Friday, September 1

BANDARI KAVU YA KWALA –VIGWAZA KUANZA KUTUMIKA JANUARI MWAKANI




Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasilino, Profesa Makame Mbarawa (wa pili kushoto), akifafanua jambo wakati akikagua mchoro wa Bandari kavu ya Kwala –Vigwaza Mkoani Pwani.
Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasilino, Profesa Makame Mbarawa (wa pili kulia), akitoa maelekezo kwa Eng. Charles Salu Ogare anayesimamia ujenzi wa bandari kavu ya Kwala-Vigwaza Mkoani Pwani.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) Eng. Deusdedit Kakoko akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasilino, Profesa Makame Mbarawa alipokagua maendeleo ya ujenzi wa bandari kavu ya Kwala –Vigwaza Mkoani Pwani.
Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasilino, Profesa Makame Mbarawa mwenye kofia ya njano akiwa katika majukumu ya ukaguzi wa ujenzi wa bandari kavu ya Kwala-Vigwaza inayojengwa mkoani Pwani.
Muonekano wa bandari kavu inayojengwa na mkandarasi Suma-KJT katika eneo la Kwala-Vigwaza inayotarajiwa kuanza kutumika Januari mwakani ikiwa katika hatua mbalimbali za ujenzi.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini , Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.


Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa ameelezea kuridhishwa kwake na kasi ya ujenzi wa bandari kavu katika eneo la Kwala Vigwaza Mkoani Pwani na kumtaka mkandarasi Suma JKT kuongeza kasi na kuzingatia ubora.

Akizungumza mara baada ya kukagua ujenzi huo ameiagiza Mamlaka ya Bandari nchini (TPA), kushirikiana na Shirika la Reli Tanzania (TRL) na Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) kuhakikisha wanaunganisha kwa haraka ili reli na barabara zinazoingia katika bandari kavu hiyo zinakamilika na hivyo kuiwezesha bandari kavu hiyo kuanza kutumika ifikapo Januari mwakani.

“TPA, TRL na TANROADS uzuri wote mko kwenye wizara moja shirikianeni na hakikisheni kilomita 15 za barabara inayoingia kwenye bandari kavu hii na kilomita moja ya reli zinajengwa haraka,” Amesema Profesa Mbarawa.

Profesa Mbarawa amemtaka Mkurugenzi Mkuu wa TPA Eng. Deusdedit Kakoko kuhakikisha ujenzi wa bandari kavu ya Kwala-Vigwaza unazingatia ubora na viwango vilivyopo katika mkataba ili kuiwezesha kuhudumia zaidi ya makontena milioni moja kwa mwaka na hivyo kupunguza msongamano katikati ya Jiji la Dar es Salaam.

“Hakikisheni eneo la bandari kavu linakuwa na maegesho ya kutosha, taa, maji ya uhakika, gari la zimamoto, uzio na mashine ya ukaguzi wa mizigo scanner itakayowezesha kupima kila mzigo unaopandishwa na kushushwa katika eneo hili,” amesisitiza Profesa Mbarawa.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa TPA Eng. Kakoko amesema TPA imejipanga kuhakikisha ujenzi huo unatumia gharama nafuu na mifumo yote ya teknolojia ya habari na mawasiliano TEHAMA inakuwepo katika bandari hiyo ili kuiwezesaha kufanya kazi kisasa na kwa ufanisi zaidi.

“Tukifanikiwa kuhamia hapa mzigo uliokuwa unasafirishwa kwa siku saba sasa utatumia siku tatu kufika Mwanza hali itakayovutia wasafirishaji wengi kutumia bandari ya Dar es Salaam na hivyo kukuza uchumi wa nchi na kuibua fursa za ajira,” amesema Eng. Kakoko.

Bandari Kavu ya Kwala –Vigwaza inayojengwa na Mkandarasi SUMA JKT ambapo takribani kiasi cha shilingi bilioni 9 kinatarajiwa kutumika katika ujenzi huo ili kuboresha huduma za usafirishaji katika bandari ya Dar es Saalaam ambapo zaidi ya hekta 500 zimetengwa kwa ajili ya ujenzi huo ambapo kwa kuanza hekta 120 sawa asilimia 24 zinajengwa katika awamu ya kwanza.

