Friday, September 29

MAADHIMISHO YA SIKU YA MAKAZI DUNIANI

Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi itajumuika na Ulimwengu wote kuadhimisha Siku ya Makazi Duniani, tarehe 02 Oktoba, 2017 – Karimjee Hall, ambapo Wadau mbalimbali wanategemewa kujumuika katika hafla hiyo, itakayoambatana na Maonyesho. 

Siku ya Makazi Duniani huadhimishwa duniani kote kila Jumatatu ya kwanza ya mwezi Oktoba. Lengo kuu la maadhimisho haya ni kutoa mwongozo kwa nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa kutafakari kwa pamoja masuala yanayohusu makazi ulimwenguni kwa kuangalia changamoto mbalimbali zilizopo na kushirikishana mbinu na mikakati ya kupambana nazo. 

Shirika la Umoja wa Mataifa linalosimamia Makazi Duniani – UN-HABITAT hutoa mwongozo kupitia kauli mbiu ambayo huongoza tafakari hiyo duniani kote. Mwaka huu maadhimisho hayo, ambayo ni ya 32 yanafanyika kwa kuongozwa na Kauli Mbiu isemayo “Housing Policies”: Affordable Homes: Tafsiri ya kauli mbiu hiyo ni “Sera za Nyumba: Nyumba za Gharama Nafuu: Kauli mbiu hii inaelekeza kutafakari namna tunavyoweza kutunga Sera za Nyumba katika nchi zetu zinazojielekeza kutatua changamoto ya upatikanaji wa nyumba, hususan za gharama nafuu ili kuwawezesha wananchi wa kipato cha chini waweze kumudu kujenga, kununua ama kupanga. 

Madhumuni ya Maadhimisho ya Siku ya Makazi kufuatana na kauli mbiu ya mwaka huu Oktoba, 2017 ni kuhakikisha kuwa Sera zetu za Nyumba na Makazi zinazingatia yafuatayo: 

· Kuwa na Nyumba na Makazi bora yenye huduma za msingi za jamii toshelezi (Inclusive housing and social services),

· Kuwa na mazingira salama ya kuishi kwa wananchi wote, hususan wenye mahitaji maalum wakiwemo watoto, vijana, wanawake, wazee na wenye ulemavu (A safe and healthy living environment for all — with particular consideration for children, youth, women, elderly and disabled),

· Upatikanaji wa usafiri na nishati endelevu zenye gharama nafuu (Affordable and sustainable transport and energy),

· Kukuza, kulinda na kuhifadhi maeneo ya wazi mijini (Promotion, protection, and restoration of green urban spaces),

· Upatikanaji wa maji safi na salama ya kunywa na mfumo thabiti wa uondoshaji majitaka (Safe and clean drinking water and sanitation),

· Uwepo wa hewa safi na ya kutosha (Healthy air quality),

· Kuwepo fursa za ajira (Job creation) ,

· Kuimarisha upangaji miji na kuboresha makazi duni (Improved urban planning and slum upgrading),

· Kuwepo na mfumo thabiti wa usimamizi wa taka (Better waste management)

Kaulimbiu iliyotolewa kwa mwaka huu, pia inahimiza nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa kutumia ngazi zote za Serikali pamoja na wadau wote muhimu kutafakari nanma ya kuibua mikakati ya kuwezesha uwepo wa nyumba bora na za gharama nafuu katika nchi zao ikiwa ni utekelezaji wa mojawapo ya Agenda Mpya ya Makazi Duniani iliyoidhinishwa Quito, Oktoba, 2016 na Malengo Endelevu ya Milenia. 

Chimbuko la maadhimisho hayo ni Azimio Namba 40/202 la Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lililopitishwa mwezi Desemba mwaka 1985 na kuanza kuadhimishwa rasmi mwaka 1986. 

IMETOLEWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI
WIZARA YA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI

EFC TANZANIA MICROFINANCE BANK LIMITED ADVERTISE FOR SALE OF PROPERTIES INDICATED BELOW

"Mafunzo ya Elimu ya ufundi yana nafasi ya kukuza ajira"- Rutayuga


Mafunzo ya elimu ya ufundi yananafasi kubwa ya kuongeza, kusaidia na kukuza ajira kwa vijana wanaosoma masomo hayo kwenye vyuo vya ufundi kwa kuajiriwa au kujitengenezea ajira wao wenyewe.

