Wednesday, June 28

Tanzania yailalamikia Kenya kukiuka taratibu za biashara Jumuiya ya Afrika Mashariki


Dar es Salaam. Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, imepeleka rasmi malalamiko yake nchini Kenya kwa kukiuka taratibu za biashara katika Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari leo (Jumatano) na Katibu Mkuu, Biashara na Uwekezaji, Adolph Mkenda imeeleza kuwa hatua hiyo imechukuliwa baada ya Kenya kupiga marufuku uingizwaji wa gesi ya kupikia kutoka Tanzania na kutoza kodi unga wa ngano unaotoka nchini.
“Walizuia gesi hiyo na kusema kuwa gesi itakayoruhusiwa kuingia Kenya ni ile itakayokuwa imepitia Bandari ya Mombasa peke yake,” imesema taarifa hiyo.
Taarifa hiyo imesema kuwa baada ya kusoma taarifa hizi Serikali ya Tanzania iliwasiliana na Serikali ya Kenya ili kupata maelezo kuhusu hatua hii ambayo ni kinyume cha taratibu za kibiashara katika Jumuiya ya Afrika ya Mashariki.
Pia taarifa hiyo imeeleza kuwa Mei 18 mwaka huu, Serikali ya Kenya ilitekeleza uamuzi wake kwa kuzuia shehena ya gesi isiingie Kenya kutokea Tanzania.
“Hatua hii ina athari kubwa kwa wafanyabiashara wa gesi ya kupikia hapa nchini pamoja na watu wote ambao ajira zao zinategemea biashara hii,” imesema taarifa hiyo.
Imesema suala hilo lilijadiliwa kwa kina katika kikao cha Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Biashara, Viwanda, Fedha na Uwekezaji la Jumuiya ya Afrika ya Mashariki kilichofanyika Juni, 2017 na kufanyiwa maamuzi.
Imesema Serikali ya Kenya ilikubali kuondoa katazo la uingizaji wa gesi kupitia Tanzania mara moja na makubaliano haya yaliingizwa kwenye kumbukumbu za mkutano ambazo ziliafikiwa na nchi zote wanachama wa Jumuiya kwa kuweka sahihi.
Pia imeeleza kuwa pamoja na makubaliano hayo, Kenya imeendelea kuzuia gesi isiingie nchini mwao kutokea Tanzania. Serikali ya Tanzania
imewasilisha rasmi malalamiko yake Kenya kuhusu suala hili.

Kamati yamchapa ‘bakora’ mbunge wa Chadema



Kamati  ya Haki Kinga na Madaraka ya Bunge imependekeza Mbunge wa Viti Maalum (Chadema) Conchesta Rwamlaza asimamishwe kuhudhuria vikao vitatu vya mkutano wa saba unaoendelea wa Bunge la bajeti baada ya kumtia hatiani kwa kusema uongo.
Julai 11 mwaka jana akichangia hotuba ya bajeti ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Rwamlaza alimtuhumu Mbunge wa Muleba Kusini (CCM) Profesa Anne Tibaijuka kuwa wakati akiwa Waziri wa wizara hiyo alitumia vibaya madaraka yake.
Rwamlaza alimtuhumu Tibaijuka kwa kujimilikisha zaidi ya ekari 4000 katika Kijiji cha Kyamnyorwa na kwamba kiasi hicho cha ardhi ni zaidi ya kiasi alichoomba kihalali ambacho ni ekari 1098.
Akisoma mapendekezo ya kamati hiyo leo (Jumatano) mwenyekiti wa kamati hiyo, George Mkuchika amesema kauli hizo zilimshushia heshima Profesa Tibaijuka mbele ya Bunge na jamii anayoiongoza.
Pia amesema kauli hiyo zilikuwa zikimgombanisha Profesa Tibaijuka na wananchi wa eneo hilo ambalo lipo ndani ya jimbo lake.

NGUVU KAZI YA TAIFA INATEKETEA KWA MATUMIZI YA DAWA ZA KULEVYA- RC DODOMA


Na Chalila Kibuda, Dodoma

Vijana wengi wanaangamia kutokana na kutumia dawa za kulevya na kufanya taifa kukosa nguvu kazi ya kufanya uzalishaji.

