Saturday, September 16

WAZIRI MKUU AZINDUA MIONGOZO YA MAFUNZO KWA WAHITIMU NA WANAGENZI


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amezindua miongozo ya Kitaifa ya Kusimamia Mafunzo ya Vitendo kwa  Wahitimu (Internship Guidelines) na Mafunzo ya Uanagenzi (Apprenticeship Guidelines) mahala pa kazi, leo (Jumamosi, Septemba 16) mjini Dodoma. 
Amesema miongozo hiyo inalenga kuongeza ari kwa waajiri na wadau wengine kushiriki katika  kutoa mafunzo ya kukuza ujuzi na stadi za kazi ili kuhakikisha wahitimu na wanagenzi wanapata stadi  za kazi na ujuzi stahiki wa kuajirika au kujiajiri. 
Waziri Mkuu amesema miongozo hiyo ambayo inakwenda kuboresha mafunzo ya uanagenzi na kwa wahitimu itachochea ukuzaji wa viwanda na kupunguza ukosefu wa ajira kwa watanzania hususan vijana. 
Amesema Serikali imekua ikipokea malalamiko kutoka kwa waajiri kwamba wahitimu wengi wa ngazi mbalimbali za mafunzo wanaingia katika soko la ajira wakiwa hawana ujuzi unaohitajika na hivyo waajiri kulazimika kutafuta wafanyakazi kutoka nje ya nchi.

Amesema baada ya kupokea malalamiko hayo Serikali, Waajiri na Wafanyakazi na walikubaliana kuimarisha mfumo wa utoaji mafunzo yanayofanyika maeneo ya kazi ili kuhakikisha mafunzo yatolewayo maeneo ya kazi yana ubora unaohitajika. 
“Kuimarisha uwezo wa nguvu kazi ya Taifa ni muhimu na njia bora ni kuboresha utoaji mafunzo kwa vitendo mahali pa kazi kwa kuweka miongozo bora itakayowaongoza wadau wote wakiwemo Serikali, Waajiri, Wafanyakazi na Vijana kutoa Mafunzo.” 
Waziri Mkuu amesema Rais Dkt. John Magufuli alipoanza kuweka malengo ya ujenzi wa viwanda, mbali na kuwezesha kukua kwa kilimo na kuongeza thamani mazao, pia alilenga kupanua wigo wa ajira za viwandani ambapo kiwanda kinaweza kuajiri watu zaidi ya 1000.

Amesema miongozo hiyo itasaidia kuboresha mazingira ya biashara nchini kwa kuhakikisha Taifa linakuwa na nguvu kazi yenye weledi wa kutosheleza mahitaji ya soko la ajira na kuvutia wawekezaji wa ndani na nje ya nchi. 
Kwa upande wake Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Bi. Jenista Mhagama amesema miongozo hiyo inaweka mfumo madhubuti wa kuandaa, kutekeleza, kusimamia, kuratibu na kufuatilia mafunzo husika mahala pa kazi. 
Pia miongozo hiyo inabainisha majukumu ya wadau muhimu wa mafunzo hayo ambayo ni pamoja na kuweka bayana utaratibu wa kugharamia mafunzo ikiwa ni pamoja na kushirikisha Serikali, waajiri na wazazi. 
“Miongozo imebainisha majukumu ya wadau katika kutoa mafunzo ambao ni Serikali, waajiri, taasisi za mafunzo, taasisi za mitaala na wanagenzi na wahitimu. Pia imebainisha vigezo vya kuwapata washiriki wa mafunzo na muda wa mafunzo.” 
Pia miongozo hiyo imebainisha mfumo wa kitaasisi wa kuratibu na kuhakikisha ubora wa mafunzo kwa kuunda kamati ya Utatu wa Taifa ya kuratibu, kufuatilia tathmini ya mafunzo chini ya usimamizi wa Ofisi ya Waziri Mkuu.
  Baadhi ya washiriki wa uzinduzi  wa Miongozo ya Mafunzo Katika Maeneo ya Kazi uliofanywa na Waziri Mkuu kwenye ukumbi wa LAPF mjini Dodoma leo.
  Baadhi ya washiriki wa uzinduzi  wa Miongozo ya Mafunzo Katika Maeneo ya Kazi uliofanywa na Waziri Mkuu kwenye ukumbi wa LAPF mjini Dodoma 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi Mkurugenzi wa Shirika la Kazi Duniani (ILO) katika Nchi za Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi, Bibi Mary Kawar kitabu baada ya kuzindua Miongozo ya Mafunzo Katika Maeneo ya Kazi kwenye  ukumbi wa LAPF mjini Dodoma Septemba 16, 2017. Watatu kushoto ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana , Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama na wapili kulia ni Waziri wa Viwanda, Biashara na  Uwekezaji, Charles Mwijage. Kulia ni Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Tekinolojia, Mhandisi Stella Manyanya na kushoto ni Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Anthony Mavunde
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipozindua  Miongozo ya Mafunzo katika Maeneo ya Kazi kwenye ukumbi wa LAPF mjini Dodoma Septemba   16, 2017. Kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana,Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama. Wapili kulia ni Mkurugenzi wa Shirika la Kazi Dunia wa Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanbda na Burundi, Mary Kawar
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na viongozi walioshiriki katika  Uzinduzi wa  Miongozo ya mafunzo Katika Maenneo ya Kazi alioufanya  kwenye ukumbi wa LAPF mjini Dodoma Septemba 16, 2017.(Picha na Ofisi ya Wziri Mkuu)

