Tuesday, September 5

Askari wa FFU akamatwa sakata la utekaji watoto wawili


Arusha.Wakati Mtuhumiwa wa matukio ya utekaji watoto, Samsom Petro (18), ambaye jana alifikishwa Arusha kwa ajili ya kuonyesha sehemu alipowaficha watoto, amebainika kuwa anaishi na kaka yake ambaye ni askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) cha mjini hapa.
Inadaiwa kuwa askari huyo pia anashikiliwa na polisi kwa mahojiano tangu Agosti 27 wakati kikosi maalum cha polisi kilipozingira nyumba aliyopanga.
Petro, ambaye alikamatwa juzi akiwa Katoro mkoani Geita, anatuhumiwa kuwateka watoto wawili, Moureen David(6) na Ikram Salim(3) na hadi jana jioni alikuwa ameandamana na polisi katika eneo la Njiro ambako alidai aliwatelekeza watoto hao.
Akizungumza na Mwananchi, Lina Kajuna ambaye ni mmiliki wa nyumba ya aliyekuwa amepanga askari huyo wa FFU, alisema ana miaka miwili tangu ampangishe.
Kajuna alisema mtuhumiwa wa utekaji, Samson Petro alifika Arusha mwezi Juni na amekuwa akiishi na kaka huyo na tangu amefika amekuwa akimuona kuwa na tabia ambazo sio nzuri, kama wizi wa kuku.
“Alipofika muda mfupi tulianza kuona matukio ya wizi nikaibiwa kuku na pesa mimi nikamlalamikia kaka yake lakini akasema tuendelee kumchunga,”alisema
Alisema baada ya hali ya wizi kuendelea, alikwenda kulalamika kwa balozi wa eneo wanaloishi ambalo ni Mtaa wa Olkeria, Daniel Kichau kutaka wamchunguze.
Hata hivyo, alisema wakati akichunguza, ndio matukio ya utekaji yakaanza na tangu Agosti 25 alitoweka nyumbani hadi jana walipopata taarifa kuwa amekamatwa.
Akizungumzia tukio hilo, mwenyekiti wa Mtaa wa Olkerian, Daudi Safari alisema jana kuwa kikosi chao cha wananchi walifika kwenye nyumba hiyo na kubaini alikuwa anaishi na askari huyo wa FFU .
“Tumemuhoji mama mwenye nyumba ametupa ushirikiano mkubwa na ni kweli Samson alikuwa anaishi kwenye nyumba yake na kaka yake ambaye alikamatwa tangu Agosti 27,” alisema.
Katika msako wa jana, polisi walikwenda peke yao na mtuhumiwa na kuwaacha wazazi wa watoto hao wakiwasubiri kituo kikuu cha polisi. Baadhi ya askari walisema wanaendelea na msako wa watoto hao.

Polisi wamkamata mwanamke aliyetaka kuwania urais Rwanda

Diane Shima Rwigara
Image captionDiane Shima Rwigara alizuiwa kuwania urais
Polisi nchini Rwanda wamesema wanamzuilia mwanasiasa wa upinzani Diane Rwigara, mamake na dadake.
Wiki iliyopita polisi walikuwa wametangaza kuwa mwanasiasa huyo anatuhumiwa kughushi nyaraka wakati alipotaka kuwania urais mapema mwezi wa 8 huku familia yake ikituhumiwa kukwepa kulipa kodi.
Kwa mujibu wa walioshuhudia, polisi wapatao 10 wameingia kwenye makazi anamoishi mwanasiasa huyo na familia yake mtaa wa Kiyovu mjini Kigali na kuruka juu ya lango baada ya kukataliwa kufunguliwa na kumkamata mwanasiasa huyo pamoja na Mamake na dadake.
Duru za polisi zimesema kwamba polisi wameamua kwenda kuwakamata baada yao kukosa kuripoti katika idara ya upelelezi ya polisi CID kwa mara kadhaa.
Juhudi za BBC kumtafuta msemaji wa polisi ili kupata maelezo zaidi hazikufanikiwa.
Wiki iliyopita, polisi wa Rwanda walitangaza kufanya upekuzi katika makazi ya mwanasiasa huyo na kutangaza kwamba ni sehemu ya upelelezi wa mwanzo kuhusu ambayo ni pamoja na kosa la kughushi nyaraka na kukwepa kulipa kodi.
Diane Rwigara alikataliwa kugombea kiti cha urais katika uchaguzi uliofanyika mwezi wa 8 uliopita na baadae akaanzisha vuguguvu la kukosoa utawala wa nchi hiyo.

Upinzani wasusia kuapishwa wabunge wapya CUF


Dodoma. Kambi ya Upinzani Bungeni imesusia kuapishwa kwa wabunge saba wa Viti Maalumu kutoka Chama cha CUF.
Wabunge hao wameapishwa leo Septemba 5 na Spika wa Bunge, Job Ndugai.
Wakati wabunge hao wakitoka ndani ya ukumbi wa Bunge, waliobaki kushuhudia ni wabunge wa CUF, Magdalena Sakaya (Kaliua), Maftah Nachuma (Mtwara Mjini) na Maulid Mtulia (Kinondoni).
Awali, wafuasi wa CUF walifika asubuhi katika viwanja vya Bunge kushuhudia kuapishwa kwa wabunge hao walioteuliwa hivi karibuni na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec).
Wafuasi hao waliambatana na Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki, Habib Mnyaa walifika wakiwa kwenye magari matatu aina ya Toyota Coaster na mengine madogo yaliyokuwa yamebandikwa picha za Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba, anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa.
Wabunge wa Viti Maalumu waliapishwa leo ni Alfredina Kaigi, Kiza Mayeye, Nuru Bafadhili, Rukia Kassim, Shamsia Mtamba, Sonia Magogo na Zainab Amir.
Hindu Mwenda, ambaye angeapishwa leo alifariki dunia Ijumaa Septemba Mosi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na kuzikwa Jumapili Septemba 3.