Hayo ameyasema leo Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Jordan Rugimbana wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya siku ya kupiga vita dawa za kulevya Duniani yaliyofanyika katika Viwanja vya Nyerere Square mkoani hapa, amesema kuwa vijana kuwa na familia wameshindwa kuwa wazalishaji kwa kuishia katika matumizi ya dawa za kulevya.

Amesema vita ya dawa za kulevya ilishatangazwa na Rais Dk. John Pombe Magufuli na wengine ni kufanya utekelezaji kuhakikisha linafanikiwa dhidi vita ya dawa za kulevya.

Rugimbana amesema kuwa Dodoma inalengwa na kuwindwa kutokana na vyuo vingi kuwepo hali ambayo vijana wanaweza kungeuka na kujiingiza katika matumizi ya dawa za kulevya.

Katika maadhimisho hayo Mkuu wa Mkoa amepiga marufuku matumizi ya shisha katika hoteli zilizopo katika mkoa wake kutokana na kuwa sehemu ya dawa za kulevya.

Aidha amemuomba Mkurugenzi wa Life and Hope Sober House ya Bagamoyo, Al- Karim Bhanji kujenga sober house katika mkoa wa Dodoma kutokana na kuwepo kwa kundi la vijana ambao wameathrika na matumizi ya dawa za kulevya.

Bhanji amesema kuwa wanaangalia uwezo katika kuweza kujenga kituo ili kuweza kuwarudisha vijana kutoka katika matumizi ya dawa za kulevya na kuwa wazalishaji katika taifa lao.

Amesema kuwa vijana wanaathirika sana na matumizi dawa za kulevya na kufanya familia zao kuwa na mzigo wa kuwategemea wazazi wakati wazazi hao walitakiwa kusaidiwa na vijana wao.

Katika maonesho hayo yameshirikisha umoja wa vituo vya kuhudumia walioathirika na dawa za kulevya Voice of Sober Houses (VOS).
Kamishina wa Mamlaka ya Kudhibiti Dawa za Kulevya nchini, Rogers Sianga akipeana mkono na Mkurugenzi wa Life and Hope, Sober House ya Bagamoyo, Al- Karim Bhanji jana wakati maandalizi ya maadhimisho ya Siku ya kupiga vita dawa za kulevya Duniani katika Viwanja vya Nyerere Square Mjini Dodoma Jana.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma , Jordan Rugimbana akipeana mkono na Mkurugenzi wa Life and Hope, Sober House ya Bagamoyo, Al- Karim Bhanji wakati alipotembelea banda la Life and Hope, Sober House ya Bagamoyo katika maadhimisho ya siku ya kupiga vita dawa za kulevya Duniani yaliyofanyika katika Viwanja vya Nyerere Square Mjini Dodoma.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma , Jordan Rugimbana akipata maelezo katika banda la Kitengo cha Kupambana na Dawa za Kulevya kutoka kwa Mkaguzi wa Jeshi la Polisi Kitengo cha Kudhibiti Dawa za Kulevya, Anastazia Sauli katika uzinduzi wa maadhimisho ya siku ya kupiga vita dawa za kulevya Duniani yaliyofanyika katika Viwanja vya Nyerere Square Mjini Dodoma.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma , Jordan Rugimbana akizungumza na katika uzinduzi wa maadhimisho ya siku ya kupiga vita dawa za kulevya Duniani yaliyofanyika katika Viwanja vya Nyerere Square Mjini Dodoma .


Kamishina Msaidizi wa Idara ya Kinga , Tiba na Utafiti ,DK. Cassian Nyadindi akitoa maelezo juu ya madhara ya matumizi ya dawa za kulevya katika uzinduzi wa maadhimisho ya siku ya kupiga vita dawa za kulevya Duniani yaliyofanyika katika Viwanja vya Nyerere Square Mjini Dodoma.


Wananchi waktembelea mabanda mbambali juu ya huduma wanazozitoa katika uzinduzi wa maadhimisho ya siku ya kupiga vita dawa za kulevya Duniani yaliyofanyika katika Viwanja vya Nyerere Square Mjini Dodoma.