SPIKA NDUGAI AZUNGUMZA NA WATUMISHI WA OFISI YA BUNGE MJINI DODOMA


\
 Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (wa pili kushoto) akizungumza wakati wa kikao cha pamoja na Watumishi wa Bunge kilichofanyika leo katika Ukumbi wa Pius Msekwa Mjini Dodoma. kulia ni katibu wa Bunge, Dkt. Thomas kashililah, Kamishna wa Tume ya Utumishi wa Bunge, Mhe. Magdalena Sakaya (wa pili kulia) na kushoto ni Kamishna wa Tume ya Utumishi wa Bunge, Mhe. Mary Chatanda
 Watumishi wa Ofisi ya Bunge wakimsikiliza Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (hayupo kwenye picha) wakati wa kikao cha pamoja cha Watumishi wa Bunge na Tume ya Utumishi wa Bunge kilichofanyika leo katika Ukumbi wa Pius Msekwa Mjini Dodoma.
 Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (wa pili kushoto) akizungumza wakati wa kikao cha pamoja na Watumishi wa Bunge kilichofanyika leo katika Ukumbi wa Pius Msekwa Mjini Dodoma. PICHA NA OFISI YA BUNGE

WANASOKA,WASANII BONGOFLEVA WAUNGANA KAMPENI YA UZALENDO KWANZA

KAMPENI ya Uzalendo Kwanza iliyoanzishwa na Wasanii wa Filamu nchini, a.k.a Bongo Muvi inazidi kupanua wigo wake baada ya kuongeza matawi yake kwa mikoa yote ya Tanzania huku ikipata wanachama wakongwe waliowahi kutamba ndani ya Soka hapa nchini. 

Akizungumza na wanahabari wakati akiwapokea wanachama wapya, Mwenyekiti wa Chama hicho, Steve Mengele 'Steve Nyerere' amesema kuwa, lengo la Chama hicho ni kuwafikia Watanzania wote kufahamu umhimu wa uzalendo, kuipenda nchi yako ikiwa ni pamoja na kushirikiana kikamilifu na Serikali ya awamu ya tano ya Rais Dkt John Pombe Magufuli katika kumuunga mkono wa kizalendo katika kuhakikisha Tanzania inasonga mbele kimaendeleo. 

"Taifa la wazalendo linaanzia darasani, tunawaomba walimu wote wawe wazalendo kufundisha darasani, manesi na madakatari wawe wazalendo kutoa huduma zao, uzalendo pia ni mhimu kusapoti vilabu vyetu vya soka na Timu ya Taifa,na Wasanii wetu wa muziki ni lazima wawe wazalendo kwa kuitangaza nchi yao kwa mambo ya Kizalendo," alisema Nyerere. 