WANANCHI WAONDOLEWA WASIWASI KUHUSU FIDIA YA MALI ZAO ZITAKAZOPITIWA NA BOMBA LA MAFUTA


Wananchi Mkoani Singida wameondolewa wasiwasi kuhusu fidia ya mali au ardhi yao ambayo itapitiwa na mradi wa bomba la mafuta kutoka Uganda hadi Tanga kwakuwa hawatapunjwa bali itazingatia vigezo vya kimataifa na kitaifa.

Mkuu wa Wilaya ya Singida Elias Tarimo amesema hayo mapema leo wakati wa kikao na wataalamu wanaofanya uthamini wa mali na ardhi ambayo itapitiwa na mradi huo.

Tarimo amesema wananchi na taasisi zote wanapaswa kutoa ushirikiano kwa kutaja gharama kulingana na thamani halisi ya mali zao na sio kuongeza gharama za juu kwakuwa vigezo vya kitaifa na kimataifa vitazingatiwa.

“wananchi wengine wasio waaminifu wananweza wakataja pesa kubwa au hata kuvamia maeneo ambayo siyo yao ilimradi wapate tu pesa, nawasihi wasifanye hivyo kwakua watakuwa wanakwamisha mradi huu muhimu sana kwa maendeleo ya taifa letu na majirani zetu Uganda”, amesema na kuongeza kuwa
Mkuu wa Wilaya ya Singida Elias Tarimo akizungumza katika kikao na wataalamu watakaofanya uthamini wa mali na ardhi kwa ajili ya fidia katika mradi wa bomba la mafuta la Kutoka Uganda hadi Tanga.


Mthamini wa ardhi kutoka ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida Chiku Mkina (aliyevaa miwani) na wataalaamu wengine wakisikiliza kwa makini mada katika kikao kilichohusu uthamini wa mali na ardhi kwa ajili ya fidia katika mradi wa bomba la mafuta la Kutoka Uganda hadi Tanga.
Katibu Tawala Mkoa wa Singida Dkt Angelina M Lutambi akichangia mada katika kikao kilichohusu uthamini wa mali na ardhi kwa ajili ya fidia katika mradi wa bomba la mafuta la Kutoka Uganda hadi Tanga.
Mkurugenzi wa kampuni ya Dighy Welly Dkt Jan Perold akiwasilisha mada katika kikao kilichohusu uthamini wa mali na ardhi kwa ajili ya fidia katika mradi wa bomba la mafuta la Kutoka Uganda hadi Tanga.


Mwakilishi wa Serikali katika zoezi la Uthamini kutoka Wizara ya Nishati na Madini Linus Kinyondo akizungumza na wataalamu wa mkoa wa Singida katika kikao kilichohusu uthamini wa mali na ardhi kwa ajili ya fidia katika mradi wa bomba la mafuta la Kutoka Uganda hadi Tanga.
Mhandisi wa Ujenzi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida Simwela Nuru Martin akifuatilia kwa makini kikao kilichohusu uthamini wa mali na ardhi kwa ajili ya fidia katika mradi wa bomba la mafuta la Kutoka Uganda hadi Tanga.

BOT YAKANUSHA TAARIFA KUHUSU KUBADILISHA FEDHA

Benki Kuu ya Tanzania inapenda kuutaarifu umma kupuuza taarifa zinazozunguka katika mitandao ya kijamii kwamba kutakuwa na ‘mabadilisho ya fedha zote za zamani kuanzia tarehe 04/09/2017 hadi tarehe 01/12/2017’. 

Taarifa hizo ni za uongo na hazijatolewa na Benki Kuu ya Tanzania. Wananchi mnaombwa kuendelea na taratibu zenu za kawaida za kufanya miamala yenu mbalimbali kwa kutumia fedha zetu kama kawaida. 

Aidha, Benki Kuu ya Tanzania inawaasa watumiaji wa mitandao ya kijamii kutumia vizuri nyenzo hiyo ya kupashana habari na kuacha kuzusha uongo ambao unaleta usumbufu usio wa lazima kwa wananchi.

Imetolewa na:
Idara ya Uhusiano wa Umma na Itifaki
Barua pepe: info@bot.go.tz

Simu: +255 22 2233167

MKEMIA MKUU WA SERIKALI: HUDUMA ZETU ZINAPATIKANA KOTE NCHINI

Na. Georgina Misama – MAELEZO

Serikali kupitia Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali inafanya maboresho katika maabara zake za kanda zilizopo kote nchini ili kusogeza huduma hiyo kwa wananchi.

