Monday, August 28

IGP SIRRO AFUNGUA MAFUNZO YA KIJESHI MKOANI KILIMANJARO


Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro, akizungumza na baadhi ya askari wa Jeshi hilo wanaoshiriki mafunzo ya wiki mbili ya kuwajengea Uwezo na Ujasiri wakati wanapotekeleza majukumu yao muda mfupi kabla ya kufungua rasmi mafunzo hayo yanayofanyika katika chuo cha Polisi Moshi CCP mkoani Kilimanjaro jana. Picha na Jeshi la Polisi.
Baadhi ya askari wa Jeshi la Polisi nchini kikosi cha kutuliza Ghasia (FFU) wanaoshiriki mafunzo ya wiki mbili ya kuwajengea Uwezo na Ujasiri wakati wanapotekeleza majukumu yao wakiwa tayari kumuonyesha Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro (hayupo pichani), moja ya mbinu mahiri za kukabiliana na matishio ya kiuhalifu na wahalifu, mafunzo hayo yanayofanyika katika Chuo cha Polisi Moshi CCP. Picha na Jeshi la Polisi.

TAARIFA YA MKEMIA WA SERIKALI

SAMPULI YA MKOJO WA MASOGANGE UNACHEMBECHEMBE ZA DAWA ZA KULEVYA.


Na Karama Kenyunko, Globu ya Jamii.
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu leo imepokea taarifa ya mkemia wa Serikali iliionesha kwamba sampuli ya mkojo wa Video Queen, Agnes Gerald "Masogange" una chembechembe za dawa za kulevya.

Mahakama imepokea sampuli hiyo kama kielelezo namba moja kwa cha ushahidi upande wa mashtaka ambapo baada ya pingamizi la upande wa lilitokuwa likitaka kisipokelewe kutupiliwa mbali

 Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri amesema pingamizi la upande wa utetezi kuwa fomu zilizopelekwa kwa mkemia hazikufata sheria limetupiliwa mbali.

Amesema shahidi wa kwanza ambaye ni Elia Mulima anahaki ya kuandaa ripoti, kupima sampuli na kutoa ripoti mahakamani.
Ameongeza polisi walipeleka maombi kwa mkemia wa serikali na kwamba ni wazi mshitakiwa alienda kwa mkemia na askari wawili na kumpatia kontena kwa ajili ya kuweka sampuli ya mkojo.
Kesi imeahirishwa kwa muda.
.........UP DATES........
Shahidi namba mbili katika kesi hiyo, mpelelezi kutoka kituo cha polisi cha Kati, WP Judith ameieleza mahakama kuwa  alishuhudia Masogange akitoa sampuli ya mkojo kwa kuwa alisimama mlangoni.
Amedai kuwa alipewa chupa ya plastiki yenye namba ya maabara 446/2017 na kumuelekeza Masogange jinsi ya kufanya ambapo alipata sampuli ya mkojo huo.
Akiongozwa na Wakili wa Serikali, Constantine Kakula, amedai Februari 15, mwaka huu aliitwa na Kaimu Mkuu wa Upelelezi, Ramadhan Kingai amchukue mshitakiwa Masogange na kumpeleka kwa Mkemia wa Serikali ambapo yeye akifuatana na Askari Polisi, Sospeter pamoja Masogange walienda kwa mkemia na kwamba saa 7 mchana walifika.
Akihojiwa na Wakili wa utetezi, Reuben Simwanza ambaye alimtaka shahidi huyo kueleza  alikabidhiwa na nani chupa hiyo na kwamba mkojo ulikuwa na rangi oshahidi alieleza kuwa ulikuwa na rangi ya njano mpauko.
Kesi hiyo itaendelea Agosti 31, mwaka huu.

AWA ZA KUKABILIANA NA UGONJWA WA MALARIA

KAMPUNI GUILIN PHARMACEUTICALS TANZANIA LIMITED YAZINDU TAWI HAPA NCHINI KWAAJILI YA KUTENGENEZA NA KUSAMBAZA DAWA ZA KUKABILIANA NA UGONJWA WA MALARIA.

