Monday, October 2

Maandalizi ya Utafiti wa mafuta Ziwa Eyasi, Tanganyika Yaanza



Picha Na 1
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani, (mbele) akiongoza kikao kilichoshirikisha wataalam kutoka Uganda,  Idara ya Nishati, Wizara ya Nishati na  Madini, Shirika la Maendeleo  ya Petroli  Tanzania (TPDC) na Mamlaka  ua Udhibiti wa Shughuli za Mkondo wa Juu wa Mafuta (PURA) kabla ya kuanza ziara katika Ziwa Eyas Wembere lililopo mkoani  Singida.
Picha Na 2
Wataalam kutoka ,  Idara ya Nishati, Wizara ya Nishati na  Madini, Shirika la Maendeleo  ya Petroli  Tanzania (TPDC) na Mamlaka  ua Udhibiti wa Shughuli za Mkondo wa Juu wa Mafuta (PURA) wakifuatilia maelekezo  yaliyokuwa yanatolewa na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani (hayupo  pichani).
Picha Na 3
Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Maendeleo ya Madini Nchini Uganda, Robert Kasande (kulia) pamoja na wataalam kutoka Uganda wakifuatilia ufafanuzi  uliokuwa unatolewa na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani (hayupo  pichani)
Picha Na 4
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Dkt. Mhandisi  Juliana Pallangyo (kushoto mbele) akieleza jambo katika kikao hicho.
Picha Na 5
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani akielezea hali ya utafiti wa mafuta na gesi nchini.
Picha Na 6
Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Maendeleo ya Madini Nchini Uganda, Robert Kasande akifafanua jambo katika kikao hicho.
Picha Na 7
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Nishati na Madini, Asteria Muhozya (kulia) akibadilishana mawazo na Meneja Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki, Salum Mnuna katika kikao hicho
…………………

Asteria Muhozya na Greyson Mwase.
Timu ya wataalam kutoka Uganda imewasili nchini Tanzania kwa ajili ya kubadilishana uzoefu na wataalam wa Tanzania katika utafiti wa mafuta. Mbali na kubadilishana uzoefu wataalam hao watafanya ziara Ziwa Eyasi Wembere lililopo mkoani  Singida.

Kabla ya kuanza kwa ziara hiyo wataalam hao leo tarehe 2 Oktoba, 2017  wamefanya  kikao kilichoongozwa na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani na kuwashirikisha Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo pamoja na wataalam kutoka Idara ya Nishati, Wizara ya Nishati na Madini, Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) na Mamlaka ya Udhibiti wa Shughuli za Mkondo wa Juu wa Mafuta (PURA).

Akizungumza katika kikao hicho, Dkt. Kalemani amesema  maandalizi hayo ni  juhudi za Rais wa Jamhuri  ya Muungano wa  Tanzania, Dkt. John Magufuli za kuhakikisha kuwa rasilimali ya mafuta inagunduliwa na kuanza kuleta manufaa kwa wananchi, ambapo wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi la Ujenzi wa Mradi ya Bomba la Kusafirisha Mafuta  Ghafi la  Afrika Mashariki kutoka Hoima nchini Uganda hadi Tanga nchini Tanzania tarehe 5 Agosti, 2017 alieleza kuwa wataalam waliogundua mafuta katika Ziwa Abert nchini Uganda kushirikiana na wataalam wa Tanzania katika utafiti wa mafuta katika Ziwa Tanganyika na  Eyasi nchini Tanzania.

Dkt. Kalemani amesema baada ya Rais wa Uganda kukubali ombi hilo yalianza maandalizi kupitia vikao mbalimbali ambapo hatua iliyofikiwa kwa sasa ni wataalam kukutana na kubadilishana uzoefu kabla ya kuanza kwa shughuli za utafiti katika maziwa husika.

Amesema wataalam wataanza kwa kufanya ziara ya siku mbili katika Ziwa Eyasi Wembere mkoani Singida ili kupata picha halisi kabla ya kuanza kwa majadiliano ya kubadilishana mawazo ya namna bora ya utafiti katika maziwa husika.