Akiongea na waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam, Kaimu Meneja Masoko, Mawasiliano na Huduma kwa Wateja kutoka Mamlaka hiyo Cletus Mnzava alisema kwamba Mamlaka inafanya maboresho katika Ofisi zake za kanda kwa kuboresha miundombinu na kuzipatia vifaa vya maabara vya kisasa.“Lengo kuu la kuimarisha Maabara zetu za kanda ni kusogeza huduma karibu na wananchi kote nchini ili kuwaondolea ulazima wa kuja kufuata baadhi ya huduma kwenye ofisi zetu za Dar es salaam”. Alisema Mnzava

Mnzava amesema sehemu ya maboresho hayo ni pamoja na kujenga majengo ya kudumu ya Ofisi za Mamlaka katika kanda ili kuwekeza katika mitambo ya kisasa na ya kudumu. Aidha, ujenzi wa jengo la Ofisi za Kanda za Nyanda za Juu Kusini unatarajiwa kukamilika mwaka huu wa fedha.

Akizitaja Ofisi hizo za kanda Mnzava anasema kuna kanda ya Ziwa ambayo inahudumia mikoa ya Mwanza, Bukoba, Simiyu, Mara, Shinyanga, Geita na Kigoma, na kanda ya Kaskazini kwa ajili ya mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Tanga na Manyara. Kwa mikoa ya Dodoma, Singida, Morogoro, Tabora na Iringa inahudumiwa na ofisi za Kanda ya Kati, wakati Kanda ya Mashariki ni kwa ajili ya Mikoa ya Dar es salaam na Pwani.

Vilevile kuna Kanda ya Nyanda za Juu Kusini kwa ajili ya Mikoa ya Mbeya, Katavi, Songwe, na Rukwa na Kanda ya Kusini kwa ajili ya kuhudumia mikoa ya Lindi, Mtwara na Songea.Mamlaka pia imejipanga kuanzisha Maabara yenye vifaa vya kisasa kwa kanda ambazo bado hazina maabara hizo ili kutoa huduma kwa weledi na ufanisi kulingana na mahitaji ya eneo husika.

Mzava anasema ili kuendana na kasi ya Serikali ya awamu ya tano, Mamlaka imeimarisha shughuli zake za ukaguzi kwa mipaka yote nchini, ambapo kwa mipaka mikubwa kama vile Namanga na Tunduma huduma hizo za ukaguzi hutolewa kwa masaa 24.

Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali inawaasa watanzania kujenga utamaduni wa kuzitumia Ofisi zake za Kanda kwa lengo la kufanya kazi zinazoweza kufanyika kwa haraka kwenye Kanda husika badala ya kutegemea zaidi Maabara zilizoko Ofisi za Dar es salaam.

Kaimu Meneja Masoko, Mawasiliano na Huduma kwa Wateja wa Mamlaka ya Maabara ya Mkemi Mkuu wa Serikali Bw.Cletus Mnzava akiwasomea Waandishi wa Habari (hawapo pichani) baadhi ya mikakati ya mamlaka ya hiyo kuhusu uimarishwaji wa ofisi zao hapa nchini, kulia ni Afisa Mawasiliano wa Mamlaka hiyo Bw. Silvester Omary katika mkutano uliofanyika katika ukumbI wa Idara ya Habari (MAELEZO) Jijini Dar es Salaam leo.
Kaimu Meneja Masoko, Mawasiliano na Huduma kwa Wateja wa Mamlaka ya Maabara ya Mkemi Mkuu wa Serikali Bw.Cletus Mnzava akisisitiza jambo kwa Waandishi wa Habari( hawapo pichani) katika mkutano wa mamlaka hiyo katika ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) leo Jijini Dar es Salaam .
Baadhi ya Waandishi wa Habari wakifuatilia mkutano wa Kaimu Meneja Masoko, Mawasiliano na Huduma kwa Wateja wa Mamlaka ya Maabara ya Mkemi Mkuu wa Serikali Bw.Cletus Mnzava katika mkutano wa Mamlaka hiyo ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) leo Jijini Dar es Salaam.
Picha na: Paschal Dotto(31.08.2017