Wacheza soka ambao wamejiunga na Uzalendo Kwanza ni; Mwanamtwa Kihwelo, Monja Liseki, Abdallah Kaburu, Dotto Mokili na wengine.Aidha Nyerere amewaasa wanachama hao na Watanzania wote kuunganisha nguvu ya pamoja ili kulinda kazi zao za sanaa sambamba na kuwafanya Watanzania kupenda vilvivyo vyao mfano, kazi za wasanii wa ndani ili kukuza kipato chao na kuinua uchumi wa nchi. 

Mbali na hao, msanii wa Bongo Fleva, atambulikae kwa jina la Ruby pia amejiunga na kampen ya Uzalendo Kwanza,Msanii huyo amepewa jukumu la kutunga nyimbo za Uzalendo na video zake ili kufikisha ujumbe kwa wananchi wote.

Katika hatua nyingine,Uongozi wa Uzalendo kwanza umetoa msaada wa vyakula mbalimbali na kiasi cha fedha tasilimu Laki tano kwa aliyewahi kuwa mpiga picha wa Magazeti ya Serikali (Habari Leo &Daily News),Athuman Hamis ambaye alipata ulemavu wa kudumu kufuatia ajali aliyoipata akiwa kwenye majuku yake ya Kazi ikiwa yapata miaka kumi sasa tangu kutokea kwa tukio hilo.

Steve Nyerere amemaliza kwa kuwaasa Wasanii wenzake kuendelea kuwa Wazalendo na kuwakumbusha kujiunga katika mifuko ya hifadhi ya kijamii,amesema kuwa mfuko wa hifadhi ya Jamii PPF wameanza kwa kuidhamini kampeni yao ya Uzalendo Kwanza,huku wakionesha utayari mkubwa wa kuwasaidia iwapo wataamua kuendelea kujiunga katika mfuko huo na ukawa mkombozi kwao.
Mmoja wa Mabalozi wa Kampeni ya Uzalendo Kwanza akiwasili kwenye mkutano,Athuman Hamis aliyewahi kuwa mpiga picha wa Magazeti ya Serikali (Habari Leo &Daily News), ambaye alipata ulemavu wa kudumu kufuatia ajali aliyoipata akiwa kwenye majuku yake ya Kazi ikiwa yapata miaka kumi sasa tangu kutokea kwa tukio hilo.
Mwenyekiti wa kampeni ya Uzalendo kwanza Steve Mengele almaarufu kwa jina la Steve Nyerere akimkabidhi bahasha yenye kiasi cha fedha shilingi laki tano pamoja na msaada wa vyakula mbalimbali kwa aliyewahi kuwa mpiga picha wa Magazeti ya Serikali (Habari Leo &Daily News),Athuman Hamis ambaye alipata ulemavu wa kudumu kufuatia ajali aliyoipata akiwa kwenye majuku yake ya Kazi ikiwa yapata miaka kumi sasa tangu kutokea kwa tukio hilo.
Mwenyekiti wa kampeni ya Uzalendo kwanza Steve Mengele almaarufu kwa jina la Steve Nyerere akimnyanyua Mzee Rajab Shabani mkazi wa Mburahati ambaye ni mlemavu wa miguu (kwa miaka mitano sasa),kumkalisha kwenye kiti cha matairi matatu (Wheel chair),ikiwa ni sehemu ya msaada uliotolewa na Wadau wa kampeni hiyo wakishirikiana na uongozi wa kampeni ya Uzalendo kwanza. 
Pichani kati ni Mwenyekiti wa kampeni ya Uzalendo Kwanza , Steve Mengele 'Steve Nyerere' akizungumza na Waandishi wa habari mapema leo jijini dar,wakati akiwapokea wanachama wapya walioamua kujinga na kampeni hiyo.Pichani kulia ni Mjumbe Halima Yahya na kushoto ni Misayo Ndumbagwe. 
Pichani kati (njano) Mwenyekiti wa kampeni ya Uzalendo Kwanza , Steve Mengele 'Steve Nyerere' akiwatambulisha wanamichezo wazalendo wa zamani katika Soka na Waigizaji wengie mahiri mbele ya Waandishi wa habari mapema leo jijini dar,walioamua kujiunga na kampeni hiyo ya Uzalendo Kwanza.
Pichani Kati ni Msanii wa bongofleva Hellen Majeshi a.k.a Ruby ambaye pia ametangazwa kujiunga na kampeni hiyo ya Uzalendo Kwanza. 