 Picha ya pamoja.

Sehemu ya wananchi wakiwa katika maadhimisho ya siku ya kupiga vita dawa za kulevya Duniani yaliyofanyika katika Viwanja vya Nyerere Square Mjini Dodoma.



RAIS DKT MAGUFURI AKUTANA NA WATAALAMU WA NISHATI KUTOKA ETHIOPIA NA TANZANIA, KAMATI ZA UCHUNGUZI WA MCHANGA WA MADINI (MAKINIKIA)





Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wajumbe wa Kamati mbili alizoziteua za Uchunguzi wa Mchanga wa  Madini (Makinikia) Ikulu jijini Dar es Salaam leo Juni 28, 2017.PICHA NA IKULU
 Katibu Mkuu kiongozi Balozi John Kijazi (kulia) akiongea na Waziri wa Maji, Umwagiliaji na Umeme wa Ethiopia Dkt. Seleshi Bekele anayaongoza ujumbe kutoka kwa Waziri Mkuu wa nchi hiyo iliyopo nchini kusaidia mchakato wa ujenzi wa Dam (bwawa la kuzalisha umeme)  la Steigler’s Gorge kabla ya kukutana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam leo Juni 28, 2017. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Waziri wa Maji, Umwagiliaji na Umeme wa Ethiopia Dkt. Seleshi Bekele anayaongoza ujumbe kutoka kwa Waziri Mkuu wa nchi hiyo iliyopo nchini kusaidia mchakato wa ujenzi wa Dam (bwawa la kuzalisha umeme)  la Steigler’s Gorge  Ikulu jijini Dar es salaam leo Juni 28, 2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Waziri wa Maji, Umwagiliaji na Umeme wa Ethiopia Dkt. Seleshi Bekele na ujumbe kutoka kwa Waziri Mkuu wa nchi hiyo iliyopo nchini kusaidia mchakato wa ujenzi wa Dam (bwawa la kuzalisha umeme)  la Steigler’s Gorge  Ikulu jijini Dar es salaam leo Juni 28, 2017 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika picha ya pamoja na Waziri wa Maji, Umwagiliaji na Umeme wa Ethiopia Dkt. Seleshi Bekele na ujumbe kutoka kwa Waziri Mkuu wa nchi hiyo iliyopo nchini kusaidia mchakato wa ujenzi wa Dam (bwawa la kuzalisha umeme)  la Steigler’s Gorge  pamoja na jopo la wataalamu wa Tanzania wanaosimamia mradi huo Ikulu jijini Dar es salaam leo Juni 28, 2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipeana mikono  na Waziri wa Maji, Umwagiliaji na Umeme wa Ethiopia Dkt. Seleshi Bekele baada ya kupata picha ya pamoja na ujumbe wake kutoka kwa Waziri Mkuu wa nchi hiyo iliyopo nchini kusaidia mchakato wa ujenzi wa Dam (bwawa la kuzalisha umeme)  la Steigler’s Gorge  pamoja na jopo la wataalamu wa Tanzania wanaosimamia mradi huo Ikulu jijini Dar es salaam leo Juni 28, 2017

RAIS MSTAAFU BENJAMIN MKAPA NA WAZIRI MKUU MSTAAFU DKT. SALIM AHMED SALIM KATIKA MSIBA WA RAIS WA ZAMANI WA BOTSWANA SIR KETUMIRE MASIRE MJINI GABERONE

