Wednesday, August 9

MALIPO YA KODI YA ARDHI PAMOJA NA TOZO NYINGINE SASA KULIPWA KIELEKTRONIKI.


Na ELIAFILE SOLLA 

Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imeanza rasmi kutumia mfumo wa kielektroniki wa Government electronic Payment Gateway (GePG) katika makusanyo ya kodi ya pango la ardhi pamoja na tozo nyingine zinazotokana na sekta ya ardhi nchini. 

Mfumo huu utamrahisishia mwananchi kulipa kodi ya pango la ardhi popote alipo, ikiwa ni pamoja na kulipia tozo nyingine mbalimbali za sekta ya ardhi. Pia mfumo wa GePG, utamuwezesha mwananchi au mmiliki wa kipande cha ardhi, kujua anadaiwa kiasi gani cha kodi ya pango la ardhi na kulipia popote alipo bila kusumbuka kufuata huduma hizo katika vituo vya makusanyo. 

Majaribio ya ukusanyaji kodi ya pango la ardhi kwa kutumia mfumo wa kielektroniki yalifanywa katika mikoa ya Dar es Salaam na Pwani, baada ya mafanikio makubwa kuonekana elimu ikatolewa kwa watendaji wote wa sekta ya ardhi katika Halmashauri zote za mkoa wa Dar es salaam kabla ya zoezi hilo kuhamishiwa mikoani. 

Mwananchi yeyote anayemiliki kiwanja au shamba lililopimwa na kuwa na hati, ataweza kutumia simu yake ya mkononi kujua kiasi cha kodi ya pango la ardhi anachodaiwa na kukulipa kwa kutumia simu yake ya mkononi pia. 

Kwa zile huduma nyingine za sekta ya ardhi ambazo zinahusisha malipo kama vile upekuzi katika daftari la msajili (official serach), mwananchi atapaswa kutembelea ofisi za Wizara ya ardhi zilizo katika eneo lake na kupatiwa makadirio ya kulipia huduma husika pamoja na namba ya malipo itakayomuwezesha kulipia aidha kwa njia ya benki au simu ya mkononi. 

Kwa sasa kikosi kazi kinachotoa mafunzo juu ya matumizi ya mfumo huu kimeshaanza kuelemisha mikoa mingine baada ya kupata mafanikio mazuri katika mkoa wa Dar es Salaam. Lengo kubwa la kutumia mfumo huu ni kuongeza ufanisi katilka ukusanyaji wa maduhuli ya serikali pamoja na kurahisisha ulipaji kodi ya pango la ardhi nchini.


Wataalamu kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi wakitoa elimu jinsi ya kutumia mfumo wa Government electronic Payment Gateway kwa watendaji wa Halmashauri ya Kinondoni. 


Watendaji wa Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya ya Kinondoni wakipewa mafunzo jinsi mfumo mpya wa ukusanyaji maduhuli ya Serikali utakavyokuwa unatumika.
 

Elimu ya jinsi ya kutumia mfumo mpya wa kielektroniki ikitolewa kwa watendaji wa manipaa ya Temeke jijini Dar es Salaam. 

MAMLAKA YA MAJI SAFI NA USAFI WA MAZINGIRA MJINI MOSHI (MUWSA) YAWASOGEZA HUDUMA YA MAJI KATIKA KIJIJI CHA NEWLAND WILAYANI MOSHI.


Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji,Prof Kitila Mkumbo akitia saini katika kitabu cha wageni alipotembelea Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA) kwa ajili ya uzinduzi wa mradi wa Maji katika kijiji cha Newland. 
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi,(MUWSA) Joyce Msiru akizungumza wakati wa utamburisho wa wajumbe wa Bodi ya Mamlaka hiyo kwa katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji,Prof Kitila Mkumbo alipotembelea Mamlaka hiyo. 
Baadhi ya Wajumbe wa Bodi ya Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa MAzingira mjini Moshi (MUWSA) .
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA) Joyce Msiru akimkaribisha Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji Prof,Kitila Mkumbo katika eneo la Shabaha kwa ajili ya uzinduzi wa tanki la Maji linalohifadhi maji kwa ajili ya wakazi wa kijiji cha Newland.
Tenki la kuhifadhia Maji kwa ajili ya Mradi wa Maji yanayosambazwa katika kijiji cha Newland.
Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Utalii,Prof Kitila Mkumbo akizindua tenki la Maji katika eneo la Shabaha kwa ajili ya wakazi wa kijiji cha Newland.kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakuruenzi wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi,(MUWSA) Prof Faustine Bee na kushoto mwa katbu Mkuu ni Mjumbe wa Bodi hiyo ,Bi Hajira Mmambe.

Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji ,Prof Kitila Mkumbo akiwabebesha maji wawakilishi wa wananchi wa kijiji cha Newland mara baada ya kuzindua mradi wa maji katika eneo hilo.
Diwani wa kata ya Mabogini kilipo kijiji cha Newland ,Emanuel Mzava akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa mradi wa maji katika kijiji hicho ambacho wakazi wake wamekuwa wakikabiliwa na changamoto ya upatikanaji wa huduma ya maji katika kijiji hicho. 

Baadhi ya Viongozi wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Maji safi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA) wakiwa katika uzinduzi huo.
Baadhi ya wafanyakazi wa MUWSA wakiwa katika uzinduzi huo.
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi ,(MUWSA) Joyce Msiru akitoa taarifa ya Mamlaka hiyo kwa Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji ,Prof ,Kitila Mkumbo (Hayupo pichani) alipofanya uzinduzi wa mradi wa maji katika kijiji cha Newland.
Mkurugenzi MUWSA ,Joyce Msiru akikabidhi taarifa kwa katibu Mkuu Wizara ya maji na Umwagiliaji Prof Kitila Mkumbo. 
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA) Prof ,Faustine Bee akizungumza kaika uzinduzi huo.
Mjumbe wa Bodi a Wakurugenzi wa MAMLAKA YA mAJI SAFI NA uSAFI WA mazngira mjini Moshi(MUWSA) Hajira Mmambe akisalimia wakati wa uzinduzi wa mradi wa maji wa katika kijiji cha Newland.
Katibu tawala mkoa a Kilimanjaro na Mjumbe wa Bodi ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA) Mhandisi ,Aisha Amour akitoa salamu wakati wa uzinduzi wa mradi huo. 
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Moshi ,Raymond Mboya akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi huo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii,Prof Kitila Mkumbo akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi wa maji safi katika kijiji cha Newland kilichopo kata ya Mabogini wilaya ya Moshi. 
Mmoja wa wakazi wa kijiji cha Newland akicheza kwa furaha baada ya maji kuanza kutoka katika kijiji hicho.
Kikundi cha Burudani cha Msanja kikitoa burudani wakati wa uzinduzi wa mradi wa majisafi katika kijiji cha Newland kilichopo kata ya Mabogini wilaya ya Moshi.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,Kanda ya Kaskazini.

ZIARA YA MANAIBU WAZIRI UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA WA JULIUS NYERERE NA MAMLAKA YA BANDARI TANZANIA