Kamati ya Bunge, Profesa Mukandala wavurugana kamati ya Bunge

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Udsm), Profesa Rwekaza Mukandala 
Dodoma.Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Udsm), Profesa Rwekaza Mukandala na Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) jana walipishana katika hoja ya watu wanaotakiwa kujibu maswali kuhusu fedha za taasisi hiyo.
Wakati Profesa Mukandala akisema yeye ndiye afisa masuhuri wa taasisi hiyo, PAC ilisema anayetakiwa kuwajibika kwa masuala hayo ni mwenyekiti wa Baraza la Udsm.
Hiyo ilitokea jana baada ya wabunge kubaini kasoro katika taarifa za hesabu za UDSM, hasa ujenzi wa maduka ya Mlimani City na kuhoji sababu za mwenyekiti huyo kutoenda pamoja na uongozi wa chuo mbele ya kamati.
Hata hivyo, PAC ililazimika kuahirisha kikao hicho cha kupitia hesabu za taasisi hiyo baada ya mwenyekiti huyo, Peter Ngumbullu kutohudhuria.
Wabunge pia walihoji sababu za wakuu wa idara kuwakilishwa kwenye kikao hicho.
Baada ya mwenyekiti wa kamati hiyo, Naghenjwa Kaboyoka kutaka kujua sababu za mwenyekiti huyo kutofika, makamu mkuu wa chuo hicho, Profesa Rwekaza Mukandala alisema barua ya wito iliwaelekeza waje na mhasibu, ofisa ugavi na wakuu wengine wa idara ambao anaona watamsaidia kujibu hoja za ukaguzi.
“Kwa hiyo naomba msamaha wako mheshimiwa mwenyekiti. Labda sikuelewa vizuri lakini mimi nilifuata maelekezo ambayo tulikuwa tumepewa,” alisema Profesa Mukandala.
Kutokana na majibu hayo, Kaboyoka alitaka kumjua ofisa masuhuri na kujibiwa na Profesa Mukandala kuwa kwa kawaida ni makamu mkuu wa chuo.
Makamu mwenyekiti wa kamati hiyo, Aeshi Hillaly alisema ni lazima mwenyekiti huyo afike mbele ya kamati hiyo.
“Sijui kama ulikuwa umejipanga. Lakini aliyekuwa anatakiwa kujibu hapa ni ofisa masurufu ambaye ni mwenyekiti. Sasa sijui kama uliamua kuja mwenyewe ili kutukomoa sisi ama ulipata barua yenye maelekezo haya,” alisema Aeshi.
Alisema kikao hicho kisingeweza kuendelea kwa sababu kutokuwepo kwa mwenyekiti wa bodi.
Mbunge wa Nyamagana (CCM), Stanslaus Mabula alihoji sababu za kuwepo watu wanaokaimu na kushauri kuwa siku ya kikao kingine wafike wakuu wa vitengo husika.
Naye Profesa Mukandala aliwahakikishia wabunge hao kuwa katika uongozi wakati amekuwa akitii mamlaka na hasa pale anapoamriwa kufanya jambo kwa maandishi.
“Kwa hiyo nikiri kwamba hata mimi nilishangaa barua haikumtaja mwenyekiti kwa sababu mara zote nilipoitwa na kamati hii, nilikuja na mwenyekiti na hata wakati mwingine nilifikiria kumwambia makamu mwenyekiti,” alisema.
Lakini Kaboyoka alisema:“Mnajua kuwa kuna mambo ambayo hayaendi sawa, sikuona sababu yoyote kwamba mmekuja bila mwenyekiti wa baraza. Mnajua hapo nyuma kuna mambo mengi sana mmekiuka ambayo mlipewa na kamati hii ya Bunge, sijui kama mnajua mamlaka ya kamati hii.
“CAG ndio jicho letu, akileta hapa si ni sehemu ya Bunge kwa sababu tumepewa dhamana ya kupitia na kutoa maelekezo na wahusika wanapaswa kutekeleza.
“Kutokana na hayo tunawapa hadi keshokutwa mje kwenye kamati na mwenyekiti ndio tutaweza kujadiliana.”
Pia Kaboyoka aliagiza maofisa wote watakaofika kesho wawe waliopewa dhamana na si wanaokaimu kama walivyojitambulisha jana.
“Hesabu zenu zimekaa ndivyo sivyo kwa hiyo tunataka kufanyia kazi, kamati ipate muda wa kujikita zaidi siku ya kesho (leo) na kesho kutwa (kesho),” alisema.