MAAFISA WA WIZARA YA USHIRIKIANO WA MAENDELEO YA UJERUMANI WATEMBELEA MAHAKAMA YA AFRIKA

Afisa Mawasiliano Mwandamizi wa Mahakama ya Afrika na Haki  za Binadamu(AfCHPR)Sukhdev Chatbar(kulia)akiwaongoza wageni kutoka Wizara ya ushirikiano wa maendeleo ya Ujerumani kupitia taasisi zake GIZ na AGA waliotembelea mahakama hiyo wamekua ni wadau wakubwa katika kusaidia miradi mbalimbali ya mahakama hiyo.
Mkutubi wa Maktaba ya mahakama hiyo,Revina Moshi akizungumza na maafisa kutoka
shirika la maendeleo ya kimataifa ya Ujerumani(GIZ),kutoka kushoto ni Afisa wa Wizara ya maendeleo ya Ujerumani anayehusika na Umoja wa Afrika(AU) ofisi ya Addis Ababa,Ethiopia,Barbara Schaefer,Janina Hasse kutoka Berlin,Mkuu wa taasisi za GIZ na AGA,Hartmut Krebs 
Mkuu wa taasisi za GIZ na AGA,Hartmut Krebs akiangalia sehemu ya machapisho kwenye maktaba ya AfCHPR. 
Msajiliwa mahakama ya Afrika na Haki za Binadamu(AfCHPR),Dk Robert Enno(kulia)akizungumza na ujumbe kutoka taasisi za Wizara ya maendeleo ya Ujerumani waliotembelea mahakama hiyo. 
Msajili wa mahakama ya Afrika na Haki za Binadamu(AfCHPR),Dk Robert Enno akimkabidhi zawadi  Afisa wa Wizara ya maendeleo ya Ujerumani anayehusika na Umoja wa Afrika(AU) ofisi ya Ethiopia,Barbara Schaefer. 

DKT PALLANGYO AKUTANA NA KAMPUNI YA M & P EXPLORATION PRODUCTION TANZANIA LIMITED

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo (kulia) akiongoza kikao kilichoshirikisha watendaji kutoka Kampuni inayojihusisha na utafiti na uchimbaji wa gesi ya M & P Exploration Production Tanzania Limited, Wizara ya Nishati na Madini, Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC)
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo (kulia) akizungumza na Meneja Mkuu kutoka Kampuni inayojihusisha na utafiti na uchimbaji wa gesi ya M & P Exploration Production Tanzania Limited, Christophe Maitre ( kushoto) katika kikao hicho.
Sehemu ya watendaji kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) wakifuatilia maelekezo yaliyokuwa yanatolewa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo (hayupo pichani) katika kikao hicho


…………………..


Leo Agosti 31, 2017 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo amekutana na Kampuni inayojihusisha na utafiti na uchimbaji wa gesi ya M & P Exploration Production Tanzania Limited kwenye Ofisi za Wizara ya Nishati na Madini zilizopo jijini Dar es Salaam lengo likiwa ni kujadili namna ya kuendeleza gesi ya Mnazi Bay. Kikao hicho pia kilishirikisha watendaji kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC)