 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati), akizungumza na Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Edwin Ngonyani (kushoto), wakati wa ziara ya kutembelea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, lengo ikiwa ni kukagua masuala mbalimbali ikiwemo Ulinzi, Usalama, Miundombinu,Utolewaji wa visa,udhibiti uingiaji wa dawa za kulevya  na uingiaji na utunzaji kumbukumbu za watalii wanaoingia nchini.Kulia ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Mhandisi Ramo Makani. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akimuuliza swali Mkuu wa Uhamiaji Kituo cha Uwanja wan DEGE wa Kimataifa Julius Nyerere, Fulgence Mutarasha,  wakati wa ziara iliyowajumuisha Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhandisi Ramo Makani na Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Edwin Ngonyani, lengo ikiwa ni kukagua masuala mbalimbali ikiwemo Ulinzi, Usalama, Miundombinu,Utolewaji wa visa, uingiaji na utunzaji kumbukumbu za Watalii wanaoingia nchini.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
 Mkuu wa Kitengo cha Uzingatiaji Viwango wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege nchini, Paul Rwegasha, akifafanua jambo wakati wa ziara iliyojumuisha  Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Edwin Ngonyani(kushoto), Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhandisi Ramo Makani (wapili kushoto)  na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(kulia).Lengo la ziara hiyo ni kukagua masuala mbalimbali ikiwemo Ulinzi, Usalama, Miundombinu,Utolewaji wa visa, uingiaji na utunzaji kumbukumbu za Watalii wanaoingia nchini.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi 
 Meneja Huduma za Abiria wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere, Damas Temba, akielezea jinsi huduma ya kukagua mizigo inavyofanyika katika sehemu ya mizigo wakati wa ziara ya Manaibu Waziri, Mhandisi Hamad Masauni (Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi), Mhandisi Ramo Makani(Wizara ya Maliasili na Utalii) na Mhandisi Edwin Ngonyani(Wizara ya UIjenzi, Uchukuzi na Mawasiliano), ikiwa na lengo kukagua masuala mbalimbali ikiwemo Ulinzi, Usalama, Miundombinu, Utolewaji wa visa, uingiaji na utunzaji kumbukumbu za Watalii wanaoingia nchini.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
CAP PIX 5
 Meneja Mradi Ujenzi wa Uwanja Mpya wa Ndege wa Kimataifa  wa Julius Nyerere, Ray Blumrick, akitoa maendeleo ya ujenzi wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Edwin Ngonyani(kulia), Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhandisi Ramo Makani(wapili kulia) na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (watatu kulia), lengo la ziara hiyo ni kukagua kukagua masuala mbalimbali ikiwemo Ulinzi, Usalama, Miundombinu, Utolewaji wa visa, uingiaji na utunzaji kumbukumbu za Watalii wanaoingia nchini.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
 Mkuu wa Kitengo cha Uzingatiaji Viwango wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege nchini,Paul Rwegasha, akifafanua jambo wakati wa ziara iliyojumuisha  Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Edwin Ngonyani (kushoto), Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhandisi Ramo Makani (wapili kushoto)  na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia).Lengo la ziara hiyo ni kukagua masuala mbalimbali ikiwemo Ulinzi, Usalama, Miundombinu, Utolewaji wa visa, uingiaji na utunzaji kumbukumbu za Watalii wanaoingia nchini.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi 
 Meneja Mradi Ujenzi wa Uwanja Mpya wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Ray Blumrick, akizungumza na Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni baada ya kumaliza kutembelea ujenzi huo.Lengo la ziara hiyo ni kukagua kukagua masuala mbalimbali ikiwemo Ulinzi, Usalama, Miundombinu, Utolewaji wa visa, uingiaji na utunzaji kumbukumbu za Watalii wanaoingia nchini.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
 Naibu Mkurugenzi Mamlaka ya Bandari Tanzania, Lazaro Twange (katikati), akiwaonyesha ramani ya bandari ya Dar es Salaam, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Mhandisi Ramo Makani(kulia) na Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni wakati wa ziara ya viongozi hao lengo ikiwa ni kukagua masuala mbalimbali ikiwemo Ulinzi, Usalama, Miundombinu, Utolewaji wa visa, uingiaji na utunzaji kumbukumbu za Watalii wanaoingia nchini.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Naibu Mkurugenzi Mamlaka ya Bandari Tanzania, Lazaro Twange,  akifafanua jambo kwa  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhandisi Ramo Makani(wapili kulia) na Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni (kulia), wakati wa ziara ya viongozi hao, lengo ikiwa ni kukagua masuala mbalimbali ikiwemo Ulinzi, Usalama, Miundombinu, Utolewaji wa visa, uingiaji na utunzaji kumbukumbu za Watalii wanaoingia nchini.Kushoto ni Mkuu wa Kikosi cha Polisi Bandarini,Matanga Mbushi.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi 

IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI-WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