Balozi: Nilishuhudia kichwa kikiungua moto kwa mganga


Balozi wa Nyumba 10 katika Kitongoji cha Chang’ombe Kijiji cha Chamwino Ikulu, Simango Asheri amesema alishuhudia mwili wa Mariam Said (17) anayedaiwa kuuawa nyumbani kwa mganga wa kienyeji, Ashura Mkasanga (33) ukiwa utupu, umetenganishwa kichwa na kiwiliwili huku ukiingua moto kichwani.
Mauaji hayo yalitokea Agosti 8 mwaka huu saa 10 usiku, umbali wa kilometa mbili kutoka mahali ilipo Ikulu ya Chamwino mkoani hapa.
Akizungumza nyumbani kwake hivi karibuni Asheri alisema wakati akiwa anafanya shughuli zake za ujenzi nyumbani kwake saa 3 asubuhi alipita mwenyekiti wa tawi la CCM akamweleza kuhusu tukio hilo.
“Akaniambia kuna mtu kafa kwa Malita Mkasanga (Ashura), tukakimbia (kwenda) mwenzangu alikuwa na baiskeli mimi nilikuwa peku, tukafika tukakutana na wazee wamekaa tukakaribishwa nendeni mkaangalie tukio,” anasema.
“Tulipofika ndani tukakuta mtu amelala chali sebuleni kuangalia tukaona moto unaendelea kufuka kichwani, alikuwa hana nguo, tulitoka lakini baada ya muda tuliingia tena kutazama tukakuta shingo imesogezwa kwa kukatwa,” anasema.
Balozi huyo anasema walipomuuliza Ashura ilikuaje hadi mtu huyo akafia nyumbani kwake, aliwaambia kuwa akiwa amelala ndani mtoto wake wa kiume alisikia kelele nje.
“Alituambia kuwa marehemu alipiga mlango na kuingia ndani na kudondoka sebuleni huku moto ukaendelea kuwaka, tuliendelea kumuhoji kama mlango uliokuwa umefungwa aliupiga na kuingia ndani mbona ni mzima haukuvunjika, alijibu hata yeye anashangaa,” anasema.
Alipobanwa na wazee wa kijiji kuhusu ni wapi majivu yaliyokuwa ndani ya nyumba hiyo yalipotokea, aliwajibu kuwa hata yeye anashangaa kwa sababu hajui yalipotoka.
“Alipoulizwa kuhusiana na mchanga uliokuwepo ndani ya nyumba hiyo, pia alijibu anashangaa ulipotokea. Kutokana na majibu hayo tulimwacha tukiwasubiri polisi waje,” anasema.
Asheri anasema kuwa pembeni mwa mwili wa marehemu kulikuwa na lundo la mchanga ambalo baada ya kufukuliwa ilibainika kuwa chini kulikuwa na damu iliyofukiwa.

Uhalali wa kazi ya mganga
Hata hivyo, balozi huyo anapoulizwa iwapo alikuwa anafahamu kuwa Ashura alikuwa mganga wa kienyeji, anasema hafahamu na kwamba watu wanaofanya shughuli hizo kijijini hapo wote wanajulikana.
“Wanasema kuwa ni mganga, lakini mimi tangu amehamia hapa miaka mitano hivi namfahamu kama mkulima na mumewe anafanya kazi katika gari moja la kusombea mchanga huko,” anasema.
Badala yake anasema kuwa Ashura alikuwa akishiriki vizuri shughuli za jamii yake kwa kuchanga michango mbalimbali na  kushiriki kwenye mikutano ya kitongoji na kijiji.

Ndugu wachukua watoto
Mjomba wa mumewe wa mganga huyo ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini, anasema baada ya tukio hilo polisi waliwachukua watu wote waliokuwepo ndani ya nyumba hiyo wakiwemo watoto.
“Lakini baadaye tuliambiwa kuwa watoto wameachiwa wamerudi nyumbani, tukaamua twende tukawachukue ili ndugu wa marehemu wasije wakawadhuru,” anasema.
Anasema watoto hao walipelekwa kwa bibi yao na wataishi huko hadi wazazi wao watakapomaliza matatizo yaliyojitokeza.
“Huyu ndugu yetu awali alikuwa akiishi na dada yangu, lakini walikuwa hawaelewani kwasababu mama yake alikuwa akimwambia aachane naye kwasababu ni mshirikina lakini alikataa,” anasema.
Anaongeza kuwa baada ya muda walinunua shamba na hivyo kuondoka kwa mama yake na kwenda kuanzisha mji wao.
Hata hivyo, mmoja wa watoto wa mganga huyo, (jina tunalihifadhi), anasema kuwa siku ya tukio hakulala nyumbani.
“Niliporudi nyumbani asubuhi ndiyo nilikutana na tukio hilo wala sikufahamu ilikuaje,” anasema mtoto huyo ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha pili katika moja ya shule wilayani humo.

Nyumbani kwa mganga
Mazingira ya nyumba hiyo ambayo ipo umbali wa takriban mita 300 kutoka kwa majirani zake, yamegubikwa na utulivu mkubwa huku milango ikiwa imefungwa.
Nje ya nyumba hiyo iliyojengwa kwa matofali ya udongo kuna kisima kilichochimbwa kienyeji kikiwa na maji machache, mabua ya mtama uliovunwa na pembeni kukiwa na nyumba iliyoanza kujengwa kwa matofali ya saruji.
Inaelezwa kuwa katika nyumba ya jirani kuna mzee anaishi lakini hata hivyo wakati mwandishi wa habari hizi
anafika hakukuwa na mtu.
Hata hivyo, tofauti na matukio mengine hakuna kiongozi wa kijiji hicho cha Chamwino Ikulu aliyekuwa tayari kuelezea tukio hilo kwa sababu mbalimbali.