“ Sisi kama  Tanzania  tupo  tayari kubadilishana uzoefu na wataalam wa Uganda kwenye utafiti wa mafuta na kuanza kazi mara moja;  hata hivyo pia tupo  tayari kubadilishana nao uzoefu  kwenye masuala ya  gesi kwa kuwa tuna utaalam huo, lengo likiwa ni kuimarisha sekta hizi za mafuta na gesi kwa nchi zote mbili,” amesema  Dkt. Kalemani.

Ameongeza kuwa kwa kuwa Tanzania ina uzoefu mkubwa kwenye utafiti wa gesi asilia, wapo tayari kutuma wataalam nchini Uganda kushirikiana kwenye utafiti wa gesi nchini Uganda.

Kwa upande wake Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Maendeleo ya Madini Nchini Uganda na kiongozi  wa ujumbe huo, Robert Kasande amesema kuwa wapo tayari kubalishana uzoefu ambapo watalenga katika kuangalia tafiti zilizowahi kufanyika nyuma, kutembelea maeneo husika na kuweka mikakati ya namna bora ya kufanya utafiti kwa ubora wa hali ya juu kwa kushirikiana na  Tanzania.

Diamond asimamisha shughuli Hospitali ya Amana


Mwanamuziki wa kizazi kipya Diamond Platnumz amesherehekea siku yake ya kuzaliwa leo kwa kutembelea hospitali ya Amana ambako amesababisha shughuli zisimame kwa muda.
Katika ziara yake hiyo aliyoifanya leo Jumatatu, Diamond ametoa vifaa tiba vyenye thamani ya Sh4 milioni.
Muda wote aliokuwa hospitalini hapo wagonjwa na waliokuwa wakiwahudumia walitoka kwa ajili ya kumuona msanii huyo.
Diamond ambaye sasa anatamba na ngoma yake ya Hallelujah, amesema alifikia uamuzi wa kwenda kwenye hospitali hiyo kwa kuwa ndiyo mahali alipozaliwa.
Amesema anajivunia kuwa na watu wazuri wa karibu ambao wanamshauri kurudisha kwenye jamii inayomzunguka.
"Najua hospitali kuna mahitaji mengi nikaona kwa uwezo wangu mdogo nami nishiriki kusaidia mahali nilipozaliwa siku ya leo ili nipate pia fursa ya kuwaona watoto waliozaliwa tarehe kama yangu,"

"Nafahamu kuna changamoto nyingi, niwasihi watu wengine waangalie ni namna gani wanaweza kusaidia," amesema Diamond.
Kaimu mganga mkuu wa hospitali hiyo, Shaany Mwaruka amempongeza Diamond kwa uamuzi huo na kutaka watu wengine waige mfano huo.
"Ungeweza kusherehekea siku yako ya kuzaliwa kwa kufanya chochote kile, lakini ukakumbuka mahali ulipozaliwa."
Dk Mwaruka amesema hospitali hiyo inakabiliwa na changamoto ya vifaa tiba kutokana na idadi kubwa ya watu wanaowahudumia.
Kwenye ziara hiyo Diamond ameambatana na meneja wake, Said Fella.

