Sunday, September 10

Upepo na mvua kali za kimbunga Irma zaipiga Cuba

Kimbunga Irma CubaHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionUpepo mkali umevunja paa za majengo Remedios, Cuba
Kiwango kamili cha uharibifu unaotokana na kimbunga Irma huko Cuba bado hakijulikani lakini hakuna shaka kuwa kimbunga hicho kimepiga miji na vijiji vilivyopo kaskazini mwa pwani ya kisiwa hicho.
Wakati mvua kubwa ilipoanza kunyesha bado kilikuwa ni kimbunga chenye uzito wa daraja la tano,ni mara ya kwanza kimbunga kikubwa kiasi hicho kupiga katika eneo hilo katika muda wa zaidi ya miaka 80.
Kumekuwa na taarifa za mawimbi makubwa yaliopiga na kuvunja kuta baharini hususan katika kijiji kunakofanyika uvuvi Caibarien.
Ukisogea zaidi katika pwani kwenye jimbo la Camaguey, watu wengi wanakabiliwana ukosefu wa umeme na usafiri umetatizika kuelekea maeneo ya nje.
Kimbunga Irma kikiandamana na upepo mkali.Haki miliki ya pichaREUTERS
Image captionKimbunga Irma kikiandamana na upepo mkali.
Mawasiliano pia yamekatizwa kwa ukubwa katika nchi ambayo tayari ilikuwa inakabiliwana matatizo ya miundo mbinu kwa upande wa mawasiliano kabla ya kuwasili kwa kimbunga hicho.
Baadhi ya maeneo makuu ya kitalii pia yapo katika eneo la pwani na kila jengo kuanzia hoteli za kifahari hadi vijumba vidogo vimejipata katikati ya njia inayopita kimbunga Irma.
Iwapo uharibifu unaoshuhudiwa katika maeneo mengine ya visiwa vya Caribbean ni wa kweli, raia wengi wa Cuba wanahofia hali mbaya mno.
Huenda kimbunga hicho kikaendelea katika eneo linalozunguka Cuba kwa saa kadhaa kabla ya kugeuza muelekeo kurudi baharini na kuelekea kusini mwa Marekani.

No comments:

Post a Comment