Waganga wazungumza
Akizungumza hivi karibuni mmoja wa waganga wa tiba asilia mjini hapa, Dk Harun Kifimbo anasema Serikali ihakikishe mipango inayopangwa kudhibiti watu wanaojifanya waganga wa tiba asilia inasimamiwa.
“Tatizo pia liko kwa baadhi ya waratibu wanaotoa vyeti kwa waganga wasiostahili na ndiyo wanaofanya mambo haya ambayo yanaenda kinyume na tiba ya asili,” anasema Kifimbo.
Anasema chama cha waganga wa tiba asili mkoani Dodoma kimepanga kuendesha msako na kuwakamata watu wanaojishughulisha na tiba hizo bila kuwa na leseni, cheti cha kuthibitishwa mahali wanapofanyia kazi zao na dawa zao kutokuwa na usajili kwa mujibu wa sheria.
Hata hivyo, anawalamu baadhi ya waganga kuwa wamekuwa wakijiharibia mambo yao wenyewe kwa kufanya mambo ambayo yanakatazwa kisheria wakati Serikali imewawekea mazingira mazuri ya kufanyia kazi.

Polisi waendelea na uchunguzi
Aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Lazaro Mambosasa ambaye sasa amehamishiwa Dar es Salaam, alisema waliwakamata watuhumiwa 11 na kuwahoji, kati yao watano wanaendelea kuwa chini ya ulinzi.
“Kule Chamwino wanamamlaka ya kuwafikisha mahakamani wakimaliza uchunguzi wao,” anasema.
Mambosasa alisema jumla ya watu 11 walikamatwa katika tukio hilo ambalo Mariam aliuawa kwa kukatwa shingo yake na kutenganishwa na kiwiliwili na kuchomwa moto kichwa chake na kubakia vufu lisiloweza kutambuliwa sura yake.
“Baadhi ya sehemu za mwili wake ziliunguzwa kwa moto ambazo ni mkono wa kushoto, shingo, kifuani na sehemu za siri,” alisema.
Alisema mazingira ya tukio hilo yanaonyesha kuwa mganga huyo asiyekuwa na kibali cha kuendesha shughuli za tiba asili analaza wagonjwa nyumbani kwake, anafanya matambiko, anapiga ramli chonganishi na anafanya tohara.
“Katika nyumba yake alikutwa kalaza watu wanane kati yao wanawake sita na wanaume wawili,” anasema.
Hata hivyo, anasema hakuna maelezo ya kutosha jinsi gani marehemu alifika kijijini hapo kutoka Kigoma na kwamba polisi inafanya uchunguzi zaidi wa tukio hilo.
“Tukio hili halikubaliki hapa Dodoma na mahali popote ni fedheha kubwa sana kwa wanachamwino kuendelea kukumbatia ushirikina katika karne hii na Serikali imesogeza huduma za afya karibu na jamii, lakini bado hawataki kwenda kutibiwa hospitali na kukubali kuuawa kwa fedheha na waganga wachonganishi wa jadi,” anasema.