Rais Mstaafu Mhe Benjamin William Mkapa na Waziri Mkuu Mstaafu Dkt. Salim Ahmed Salim wakiwa na Rais Mstaafu wa Msumbiji Mhe. Armando Emilio Gwebuza wakiwa kwenye misa ya Kitaifa kuomboleza kifo cha Rais mstaafu wa Botswana Sir Ketumire Masire katika ukumbi wa Sports Centre wa Chuo Kikuu cha Botswana mjini Gaborone leo. Marehemu Masire anatarajiwa kuzikwa kesho kijijini kwake Kanye, kilomita 80 kutoka Gaborone
Waziri Mkuu Mstaafu Dkt. Salim Ahmed Salim akiwa kwenye misa ya Kitaifa kuomboleza kifo cha Rais mstaafu wa Botswana Sir Ketumire Masire katika ukumbi wa Sports Centre wa Chuo Kikuu cha Botswana mjini Gaborone leo. Marehemu Masire anatarajiwa kuzikwa kesho kijijini kwake Kanye, kilomita 80 kutoka Gaborone
Rais Mstaafu Mhe Benjamin William Mkapa akiwa kwenye misa ya Kitaifa kuomboleza kifo cha Rais mstaafu wa Botswana Sir Ketumire Masire katika ukumbi wa Sports Centre wa Chuo Kikuu cha Botswana mjini Gaborone leo. Marehemu Masire anatarajiwa kuzikwa kesho kijijini kwake Kanye, kilomita 80 kutoka Gaborone
Waziri Mkuu Mstaafu Dkt. Salim Ahmed Salim na Rais Mstaafu wa Msumbiji Mhe. Armando Emilio Gwebuza wakiwa kwenye misa ya Kitaifa kuomboleza kifo cha Rais mstaafu wa Botswana Sir Ketumire Masire katika ukumbi wa Sports Centre wa Chuo Kikuu cha Botswana mjini Gaborone leo. Marehemu Masire anatarajiwa kuzikwa kesho kijijini kwake Kanye, kilomita 80 kutoka Gaborone
Rais Mstaafu Mhe Benjamin William Mkapa akihojiwa na kituo cha TV cha Afrika Kusini cha SABC kwenye misa ya Kitaifa kuomboleza kifo cha Rais mstaafu wa Botswana Sir Ketumire Masire katika ukumbi wa Sports Centre wa Chuo Kikuu cha Botswana mjini Gaborone leo. Marehemu Masire anatarajiwa kuzikwa kesho kijijini kwake Kanye, kilomita 80 kutoka Gaborone
Rais Mstaafu Mhe Benjamin William Mkapa na Waziri Mkuu Mstaafu Dkt. Salim Ahmed Salim wakiwa na Rais Mstaafu wa Msumbiji Mhe. Armando Emilio Gwebuza wakiwa kwenye misa ya Kitaifa kuomboleza kifo cha Rais mstaafu wa Botswana Sir Ketumire Masire katika ukumbi wa Sports Centre wa Chuo Kikuu cha Botswana mjini Gaborone leo. Marehemu Masire anatarajiwa kuzikwa kesho kijijini kwake Kanye, kilomita 80 kutoka Gaborone

Mfanyabishara Mo Ibrahim na afisa wa mambo ya nje wa Tanzania 
Rais Mstaafu wa Msumbiji Mhe. Armando Emilio Gwebuza akiwa kwenye misa ya Kitaifa kuomboleza kifo cha Rais mstaafu wa Botswana Sir Ketumire Masire katika ukumbi wa Sports Centre wa Chuo Kikuu cha Botswana mjini Gaborone leo. Marehemu Masire anatarajiwa kuzikwa kesho kijijini kwake Kanye, kilomita 80 kutoka Gaborone
Waziri Mkuu Mstaafu Dkt. Salim Ahmed Salim akiwa kwenye misa ya Kitaifa kuomboleza kifo cha Rais mstaafu wa Botswana Sir Ketumire Masire katika ukumbi wa Sports Centre wa Chuo Kikuu cha Botswana mjini Gaborone leo. Marehemu Masire anatarajiwa kuzikwa kesho kijijini kwake Kanye, kilomita 80 kutoka Gaborone
Rais Ian Khama wa Botswana akiongoza wakati wa nyimbo ya Taifa ikipigwa
Rais Ian Khama wa Botswana akiongoza wakati wa nyimbo ya Taifa ikipigwa
Rais Mstaafu Mhe Benjamin William Mkapa na Waziri Mkuu Mstaafu na Rais Mstaafu wa Msumbiji Mhe. Armando Emilio Gwebuza wakiwa kwenye misa ya Kitaifa kuomboleza kifo cha Rais mstaafu wa Botswana Sir Ketumire Masire katika ukumbi wa Sports Centre wa Chuo Kikuu cha Botswana mjini Gaborone leo. Marehemu Masire anatarajiwa kuzikwa kesho kijijini kwake Kanye, kilomita 80 kutoka Gaborone
Rais Mstaafu Mhe Benjamin William Mkapa na Rais Mstaafu wa Botswna Mhe. Festus Moghae wakonge na mfanyabishara Mo Ibrahim kwenye misa ya Kitaifa kuomboleza kifo cha Rais mstaafu wa Botswana Sir Ketumire Masire katika ukumbi wa Sports Centre wa Chuo Kikuu cha Botswana mjini Gaborone leo. Marehemu Masire anatarajiwa kuzikwa kesho kijijini kwake Kanye, kilomita 80 kutoka Gaborone