Mauaji Las Vegas: Tunayoyafahamu kufikia sasa kuhusu shambulio Marekani

Mamia ya watu waliokuwa wanahudhuria tamasha walijaribu kujificha na wengine kukimbilia usalamaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionMamia ya watu waliokuwa wanahudhuria tamasha walijaribu kujificha na wengine kukimbilia usalama
Mzee wa miaka 64 aliwafyatulia risasi watu waliokuwa wanahudhuria tamasha ya muziki na kuwaua watu zaidi ya 58. Watu wengine 515 wanauguza majeraha.
Mshambuliaji alijipiga risasi, polisi wanasema.
Kulitokea nini?
Watu takriban 22,000 walikuwa wanahudhuria tamasha ya muziki wa country usiku wa Jumapili katika eneo la wazi karibu na uwanja mdogo wa ndege wa Las Vegas.
Milio ya kwanza ya risasi ilisikika mwendo wa saa nne usiku saa za Las Vegas (05:00 GMT).
Mshambuliaji aliwafyatulia watu risasi kutoka ghorofa ya 32 katika hoteli ya Mandalay Bay na baadaye akajiua kwa kujipiga risasi.
Taarifa za awali zilikuwa zimesema kuwa aliuawa na polisi.
Walioshuhudia wanasema mamia ya risasi zilifyatulia na kwamba walisikia milioni ya bunduki za rashasha.
KuliZbuka mtafaruku na watu walikimbia huku na kule uwanjani wakijaribu kujificha.
Polisi wanasema kwamba taarifa kuwa kulikuwa na ufyatuaji wa risasi katika maeneo mengine ya uwanja wa ndege wa Las Vegas zilikuwa za uongo.
Las Vegas crime sceneHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Eneo la mauaji
Image captionEneo la mauaji
Mshukiwa ni nani?
Polisi wamesema wanaamini Stephen Paddock mwenye umri wa miaka 64 ndiye aliyehusika.
Hata hivyo, hawajasema chochote kuhusu nia ya mauaji hayo.
Mkuu wa polisi Joe Lombardo amesema maafisa wa polisi walipata hadi bunduki 10 katika chumba chake.
"Hatujapata maelezo yoyote baada ya uchunguzi au maelezo kumhusu mhusika huyo ambayo ni ya kukera (au kudokeza angetekeleza uhalifu)," Lombardo amesema.
"Jambo pekee tunaloweza kusema ni kwamba alitajwa katika kisa kimoja miaka michache iliyopita na kisa hicho kilishughulikiwa kama kisa cha kawaida katika mfumo wetu wa mahakama."
Maafisa wanaamini amekuwa hotelini humo tangu 28 Septemba.
Kakae Eric Paddock ameambia Reuters kwamba: "Hatuna habari zozote (kuhusu nia). Tumegutuka sana. Tumeshangazwa sana na tunatuma rambirambi zetu kwa jamaa za waathiriwa."
Kundi linalojiita Islamic State limedai kuhusika lakini halitajoa ithibati yoyote.
"Mshambuliaji huyo wa Las Vegas alisilimu miezi michache iliyopita," kundi la Islamic State limesema kupitia taarifa.
Stephen PaddockHaki miliki ya pichaUNDATED IMAGE
Image captionStephen Paddock
Kumetolewa wito wa kutafutwa kwa "mhusika mweingine" kwa jina Marilou Danley, 62, ambaye maafisa wanasema alikuwa anasafiri na mshambuliaji kabla ya kisa hicho kutokea.
Mwanamke huyo anaaminika kuwa alikuwa amesafiri nje ya Marekani.
Polisi wakiwa nje ya hoteli ya Mandalay BayHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionPolisi wakiwa nje ya hoteli ya Mandalay Bay
ShambulioHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Ni watu wangapi wameuawa?
Waliofariki wamefikia zaidi ya 58, kwa mujibu wa polisi.
Watu 515 wamepelekwa hospitalini wakiwa na majeraha.
Watu 14 wanaaminika kuwa katika hali mahututi, kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters.
Mauaji

What has the president said?

Katika kituo na wanahabari White House, Rais Donald Trump amesema mauaji hayo ni "kitendo cha uovu".
Amewapongeza pia polisi wa Las Vegas kwa kuzuia mauaji zaidi, akisema walichukua hatua upesi sana.
Awali, rais huyo aliandika kwenye Twitter kuhusu shambulio hilo.