 Katibu Mkuu wa wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya (wa kwanza kushoto) akizungumza waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu uzinduzi wa tawi la kampuni mpya ya kimataifa toka nchini China iitwayo Guilin Pharmaceuticals Tanzania Limited itakayotengeneza na kusambaza dawa za kukabiliana na ugonjwa wa Malaria kali iitwayo Artesun nchini Tanzania. (wa pili kulia ni Mwakilishi Mkuu wa China kwenye masuala ya uchumi na biashara nchini Tanzania (wa pili kushoto) Makamu mkuu wa Rais wa kampuni ya Guilin Pharmaceutical Tanzania Lily Su (katikati) na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo Ashok Pandey.
 Katibu Mkuu wa wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt Mpoki Ulisubisya akipitia baadhi ya nakara za karatasi zilipewa katika uzinduzi wa uzinduzi wa tawi la kampuni mpya ya kimataifa toka nchini China iitwayo Guilin Pharmaceuticals Tanzania Limited itakayotengeneza na kusambaza dawa za kukabiliana na ugonjwa wa Malaria kali iitwayo Artesun nchini Tanzania.
Katibu Mkuu wa wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt Mpoki Ulisubisya (wa kwanza kushoto) akiwa katika picha ya pamoja  mara baada ya uzinduzi wa tawi la kampuni mpya ya kimataifa toka nchini China iitwayo Guilin Pharmaceuticals Tanzania Limited itakayotengeneza na kusambaza dawa za kukabiliana na ugonjwa wa Malaria kali iitwayo Artesun nchini Tanzania. (Wa pili kulia ni Mwakilishi Mkuu wa China kwenye masuala ya uchumi na biashara nchini Tanzania (wa pili kushoto) Makamu mkuu wa Rais wa kampuni ya Guilin Pharmaceutical Tanzania Lily Su (katikati) na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo Ashok Pandey.

YALIYOJIRI KWENYE UZINDUZI WA MFUKO WA ELIMU WILAYANI IKUNGI


BMG Habari.
Jumamosi iliyopita, Agost 19,2017 Wilaya ya Ikungi mkoani Singida ilizindua rasmi “Mfuko wa Elimu Ikungi” ulioanzishwa wilayani humo kwa lengo la kusaidia utatuzi wa kero za elimu ikiwemo uhaba wa maabara, madarasa, vyoo pamoja na nyumba za waalimu.

Katika uzinduzi huo, pia zilifanyika shughuli kadhaa ikiwemo uzinduzi wa ligi ya soka ya “Ikungi Elimu Cup 2017” yenye lengo la kuhamasisha wananchi pamoja na wadau mbalimbali kuchangia Mfuko wa Elimu Ikungi, uzinduzi wa zoezi la ufyatuaji wa matofali ambapo kila Kata wilayani Ikungi imeazimia kufyatua matofali elfu kumi.

Karibu kwa dakika chache kutazama yaliyojiri kwenye uzinduzi huo ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt.Rehema Nchimbi ambaye aliwakilishwa na Katibu Tawala mkoani humo Dkt.Angeline Lutambi huku mwenyeji wake akiwa ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi na mlezi wa Mfuko wa Elimu Ikungi, Mhe.Miraji Jumanne Mtaturu. Tazama video hapo chini. 

NMB HOLDS A BUSINESS EXECUTIVE NETWORK MEETING FOR TOP END BUSINESS AND CORPORATE CUSTOMERS IN DAR

The NMB Bank’s Managing Director - Ms Ineke Bussemaker making opening remarks at the Executive Network event organized by NMB Bank in Dar es Salaam over the weekend. Over 150 high end customers attended the event where they also benefited from TAX training organized by Pricewaterhousecoopers.
NMB Bank Managing director, Ms Ineke Bussemaker exchages views with Checknoctras Limited Head of Operations Mr Balraj Bhatt (left) and Head of Finance for the same company at the Executive Network event organized by NMB Bank in Dar es Salaam over the weekend. Over 150 high end customers attended the event where they also benefited from TAX training organized by Pricewaterhousecoopers.