Baadhi ya Wasanii mbalimbali wa Bongo movie wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye mkutano huo na Waandishi wa Habari uliofanyika mapema leo,jijini Dar.

STEVE NYERERE: WASANII FUNGENI MIDOMO YENU, UZALENDO KWANZA


Wakimbizi 18 wa Burundi wauawa DR Congo

Baadhi ya wakimbizi wa BurundiHaki miliki ya pichaAFP
Image captionBaadhi ya wakimbizi wa Burundi
Maafisa wanasema kuwa takriban wakimbizi 18 wa Burundi wameuawa na vikosi vya usalama mashariki mwa taifa la Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo .
Wengi wengine wamejeruhiwa.
Maafisa wa DR Congo pamoja na wanajeshi wanadaiwa kuwafyatulia risasi wakimbizi hao walipokuwa wakifanya maandamano ya kupinga mpango wa kuwarudisha nyumbani.
Makumi la maelfu ya raia wa Burundi walitoroka taifa hilo wakati za wa ghasia za 2015 kufuatia hatua ya rais Pierre Nkurunziza kuwania muhula mwengine wa tatu.
Tanzania yatahadharisha wahalifu waliotoka Burundi
Utawala wa Burundi unasema kuwa ni salama kwa raia kurudi nyumbani .

''Wapenzi 20 wa jinsia moja'' wakamatwa Zanzibar

Wapenzi wa jinsia moja
Image captionWapenzi wa jinsia moja
Mamlaka ya kisiwani Zanzibar imewakamata watu 20 wanaotuhumiwa kushiriki katika mapenzi ya jinsia moja, kisa hicho cha hivi karibu kikitokea wakati wa msako dhidi ya watu wa jinsia moja katika kisiwa hicho cha Afrika mashariki.
Wanawake 12 na wanaume 8 walikamatwa kufuatia uvamizi wa polisi katika hoteli moja ambapo washukiwa hao walikuwa wakishiriki katika warsha kulingana na afisa mkuu wa polisi Hassan Ali.
''Ni kweli tuliweza kuwakamata kwa sababu tunashuku kwamba walikuwa wakishiriki katika mapenzi ya jinsia moja kitu ambacho ni kinyume na sheria kisiwani zanzibar na ni ukiukaji wa wa sheria za taifa la Tanzania'', alisema akiongezea kuwa polisi wataongeza doria zao dhidi ya makundi kama hayo.
Mapenzi ya jinsia moja ni uhalifu nchini Tanzania na ngono miongoni mwa wanaume ni hatia inayovutia kifungo cha kati ya miaka 30 jela na kifungo cha maisha.
Mamlaka ya Tanzania hivi majuzi ilifanya msako dhidi ya wapenzi wa jinsia moja, mnamo mwezi Septemba 2016 , serikali ilisitisha kwa muda miradi ya ukimwi ya wapenzi wa jinsia moja.
Mnamo mwezi Februari , serikali ilisitisha huduma za vituo 40 vya afya vya kibinafsi kwa madai kwamba vilikuwa vikitoa huduma kwa wapenzi wa jinsia moja.

Makombora ya Korea Kaskazini yanaweza kutungua ndege za abiria?