Rais Mstaafu Mhe Benjamin William Mkapa na Waziri Mkuu Mstaafu na Rais Mstaafu wa Msumbiji Mhe. Armando Emilio Gwebuza wakifuatilia misa ya Kitaifa kuomboleza kifo cha Rais mstaafu wa Botswana Sir Ketumire Masire katika ukumbi wa Sports Centre wa Chuo Kikuu cha Botswana mjini Gaborone leo. Marehemu Masire anatarajiwa kuzikwa kesho kijijini kwake Kanye, kilomita 80 kutoka Gaborone
Rais Mstaafu Mhe Benjamin William Mkapa na Waziri Mkuu Mstaafu Dkt. Salim Ahmed Salim wakiwa na Rais Mstaafu wa Msumbiji Mhe. Armando Emilio Gwebuza wakiwa kwenye misa ya Kitaifa kuomboleza kifo cha Rais mstaafu wa Botswana Sir Ketumire Masire katika ukumbi wa Sports Centre wa Chuo Kikuu cha Botswana mjini Gaborone leo. Marehemu Masire anatarajiwa kuzikwa kesho kijijini kwake Kanye, kilomita 80 kutoka Gaborone
Rais Mstaafu Mhe Benjamin William Mkapa na Mama Anna Mkapa na viongozi wengine wakitoka ukumbini baada ya  misa ya Kitaifa kuomboleza kifo cha Rais mstaafu wa Botswana Sir Ketumire Masire katika ukumbi wa Sports Centre wa Chuo Kikuu cha Botswana mjini Gaborone leo. Marehemu Masire anatarajiwa kuzikwa kesho kijijini kwake Kanye, kilomita 80 kutoka Gaborone

CUF KUIFIKISHA KORTINI WAKALA WA USAJILI, UFILISI NA UDHAMINI (RITA)