 Kaimu katibu mtendaji wa baraza la taifa elimu ya ufundi (Nacte), Dkt, Adolph Rutayuga amesema hayo leo jijini dar es Salaam wakati wa ufunguzi wa warsha ya mradi wa kuimarisha elimu na mafunzo ya ufundi nchini yaliyoandaliwa na UNESCO.
Akizungumza kwa niaba ya Katibu mkuu wizara ya elimu,sayansi na teknolojia, Dkt, Rutayuga amesema nia kubwa ya mradi huo ni kuangalia ufundi unaumuhimu gani kwenye sekta ya uchumi hasa unapozungumzia sekta ya uchumi wa viwanda. Aidha tunaangalia ubora wa mafunzo yanayotolewa kwenye elimu ya ufundi sababu kukiwa na vyuo vingi ambavyo vinaendeshwa katika ubora usiotakiwa, wanafunzi wanaotoka kwenye vyuo hivi hawatakuwa wazuri. 
“Tunalenga kujenga mazingira ya kutoa mafunzo bora kwenye elimu ya ufundi, elimu iliyobora kwa kusapoti walimu wanaofundisha,miundombinu ya kujifunza na kufundishia na pia kujaribu kuangalia mahusiano yaliyopo kati ya viwanda na soko la ajira kwa kile kinachotolewa kwenye vyuo vya ufundi.
 Ameongeza,kama suala zima la mambo ya mitaala, linaweza kuboreshwa, na ile dhana potufu ya kizamani iliyokuwepo kwamba kwamba Tivet ni kwa wale walioshindwa,inapaswa iondoke, watu wajue kwamba mchango mkubwa kwenye uchumi unafanywa na hawa watu kwenye sekta ya kati “Malengo makubwa ni kujaribu kuinua ubora wa mafunzo yanayotolewa na vyuo vya ufundi, kuinua umuhimu mafunzo ya ufundi na Jinsi inavyoweza kisaidia kwenye maendeleo ya kukuza uchumi,” amesema. 
Naye, Kaimu Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Axel Plathe amesema warsha hiyo itajadili kwa undani vitendo vya ufanisi, utekelezaji na jukumu la uwezo ambao kila wadau watafanya katika mradi uliopendekezwa chini ya maeneo matatu umuhimu, ubora na mtazamo wa elimu na ujuzi wa kiufundi. “Elimu bora kwa Afrika itatekelezwa kuanzia mwaka huu hadi 2021 kwa lengo la kukuza elimu na ujuzi wa kitaaluma na mafunzo ambayo ni muhimu kwa mahitaji ya soko la ajira na mahitaji ya watu binafsi na jamii”amesema Plathe. Na Karama Kenyunko, Blogu ya Jamii .Kaimu Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Axel Plathe akizungumza washiriki wa warsha ya kuzindua Mradi wa mpango wa kuimarisha elimu na mafunzo ya ufundi nchini yaliyoandaliwa na UNESCO warsha hiyo imefanyika jijini Dar es Salaam leo. Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa elimu ya Ufundi (NACTE), Adolf Rutayuga akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia wakati wa Warsha hiyo iliyoandaliwa na Unesco ya kuimarisha elimu na mafunzo ya ufundi nchini jijini Dar es Salaam.Baadhi ya washririki na Meza kuu wakiwa katika warsha ya uzinduzi wa Mpangowa kuimarisha elimu na mafunzo ya ufundi nchini katika warsha iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo.

Baadhi ya washririki wa Warsha ya kuzindua mpango wa kuimarisha elimu na mafunzo ya ufundi nchini jijini Dar es Salaam.Baadhi ya washiriki Warsha ya kuzindua mpango wa kuimarisha elimu na mafunzo ya ufundi nchini katika warsha iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo.Kaimu Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Axel Plathe na Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa elimu ya Ufundi (NACTE), Adolf Lutayuga wakiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa warsha ya kuzindua mpango wa kuimarisha elimu na mafunzo ya ufundi nchini warsha iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo.Mtoa maada akizungumza na washiriki wa warsha ya kuzindua mpango wa kuimarisha elimu na mafunzo ya ufundi nchini warsha iliyofanyika jijini Dar es Salaam. (Picha na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.)