Manji atinga mahakamani kivingine, hakimu awaonya polisi


Dar es Salaam. Mfanyabiashara Yusuf Manji, anayekabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi, jana alitinga Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akiwa na muonekano mwingine tofauti na wiki chache zilizopita.
Manji alionekana kuwa tofauti kwani alivaa suti nyeusi na kunyoa ndevu tofauti na siku nyingine ambako amekuwa akitinga mahakamani akiwa amevaa fulana nyeusi ya mikono mirefu na suruali ya ‘jeans’ rangi ya bluu huku akiwa na nywele pamoja na ndevu nyingi.
Mbali na kutinga akiwa ‘ametokelezea’ kama msemo wa vijana wa siku hizi, kwa kuvaa suti hiyo sambamba na tai shingoni na viatu vyeusi, mshtakiwa huyo pia alionekana kuwa amechangamka tofauti na siku nyingine.
Manji na wenzake watatu walifikishwa jana mahakamani hapo kwa hati ya kutolewa mahabusu kwa ajili ya kwenda kuhojiwa polisi.
Tayari, Mahakama imeruhusu Manji na wenzake kwenda kuhojiwa na polisi kuhusiana na kesi ya uhujumu uchumi inayowakabili kwa lengo la kukamilisha upelelezi.
Hatua hiyo imekuja baada ya upande wa mashtaka kuieleza mahakama kuwa waliomba hati ya kuwatoa washtakiwa mahabusu ili kufanyiwa mahojiano katika kesi namba 33/2017 na kwamba washtakiwa hao walikabidhiwa mikononi mwa polisi.
Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi alisema aliandikiwa barua na Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam (ZCO), akiomba washtakiwa hao waende wakahojiwe polisi.
Alisema Mahakama imekuwa ikisisitiza kesi za uhujumu uchumi zikamilishwe upelelezi ili ziweze kusikilizwa.
“Tusingeweza kukataa maombi hayo kwa sababu tutapingana na kauli yetu ya kukamilisha upelelezi. Ndiyo maana tumetoa hati ya kuwatoa mahabusu kwa ajili ya mahojiano na hii si mara ya kwanza kuwatoa washtakiwa mahabusu kwa ajili ya upelelezi,” alisema Hakimu Shaidi.
Hakimu Shaidi aliwataka polisi kuzingatia haki za washtakiwa kwa kuhakikisha wanakuwa na afya njema na wapate uhuru wa kuwakilishwa na mawakili wao kwenye jambo lolote na isiwe kificho.
Hakimu aliwakabidhi washtakiwa hao kwa Koplo Dotto kama barua inavyoelekeza kwa kuwa Sajenti Mkombozi ambaye alitakiwa kukabidhiwa hakuwepo. Washtakiwa hao wanatakiwa kurudishwa kesho (leo) katika muda wa kazi.
Mbali na Manji, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Deogratius Kisinda (28), Abdallah Sangey (46) na Thobias Fwere (43).
Akiwasilisha maombi hayo, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Mutalemwa Kishenyi aliomba mahakama iruhusu washtakiwa wakabidhiwe kwa polisi ili kutimiza matakwa ya upelelezi.
Kishenyi alidai kwamba Kifungu cha 59 (1) cha Mwenendo wa Makosa ya Jinai, kinawapa mamlaka polisi kufanya upelelezi.
Akijibu hoja hizo, wakili wa utetezi, Hudson Ndusyepo alidai kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kutoa amri kama ilivyoombwa na upande wa mashtaka kwa sababu shauri hilo halijapata hati ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kuipa mamlaka kusikiliza shauri hilo.
Ndusyepo alidai kuwa mahakama hiyo imefungwa mikono ya kutoa amri dhidi ya maombi hayo.
Pia alidai kifungu cha sheria kilichotajwa na upande wa mashtaka, kinazungumzia ufanyaji wa upelelezi kwa ujumla.
Wakili mwingine wa utetezi, Hajra Mungula alidai kuwa washtakiwa hao wako chini ya ulinzi na kwamba upande wa mashtaka uliwashtaki huku ukijua kwamba haujakamilisha upelelezi na umetoa hati ya kuzuia dhamana.
“Tunaomba ombi hili likataliwe na upande wa mashtaka uelekezwe kuzingatia sheria na haki za washtakiwa,” alisema Mungula.
Hata hivyo, Wakili Kishenyi alisema Mahakama imekuwa ikisisitiza kukamilisha upelelezi na kwamba wanachofanya ni sehemu ya kuukamilisha.
Pia alidai kuwa washtakiwa hao wanayo haki ya kuwakilishwa hivyo maombi yao yakubaliwe.
Hakimu Shaidi alikubaliana na ombi la upande wa mashtaka na kuwaruhusu washtakiwa hao kwenda kuhojiwa.

Marekani yailaumu Korea Kaskazini kwa kuomba vita

Haley amesema teknolojia ya Korea ya Kaskazini kwenye mabomu ya nyukilia ni ya hatari na haina mfano
Image captionHaley amesema teknolojia ya Korea ya Kaskazini kwenye mabomu ya nyukilia ni ya hatari na haina mfano
Balozi wa Marekani kwenye Umoja wa Mataifa ameilaumu Korea ya Kaskazini kwa kulazimisha vita kutokana na majaribio yake ya makombora ya mara kwa mara.
Nikki Haley ametaka kuwepo kwa muda wa dharura wa Baraza la Umoja wa Mataifa utakao jibu majaribio hayo kwa hatua kali.
"Vita sio kitu ambacho Marekani ingetaka," alisema. "Hatutaki vita kwa sasa lakini uvumilivu wa nchi yetu hautuzuii."
Baadae, kupitia mazungumzo ya simu na Rais Trump, Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amesema atahimiza kuwepo kwa vikwazo vikali kutoka umoja wa nchi za ulaya dhidi ya Pyongyang.
Hata hivyo, China imesisitiza wito wake wa kutaka pande zote zirudi katika meza ya mazungumzo.
Baraza la usalama la umoja wa mataifa mara ya mwisho liliweka vikwazo kwa Korea Kaskazini juu ya bidhaa zake mwezi Agosti
Image captionBaraza la usalama la umoja wa mataifa mara ya mwisho liliweka vikwazo kwa Korea Kaskazini juu ya bidhaa zake mwezi Agosti
Ripoti zinasema kuwa Korea Kaskazini inajiandaa kwa majiribio mengie ya makombora.
Siku ya Jumapili ilifanya jaribio la bomu la chini ya ardhi lililoaminika kuwa na nguvu ya kati ya kilotani 20 na 120.
Kifaa hicho hicho kinaweza kuwa na nguvu mara tatu zaidi ya bomu lililotumiwa kuharibu mji wa Hiroshima mwaka 1945.
China haitaki kuwepo nchi yenye silaha za nyuklia ya Korea Kaskazini na mara kwa mara imeeleza msimamo wake kwa nchi hiyo.
Lakini pia haitaki kuona utawala wa Korea Kaskazini ukiondolewa madarakani. Hii itasababisha mamilioni ya wakimbizi kukimbia kwenda China na kuchangia kuungana kwa Korea ambayo itakuwa chini ya ushawishi wa Marekani.

