ya nje wa chama hicho, John Mrema anasema kwa muda wa miaka miwili viongozi wa chama hicho walishindwa kuongea na wananchi hivyo chama kiliona ni fursa ya kipekee kuwafikia.
“Haikuwa mikutano tu ya kata pekee tulitumia mikutano hiyo kuzungumza na Taifa, tulitumia fursa vizuri ndiyo maana leo sasa kila mmoja anajua kinachoendelea.”
Anasema kuwa pia walitumia fursa hiyo kuwaleza wananchi ahadi ambazo ziliahidiwa na Rais John Magufuli, mfano ile ya Sh50 milioni kwa kila kijiji ili wajue Serikali yao imeshindwa kutekeleza ahadi zake.
Anaongeza kuwa kwa kuwatumia viongozi wake wakuu wamepata manufaa makubwa na wanaamini itachochea ushindi katika uchaguzi huo.
“Leo tunashuhudia hata wenzetu wamezinduka, wakati tunaanza waliona kama hili haliwahusu lakini sasa unasikia Lukuvi yupo mkoa huu na Kinana yupo Arusha,” anasema.
ACT-Wazalendo hawakuwa nyuma
Kama ilivyokuwa kwa Chadema, Kiongozi wa Chama hicho, Zitto Kabwe hakuwa nyuma, alitumia kampeni hizo kukinadi chama chake katika mikoa mbalimbali kuhakikisha anatoa fursa ya kuzungumza na wananchi kuhusu hoja mbalimbali za kitaifa.
CCM waibuka
Hata hivyo, hali ilikuwa tofauti kwa CCM ambayo katika kipindi chote ilionekana kutumia vigogo wake wachache tofauti na miaka iliyopita.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Mwigulu Nchemba na baadaye mbunge wa Mtama, Nape Nnauye ndiyo walionekana katika wiki za kwanza za kampeni katika mikoa ya Dar es Salaam na Mtwara.
Lakini tangu kumalizika kwa vikao vya uongozi vya chama hicho ambavyo pamoja na mambo mengine vilikuwa na jukumu la kufanya tathimini ya uchaguzi huo mdogo, vigogo kadhaa wa chama hicho walianza kuonekana wakiongeza nguvu katika maeneo mbalimbali.
Mara baada ya chama hicho kumsamehe aliyekuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake (UWT), Sophia Simba siku inayofuata alionekana katika kampeni akimnadi mgombea wa chama hicho jijini Dar es Salaam.
Si Simba pekee pia Katibu Mkuu wa chama hicho Abdulrahman Kinana na Nape nao waliibukia katika majukwaa ya kampeni mkoani Arusha wakiongeza nguvu ili kuhakikisha chama chao kinapata ushindi.
Vilevile, kada maarufu na waziri wa zamani, Stephen Wasira na Mwenyekiti wa wazazi anayemaliza muda wake, Abdallah Bulembo pia waliibukia Mwanza.
Wachunguzi wa masuala ya siasa wanasema hatua ya chama hicho tawala kuamua kupeleka vigogo wao katika kampeni dakika za lala salama utakisaidia kukiongezea kura.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kikatoliki Ruaha, Profesa Gaudens Mpangala anasema kipindi cha kampeni ndiyo muda mzuri wa kutumia fursa ya kuzungumza ajenda za chama ili zieleweke kwa wapiga kura.
“Ni fursa nzuri. Wapinzani wameliona hili ndiyo maana wakaamua kutumia nafasi hiyo kupeleka hoja kwa wananchi ili kupinga yale yote yaliyokuwa yakiwaminya ili wananchi waamue.”
Profesa Mpangala anatoa mfano kuwa kwa muda wote wa miaka miwili hakukuwa na usawa katika shughuli za kisiasa nchini kutokana na chama tawala kutumia shughuli za kiserikali kufanya siasa huku upinzani ukikatazwa kufanya hivyo. Hawakuwa na njia nzuri kama wasingetumia nafasi hiyo walioipata katika kampeni.
Alisema mara kadhaa Rais akiwa katika ziara za kiserikali amekuwa akichomekea masuala mbalimbali ya kisiasa. Hakukuwa na usawa hata kidogo kwani walizuiwa kufanya siasa, hivyo fursa waliyoipata wameitumia vyema.
Hata hivyo, Profesa Mpangala anatahadharisha kuihusu mwenendo wa polisi wa kupiga mabomu ya machozi na kuwakamata wapinzani akisema ni kunanyima haki za msingi.
Anasema kipindi cha kampeni wanasiasa waachiwe wafanye kampeni za kistaarabu ili kuweka usawa badala ya kuwatisha kwa kuwakamata.
Hata hivyo, Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dk Benson Bana anasema tafiti mbalimbali zinaonyesha kuwa chaguzi za marudio kwa sehemu nyingi hazina mvuto sana na haziwezi kubadili upepo wa kisiasa nchini.
“Watu wanachagua mbunge au diwani katika kata moja, unawezaje kubadili matokeo ya kata zaidi ya 2,000 zilizokuwepo,” anasisitiza Dk Bana.