North Korean missile launchHaki miliki ya pichaAFP
Korea Kaskazini wanaporusha makombora kupitia anga ya Japan hadi kwenye bahari ya Pacific, makombora hayo hupitia anga ya kimataifa - juu ya eneo ambalo ndege za kubeba abiria na mizigo hupitia.
Ving'ora vilipolia Japan na kuwaonya raia watafute hifadhi, je, kuna uwezekano wa makombora ya Korea Kaskazini kugonga ndege iliyowabeba abiria?
Ni swali ambalo watu wamekuwa wakijiuliza kwani Pyongyang hurusha makombora yake bila kutoa tahadhari.
Uwezekano ni mdogo sana, lakini wataalamu wanasema kwamba ni jambo linaweza kutokea - kwamba kombora litungue ndege.
"Iwapo ndege ya abiria itagongwa na kombora, shinikizo za kuitaka Marekani na washirika wake wachukue hatua za kijeshi zitakuwa juu sana," anaonya Vipin Narang, profesa ambaye ni mtaalamu wa masuala ya Asia Kusini katika chuo kikuu cha teknolojia cha MIT.

Mambo yanavyoweza kwenda kombo

"Majaribio haya ya makombora yanaweza kuwa hatari kwa ndege za abiria na za mizigo," anakariri Ankit Panda, mhariri katika jarida la The Diplomat.
Korea Kaskazini huwa hawatangazi ni wakati gani watatekeleza makombora yao na yatapitia wapi.
Kawaida, nchi hutoa tahadhari kuhusu majaribio kama hayo na kufahamisha mashirika ya ndege pamoja na meli maeneo ambayo wanafaa kukwepa.
"Ni vigumu kupima hatari yenyewe hata hivyo," anasema Bw Panda. "Ni kiwango cha chini sana. Itakuwa ni kupima uwezekano wa vitu viwili vidogo kwa kiasi ukilinganisha na bahari au anga, vikikutana."
Hwasong missile at North Korean military paradeHaki miliki ya pichaAFP
Image captionKorea Kaskazini mara kwa mara huonesha makombora yake Pyongyang
Korea Kaskazini, sawa na nchi nyingine, hupokea takwimu na maelezo muhimu kuhusu safari za ndege.
Hivyo badi, wanasayansi wake wanaweza kuchunguza wakati wanataka kurusha makombora yao na kujua ni wapi hakutakuwa na ndege zinazopita.
"Pyongyang bila shaka wangetaka kupunguza hatari ya kutokea kisa kama hicho. Kando na jinsi watu wengine wanaweza kufikiria, hawawezi kutaka jambo kama hilo litokee. Watatafuta njia ambayo itapunguza sana hatari."
Lakini bado kuna hatari na hii inaweza kuzidishwa na mambo mawili:
  • kombora likose njia na kuelekea eneo lenye shughuli nyingi angani au baharini
  • kombora lisambaratike likiwa bado linapaa angani na kuachia vifusi
Pyongyang mara nyingi hurusha makombora yake kupitia sehemu ambayo ni nyembamba zaidi Japan na ambapo hawatarajii kuwe na ndege nyingi, anasema Narang.
Lakini hilo linategemea ufanisi wa majaribio yenyewe.
Kombora lililorushwa Ijumaa linaaminika kuwa aina ya Hwasong 12 ambalo majaribio yake ya awali yaliyofanywa na taifa hilo yalionyesha kiwango chake cha kufanikiwa ni kidogo.
"Kwa hivyo inawezekana sana kwamba mambo yaende kombo na kombora liingie katika eneo lenye shughuli nyingi."