Uchaguzi mpya wa urais Kenya kufanyika Oktoba 17

Wafula ChebukatiHaki miliki ya pichaAFP/GETY
Tume ya Taifa ya uchaguzi nchini Kenya imetangaza kwamba uchaguzi mpya wa urais nchini humo utafanyika tarehe 17 Oktoba.
Mwenyekiti wa tume hiyo Wafula Chebukati amesema uchaguzi huo utashirikisha wagombea wawili pekee wa urais, Rais Uhuru Kenyatta na waziri mkuu wa zamani Raila Odinga.
"Hakutakuwa na uteuzi mpya wa wagombea wa urais katika uchaguzi huo upya. Waliopinga matokeo ya uchaguzi kortini, Bw Raila Odinga na mgombea mwenza wake Stephen Kalonzo Musyoka na mshtakiwa wa tatu Rais Uhuru Kenyatta na mgombea mwenza wake William Samoei Ruto, watakuwa ndio wagombea pekee," taarifa ya bw Chebukati imesema.
Katika kufutilia mbali matokeo ya uchaguzi uliofanyika tarehe 8 Agosti, Mahakama ya Juu iliiwekea lawama Tume ya Uchaguzi
Majaji wa tume hiyo hawakuandaa uchanguzi huo kwa viwango vilivyowekwa kwenye katiba na sheria za uchaguzi, na kwamba kulitokea kasoro nyingi sana katika mchakato wa kupeperusha matokeo.
Rais Uhuru Kenyatta (kushoto) na kiongozi wa upinzani Raila Odinga ndio pekee watawaniaHaki miliki ya pichaAFP/GETTY IMAGES
Image captionRais Uhuru Kenyatta (kushoto) na kiongozi wa upinzani Raila Odinga ndio pekee watawania
Bw Chebukati amesema tume hiyo inafanyia utathmini mifumo na taratibu zake kwa ajili ya uchaguzi huo mpya.
Mwenyekiti huyo hata hivyo ametoa wito kwa Mahakama ya Juu kutoa hukumu ya kina kuhuhusu kesi iliyowasilishwa na Bw Odinga kupinga ushindi wa kenyatta ili kuiwezesha "tume kutambua maeneo ambayo yanahitaji kuboreshwa katika usimamizi wa uchaguzi mpya".
Majaji wa mahakama ya juu waliahidi kutoa hukumu kamili kabla ya tarehe 22 mwezi huu.
Kwa mujibu wa matokeo yaliyotangazwa na IEBC kuhusu uchaguzi uliofanyika tarehe 8 Agosti, Rais Kenyatta alipata kura 8,203,290 huku naye Raila Odinga akipata kura 6,762,224.
Upinzani ulipinga matokeo hayo ukisema mitambo ya tume hiyo ya uchaguzi iliingiliwa kumfaa Bw Kenyatta
IEBC ilikuwa na muda wa hadi tarehe 31 Oktoba kikatiba kuandaa uchaguzi mpya.
Lakini waziri wa elimu alikuwa ameomba tume hiyo kuandaa uchaguzi huo mapema ili kutovuruga mitihani ya kitaifa ya darasa la nane na kidato cha nne ambayo imepangiwa kufanyika kuanzia mwishoni mwa Oktoba.

