Akizungumza mbele ya Waziri wa Elimu, Profesa Joyce Ndalichako, Mbunge wa Mkuranga(CCM), Abdalah Ulega amesema licha ya kuwepo kwa uhitaji wa walimu bado idadi ya walimu wanaoletwa katika wilaya hiyo huwa wameelekezwa katika shule zenye utoshelevu.
"Tatizo hili ni kikwazo tena si katika elimu tu pia afya ambako kuna zahanati zina muhudumu mmoja wakati kuna maeneo yanahitaji kubwa," alisema.
Alisema Wilaya ya Mkuranga ni miongoni mwa maeneo nchini ambayo yana mwamko mdogo wa elimu huku kukiwa na idadi kuwa ya wahitimu ambao hawakufanya vizuri mitihani hivyo kutoendelea na masomo.
Mbunge huyo amemuomba Profesa Ndalichako kutimiza adhma ya muda mrefu ya wananchi kwa kusaidia ujenzi wa chuo cha mafunzo ya ufundi (VETA) ili kuzalisha wataalamu wengi katika kuelekea nchi ya viwanda.
"Kwa kipindi kirefu baraza la madiwani liliadhimia na tukaandaa na eneo kabisa tayari kwaajili ya ujenzi, hatutapenda kuona kuwa vijana wetu wanaenda kuwa manamba katika viwanda ambavyo vinaendelea kujengwa na kuboreshwa kila kukicha badala ya kuendeshe mitambo," alisema.
No comments:
Post a Comment