PROF. MAGHEMBE AFUNGUA MKUTANO WA KIMATAIFA WA NCHI 21 DUNIANI KWA AJILI YA KUJADILI UKUKUZAJI WA SEKTA YA UPANDAJI WA MITI KIBIASHARA

Waziri wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe akizungumza mkoani Morogoro jana wakati wa ufunguzi wa mkutano wa pili wa Mashirika yanayohamasisha upandaji wa miti kibiashara na uzalishaji wa mazao ya misitu barani Afrika, mkutano huo wa siku mbili umewashirikisha wajumbe kutoka nchi 21 duniani kwa lengo la kubadilishana mawazo juu ya kuboresha uzalishaji na upatikanaji wa masoko. Aliwataka wajumbe hao kujadili namna ya kuwawezesha wakulima wa miti wakati wanasubiri kuvuna mazao yao waweze kujishuulisha na kilimo cha mazao ya muda mfupi kwa kutumia mbinu bora za kisayansi ili waweze kujikimu kimapato.
Waziri wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe akizungumza mkoani Morogoro jana wakati wa ufunguzi wa mkutano wa pili wa Mashirika yanayohamasisha upandaji wa miti kibiashara na uzalishaji wa mazao ya misitu barani Afrika, mkutano huo wa siku mbili umewashirikisha wajumbe kutoka nchi 21 duniani kwa lengo la kubadilishana mawazo juu ya kuboresha uzalishaji na upatikanaji wa masoko. 
Baadhi ya wajumbe kutoka nchi 21 duniani wakifuatilia mkutano huo. Nchi hizo ni Burkina Faso, Chad, Ethiopia, Gambia,Ghana, Italy, Mali, Niger, Nigeria, Senegal, Sudan, Liberia, Cameroon, Swaziland, Finland, Zambia, Canada,Mozambique, Zimbabwe, Kenya na Tanzania.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Steven Kebwe akizungumza katika mkutano huo. Aliwataka wajumbe wa mkutano huo kujadili na kuishauri dunia namna bora ya kutunza na kuendeleza misitu kwa faida ya kizazi cha sasa na kijacho ikiwemo utekelezaji wa sheria za usimamizi wa misitu.
Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyuki, Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Ezekiel Mwakalukwa akizungumza katika mkutano huo ambapo aliwataka wajumbe kujadili kwa uwazi kuhusu mikakati mbalimbali ya kukabiliana na changamoto za sekta ya misitu na kwamba Serikali kupitia Wizara itapokea maoni na mapendekezo yao kwa ajili ya kuyafanyia kazi ili kuimarisha ustawi wa sekta hiyo. 
Waziri Maghembe akieleza jambo kwenye ka mkutano huo ambapo aliwataka wajumbe wajumbe wajadili namna bora ya kuwafundisha wakulima wa miti kufanya kilimo bora ikiwa ni pamoja na mafunzo uvunaji wa hewa ukaa ili kuwainua kimapato. Aliwataka pia kusaidia wakulima wa miti katika upatikanaji wa masoko ya uhakika.
  Prof. Maghembe akisisitiza jambo kwenye mkutano huo.
Waziri wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe akizungumza mkoani Morogoro jana na baadhi ya viongozi waliondaa mkutano wa pili wa Mashirika yanayohamasisha upandaji wa miti kibiashara na uzalishaji wa mazao ya misitu barani Afrika muda mfupi kabla ya kufungua mkutano huo wa siku mbili uliowashirikisha wajumbe kutoka nchi 21 duniani kwa lengo la kubadilishana mawazo juu ya kuboresha uzalishaji na upatikanaji wa masoko. 
  Baadhi ya wajumbe walishiriki mkutano huo kutoka nchi 21 duniani.
 Waziri wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe (kushoto) akizungumza na Mbunge kutoka Kenya, Chariti Katambi mkoani Morogoro jana baada ya kufungua mkutano wa pili wa Mashirika yanayohamasisha upandaji wa miti kibiashara na uzalishaji wa mazao ya misitu barani Afrika, mkutano huo wa siku mbili umewashirikisha wajumbe kutoka nchi 21 duniani kwa lengo la kubadilishana mawazo juu ya kuboresha uzalishaji na upatikanaji wa masoko. 
Waziri wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe akizungumza na waandishi wa habari mkoani Morogoro jana baada ya kufungua mkutano wa pili wa Mashirika yanayohamasisha upandaji wa miti kibiashara na uzalishaji wa mazao ya misitu barani Afrika, mkutano huo wa siku mbili umewashirikisha wajumbe kutoka nchi 21 duniani kwa lengo la kubadilishana mawazo juu ya kuboresha uzalishaji na upatikanaji wa masoko. 
Picha ya pamoja na washiriki wa mkutano huo. (PICHA NA HAMZA TEMBA - WMU)