UDSM matatani mbele ya kamati ya Bunge


Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Udsm) kimeingia matatani baada ya Kamati ya Bunge ya Hesabu Serikali (PAC) kuwakalia kooni kuhusu hesabu zao za mwaka 2015/16.
Hata hivyo, kamati hiyo ililazimika kuahirisha kikao kilichokuwa kikipitia hesabu za chuo hicho hadi kesho baada ya mwenyekiti wa baraza la chuo hicho, Peter Ngumbullu kutofika katika kikao hicho.
Mwenyekiti wa kamati hiyo, Naghenjwa Kaboyoka alimuhoji  makamu mkuu wa chuo hicho, Profesa Rwekaza Mukandala kwanini mwenyekiti wa baraza hilo hayupo.
Akijibu Profesa Mukandala alisema kuwa barua ambayo waliipata ya wito iliwaelekeza waje na mhasibu, ofisa ugavi na wakuu wengine wa idara ambao anaona watamsaidia kujibu hoja za ukaguzi.
"Kwa hiyo naomba msamaha wako mheshimiwa mwenyekiti labda sikuelewa vizuri lakini mimi nilifuata maelekezo ambayo tulikuwa tumepewa,"alisema Profesa Mukandala.
Kufuatia majibu hayo, Kaboyoka alihoji ofisa masuhuri ni nani ambapo Profesa Mukandala alijibu kuwa anachofahamu yeye ndio ofisa masuhuri(Makamu Mkuu wa Chuo).
Hata hivyo makamu mwenyekiti wa kamati hiyo, Aeshi Hillaly alisema ni lazima mwenyekiti huyo kufika kwenye kamati hiyo.
“Sijui kama ulikuwa umejipanga. Lakini aliyekuwa anatakiwa kujibu hapa ni maofisa masurufu ambaye ni mwenyekiti, sasa sijui kama uliamua kuja mwenyewe ili kutukomoa sisi ama ulipata barua yenye maelekezo haya,”alisema Aeshi.
Alisema kikao hicho kisingeweza kuendelea kwa sababu mwenyekiti hayupo.
Mbunge wa Nyamagana (CCM), Stanslaus Mabula alihoji katika utambulisho wa watendaji hao ameona kuna makaimu wengi hivyo ni vyema watakapofika tena kwenye kamati hiyo waje wakuu wa vitengo husika.
Akijibu Profesa Mukandala aliwahakikishia wabunge hao kuwa na kwamba katika utendaji wake wa kazi za kuongoza chuo kikuu hicho amekuwa akitii mamlaka na hasa pale amuamriwa kufanya jambo kwa maandishi.
“Kwa hiyo nikiri kwamba hata mimi nilishangaa barua haikumtaja mwenyekiti kwa sababu mara zote nimeitwa katika kamati hii nimekuja na mwenyekiti na hata wakati mwingine nilifikiria kumwambia makamu mwenyekiti,” alisema.
Hata hivyo, alisema kuwa alipata ujumbe mfupi wa kuwataja watu ambao wanatakiwa kufika mbele ya kamati hiyo.
Baada ya malumbano, Kaboyoka alisema kuwa UDSM wanafahamu kuwa si mara yao ya kwanza kufika katika kikao cha kamati hiyo.
“Mnajua kuwa kuna mambo ambayo hayaendi sawa, sikuona sababu yoyote kwamba mmekuja bila mwenyekiti wa baraza. Mnajua hapo nyuma kuna mambo mengi sana mmekiuka ambayo mlipewa na kamati hii ya Bunge, sijui kama mnajua mamlaka ya kamati hii,”alihoji.
“CAG ndio jicho letu akileta hapa sie ni sehemu ya Bunge kwa sababu tumepewa dhamana ya kukaka kupitia na kutoa maelekezo na wahusika wanapaswa kutekeleza.”
“Kutokana na hayo tunawapa hadi keshokutwa mje kwenye kamati na mwenyekiti ndio tutaweza kujadiliana,”alisema.
Pia Kaboyoka aliagiza kuagiza maofisa wote watakaofika kesho wawe mwenyewe sio makaimu kama walivyofanya jana.
“Hesabu zenu zimekaa ndivyo sivyo kwa hiyo tunataka kufanyia kazi, kamati ipate muda wa kujikita zaidi siku ya kesho (leo) na kesho kutwa (kesho),”alisema.
Miongoni mwa miradi ambayo imeibua hoja nyingi katika ripoti ya ukaguzi wa CAG ni mradi wa ujenzi wa maduka wa Mlimani City, hoja ambazo hazijatolewa majibu na baraza la chuo.

Kampuni zamwagia klabu Sh3.7b


“Tumeamua kuidhamini Mbao FC tukiamini kuwa itafanya vizuri zaidi katika ligi na Ifahamike  kampuni yetu imekuwa na idadi kubwa ya wateja Kanda ya Ziwa inapotoka Mbao hivyo kupitia udhamini huu nadhani tutazidi kujiweka karibu na wateja wetu.” Kulwa Bundala- Ofisa Masoko GF Trucks & Equipments. 
Dar es Salaam. ‘Chema chajiuza…’ ndiyo hali inayoonekana kwa sasa kwa katika Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya klabu nane kuvutia udhamini wa kampuni 13 wenye thamani ya Sh 3.7 bilioni.
 Tofauti na misimu iliyopita ambayo kampuni tano tu ndizo zilikuwa zinadhamini timu za Ligi Kuu kwa kuwekeza kiasi kisichozidi Sh2 bilioni, msimu huu kuna ongezeko la kampuni nane ambazo zimemwaga kiasi hicho cha Sh3.7 bilioni  na kuvunja rekodi ya tangu kuanzishwa kwa ligi hiyo miaka 50 iliyopita.
Fedha hizo za udhamini ni tofauti na udhamini wa jumla wa ligi unaotolewa na kampuni ya mawasiliano ya Vodacom sambamba na ule wa haki za maonyesho ya televisheni wa kampuni ya Azam Media.
Katika kundi hilo la timu nane zilizovutia idadi kubwa ya kampuni kuzidhamini, Singida United inaongoza ikiwa chini ya udhamini wa kampuni sita tofauti na kuingizia  klabu hiyo Sh630 milioni.
Singida United iliyopanda daraja msimu huu, inapata Sh250 milioni kutoka kampuni ya utengenezaji na usambazaji wa mbolea ya Yara na pia inapata kiasi kama hicho kutoka kampuni ya SportPesa.
Kampuni nyingine nne ambazo zimeimwagia fedha Singida United ni Oryx Energy walioipa Sh100 milioni, NMB (Sh.10 milioni), Halotel (Sh10 milioni) na Puma Energy wameipa timu hiyo kiasi cha Sh10 milioni.