NMB Bank Plc has today organized a customer networking meeting with its top end Business Customers and Corporates. The meeting attracted over 150 customers from Dar es Salaam. The discussion of the meeting focused on ways to improve business and the impact of the 2017/2018 budget for businesses relationship between the bank and its customers. 

The NMB Business Executive Network is organized in large commercial cities of Dar es Salaam, Mwanza, Arusha, Morogoro, Mbeya, Mtwara, Kilimanjaro and soon to launch in Dodoma. The NMB Managing Director – Ineke Bussemaker, said that the aim of holding such meetings is to strengthen business relations with its top end business and corporate customers. 

“NMB is committed in ensuring that customers get the best service while the bank supports to their business growth. The bank has done major improvements and innovations to suit the need of customers. Private Banking and the launch of business centers in big cities are among the improvements,” said Ineke. 

Ms Bussemaker further said “the improvements done by the bank so far will help to bring services more closely to this segment of customers. They will not only get the best services but also acquire financial, regulatory, business and forex information in order to become and remain competitive.” She further said after the banks successfully implemented the business clubs which targeted Micro, Small and Medium Enterprises (MSME), the bank decided to start the business executive network to bring in the large business customers. [caption id="attachment_81124" align="aligncenter" width="500"]
NMB Bank Managing Director - Ms Ineke Bussemaker exchages views stockholders at the Business Executive Network event organised by NMB Bank in Dar es Salaam over the weekend. Over 150 high end customers attended the event where they also benefited from TAX training organized by Pricewaterhousecoopers.
NMB Bank Managing Director - Ms Ineke Bussemaker exchages views stockholders at the Business Executive Network event organised by NMB Bank in Dar es Salaam over the weekend. Over 150 high end customers attended the event where they also benefited from TAX training organized by Pricewaterhousecoopers.

RPC MSANGI AWATAKA WAANDISHI WA HABARI KUTUMIA KALAMU ZAO VIZURI ILI KULINDA AMANI YA NCHI


Na David John Mwanza

JESHI la Polisi mkoa wa Mwanza limewataka waandishi wa habari nchini kuhakikisha wanatumia kalamu zao kwa uweledi na uadilifu mkubwa katika kuhabarisha umma, mambo muhimu ya nchi na kwamba waepuke kutumiwa na watu wachache ambao mara zote hawalitakii mema Taifa.

Kauli hiyo imetolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Rpc Mohamed Msangi wakati wa mahojiano maalumu na mwandishi wa habari hizi ambaye aliongozana na Naibu katibu kuu wa Taasisi ya kutetea haki za binadamu nchini TAHURA Habibu Rajabu jana.

Kamanda Msangi mbali na mambo mengine alisema kuwa waandishi wa habari wanadhamana kubwa katika kuhakikisha Taifa linaendelea kuwa salama kwani kama kalamu zao zitatumika vibaya ni rahisi kuvunja usalama ambao umejengwa na waasisi wa Taifa.

"Nitowe wito kwa waandishi wa habari ni vema wakaongeza uzalendo na uchungu kwa nchi yao na hasa kuhakikisha mnatumia kalamu zenu kwa ustadi wa hali ya juu na kuepuka kutumiwa na watu ambao hawalitakii mema taifa,".alisema Msangi

Aliongeza kuwa katika suala la kulinda amani linatakiwa kwa kila mtanzania, kwani hata mwandishi wa habari ni mtanzania na pindi usalama utakapokosekana haitajalisha nafasi ya mtu hivyo lazima waandishi wa habari wanatakiwa kuwa wazalendo la kuhakikisha wanapigania taifa lao kwa nguvu zote.

Msangi alifafanua kuwa watanzania wasidanganywe kwani uhuru ambao unapatikana hapa nchini huwezi kupata mahala pengine popote hivyo ni lazima kujiepusha na watu ambao wanataka kujipatia umaalufu kwa mgono wa watu wengine wakiwemo wandishi wa habari.

Akizungumzia hali ya usalama katika mkoa wa mwanza Kamanda Msangi alisema jiji hilo lipo salama na watu wanaendelea na shughuli zao kama ilivyo maeneo mengine huku akikiri kuwepo kwa matukio madpmadogo ambayo kimsingi jeshi la Polisi linaendelea na uperesheni zake za kila siku.