Upinzani Kenya waitisha maandamano makubwa wiki ijayo

Raila OdingaHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionRaila Odinga
Muungano wa upinzani nchini Kenya umeitisha maandamano ya umma kupinga mapendekezo ya kuifanyia mabadiliko sheria ya uchaguzi.
Wabunge wanaoegemea upande wa serikali wanafanya hima kupitisha mswada ambao utamwezesha Uhuru Kenyatta kutangazwa rais bila ya kufanyika uchaguzi ikiwa upinzani utasusia marudio ya uchaguzi tarehe 26 mwezi Oktoba.
Wanachama wa upinzani walitoka nje wakati upande wa serikali ukitumia wingi wake bungeni kuharakisha mabadiko ambayo yatasababisha mswada huo kuwa sheria kabla ya marudio ya uchaguzi.
Kati ya yale yaliyo kwenye mswada huo ni kuruhusu mgombea kutangazwa rais bila ya kufanyika uchaguzi ikiwa mgombea mwingine atasusia uchaguzi.
Marudio hayo ya uchaguzi yana wagombea wawili, Rais Uhuru Kenyatta na Raila Odinga.
Mswada huo pia unasema kuwa mahakama ya juu haiwezi kufuta matokeo ikiwa mfumo wa eletroniki utafeli
Kufeli kwa mfumo wa kupiga kura kwa njia ya eletroniki ndio ilikuwa sababu kuu ya kufutwa kwa matokeo ya urais.
Mgombea wa Upinzani Raia Odinga amekashifu hatua hizo kama jaribio la kuiba kura na kumpendela rais Uhuru Kenyatta.
Ametisha maandamano ya kote nchini kila Jumatatu na Ijumaa kuanzia wiki ijayo.

Burundi hali si Shwari; Amnesty International

Amnesty
Image captionAmnesty International limeonya juu ya usalama wa wakimbizi wa Burundi wanaorudi nchini kwao kutoka Tanzania
Shirika la kimataifa linalotetea haki za binadamu la Amnesty International limeonya kuwa Maelfu ya wakimbizi wa Burundi wanaorudi nchini kwao kutoka Tanzania wanakabiliwa na hatari za kiusalama nchini mwao.
Mwezi uliopita, Tanzania, Burundi na shirika la umoja wa mataifa linalohudumia wakimbizi UNHCR walikubaliana kwamba kufikia mwisho wa mwaka huu wawe wamewarejesha wakimbizi elfu kumi na mbili wanaoishi Tanzania na wanataka kurudi kwao Burundi kwa hiari.
Lakini Amnesty International linasema, mpango huu unahatarisha maisha ya maelfu ya wakimbizi na linaamini kuwa wakimbizi wengi wanarejeshwa nyumbani kwao kutokana msukumo wa ushawishi kutoka serikali ya Tanzania na Burundi.
Shirika hilo limedai kuwa hali ya usalama bado sio shwari katika ripoti yao inayotoka leo, wanasema visa vya kuteswa, kufungwa bila makosa, kubakwa na hata kuuwawa bado vinaendelea.

