Saturday, September 16

Makombora ya Korea Kaskazini yanaweza kutungua ndege za abiria?

North Korean missile launchHaki miliki ya pichaAFP
Korea Kaskazini wanaporusha makombora kupitia anga ya Japan hadi kwenye bahari ya Pacific, makombora hayo hupitia anga ya kimataifa - juu ya eneo ambalo ndege za kubeba abiria na mizigo hupitia.
Ving'ora vilipolia Japan na kuwaonya raia watafute hifadhi, je, kuna uwezekano wa makombora ya Korea Kaskazini kugonga ndege iliyowabeba abiria?
Ni swali ambalo watu wamekuwa wakijiuliza kwani Pyongyang hurusha makombora yake bila kutoa tahadhari.
Uwezekano ni mdogo sana, lakini wataalamu wanasema kwamba ni jambo linaweza kutokea - kwamba kombora litungue ndege.
"Iwapo ndege ya abiria itagongwa na kombora, shinikizo za kuitaka Marekani na washirika wake wachukue hatua za kijeshi zitakuwa juu sana," anaonya Vipin Narang, profesa ambaye ni mtaalamu wa masuala ya Asia Kusini katika chuo kikuu cha teknolojia cha MIT.

Mambo yanavyoweza kwenda kombo

"Majaribio haya ya makombora yanaweza kuwa hatari kwa ndege za abiria na za mizigo," anakariri Ankit Panda, mhariri katika jarida la The Diplomat.
Korea Kaskazini huwa hawatangazi ni wakati gani watatekeleza makombora yao na yatapitia wapi.
Kawaida, nchi hutoa tahadhari kuhusu majaribio kama hayo na kufahamisha mashirika ya ndege pamoja na meli maeneo ambayo wanafaa kukwepa.
"Ni vigumu kupima hatari yenyewe hata hivyo," anasema Bw Panda. "Ni kiwango cha chini sana. Itakuwa ni kupima uwezekano wa vitu viwili vidogo kwa kiasi ukilinganisha na bahari au anga, vikikutana."
Hwasong missile at North Korean military paradeHaki miliki ya pichaAFP
Image captionKorea Kaskazini mara kwa mara huonesha makombora yake Pyongyang
Korea Kaskazini, sawa na nchi nyingine, hupokea takwimu na maelezo muhimu kuhusu safari za ndege.
Hivyo badi, wanasayansi wake wanaweza kuchunguza wakati wanataka kurusha makombora yao na kujua ni wapi hakutakuwa na ndege zinazopita.
"Pyongyang bila shaka wangetaka kupunguza hatari ya kutokea kisa kama hicho. Kando na jinsi watu wengine wanaweza kufikiria, hawawezi kutaka jambo kama hilo litokee. Watatafuta njia ambayo itapunguza sana hatari."
Lakini bado kuna hatari na hii inaweza kuzidishwa na mambo mawili:
  • kombora likose njia na kuelekea eneo lenye shughuli nyingi angani au baharini
  • kombora lisambaratike likiwa bado linapaa angani na kuachia vifusi
Pyongyang mara nyingi hurusha makombora yake kupitia sehemu ambayo ni nyembamba zaidi Japan na ambapo hawatarajii kuwe na ndege nyingi, anasema Narang.
Lakini hilo linategemea ufanisi wa majaribio yenyewe.
Kombora lililorushwa Ijumaa linaaminika kuwa aina ya Hwasong 12 ambalo majaribio yake ya awali yaliyofanywa na taifa hilo yalionyesha kiwango chake cha kufanikiwa ni kidogo.
"Kwa hivyo inawezekana sana kwamba mambo yaende kombo na kombora liingie katika eneo lenye shughuli nyingi."

Tahadhari

Ingawa uwezekano wa tukio kama hilo kutokea ni mdogo, mashirika ya ndege yamekuwa yakichukua tahadhari.
"Baadhi ya amshirika ya ndege yamekuwa yakibadilisha njia ya safari na kuepuka kupitia anga ya Korea Kaskazini na Hokkaido," anasema Ellis Taylor mtaalamu wa uchukuzi katika shirika la FlightGlobal.
Mapema Agosti Air France waliongeza maeneo yanayozunguka Korea Kaskazini kuwa miongoni mwa maeneo ambayo ndege zao hazifai kupitia.
Air France aircraftHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionAir France walibadilisha njia yao ya kuelekea Japan
"Uamuzi wao waliuchukua baada ya moja ya ndege zao kuwa umbali wa 100km (maili 62 ) kutoka kwenye kombora moja lililofanyiwa majaribio na Korea Kaskazini awali. Safari za ndege zao kwenda Tokyo na Osaka sasa zinachukua dakika 10 hadi 30 zaidi."
Visa kama vile kutunguliwa kwa ndege ya MH17 nchini Ukraine vina baada kwamba mashirika pia yanafahamu uwezekano wa ndege zao kutambuliwa kimakosa na kushambulia maeneo yenye mizozo ya kivita.
Hii ina maana kwamba hali ya wasiwasi ikiendelea kuchacha, mashirika zaidi ya ndege yatakwepa rasi ya Korea.

No comments:

Post a Comment