"Mwanza iki shwari na hata ninyi wenyewe mnaona kama watu wanaendelea na kazi zao japo matukio madogo madogo hayakosekani hususani uwizi wa pikipiki na kadhalika lakini askari wangu wako wanaendelea na majukumu yab kuhakikisha mambo yanaendelea kuwa salama."alisema Msangi.

Pia aliwataka wananchi wa mwanza ma tanzania kila mtu kujitambua na zaidi kuhakikisha kauli ya viwanda wanaipiokea kwa kufanya kazi huku akibainisha wao kama mkoa wameshatenda maeneo kwa ajili ya kukaribisha uwekezaji kwa manufaa ya nchi huku akisisitiza kwa kuzitaka taasisi za haki za binadamu kuwa makini kupokea malalamiko ya watu pasipo kuyachunguza kwa kina.

"Nivema taaisis za zinateteta haki za binadamu kufanya kazi zao kwa uweledi na kuhakikisha malalamiko wanayoletewa wanayafanyia kazi kabla ya kuchukua hatua ambazo mwisho wa siku zinaleta madhara kwa wananchi husika.alisema Msangi.

Ambapo kwa upande wake Naibu katibu mkuu wa Tahura Habibu Rajabu aliunga mkono kauli ya RPC Msangi huku akishauri kwamba wananchi wajitahidi kuleta malalamiko kwa wakati na si kusubiri muda mwingi umepita lakini hata wakileta ukifanya uchunguzi kwa kina unakuta alalamiko mengi ni yakweli lakini mengine ni siasa tu.

MKURUGENZI WA TAKWIMU ATEMBELEA OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU MKOANI DODOMA.


Muonekano wa jengo jipya la Makao Makuu ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu linaloendelea kujengwa mkoani Dodoma.
Muonekano wa jengo jipya la Makao Makuu ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu linaloendelea kujengwa mkoani Dodoma.
Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Dkt. Albina Chuwa akikagua ujenzi wa ofisi hiyo unaoendelea mkoani Dodoma. Wa kwanza kulia ni Mhandisi John Ainainyi Njau kutoka Benki ya Dunia nchini Tanzania.
Mkandarasi wa majengo kutoka kampuni ya Hainan International Ltd inayojenga Ofisi ya Taifa ya Takwimu mkoani Dodoma akitoa maelezo kwa Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina chuwa wakati alipotembelea kukagua ujenzi wa ofisi hiyo.
Baadhi ya Wakurugenzi na Maafisa waandamizi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) walioambatana na Mkurugenzi Mkuu wa ofisi hiyo Dkt. Albina Chuwa (hayupo pichani) kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo jipya la Makao Makuu ya ofisi hiyo mkoani Dodoma. (PICHA ZOTE NA VERONICA KAZIMOTO).

Homa ya nguruwe yawaua watu 1,000 nchini India

Wadi Ahmedabad.Haki miliki ya pichaAFP
Image captionVifo vilivyotokana na homa ya nguruwe vimeongezeka sana mwaka huu
India inaonekana kukabiliwa na mlipuko wa ugonjwa wa homa ya nguruwe baada ya watu 1,094 kuthibitishwa kufariki kutokana na ugonjwa huo katika kipindi cha miezi minane iliyopita, taarifa rasmi ya serikali imesema.
Katika wiki tatu zilizopita, idadi ya vifo imekuwa juu sana, ambapo watu 342 wamefariki.
Jumla ya visa 22,186 vya maambukizi ya ugonjwa huo vimeripotiwa nchini humo.
Idadi ya watu waliofariki mwaka huu ni mara nne zaidi ya idadi iliyoripotiwa katika kipindi sawa na hicho mwaka 2016 ambapo visa vya ugonjwa huo vilikuwa vimeshuka sana.
Jimbo la Maharashtra magharibi mwa nchi hiyo ndilo lililoathirika zaidi ambapo waliofarikini ni 437 kwa mujibu wa takwimu za wizara ya afya.
Jimbo hilo linafuatwa na jimbo jirani la Gujarat lililoshuhudia vifo 297.
India ilikabiliwa na mlipuko mbaya wa homa hiyo miaka miwili iliyopita ambapo zaidi ya watu 1,900 walifariki.
Lakini visa vilishuka mwaka 2016 ambapo ni watu 265 waliofariki, lakini mwaka huu visa vimeongezeka tena.
Mlipuko mbaya zaidi wa homa hiyo nchini humo ulitokea 2009-2010, ambapo watu 50,000 waliambukizwa na wengine 2,700 kufariki kote nchini humo.
Dkt Sanjay Gururaj, mkurugenzi wa kimatibabu katika hospitali ya Shanthi, ambayo ni hospitali ya kibinafsi, amesema si lazima kwa hospitali za kibinafsi kupiga ripoti kuhusu visa vya maambukizi ya homa hiyo kwa serikali.
"Takwimu za serikali kwa hivyo zinaweza kuwa ni kionjo tu," amesema.