INTERNATIONAL KARATE SEMINAR & GRADING (GASSHUKU) KUANZA LEO UKUMBI WA DON BOSCO DAR ES SALAAM


Japan karate Association/World Federation - Tanzania (JKA/WF-TZ), ni shirikisho la mchezo wa karate wa asili ya Japani tawi la Tanzania, lenye usajili wa kimataifa toka makao makuu ya shirikisho hilo Tokyo Japan na pia hutambuliwa na Shirikisho la Karate la Dunia (World Karate Federation). JKA/WF-TZ ilipata usajili rasmi mwaka 2006, na ilishafanya semina na mashindano mengi ya kimataifa ndani na nje ya nchi. Hivi sasa shirikisho lina timu ya Taifa ya karate inayojindaa na mashindo ya Afrika mwakani (2018), Mashindano ya Dunia (2019), Mashindano ya Olympics (2020), na pia mashindao mengine ya ndani na nje ya nchi.
Pamoja na kuendelea na maandalizi ya Timu ya Taifa sisi (JKA/WF-TZ) tunarajia kuendesha Mafunzo ya Karate na kufanya mitihani ya Kimataifa (International Karate Seminar & Grading ama Gasshuku), yatakayofanyika katika ukumbi mkubwa wa Don-Bosco Upanga, kuanzia  tarehe 1-4 Septemba 2017. Saa 6:00 Mchana hadi saa 9:00 Alasiri.
Mafunzo na Mitihani hiyo itaongozwa na Mkufunzi (Master) Shihan Koichiro Okuma, kutoka Makao Makuu ya JKA Tokyo Japan, ambaye aliendesha mafunzo kama haya mwaka jana mwezi wa tisa, eneo lile lile la Don-Bosco Upanga. Mafunzo haya yatajumuisha nchi zote za ukanda wa Afrika mashariki na kati, zikiwemo wenyeji Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Malawi, Zimbabwe, Zambia, DRC, Angola, Afrika Kusini, Ufaransa, nk. Hadi sasa mataifa ya Kenya, Uganda, Malawi, Zimbabwe, Angola, Afrika kusini na Japan, yameshawasili nchini  kuhudhuria mafunzo haya. Na tunatarajia kupata wageni wengi zaidi kadri muda unavyosogea.
Katika mafunzo hayo tunatakuwa na sherehe za ufunguzi siku ya kwanza (tar 1/9/2017 ) na sherehe kubwa siku ya mwisho (tar 4/9/2017) ambapo watahiniwa waliofuzu mafunzo watakabidhiwa vyeti na leseni zao siku hiyo ya mwisho, na wahudhuriaji watakabithiwa vyeti. Katika sherehe hizo, tunatarajia kuwa na Mgeni Rasmi toka BMT ambaye ni Katibu Mkuu, Bwana Mohamed kiganja. na pia tutakuwa mgeni toka Ubalozi wa Japani nchini.

Faida za ujio wa Shihan Koichiro Okuma (Toka Japan) na kuendesha mafunzo haya nchini:
Kwanza kama Taifa, tutakuwa tumeitangaza nchi yetu (Tanzania) kimataifa kutokana na wageni wanaokuja kutoka nje na kwenda kusambaza habari zetu huko kwao, pia kuangaziwa na  vyombo vya habari vya kimataifa, hasa katika suala na michezo, utalii nakibiashara.

Pili sisi kama JKA/WF-Tanzania, tutaongeza ujuzi kwa Wakufunzi/Walimu (Instructors), Waamuzi (Judges) wa  Wachezaji (Karatekas) wa huu mchezo hapa nchini. Pia Shihan Okuma ataangazia matayarisho ya timu yetu ya Taifa inayojiandaa kwa mashindano ya Afrika mwakani (2018), mashindano ya Dunia (2019) na mashindano ya Olympics (2020). Sisi JKA/WF-Tanzania tutatumia fursa hii kuvuna mbinu mbinu mabalimbali za kushinda mashindano ya kimataifa na namna kuindaa timu kisaikolojia na kimwili/kimazoezi pia, katika hali ya kiutaalam zaidi.
Wenu katika michezo,

Nestory Fedeliko (FEDE)
Katibu Mtendaji, JKA/WF-Tanzania.

SHEIKH SHARIFF MAJINI KUFANYA DUA NZITO MAGOMENI.


Sheikh Shariff Majini kwa siku mbili mfululizo atafanya Dua maeneo ya Magomeni wilayani Kinondoni Jiji la Dar es salaam.

Dua itafanyika katika viwanja vya Mtambani jirani na ofisi za Serikali ya Mtaa na Dua hiyo itakuwa ni ya hadhara lakini pia ni ya pamoja ili kuifanya kuwa na nguvu.

Huu ni mfululizo wa Dua za Sheikh maeneo mbali mbali Nchini.

Kabla ya Magomeni Sheikh amefanya DUA katika mikoa ya Dodoma, Arusha, Tanga, Temeke, Viwanja vya TP Darajani na Ukumbini STARLIGHT.

MIGOGORO MINGI YA ARDHI NI KUTOKUJITUMA KWA WATU WETU - RC GAMBO

"Migogoro mingi ya Ardhi ni kutokujituma kwa watu wetu" RC Gambo
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo wakati anahitimisha mkutano wake na wananchi wa wilaya ya Karatu wenye kero mbalimbali za Ardhi,Nyumba na Makazi.