CHAMA cha Wananchi (CUF), kinatarajia kumfikisha mahakamani  Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA) 
 kwa kukiuka taratibu za sheria ya wadhamini kwa kutojiridhisha juu ya uhalali wa majina ya Bodi ya Wadhamini yaliyofikishwa kwake kama yalipitishwa na kikao halali cha chama kwa mujibu wa katiba.
Kauli hiyo ameitoa Katibu  Mkuu wa Chama hicho, Maalim Seifjijini Dar es Salaam leo wakati akizungumza na waandishi wa habari.
Alisema wanachukua hautua hiyo kutokana RITA kushindwa kutumia mwongozo na weledi katika kutekeleza majukumu yao na badala yake wamesukumwa na utashi binafsi kwa ajili ya hujuma dhidi ya chama hicho.
“Chama chetu kimepatwa na mshituko mkubwa sana, kuona taasisi kubwa nan yeti yenye dhamana kubwa katika nchi inaweza kufanya vitendo vya ovyo. RITA ni taasisi inayobeba maisha ya watu ya kila siku. Licha ya kusajili Bodi za Wadhamini, inasajili vizazi na vifo, ndoa, talaka na inatunza wosia kwa ajili ya mirathi,” alisema Maalim.
Alisema michakato wa kufungua kesi hiyo inaanza leo ambapo alieleza kuwa tayari wamekwisha agiza mwawakili kulishughulikia. Kutokana na matarajio ya ufunguzi wa kesi hiyo watawasilisha maombi mbele ya Mahakama Kuu kuitaka isimamishe kesi nyingine zote walizofungua kuhusiana na kadhia hiyo hadi hapo shauri linalohusu uhalali wa maamuzi ya RITA  litakapoamuliwa.
Maalim alisema kusajiliwa kwa bodi hiyo ambayo aliiita kuwa ni bodi feki, alieleza kwamba ni mwendelezo wa kukihujumu na kukidhoofisha chama kunakofanywa dola kupitia kwa Msajili wa Vyama vya Siasa pamoja na Profesa Ibrahim Lipumba na kundi lake.
Alitaja mambo manne ambayo yalikuwa msukumo wa kusajiliwa kwa bodi hiyo. Alisema kuwa ni kwa ajili ya kufuta kesi zote zilizofunguliwa na ambazo zinawaelemea licha ya kutumia nguvu kubwa ya dola, kufungua akaunti mpya ya benki ili kumwezesha Profesa Lipumba kupata ruzuku.
Aliongeza mengine kuwa ni Bodi hiyo kuwezesha udhibiti wa Ofisi za Makao Makuu, Zanzibar pamoaja na kumwondoa madarakani Katibu Mkuu Maalim Seif Hamad na hivyo kufanikisha njama za kuwapokonya haki Wazanzibar kwa maamuzi yao ya Oktoba 25 mwaka 2015.
Hamadi alisema kamwe  haki ya Wazanzibar haitapotea na kuahidi kuwa ndani ya miezi mitatu haki hiyo itakuwa imepatikana.
Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi(CUF), Maalim Seif Sharif Hamad, akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu madai ya muendelezo wa hujuma dhidi ya chama hicho zinazofanywa na ofisi ya msaji wa vyama vya siasa nchini. Kulia ni Mbunge wa Viti Maalumu wa chama hicho, Seveline Mwijage.
 Maofisa wa Chama hicho wakiwa meza kuu wakati wa mkutano na wanahabari.
 Wabunge wa chama hicho wakiwa kwenye mkutano huo.
 Baadhi ya wanahabari wakiwa kwenye mkutano huo.
 Wapiga picha kutoka vyombo mbalimbali wakichukua taarifa hiyo.

TAKUKURU YAENDELEA KUWASHIKILIA RAIS WA TFF MALINZI NA KATIBU WAKE MWESIGWA


Na Zainab Nyamka-Globu ya Jamii.
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) imethibitisha kuwashikilia Rais wa TFF Jamal Malinzi na Katibu Mkuu wake Selestine Mwesigwa kwa mahojiano.
Afisa uhusiano wa TAKUKURU Musa Misalaba amesema, ni kweli wanawashikilia viongozi wa TFF kwa ajili ya mahojiano ambapo wamekuwa wakifanya uchunguzi kwa muda mrefu kabla ya kuamua kuwashikilia kwa ajili ya mahojiano.
“Ni kweli kwamba tunaendelea na uchunguzi dhidi ya viongozi mbalimbali wa TFF na uchunguzi huo tumekuwa nao kwa muda mrefu lakini kuhusu kuwashikilia kwa nini, bado ni siri yetu upande wa uchunguzi, katika uchunguzi tunaongozwa na misingi ya sheria, kanuni na taratibu hatuwezi tukaweka wazi kila jambo.”

Misalaba amesema kuwa Jambo la msingi ambalo wananchi wanatakiwa kuelewa ni kwamba, kuna uchunguzi ambao wanaendelea nao ambao umekuwa ukifanywa kwa muda mrefu na kuhusiana kuwashikilia Malinzi na Mwesigwa wamesema muda wa uchunguzi ukikamilika watawapeleka mahakamani.
“Tunawashikilia na bado tuko nao chini ya ulinzi wetu , tunaongozwa na sheria tutakapomaliza uchunguzi wetu tutaweka wazi kama ni kuwaachia ila ushahidi ndio utakaoamua lakini ni lini ni swala kiuchiunguzi, lakini ni siri ya uchunguzi.”
Hivi karibuni gazeti la Nipashe liliandika mfululizo wa makala zilizokuwa zikielezea tuhuma za ufisadi zilielekezwa kwa Malinzi na viongozi wenzake wa TFF.

Rais wa TFF Jamal Malinzi na Katibu Mkuu wake Selestine Mwesigwa.