Mabalozi wakosoa serikali na upinzani Kenya kuhusu uchaguzi mpya

Wafuasi wa upinzani wameandamana leo miji mbalimbali kushinikiza mabadiliko katika tume ya uchaguziHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionWafuasi wa upinzani wameandamana leo miji mbalimbali kushinikiza mabadiliko katika tume ya uchaguzi
Mabalozi wa nchi za Magharibi wamewashutumu viongozi wa upinzani na viongozi wa serikali nchini Kenya huku nchi hiyo ikiendelea kujiandaa kwa maruduo ya uchaguzi wa urais baadaye mwezi huu.
Wawakilishi hao wa nchi 13 pamoja na Umoja wa Ulaya wamesisitiza kwamba uchaguzi mpya unafaa kuwa "bora kuliko uliofanyika awali (mwezi Agosti) - uwe huru, wa kuaminika na wa Amani".
Taarifa yao ya pamoja imetolewa baada ya mkutano kati yao na maafisa wakuu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (IEBC).
Kwenye taarifa hiyo, mabalozi hao wakiwemo Robert Godec wa Marekani, Susie Kitchens wa Uingereza na Jutta Jardfelt wa Ujerumani, wametoa wito kwa wadau kuheshimu uhuru wa tume hiyo ya uchaguzi na kuiacha ifanye kazi yake bila kuingiliwa.
Mapema leo, wafuasi wa muungano wa upinzani National Super Alliance walitawanywa na polisi walipojaribu kuandamana nje ya afisi kuu za IEBC, Nairobi kushinikiza mabadiliko katika tume hiyo.
Balozi wa Marekani nchini Kenya Bob Godec amesema juhudi za chama tawala kutaka kurekebisha sheria za uchaguzi kabla ya kufanyika kwa uchaguzi huo "zinazidisha wasiwasi na uhasama wa kisiasa".
Kadhalika, ameushutumu upinzani kwa kutishia kususia uchaguzi huo.
Mgombea wa upinzani Raila Odinga amesisitiza kwamba "hakutakuwa na uchaguzi" iwapo maafisa ambao anadai walihusika katika kuvuruga uchaguzi uliopita hawataondolewa kwenye tume hiyo.
Wafuasi wa Rais Uhuru Kenya wamekuwa wakidai mahakama iliwapokonya ushindiHaki miliki ya pichaAFP
Image captionWafuasi wa Rais Uhuru Kenya wamekuwa wakidai mahakama iliwapokonya ushindi
"Hii ni fursa kwa pande zote mbili kuonyesha sifa za uongozi bora, kuimarisha demokrasia ya Kenya na kuinua hadhi ya taifa hili kimataifa. Inasikitisha kwamba kwa sasa mambo yanaonekana kutokea kinyume," alisema Bw Godec.
Majaji wa Mahakama ya Juu walipokuwa wakifuta matokeo ya uchaguzi wa awali walisema haukuwa wa wazi na kwamba ilikuwa vigumu kubaini nani alishinda kwa njia halali.
Waliiamuru IEBC kuandaa uchaguzi wa marudio na kufuata kikamilifu katiba na sheria za uchaguzi.
Majaji hao walisema hawatasita kufuta tena matokeo ya uchaguzi iwapo uchaguzi mpya hautaandaliwa kwa kufuata katiba na sheria za uchaguzi.
Upinzani Nasa umetishia kuandaa maandamano kila Jumatatu na Ijumaa kushinikiza mageuzi katika IEBC.

Wafuasi wa upinzani Kenya waandamana kushinikiza mageuzi IEBC

Polisi walirusha gesi ya kutoa machozi kuwatawanya waandamanaji kadha waliokusanyika NairobiHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionPolisi walirusha gesi ya kutoa machozi kuwatawanya waandamanaji kadha waliokusanyika Nairobi
Wafuasi wa muungano wa upinzani nchini Kenya National Super Alliance (Nasa) wamejitokeza katika baadhi ya miji nchini humo kushinikiza kuondolewa kazini kwa baadhi ya maafisa wakuu wa tume ya taifa ya uchaguzi.
Maafisa wa usalama Kenya wamekuwa kishika doria karibu na jumba la Anniversary Towers zilipo afisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi (IEBC) jijini Nairobi.
Muungano wa Nasa ukiongozwa na Raila Odinga umetangaza maandamano ya kila Jumatatu na Ijumaa kushinikiza kuondolewa kwa afisa mkuu mtendaji wa IEBC Ezra Chiloba na maafisa wengine wakuu kwa tuhuma kwamba walihusika katika makosa yaliyochangia kufutwa kwa matokeo ya uchaguzi mkuu uliofanyika tarehe 8 Agosti.
Hayo yakijiri, mabalozi kutoka nchi kadha za Magharibi wameilaumu serikali ya Kenya pamoja na upinzani, kabla ya kufanyika kwa shughuli za upigaji kura baadaye mwezi huu.
Kwa njia ya taarifa ya pamoja wanadiplomasia wa mataifa 13 na jumuia ya bara Ulaya EU, walikosoa upinzani nchini Kenya kwa kutishia kususia marudio ya uchaguzi mkuu, na chama tawala kwa kujaribu kubadilisha sheria za uchaguzi katiba kabla ya marudio ya uchaguzi huo mkuu.
Uchaguzi mpya utafanyika tarehe 26 Oktoba lakini Nasa wanasema sharti mabadiliko yafanywe kwenye tume hiyo kabla yao kukubali kushiriki katika uchaguzi huo.

