Huwa inajulikana kwa watu wote kwamba talaka ni sehemu ya maisha ya ndoa. Tangu enzi na enzi kwenye mizizi ya uwepo wetu imekuwa ikitoa mwanya kwa watu wawili walioshindwa kuishi pamoja kwa hali ya amani kuachana. Ila ili kuelewa sababu ya talaka ni lazima kwanza tuelewe maana yake na kwanini ikawepo na hapo ndipo tutapiga hatua moja ya kupata ufumbuzi.
Kwa mujibu wa National Center for Health Statistics, 43% ya ndoa za kwanza huishia kwenye talaka ama kutengana ndani ya miaka 15 na pia 75% ya hao wanao talikiana huoa ama kuolewa tena, nusu yao ndani ya miaka mitatu tangu wapate talaka. Kwa Marekani U.S. Bureau of Census iliripoti kwamba mwaka 1970, kulikuwa na talaka milioni 4.3, mwaka 1994, namba iliongezeka kufikia milioni 17.4 na wanawake ndio waliongoza kwa kuomba talaka ambapo theluthi mbili ya walioolewa waliomba talaka ndani ya Marekani pekee. Ushahidi wao ulionyesha kuwa ndani ya Marekani wanawake walisababisha uvunjifu wa ndoa kwa asilimia 90.
Talaka ni zoezi ambalo ni libaya na la kuumiza kwenye maisha ya binaadamu na uzito wake ni wa pili baada ya kifo cha mmoja wa wanandoa. Ila imeonyesha pia ndani ya siri za biashara hiyo kwenye ukuaji wa kinasabia vurugu na migongano huleta matibabu ya ndani zaidi na pia kukuza kimtazamo. Kama kifo kilivyo talaka huleta mtazamo wa ndani zaidi na kutafuta maana ambayo nyakati nyingine huleta suluhisho mfano: jinsi ya kuweza kuhimili mitikiso ya ndoa nyingine ikawa utaoa ama kuolewa tena. Hivyo nyakati nyingine kuna faida ya kuwepo kwa talaka kwani mmoja anakuwa amekua zaidi kimtazamo kuliko alipooa ama kuolewa mara ya kwanza. Pia wanaume ama wanawake waliooa ama kuolewa na kupata talaka wanakuwa makini na niwazuri zaidi kwenye ndoa zao za baadae.
Huzuni na maumivu kwa watu ni sentensi ambayo inapelekea talaka kuwepo. Hii nizawadi itakayoendelea kutoka mpaka hapo tutakaposimama tukatulia na kusikiliza kwa makini. kuzuia uongezeko wa talaka si jibu sahihi jibuni kuzuia mahusiano yasiyo na muelekeo tija na usahihi unaopaswa. Hatuhitaji wataalamu wa akili ya binadamu kutusaidia kwenye hili kupunguza talaka ila tunaweza pale tutakapoangalia kwanini tuko katika mahusiano na nini tunategemea ama tunatarajia kupata kutokana nayo. Kuweka mambo hadharani ni hatua moja mbele kuliko kuficha ambako ni hatua tano nyuma. Chukua muada kupata uelewa mzuri wa ndoa na mahusiano kabla ya kuamua kujitumbukiza ndani yake.
Inashauriwa kwamba ni uamuzi wa busara na sahihi ni kuepuka talaka. Ila kama haizuiliki sababu ya migongano na ugomvi usioisha talaka ina sababu chanya kwa wote watoto na wazazi. Kuna tafiti nyingi zimeeleza kuhusu uharibifu unaotokana na familia kutengana hasa kwa watoto ila ni muhimu mtoto kulelewa na wazazi walio na furaha wakati wote kuliko wanaolelewa na wazazi ambao hawana furaha ya kuwa pamoja. Na pia watoto wenye furaha huleta watu wazima wenye furaha. Hivyo kama wazazi wanaweza kuishi pamoja kwa furaha ni vizuri ila kama hawawezi ni vizuri wakaachana ili kumuokoa mtoto.
Ila ushauri ni mmoja tu kama unataka kupata au kutoa talaka kwanza tafuta ushauri kwa mtu au watu walioshapitia uamuzi huo kabla.
Utajiuliza swali je, kuongezeka kwa talaka ni tatizo?
Katika mahusiano kuna sababu au kwa mawazo yangu njia kuu tatu zilizosababisha talaka kuongezeka.
1. Uwezeshaji wa wanawake: Wanawake wengi wataipinga hii ila karne zilizopita wanawake hawakuwa na uwezo wa kuwaacha wanaume zao pia hawakuwa na uwezo wa kuchagua waume wa kuwaoa so sababu tafiti zinaonyesha kuwa wanawake wengi ndio wa kwanza kuomba talaka siku hizi wanaume karne hizo zilizopita waliweza kuziepuka kwani wao ndio walikuwa waamuzi wa mwisho.