Kambi ya jeshi yashambuliwa Somalia

Wanamgambo wa AlshabaabHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Taarifa kutoka Somalia zinasema wanamgambo wa Alshabaab wameishambulia kambi ya jeshi katika mji wa Barire magharibi mwa mji mkuu Mogadishu.
Shambulio hilo limetokea Ijumaa alfajiri na wakaazi wanasema waliamshwa kwa sauti za milipuko miwili mikubwa.
Kundi la Alshabaab limekiri kuhusika na shambulio hilo na limeeleza kwamba liliidhibiti kambi ya jeshi la Somalia na kufanikiwa kuwaua wanajeshi kadhaa.
Hatahivyo maafisa wa serikali katika eneo hilo wamekana tuhuma hizo za Alshabaab, lakini wamekiri kwamba kumekuwa na shambulio.
Wameahidi kutoa taarifa zaidi baadaye.
Kambi hiyo ya jeshi mjini Barire katika eneo la Lower Shabelle ni mojawapo ya kambi zilizo bora na zenye vifaa vya hali ya juu vya kijeshi nchini Somalia.
Katika siku za hivi karibuni kundi la Alshabaab limebadili mtindo wake wa mashambulio kwa kutokabiliana na vikosi vya usalama moja kwa moja, badala yake vimekuwa sasa vikishambulia kambi za jeshi katika maeneo tofuati Somalia.
Wiki kadhaa zilizopita raia 10 waliuawa katika operesheni ya pamoja ya jesh la Somalia na Marekani katika eneo hilo.
Serikali ya Somalia ilidai kwamba si raia waliouawa bali ni wapiganaji wa Alshabaab, lakini baadaye ilibadili kauli na kuthibitisha kwamba ni wakulima na iliahidi kulipa fidia.

IS imetoa kanda ya sauti ya Abu Bakr al-Baghdadi.

BaghdadiHaki miliki ya pichaAFP
Image captionUrusi na Iran zimesema kiongozi huyo amekufa lakini Marekani imekataa
Wanamgambo wa Islamic State wametoa kile kinachoonekana kuwa ni kanda ya sauti ya kiongozi wa kundi hilo, Abu Bakr al-Baghdadi.
Mzungumzaji aliye na sauti kama ya kiongozi huyo wa IS anasikika akitaja tishio la hivi karibuni la Korea kaskazini dhidi ya Japan na Marekani.
Anazungumzia pia vita vya kupigania ngome za IS kama Mosul, mji uliodhibitiwa upya na vikosi vya Iraq mwezi Julai.
Baghdadi,ambaye anasakwa hajaonekana mbele ya umma tangu Julai 2014 jambo lililozusha uvumi mkubwa kuhusu hatma yake.
Mwisho alipoonekana alikuwa anatoa hotuba katika mskiti mkubwa wa al Nuri mjini Mosul baada ya IS kuudhibiti mji huo na kulitangaza kuwa eneo wanalo litawala.
Aliopulizwa kuhusu kanda hiyo ya sauti, msemaji wa vikosi vya Marekani vinavyopigana na IS, Ryan Dillon, amesema "pasi kuwepo ushahidi wa kuthibitishwa wa kifo chake, tumeendelea kuamini kwamba yuko hai".
Msemaji wa idara ya ulinzi ameiambia BBC: "tunahafahamu kuhusu kanda hiyo ya sauti inayodaiwa kuwa ya Abu Bakr Al-Baghdadi na tunachukua hatua kuikagua.
Wakati hatuna sababu ya kuwa na shaka ya uhalisi wake, hatuwezi kuithibitisha kwa hivi sasa."
Kundi la wanamgambo wa kiislamu IS, lilitambulika kwa ghasia dhidi ya raia na wafungwa, limesukumwa nyuma Iraq na Syria mwaka huu.