"Toka nianze mikutano mikutano hii na wakazi wa Jiji la Arusha na leo nipo hapa Karatu migogoro mingi si mikubwa kama inavyoonekana bali inachangiwa na uzembe wa watu wetu katika mabaraza ya Ardhi na mahakama kutokutimiza wajibu wao ipasavyo" alisema Gambo.

Katika mikutano hiyo maalum ambayo mkuu huyo wa mkoa ameshaifanya katika jiji la Arusha na Karatu amekutana na migogoro mingi ambayo kiuhalisia imeshasuluhishwa katika hatua mbalimbali za kimaamuzi lakini wananchi hao hawajapewa mrejesho.

"Tatizo letu sisi watendaji ni kutokuwaandikia watu hawa wa nini tumekifanya katika maamuzi yetu na kutokuweka kumbukumbu sahihi, kama mmeshughulikia tatizo la mtu mpeni mrejesho kwa maandishi na kama ataona hajaridhika mshaurini hatua zaidi za kufuata na jambo hilo liwekwe kwenye kumbukumbu zetu ili akija wakati mwingine tusipate shida kwa kudhani ni jambo jipya" alisisitiza Mhe Gambo.

Vilevile amemuagiza Kamishna wa Ardhi kutuma timu maalum itakayoshughulikia kero hizo ndani ya muda mfupi na kuyafanyia ukaguzi mabaraza yote ya Ardhi wilaya za Arusha mjini na Kararu.

"Kamishna nitakutana mara baada ya ziara ya mwenge kupita mkoani mwetu ulete timu maalum itakayopiga kambi hapa kumaliza kero hizi kwani hapa kuna wengine wala hawana migogoro ya ardhi bali wamevamiwa kwenye maeneo yao watu kama hawa polisi ndio sehemu husika na sio kwenye mabaraza ya ardhi, vilevile ukayafanyie ukaguzi mabaraza ya Ardhi ya Arusha mjini na Karatu kwani nayo sioni kama wanafanya kazi zao sahihi sana" aliagiza mkuu huyo wa mkoa.

Katika mikutano hiyo maalum aliyoianza tarehe 29/08/2017 kwa Jiji la Arusha na tarehe 30/08/2017 kwa wilaya ya Karatu Mkuu huyo wa mkoa ameambatana na wataalam wa Ardhi toka ofisi ya Kamishna wa Ardhi,Msajili wa hati Kanda, wataalam wa Ardhi mkoa wa Arusha, mwanasheria toka ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali na wataalam mbalimbali toka halmashauri husika.

Mkoa wa Arusha ni miongoni mwa mikoa inayoongoza kwa kua na migogoro mingi ya Ardhi na ya muda mrefu.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. Mrisho Gambo(katikati) akiendesha mkutano wa kuwasikiliza wanachi wa Jiji la Arusha kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Arusha Mjini, Fabian Daqqaro na kulia ni Kaimu katibu Tawala Mkoa wa Arusha Bwana. Chitukuro .
Baadhi ya wananchi wa Jiji la Arusha wakisubiri kumuona mkuu wa mkoa wa Arusha na kumweleza kero zao
Wananchi wa wilaya ya Karatu wakiwa katika makundi kusubiri kuonana na RC Gambo na kutoa malamimiko yao.

KAMISHNA WA MADINI ASHIRIKI ZOEZI LA UHAKIKI WA DHAHABU INAYOSAFIRISHWA NJE


Na Veronica Simba – Geita

Kamishna wa Madini Tanzania, Mhandisi Benjamin Mchwampaka, ameshuhudia na kushiriki katika zoezi la kuhakiki na kufunga madini ya dhahabu katika Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM), kabla ya kusafirishwa kwenda nje ya nchi.

Kamishna Mchwampaka alishiriki zoezi hilo hivi karibuni, akiwa katika ziara ya kazi mkoani Geita kukagua shughuli mbalimbali za sekta ya madini. 

Zoezi la uhakiki na ufungaji wa dhahabu inayosafirishwa, hufanyika katika chumba maalum kijulikanacho kama gold room kilichopo mgodini na hushirikisha maafisa mbalimbali wa Serikali kutoka Jeshi la Polisi, Wizara ya Nishati na Madini na Mamlaka ya Mapato Tanzania pamoja na maafisa wa Mgodi.