2. Kufanyia mazoezi chaguo zetu: Kwa ukweli ulio sahihi kukubali kwamba ulifanya kosa ni ngumu na kufanya sahihisho ndio ngumu zaidi. ila talaka ni uelewa wa kuonyesha kwamba mambo hayaelekei yalivyotakiwa au yalivyokusudiwa. Kwa sasa talaka imekuwa ni kama sahihisho la kosa ambalo lilitokea nalo ni kuchagua mke ama mume asiyekufaa.
3. Furaha muhimu: Wakati watu huachana sababu wanakosa furaha ndani ya ndoa inamaanisha thamani ya furaha zao ni muhimu kwao hivyo labda talaka inaweza kuwa ni ishara ama alama nzuri kwamba kwa sasa wanaweka juu thamani ya utu wao kuliko mambo ya mpito tu kama fedha, uzuri n.k
Ila swali bado lipo je, talaka ni tatizo ama la?
Jibu langu ni hili talaka sio hata sababu. Ila tuu ni kutokana na uzingatiaji wa talaka ndio unatufanya tusahau matatizo halisi ambayo tungeyaongelea. Uongezekaji wa talaka ni dalili za ugonjwa ambao hatuufanyii uchunguzi inavyotakiwa na pia bila ya kujua namna ya kudhibiti ugonjwa huo.
Talaka si tatizo? Kuna matatizo makubwa kwenye mahusiano yasiyo na mwelekeo mwema ila watu hawachukui njia ya talaka kuweza kufika mahala ila kuweza kuacha kitu nyuma. Na kitu hicho ni mahusiano yasiyo sahihi. Tatizo letu ni kuhamasishwa kuoana kwa ajili ya kuanza familia, kutulia ama kuepukana na dhambi za ngono bila ya kufundishwa nini kinahusishwa ndani ya mahusiano sahihi na ni nini tutafanya kuweza kufanya ndoa zetu kuwa ni nyumba za furaha na si kifungo cha matatizo. Kwa hili hata ule usemi usemao, "tunafunga pingu za maisha" ungebadilishwa ili kuleta taswira ya furaha na si neno pingu kwani pingu ni neno linalohusisha huzuni.
Nilipokuwa na miaka 24 mtu mmoja wa dini aliniambia nimeshachelewa miaka kadhaa kuoa, je nilitakiwa kuwahi ili niendane na miaka ama nitafute furaha ya ndoa? Wengi hufanya kosa hilo. Maongezi ya ndoa na faida zake ni muhimu ila ushauri wa namna ya kumchukulia na kumtendea mwenza wako pamoja na matarajio yatakayopatikana kutoka kwenya mahusiano na jinsi ya kukabili matatizo nyakati nyingine husahaulika. Na hapo ndipo ugumu unajitokeza. Furaha mara nyingine haihusishwi kwenye formula ya ndoa. Ni kitu ambacho watu hukiruka. Ila furaha ni kitu muhimu sana na ni kama roho ya mahusiano na tunatakiwa tuifanye ni moja ya lengio la ndoa. Njia moja ya kufanya hilo ni kuangalia dalili za mahusiano yasiyo sahihi mfano: mahusiano ambayo mmoja ama wote wawili walio ndani yake wakaona hayaleti mabadiliko ndani ya maisha yao, mahusiano yanatakiwa yalete mabadiliko katika kila nyanja.
Kufikiria watoto: wazazi wengu huambiwa msipeane talaka sababu ya watoto fikirieni watoto nakadhalika ila talaka sio tatizo kwa watoto ugomvi na kutokuwa na raha katika mahusiano ndio tatizo kwa watoto. Mahusiano yasiyo sahihi ndio tatizo kwa watoto. Kwani wawili hao hawawezi kuwakuza watoto katika misingi bora wakati ndoa yao si bora. Talaka ni jawabu la matokeo ya mahusiano yasiyo sahihi ambayo hufumbiwa macho. Watoto watakuwa bora kama hawataishi kwenye familia zenye migongano ya kimahusiano zaidi ya kuwa kwenye familia zinazoonyesha ishara mbaya ambazo watazifuata wakati wanapokua wakubwa. Hivyo tusielemee kulaumu talaka kwanza tulaumu mahusiano mabovu ya wanaopeana talaka.
Nadhani mpaka hapo mmepata picha kamili kuhusu suala hili la talaka ila huo ni mtizamo tuu.