Mgombeaji mmoja wa kiti cha Ubunge wa upinzani nchini Kenya ameokolewa kutoka bara hindi baada ya mashua alimokuwa akisafiria kuzama katika bara hindi maeneo ya Lamu.
Bwana Shekue Kahae alikuwa na familia yake , ambao bado hawajapatikana.
Kwa mujibu wa Kamishna wa Kaunti ya Lamu Joseph Kanyiri, mashua hiyo ilizama baada ya kukumbwa ma mawimbi makali ambayo kwa sasa yanakumba bahari hindi, maeneo ya lamu na viunga vyake. Aidha mawimbi hayo pia yametatiza shughuli za uokoaji .
Maafisa wa Polisi pamoja na wenyeji wa Lamu wenye uzoefu wa kuogelea wanasaidiana katika shughuli hiyo.
Ndio walimwokoa Bw Kahae, ambaye aligombea kiti cha Ubunge katika sehemu hiyo kwa chama cha Upinzani cha ODM na kushindwa katika uchaguzi mkuu uliofanyika Jumanne iliyopita.
Lakini familia yake ya watu 10 aliokuwa nao kwenye mashua hiyo iliyokumbwa na mkasa bado hawajapatikana, ila mwili mmoja tu. Shughuli za kuwatafuta wahanga wengine wa mkasa huo bado zinaendelea.
Hii ni ajali ya pili ya mashua kutokea kwenye sehemu hiyo kutokana na mawimbi makalia. Mnamo mwezi Juni, watu wanane waliaga dunia mashua yao ilipopinda na kuzama.