NEWS ALERT: MAKONDA, TEF NA RUGE WAMALIZA TOFAUTI ZAO


Video Courtesy of MCL

Na Georgina Misama, MAELEZO
Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda na Mkurugenzi wa Uzalishaji na Vipindi wa Clouds Media Group Ruge Mutahaba wamekubaliana kumaliza tofauti zao na kuvitaka vyombo vya habari kuanza kuandika habari zinazomuhusu Mkuu wa Mkoa kama ilivyokuwa awali.
Akiongea na waandishi wa habar jijini Dar es salaam leo, Mwenyekiti wa TEF Theophil Makunga alisema kwamba wiki chache zilizopita viongozi wa jukwaa la Wahariri walikutana na Mkuu wa Mkoa ili kumsikiliza na kufikia muafaka kwa suala la Vyombo vya Habari kususia kazi zake.

“Adhabu tuliyoitoa haikuwa na muda maalum (Open ended) hivyo tusingeweza kuendelea kukaa katika mgomo huu kwani tayari muda mrefu ulishapita. Tulipoenda ofisini kwa Mkuu wa Mkoa, alitueleza mazingira yaliyopelekea yeye kufanya tukio lile Clouds na kwa pamoja tulikubaliana kuyamaliza kwani yaliyopita si ndwele sasa tugange yajayo”. Alisema Makunga.
Makunga alisema haikuwa rahisi kufikia muafaka huo, kwani walifanya majadiliano na Makonda zaidi ya mara moja hatimaye Alhamisi ya wiki iyopita walihitimisha mazungumzo yao na wote walikubaliana kufanya mkutano huu wa pamoja ili kuujulisha Umma kukoma kwa kifungo cha vyombo vya habari katika kuripoto kazi za Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam.
Kwa upande wake Makonda alisema kwamba waandishi wote wanafahamu upendo wake kwa vyombo vya habari, jambo ambalo kamwe halitokaa libadilike. Amekuwa tayari kukaa mezani na viongozi wa TEF kwa maslahi ya Umma kwani wote wanafanya kazi moja kwa maendeleo ya Taifa.
“Tumekubaliana na viongozi wenzangu baada ya kuja ofisini kwangu, kunisikiliza na kunihoji maswali sio chini ya masaa matatu. Mwishoni waliona hakuna haja ya kuendelea na kifungo kwa manufaa ya watanzania, pande zote mbili tumejifunza kutokana na tukio lile, na hatutegemei jambo lile kujirudia tena” Alisema Makonda
Akiongelea mahusiano yake na  Mutahaba, Mkuu wa Mkoa alisema kwamba wao ni marafiki wa siku nyingi nje ya kazi, na kwa heshima ya Mhe. Rais, wamekubali kuweka tofauti zao pembeni, kusameheana na kupendana ili kuendelea kufanya kazi kwa kushirikiana kama ilivyokuwa awali.
Akitolea ufafanuzi jambo hilo, Mutahaba alisema kwamba kwake yeye anajiona kama abiria katika lori ambalo Rais ni dereva, anajua tofauti zao na Makonda zimekuwa kero kwa Mhe. Rais hivyo bila kujali kauli yoyote ya Makonda, haoni sababu ya kuendeleza tofauti zao.
“Mhe. Rais ameshasema jambo hili liishe na tuendee na kazi, sioni sababu ya kuendelea kwa heshima ya kauli yake. Kwangu mimi haijalishi kama Makonda ameomba radhi au hajaomba, lakini naona umuhimum wa kulimaliza jambo hili ili kuruhusu mambo mengine yaendelee kwa maslahi ya Taifa. Alisema Mutahaba.
Takribani miezi 5 sasa imepita toka TEF kutoa tamko la kususia kazi za Mkuu wa Mkoa wa Dar es saam Paul Makonda ikiwa ni adhabu baaba ya Makonda kudaiwa kuvamia kituo cha utangazaji cha Clouds.   

TEF WAONDOA ZUIO LA KUTOKUTOA HABARI ZA MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM, MAKONDA.


