Tuesday, September 5

Polisi wamkamata mwanamke aliyetaka kuwania urais Rwanda

Diane Shima Rwigara
Image captionDiane Shima Rwigara alizuiwa kuwania urais
Polisi nchini Rwanda wamesema wanamzuilia mwanasiasa wa upinzani Diane Rwigara, mamake na dadake.
Wiki iliyopita polisi walikuwa wametangaza kuwa mwanasiasa huyo anatuhumiwa kughushi nyaraka wakati alipotaka kuwania urais mapema mwezi wa 8 huku familia yake ikituhumiwa kukwepa kulipa kodi.
Kwa mujibu wa walioshuhudia, polisi wapatao 10 wameingia kwenye makazi anamoishi mwanasiasa huyo na familia yake mtaa wa Kiyovu mjini Kigali na kuruka juu ya lango baada ya kukataliwa kufunguliwa na kumkamata mwanasiasa huyo pamoja na Mamake na dadake.
Duru za polisi zimesema kwamba polisi wameamua kwenda kuwakamata baada yao kukosa kuripoti katika idara ya upelelezi ya polisi CID kwa mara kadhaa.
Juhudi za BBC kumtafuta msemaji wa polisi ili kupata maelezo zaidi hazikufanikiwa.
Wiki iliyopita, polisi wa Rwanda walitangaza kufanya upekuzi katika makazi ya mwanasiasa huyo na kutangaza kwamba ni sehemu ya upelelezi wa mwanzo kuhusu ambayo ni pamoja na kosa la kughushi nyaraka na kukwepa kulipa kodi.
Diane Rwigara alikataliwa kugombea kiti cha urais katika uchaguzi uliofanyika mwezi wa 8 uliopita na baadae akaanzisha vuguguvu la kukosoa utawala wa nchi hiyo.

No comments:

Post a Comment