China ambaye ni nchi yenye soko kubwa zaidi la magari ina mipango ya kupiga marufuku uundaji na uuzaji wa magari yanayotumia mafuta ya diesel na petroli
Naibu waziri wa viwanda nchini humo alisema wameanaa utafiti lakini badoo hawajaamua ni lini marufuku hiyo itaanza kutekelezwa.
"Hatua hizo bila shaka zitalea mabadiliko makubwa katika sekta yetu ya magari," alisema Xin Guobin.
China iliunda magari milioni 28 mwaka uliopita, takriban thuluthi moja ya magari yote yaliyoundwa duniani.
Uingereza na Ufaransa tayari wametangaza mipango ya kupiga marufuku magari mapya yanayotumia mafuta ya diesel na petroli ifikapo mwaka 2040 kama sehemu ya njia za kuzuia uchafuzi wa hewa.
Kampuni ya kichina ya kuunda magari ya Volvo, ilisema mwezi Julai kuwa magari yake yatatumia umeme ifikapo mwaka 2019.
Makampuni mengine duniani yakiwemo Renault-Nissan, Ford na General Motors yote yanashughulikia mipango ya kuunda magari yanayotumia umeme.