Friday, September 29

Kambi ya jeshi yashambuliwa Somalia

Wanamgambo wa AlshabaabHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Taarifa kutoka Somalia zinasema wanamgambo wa Alshabaab wameishambulia kambi ya jeshi katika mji wa Barire magharibi mwa mji mkuu Mogadishu.
Shambulio hilo limetokea Ijumaa alfajiri na wakaazi wanasema waliamshwa kwa sauti za milipuko miwili mikubwa.
Kundi la Alshabaab limekiri kuhusika na shambulio hilo na limeeleza kwamba liliidhibiti kambi ya jeshi la Somalia na kufanikiwa kuwaua wanajeshi kadhaa.
Hatahivyo maafisa wa serikali katika eneo hilo wamekana tuhuma hizo za Alshabaab, lakini wamekiri kwamba kumekuwa na shambulio.
Wameahidi kutoa taarifa zaidi baadaye.
Kambi hiyo ya jeshi mjini Barire katika eneo la Lower Shabelle ni mojawapo ya kambi zilizo bora na zenye vifaa vya hali ya juu vya kijeshi nchini Somalia.
Katika siku za hivi karibuni kundi la Alshabaab limebadili mtindo wake wa mashambulio kwa kutokabiliana na vikosi vya usalama moja kwa moja, badala yake vimekuwa sasa vikishambulia kambi za jeshi katika maeneo tofuati Somalia.
Wiki kadhaa zilizopita raia 10 waliuawa katika operesheni ya pamoja ya jesh la Somalia na Marekani katika eneo hilo.
Serikali ya Somalia ilidai kwamba si raia waliouawa bali ni wapiganaji wa Alshabaab, lakini baadaye ilibadili kauli na kuthibitisha kwamba ni wakulima na iliahidi kulipa fidia.

No comments:

Post a Comment