Tahadhari

Ingawa uwezekano wa tukio kama hilo kutokea ni mdogo, mashirika ya ndege yamekuwa yakichukua tahadhari.
"Baadhi ya amshirika ya ndege yamekuwa yakibadilisha njia ya safari na kuepuka kupitia anga ya Korea Kaskazini na Hokkaido," anasema Ellis Taylor mtaalamu wa uchukuzi katika shirika la FlightGlobal.
Mapema Agosti Air France waliongeza maeneo yanayozunguka Korea Kaskazini kuwa miongoni mwa maeneo ambayo ndege zao hazifai kupitia.
Air France aircraftHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionAir France walibadilisha njia yao ya kuelekea Japan
"Uamuzi wao waliuchukua baada ya moja ya ndege zao kuwa umbali wa 100km (maili 62 ) kutoka kwenye kombora moja lililofanyiwa majaribio na Korea Kaskazini awali. Safari za ndege zao kwenda Tokyo na Osaka sasa zinachukua dakika 10 hadi 30 zaidi."
Visa kama vile kutunguliwa kwa ndege ya MH17 nchini Ukraine vina baada kwamba mashirika pia yanafahamu uwezekano wa ndege zao kutambuliwa kimakosa na kushambulia maeneo yenye mizozo ya kivita.
Hii ina maana kwamba hali ya wasiwasi ikiendelea kuchacha, mashirika zaidi ya ndege yatakwepa rasi ya Korea.

Balozi aomba kumpeleka Rais Magufuli Marekani

Rais John Pombe Magufuli wa Tanzania
Image captionRais John Pombe Magufuli wa Tanzania
Kaimu balozi wa Marekani nchini Tanzania Dkt Inmi Patterson amesema kuwa angependa kumpeleka rais John Pombe Magufuli nchini Marekani kwa ziara ya wiki tano.
Kulingana na gazeti la The Citizen nchini Tanzania, alitoa matamshi hayo mjini Dar es Salaam hivi majuzi wakati wa sherehe fupi ya kumkaribisha afisa wa maswala ya umma katika ubalozi huo Bi Bribille Ellis.
''Mwalimu Nyerere alitembelea Marekani miaka 1960 kwa ziara ya wiki tano.
Wiki tano ni wakati mrefu na aliweza kutembelea miji kadhaa...Ningependa kumpeleka rais Magufuli kwa ziara ya wiki tano nchini Marekani'', alisema na kuvutia kicheko kutoka kwa umma uliokuwepo.
Gazeti hilo lilimnukuu bi Patterson akisema kuwa katika uzoefu wa uongozi na programu za kubadilishana kama zile zilizotekelezwa na Mwalimu Nyerere 1960 zimefuatiliwa kwa sababu zilikuwa muhimu katika kuimarisha uhusiano kati ya Marekani na Tanzania.
Akimnukuu mtangazaji maarufu wa redio nchini Marekani, Edward Murrow, Bi Patterson alisema kuwa kwa uhusiano wa taasisi na mataifa kuimarika , lazima uanze katika kiwango cha kibinafsi.
Rais Magufuli hajawahi kutembelea taifa lolote nje ya Afrika tangu alipochaguliwa kuwa rais mnamo mwezi Oktoba 25.
Amekuwa akisisitiza kwamba ana kazi nyingi za kufanya nchini na kwamba kile ambacho kinaweza kufanywa kimataifa kinaweza kufanywa na mabalozi wa Tanzania waliopo mataifa hayo.

Mwanamke mkongwe zaidi duniani aaga dunia

Mwanamke mkongwe zaidi duniani Violet Mos Brown aaga duniaHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionMwanamke mkongwe zaidi duniani Violet Mos Brown aaga dunia
Mwanamke mmoja wa Jamaica anayedhaniwa kuwa mtu mkongwe zaidi duniani Violet Mos Brown amefariki akiwa na umri wa miaka 117.
Waziri Mkuu wa Jamaica alitangaza kufariki kwa mwanamke huyo kupitia mtandao wa Twitter.
Vyombo vya habari vya nchini vilisema alifariki kwa utulivu katika hospitali moja katika mji wa Montego Bay.
Violet Moss Brown, aliyekuwa mtu mkongwe zaidi mapema mwaka huu, alizaliwa mwaka 1900.
Alisema kuwa aliweza kuishi muda mrefu na kwamba aliweza kula karibu kila kitu isipokuwa ngurue na kuku.
Alisema pia hakunywa pombe kali.