Nyusi kuwania tena urais Msumbiji 2019

Nyusi alishinda uchaguzi 2015Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Rais wa Msumbiji Filipe Nyusi ameidhinishwa na chama tawala cha Frelimo kuwania tena urais nchini humo.
Uchaguzi mkuu nchini humo utafanyika mwaka 2019.
Alipochaguliwa mwaka 2015, Nyusi alipata asilimia 57 ya kura zilizopigwa na kumshinda mpinzani wake wa karibu Afonso Dhlakama, kiongozi wa chama cha upinzani cha National Resistance (Renamo).
Dhlakama alipata 37% ya kura zilizopigwa.
Renamo - ambao walipigana vita vya muda mrefu vya wenyewe kwa wenyewe dhidi ya Frelimo ambavyo vilifikia kikomo 1992 na kusababisha vifo vya watu zaidi ya milioni moja - walipinga matokeo hayo.
Licha ya ukuaji mzuri wa uchumi, zaidi ya nusu ya raia 24 wa Msumbiji wameendelea kuishi maisha ya ufukara.

Mzee wa miaka 60 afia kwa mganga wa kienyeji akiongezewa nguvu za kiume


Shinyanga. Mzee Joseph Sahn (60), mkazi wa Kijiji cha Nzonza wilayani Shinyanga amefia kwa mganga wa kienyeji Robert Mkoma mkazi wa kijiji hicho wakati akimpatia matibabu ya kumuongezea nguvu za kiume kwa kutumia pampu ya baiskeli.
Akizungumza ofisini kwake leo Jumatatu, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Shinyanga, Simon Haule amesema tukio hilo lilitokea jana Jumapili saa 10:00 jioni nyumbani kwa mganga huyo, alipokuwa anamuwekea dawa ya unga kupitia tundu la uume wake kisha kuanza kuisukuma kwa kutumia pampu ya kujaza upepo kwenye baiskeli.
Kamanda Haule amesema wakati akipampu ili dawa hiyo iingie vizuri ndani, mzee huyo alianza kutokwa damu nyingi kwenye tundu hilo na kisha kuishiwa nguvu. 
“Kutokana na kutokwa damu nyingi ilisababisha kifo cha mzee huyo, ambapo tayari jeshi la polisi linamshikilia mganga huyo kwa tuhuma za kusababisha kifo cha mzee Joseph,” amesema Kamanda Haule
Amesema mtuhumiwa atafikishwa mahakamani ili ajibu tuhuma zinazomkabili. 
Kamanda Haule aliwataka wananchi kuacha kuona waganga kuwa kimbilio la matatizo yao badala yake wakimbile hospitalini au kwenye vituo vya afya vilivyokaribu nao.

Jimbo la Sugu ‘lawapasua’ kichwa CCM Mbeya


Mbeya. Chama cha Mapinduzi (CCM) Mbeya Mjini kimesema safu ya viongozi wa jumuiya za chama hicho zilizofanyika mwishoni mwa mwezi uliopita zitawasaidia kurudisha jimbo la Mbeya Mjini na halmashauri mikononi mwake katika Uchaguzi Mkuu wa 2020.
Katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, CCM Mbeya Mjini ilishindwa kumng’oa mbunge wa jimbo hilo,   Joseph Mbilinyi 'Sugu’ (Chadema) lakini ilijikuta ikipoteza viti vingi vya udiwani jambo lililofanya Chadema kunyakuwa na halmashauri ya jiji hilo baada ya Chadema kuwa na viti 26 vya udiwani na CCM kumi.
Kwa nyakati tofauti viongozi waandamizi wa CCM Mbeya Mjini wamesema   mfumo wa uchaguziulioanzishwa sasa na chama hicho unaondoa msuguano na makundi yanayojenga fitina, majungu na usaliti tofauti na hapo awali.
Katibu wa Umoja wa Wazazi-CCM Wilaya ya Mbeya, Sadick Kadulo amesema   kwa sasa CCM ipo makini katika chaguzi zake lengo ni kuona inakuwa na viongozi wenye uwezo wa kukisaidia chama kukomboa jimbo na halmashauri.
“Mapinduzi haya ya kimuundo ndani ya chama chetu yana tija sana tofuati na huko nyuma kwani wakati ule ilikuwa rahisi sana wagombea kucheza rafu  ndani na nje ya chama, na hii ndio iliyotufanya tupoteze jimbo kwa mara ya pili lakini kubwa zaidi tukapoteza halmashauri,”