Mapungufu ya UN katika mzozo wa Rohingya

Mamia kwa maelfu ya wakimbizi wa Rohingya wakiwa kambini BaghladeshHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionMamia kwa maelfu ya wakimbizi wa Rohingya wakiwa kambini Baghladesh
Uchunguzi wa BBC umeibua maswali mazito kuhusiana na Umoja wa mataifa ulivyoshughulikia hali ya machafuko ya Rohingya.
Nyaraka zilibainika na mahojiano yanaonyesha kuwa Umoja wa mataifa na serikali ya Myanmar waliwazuia maofisa waliokuwa wakiibua matatizo ya watu wa Rohingya dhidi ya serikali ya Burma.
Maofisa wa umoja wa mataifa kwa mujibu wa uchunguzi wa BBC waliwazuia wafanyakazi wa haki za binadamu kuingia katika maeneo muhimu ili kutoa misaada.
RohingyaHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionBaadhi ya maeneo ya Rohingya
Umoja wa mataifa wa Myanmar katika kuendelea kupinga uchunguzi wa BBC unasema kuwa umekuwa mstari wa mbele kusaidia raia, ambapo hata waliokimbia nchi walisaidiwa ulinzi na umoja wa mataifa na sasa wanaendelea kuhudumiwa katika katika kambi za wakimbizi.
Hata hivyo vyanzo kutoka ndani ya umoja wa mataifa nchini humo vimeiambia BBC miaka mine iliyopita kabla ya mzozo huu wa sasa, mkuu wa Umoja wa mataifa wa Myanmar raia wa Canada Renata Lok Dessallin alizuia makundi ya wanaharakati wa haki za binadamu kufika katika maeneo ya Rohingya.
Pia alijaribu kuzuia uhamasishaji kuhusiana na vurugu za eneo hilo pamoja na kuwaondoa wafanyakazi waliojaribu kutuliza mzozo huo kwa kuendesha mikutano na makongamano.
Zaidi ya watu laki tano wa Rohingya wamekimbilia nchi jirani ya Bangladesh.

Watu 22 wafariki katika mkanyagano kwenye reli Mumbai

Barabara ya Elphinstone inaunganisha njia mbili za reli MumbaiHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionBarabara ya Elphinstone inaunganisha njia mbili za reli Mumbai
Watu kumi na wawili wameuawa na wengine zaidi ya 30 kujeruhiwa, kufuatia kisa cha mkanyagano baada ya daraja moja kuporomoka karibu na kituo cha treni, mjini Mumbai India.
Waliyoshuhudia wanasema, daraja hilo huenda liliporomoka kutokana mvua kubwa iliyokuwa ikinyesha wakati huo, hali ambayo iliwafanya watu kukimbilia mahala hapo kujikinga.
Mwandishi wa BBC mjini Mumbai, anasema mamlaka imekuwa ikilaumiwa kwa kutelekeza miundo mbinu katika mji huo licha ya kuwa mji huo unapokea watu wengi kila siku.
Nilibakwa nikiwa na miaka 10, lakini nimejifunza kuwasamehe watu
Watu waliojeruhiwa wamefikishwa katika hospitali iliyo karibu na maafisa wakuu wa reli wapo katika eneo la mkasa.
Msemaji wa shirika la reli Anil Saxena ameambia waandishi habari kuwa daraja hilo lililofunikwa lilikuwana shughuli nyingi kwasababu idadi kubwa ya wasafiri waliokuwa wanajikinga na mvua kubwa walijaribu kuondoka kwa wakatimmoja na abiria wengine.
Ameongeza kuwa mkasa huo utachunguzwa.
Tizama pia:

Ijue ‘dawa’ sahihi ya kutokomeza uvivu sugu kazini


Kila siku tunaamka asubuhi kwa ajili ya kuanza pilikapilika za kupambana na hali zetu za maisha. Katika mihangaiko hiyo ya kila siku, baadhi yetu wanafanikiwa kutimiza malengo yao na wengine hawafanikiwi.
Siyo kwamba wanaofanikiwa wanafanya kazi dunia nyingine la hasha. Sehemu kubwa ya wanaofanikiwa wanajituma zaidi kikazi kwa kuziishi ndoto zao huku wakitafuta suluhu mbadala kila wanapokumbana na vikwazo.
Upande wa pili wa wale wanaofeli kila mara kuna vitu wanavifanya kinyume na wanaofanikiwa.
Hata hivyo, miongoni mwa sababu kubwa zinazofanya watu wengi wasifanikiwe ni uvivu. Uvivu una hatua za ukuaji. Kuna uvivu unaochipukia, uvivu ‘kijana’ na uvivu sugu.
Kama ilivyo kwa tabia nyingine za binadamu, uvivu unajengwa na mtu husika kutoka ule unaochipukia hadi sugu.
Baadhi ya watu vivu sugu huanza tangu wakiwa watoto wadogo kutokana na malezi hafifu ya wazazi au walezi wao.
Madhara ya uvivu ni makubwa kwa maisha ya mwanadamu kiafya, kijamii na kiuchumi.
Mvivu yeyote anapata shida kuanzia kwenye kuutunza mwili wake hadi kazini kwake. Hakuna jambo litakalokuwa rahisi kwake.
Hata hivyo, uvivu unaweza kutokomezwa na kumrudisha mtu husika katika ari ya uchapakazi na kuchochea mafanikio yake. Miongoni mwa tabia zinazoweza kuutokomeza uvivu sugu ni kuwa na malengo.
Utaratibu wa kupanga malengo unasaidia kupata dira kwa kila myu akifanyacho. Panga malengo katika nyanja zote za maisha kuanzia mipango ya afya, kijamii na kiuchumi.
Weka muda pendekezwa utakaokuwa na ukomo wa kufikia malengo husika. Mfano, kama ni mfanyakazi ainisha malengo binafsi unayotaka kufikia kazini na maisha binafsi.
Kwa malengo ya kazini ambayo mara nyingi huwa na muda maalumu wa kuyafikia, yabainishe wazi na ikiwezekana punguza muda wa kuyafikia.
Fanya hivyo pia kwa malengo binafsi kama ni kuanzisha biashara ndani ya kipindi cha miezi mitatu, ufanye hivyo huku ukitekeleza mikakati ya kulifikia lengo hilo ikiwamo kutafuta mtaji na wateja. Malengo yenye ukomo wa muda wa kuyafikia yanaleta hamasa ya kujituma wakati wote na yanapunguza tabia ya ubongo kujisemea “aaah nitayafikia tu muda bado”.Hamasa hiyo inakufanya muda wote utafute mbadala kwa kila kitu kinachokukwamisha ili mradi ufikie malengo yako.
Tabia hii inaondoa moja kwa moja uvivu sugu unaochelewesha mafanikio kutokana na mawazo ya kuwa siku zote muda upo.
Amka mapema kila siku
Tabia ya kuchelewa kuamka ni moja ya kiashiria kikubwa cha uvivu sugu.
Huanza taratibu na mwisho huwa tabia inayomfanya mtu akose fursa lukuki katika maisha.
Uvivu wa kuchelewa kuamka huwafanya watu kuchelewa kazini na kwenye mikutano. Unafanya watu wafanye vitu kwa haraka bila umakini kwa kuwa wana muda mfupi wa kujiandaa na kutekeleza kazi zao.
Ili niwahi kazini na kupata muda wa kufanya mazoezi asubuhi, mapema mwaka huu nilipanga kuamka Saa 11 alfajiri.
Niliseti simu yangu iniamshe muda huo. Uamuzi huu ulikuja baada ya kujikuta nalala hadi Saa 12.30 asubuhi kiasi cha kunifanya nichelewe kazini siku kukiwa na foleni kubwa.
Nilibaini siku nikichelewa kuamka kiwango cha utendaji kazi pia kinashuka tofauti na siku ninazowahi kufika ofisini.
Japo inakuwa ngumu kwa siku za mwanzo, lakini ukizoea inakuwa sehemu ya maisha yako na unapata muda mwingi wa kufanya kazi.
Mtaalamu wa Baiolojia wa Chuo Kikuu cha Havard nchini Marekani, Christoph Randler 2008 alibaini katika utafiti wake, watu wanaoamka mapema huwa makini zaidi na wanatumia muda mwingi kutekeleza malengo yao kuliko wale wanaochelewa kuamka.
Jihadhari na vikao vinavyopoteza muda