JUKWAA la wahariri Tanzania (TEF) laondoa zuio la kutokutoa habari za Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Mkonda jijini Dar es Salaam leo.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo,
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Theophil Makunga amesema kuwa " Mgogoro huu kati ya Jukwaa la wahariri wa habari na tasnia ya habari  na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Mkonda umefika mwisho tunarusu sasa habari zake ziandikwa  mgogoro ule uliokuwepo yaliyopita si ndwele tugange yajayo"

Tamko hilo la TEF limekuja mara baada ya Machi 22 mwaka huu kutoa tamko lao kwa vyombo vya habari  lililokuwa likisema "Zinalaani vikali vitendo vya Mkuu wa Mkoa katika kuvamia chombo cha habari cha Clouds Media akiwa ameambatana na Askari wenye silaha.
 Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Theophil Makunga akizungumza na waandishi wa habari pamoja na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari jijini Dar es Salaam kwaajili ya kuondoa adhabu aliyopewa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ambayo alikua nayo ikiwa Jukwaa hilo la wahariri lilimfungia kwa  kutokutoa habari yoyote kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi wa Vipindi na uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba.
Kulia ni Mkurugenzi wa Vipindi na uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba akizungumza na waandishi wa  habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa Jukwaa la wahariri kuondoa zuio kutotoa habari zamkuu wa ,Mkoa wa Dar Es Salaam leo.
Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati Jukwaa la wahariri Tanzania (TEF) wakiondoa zuio la kutokutoa habari yoyote kwenye chanzo cha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kwenye vyombo vya habari  sasa kuanzia leo habari za mkuu wa Mkoa wa Mkoa zitakuwa zikitoka kwenye vyombo vya habari. katikati ni Makamu Mwenyekiti wa Jukwaa la wahariri Tanzania(TEF), Deodatus Balile  na kushoto ni Mkurugenzi wa Vipindi na uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba.
Katikati ni  Makamu Mwenyekiti wa Jukwaa la wahariri Tanzania(TEF), Deodatus Balile  akizungumza katika mkutano wa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda na kushoto ni Mkurugenzi wa Vipindi na uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba.
 Picha na Avila Kakingo, Blog ya Jamii.

MGOMBEA URAIS TFF FREDRICK MWAKALEBELA AJA NA MAMBO KUMI YA KUINUA SOKA NCHINI


Mgombea Urais katika Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini, Fredrick Mwakalebela ametaja mambo kumi atakayo fanya katika kuinua mpira hapa nchini kama atapata ridhaa ya kuwa Rais wa TFF.
Akizungumza na Waandishi wa Habari wakati uzinduzi wa kampeni yake Mwakalebela amesema kuwa kwa kwanza ataanza na Utawala bora kwa Kuweka misingi ya wazi katika mapato na matumizi ya TFF, Kuzifanya kamati za TFF kuwa huru na kufanya kazi bila kuingiliwa, kuiangalia upya Agenda ya kupunguza idadi ya wajumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF ili tuweze kupanua wigo wa wadau wa mpira wa miguu kutuwakilisha kwa wingi katika mkutano mkuu.

Amesema kuwa pia ataweza kusimamia matakwa ya katiba ya shirikisho la mpira wa miguu Tanzania kwa kufanya vikao na mikutano inayotambuliwa kikatiba, kuwa na vyombo imara vya usimamizi ndani ya shirikisho ili kuleta matokeo chanya yenye ufanisi katika soka.

Mwakalebela amesema ataweza kusaidia Timu za Taifa ,wanaume,Wanawake na Vijana kwa Kuwa na makocha wenye viwango vya juu ikiwa ni pamoja na Kurudisha hamasa kwa watanzania kuzipenda timu za Taifa kwa kuongeza idadi kubwa za wachezaji wa ndani kucheza nje ya nchini pamoja na kucheza FIFA date zote na Kuziweka timu kambini kwa wakati
idha katika mpango huu wa pili ataweza Kuanzisha na kusimamia Academy nyingi Tanzania kwa kuhakikisha timu zinapata mechi nyingi za kirafiki na kimataifa kuandaa mashindano ya kimataifa Kuwa na mfadhili wa kugharimia mpango kazi wa timu za Taifa.