Morgan Tsvangirai apelekwa Afrika Kusini kwa matibabu

Morgan Tsvangirai apelekwa Afrika Kusini kwa matibabu
Image captionMorgan Tsvangirai apelekwa Afrika Kusini kwa matibabu
Kiongozi wa upinzani wa Zimbabwe, Morgan Tsvangirai, amepelekwa Afrika Kusini kwa matibabu.
Wafuasi wa chama chake cha MDC, wanasema hali yake siyo mbaya sana, na inatokana na kujituma sana.
Mwaka jana, Bwana Tsvangirai alipatikana na saratani.
Mwandishi wa BBC nchini Zimbabwe, anasema watu wengi wanauliza, iwapo Bwana Tsvangirai, ni mzima vya kutosha, kuweza kuongoza muungano wa upinzani, dhidi ya Rais Robert Mugabe, katika uchaguzi wa mwaka ujao.
Rais Mugabe, mwenye umri wa miaka 93, ameiongoza Zimbabwe tangu mwaka wa 1980.

Kim Jong-un: Jeshi letu lazima liwe sawa na la Marekani

Rais Kim Jong un wa Korea kaskazini ameapa kwamba atahakikisha kuwa jeshi la taifa hilo lina uwezo sawa na ule wa MarekaniHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionRais Kim Jong un wa Korea kaskazini ameapa kwamba atahakikisha kuwa jeshi la taifa hilo lina uwezo sawa na ule wa Marekani
Korea Kaskazini imetangaza kuwa lengo lake kuu kijeshi kwa sasa ni kuhakikisha inakuwa na uwezo sawa na Marekani.
Shirika la habari la Korea Kaskazini lilitoa taarifa hiyo baada ya kombora la majaribio la mwisho kufanywa, ikisema kuwa kiongozi wa taifa hilo, Kim Jong-Un, amesema kuwa hataki kusikia Marekani ikisema itakabiliana na Korea Kaskazini kijeshi.
KIongozi wa taifa hilo Kim Jong un ameapa kuhakikisha kuwa taifa hilo linaafikia mpango wake wa kinyuklia kulingana na vyombo vya habari vya taifa hilo.
Lengo lake ni kuhakikisha jeshi la tifa hilo lina uwezo sawa na lile la Marekani kulingana na chom,bo cha habari cha KCNA kilichomnukuu kiongozi huyo.
Rais Kim Jong Un pamoja na maafisa wakuu wa jeshi wakisherehekea urushaji wa kombora jingineHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionRais Kim Jong Un pamoja na maafisa wakuu wa jeshi wakisherehekea urushaji wa kombora jingine
Matamshi ya bwana Kim yanajiri baada ya taifa hilo kufanyia majaribio kombora lake kupitia anga ya Japan, likitajwa kuwa kombora lililosafiri kwa umabli mkubwa zaidi
.Hatua hiyo imesbabishwa mgawanyiko miongoni mwa mataifa ambayo yaliunga nyuma ya uMoja wa Matifa dhidi ya Korea kaskazini siku chache zilizopita.
Lazima tuyaonyeshe mataifa yaneye uwezo mkubwa vile taifa letu litakavyokamilisha mpango wake wa kinyuklia licha ya vikwazo visivyoisha, bwana Kim alinukuliwa na chamobo cha habari cha KCNA
Alisema kuwa lengo la Korea Kaskazini ni kuwa na jeshi lenye uwezo sawa na lile la Marekani ili kuwazuia watawala wa marekani kutotaja swala la kuchukua hatua za kijeshi dhidi ya Korea Kaskzini
Makombora ya Korea kaskazini yaliofanyiwa majaribio
Image captionMakombora ya Korea kaskazini yaliofanyiwa majaribio
Katika mkutano wa dharura, baraza la Usalama la umoja wa Mataifa, lilishutumu Korea Kaskazini kwa kufyatua Kombora juu ya Japan, lakini likasisitiza kuwa hakutakuwepo na vikwazo zaidi dhidi ya taifa hilo.
Awali Marekani ilionya kuwa Korea Kaskazini itashambuliwa kijeshi iwapo vikwazo ilivyowekewa havitatekeleza chochote.
Lakini Uchina kwa upande wake ilihimiza Marekani ikome kutoa vitisho na badala yake ianze kufanya mashauriano.