Unaweza kuwahi kuamka ukiwa na malengo madhubuti katika kazi na maisha yako, lakini kwa bahati mbaya mfumo wake wa kushiriki vikao vya kikazi au vya kijamii ukakufanya ushindwe kufikia mipango yako. Tabia ya kuendekeza vikao virefu visivyo na ulazima, hugeuka kuwa uvivu sugu.
Jaribu kufikiri, upo kazini umetingwa na majukumu na ghafla anakuja mtu aliyemaliza kazi zake anaanzisha mazungumzo yasiyo ya kikazi unayojikuta yanaenda zaidi ya nusu saa. Muda huo ambao umeupoteza hauwezi kurudi na haukuwa kwenye mipango yako.
Pia, kuna baadhi ya vikao ofisini huwa virefu bila ya ulazima. Jaribu kushauri wenzio kufupisha ili mpate muda wa kuyatekeleza mnayoyajadili. Jiwekeeni utaratibu wa kuwa na mtunza muda anayekumbusha kila wakati.
Kama wewe ni mwenyekiti wa kikao, hakikisha hamtoki nje ya mada ili kulinda muda. Wajumbe pia mnatakiwa kumkumbusha mwenyekiti juu ya jambo hilo. Ukikaa kimya, wewe ndiye utakayeathirika na upotevu huo wa muda ambao baadaye wakati wa tathmini ya kazi utahesabika kuwa ni sehemu ya uvivu sugu.
Ili kufanikiwa hili, ni vema ukapanga ratiba ya kazi zako na masuala ya kijamii.
Hakikisha kila kikao kipo kwenye ratiba isipokuwa vile vya dharura ambavyo kwa namna nyingine huwezi kuvikwepa.
Kwa vikao vinavyohusu watu wawili na vinahitaji kutoka nje ya ofisi, jaribu kuvifanya kwa kutumia teknolojia ya video kama Google Hangouts, Skype au Whatsapp.
Teknolojia kwa sasa inaokoa muda na fedha na inakufanya ufanye kazi nyingi na vikao vingi ndani ya muda mfupi.
Usipuuze vitu vidogo vidogo
Uvivu huanza na kupuuza vitu vidogo vidogo katika maisha na baadaye hugeuka kuwa tabia sugu inayopuuza mambo makubwa.
Mfano, ni rahisi mtu kuamka na kutotandika kitanda. Tabia hii inakua hadi kwenye maeneo mengine ya maisha. Anakunywa chai na kuacha kikombe juu meza nyumbani. Baadaye tabia ya kuacha vikombe bila kuosha inahamia ofisini. Anaweza kuacha vifaa vya kazi vimezagaa kwa sababu tu “kuviweka vizuri kutampotezea muda”.
Ufanyaji wa mambo unayodhani ni madogo unakufanya uwe mwajibikaji kila wakati.
Mtu anayepuuza vitu anavyodhani ni vidogo siku moja vitamgharimu kupata vikubwa. Uzembe huo ni matokeo ya uvivu.
Hivyo, ukitaka uondokane na uvivu sugu anza kufanya vitu unavyohisi ni vidogo. Amka asubuhi na utandike kitanda vema. Weka kila kitu mahali pake chumbani kwako.
Kwa wale waliooa au kuolewa hawana budi kusaidiana katika kujenga tabia hii ya uwajibikaji.
Baada ya muda mfupi uvivu utatoweka maeneo yote na utakuwa mtu mwenye kiwango kikubwa cha uzalishaji.
Hii inasaidia hata kwa viongozi ofisini kubaini tabia za kizembe na kama zitaachwa, huigharimu kampuni kiutendaji au wakati mwingine huleta hasara kubwa ya fedha.
Kwa kuwa sehemu kubwa tunafanya kazi ama za kujiajiri au kuajiriwa ili kujiingizia vipato ni vema tukautokomeza uvivu.
Ukiukabili ni rahisi kufanya vema kwenye kila nyanja ya maisha.
Uvivu unatufanya tuziweke rehani afya zetu kwa kushindwa kufanya mazoezi kila wakati.
Unatufanya tukose fursa muhimu za maisha kwa kuchelewa kufika kwenye mikutano ama kazini.
Unafanya tuchelewe kutimiza ndoto zetu kwa dhana tu muda upo na kubwa kuliko yote unatufanya tuwe walalamikaji wakubwa na kujiaminisha kuwa hatukubarikiwa kuwa na maendeleo.Wachapakazi wanafanikiwa kwa sababu wana malengo, hawapotezi muda, wanajali kila kitu vikiwamo vile unavyoona ni vidogo na huamka mapema kwa kuwa kulala sana kwao ni kutafuta umaskini.
Nuzulack Dausen ni Mwandishi mwandamizi wa biashara na teknolojia wa Mwananchi Communications Ltd (MCL) +255714382434/ 0764176793