Katika mpango wake wa tatu Mwakalebela amesema atashirikiana naVilabu kwa Kupitia upya mikataba ya sasa ili kuiboresha na kuleta tija katika vilabu pia ameadhimia kuongeza idadi ya mashindano ili kuongeza ufanisi kwa wachezaji na Taifa kwa ujumla.

Ameongeza ataweza kuboresha kanuni zetu kuwa zenye tija na ufanisi hili kuongeza mapato ya vilabu kwa kuifanya Bodi ya Ligi kuwa huru nakuweza kuboresha viwanja vya mashindano pamoja na kuongeza idadi ya wadhamini kwa kufanya mpira kuwa starehe na biashara.

Katika kusaidia Vyama vya Soka vya Mikoa Mwakalebela amesema kuwa atafanikisha kupatikana kwa vitendea kazi kama mipira,kompyuta,printers na thamani za ofisini na kuwawezesha kuwapatia Wadhamini wa kudumu kwa ajili ya ofisi kujiendesha na kuwapatia ruzuki za kila mwezi kwa shughuli za chama kwa kuongeza idadi ya mashindano mikoaniKuboresha viwanja na ofisi za mikoani kuwapatia viongozi mafunzo ya kuwajengea uwezo ndani na nje ya nchi.

Katika kusaidia Vyama Shiriki Waamuzi,Tiba Michezo,Waamuzi,Tiba Michezo,Makocha,Wanawake,Sputanza kwa Kutoa Mafunzo ya ndani na nje ya nchi ili kuwajengea uwezo, Kuwapatia ruzuku kwa ajili ya shughuli za kila siku na kuwapatia wadhamini kwa kuwapatia vitendea kazi.

Katika kuboresha Sekretarieti Mwakalebela amesema atawezesha Sekretarieti kuwa na watendaji wenye weledi na uwezo katika maeneo yao ya kazi kwa Kuajiri watendaji kwa kuzingatia sifa na vigezo katika nafasi husika.
Kuongeza uadilifu katika utendaji kazi.
Kusimamia watendaji waweze kutimiza wajibu wao kwa kuzingatia uhitaji wa wadau wa soka nchini.
Kuwajengea uwezo kwa kuwapatia mafunzo ndani na nje ya nchi.
Katika Mahusiano na Wadau Mwakalebela amesema
Ili kupata mafanikio chanya katika maendeleo ya soka ni lazima kuhakikisha  wadau wanashirikishwa ipasavyo, hivyo nitahakikisha natambua nafasi ya wadau na kushirikiana nao,Serikali pamoja na Vyombo vyake,Wachezaji wa sasa na wale wa zamani,Wanahabari, Taasisi, Mashirika na Kampuni mbalimbali,Mashabiki na wapenzi wa mpira,Wadhamini na wafadhili,Wamiliki wa viwanja vya michezo, Watanzania wote kwa ujumla.
Katika uwekezaji wa Kitega Uchumi Mwakalebela ametaja kuwa Mafanikio ya mpira yanahitaji rasilimali fedha, kwa kulitambua hilo, nitahakikisha kunafanyika uwekezaji wa jengo la kisasa la kitega uchumi katika uwanja wa kumbukumbu ya Karume ili kuweza kusaidia ufanikishaji.
Amesema Uwezeshaji wa ruzuku kwa wanachama wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania,Kusaidia maendeleo ya mpira wa miguu katika ngazi mbalimbali kutokana na uhitaji,Mafunzo kwa wanachama,Vitendea kazi kwa wanachama,Uboreshaji wa ofisi za TFF kuwa zakisasa zaidi.