Wanaoifuatia Singida United kwa kuvutia idadi kubwa ya wadhamini ni Mbeya City inayoingiza Sh350 milioni kutoka na udhamini wa kampuni tatu ambazo ni Binslum Tyres inayotoa Sh150 milioni kwa mwaka, Coca-Cola (Sh.80 milioni) pamoja na Sports Masters inayoipa Sh120 milioni.
Mbao FC ina udhamini wa jumla wa Sh 165milioni kutoka kampuni mbili, baada ya kusaini mkataba wa mwaka mmoja wenye thamani ya Sh140 milioni kutoka GF Trucks & Equipments pamoja na ule wa zaidi ya Sh25 milioni kutoka Hawaii Products Supplies Limited wazalishaji wa maziwa ya unga ya Cowbell.
Simba na Yanga kila moja inalamba udhamini kutoka SportPesa wakati Azam inapata udhamini wa Benki ya NMB huku Ndanda ikipigwa jeki na kampuni ya Motisum inayojishughulisha na uuzaji wa vifaa vya ujenzi na maji ya kunywa. Lipuli ina udhamini wa kampuni ya ubunifu wa mavazi ya Speshoz.
Hata hivyo licha ya kudhaminiwa na kampuni moja, Yanga na Simba zimekuwa vinara wa kukusanya fedha nyingi za udhamini  kila moja inapata kiasi cha Sh950 milioni kutoka SportPesa, zikifuatiwa na Singida United (Sh 650 milioni) huku Azam wakivuna Sh600 milioni.
Mbeya City wanashika nafasi ya tano wakiwa wanapokea kiasi cha Sh.350 kupitia udhamini wa kampuni za Binslum, Coca-Cola na Sports Masters, wakifuatiwa  na Mbao FC inayovuna Sh. 165 milioni, Ndanda wanavuna zaidi ya Sh100 milioni kwa mwaka huku Lipuli FC wakipata Sh17.5 milioni.
Ofisa habari wa TFF, Alfred Lucas alisema shirikisho hilo litaendelea kutengeneza mazingira mazuri kwa lengo la kuvutia zaidi kampuni kudhamini timu za Ligi Kuu, Ligi Daraja la Kwanza na Ligi Daraja la Pili.
“Kama inavyofahamika kuwa shirikisho limekuwa likifanya juhudi za dhati kuvutia wadhamini, lakini tutakuwa wachoyo wa fadhila iwapo tukishindwa kuwashukuru wadhamini wetu wakuu wa ligi ambao ni Vodacom na Azam Media wamekuwa chachu ya kuvutia wawekezaji wengine kujitokeza na kudhamini klabu.
Bado tunaendelea kukaribisha kampuni kujitokeza kuzidhamini klabu zetu nyingi zinakabiliwa na ukata na kwa kuthibitisha hilo, tumeweka kanuni ambayo inazipa nafasi klabu kuweka matangazo ya wadhamini wao katika mechi zinazocheza viwanja vya nyumbani,” alisema Lucas.
Kanuni hiyo inayosemwa na Lucas ambayo inatoa fursa kwa klabu kumtangaza mdhamini ni ile ya 13 (6) ambayo inafafanua hivi,” Klabu Mwenyeji itakuwa na nafasi ya kuweka hadi mabango 10 ya mdhamini/wadhamini wake.” 
Ofisa masoko wa kampuni ya GF Trucks & Equipments, Kulwa Bundala alisema: “Hii ni mara ya kwanza kwetu kudhamini michezo.
Tumeamua kuidhamini Mbao FC tukiamini kuwa itafanya vizuri zaidi katika ligi. “Ifahamike  kampuni yetu imekuwa na idadi kubwa ya wateja Kanda ya Ziwa inapotoka Mbao hivyo kupitia udhamini huu nadhani tutazidi kujiweka karibu na wateja wetu,” alisema Bundala.
 Mkuu wa idara ya masoko wa kampuni ya Motisun wanaoidhamini Ndanda FC, Edward Mlyansi alisema udhamini wao kwa timu hiyo utanufaisha pande zote mbili.
“Udhamini huu bila shaka utakuwa na faida kwetu sisi kama Motisun pamoja na Ndanda na ndio maana tunawadhamini kwa mwaka mmoja,” alisema Mlyansi.

Polisi 95 waugua Kipindupindu Kenya


Jumla ya Polisi 95 waliokuwa wamepelekwa kuimarisha usalama kuhusu kufutwa kwa uchaguzi wameugua ghafla Kipindupindu.
Mlipuko huo wa Kipindupindu umesababisha polisi hao kulazwa kwenye vituo mbalimbali vya Afya.
Ofisa Utawala wa Hospitali ya Sinai ,Paulo Dullo alidhibitisha kulazwa maofisa 30 huku wengine wakisambazwa kwenye hospitali nyingine.
Mtendaji Mkuu wa Kituo cha Afya Kaunti ya Nairobi,Bernard Muia alisema kwamba jumla ya polisi 95 wamesambazwa kwenye vituo hivyo vilivyopo nchini humo.
Awali ilielezwa kwamba Polisi hao ni miongoni mwa walioongezwa Ijumaa iliyopita,kufuatia hukumu ya Mahakama Kuu ambayo ilitengua matokeo ya Uchaguzi uliofanyika Agosti 8 na kumpa ushindi Uhuru Kenyatta.

The number of police officers who have contracted Cholera in Nairobi has risen by more than 30.
The city county’s Health Chief Executive Bernard Muia on Monday said 95 officers, from 59 on Sunday, had been affected by the disease after eating suspected contaminated food at the Nairobi area Police Canteen.
CANTEEN
The officers from various parts of the country were part of the team deployed to maintain security ahead of Supreme Court judgment on Raila Odinga’s election petition on Friday.
Consequently, the city county has temporarily closed the Nairobi area police canteen.
Speaking at Sinai Hospital where 50 patients are admitted, Dr Muia said they suspected the canteen could have been the source of the outbrea