Homa ya nguruwe ni nini?
  • Ni ugonjwa wa kupumua unaosababishwa na virusi ya influenza aina A, vinavyofahamika kama H1N1
  • Chanzo chake ni kwenye nguruwe, lakini sasa huambukiza binadamu na huenezwa kwa kupiga chafya au kukohoa.
  • Dalili za ugonjwa huo zinakaribiana na za homa ya msimu - homa kali, kukohoa, maumivu kooni, maumivu mwilini na mzizimo.
  • Wanaoathirika zaidi huwa wajawazito, watoto wa chini ya miaka mitano, wazee wa zaidi ya miaka 65 na wale wenye matatizo mengine ya kiafya.
  • Virusi hiyo vilitambuliwa mara ya kwanza nchini mexico mwaka 2009 na vikaenea upesi maeneo mengine duniani.

Taasisi ya JKCI yapata msaada wa runinga nne



Taasisi ya Tulia Trust Foundation kwa kushirikiana na DSTV na TSN,imetoa msaada wa runinga nne na ving'amuzi vya DSTV kwa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI).
Pia imetoa maboksi mawili ya maziwa ya unga. Msaada huo unatokana naombi la JKCI kwa mashirika mbalimbali kusaidia juhudi za Serikali katika kuboresha huduma kwenye taasisi hiyo.
Dk Tulia Ackson, ambaye ni mwanzilishi wa taasisi ya Tulia amesema msaada wa runinga utawasaidia watoto kujifunza mambo mbalimbali na kupata burudani.
"Watoto wanapokuwa hapa muda mwingi wanawaza ugonjwa, lakini ikiwa wataangalia runinga watakuwa na muda wa kujifunza hesabu na mambo mengine kupitia vipindi na kuangalia katuni.Hata wazazi wataweza kuangalia taarifa za habari kujua nini kinaendelea," amesema.
Dk Tulia ambaye pia ni Naibu Spika wa Bunge amesema, "Kumekuwa na shida katika kuwachangamsha watoto kutokana upungufu wa wafanyakazi na bajeti hairuhusu kununua  vifaa hivi."
Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI, Profesa Mohamed Janabi amesema amefurahishwa na msaada huo na kukaribisha wadau wengine wajitokeza kuchangia nguvu ambazo Serikali inaweka katika kuboresha huduma za afya katika taasisi hiyo.