Katika kuboresha Bodi ya ligi Mwakalebela amesema Bodi ya Ligi itakuwa huru kwa kuijengea uwezo kwa kuongeza wafadhili na Kuwa na Mpango kazi ambao utasaidia kuifanya bodi hiyo kufanya kazi kwa ufanisi pasipo kuingiliwa.
Katika kuboresha Miundombinu Mwakalebela amesema kuwa kwa Kushirikiana na wamiliki wa viwanja ataweza kuviboresha hili kuwa na nyasi bandia katika kila kanda kwa kuwa na Viwanja vyenye hadhi na sio kuta tu peke yake.

NANE NANE

MWENYEKITI WA BODI YA NHIF MHE. MAKINDA ATEMBELEA BANDA LA NHIF KATIKA MAONESHO YA NANENANE DODOMA NA KUSISITIZA UMUHIMU WA KILA MWANANCHI KUWA NA BIMA YA AFYA.


Mwenyekiti wa Bodi ya NHIF Mhe. Anne Makinda ametembelea Maonesho ya Nanenane katika Viwanja vya Nzuguni Mjini Dodoma ambapo alikuwa mgeni rasmi wa siku hiyo. Mhe. Makinda alisisitiza umuhimu wa kila mtanzania kuwa na bima ya afya ili kuwa na uhakika wa matibabu na kuweza kutimiza majukumu yake ya kila siku na kuepukana na umaskini.

Alisema ‘…. tunajua kuwa katika zama hizi tunatakiwa kuchapa kazi kama Mhe. Rais wetu anavyotuhimiza, lakini ili tuweze kuendana na kasi hii hatuna budi kuwa na uhakika na afya zetu na Serikali imetuletea utaratibu huu wa bima ya afya ambao ni rahisi kwa kila mtu kujiunga na kuwa na uhakika wa matibabu pindi anapougua”

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF Bw. Bernard Konga amesema NHIF imejipanga kutoka na kwenda kuwafuata watu walipo ili kuweza kuwasajili na huduma za Mfuko huo. Alisema kwa sasa Mfuko unafanya kampeni ya uhamasishaji wa huduma ya bima ya afya kwa watoto walio chini ya miaka 18 ijulikanayo kama TOTO AFYA KADI. “Mfuko umeanza kufanya usajili kwa wingi katika maeneo mbalimbali karibu na watu walipo ambapo kila mtoto anachangiwa sh. 50,400 tu kwa mwaka” alisema Bw. Konga.

Huduma hii ya TOTO AFYA KADI imezinduliwa rasmi na Waziri wa Afya Mendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wiki iliyopita ambaye alisema kuwa watoto ambao ni asilimia 51 ya watanzania wote wanahitaji kuwa na uhakika wa matibabu na alihimiza kuweka mikakati madhubuti kuhakikisha watoto hawa wanapata huduma hiyo.

Naye Meneja wa NHIF Mkoani Dodoma, Bi. Salome Manyama amesema wazazi na walezi wamepata mwitikio na kufika kusajili watoto wao katika huduma ya TOTO AFYA KADI katika maonesho hayo. Ameongeza kusema kuwa umma uko tayari na wamejipanga kuendeleza kampeni hiyo katika maeneo ya karibu zaidi na wananchi.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya NHIF Mhe. Anne Makinda akisaini
kitabu cha wageni kwenye banda la NHIF jijini Dodoma alipotembelea maonesho ya Nanenane yanayofanyika kwenye viwanja vya Nzuguni jijini humo.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF Bw. Bernard Konga na viongozi wengine wa NHIF wakimsikiliza kwa makini Mwenyekiti wa Bodi ya NHIF alipotembelea banda hilo Jijini Dodoma kwenye maonesho ya Nanenane.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa NHIF Mhe. Anne Makinda akisalimiana na mmoja wa maofisa wa NHIF waliokua wakishiriki maonesho ya Nanenane Jijini Dodoma.

Meneja wa NHIF mkoani Dodoma Bi. Salome Manyama akielezea jambo kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa NHIF Mhe. Anne Makinda ambaye
pia alitembelea banda hilo kama mgeni Rasmi wa maonesho hayo ya Nanenane yaliyokua yakifanyika jijini Dodoma kwenye viwanja vya Nzuguni.