“Lakini naamini hii safu tuliyoipata katika jumuiya zote za CCM ni makini na imara kutokana na mfumo wake, hivyo katika chaguzi za Serikali za Mitaa mwaka 2019 tutashinda kwa kishindo lakini pia 2020 tutakomboa jimbo na halmashauri pia,” amesema Kadulo.
Akiwa wilayani Mbarali, Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Mbeya, Dk Mary Mwanjelwa amewaambia wafuasi wa CCM kwamba chuki, ubinafsi, usaliti na fitina ndizo zinazokiumiza chama chake Mbeya Mjini na kusababisha kuanguka katika chaguzi zake tofauti na wilaya nyingine za mkoa huo.
“Mimi ni Mbunge wa Viti Maalumu mkoa mzima wa Mbeya, nina wilaya sita, lakini sijaona mbunge kama mbunge wa Mbarali (Haroon Pirmohamed) na hili nalizingumza bila kumung’unya maneno, Mbarali tumepata mbunge ambaye ni lulu tumtumie’.
Hata hivyo amesema jimbo la Mbeya Mjini ndio kioo cha mkoa mzima wa Mbeya hivyo ni aibu kuona upinzani ndio unaotawala kuanzia ubunge hadi halmashauri, hivyo anaamini katika safu za viongozi wapya waliopatikana hawataendekeza makundi ambayo huwa yanawagharimu siku za uchaguzi, badala yake watakuwa kitu kimoja.

VIDEO-Lema adai Takukuru waanza kuwachunguza madiwani Arusha

Wabunge wa Chadema, Joshua Nassari (Arumeru Mashariki), Godbless Lema ( Arusha Mjini) na Mchungaji Peter Msigwa(Iringa Mjini) wamesema uchunguzi dhidi ya tuhuma za rushwa unaowakabili waliokuwa madiwani wa Arusha na baadhi ya viongozi wa mkoa huo umeanza.
Wabunge hao wamesema hayo leo muda mfupi baada ya kuwasilisha ushahidi wa tuhuma hizo kwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Valentino Mlowola.
"Tumepokelewa vizuri sana na Kamisha wa Takukuru na timu yake...tumewapa ushahidi na wamesema wameshaanza kuufanyia kazi," amesema Lema.
Amesema Mlowola amewahakikishia taasisi hiyo ni huru na wataufanyia kazi bila kujali kwamba umewasilishwa na upinzani.
Lema amesema Rais John Magufuli anapaswa kuliona hilo na kuchukua hatua ili uchunguzi uweze kufanyika vizuri.
Kwa upande wake Nassari amesema amemkabidhi flash ya kile alichokisema jana Arusha na nyongeza huku akisisitiza kwamba watatoa ushahidi zaidi.

"Tumesema tuna ushahidi, kama hawaamini na wakiendelea kujibu tutatoa zaidi ya hapa na mimi kesho nitakuja kufungua jalada hapa Takukuru," amesema Nassari
Kuhusu mkanganyiko wa tarehe katika video yenye ushahidi, Nassari amesema: "Hiyo ni ‘setting’ tu lakini anayebisha aseme huyo si DC, si ofisi yake na wakibisha  tutatoa ushahidi zaidi ya huu."
Kwa upande wake, Mchungaji Msigwa amesema kilichotokea Arusha kinafanana na Iringa.
"Nami nitakuja kuandika maelezo ya kilichotokea Iringa kwani ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Wilaya zinahusika," amesema Mchungaji Msigwa.
Mwananchi imezungumza kwa njia ya simu na Mlowola kuhusu ujio wa wabunge hao ambapo amesema: 'Nipo kikaoni, mtafute msemaji kwa suala hilo."
Msemaji wa Takukuru, Mussa Misalaba amesema alipoulizwa amesema, “Sipo ofisini, kwani nilikuwa safari, kesho nitakuwa ofisini hivyo nitaweza kuongelea hilo."
Wabunge hao waliwasili Takukuru saa 8.39 mchana na ilipofika saa 10.04 jioni walitoka ndani na kuzungumza na waandishi wa habari.