Kimbunga Harvey: Watu 2,000 waokolewa kutoka kwa mafuriko Houston, Marekani

Maafisa karibu 3,000 wa idara ya kulinda bahari wanasaidia katika uokoaji Houston na viunga vyakeHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionMaafisa karibu 3,000 wa idara ya kulinda bahari wanasaidia katika uokoaji Houston na viunga vyake
Watu takriban 2,000 wameokolewa kutoka kwa mafuriko katika mji wa Houston na viunga vyake, huku kimbunga Harvey kikiendelea kusababisha mvua kubwa sana maeneo ya jimbo la Texas.
Kumekuwa na ripoti za kutokea kwa vifo pamoja na magari kadha kuzidiwa na nguvu za maji.
Hata hivyo, uchunguzi bado unaendelea, afisi ya liwali mkuu wa wilaya ya Harris, Darryl Coleman amesema.
Gavana wa Texas Greg Abbott ameambia wanahabari kwamba hawezi kuthibitisha vifo vinavyodaiwa kutokana na mafuriko hayo.
Idara ya Taifa ya Hali ya Hewa (NWS) imesema hali ambayo inashuhudiwa katika eneo hilo haijawahi kushuhudiwa awali.
Idara hiyo imesema kulitokea mafuriko ya ghafla eneo la katikati mwa mji wa Houston, na uchukuzi umetatizika.
Vyumba vingi vya kutoa hifadhi wakati wa majanga vimefunguliwa, ukiwemo ukumbi mmoja wa mikutano.
Gavana Abbot amesema barabara karibu 250 zimefungwa Texas na kwamba ameiomba serikali kuu itangaze janga katika wilaya 19, ombi ambalo limeidhinishwa na Rais Donald Trump.
"Tutaendelea kupokea mvua kubwa," amesema gavana huyo.
Flooded downtown Houston is seen from a high rise building along Buffalo BayouHaki miliki ya pichaTWITTER/@CAROLEENAM/REUTERS
NWS awali walisema walikuwa wamepokea taarifa za vifo vitano, lakini wamesema wameweza kuthibitisha kifo cha mtu mmoja pekee eneo la Houston.
Kufikia sasa, watu wawili wamethibitishwa kufariki tangu kimbunga hicho kilichofika maeneo ya bara, katika wilaya ya Aransas, ambapo Rockport ndio mji mkuu, mtu mmoja alifariki baada ya nyumba yake kushika moto Ijumaa usiku.
Na eneo la Houston, mwanamke mmoja alifariki akiendesha gari katika barabara zilizokuwa zimefurika maji Jumamosi.
Meya wa Houston Sylvester Turner amewashauri wakazi kutopigia simu maafisa wa huduma za dharura ila tu iwapo maisha yao yanatishiwa na wanahitaji kuokolewa kwa dharura.
"Msiingie barabarani. Msifikirie kwamba kimbunga kimepita," amesema.
Mjini Washington, ikulu ya White House imesema Rais Trump atazuru Texas Jumanne kutathmini uharibifu uliosababishwa na kimbunga hicho.
Bw trump alikuwa amesema awali kwamba angezuru eneo hilo haraka iwezekanavyo lakini kwa kuhakikisha kwamba hatatatiza juhudi za uokoaji.
A vehicle partially submerged by floodwaters in HoustonHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionMaafisa wa hali ya hewa wamesema vifo vingi hutokea magari yanaposombwa na maji
Hurricane Harvey August 27, 2017 in HoustonHaki miliki ya pichaAFP
Image captionHouston ni moja ya miji yenye watu wengi zaidi Marekani
Kufikia saa nane adhuhuri saa za Texas Jumapili, NWS walisema mji wa Houston ulikuwa umeandikisha mvua ya kina cha sentimeta 64.8 (inchi 25.50) kwa mwezi Agosti, na kuufanya kuwa mwezi wenye mvua kubwa zaidi katika historia ya mji huo.
The path of Harvey