Akizungumzia lengo la maafisa wa Serikali kutoka sekta husika kushiriki katika zoezi hilo; Kamishna Mchwampaka alieleza kuwa ni kwa Serikali kujiridhisha na thamani ya dhahabu inayosafirishwa ili kuhakikisha inapata mapato stahiki na kuepusha udanganyifu wowote unaoweza kujitokeza.

“Katika hili, tuko imara na makini. Ni lazima tuhakikishe kuwa Serikali inapata mapato stahiki kulingana na dhahabu inayosafirishwa. Ndiyo maana unaona maafisa wetu kutoka sekta zote muhimu wanashiriki kikamilifu katika zoezi hili.”

Aliwataka watanzania kuondoa hofu na kuiamini Serikali ya Awamu ya Tano inayowaongoza kuwa iko makini na imejipanga kusimamia kikamilifu maslahi ya wananchi.

Kamishna wa Madini yuko katika ziara ya kazi Kanda ya Ziwa kukagua shughuli mbalimbali za sekta husika.


Kamishna wa Madini Tanzania, Mhandisi Benjamin Mchwampaka (mwenye koti), akihakiki uzito wa Mkuo wa Dhahabu, katika Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) kabla ya kufungwa na kusafirishwa nje ya nchi. Wengine pichani ni baadhi ya maafisa wa Serikali na GGM.
Kamishna wa Madini Tanzania, Mhandisi Benjamin Mchwampaka (mwenye koti-kulia), akishuhudia Mkuo wa Dhahabu wenye uzito wa kilogramu 26, ukiwekwa ndani ya mfuko maalum kabla ya kufungwa kwa ajili ya kusafirishwa nje ya nchi. Wengine pichani ni baadhi ya maafisa wa Serikali na GGM.
Afisa kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Anuari Fadhili akiweka ‘seal’ maalum ya Serikali kwenye Kasha lenye Mkuo wa Dhahabu baada ya ukaguzi katika Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM), kabla ya kusafirishwa kwenda nje ya nchi. Wanaoshuhudia ni Kamishna wa Madini Tanzania, Mhandisi Benjamin Mchwampaka (katikati) na maafisa wengine wa Serikali na GGM.
Kamishna wa Madini Tanzania, Mhandisi Benjamin Mchwampaka (katikati),  akitoa maelekezo kwa maafisa wa Serikali pamoja na wale wa Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM), kuhusu zoezi la uhakiki na ufungaji dhahabu inayosafirishwa nje ya nchi.

Kasha lenye Mkuo wa Dhahabu katika Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM), lililohakikiwa na kufungwa tayari kwa kusafirishwa nje ya nchi.

Kamishna wa Madini Tanzania, Mhandisi Benjamin Mchwampaka (katikati) na timu yake, wakiondoka ndani ya eneo la Mtambo/kiwanda cha kuchakata dhahabu katika Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM), baada ya kushiriki zoezi la uhakiki na ufungaji wa dhahabu inayosafirishwa nje ya nchi. Pamoja nao ni maafisa wa GGM. 

MUDA WA KUJISAJILI KATIKA MFUKO WA FIDIA KWA WAFANYAKAZI (WCF) WAONGEZWA


SWALA YA EID EL HAJJ KATIKA MSIKITI WA KIGOGO JIJINI DAR ES SALAAM LEO


 Sehemu ya waumini wa dini ya Kiislam wakiwa kwenye ibada ya swala ya Eid el Hajj iliyoswaliwa katika Uwanja wa Msikiti wa Kigogo, Jijini Dar es salaam leo. Sikukuu ya  Eid el Hajj husherehekewa na waislam duniani, ambapo Waislamu huisherekea sikukuu ya hii kwa kuchinja mnyama ikiwa ni kuheshimu kitendo alichokifanya Nabii Ibrahim (vitabu vya dini vimeeleza).
 Ibada ya Eid el Hajj iliyoswaliwa katika Uwanja wa Msikiti wa Kigogo, Jijini Dar es salaam ikiendelea.
 Waumini wakisikiliza mawaidha.
Kama ilivyo kawaida ya siku hii, hapa ni baadhi ya waumini wakinunua mbuzi kwa ajili ya kuchinja.