Uharibifu wa Kimbunga Harvey Marekani

Brad Matheney akimsaidia mtu mwenye kiti cha magurudumu GalvestonHaki miliki ya pichaAFP
Image captionKimbunga hicho kimesababisha mafuriko katika maeneo mengi
Kimbunga Harvey kilifika maeneo ya Marekani bara Ijumaa jioni na kusababisha mvua kubwa na upepo mkali.
Upepo wa kasi ya hadi 130mph (215 km/h) ulipiga maeneo ya pwani ya Texas.
Kimbunga hicho ndicho kibaya zaidi kuwahi kupiga maeneo ya Marekani bara katika kipindi cha miaka 13 na kimesababisha uharibifu mkubwa maeneo hayo.
Mji wa Rockport ni miongoni mwa maeneo yaliyoathiriwa zaidi. Magari na majumba yaliharibiwa katika uwanja wa ndege wa mji huo...
Destroyed vehicles and buildings at Rockport AirportHaki miliki ya pichaAFP
...sawa na ndege kadha ndogo.
A light plane sits upside down at Rockport AirportHaki miliki ya pichaAFP
Mji wa Rockport ulipigwa na kimbunga hicho usiku kucha.
A Rockport firefighter goes door to door on a search and rescue mission as he looks for people that may need helpHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
A woman walks away from a destroyed apartment buildingHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Jessica Campbell hugs Jonathan Fitzgerald (L-R) after riding out Hurricane Harvey in an apartment on August 26, 2017 in Rockport, TexasHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
A man tries to kick open a door of an apartment to find his friendsHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Wakazi wa mji wa pwani Corpus Christi pia waliathirika pakubwa. Nguvu za umeme zilikatika na eneo lote likajaa giza.
Stewart Adams, of San Marcos, Texas, battles the winds in Corpus Christi U.S. on 25 August, 2017Haki miliki ya pichaREUTERS
Local residents sit at the bar in the dark after a citywide power failure as Hurricane Harvey hit Corpus Christi, Texas, on August 25, 2017Haki miliki ya pichaAFP/GETTY IMAGES
A man walks near the bay waters as they churn from approaching Hurricane Harvey on August 25, 2017 in Corpus Christi, TexasHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
People walk through high winds in Corpus ChristiHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Jumamosi, wengi waliamka kupata barabara hazina watu na majumba yameharibiwa. katika baadhi ya maeneo, moto ulizuka.
Lakini uharibifu katika mji huo haukufikia uharibifu ulioshuhudiwa Rockport.
A burnt out house and cars that caught fire are seen after Hurricane Harvey hit Corpus Christi, Texas on August 26, 2017Haki miliki ya pichaAFP
A white SUV car is seen submergedHaki miliki ya pichaAFP
Ijumaa, kabla ya kimbunga kufika bara, watalii wanaopenda kufuatilia vimbunga walikuwa wamefika kwenye fukwe kujionea mawimbi na kupiga picha. Wengi baadaye walikimbilia maeneo salama.
A resident photographs the beach in Corpus ChristiHaki miliki ya pichaAFP/GETTY
Watu wengi walihama miji na biashara kufungwa kuzuia uharibifu.
Sign on a business reading Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Maafisa wameonya kwamba maeneo mengi yatashuhudia mafuriko mabaya katika kipindi cha siku chache zijazo.
Tayari kumetoka mafuriko Galveston.
People walk dogs through flooded streets as the effects of Hurricane Henry are seen August 26, 2017 in Galveston, TexasHaki miliki ya pichaAFP
Na mjini Port Lavaca.
Floodwaters outside a house in Port LavacaHaki miliki ya pichaREUTERS
Mjini San Antonio, wanyama pia walihamishwa...
Horses are evacuated in San AntonioHaki miliki ya pichaAFP/GETTY
Wakazi wa Houston - mji wa nne kwa wingi wa watu Marekani - wamekuwa wakijiwekea chakula cha akina. Rafu nyingi katika maduka ya jumla hazina bidhaa.
Woman looks over bare refrigerator shelves in a Walmart in HoustonHaki miliki ya pichaREUTERS
Kimbunga Harvey kimeathiri sana uchimbaji wa mafuta Ghuba ya mexico pamoja na uchukuzi wa ndege.
Asilimia 45 ya usafishaji wa mafuta Marekani hufanyika katika ghuba hiyo.
Tangi la mafuta liliharibiwa akribu na mji wa Seadrift, katika wilaya ya Calhoun.
An oil tank damaged by Hurricane Harvey is seen near Seadrift, Texas, August 26, 2017Haki miliki ya pichaREUTERS
Picha za Nasa zimeonesha kimbunga hicho kilivyoonekana kutoka anga za juu.
This NASA image from August 25, 2017, taken by NASA astronaut Jack Fischer shows Hurricane Harvey (top) from the cupola module aboard the International Space Station.Haki miliki ya pichaAFP/NASA